CV ya Meku kwa Ngosha


[update] Wanafunzi wamkataa mwalimu wakimtuhumu kulawiti wanafunzi wa kiume

Mei 29, 2016 -- MAKAMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele , Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa katika Mahakama ya mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake.

Mshtakiwa huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000 mahakamani.

Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya sekondari Usevya kati ya Novemba 2015 na Aprili 2016.

Alieleza mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa alimuingilia mwanafunzi wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa aliahirisha shauri hilo hadi Juni 26 , mwaka huu litakapotajwa tena.

Inadaiwa kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake.

Kufuatia msimamo wa wanafunzi hao iliwalazimu Ofisa Elimu mkoa wa Katavi, Everest Hunji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashari ya Mpimbwe wilayani Mlele, Evaristo Kiwale kufika shuleni hapo Jumatatu jioni na kuzungumza na wanafunzi hao.

Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Kiwale alisema vitendo vya ushoga havikubaliki na kwamba tayari hatua stahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria.

“Msitaharuki mnapomuona mwalimu huyo mitaani msidhani hajachukuliwa hatua yoyote ile,” alisisitiza.

******************************

Mei 20, 2016 -- Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa kiume wanaosoma kidato cha tano katika shule ya Sekondari Usevya, Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi wamemkataa Mwalimu wao (jina tunalo) wakimtuhumu kuwafanyia vitendo vya ulawiti.
Wakizungumza kwa masikitiko na waandishi wa habari shuleni juzi jioni mbele ya Afsa Elimu Mkoa wa Katavi, Everest Hunji, baadhi ya manafunzi ambao ni mwenyekiti wa serikali ya wainafunzi wa Sekondari ya Usevya Moshi Ramadhani na Katibu Joniour Mgallah, walisema vitendo anavyofanya mwalimu huyo vimewaathiri kisaikolojia na kudhorotesha ufaulu wao kimasomo.
''Kwa kweli sisi wanafunzi tunakiri mwalimu ambae jina lake tunalo amekuwa akitumia Madaraka yake ya umakamo mkuu wa shule vibaya,Hususani anapokukamata na kosa hapa shuleni badala ya kukupa adhabu ya kulingana na kosa ulilofanya anakuomba kujamiiana naye huku akijua kuwa anayetaka kufanya naye mambo hayo ni mwanaume na utakapokataa anatishia kukufukuza shule,'' walisema.
Wanafunzi hao waliendelea kufafanua kuwa mwalimu huyo tayari ameshatekeleza vitendo hivyo vya ulawiti kwa baadhi ya wanafunzi na kuongeza kuwa wapo tayari kutoa ushahidi mahakamani kama kutahitajika kufanya hivyo.

Sambamba na hayo, walisema kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwatumikisha wanafunzi katika shughuli zake binafsi za uzalishaji kwa kuwapeleka kufanya kazi kwenye mashamba yake.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Erasto Kiwale ambaye aliambatana na Afisa Elimu Mkoa wa Katavi, Everest Hunji alisema Kitendo hicho hakikubaliki na tayari hatua sitahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria, hivyo wanapomwona mwalimu huyo mitaani wasidhani hajachukuliwa hatua.

Afisa Elimu Mkoa wa Katavi, Everest Hunji aliwataka wanafunzi kuwa watulivu na kuziacha mamlaka husika kulishughulikia suala hilo huku akiwaahidi kuwa malalamiko yao yatashughulikiwa ipasavyo.
  • Taarifa ya Walter Mguluchuma - Mlele.

Call for nomination: Africa Food Prize

The Africa Food Prize evolved from the Yara Prize, which was established in 2005.

The Africa Food Prize is the preeminent award recognizing an outstanding individual or institution that is leading the effort to change the reality of farming in Africa—from a struggle to survive to a business that thrives.

The US $100,000 prize celebrates Africans who are taking control of Africa’s agriculture agenda. It puts a spotlight on bold initiatives and technical innovations that can be replicated across the continent to create a new era of food security and economic opportunity for all Africans.

Do you need more information? Please click here to open a PDF 

Do you know the perfect candidate for the Africa Food Prize? www.africafoodprize.org

---
Thanks "YakeYako" for sharing this with us.

Watatu wakamatwa na kadi 19 za benki za watu tofauti wakitoa fedha ATM ya NMB

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .

Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea, wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.

Nyanda ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea feda .

Amesema baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha.

Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi cha fedha taslimu shilingi 3,680,000.

Amezitaja Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC 61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237, AC 61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.

Kaimu kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac 61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC 70408100131.

Amesema watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika na bado watuhumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .

Kaimu kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za namba zao za siri za kadi wanazozitumia za ATM za kwenye benki .
  • Taarifa ya Walter Mguluchuma - Katavi

Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 27, 2016Maagizo ya WM Majaliwa baada ya kusafiri kwa mabasi yaendayo harakaTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

*Ataka watu walipe tiketi rasmi, wafuate taratibu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua utendaji kazi kwenye mabasi ya mwendokasi yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa ambazo amesema zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea. 

Waziri Mkuu ambaye alilipa nauli na kupanda basi namba 23 lenye usajili namba T125 DGW kuanzia kituo cha Ferry, Kivukoni, ametumia muda wa dakika 50 kufika Kimara mwisho kwa kutumia usafiri huo. 

Waziri Mkuu alipanda basi hilo saa 3:30 asubuhi na lilianza safari saa 3:33 baada ya kusubiri wengine wapande. Kwa wastani ililtumia kati ya dakika mbili hadi tatu kutoka kituo kimoja hadi kingine. Basi hilo liliwasili Kimara Mwisho saa 4:23 asubuhi. 

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Kimara mwisho mara baada ya kumaliza ziara hiyo fupi ya ukaguzi leo (Ijumaa, Mei 27, 2016), Waziri Mkuu alisema aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla ili kuangalia matumizi ya njia za mabasi yakoje na pia kuona abiria wanaelewa vizuri namna ya kuitumia huduma hiyo. 

Amesema ameridhishwa na mradi unavyofanya kazi ila ameelezwa kuna usumbufu kwenye mageti wakati abiria wanapotaka kuthibitisha tiketi zao hasa wakati wa asubuhi kunapokuwa na msongamano wa abiria. Pia alielezwa kwamba kuna baadhi ya abiria wanakuja na tiketi za jana yake jambo ambalo linaleta usumbufu kwa sababu hazitambuliki kwenye mfumo wao. 

“Nimeridhishwa na uharaka wa njia kwa sababu na mimi mwenyewe nimetumia dakika 50 kufika hapa ingawa kuna maeneo nimeona kuna haja ya kuwa na taa maalum za kuzuia magari (special sensors) wakati mabasi yakipita ili kuepusha ajali,” alisema. 

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na mtaa wa Samora, Morogoro na Jamhuri na makutano ya Morogoro na Kisutu. 

Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waende na tiketi rasmi badala ya kutumia tiketi za jana kwa sababu kufanya hivyo ni makosa na mtu anakuwa amedhamiria. “Hawa watachukuliwa hatua za kinidhamu. Mtu akija na tiketi ya jana akamatwe na kupelekwa polisi, huyu atakuwa amedhamiria,” alisema Waziri Mkuu wakati akiongea na mhudumu mmoja katika kituo cha Kimara Mwisho. 

“Ninawasihi wananchi wanaotumia usafiri huu wajifunze kufuata utaratibu na kuwasisitizia kuwa kila abiria aje na tiketi ambayo ni rasmi,” alisema na kuongeza: “Haya mabasi nimebaini yako vizuri. Ninatoa msukumo kwa watumishi wa umma wapande mabasi haya ili kupunguza msongamnao wa magari barabarani.”

Katika kupiunguza baadhi ya changamoto, Waziri Mkuu alisema Serikali itasimamia uboreshaji wa ukataji tiketi ili kuondoa usumbufu kwa abiria. Pia alivionya vyombo vya moto viache kutumia njia maalum ya mabasi hayo. 

Pia aliwataka polisi wanaofanya doria za usiku kupita kwenye fly-overs na kuwaondoa watu wanaolala kwenye maeneo kwani wanahatarisha usalama wa watu wanaotumia njia hizo. “Zile siyo sehemu za kulala, wanaofanya hivyo wanahatarisha usalama wa watumiaji wa njia hizo, kwa hiyo polisi wakiwakuta watu wa aina hiyo wawakamate mara moja,” alisema. 

Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga ambaye alifuatana na Waziri Mkuu kaktika ziara hiyo, alisema amepiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali. 

“Tulishapiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali, ninawasihi madereva watambue hili na watii,” alisema. 

Machi 22, mwaka huu Waziri Mkuu alitembelea soko la Feri kwa lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo (kuzuia moshi) na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi. 

Aprili 15, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya kikao na kuwaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza pindi majaribio yakianza. 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

IJUMAA, MEI 27, 2016.

Sabodo offers 1bn/- if Tanzania gov stabilizes shilling


4 tips: How to maximize space and properly pack items for a trip


Travel blogger Kate McCulley showed Inside Edition some great packing secrets that will make your life easier — and much more organized.
  1. To maximize space and keep items arranged properly in your bag, use packing cubes. To get the clothes inside the cubes, McCulley instructed to “line the shirts up with sleeves together, then add pants.”
  2. Use the middle space for smaller items. Then start folding and tucking each piece in, until you have a compact bundle. If that technique isn't for you, rolling your clothes could be the next best thing. “It saves so much space and keeps your clothes crease-free. In fact, if you roll your everything, you can probably fit five extra items in your suitcase."
  3. Since shoes take up so much space in luggage, McCulley advises putting socks inside the footwear to save space. 
  4. For your jewelry, McCulley has a nifty tip: Put them inside a pill container so nothing is loose or unorganized in your bag.
Also watch Expedia's 8 Packing Techniques demonstrated in the following video.


[video] Hotuba ya Rais Magufuli kwenye mkutano na makandarasi Mei 26, 2016Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Diamond Jubilee kwa ajili ya Ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo kuhusu katapila linalotumika katika kazi mbalimbali za ujenzi mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli na Rais mstaafu Kikwete huko Ikulu leo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

$24.97 (from $59) Black & Decker PowerPro Wide-Mouth 10-Cup Food Processor, Black

Huge price drop! $350 (from $1,595) PuraSleep CoolFlow Memory Foam Mattress - Made in USA - 10-Yr Warranty - Queen, King, Full, Twin
Neat Feat Beauty Buzz 3 in 1 Callus and Dry Skin Remover with Epilator and Shaving Head

Price drop: Tiger 10-Cup Rice Cooker with Food Steamer & Slow Cooker, Stainless Steel Black

Yellow Gold-Plated Sterling Silver Diamond-Accent Floral Dangle Earrings

Anusurika kifo baada ya kujirusha kutoka kwenye mmara wa simu
Kijana mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.

Tukio hilo limetokea hii leo baada ya kijana huyo kuupanda mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morali kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.

Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.
  • BMG

Amazon deal: $190 (usually $475) Seiko Women's Japanese Quartz Gold Watch