Watu "waliojitambulisha ni askari" waua watu 8 Mikocheni, Tanga


Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje 2016

Taarifa ya uteuzi wa M/Kiti na Wajumbe wa Bodi za TANESCO, STAMICO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt. Alex L. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia tarehe 31/5/2016 hadi tarehe 30/5/2019;
 1. Dkt. Samwel Nyantahe
 2. Dkt. Lugano Wilson
 3. Bw. David Elias Alal
 4. Mhandisi Stephen Peter Mabada
 5. Mhandisi Leonard R. Masanja
Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuanzia tarehe 30/5/2016 hadi 29/5/2019wajumbe hao ni :
 1. Bw. Abdalah H. Musa
 2. Dkt. Coretha Komba
 3. Bw. Felix M. Maagi
 4. Dkt. Lightness Mnzava
 5. Bw. John B. Seka 
Uzinduzi wa Bodi hizo utafanyika Makao Makuu ya Mashiriki hayo Siku ya Alhamisi tarehe 2 Juni, 2016,saa 4:00 asubuhi kwa Bodi ya STAMICO na saa 8:00 mchana kwa Bodi ya TANESCO.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
31 MEI, 2016

Tanga: Ahukumiwa kwenda jela mwaka 1 kwa kuuza kitoweo cha nyama ya mbwa

Mtuhumiwa na kithibitisho
Kijana Mmoja aliyejulikana kwa jina la Zakaria Mswaki mkazi wa Mlalo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga amehukumiwa na mahakama ya mwanzo Mlalo Wilayani humo kifungo cha mwaka mmoja jela kwa tuhuma za kukutwa akiuza nyama ya mbwa.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni ambapo asilimia kubwa ya watu katika mji huo mdogo uliopo katika Wilaya hiyo walinunua nyama hiyo na kula bila kujua ambapo mshtakiwa alikiri shitaka hilo mbele ya mahakama hiyo.

Mshtakiwa huyo alidai chanzo cha kujihusisha na biashara hiyo haramu ni kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili kwa kipindi kirefu sasa hali iliyompelekea kujiingiza katika biashara hiyo.

Mshtakiwa huyo alikiri shitaka hilo mbele ya mahakama na kudai ugumu wa maisha ndio chanzo cha yeye kufanya biashara hiyo.

Sambamba na hayo Mshtakiwa huyo alipelekwa gerezani Wilayani humo kwa ajili ya kutumikia adhabu yake huku akiwaacha wananchi wa mji huo na butwaa na hasira kwa kulishwa nyama ya mbwa.

Orodha ya nyongeza ya majina ya waliochaguliwa kujiunga JKT 2016


NYONGEZA YA MAJINA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2016.

VIJANA WAFUATAO WAMEONGEZWA KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KATIKA MAKAMBI MBALIMBALI KAMA INAVYOONEKANA HAPO CHINI.

PIA BAADHI YA VIJANA WAMEHAMISHWA MAKAMBI KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI

WARIPOTI KWENYE MAKAMBI KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI KABLA YA TAREHE 05 JUNI 2016.

S/NOJINASHULEKIKOSI
1ABDILLAH RAMADHANI HAJILILIAN KIBOMGAMBO JKT
2ABDUL M. MTEKETABENJAMIN WILLIAM MKAPAMGAMBO JKT
3ABDULAZIZ SALUM AHMADPIUS SEC.SCHOOLMARAMBA JKT
4AGNES PETER MAGANGAFLORIAN SECRUVU JKT
5AGNESS EMMANUEL KITANDUST. MARY GORETIRUVU JKT
6AGNESS PETER MAGANGAMARAMBA JKT
7AJUAE DAVIS AMINIELIKANEMBWA JKT
8ALEX MLOSOBINZA HIGH SCHOOLMARAMBA JKT
9ALFRED AIDAN MBANOKIGONSELA HIGH SCHOOLRUVU JKT
10ALLY KAFERA ALLYMBEZI BEACH SEC.KANEMBWA JKT
11ALVIN ISMAEL MAKUNDIST JOSEPH CATHEDRAL HIGH SCHOOLRUVU JKT
12AMBWENE FRANK MWAKANEMAUWEMBA SECMARAMBA JKT
13AMOS ASEGENSUMBARUVU JKT
14AMOS KINGUOLD MOSHI SECMARAMBA JKT
15ANNA JORAM TIMBAROSMIN SEC.SCHOOLRUVU JKT
16ANNA M. JANUARYCHIEF IHUNYO SEC SCHOOLMSANGE JKT
17ANTIA PANCRAS KAKWERAKIFUNGIRO HIGH SCHOOLRUVU JKT
18AVITUS MUSHABIBAGAMOYO SEC.RUVU JKT
19BEATRICE BONFACEMAZINDE JUUMARAMBA JKT
20BEAUTNESS JOHN NJAUASHIRA SEC.RUVU JKT
21BENJAMIN STEPHEN NYANDAMWENGE HIGH SCHOOLRUVU JKT
22BERNADINAH T. MAYOMBYABAOBAB SEC. SCHOOLRUVU JKT
23BIBIANA CLETUS NJOKHADODOMA SEC. SCHOOLRUVU JKT
24BONIFACE DEOGRATIUSKWIRO SEC SCHOOLRUVU JKT
25BONIFACE JOHNNDANDA SECONDARY SCHOOLRUVU JKT
26BRENDA JOHN BABUVISITATION BETHEL GIRLSMARAMBA JKT
27BUNURI JUMAST. MARY GORETIRUVU JKT
28CALISTER MKOLORUVU GIRLS HIGH SCHOOLRUVU JKT
29CAROLINE HENRY KABOGOMARAMBA JKT
30CAROLINE SOSTHENES MAHERIJITEGEMEERUVU JKT
31CECILIA MPEMBABAOBAB SEC. SCHOOLRUVU JKT
32CLEMENCE GWINOOVERLAND HIGH SCHOOLRUVU JKT
33COSTANTINE PETERNSUMBA SECRUVU JKT
34DANIEL BENEDICT MASHIKUMAKIBA SECONDARYMAKUTOPORA JKT
35DAVID L. MARIBARUNZEWE HIGH SCHOOLRUVU JKT
36DAVID R. MKUMBOWAJA BOYS SEC.RUVU JKT
37DENIS G SADALATOSA MAGANGAMARAMBA JKT
38DEOUS SILIVESTA LUBINGABAGAMOYO SEC.RUVU JKT
39DIALO MNYUKINDANDA SECONDARY SCHOOLMAFINGA JKT
40DICKSON JOCTAN MATOGOALPHA SECONDARYMARAMBA JKT
41DONAT ERENEST MAJALAILIBORU SEC SCHOOLMAKUTOPORA JKT
42DONATH ERNEST MAJALAELBORU SEC.MAKUTOPORA JKT
43DORCUS DEOGRATIUSJANGWANIRUVU JKT
44EDDAH SAUL ASWILETUSIIME HIGH.RUVU JKT
45EDWARD MMBARA MKIZUPIUS SEC.SCHOOLMARAMBA JKT
46ELAIN DIDAS MUTABINGWATUSIIME SEC.RUVU JKT
47ELIAN E. NGONDOJITEGEMEE HIGHRUVU JKT
48ELINAZI YOAZ MSUYAKALIUA SECONDARYRUVU JKT
49ELIZABETH DANIEL KIYABOMASWA GIRLS SECONDARYMGAMBO JKT
50ELIZABETH MWAKITEGABWAWANI HIGH SCHOOLRUVU JKT
51ELVIS MAHENGE SIMONSWILA SEC.RUVU JKT
52EMMA A. KILONZOBAOBAB SEC. SCHOOLRUVU JKT
53EMMANUEL PHILIPOMASECHU SEC.MGAMBO JKT
54EVELYNE SCARIONJANGWANI SEC. SCHOOLRUVU JKT
55EZEKIEL KWAKA MSESEBWIRU SEC.RUVU JKT
56FABE MAGNUS NGONYANIMAKUTOPORA JKT
57FANUEL VICTOR KISIRIMINAKI SEC. SCHOOLRUVU JKT
58FELICIAN PASCHAL ULAYARUVU JKT
59FESTO MWAKAYOLOYOLA HIGH SCHOOLRUVU JKT
60FRANCES MASHAKA LUJAJICONSOLATHA SEM.RUVU JKT
61FRODIANUS FIDERIKARATU SECONDARY SCHOOLRUVU JKT
62GABRIEL PATRICK LWESYATUSIIME SEC.MLALE JKT
63GAUDENSIA MOHAMED MWALUNGWELUGOBA SEC.MAKUTOPORA JKT
64GEORGE STANSLAUS SHAYOST. MATHEW SECONDARYRUVU JKT
65GEORGIA ISHENGOMAMBEYA DAY SEC.RUVU JKT
66GERVAS PASCHAL KIHANGATUSIIME SEC SCHOOLRUVU JKT
67GETRUDE J. MASIMBANIOVERLAND HIGH SCHOOLRUVU JKT
68GIFTI A. LUGOMEKIBITI SECONDARYMARAMBA JKT
69GLORIA ALBERT MARINGOST.CHRISTINARUVU JKT
70GODFREY CHRISTIAN ROEBERTST GASPER MSOLWARUVU JKT
71GOODLUCK JOHN WILLSONJITEGEMEEMGAMBO JKT
72GREEN EUSTADKIRAENI GIRLSRUVU JKT
73GROLIA GODWIN KAHWAMKOLANI SECONDARY SCHOOLMAFINGA JKT
74HAJI SHEMHILUUWATA SEC.RUVU JKT
75HAPPINESS MGURUIFAKARA SEC.RUVU JKT
76HARRISON DAVID MRANGOALPHA SECONDARYRUVU JKT
77HASSAN RAJABU NJAULYAMUNGO SEC. SCHOOLRUVU JKT
78HAWA ISSA MDENG'OPIUS SEC.SCHOOLMARAMBA JKT
79HAWA ISSA MDENG'OPIUS SECONDARY SCHOOLMARAMBA JKT
80HERI MOHAMED MKUMBEGETUSIIME SEC.SCHOOLRUVU JKT
81HERIETH MAHENGEST. CHRISTINA SEC. SCHOOLRUVU JKT
82HINDU HAMIS MRISHOBAOBAB SEC.RUVU JKT
83IBRAHIM ABDALLAHPUGU SECRUVU JKT
84IELEEN DIDAS MUTABINGWATUSIIME SEC.RUVU JKT
85IMELDA IGNAS MBUNDAJANGWANI SEC. SCHOOLMAKUTOPORA JKT
86INZARI CHARLES LUGUTUBENJAMIN WILLIAM MKAPA HIGH SCHOOLBULOMBORA JKT
87IRENE KYENKUNGUROLETO GIRLSRUVU JKT
88JACKLINE ADAM LEYNAKOROGWE GIRLSMGAMBO JKT
89JACKLINE HERBET STEWARTHUWEMBA SECMARAMBA JKT
90JACKSON LUPAKISYO MWAIPUNGUTUSIIME SEC.RUVU JKT
91JAFARI S. JAFARIVUDOI HIGH SCHOOLRUVU JKT
92JANE MGINJA MTIMBAIKUNGI HIGH SCHOOLRUVU JKT
93JANETH FORTUNATUS WAMBURALOLEZA HIGH SCHOOLRUVU JKT
94JANETH V. KILONZOBAOBAB SEC. SCHOOLRUVU JKT
95JAPHET MASOTAUWEMBA SECMARAMBA JKT
96JASMIN MARTINKIBASILA SEC. SCHOOLRUVU JKT
97JASMIN MARTIN SHAYOKIBASILA SECMARAMBA JKT
98JASMINE RASULITENDE GIRLS HIGHRUVU JKT
99JASON STEVENMINAKI SECRUVU JKT
100JIDIRU IZADINI KALOKOLATARIME SEC.RUVU JKT
101JOHANITHA JOHNNATTA GIRLS SCHOOLMAFINGA JKT
102JOHNSON JONATHAN JOHNKIBITI HIGHRUVU JKT
103JORAM MBOMA JONATHANMAGUFURI HIGHRUVU JKT
104JOSEPH E. JOHNSONLYAMUNGO SECONDARY SCHOOLMARAMBA JKT
105JOSEPH REGNALD TUNGALAZAJITEGEMEE SEC. SCHOOLRUVU JKT
106JOSEPH TARIMOMAJENGO HIGH SCHOOLRUVU JKT
107JOSEPHINE BONIFACE MHANDOTUSIIME HIGH SCHOOLRUVU JKT
108JUENI MALIJANIKIGONSELA HIGH SCHOOLRUVU JKT
109JUSTINE REGNALD MAKENESTAR HIGH SCHOOLRUVU JKT
110KELVIN GEDION LEMNGEMWIKA SECONDARYMARAMBA JKT
111KHADIJA E. KALONGATUSIIME SEC.RUVU JKT
112KIBIBI HASAN JAMBIAMBEZI BEACHMARAMBA JKT
113LAULENCIA ENGITRAUDAUWEMBE SECONDARY842KJ
114LEAH THOMAS MTWEVETINDE GIRLSRUVU JKT
115LILAN HENRY CASTORYIRINGA GIRLS SEC. SCHOOLMAKUTOPORA JKT
116LILIAN KANG'WA MASANJAST CHRISTINA HIGH SHOOLRUVU JKT
117LUCIA JORAM TIMBAWERUWERU SEC. SCHOOLRUVU JKT
118LUGENDO LUCAS CHAPUGAJITEGEMEE SEC. SECONDARYRUVU JKT
119MARIAM M. JUMAMASWA GIRLS HIGH SECONDARY SCHOOLRUVU JKT
120MARIAM WAMBURACHIEF IHUNYO SEC SCHOOLMSANGE JKT
121MARIAMU S LIPENDEMTWARA TECHMAKUTOPORA JKT
122MARKO MICHAEL KASONIST. ANTHONYRUVU JKT
123MARTIN EWALD MALYAWEREKISARIKA HIGH SCHOOLRUVU JKT
124MARTINA GEORGE MWAILUSIZANAKI HIGH SCHOOLRUVU JKT
125MARY ANTHONY MASSAWEJITEGEMEE SEC. SECONDARYRUVU JKT
126MARY I MREMADAKAWA HIGH SCHOOLMAKUTOPORA JKT
127MASTERBETTER JOHNRUVU GIRLS HIGH SCHOOLRUVU JKT
128MATHIAS BAHATI ORESTIST. MATHEWMAKUTOPORA JKT
129MESHACK MARTIN LYIMUPIUS SEC.SCHOOLMARAMBA JKT
130MESHACK MARTIN LYIMUPIUS SECONDARY SCHOOLRUVU JKT
131MICHAEL DEOGRATIUS NJAULWANDAI HIGH SCHOOLMGAMBO JKT
132MIRIAM M. JUMAMASWA GIRLS SECONDARY SCHOOLRUVU JKT
133MUSSA KALUME AGUSTINEGEITA SEC.RWAMKOMA JKT
134MUSSA S. MAIGESHINYANGA SEC SCHOOLRUVU JKT
135MWAMINI KADUMATAMBAZARUVU JKT
136NAISHOOKI WILBERT OLE-MBILELOYOLA HIGH SCHOOLRUVU JKT
137NAOMI ENMANUEL LEKASHINGOST.MARY GORETI SECONDARY SCHOOLMARAMBA JKT
138NASRA NURDIN YUSSUPHBABRO JOHNOSONRUVU JKT
139NEEMA JAMES MANYAMABAOBAB SEC.RUVU JKT
140NEEMA MAIKO MASAGASICORNERSTONE SEC.RUVU JKT
141NEEMA MSUYAJITEGEMEE HIGH SECONDARYRUVU JKT
142NESTARY AGATHON NDUNGURUMAKITA SEC.MAFINGA JKT
143NESTARY AGATON NDUNGURUMKITA SEC.SCHOOLMAFINGA JKT
144NICODEMO JACOBMUSOMA SECRUVU JKT
145NOEL JAMES MWAKISOMBEMINAKI HIGH SCHOOLRUVU JKT
146NORBERT NOELGALONOS SECONDARY SCHOOLKANEMBWA JKT
147NUSRAT ZAKARIAOVERLAND HIGH SCHOOLRUVU JKT
148OCTAVIAN BUBERWAKILOSA SECONDARY SCHOOLRUVU JKT
149OMARI DIWANI OMARIKISIMIRI HIGH SCHOOLRUVU JKT
150OMARY MAKOTA ALLYMBEZI BEACH SEC.KANEMBWA JKT
151PAUL KATUNZILYAMUNGO SECONDARY SCHOOLMSANGE JKT
152PRISCILA WENDE MGANACANONNOSA HIGH SCHOOLMAKUTOPORA JKT
153PROJESTUS H.CHAMAHANGAUSAGARA SECRUVU JKT
154RACHEL DAVID ISSAMECANNASSA HIGH SCHOOLRUVU JKT
155RACHEL DAVID ISSAMECANNOSA HIGH SCHOOLRUVU JKT
156RACHEL RAYMOS FOYAMSUFINI HIGH SCHOOLRUVU JKT
157RAHEL FESTUS ISOKOZAVWAWA SEC.SCHOOLRUVU JKT
158RAMADHANI ALLY NJERANYARUBANDA SECRUVU JKT
159RAMADHANI MBWAMBOSAME HIGH SCHOOLMARAMBA JKT
160RAMADHANI RAJABU RAMADHANIBAGAMOYO HIGH SCHOOLRUVU JKT
161RAMADHANI RAJABU RAMADHANIBAGAMOYO HIGH SCHOOLRUVU JKT
162RECHO DANIEL MWALIMUINABOISHU HIGH SCHOOLMAKUTOPORA JKT
163REHEMA DEUS RUBALEJITEGEMEE SECONDARYRUVU JKT
164REHEMA SHAWARI IKAJICANNOSA HIGH SCHOOLMARAMBA JKT
165REMIDIUS REYMOND MUTATUSIIME SEC SCHOOLRUVU JKT
166RETISIA SAANANEST.JOSEPH SEMINARY SECRUVU JKT
167RIDHIWANI SHABANI MAKUMBIMWINYI HIGH SECMGAMBO JKT
168RISHAD KIHOMO MLELWABAOBAB SEC. SCHOOLRUVU JKT
169ROGERS JOHN EZEKIELIGUNGA HIGH SCHOOLRUVU JKT
170ROMAN CASTORYKILOSA HIGH SCHOOLRUVU JKT
171ROSEMARY T. MASIAGACHIEF IHUNYO SEC SCHOOLMSANGE JKT
172SADICK HASHIM MWAISAKALYAMUNGO SEC. SCHOOLRUVU JKT
173SAIMON P. SOZIGWAENABOISHU SECONDARYMARAMBA JKT
174SALA A. MWAKAJWANGAMILUNDIKWA SEC SCHOOLRUVU JKT
175SALEHE MACHIBYA JONIORST.METHEWMGAMBO JKT
176SALMIN AMRIKIGONSERA SECONDARYMARAMBA JKT
177SALOME AMOSOVERLAND HIGH SCHOOLRUVU JKT
178SALOME SHITUNGURUST.JOSEPH SEMINARY SECRUVU JKT
179SHUKRANI MWAIPWISISONGES SECONDARY SCHOOLMAFINGA JKT
180SIMON P. SOZIGWAENABOISHU SECRUVU JKT
181SOLINA SABASRUVU HIGH SCHOOLRUVU JKT
182SOPHIA DEUS RUBALERUVU SECONDARYRUVU JKT
183SOPHIA S. MATHIASMAWENZI SEC.MARAMBA JKT
184STEPHEN F. NDALUSELUGUFU BOYS SEC.SCHOOLRUVU JKT
185STIVEN NDALUSOLUGUFU HIGH SCHOOLRUVU JKT
186SUSAN PATRICK MNASIZUALLIANCE GIRLSRUVU JKT
187SWEED IDDALFA HIGH SCHOOLRUVU JKT
188TATU HAMAD HATIBUMOROGORO SECRUVU JKT
189TATU JUMA MYOVELAMANYUNYU GIRLSMARAMBA JKT
190TOMESTECLES H.CHAMAHANGAKIGONSELA SECRUVU JKT
191TUMAINI JOHN MAKUNENGEKAWAWA SECONDARYBULOMBORA JKT
192TUMPALE JAPHETOVERLAND HIGH SCHOOLRUVU JKT
193VAILET GEORGE SIMBAKIBONDO GIRLS HIGHRUVU JKT
194VALERIAN VEREMUND CHARLEKOROGWE GIRLSMAFINGA JKT
195VERONICA CASMIR NDAMBARIKARUVU GIRLSMAKUTOPORA JKT
196VERUS THOBIAS KASONSOST. ANNE MARIERUVU JKT
197VERUS TOBIAS KASONSOST ANNE MAKIE DSMRUVU JKT
198VICTOR DAUDI ANYASIMEMARIAN BOYSRUVU JKT
199VICTOR L. AMBELEMBALIZI SEC.RUVU JKT
200VICTORY HENRYMARIAN BOYS SCHOOLRUVU JKT
201WALTER FRUGENCE SAMKYOVERLAND HIGH SCHOOLRUVU JKT
202WILLIAM OSIAS MWANYIKATUSIIME SEC SCHOOLRUVU JKT
203WILLIAM PATRICK ASSEYBENDEL MEMORIAL ACADEMYMGAMBO JKT
204YASSER HAMAD MALESAJITEGEMEE HIGH SECMARAMBA JKT
205ZAMDA MWALIMUKOROGWE GIRLSMAKUTOPORA JKT

Tangazo la mabadiliko ya tarehe ya kuripoti kwenye makambi ya JKT 2016


TANGAZO


MABADILIKO YA TAREHE YA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2016.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia umma mabadiliko ya tarehe ya kuripoti makambini vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2016 na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2016.

Taarifa ya awali kwa vyombo vya habari nchini ilianisha tarehe ya kuripoti kuwa ni tarehe 01 June hadi tarehe 05 Juni 2016. Tarehe hiyo imeafanyiwa mabadiliko badala yake vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 07 June hadi tarehe 10 June 2016 bila kukosa.

Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwezie.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 31 Mei 2016

Kiwanda cha Wachinda Dodoma chafungwa kwa kuchinja na kusindika nyama ya punda

Baraza la Taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC) limekifungia kiwanda cha Huwa Cheng Company Limited kilichopo mjini Dodoma na kukitoza faini ya shilingi milioni 200 baada ya kubaini kiwanda hicho kinajihusisha na usindikaji wa nyama ya punda, jambo ambalo ni kinyume na utamaduni wa watanzania huku mazingira ya shughuli hiyo yakiwa hatarishi kutokana na uchafu unaozalishwa kuzagaa kwenye makazi ya watu.

Mabishano makali yalizuka baina ya wamiliki wa kiwanda husika ambao ni raia wa China na maofisa wa NEMC, yaliyochukua muda mrefu, kabla ya maofisa hao kutoa tamko la kufungwa kwa kiwanda hicho.

Kiwanda hicho ambacho kwa siku kinadaiwa kuchinja punda wasiopungua 200, inaelezwa kuwa kinaharibu kizazi cha wanyama hao ambao uzao wake unatajwa kuwa ni mdogo hali inayotishia idadi ya wanyama hao ambao kwa Kanda ya Kati hutumiwa katika kazi mbalimbali.

Mohamed Hamis ambaye ni meneja msaidizi wa kiwanda hiki ambaye amezungumza kwa niaba ya raia hao wa Uchina, anasema nyama hizo za punda zinasafirishwa kwenda kuuzwa nchini China.

Wakazi wa mji wa Dodoma wanatupa lawama kwa mamlaka za mkoa kutobaini kiwanda hicho na kukichukulia hatua huku kukiwa na taarifa ya nyama hizo kuzagaa na kuuzwa katika maeneo mbalimbali ya mji huo hasa kwenye mabaa na migahawa ya vyakula. [via GSengo blog]

Tahadhari kutoka Bagamoyo kwa wanaokwenda kununua maeneo ya ardhi

TAHADHARI KUTOKA BAGAMOYO

Ukija Bagamoyo kununua kiwanja au shamba, usikumbuke kuja na hela yako peke yake, bali pia kumbuka kuja na AKILI ZAKO! Bila hivyo UTABAMBIKIWA HIVI:-
 1. SHAMBA AU KIWANJA FEKI.
 2. MWENYEKITI wa Kijiji FEKI.
 3. AFISA MTENDAJI wa Kijiji FEKI.
 4. MUUZAJI wa Kiwanja/Shamba FEKI.
 5. SHAHIDI FEKI.
 6. JIRANI anayejifanya ndio anapakana na kiwanja au shamba unalouziwa, FEKI.
 7. WATOTO FEKI - wataitwa kuchezacheza ili muuzaji aonekane ana familia na si mhuni.
 8. MKE wa muuzaji, kwamba ataitwa kukusalimia - FEKI
 9. NYARAKA FEKI 
 10. MIHURI FEKI
 11. OFISI ya Kijiji FEKI - bendera ya taifa itawekwa nje ya ofisi kama boshen.
 12. Siku ukigundua umeuziwa kiwanja cha mtu au shamba lililoko katika mradi wa EPZA, hao wahusika wote huwaoni na ndipo utagundua kuwa hata namba zao za simu ni FEKI.
Kuweni makini, kwani ukishapigwa hela zako za mkopo wa BAYPORT/CRDB/AMANA BANK/ACCESS BANK, PSPF, LAPF, PPF na nani mwingine sijui, fahamu kuwa vitisho vya Polisi au kuwaroga, havitasaidia. Hawa jamaa kwa jinsi walivyo smart,hutawapata kwa polisi na wala hawarogeki. 

USIJE UKASEMA ULIKUWA HUJUI! NIMEKUKANYA.

TAHADHARI KABLA YA HATARI.

-------
via WhatsApp

Kauli hizi za Mbunge Keissy ndiyo zitadumisha Muungano?


Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 31, 2016[audio] Dada wa marehemu Anathe na Erasto Msuya asimulia masaibu

Tafadhali bofya kitufe cha pleya iliyopachikwa hapo chini kusikiliza alivyozungumza na Gea Habib wa kipindi cha "Heka Heka" cha radio Clouds FM.

Watanzania 408 wanatumikia vifungo nchi za nje kwa kusafirisha dawa za kulevya

Watanzania 408 wanatumikia vifungo nje ya nchi na wengine kukabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kusafirisha dawa za kulevya.

Taarifa hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Akizungumzia Watanzania waliokamatwa kwa dawa hizo Mahiga amesema wanakabiliwa na adhabu hizo katika magereza mbalimbali duniani baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na biashara haramu.

Mahinga alitaja idadi yao na nchi ambazo wanashikiliwa kuwa ni Brazil (41), China (266), Iran (68), India (9), Nepal (4), Oman(3), Thailand (14) na Umoja wa Falme za Kiarabu (3). [MWANANCHI]

Mtalaka wa Anathe yaelezwa alienda kwa marehemu kwa pikipiki siku ya tukio

SIKU chache baada ya dada wa bilionea Erasto Msuya kuuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada Kigamboni, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema linamshikilia mume wa marehemu kwa tuhuma za kuhusika na kifo hicho.

Mbali na hilo, pia jeshi hilo linamsaka mfanyakazi wa ndani wa marehemu Anathe Msuya ambaye anadaiwa kuondoka siku moja kabla ya kutokea kwa mauji hayo ya kinyama.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema wamelazimika kuunda jopo linaloshirikisha vigogo watano wa jeshi hilo ambao ni wataalamu wa upelelezi ili kubaini kwa undani mauaji hayo ya kutisha.

Pamoja na hali hiyo, imebainika katika uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi, mume wa marehemu Anethe anahusishwa na mauaji hayo ambapo inadaiwa kuwa alikwenda nyumbani kwa marehemu akiwa na pikipiki siku ya tukio hilo.

“Mtuhumiwa huyo tunaendelea kumshikilia kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili tuweze kubaini mtandao mzima uliohusika katika tukio hilo.

“Niwahakikishie kwamba watu waliotekeleza mauaji hayo tutawakamata tu, na watakuwa mfano kwa wengine, kama mtu amegombana na mwenzake hakuna haja ya kumuua, wanawake na wanaume wamejaa kibao unaweza ukatafuta mwingine ukaoa au ukaolewa na si kufanya mauaji ya kinyama kiasi hicho,” alisema Kamanda Sirro.

Kutokana na hali hiyo kamanda huyo wa polisi aliwataka wananchi kuwa na subira ili kuwapa nafasi ya kufuatilia tukio zima.

Kifo cha Anethe kilitokea Mei 26 mwaka huu katika eneo la Kibada blok 16 Kigamboni akidaiwa kuchinjwa na watu wasiofahamika.

Taarifa za ndani ambazo gazeti hili lilizipata toka Mbezi Makonde uliko msiba wa Anethe, zinaeleza kuwa matukio yanayofanana na hayo yamekuwa yakiiandama familia hiyo tangu kaka yao Erasto auawe mwaka 2013.

Mmoja wa wanafamilia hiyo alisema baada ya Erasto kupigwa risasi, dada yao aliyetajwa kwa jina la Antuja naye alimwagiwa kitu kinachohisiwa kuwa ni sumu wakati akiwa amelala chumbani na hivyo kumuathiri.

Wakati akimwagiwa sumu hiyo, inaelezwa kuwa Antuja ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo, alikuwa amelala pamoja na mtoto wa marehemu Anethe aitwae Allan.

Tukio jingine ni lile lililotokea Desemba mwaka jana ambapo dada yake aitwae Ester na muwewe walipigwa risasi za mgongoni na kifuani wakiwa katika baa ya Hongera iliyopo Bamaga Sinza, Dar es Salaam.

Kutokana na matukio hayo kuiandama familia yao, baadhi ya ndugu wamesema yanatokana na visasi ambavyo wanasema kuisha kwake kutatokana na Rais John Magufuli kuingilia kati.

Kuhusu maisha ya kimapenzi ya marehemu Anethe, ndugu huyo alisema hayakuwa mazuri.

Alisema Anethe aliolewa na kwa bahati mbaya ndoa yake ilikaa mwaka mmoja ikaingia migogoro na hivyo kuachana na baba watoto wake.

Majirani wa marehemu Anethe walikataa kuzungumza chochote juu ya tukio hilo wakisema hakuna wanalolifahamu zaidi ya kuona askari wakiwa na gari waliofika nyumbani hapo juzi na kisha kuuchukua mwili na kuondoka nao.

Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Anethe alikuwa mstari wa mbele katika kesi ya mauaji ya kaka yake bilionea Erasto Msuya ambayo inaendelea kusikilizwa hadi sasa Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Kaka yake huyo aliuawa kwa kumiminiwa risasi 22 Agosti 7, 2013 katika Uwanja wa ndege wa KIA na hadi sasa watu saba wanashikiliwa kwa kosa hilo.SIKU chache baada ya dada wa bilionea Erasto Msuya kuuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada Kigamboni, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema linamshikilia mume wa marehemu kwa tuhuma za kuhusika na kifo hicho.

Mbali na hilo, pia jeshi hilo linamsaka mfanyakazi wa ndani wa marehemu Anathe Msuya ambaye anadaiwa kuondoka siku moja kabla ya kutokea kwa mauji hayo ya kinyama.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema wamelazimika kuunda jopo linaloshirikisha vigogo watano wa jeshi hilo ambao ni wataalamu wa upelelezi ili kubaini kwa undani mauaji hayo ya kutisha.

Pamoja na hali hiyo, imebainika katika uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi, mume wa marehemu Anethe anahusishwa na mauaji hayo ambapo inadaiwa kuwa alikwenda nyumbani kwa marehemu akiwa na pikipiki siku ya tukio hilo.

“Mtuhumiwa huyo tunaendelea kumshikilia kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili tuweze kubaini mtandao mzima uliohusika katika tukio hilo.

“Niwahakikishie kwamba watu waliotekeleza mauaji hayo tutawakamata tu, na watakuwa mfano kwa wengine, kama mtu amegombana na mwenzake hakuna haja ya kumuua, wanawake na wanaume wamejaa kibao unaweza ukatafuta mwingine ukaoa au ukaolewa na si kufanya mauaji ya kinyama kiasi hicho,” alisema Kamanda Sirro.

Kutokana na hali hiyo kamanda huyo wa polisi aliwataka wananchi kuwa na subira ili kuwapa nafasi ya kufuatilia tukio zima.

Kifo cha Anethe kilitokea Mei 26 mwaka huu katika eneo la Kibada blok 16 Kigamboni akidaiwa kuchinjwa na watu wasiofahamika.

Taarifa za ndani ambazo gazeti hili lilizipata toka Mbezi Makonde uliko msiba wa Anethe, zinaeleza kuwa matukio yanayofanana na hayo yamekuwa yakiiandama familia hiyo tangu kaka yao Erasto auawe mwaka 2013.

Mmoja wa wanafamilia hiyo alisema baada ya Erasto kupigwa risasi, dada yao aliyetajwa kwa jina la Antuja naye alimwagiwa kitu kinachohisiwa kuwa ni sumu wakati akiwa amelala chumbani na hivyo kumuathiri.

Wakati akimwagiwa sumu hiyo, inaelezwa kuwa Antuja ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo, alikuwa amelala pamoja na mtoto wa marehemu Anethe aitwae Allan.

Tukio jingine ni lile lililotokea Desemba mwaka jana ambapo dada yake aitwae Ester na muwewe walipigwa risasi za mgongoni na kifuani wakiwa katika baa ya Hongera iliyopo Bamaga Sinza, Dar es Salaam.

Kutokana na matukio hayo kuiandama familia yao, baadhi ya ndugu wamesema yanatokana na visasi ambavyo wanasema kuisha kwake kutatokana na Rais John Magufuli kuingilia kati.

Kuhusu maisha ya kimapenzi ya marehemu Anethe, ndugu huyo alisema hayakuwa mazuri.

Alisema Anethe aliolewa na kwa bahati mbaya ndoa yake ilikaa mwaka mmoja ikaingia migogoro na hivyo kuachana na baba watoto wake.

Majirani wa marehemu Anethe walikataa kuzungumza chochote juu ya tukio hilo wakisema hakuna wanalolifahamu zaidi ya kuona askari wakiwa na gari waliofika nyumbani hapo juzi na kisha kuuchukua mwili na kuondoka nao.

Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Anethe alikuwa mstari wa mbele katika kesi ya mauaji ya kaka yake bilionea Erasto Msuya ambayo inaendelea kusikilizwa hadi sasa Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Kaka yake huyo aliuawa kwa kumiminiwa risasi 22 Agosti 7, 2013 katika Uwanja wa ndege wa KIA na hadi sasa watu saba wanashikiliwa kwa kosa hilo.

Uongozi UDom walaumiwa

LAANA zimeanza kumiminwa kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDom) hususan walisosababisha kusimamishwa masomo kwa wanafunzi 7802, anaandika Dany Tibason.

Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imetoa tamko la kulaani kitendo cha cha wanafunzi hao wa programu maalumu ya ualimu wa msingi na sekondari, walio rudishwa nyumbani bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri wao na mazingira waliyokuwa wanaishi.

Tamko hilo limetolewa leo na Lameck Thomas, katibu wa jumuiya hiyo na kwamba, lawama zimekuwa zikitupwa kwa walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na upande mmoja ambao ni menejimenti ya chuo kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao.
“Kama jumuiya tumeona sio busara kukaa kimya bila kuelezea suala hili kwa usahihi wake kwani ni kuifanya jamii kuamini katika maelezo yaliyo wasilishwa serikalini na upande wa menejimenti ya chuo…, siyo kweli kuwa waalimu tuligoma kufundisha program hii kama inavyoelezwa sehemu mbalimbali,” amesema Thomas.
Amesema kuwa, tatizo kubwa ni kutoelewana kati ya walimu na menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa program hiyo chuoni hapo.
“Matatizo haya yamelalamikiwa sana na walimu tangu kuanzishwa kwa program hii na kumekuwa hakuna dalili yoyote ya ufumbuzi huku wakiendelea kufundisha kwa uzalendo mkubwa” amesema.
Amesema kuwa, jumuiya ya wanataluma inapata hisia kuwa wizara imeamua kwa makusudi kushirikiana na uongozi wa UDOM kupotosha uhalisia wa jambo hilo kwani hakuna hata wakati mmoja ambapo wamefanya mawasilianao na walimu kupata taarifa kutoka upande wao.
“Katika kutafuta ufumbuzi wakati wa mgogoro, serikali kupitia Naibu Waziri wa Elimu ilifanya kikao na menejimenti ya chuo kwa kushirikiana na viongozi wa Udomasa Mei 19 chuoni hapo.
“Katika kikao hicho, wajumbe walikubaliana kwa pamoja kuundwa kwa kamati ndogo ya kufuatilia suala hili ikijumuisha wajumbe mchanganyiko toka menejimenti ya chuo na Udomasa ikiongozwa na mwenyekiti atakaye toka nje ya chuo ili kuifanya iwe huru zaidi,” amesema.
Ameongeza kuwa, chakushangaza zaidi kamati hiyo haikuwa huru kutokana na menejimenti ya UDOM kutupilia mbali mapendekezo ya jumuiya ya wanataaluma hasa katika majina ya wajumbe waliochaguliwa kuingia kwenye kamati hiyo.

Amesema kuwa, kamati hiyo ambayo haikushirikisha wajumbe walioteuliwa na wahadhiri ilitakiwa kumaliza muda wake tarehe 30 Mei na mpaka sasa jumuiya ya wanataaluma haina taarifa yoyote juu ya ufanyaji kazi wa kamati hiyo.
“Kama jumuiya pia tunasikitishwa na upotoshwaji makusudi wa taarifa unaofanywa na watu mbalimbali kwa kuwasukumia walimu lawama moja kwa moja bila kuwasiliana na walimu hata mara moja,” amesema.
Amesema kuwa, alichosema waziri tarehe 30 Mei ni taarifa ya upande mmoja ambayo haitasaidia katika utatuzi wa kudumu wa suala hilo kutokana na ukweli kuwa, walimu nao wana mambo mengi ya kuzungumza juu ya mgogoro huo ikiwemo madai yao.

Amesema kuwa, jumuiya hiyo haijawahi kuulizwa lolote juu ya uhaba wa walimu pamoja na kuwepo kwa taarifa za tatizo hilo katika chuo hicho.
“Mfano, mpaka sasa katika koleji ya Sayansi Asilia na Hesabu kuna upungufu wa walimu 128 waliokuwa wanahitajika kufundisha program hiyo kwa ufanisi
“…kwa muhula uliopita ni walimu 72 tu ndiyo walio beba mzingo wa upungufu huo na kwa muhula huu hali ilikuwa inaelekea kuwa mbaya sana,” amesema.
Amesema kuwa, wingi wa wanafunzi na uhaba wa walimu ulisababisha upangaji wa ratiba ya kufundisha kuwa ngumu kutokana na kozi kugawanya katika mikondo mingi ambayo walimu walilazimika kuifundisha huku wakiwa na majukumu ya kufundisha kozi za shahada na majukumu mengine.
“Changamoto hizi za ufundishaji imekuwa ngumu kwa menejimenti kuzifahamu kutokana na ukweli kwamba, wengi wao hawafundishi hivyo ni vigumu kupata maumivu yanayotokana na majukumu haya makubwa,” amesema.
Hata hivyo amesema kuwa, wanawakaribisha viongozi na wananchi mbalimbali kutembelea chuo chetu ili kujionea mazingira ya ufundishaji yalivyo na kuhakikisha wanayo yaeleza. [MwanaHALISI Online]

SISI ZA KUTIMULIWA WANAFUNZI UDOMSABABU za wanafunzi 7,800 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutimuliwa sasa zipo hadharani,ananadika Aisha Amran.

Ni kutokana na kuwepo kwa mgogoro kati ya chuo hicho na wafanyakazi wake ambao umekwenda moja kwa moja kuathiri wanafunzi hao.

Chama cha Taasisi za Elimu ya Juu, Tawi la UDOM (THTU) kimeeleza kuwa, mgongano uliopo kati ya viongozi wa chuo hicho na wafanyakazi wake.

Ni kutokana na walimu wanaofundisha wanachuo hao kutolipwa fedha zao na chuo jambo lililosababisha kuchelewa kuendelea na masomo na hata kuibua mgogoro huu.

Hivi karibuni UDOM kilitoa taarifa ya kusimamisha wanafunzi hao wa kozi maalumu ya ualimu wa Sayansi, Hisabati na Teknolojia kwa ngazi ya Stashahada na kisha kutaka waondoke chuoni hapo mara moja. Tangazo hilo lilieleza kuwa, kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejeshwa majumbani na kwamba wataelezwa mustakabali wao. Kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.

Taarifa ya THTU iliyosainiwa na Nashon Chache, mwenyekiti wake inaeleza kuwa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (DVC-ARC) ndio chanzo kutokana na kushindwa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinakwenda kama zilivyotarajiwa.

Pia mwingine anayetajwa kuwa sehemu ya tatizo hilo ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala (DVC-PFA).

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mgogoro huo unaweza kuwiana na ule uliotokea mwaka 20014/15 ambao ulisababishwa kuundwa kwa Kamati ya Uratibu (SC) na kwamba chama hicho kinaamini kuwa, kama ofisi ya DCV-PFA ingekuwa makini, mgogoro huo usingekuwepo.
“Badala ya kufanya kazi hii kwa ari, weledi na uaminifu kama ilivyostahili, viongozi hawa wawili wameamua kuwa waongo, wasiojali maslahi ya wanafunzi na umma na taasisi wanayoiongoza katika ujumla wake,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa, mgogoro huo ulianza wakati walimu walipotakiwa kulipwa kwa kufanya kazi ya ziada ya kuwafundishwa wanafunzi hao.

Na kwamba, kutokuwa tayari kwa viongozi hao kukaa meza moja na walimu waliokuwa wakifundisha wanafunzi hao, ndiko kulikozidisha tatizo zaidi.
“…badala yake wanamlazimisha mkuu wa chuo kutatua mgogoro bila kumpa nyenzo, bili maana yake ni kufanya mambo bora liende,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, kutokana na makubaliano ya mapendekezo ya kamati maalim ya uratibu, walimu hao wa ziada walitakiwa kulipwa Sh. 1,000,000 lakini haikutekelezwa.

Hivyo, mvutano wa malipo hayo ndio uliosababisha wanafunzi kuchelewa kuanza masomo yao ya muhula wa pili ambapo Makamu Mkuu wa chuo alipobaini hivyo, aliamuru malipo yafanyike ili wanafunzi waendelee na masomo.

Hata hivyo, baada ya agizo hilo, ofisi husika haikutekeleza agizo hilo jambo lililoibua matatizo mengine na hata hatua mgogoro huoo kufikia hapa. [MwanaHALISI Online]

Mgomo UDSM "kimeeleweka" cheki imetoka

Wanafunzi UDSM katika mgomo leo
Kwa mujibu wa gazeti la MwanaHALISI Online, leo Mei 31, 2016 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waligoma kusitisha mgomo wao mpaka pale pesa za kujikimu zitakapoingizwa kwenye akaunti zao.

Mgomo huo ulianzishwa baada ya kucheleweshwa fedha zao za kujikimu zinazotolewa kila baada ya siku 60.

Wanafunzi hao walikuwa wakidai fedha hizo baada ya kupita siku tano bila kupewa taarifa yoyote ikiwemo kwamba, serikali haina fedha.

Mgomo huo ulianza saa mbili asubuhi na kuendelea hadi mchana kwa ahadi ya kutokukoma kutokana na msimamo wa wanafunzi hao wa kutoacha kugoma mpaka watakapopatiwa haki yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Prof. Rwekaza Mkandara, Makamu Mkuu wa UDSM amesema kuwa, fedha hizo zingetolewa kabla ya kufuka Saa 12 jioni.

Awali msimo wa wasomi hao ulimtaka Paul Makonda (Mkuu wa Dar es Salaam), Ally Salum Hapi, (Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni) na Boniface Jacob (Meya wa Manispaa ya Kinondoni), kuzungumza nao.

Erasmi Leon, Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDSM na Mshangama Shamira, makamu wake wamesema kuwa, mgomo husika utaendelea mpaka pale watakapothibitisha kuwa, fedha zao zimeingia katika akaunti zao.

Wanafunzi walikusanyika katika eneo la Revolution Square lililopo chuoni hapo kwa amani huku wakiimba nyimbo mbalimbali za uzalendo.

“Kama sio juhudi zako Nyerere…, Sitasimama maovu yakitawala…., Vijana tusilale bado mapambano…. alisema Nyerere vijana wote tumelegea sharti tuanze mchakamchaka….” Wamesikika wakiimba.

Mpaka mchana unaisha, viongozi waliowahitaji kuzungumza nao hawakuwa wemefika kwenye eneo hilo.


 • UPDATE: wavuti. imepata picha kupitia WhatsApp kwa maeleo kuwa ni nakala ya idhini halisi ya malipo ya madai ya wanachuo hao, iliyotolewa leo.