Masaibu ya Kitwanga na athari zake kiusalama (wa Taifa)

[...] Ikumbukwe kuwa hadi muda huu hatufahamu kuwa ‘tatizo la ulevi wa Kitwanga’ limeathiri vipi utendaji wake wa kazi kama Waziri wa wizara nyeti ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kiusalama, hakuna kitu majasusi kutoka nchi za nje wanaombea kama kukutana na mtendaji wa serikali katika eneo nyeti ambaye ana udhaifu kama huo wa ulevi. Na ninaamini kuwa ndugu zangu wa Idara ya Usalama wa Taifa wanafahamu fika jinsi majirani zetu walivyojaza majasusi ndani ya Tanzania yetu, hususan baada ya ujio wa Dkt Magufuli unaoanza kuifanya nchi yetu kuwa tishio kiuchumi kwa majirani zetu.
Ni matumaini yangu makubwa kuwa kutafanyika uchunguzi wa kina kuhakikisha kuwa mapungufu ya Kitwanga hayakuathiri usalama wa taifa letu kwa maana ya kwamba hakuna aliyetumia ‘ulevi wake’ kum- “blackmail” ili atoe siri za serikali.

Kiu kubwa kwa Watanzania kwa muda huu ni kuona Bunge litachukua hatua gani dhidi ya ‘mwenzao.’ Hata hivyo, ishara mbaya zimeanza kuonekana baada ya Naibu Katibu wa Bunge, John Joel, kunukuliwa akidai kuwa “hakuna kifungu chochote cha kanuni za Bunge kinachomzuwia mtu kuingia Bungeni akiwa amelewa.” Yaani hawa waheshimiwa wana kinga dhidi ya Kanuni za Utumishi wa Umma zinazokataza “tabia inayovunja heshima ya utumishi kwa umma hata nje ya mahali pa kazi” kwa mfano ulevi.

Lakini kubwa zaidi ni kuona kuwa ‘kutumbuliwa’ kwa Kitwanga haukuathiri uchunguzi wa suala tete la Lugumi. Kimsingi, kwa kutolewa uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kamati Teule ya Bunge inayochunguza suala hilo sasa haina kisingizio chochote cha kutowapatia Watanzania kile wanachostahili: ukweli kamili kuhusu suala hilo.]
Vifungu hivi vimenukuliwa kutoka kwenye makala ya Evarist Chahali iliyochapishwa katika gazeti la RAIA MWEMA la Mei 25, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 30, 2016ShaYu: Mataifa dhaifu ni mataifa yaliyokosa maarifa

Kwa wenye hekima maisha ni fumbo ambalo linapaswa kufumbuliwa. Na Dunia ni chuo ambacho binadamu anatakiwa kujifunza kila siku ili kufikia ukuaji wake wa mwisho kiakili. Chuo hiki ni kikubwa kuliko chuo chochote na wahitimu wake huvikwa tuzo ya ufalme.

Kwasababu hatukuumbwa tuishi pekee, bali tuliumbwa tuishi ili tujifunze na ili tukue. Tena Binadamu hakui kama mti tu kwa mfumo wa kimaumbile bali akili yake lazima pia ikue. Na aweze kuwa na nguvu ya kuchanganua jema na baya. Aondokane na ujinga. Na AFUATE njia iliyo sahihi. Kwasababu ni katika njia iliyosahihi ndio kwenye misingi iliyo imara. Ni wajibu wetu kukusanya maarifa kadiri ya uwezo wetu. Ni katika maarifa binadamu hupata STRENGTH na sio katika ujinga. Ujinga ni udhaifu. Mataifa dhaifu ni mataifa yasiyo na maarifa.

Tunakamata samaki kwasababu tuna uelewa mkubwa zaidi yao. Vile vile kuku, mbuzi na Ng'ombe tunafuga, Kwasababu uwezo wa akili zetu ni mkubwa zaidi yao ndio maana tunawatawala.

Na binadamu na mataifa wanatofautiana katika uelewa pia na utumiaji wa akili zao kutafuta na kukuza maarifa. Mataifa yenye watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri watayatawala mataifa ya watu wajinga. Wana nguvu ya kuvumbua vitu na silaha kutawala wajinga. Watu waliowekeza katika mambo ya kijinga yasiyo na manufaa watatawaliwa.

Kama kuna ulafi ambao binadamu anapaswa kuwa nao, ni ulafi wa kutafuta maarifa ili yamuongoze katika maisha yake. Na kuuvamia na kuuteka kisha kuufunga kamba ujinga na upumbafu, ambao una madhara makubwa kwa maisha ya binadamu na hata katika mataifa. Ni heri kuwa maskini kuliko kuwa tajiri mpumbavu na mjinga ambae njia zake sio nzuri.

Makosa mengi tunayofanya yanatokana na kukosa maarifa ya kutosha na busara ya kuongoza maisha yetu. Kwahiyo ni muhimu kwetu kutafuta maarifa ambayo yatatusaidia kufanya maamuzi yenye hekima. Roho nyingi zimeangamia kwa kutenda matendo ambayo sio sahihi na kujikuta kwenye majuto. Na majuto ni mjukuu.

Tunaweza kubadilika tunaweza kubadili njia zetu. Na njia pekee yenye matumaini ni njia ya mwanga. Ni muhimu kwetu kutafuta tochi ambayo itamulika maisha yetu na tochi hiyo ni maarifa. Hakuna kiza ambacho kitafunika tochi ya maarifa.

Kwa uwepo wetu katika dunia hii tuna wajibu mmoja mkuu. Kutafuta mwanga ambao utaongoza maisha yetu kwa kizazi hiki na kinachokuja na huo ndio wajibu wetu mkuu. Kufanya jitihada kadiri ya uwezo wetu kuwa karibu na Mungu na kuacha matendo ya gizani.

Na tujue kwamba mataifa dhaifu yote duniani ni mataifa yaliyopungukiwa maarifa. Ni wajibu wetu wa dhati kabisa kutafuta maarifa ili yatukomboe.

Shepherd of the Lord.

--------
Shaaban Yusuph

[video] Mkuchika akisoma maazimio ya Kamati: Wabunge 7 wazuiwa kuhudhuria vikao vya Bunge

UPDATE: Mei 31, 2016...


***********

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge limepitisha azimio la kuwasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge baadhi ya wabunge wa Kambi ya Upinzani waliohusika katika kufanya vitendo vya vurugu ndani ya ukumbi na kudharau Mamlaka ya Spika Januari, 27, 2016.

Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Mhe. Kabwe Zubeir Ruyangwa Kabwe, Mhe. John Heche, Mhe. Halima Mdee, Mhe. Tundu Lissu, Mhe. Godbless Lema, Mhe. Pauline Gekul na Mhe. Esther Bulaya.

Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Akisoma adhabu hizo Mwenyekiti wa kamati hiyo yenye wajumbe 15 Mhe.George Huruma Mkuchika amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo kwa kuwaita na kuwahoji wahusika ulibaini kuwa wabunge hao walitenda kosa kwa kukiuka kanuni zinazoliongoza bunge hilo.

Imebainishwa kuwa Mhe.Zitto Kabwe alivunja masharti ya Kifungu cha 24(c), (d) na (e) cha Sheria ya Haki na Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 60(2) na (12) , 74(1) na (b) kwa kusimama na kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau mamlaka ya Spika.

Kamati hiyo ilibaini kuwa Mhe.Godbless Lema, Mbunge wa Arusha alivunja Masharti ya kifungu cha 24 (c),(d) na (e) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 pamoja na Kanuni ya 74(1) (a) na (b) ya kanun hiyo Kudharau Mamlaka ya Spika.

Kwa upande wa Mhe.John Heche alivunja kanuni ya 72 (1) na 68(10) ya kanuni za Bunge kwa kuendelea kusimama na kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa mwongozo na kuongeza kuwa vitendo hivyo vilivuruga shughuli za Bunge.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati hiyo Mhe.Halima Mdee, Mhe.Tundu Lissu,Mhe Pauline Gekul na Mhe.Ester Bulaya walivunja masharti ya kifungu cha 24 (c), (d) na (e) cha sheria ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 72 (1)68 (10), 60(2) na 12 na 74(1) (a) na (b) kwa kusimama na kuendelea kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi, kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau Mamlaka ya Spika.

Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Mhe. Ester Bulaya na Mhe.Tundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao vyote vya Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya Spika.

Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul, Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.

Adhabu hizo Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016 kwa kuwa alipatikana na kosa moja na pia kwa kuwa alitoa ushirikiano kwa kamati kwa kufika na kujibu maswali yote kama alivyoulizwa pamoja na kuheshimu vikao vya kamati na Mwenyekiti aliyeongoza vikao hivyo.

Pamoja na adhabu hizo Kamati hiyo imetoa maoni na mapendekezo kuwa Bunge liandae mafunzo ya kutosha kwa wabunge wote kuhusu matumizi ya uzingatiaji sahihi wa kanuni sahihi wa kanuni za Kudumu za Bunge hasa kanuni za majadiliano ndani ya Bungeni.

Aidha, Kamati hiyo imesema kuwa ipo haja ya kutungwa kwa kanuni za maadili kwa wabunge wote kama kifungu cha 12 A Cha Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kinavyoelekeza ili kuweza kudhibiti nidhamu kwa wabunge kwa kuhakikisha heshima na hadhi ya Bunge inadumishwa.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge wakichangia kwa nyakati tofauti kuhusu suala hilo wamesema kuwa ipo haja ya Bunge kurudisha heshima yake kwa wabunge wote kuheshimiana na kutoa michango yenye staha kwa kuzingatia nafasi walizonazo katika jamii.

Wamesema kuwa michango wanayoitoa ndani ya Bunge hilo lazima ijikite katika masuala yanayowahusu wananchi wanaowawakilisha badala ya mambo yanayochochea vurugu na kulifanya Bunge lipoteze heshima yake katika jamii.

Aidha, wabunge hao wamekubali kwa kauli moja kuanza upya kuzingatia kanuni zinazoendesha vikao vya Bunge huku wakimtaka Spika wa Bunge au Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutosita kuchukua hatua za haraka kwa mbunge yeyote atakayekiuka utaratibu na kanuni zilizowekwa.

J.Crew: How to Find a Suit that Fits - 4 tips


1. SEAMS LEGIT
The jacket’s shoulder seams should fall squarely at the edge of your natural shoulder, not short of or beyond it. Make sure to get this one right, or everything else will be thrown off.


2. THE END RESULT
Your sleeve should end right near your wristbone (enough to expose ¼" to ½" of shirt cuff).


3. IT TAKES TWO
When you fasten the top button on a two-button suit, you should be able to fit two horizontal fingers between your chest and the jacket (snug but not pulling). You should also be able to fit two vertical fingers’ worth of room in the waist of your pants when they’re fastened.


4. THE LONG AND SHORT OF IT
The jacket’s bottom hem should fall near the base of your front pockets—just far enough to cover your rear when seen from the back.

Source: jcrew.com

Symbion Power: Statement in response to Sunday's media reports

WASHINGTON, DC – MAY 30, 2016 – Following today’s news articles in Tanzania, Symbion Power has issued the following statement from the firm’s Washington, DC office to reporters with the aim of correcting the misleading and wholly untrue statements made to the media by the Managing Director of the Tanzania Electric Supply Company Limited, Mr. Felchesmi Mramba.

“We continue to be astonished by the revisionist theories of Mr. Mramba who is a high level Tanzania government official and the fact that he uses the media to present them. Apart from a single letter, which he back-dated by 10 days in which he suggested ceasing negotiations with Symbion, he has never discussed any of the issues he is now raising. Shockingly, Mr. Mramba is not being truthful and open. Here are just a few of the facts Mr. Mramba has ignored”:

The Power Purchase Agreement


“There is no question whatsoever that the PPA is a valid and binding document signed by TANESCO’s Managing Director, Mr. Mramba. In signing the PPA, Mr. Mramba was acting with the express written approval the Director General of Energy, who approved the PPA with Symbion by letter dated 4 November 2015. The PPA was also approved by Attorney General Temi by letter dated 4 December 2015. The PPA with Symbion dated 10 December 2015 was signed by Mr. Mramba, whose signature was witnessed by Godson Makia, TANESCO’s Chief Legal Counsel, as well as two senior executives of Symbion.

Symbion’s’ Tanzania CEO was told to collect the fully executed version at 10.30 am from TANESCO Head Office on 10th December. Mr. Mramba and the Legal Counsel of TANESCO, Mr. Godson Makia were at a board of Directors meeting until 11.30 am, and when they came out he was directed to the ground floor to meet Mr. Shirima who took him to the Senior Strategic Manager’s Office to collect the full PPA signed on every page by Mr. Mramba. Symbion signed the dispatch book as confirmation of receipt.

For Mr. Mramba to deny that the PPA he signed and issued to Symbion is invalid is patently dishonest.”

Law Suits

“For five (5) whole years TANESCO has failed to fully pay Symbion and we have been owed between $25 million and $80m dollars at any one time. Those amounts are enormous. Is it therefore surprising to anyone that Symbion itself has debts and cash flow issues in Tanzania. But, for that entire 5-year period we have always kept the lights on, we went ahead and built two (2) emergency plants when Tanzania would have been in darkness due to low water levels at Mtera, Kihansi and Kidatu hydro-power plants. Now, when the dams are finally full in 2016, TANESCO attempts to terminate its agreements.

Indeed, it was the government of President Jakaya Kikwete that supported and encouraged Symbion to acquire the Ubungo power plant and build the two (2) emergency plants in Dodoma and Arusha because the country was in dire circumstances and needed power during that time.

Certain creditors of Symbion decided to take legal action because their patience had run out. Unfortunately, some of them submitted drastically inflated claims and some, such as that of RSS are spurious. Mr. Mramba also mentions a lawsuit for a debt from East African Cables. That company is actually owned by TANESCO, and they sued Symbion for $3m dollars when the debt was actually around $2m dollars. Now, Mr. Mramba uses that as his theory for why TANESCO is concerned about Symbion. TANESCO owed Symbion over $50m dollars at the time, yet they sue Symbion for $3m.

Despite all of this Symbion has never sued TANESCO or switched off the power plant despite the continuous breach of our contract for almost five (5) years. This was simply because the people who suffer when we switch off are the innocent people of Tanzania. We are sure that Mr. Mramba does not suffer because he probably has a diesel generator at home. It is the local population who suffer when the black outs occur.

TANESCO has not paid Symbion anything for 2015 and 2016 but we have continued to operate and give people power. How does Mr. Mramba think Symbion should operate when he does not pay Symbion and is up to two (2) years late when he does?”

Dispute Resolution

“There is a valid, enforceable contract in place and it has a clause in it that sets out how disputes between Symbion and TANESCO must be dealt with. This is for arbitration at the ICC court in Paris.
Despite false statements and retroactive excuses planted in the media by Mr. Mramba and TANESCO, we are still waiting for a reply to a letter we sent to the government almost three (3) weeks ago, on 11thMay. 

We continue to be hopeful that eventually some common sense will prevail because the continued breach of the agreement and the assessment of damages to our reputation as a consequence of the current actions of TANESCO and Mr. Mramba will be extremely expensive for Tanzania. If it eventually transpires that this turns into an international dispute, we look forward to us, TANESCO and government staff explaining these issues under oath to the judges. We will ensure the public is kept informed about this given the fabrications and untruths we are facing today. We have never seen such behavior before.

Instead of misleading the public it is about time Mr. Mramba begins to tell the truth and to start acting in the best interests of the people of Tanzania. He and whoever he is working with should be ashamed for lying to the people of Tanzania that gas fired power from Symbion and Songas is expensive, and that he is relieved to get out of our PPA, when TANESCO is buying fuel for and running an expensive oil fired power plant called IPTL, and when they do not even pay the firms who use cheap gas.

On Mr. Mramba’s own public admission, Symbion and Songas power costs around 8 to 9 cents and TANESCO charge their customers around 14 cents. So they add approximately 5 to 6 cents to the price that we charge them. 

Everyone knows that this is not the case for an oil fired power plant.

Other commentators have hinted at the fact that there is a more sinister side to this than is being presented to the public and we too are investigating the claims about the attempted monopolization of the power sector by some individuals. If that is allowed to happen, Tanzanians will pay dearly for it.”

Julie Foster
Consultant


US Mobile: +1 917 282 9310
[email protected]
www.symbion-power.com

************

WASHINGTON, DC – MAY 30, 2016 – Kufuatia makala za leo katika vyombo vya Habari nchini Tanzania; Kampuni ya Symbion Power kutoka katika Ofisi yake ya Washington,DC imetoa tamko lifuatalo kwa Waandishi kwa lengo la kusahihisha kauli mbali mbali zilizopindishwa na zisizo na ukweli kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini Tanzania Ndugu Felchesmi Mramba

“ Tunaendelea kushangazwa na nadharia za kubadilisha itikadi za Ndugu Mramba ambaye ni Afisa wa kiwango cha Juu katika Serikali na ukweli kwamba anatumia Vyombo vya habari kumuwakilisha. Mbali ya barua ; ambayo kimsingi alibadilisha tarehe ya kuandikwa kwake kwa kuirudisha nyuma kwa siku 10; ndani yake amependekeza usitishwaji wa Majadiliano na Symbion, hajawahi kujadili jambo lolote ambalo kwa hivi sasa anazungumzia. Kwa mshituko mkubwa Ndugu Mramba hakuwa mkweli na muwazi. Hapa chini ni baadhi ya mambo yaliyo ya ukweli:

Makubaliano ya Ununuzi wa Umeme

Kufuatia maombi ya TANESCO, seti (3) za Makubaliano ya Manunuzi wa Umeme ya Miaka 15 yalitiwa sahihi na Mkurugenzi Mtendaji wa Symbion Power na Afisa Fedha Mkuu mnamo tarehe 8 Disemba 2015 katika ofisi za Tanesco yakishuhudiwa na Wafanyakazi wa TANESCO ambao ni Ndugu Hieromini Shirima na Ndugu Kasinda Malale katika ofisi zilizo ghorofa ya Tisa (9). Kila ukurasa wa seti zote 3 za nyaraka ziliwekwa herufi za majina katika mkutano huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Symbion Tanzania aliambiwa kuchukua nyaraka ambazo zimekamilika saa nne na nusu asubuhi kutoka Makau Makuu ya Ofisi za TANESCO tarehe 10 Disemba. Ndugu Mramba na Mwanasheria wa TANESCO, Ndugu Godson Makia walikuwa kwenye mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi mpaka muda wa saa tano na nusu asubuhi. Na wakati aliporudi alielekezwa kwenye ghorofa ya chini kabisa kukutana na Ndugu Shirima ambaye alimpeleka Ofisi ya Meneja Mwandamizi wa Mipango kwenda kuchukua nyaraka za PPA ambazo zimetiwa sahihi katika kila Kurasa na Ndugu Mramba. Kampuni ya Symbion ilitia sahihi katika kitabu kinachothibitisha upokeaji wa Nyaraka (Dispatch book)

Baadaye na kwa mshangao Mkubwa Ndugu Mramba aliimuita Mkurugenzi wetu nchini Tanznia na kumuomba asimwambie mtu kuwa aliweka sahihi kwenye mkataba na kwamba awe subira kuhusu malipo kwa sababu aliombwa atume Nyaraka za PPA Ikulu. Ndugu Godson Makia alikuwepo kwa wakati huo. Alisema alitishwa na Viongozi na kulazimishwa kutia sahihi kwenye nyaraka inayoonyesha kuwa alikuwa hajatoa Nyaraka za PPA kwa kampuni ya Symbion ambayo alikuwa tayari ameishaipa hizo nyaraka. Ushauri wake ulikuwa kwmba nyaraka za PPA zilikuwa halali lakini tulipaswa kusubiri hati ya malipo kwa vile Serikali ilikuwa ikiipitia. Aliongeza kuwa hili jambo halingechukua muda mrefu na baada ya hapo tutaweza kuchukua malipo yetu. Ndugu Mramba alisimulia hii habari kwa baadhi ya watu wakiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni yetu iliyoko Marekani; Ndugu Paul Hinks. Kampuni ya Symbion ilikuwa nyaraka halali za PPA na tulikuwa tukizalisha Umeme. Ndugu Mramba hakusema sitisha kutoa umeme na hajawahi kufanya hivyo. Alisema kuwa alikuwa ameagizwa na Mheshimiwa Rais wa Tanzania; alisema katika mtazamo wake nyaraka za PPA zilikuwa sawia na faida za Kitaifa na alisema kuwa alimdhirishia hilo kwa kuzingatia na bei nafuu ambazo kampuni ya Symbion inauza umeme wake.

Kampuni ya Symbion ilichukulia kama utaratibu wa kawaida wa Serikali mpya kupitia mikataba yote ya Serikali kwa vile ilikuwa imetajwa kwenye baadhi ya ripoti za vyombo vya habari Vikimnukuu Waziri Mkuu kwamba Makubaliano mengi na Wawekezaji yanapitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuona kama zina maslahi ya Kitaifa. Hatukuwa hata mara moja kufikiria kuwa tutaweza kukumbana na jaribio la upande mmoja kusitisha mkataba miezi sita baadaye. Kama TANESCO ilikuwa ikifikira kuhusu hili na hawakuwahi kufikiria nyaraka za PPA kuwa na tija kwanini waliendelea kuchukua umeme wetu bure? Huu ni ukosefu wa Uaminifu kwa kiwango cha juu.

Kesi

Kwa miaka mitano (5) TANESCO imeshindwa kuilipa malipo yote Kampuni ya Symbion na tumekuwa tukidai kiasi kati ya Dola za Kimarekani Milioni 25 na Dola za Kimarekani Milioni 80 katika muda wote. Hiki ni kiasi kikubwa cha pesa. Je, Inashangaza kwa yeyote yule kwamba Symbion ina madeni na matatizo ya mzunguko wa fedha nchini Tanzania? Kwa kipindi cha miaka yote mitano (5) tumehakikisha taa zinawaka na tuliweza kusonga mbele zaidi kwa kujenga mitambo miwili ya uzalishaji umeme wa dharura pale ambapo Tanzania ingekuwa kwenye kiza kinene wakati kimo cha Maji katika Mitambo ya Mtera, Kihansi na Kidatu kilipopungua. Hivi sasa ambapo mabawa yote yamejaa mwaka 2016 TANESCO inafanya jaribio la kusitisha Mikataba

Kiukweli ilikuwa ni Serikali ya Rais Jakaya Kikwete iliyounga mkono na kuhamasisha Kampuni ya Symbion kuchukua Mitambo ya Ubungo na kujenga mitambo miwili ya uzalishaji umeme wa dharura Dodoma na Arusha kwa sababu nchi ilikuwa kwenye wakati mgumu na ilihitaji Umeme.

Baadhi ya Washikadau wa Kampuni ya Symbion wameamua kuchukua mkondo wa Kisheria kwa vile wamechoka na wameshindwa kuendelea kuvumilia. Kwa bahati mbaya baadhi yao walitoa madai yaliyotiwa chumvi mfano wale kupitia mtando wa RSS ni ya uongo na si halisi. Ndugu Mramba anataja pia kesi ya deni la Kampuni ya East African Cables. Hiyo kampuni ni mali ya TANESCO na waliishitaki Kampuni ya Symbion kwa deni la dola za kimarekani Milioni 3 wakati ambapo deni halisi lilikuwa Dola za Kimarekani Dola Million 2. Kwa wakati huo TANESCO ilikuwa inadaiwa na Kampuni ya Symbion zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 50 kwa muda ule na bado TANESCO iliishitaki Symbion kwa deni la Dola za Kimarekani milioni 3.

Pamoja na hayo kampuni ya Symbion haijawahi kuishitaki TANESCO wala kuzima Mitambo ya Kuzalisha umeme pamoja na kuwepo kwa ukiukwaji wa mkataba kwa miaka takribani mitano (5). Hii ni kwa sababu watu wanaoumia mitambo ikizimwa ni wa watu wasio na hatia ambao ni Watanzania. Tuna uhakika kuwa Ndugu Mramba hataabiki kwa vile atakuwa na jenerata nyumbani. Ni wenyeji ambao hutaabika na kukatika umeme.

TANESCO haijalipa Kampuni ya Symbion chochote kwa mwaka wa 2015 na 2016 lakini tumeendelea kufanya kazi na kusambaza umeme. Hivi Ndugu Mramba anafikiria Symbion itapaswa kutenda kazi vipi wakati hailipi Symbion na ni tayari miaka miwili imepita pale atakapofanya hivyo?

Utatuzi wa Migogoro

Kuna mkataba halali na unaotekelezeka na ndani yake kuna kipengele ambacho kinaonyeshwa jinsi gani migogoro inapaswa kutatuliwa. Hii ni kwenye usuluhishwi kwenye Mahakama ya ICC mjini Paris.

Pamoja na kauli zisizo za ukweli na zinazoibua visingizio vya zamani ambazo zimepandikizwa kwenye vyombo vya habari na Ndugu Mramba na TANESCO; bado tunasubiri majibu ya barua tuliyotuma kwa Serikali yapata wiki tatu (3) zilizopita, tarehe 11 Mei.

Tunaendelea kutumaini kuwa busara zitatumika kwa sababu kuendelea kukiuka makubaliano na makadilio ya hasara kwa jina la kampuni yetu kama matokeo ya matendo ya sasa ya TANESCO na Ndugu Mramba yatakuwa na gharama kubwa sana kwa Tanzania. Kama itapelekea kuwa yote haya yaendelee kwenye Migogoro ya Kimataifa; tutaangalia mbele yetu, TANESCO na Watendaji wa Serikali wataelezea haya mambo chini ya kiapo mbele ya MaJaji. Tutahakikisha kuwa Uma wa Watanzania unajulishwa kile kinachoendela katika kila kinachoumbwa na uongo uliopo hivi leo. Hatujawahi kuona tabia kama hii.

Badala ya kuudanganya umma wa Watanzania; ifike pahala Ndugu Mramba aanze kusema ukweli na kutenda kwa maslahi ya Umma wa Watanzania. Yeye pamoja na washirika wake wanapaswa kuona aibu kwa kudanganya Watanzania kwamba Umeme unaozalishwa kutokana na Gesi kutoka Symbion na Songas ni aghali na kwamba ataweza kutoka salama kwenye PPA yetu. Na pale TANESCO inanunua mafuta na inaendesha mitambo inayotumia mafuta kuzalisha umeme aghali iitwayo IPTL, na pale waposhindwa kulipa kampuni ambazo zinatumia gesi ya bei nafuu.

Kuhusu Kukiri kwa Ndugu Mramba mbele ya umma, Umeme kutoka Symbion na Songas unagharimu kiasi cha kati ya senti 8 na 9 na TANESCO inatoza wateja wake kiasi cha senti 14; ndio kusema inaongeza karibia kiasi cha senti 5 mpaka 6 kwa bei ambayo tunawatoza
Kila mtu anajua kuwa hii ni tofauti na kile kinachofanyika na Mitambo ya kuzalisha umeme inayotumia mafuta.

Baadhi ya wachangiaji wamegusia ukweli kuwa kuna kilichojificha zaidi ya kile kinasemwa mbele ya Umma na sisi tunachunguza hayo madai kuhusu jaribio la kuwepo mzalishaji mmoja na baadhi ya watu. Kama hii itaruhusiwa kutokea hapa Tanzania, Watanzania ndio watakaolipa gharama kubwa.

Julie Foster
Public Relations

US Mobile: +1 917 282 9310
[email protected]
www.symbion-power.com

Mpemba Effect katika blogu maarufu za Kimataifa

Erasto Mpemba na Denis Osborne (London, 2013)
Kwa mujibu wa utafiti wa Erasto Mpemba, ukitaka kufupisha muda wa maji kuganda na kuwa barafu, tumia maji ya moto badala ya maji ya joto la kawaida.

Hilo ndilo chimbuko la "Mpemba Effect" ambalo limeandikwa katika moja ya blogu maarufu kimataifa, Food Mic, "Specifically the Mpemba Effect, which explains why hot water freezers more quickly than cold water. If you want to know what happens to cause hot water to freeze faster, head here. " na Lifehacker, "This phenomenon, called the Mpemba effect, may seem backwards, but actually works reliably well. You’ll get frozen ice cubes significantly faster by starting with hot water than cold. One explanation has to do with the molecular forces that occur between the oxygen and hydrogen atoms within an individual water molecule"

Deal! 6-pack EnacFire Powerline Micro USB cable, high speed sync, quick charging for only $7 (reg. $39)

$29 (reg. 89) Waterproof, 12 Hour Playtime - Omaker M4 Portable Bluetooth Speaker

Njau: Mfumo wa usimamizi wa mabasi ya haraka Dar uwe kigezo kwa daladala

Nimefurahishwa sana mfumo wa usimamizi wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es salaam ambao unajali muda wa abiria kuwahi kwenda na kurudi katika shughuli za kiuchumi na kijamii pia.

Mfumo huu unawezekana kwa mabasi daladala katika ruti zote Jijini kuachana na ule mtindo wa kulala vituoni kusubiri abiria huku wakiwachelewesha abiria ambao wameshapanda kwenye mabasi husika.

Sumatra kwa kushirikiana na wamiliki wa daladala,mamlaka za Manispaa,Jiji na kikosi cha usalama barabarani wakutane kwenye meza ya mviringo kwa ajli kubuni mfumo wa usimamizi na uendeshaji wenye tija kwa wadau na Taifa kwa ujumla.

Inasikitisha sana hasa nyakati za asubuhi na jioni kuona abiria wamejaza kwenye vituo vya mabasi wakiwa na hawana mwelekeo lakini wakati huohuo mabasi ya daladala yapo kwenye vituo vikuu vya mwanzo au mwisho wa ruti wakipiga na debe na kupakia abiria kwa kufuata foleni na kugoma kuondoka hadi abiria wajazane na kwenye viti na kusimama.

---
Ray Njau

Maazimio ya KUB: Kujalidi agenda 2: Kutokuwa na imani na NS, Tulia Ackson; Kutoka nje kila awapo

UPDATE: Mei 31, 2016


Wabunge wa vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk. TuliaAckson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

Hata hivyo Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani hawamwamini tena.

Wameeleza kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili.

Kutokana na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia.

Mbowe aliwaambia hayo wabunge wenzake mjini Dodoma kwenye kikao cha dharura alichoitisha na kushirikisha waandishi wa habari.

Alisema, Dk. Tulia ndio tatizo kuu la Bunge la Kumi na Moja na kwamba, kiongozi huyo wa Bunge kila anapokuwa kwenye kiti na kuongoza Bunge, mtafaruku hutokea.

“Nitapendekeza kuwa kila kikao cha Bunge kinachoongozwa na Tulia Ackson, sote tutoke nje ili kuonesha kwamba hatuna imani naye katika kuendesha shuguli za bunge,” Mbowe alisema jana.

Utekelezwaji wa kauli ya Mbowe umeanza leo ambapo sasa Dk. Tulia amebaki na wabunge wa CCM pekee.


Kutokana na kilichotokea Bungeni leo, Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Mb) amekutana na wanahabari kwa ajili ya kufikisha maazimio ya kambi hiyo kwa umma kuwa, watajadili agenda mbili, mosi ikiwa ni ya kutokuwa na imani na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bi Tulia Ackson na pili, kutoka nje ya ukumbi wa vikao vya Bunge kila Naibu Spika huyo awapo, ikiwa ni hatu ya kuonesha kutokukubaliana na namna Bunge hilo linavyondeshwa kwa kile walichokiita, kuogonzwa na mtu asiyefahamu au kwa kupokea maagizo kutoka kwingine.

Foleni ya ununuzi wa sukari kwa bei elekezi kwenye duka la Mohammed Enterprises Ltd Singida


Baadhi ya wafanyabishara na wakazi wa manispaa ya Singida, wakiwa kwenye foleni ya kununua sukari kwenye duka la jumla jumla na reja reja la kampuni ya Mohammed Enterprises ltd mjini Singida, kama walivyokutwa na mpiga picha wetu mapema leo asubuhi. Duka la hilo limekuwa kimbilio kwa sababu linauza sukari kwa bei elekezi ya serikali ya shilingi 54,000 kwa mfuko wa kilo 25.
Mmoja wa wafanyakazi wa duka la kampuni ya Mohammed Enterprises ltd la mjini Singida Salum Mwiru,akitoa mfuko wa sukari kwa mteja.
(Picha na Nathaniel Limu).

NW Masauni aagiza kuhamishwa kutoka Dar watumishi wanaotuhumiwa rushwa Uhamiaji

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameagiza yafanywe mabadiliko makubwa katika Kitengo cha Upelelezi kwa watendaji wa Mkoa wa Dar es salaam ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika Vitengo hivyo.

Masauni ametoa maagizo hayo leo wakati alipofanya kikao na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji ambapo pia kilihudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma.

Katika kikao hicho, Masauni ameagiza watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji Kitengo cha Upelelezi katika Mkoa wa Dae es salaam wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa wahamishwe na kupelekwa katika maeneo mengine nchini.

Aidha ameagiza pia kuwa kuanzia sasa watumishi waliohudumu katika idara hiyo kwa muda mrefu katika kituo kimoja wahamishiwe maeneo mengine ili kuboresha utendaji wa kazi wa idara hiyo.

Amesema hatua hii inayochukuliwa sasa ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yatakayofanywa katika Idara ya hiyo ili kuboresha huduma zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali.

"Katika kuisafisha Idara hii, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lakini lengo kubwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa" Alisema Masauni.

Amewataka Viongozi na watumishi wote wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wizara hiyo kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili ya kazi na waepuke vitendo vya kupokea rushwa na uzembe kazini.

Kuhusu Utaratibu wa Ajira za Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Masauni amesema kuwa Serikali inapitia upya utaratibu wa ajira katika Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama yaliyopo katika Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi ili kuhakikisha kuwa wanaojiriwa katika vyombo hivyo ni wale tu wenye sifa zinazostahiki

Pia ameagiza Idara ya Uhamiaji kuandaa Mpango mkakati ambao ni kabambe ili kuthibiti wimbi la wahamiaji haramu hapa nchini

Kuhusu matukio ya uhalifu yaliyojitokeza hivi karibuni amesema Jeshi la Polisi limechukua hatua za haraka ikiwemo uchunguzi wa matukio hayo ambapo tayari watumiwa kadhaa wamekwisha kukamatwa kuhusiana na matukio hayo

Uteuzi wa Rais Magufuli: Shabani Lila - Jaji wa Mahakama ya Rufani na Anne Makinda - Mwenyekiti NHIF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi.

Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro.Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

30 Mei, 2016

Kauli ya KUB na Wabunge waliotolewa nje wazungumzia wanavyuo 7802 waliotakiwa kuondoka vyuoni ndani ya saa 24

UPDATE: Imeongezwa video ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA) akizungumza.


Wabunge bila kujali itikadi zao za kivyama wanaonekana pichani leo Jumatatu, Mei 30, 2016 wakitoka nje ya kikao cha Bunge baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kukataa mjadala wa hoja ya dharura ya kuhusu wanafunzi wa Chuo cha Dodoma waliosimamishwa kwa maagizo ya serikali kupitia Wizara ya Elimu.
 

 Waziri husika, Prof. Ndalichako akizungumzia suala la kusimamishwa masomo na kurejeshwa nyumbani wafunzi wa vyuo mkoani Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa
kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma.

Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa Bunge leo mjini Dodoma.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Barbro Johansson iliyoko jijini Dar es salaam wakiondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara yake Bungeni mjini Dodoma.

Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatia Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson kutangaza kuliahirisha Bunge leo mjini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba nje ukumbi wa Bunge.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akizungumza jambo na wabunge leo mjini Dodoma.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Mbunge wa Kigoma Mhe. Peter Selukamba akijadiliana jambo na Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Hussein Bashe (kushoto)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu nje ya Ukumbi wa Bunge mjini.
Kikao cha 32 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asubuhi.

Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akimweleza jamboMwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum - DODOMA