Rais Magufuli ateua Mwenyekiti mpya wa Bodi TPDC

RAIS John Magufuli amemteua Profesa Sufian Bukurura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia Mei 30, mwaka huu.

Profesa Bukurura anachukua nafasi ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Michael Mwanda.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa kwa vyombo vya habari jana ilisema kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewateua wajumbe sita wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC kuanzia Juni 3, mwaka huu hadi Juni 2, 2019.

Aliwataja wajumbe hao kuwa Jaji Josephat Mackanja, Balozi Ben Moses, Profesa Abiud Kaswamila, Profesa Hussein Sosovele, Dk Shufaa Al-Beity na Mwanamani Kidaya.

Taarifa ya habari ChannelTEN Juni 4, 2016


Prof. Kitila Mkumbo azungumzia kizungumkuti cha wanafunzi UDom

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitilla Mkumbo amesema kuna mambo mawili yanayoibana Serikali katika mgogoro wa wanafunzi waliotimuliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDom).

Akizungumza jana kwenye kipindi cha ‘Kipima Joto’ kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV, Profesa Mkumbo alisema Serikali haiwezi kukwepa lawama, kwa sababu ndiyo iliyoanzisha utaratibu wa kudahili wanafunzi wa kidato cha nne kupitia mfumo maalumu kabla ya kuanza kusoma shahada ya chuo kikuu.

Pia, alisema Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), haiwezi kuhusika moja kwa moja kwenye udhaifu uliojitokeza katika udahili wa wanafunzi hao, bali Seneti ya Udom inapaswa kuwajibika katika hilo.

Alisema kuna udhaifu wa kiutendaji kwa seneti hiyo yenye mamlaka ya kudahili wanafunzi wenye sifa ambayo iliiacha kazi hiyo mikononi mwa TCU.

Mkumbo alisema kazi ya TCU ni kuidhinisha majina ya wanafunzi waliokwisha dahiliwa na chuo husika na si kuchagua.

“Chuo chochote ndicho kinachagua wanafunzi wenye sifa wanazozihitaji, inashangaza kuona Udom imefanyiwa kazi hiyo, baraza na seneti wanapaswa kuwajibika kwanza, TCU haiwezi kukichagulia chuo wanafunzi,” alisema Profesa Mkumbo.

Hata hivyo, alitoa angalizo kwa Serikali kutodharau mfumo huo wa udahili kwa wanafunzi ambao hawakuhitimu Kidato cha Sita kama ilivyoamriwa na Serikali ya Awamu ya Nne, kuwa upo na unatumika duniani kote.

“Ila kama Rais (John) Magufuli hautaki na ameona turudi kwenye mfumo wa zamani ambao mwanafunzi anapaswa kufaulu kidato cha sita ndiyo ajiunge na chuo kikuu sawa, lakini atambue kuwa kuna hasara na faida zake, vyuo vingi vinaweza kufungwa,” alisema Mkumbo

Mbali ya mfumo huo, profesa huyo alisema upo mfumo mwingine wa udahili kwa mtu yeyote mwenye umahili katika taaluma yake kusoma shahada kwa kuzingatia vigezo maalumu vilivyowekwa.

“Ila hakuna jinsi, nadhani TCU wamemsikia Rais kuwa hataki njia za mkato tena.”

Mei 29, UDom iliwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni mara moja.

Amri hiyo iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ilisema Serikali imeamua warejee kwao na wataelezwa mustakabali wao mapema iwezekanavyo.

Hata hivyo, Rais John Magufuli juzi alisema baadhi yao walikuwa vilaza, hivyo wajitafutie mahali pa kwenda huku wenye ufaulu wa daraja la kwanza na pili aliahaidi kuwa wataandaliwa utaratibu.
  • Mwananchi

Wanafunzi UDom wawashangaa waanzilishi wa programu; Wamwomba Rais Magufuli awakabili wadahili

null


Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania Unamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli kuwachukulia hatua wale wote waliodahili wanafunzi wasio na sifa katika programa maalum iliyoanzishwa katika chuo kikuu cha Dodoma na sio kuwaadhibu wanafunzi wote ambapo wengine hawakuwa na hatia.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa mtandao huo Bw Alphonce Lusako alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa Rais amesema baadhi ya wanafunzi walidahiliwa wakiwa hawana sifa za kujiunga na programu hiyo mtandao unaona kosa hilo ni la wadahili na siyo la wanafunzi, hivyo wanafunzi wenye sifa wangeachwa waendelee na masomo yao kama kawaida.

Bw Lusako amebainisha kuwa kutokana na sakata hilo, wanafunzi wengi wameathirika kisaikolojia na kukata tamaa wasijue nini cha kufanya huku wengine wakijilaumu kujiunga na programu hiyo ambayo kama sivyo, wangeendelea na Kidato cha Tano na wangekuwa wanahitimua Kidato cha Sita hivi sasa.

Aidha kwa upande wake, mwanafunzi ambaye ni mhanga wa sakata hilo, Ibrahim Abdalah amesema kuwa wanasikitika kuona hata walioanzisha program hiyo wanashindwa kujitokeza kuwatetea kwani hawakwenda kujiunga na programu hiyo kwa ridhaa zao bali ni serikali iliyoamua kuianzisha ili kukabiliana na upungufu wa walimu wa sayansi nchini.

Akisoma taarifa rasmi ya wanafunzi waliosimamishwa UDOM, Gibson Johnson alisema, wanaiomba serikali kuangalia uwezekano wa wao kuendelea na masomo yao.

“Tunaiomba na kuililia serikali iangalie wale wenye division I, II na III ituache tumalizie masomo yetu, lakini watakaokuwa na ufaulu wa chini kuanzia division IV itafute namna ya kuwasaidia,” alisema Johnson.

Wamemuomba Rais Magufuli na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kuona haja ya kuwarudisha chuoni ili kumaliza masomo yao kama ilivyopangwa, kama jambo hilo likishindikana serikali ifanye mkakati wa kuwatafutia vyuo stahiki ili wamalize masomo yao.

Kauli ya Jumuiya ya Watanzania waishio kaskazini mwa California kuhusu Balozi

JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHERN

CALIFORNIA (TCO) JUNE 3 2016 TAMKO RASMI


Jumuiya yetu ya watanzania tuishio upande wa northern California,

Tunapenda kutoa tamko rasmi kwamba hatuhusiki na wala hatujahusishwa na hatutahusika kwa njia yoyote ile kushiriki kuweka sahihi zetu kwenye barua inayosemakana ipo na inahitaji sahihi za watanzania wanaoishi hapa ili kumlazimisha au kumshinikiza Rais amuondoe Mh Balozi Masilingi.

Habari hizi zilitolewa juzi kwenye vikao vya bunge na Mh Joseph Mbilinyi alipokuwa akichangia kwenye hotuba ya waziri wa mambo ya nje. Pamoja na mengi mazuri aliyoyasema kuhusu diaspora lakini hili la kuishambulia ofisi ya ubalozi kutoshiriki na kutojali misiba ya watanzania wanaoishi USA, sio tamko letu sisi wanajumuiya na hatuhusuani na lawama hizi. Pili hili la kutaka kumuondoa Balozi Masilingi kwa nguvu nalo hatuhusiki na hatutausika kamwe. Tunatambua mchango mkubwa na ushirikiano mkubwa tunaoupata kutoka ubalozini.

Tunapenda kutoa ukumbusho kuwa sisi kama jumuiya hatujihusishi na siasa kabisa. Tunajihusisha na masuala ya kijamii katika mazingira tunayoishi na pia nyumbani.
Tunatoa pongezi kwa makundi na jumuiya nyingine za hapa usa walioliona hili na kulikemea hadharani.

Lakini pia jumuiya yetu haimzuii mtanzania yeyote miongoni mwetu kushirikishwa kwenye shughuli yoyote ile, ilimradi tu aifanye kwa utashi wake lakini si kwa jumuiya.

Asante
Erick Byorwango - Katibu mwenezi na mahusiano TCO.
Nakala: Ofisi ya ubalozi Washington DC.

Statement by the TIC regarding allegations published by The Economist about Tanzanian government

On 28th May 2016, The Economist – English Weekly Newspaper published an article with heading “Government by gesture – A president who looks good but governs impulsively” (CLICK HERE).

The article, inter-alia misinformed the public and readers that since Dr. John Pombe Joseph Magufuli came into powers last year “the country has become totally uninvestable”. The Tanzania Investment Centre (TIC) would like to point out that the information portrayed by the newspaper is inaccurate, misleading and distortion of facts.

TIC wishes to inform the public and readers of the following facts:-

1. Since President John Magufuli came into power (from December 2015 to May 2016) TIC has registered 551 investment projects worth $ 9,211.88 million. Of all these projects 229 are owned by Tanzanians, 215 projects are owned by foreigners while 107 projects are owned through joint ventures.The projects are expected to employ 55,970people and bring multiplier effects to Tanzanians.

The above registered projects by TIC for the past six months (December 2015 – May 2016) shows an increase of 20.31% compared to six months before President Magufuli came to power i.e. June-November 2015 where TIC registered 458 investment projects worth $ 5,727.29 million. Of all these projects 201 are owned by Tanzanians, 159 projects are owned by foreigners while 98 projects are owned through joint ventures. The projects are expected to employ 39,361 people and bring multiplier effects to Tanzanians.

Generally, investments have increased during President Magufuli’s era which shows high investor confidence towards his Government. Attractive laws, peace, stability good and friendly policy as well asconducive investment environment are other major factors that have attracted both FDI and domestic investment during this period in Tanzania.

2. The World Investment Report 2015 indicates that FDI rose by 14.5% in the United Republic of Tanzania. The Report noted that Tanzania, in 2014, regained its FDI inflows compared to the previous three years. In fact, its FDI inflows represented its highest level in 2014 given that it attracted slightly $ 2,142 million compared to $ 2,131 million recorded in 2013. This amount is significantly higher than the very low level of $ 640 million between 2005-2007 (pre-crisis). This achievement is due to natural gas reserves discoveries in the United Republic of Tanzania. Indeed, Tanzania remains the leading FDI’s recipient in the East African Community.

3. It is true that, the World Bank Doing Business Report 2016 ranked Tanzania 139 out of 189 countries compared to 145 out of 189 in 2014. TIC wishes to clarify thatDoing Business provides an aggregate ranking on the ease of doing business based on indicator sets that measure and benchmark regulations applying to domestic small to medium-size businesses through their life cycle. Economies are ranked from 1 to 189 by the ease of doing business ranking. Therefore this has nothing to do with the leadership of Dr. John Magufuli.

4. TIC reaffirms the public and readers that Tanzania is still the best place in East Africa to invest due to the fact that the country is peaceful and stable. Tanzania has a friendly business environment supported by good investment policy and legislation. The Fifth Phase Government under the leadership of President Magufuli continues to take measures to improve investment climate as and when need arises. Tanzania’s investment environment continues to offer predictable, transparent and strong long-term proposition to investors. Investment is legally protected against expropriation and nationalization. In terms of investment facilitation, the Tanzania Investment Centre (TIC), Zanzibar Investment Promotion Agency (ZIPA) and Export Processing Zone (EPZA) promote, coordinate and facilitate all investments in Tanzania. These are premier ports of call for investors coming to Tanzania through their well-established one-stop shop facilities. Tanzania’s geographic location position makes her as a natural regional business hub. Tanzania borders 8 countries, 6 out of which namely Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi, Zambia and Eastern part of the Democratic Republic of Congo, uses the Dar es Salaam port and Tanzania’s railways and roads for their sea freight. This presents good opportunities for investment in infrastructure development, trade, transport and logistics.

Therefore the statement that our country has become totally uninvestable has no truth in it and should be completely ignored by the public and readers.

Issued by:

ACTING EXECUTIVE DIRECTOR,
TANZANIA INVESTMENT CENTRE (TIC),
SHAABAN ROBERT STREET,
P.O. Box 938,
DAR ES SALAAM

TANZANIA

Date: 3rd May, 2016

Kinondoni yafukuza maafisa 2 na kusimamisha wengine 2

Meya wa Halmashauri ya Manispaa Kinondoni Boniface Jacob
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imefukuza kazi maafisa watendaji Kata wawili kutokana ubadhirifu fedha za umma.

Akizungumza leo na maafisa watendaji Kata, Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob amesema kuwa hawatavumilia watendaji wanaofuja fedha za umma.

Watendaji waliofukuzwa ni Ernest Misa na Ally Bwanamkuu na wengine wawili wamesimamishwa kazi kwa uchunguzi ambao ni Shaaban Kambi pamoja na Bernard Supu.

Aidha, Meya huyo amesema zipo Kata tano ambazo zimekusanya mapato vizuri na kata tano nyingine zimefanya vibaya hivyo wanatafuta dawa ya kuwaondoa watendaji waliofanya vibaya.

Jacob amesema migogoro ya ardhi imepungua kutokana na kila watendaji kuwajibika katika zao awali migogoro ilikuwa inasababishwa na wenyewe

Amesema Kinondoni wanataka kuibadili katika kuhakikisha watendaji wanawahudumia wananchi kuachana kufanya kwa mazoea.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wananchi wa kinondoni kufuata sheria katika barabara ya mabasi yaendayo haraka.

Baadhi ya wananchi wakisikiliza 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo amekutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tatizo la uhujumu wa miundombinu ya Mwendokasi.

Katika taarifa yake Mh. Hapi ameeleza kuwa katika kipindi cha siku mbili watu 49 wamekamatwa na polisi wilayani Kinondoni wakiwemo wamiliki wa magari, bajaji na bodaboda kwa makosa ya kuingilia miundombinu ya Mwendokasi kinyume cha sheria.

Kati yao watuhumiwa 43 watapelekwa mahakamani siku ya jumatatu ijayo hali inaowafanya kuyatumia mapumziko ya Juma wakiwa mahabusu.

Mh. Hapi amewataka wananchi wa Kinondoni na hasa madereva kufuata sheria, vinginevyo watakabiliana na rungu la dola.

Aidha, Mh. Mkuu wa Wilaya ameagiza Polisi wilayani Kinondoni kuendelea na zoezi la kuwakamata wale wote wanaogeuza vivuko vya barabara za DART kuwa sehemu za kulala na kujisaidia.

"Tumewaagiza Polisi kuwakamata wote wanaolala na kujisaidia kwenye vivuko vya barabara. Hata wale ambao wamesimama kule juu saa za usiku bila kazi yoyote wakamatwe na washitakiwe kwa sheria za uzembe na uzururaji. Wengine hawa ni vibaka na wengine ndio wanaolala na kujisaidia huko usiku." Alisema Hapi.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli akizungumza na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam alizungumzia juu ya uhujumu wa miundombinu ya mwendokasi na kuagiza watu hao kushughulikiwa ipasavyo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya aliutaka uongozi wa DART kuchukua tahadhari za kiusalama katika vituo vya mabasi ili kuzuia uwezekano wa kutokea tishio la usalama. Hapi aliwataka DART kuweka utaratibu wa kuwakagua abiria kwa mashine za mikono za ukaguzi ili kuhakikisha usalama wa wananchi wanaopanda mabasi hayo.
  • via Michuzi Blog