Katuni ya Ngarango Jr - SISI EM na buti la "msikale" juu ya kajamaa UPINZANI


Maelezo ya Naibu Spika baada ya CCM "kuwaombea / kuwataka" UKAWA Bungeni



Cuba yamvisha nishani Salim Ahmed Salim kwa udiplomasia; Rais mst. Mwinyi, Lowassa wahudhuria


Balozi wa Cuba Jorge Luis Lopez Tormo (kulia), akimvisha nishani Waziri Mkuu mstaafu, Salim Ahmed Salim kutokana na kutambua mchango wake katika kudumisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Cuba, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)

Balozi wa Cuba Jorge Luis Lopez Tormo (kulia) akimpongeza Salim Ahmed Salim baada ya kumvisha nishani.

Hongera.

Waziri Mkuu mstaafu, Salim Ahmed Salim akipongezwa na Adam Malima.

Baadhi yamabalozi waliohudhuria hafla hiyo.

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Baadhi ya mabalozi.

Mabalozi pamoja na maofisa wa ubalozi wakiwa katika hafla hiyo.

Wageni mbalimbali.

Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akizundua maonyesho ya picha.

Balozi wa Cuba Jorge Luis Lopez Tormo (kushoto) akimuonyesha Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi picha mbalimbali zinazoonyesha utamaduni wa watu wa Cuba.

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia) akiagana na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.





Lowassa akiagana na balozi wa Cuba.

ACT Wazalendo Leader calls for fresh elections in Zanzibar

ACT Wazalendo is a party that stands firm on democracy and the due process that comes with it, steadfast in ensuring that the voice of the people is heard and adhered too without compromising on the principles of democracy.

What has transpired in Zanzibar has left us both in awe and disgust on how certain individuals can manipulate the system to best suite their crude desire for power. Right after the nullification of the elections in Zanzibar, ACT Wazalendo was firm in its stand that democracy was being toyed with and that the Zanzibari peoples wishes were not respected. It is the party’s firm belief that Maalim Seif Sharif Hamad was the chosen president for the people and by the people.

We raised ten (10) points of caution to President Magufuli; as the custodian of democracy in the United Republic of Tanzania for him to take to task, one of them being the current situation in Zanzibar showing all signs of lacking any democratic decorum. This plea unfortunately fell on deaf ears and the outcome of this negligence was the re-run of the Zanzibar election in March, which to date still bids the question of the legality and mannerism of how it was conducted.

ACT Wazalendo continues its fight for a booming democratic environment in Zanzibar that would foster the growth of new age politicians who are not intimidated by sheer police brutality or the power of the state. With this stand, ACT Wazalendo, has continually denounced the legality of the election in Zanzibar and has chosen not to recognise the current government of Zanzibar in its totality for, if there is ever a doubt that ones rights are infringed the party will not stand by those who infringing the rights of another.

Chaos breeds fear and fear has no part in the struggle to attain justice. Dr. Shein recently has been quoted saying “I am not afraid of Maalim Seif, for he does not have no posses tanks or ammunition”. In hindsight he is right, Maalim Seif does not possess the power and might of the state, after the sabotage that took place in October 2016 he is merely a citizen and former 2nd Vice president of Zanzibar. But let us not forget that he also happens to be the leader of a group of people on the Isles, maybe he does not require military might to be feared all he needs to do is get the attention of his followers. Maybe this was the trigger effect that made the army interrogate the politician when he simply wanted to practice his democratic right to be heard.

ACT Wazalendo cannot condone the words said by Dr. Shein, for one they are beneath him and beneath any self respecting citizen of the United Republic of Tanzania, we were liberated; one half by good diplomacy and the other half by force. It would be wise for Dr. Shein to remember the seat that he is clinging on comes with its own history, and it should be a lesson to him no to mock the people by threatening them with military might, after all the Sultan of Oman, not only had his army but also the backing of the then hegemony United Kingdom, this did not stop those who could not stand injustice to stand up against military might. Words such as those uttered by Dr. Shein only work to remind us that Zanzibar is not a step sibling that we can ignore, that such mishap and insensitivity from a seasoned politician leaves the isle vulnerable to many a thing, we do not want to see our brothers and sisters shed blood…again.

As a party, ACT Wazalendo is fully aware of the hardship that faces the Zanzibar people, the political tension translates to a stagnant economy and a demoralised society. We do understand that there is a need for the people to take control of their state but we firmly believe and have not lost hope that the process be ballot and not bullet. One way of ensuring that the Zanzibari people walk away the winners and not just the politician, is for those who want to serve the people to lower themselves and consider their people first and not self gratification.

If we may, let us restart the clock again for Zanzibar, go to the ballot and ensure that the peoples wishes are respected no matter what the outcome maybe. Some may argue that how can we restart the clock? That at no point in time can a state be without a leader. For this we say, have a transitional government that comprises of members from all political players on the isles, let that government involve people who are respected by all fractions of Zanzibaris.

Possibly the greatest thing for the Zanzibari people to do is to ignore the blatant attack on their integrity and rights by Dr. Shein, for he may have not known better. Let history be a reminder for him and a point to remember for the people on the isles that throughout oppressors have met an unfavourable outcomes, we do not wish to see the same for Zanzibar no do we wish for their good name to be tarnished.

Zitto Kabwe, MP
Party Leader, ACT Wazalendo

Uchambuzi wa ACT Wazalendo wa Bajeti ya Serikali 2016/17

Maoni ya viongozi CUF kuhusu ombi la Prof. Lipumba la kurejea katika uongozi wa chama

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba hawezi kuwa na nia njema ya kukijenga chama hicho endapo atarudishwa kwenye nafasi aliyoikataa.

“Anataka kuja kukiharibu chama,” alisema Mazrui. Alifafanua kuwa tayari chama hicho kimefanya mambo mengi bila Lipumba ambaye alikuwa anaona kila kinachoendelea, hivyo alichokisema hakina mashiko kwani CUF ilisharidhia kuitisha mkutano wa uchaguzi kujaza hiyo.

Akieleza sababu alizozitoa mwenyekiti huyo, Mazrui alisema haoni chochote cha maana. “Sababu zilizomuondoa zingalipo. Kinachomrudisha ni nini?” alihoji naibu katibu mkuu huyo.

Alisisitiza kuwa Wazanzibari wanaendelea na mchakato wa kuidai haki yao iliyoporwa Oktoba 25 na hawana nafasi ya kushughulika na masuala yasiyokuwa na tija kwao, hivyo haoni kama kuna sababu ya kumjadili Lipumba na nafasi yake badala ya kuendelea pale walipo.

“CCM wanaona kinachoendelea, hivyo wameona wamtumie Lipumba kuja kuharibu mipango yetu. Hatuna muda wa kumjadili.Tunataka haki iliyoporwa,” alisisitiza.

Msimamo wa Mazrui haukutofautiana sana na ule wa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Twaha Taslima aliyebainisha kuwa amesikia taarifa za kurudi kwa Profesa Lipumba, lakini haoni uwezekano huo.

“Katiba hairuhusu hilo.Hakuna kifungu kinachotoa nafasi kwa kiongozi aliyejiuzulu kurudi kwenye nafasi yake pindi atakapotaka kufanya hivyo,” alisema Taslima.

Aliielezea Ibara ya 117 (2) iliyotumiwa na Profesa huyo kuandika barua ya kutengua uamuzi wake, kuwa inatoa tafsiri zaidi ya moja hivyo kuwapo haja ya viongozi kukutana na kujadili suala hilo kabla ya kutoa maamuzi.

Kwa kuwa hakuwapo kwenye mkutano huo, Taslima alisema: “Tunahitaji kukutana haraka na kujadili. Tutafanya mkutano wetu na tutavijulisha vyombo vya habari ndani ya wiki hii.”

Taslima alisema kipindi alichoongoza kilikuwa na changamoto nyingi ambazo ni tofauti na sasa, hivyo haoni haja ya mtu mwingine kuja wakati mambo yametulia. Chama hicho kilipanga kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo Agosti mwaka huu.

Baada ya kung’atuka kwa Lipumba, Taslima alichukua mikoba yake na kukivusha chama hicho kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, pamoja na ule wa Zanzibar ambao uliahirishwa na chama hicho kususia marudio yake Machi 20 mwaka huu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya alisema upo uwezekano wa Lipumba kurudi kwenye nafasi yake kwasababu mpaka sasa haijazibwa.

“Mwenyekiti huchaguliwa au kutenguliwa na halmashauri kuu. Haikupitisha kujizulu. Barua ya kujiuzulu itaenda pamoja na hii ya kutengua uamuzi wa awali,” alisema Kambaya.

Kauli za viongozi hao, zimekuja muda mfupi baada ya Profesa Lipumba kutangaza nia hiyo jana kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni huku akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kuombwa na viongozi wa dini, wa chama na wanachama wa CUF.

Jana, wakati anatangaza kufanya mabadiliko ya kile alichokiamua miezi 10 iliyopita, hakuruhusu maswali, ila alifafanua kile kitakachofuata baada ya kuwasilisha ombi hilo, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho: “Katibu Mkuu anashauriana na wanasheria kabla suala langu halijapelekwa kwenye halmashauri kuu kama katiba inavyosema,” alisema Profesa Lipumba.
  • via GPL

Tarifa: Manispaa ya Kinondoni yasaini Mkataba wa madawati na makampuni 9 tofauti


Lissu, gazeti la MAWIO waitwa mahakamani kujibu mashtaka ya njama na uchochezi Zanzibar

(picha: Mtanzania)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yatoa hati ya wito kwa Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu (48) na mwenzake, wa kwenda kujibu mashtaka ya kula njama na kutoa lugha ya uchochezi kwa watu wa Zanzibar.

Mbali na Lissu mshtakiwa mwingine aliyepewa wito huo ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrissa (52) huku Mhariri wa habari Simon Mkina (44) na Mchapishaji Ismail Mehboob (24) wakisomewa mashtaka hayo mapema jana.Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili wa Serikali Paul Kadushi alidai kuwa kati ya Januari 12 na 14, mwaka huu mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikula njama ya kusambaza taarifa ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio lililokuwa na kichwa cha habari cha “Machafuko yaja Zanzibar”.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Januari 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam,washtakiwa wote kwa lengo la kushawishi uchochezi kwa Watanzania Visiwani dhidi ya mamlaka za kisheria za serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Ilidaiwa kuwa walichapisha kwenye gazeti la Mawio toleo namba 182 la Januari 14 hadi 20, 2016 ikiwa na habari ya uchochezi yenye kichwa cha habari kisemacho ‘Machafuko yaja Zanzibar”.

Kadushi alidai katika shtaka la tatu, Januari 13, mwaka huu Jengo la Jamana lililopo Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mehboob, kwa lengo la kushawishi Watanzania wa Visiwani, dhidi ya mamlaka za kisheria za serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Upande wa huo wa Jamhuri ulidai katika shtaka la nne, Januari 13, mwaka huu katika Jengo la Jamana mshtakiwa Mehboob alichapisha gazeti la Mawio toleo namba 182 bila kuwa na kiapo kutoka kwa msajili wa magazeti.

Shtaka la tano, Januari 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kwa makusudi na bila kuwa na mamlaka ya kisheria waliwatishia watanzania wa Visiwani, wasijitokeze kwenye Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa waliwatishia kwamba uchaguzi huo utasababisha kutokea kwa vita na machafuko utakaosababisha umwagaji wa damu kupitia makala iliyochapishwa na gazeti la Mawio yenye kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar”.

Hakimu Simba aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka katika taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. Milioni 10 kila mmoja walitimiza masharti hayo.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya washtakiwa hayana mashiko ya kisheria mahakama iyafute na kuwaachia huru.Alidai kuwa sheria za magazeti za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara haziingiliani na Tanzania Visiwani hivyo kesi hiyo haina mashiko ya kisheria.

Wakili Kadushi aliomba muda wa siku saba kwa ajili ya kujibu hoja za utetezi.Hakimu alisema kesi hiyo itasikilizwa majibu ya hoja za Jamhuri Juni 28, mwaka huu na washtakiwa Lissu na Idrissa wafike mahakamani kusikilizwa mashtaka yao.
  • Mwene Said via Michuzi blog.

Mrema: Wapinzani wenzangu ndiyo vinara wa kuaribu demokrasia na kuwapotosha wananchi

Na Bashir Nkoromo

MWANASIASA mkongwe nchini na Naibu Waziri Mkuu mstaafu, Agustine Mrema amewataka wapinzani kumwacha Rais Dk. John Magufuli afanye kazi yake kwa kuwa amechaguliwa kihalali na bado hajamaliza hata kipindi cha kwanza cha uongozi wake.

Amewatahadharisha wananchi kuwa makini na wanasiasa kwa kuwa wapo baadhi wasio na nia njema na nchi badala yake wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi hata kama nchi inaweza kuingia kwenye majanga.

Pia amevitaka vyombo vinavyohusika na uratibu wa mambo ya siasa nchini hususan Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwatazama kwa macho mawili viongozi wa dini wanaotumia nyumba za dini kuwa majukwaa ya kisiasa huku wakiwayumbisha wananchi kwenye haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Aidha, ametaja sababu iliyomfanya ashindwe kulichukua jimbo la Vunjo ambapo pamoja na mambo mengine ni pamoja na hatua ya Rais Magufuli kumpigia debe jimboni humo jambo lililowafanya wamwonee donge na kuhamishia kampeni katika jimbo ili kuhakikisha halipati.

Hayo aliyasemwa jana mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam, alipokuwa akizungumzia hali ya kisiasa ya hapa nchini, ambapo alisema analaani kitendo cha wapinzani kudai Rais Magufuli hawatendei haki wananchi, anavunja sheria, katiba na anakiuka haki za binadamu na kuua demokrasia ya nchi.

Mrema alisema hivi sasa nchini kumeibuka vuguvugu la kisiasa hususan kwa wapinzani kutangaza serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. Magufuli imekuwa ikikiuka haki za binadamu na kuponda demokrasia jambo ambalo si la kweli kwa kuwa kila mwanasiasa yupo huru kuzungumza na kuchangia maendeleo kwa kadri anavyoweza.

Alisema wapo wanasiasa wanaodai Rais Magufuli hawatendei haki wananchi, anavunja sheria na kukiuka haki za binadamu huku wasemao hayo ndio vinara wakuu wa kukiuka haki hizo.
"Wapinzani wenzangu ndio vinara na waliokubuhu na vitendo vya kuaribu demokrasia nchini na kuwapotosha wananchi jinsi ya katiba inavyoenda nchini,"alisema Mrema.
Aliongeza kuwa kipindi cha uchaguzi mwaka jana, Mbunge wa Vunjo James Mbatia alikiuka sheria na maadili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015.

Mrema ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Vunjo, alisema NEC na taasisi zingine zinazosimamia shughuli za kisiasa nchini zinapaswa kuwa makini na baadhi ya viongozi wa dini ambao wameacha jukumu lao kuu la kuwajenga kiroho waumini wao na kutumia vyombo vya dini kama kinga yao kwenye siasa.

"Wakati wa harakati za uchaguzi mkuu wa mwaka jana wapo viongozi wa dini waliosimama kwenye nyumba za ibada na kuwahubiria wafuasi wao kwamba mwaka huu rais lazima atoke kanda ya Kaskazini na nje ya hapo hatuwezi kukubali. Maneno hayo hayapaswi kuachwa yaendelee kwa kuwa ni hatari kwa mustakabbali wa siasa na maendeleo ya demokrasi hapa nchini.
"Wananchi kuweni makini si kila mwanasiasa anayekuja mbele yenu ana nia njema na taifa hili wengine lengo lao ni kutaka nchi iingie kwenye matatizo ili wao wanufaike,"alisema.
Akizungumzia kwa nini alikosa ubunge wa vunjo kupitia uchaguzi huo, alisema hilo lilitokana na mkakati wa wapinzani wenzake ambao walimuonea donge baada ya kuungwa mkono na Rais Magufuli aliposimama jimboni humo wakati wa kampeni na kumnadi.
"Nawashangaa wapinzani wenzangu hawajui kuwa Rais Dk. Magufuli anathamini zaidi mchango wangu nilioutoa nilipokuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, jinsi nilivyokuwa nafanya kazi kwa nguvu moja kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo,"alisema.
Aidha, Mrema alisema ana uhakika endapo Dk. Magufuli atakabidhiwa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), atamtafutia nafasi ya kumsaidia kushughulika na maendeleo ya Tanzania kwa kuwa kasi yake anaimudu na ataweza kwenda nae sawa.

Hivi karibuni vyma vya upinzani hususan vinavyounda UKAWA vbimekuwa na kampeni ya kutaka kuzunguuka nchi nzima kuishitaki serikali kwa madai imekuwa ikikandamiza haki hapa nchini.

Hata hivyo, tayari polisi imepiga marufuku mikutano, makongamano na maandamano yoyote ya kisiasa kwa kuwa yanamwelekeo wa kuwachochea wananchi kukiuka sheria za nchi na kushiriki matukio ya uvunjifu wa amani.

Taarifa ya habari ChannelTEN Juni 14, 2016





Waliyozungumza Rais mstaafu Mkapa, Jenerali Ulimwengu kwenye Kigoda cha Mwalimu Nyerere 14.06.2016

Jenerali Ulimwengu akiwa kwenye Kongamano la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amesema pamoja na hatua nzuri anazochukua Rais wa sasa, Mheshimiwa John Magufuli ambazo zimepongezwa, picha kubwa inaonesha kuwa tumerudi nyuma kama miaka 50 kwenye demokrasia.

Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ulimwengu amesema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Ulimwengu ameendelea kwa kusema Mheshimiwa Kikwete anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka kwa kusababisha hasara kubwa kwa serikali na pili kuzima matumaini ya wananchi na kuwaacha wanarandaranda ambayo inaweza kuleta machafuko baadaye kama haitawezekana kutengeneza katiba ambayo itajenga mustakabali wa wananchi wa Tanzania.


Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameongea kwenye Kongamano la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kuongelea nyufa zilizopo na kusema ni kutokana kupenda kuzungumza watu badala ya sera.

Mkapa pia amegusia kuhusu kizazi kipya na amewataka watu kufatilia michango ya vijana bungeni ambao hawajafanya kazi hata miaka mitatu, uchambuzi na mbadala gani wanapeleka bungeni na kusema hapana kwenye kulalamika.

Mkapa amesema anakubali kuwa kiongozi ni lazima aweze kusikiliza na ilikuwa ni sifa mojawapo ya Mwalimu lakini watu ni hodari wa kusema nini kifanywe mpaka inafika wakati unatokea umuhimu wa kunyamazisha.
"sasa umuhimu wa kukunyamazisha wewe lazima tuutafakari, maana mara nyingine unatu-distract from the issues."

On Freedom of Expression, "...Ngoja niwaambieni basi, mimi ndiye niliyemwambia Aga Khan, njoo anzisha magazeti mengine hapa. Ya serikali na IPP hayatoshi pake yake. Nataka ku-broaden perspective, ndiyo maana ikaja kampuni ya Mwananchi na kuanzishwa kwa Citizen na Mwanchi, at my request! That's the kind of intolerance I have."