[infographic] How to measure your eyeglass frames size

What Are The Best Eyeglasses For Your Face Shape? - Infographic

Njia 6 zitakazokutoa kwenye umasikini

Makala hii tumeshirikishwa na Imani Ngwangwalu.

Kila wakati ninapopata nafasi ya kuzungumza na watu juu ya maisha nimekuwa nikilisema hili mara kwa mara kuwa maisha tunayoishi yanaongozwa na kanuni. Kanuni hizi ndizo zinazoleta matokeo ya aina fulani katika maisha yetu kila siku uwe unajua au hujui.

Kiuhalisia kutokana na kanuni hizi au njia hizi wale wanaofanikiwa hujikuta ndio wanaomudu kutumia kanuni hizi vizuri katika maisha yao na wale wasiofanikiwa na kuishia kwenye umaskini hujikuta wao ndio wanaoshindwa kutumia kanuni au njia hizi ndogo ndogo katika maisha yao.

Ni kweli kama unataka kufanikiwa na kutoka kwenye umaskini ulionao ni lazima utumie njia hizi ambazo zitakusaidia sana katika mchakato mzima wa kupata utajiri katika maisha yako. Hizi ni njia ambazo zimetumiwa na watu mbalimbali waliofanikiwa kuwatoa kwenye umaskini na hatimaye kuwa matajiri.

Kwa kadri utakavyomudu kutumia njia hizi za mafanikio utakuwa unajitengenezea uwezo mkubwa wa kufanikiwa kwa kile unachofanya. Njia hizi ni zipi ambazo zinaweza kukutoa kwenye umaskini na hatimaye kukufanya kuwa tajiri?

Hizi ndizo njia zinazoweza kukutoa kwenye umaskini:-

1. Amua kuwa tajiri.

Ili uweze kutoka kwenye umaskini ulionao hatua ya kwanza unayotakiwa kuchukua ni kuhakikisha unaamua kuwa tajiri. Maamuzi ya kuwa tajiri ni muhimu sana kwako kwani chochote utakachopania katika maisha yako utakipata, hii ikiwa na maana kuwa mtu ana uwezo wa kufanikisha kile anachoamini anaweza na si zaidi.

Kama kwenye maisha yako umeamua kuwa tajiri, utakuwa tajiri kweli kikubwa maamuzi yako tu umeamua maisha yako yawe vipi. Kama upo kwenye safari ya kuelekea kwenye utajiri ambayo hata mimi ninayo ni lazima ufanye kile unachotafuta, kionekane kinawezekana kwako, weka malengo yatakayokufanya uendelee mbele zaidi kila siku.

2. Kuwa na mipango ya uhakika.

Kama una nia kweli ya kutoka kweli kwenye umaskini ulionao, hakikisha pia una mipango ya uhakika ya kukutoa pale ulipo. Kama unataka kufanya kitu fulani, tafuta njia itakayokutoa na hasa tafuta mtu mwingine aliyewahi kufanikisha jambo hilo unalotaka kulifanya.


Weka mipango ya uhakika na inayowezekana kwako kuifikia. Jifunze haya yote kwa wale waliofanikiwa zaidi yako. Unapokuwa na mipango ya uhakika inakuwa ni rahisi sana kwako kuifatilia na kiutekeleza. Acha kupanga mipango yako bila ya kuifatilia, ipange mipango yako kisha uifatile. Ikiwa huwezi kufatilia mipango yako nani ataifatilia?

3. Jifunze kutokukata tamaa mapema.

Hii ni njia muhimu sana kwako ya kukufanya wewe kuwa tajiri na kukutoa kwenye umaskini ulionao. Ukiwa na uwezo wa kupambana na vikwazo, ndicho kitu kitakachokufanya ufanikiwe zaidi, na si kukata tamaa na kuacha. Kila safari ya mafanikio ina changamoto zake na vikwazo vyake, hivyo inabidi kukabiliana navyo.

Utaweza kufika kule unakotaka , ikiwa utakuwa uko tayari kupambana na vikwazo vitakavyotokea njiani. Vikwazo vyote ni nafasi ya kufanikiwa kama utajifunza kitu kwenye hivyo vikwazo au matatizo yanayokuzunguka.

4. Jifunze kufanyia kazi ndoto zako kila siku.

Hii iko wazi kabisa ikiwa utaendelea kufikiria tu, unalofikiria litaendelea milele kubaki kwenye fikra zako na si zaidi. Ni lazima ufanye mambo kwa vitendo ili uweze kujikwamua na umaskini. Unatakiwa kuanzia mahali fulani hasa pale ulipo.

Mpaka utakapoanza ndipo utakapopata matokeo yatakayokusaidia kuweka misingi bora na mwelekeo wako. Ndege ni lazima ianze kwa kuruka inapofika hewani huanza kujiweka sawa ili upate mwelekeo mzuri wa kule inakokwenda.

Ni lazima uanze na mahala fulani popote, si lazima iwe mahala maalumu kama unavyofikiri, wewe anza tu kufanyia kazi ndoto zako mambo mengine yatajipanga mbele ya safari. Acha kusita sita fanyia kazi ndoto zako ili ufanikishe kile unacholenga.

5. Jifunze kuwa na bajeti maalumu katika maisha yako.

Unapokuwa na bajeti hii itakusaidia wewe kuwa na taarifa nyingi za matumizi na mapato ya pesa zako binafsi na za biashara zako. Ikiwa kila siku unaishi maisha ya kutoweka kumbukumbu hiyo itakusababishia kutojua wakati unapopoteza fedha bila ya sababu hadi hali yako itakapokuwa mbaya zaidi.

Jijengee utaratibu wa kujiwekea bajeti hii itakufanya hautatumia pesa hovyo na hizo pesa utakazozotunza zitakusaidia sana katika kuwekeza pale zitakapokuwa nyingi na hatimaye zitakutoa kwenye umaskini.

6. Jijengee tabia ya kijiendeleza zaidi.


Ni watu wachache sana ambao huwa na tabia ya kujiendeleza kwa kujisomea mara baada ya kumaliza masomo. Kama unataka kuondokana na umaskini hakikisha unasoma mambo mengi na mapya ili kukabiliana na changamoto zaidi za dunia ya sasa.

Bahati mbaya sana mfumo wetu wa elimu tulionao sasa hautusaidii sana kuhusiana na hali halisi ya maisha yetu, hivyo usifikirie kwamba kwa vile umefika chuoni, basi una kila nyenzo ya kukufanya ufanikiwe. Unatakiwa kuendelea kujifunza, watu wenye mafanikio ni watu wakujifunza sana katika maisha yao yote.

Kumbuka ukitaka kufika hadi kwenye kilele cha mafanikio unaweza endapo tu utaamua mwenyewe, hizo ndizo njia muhimu unazoweza kuzitumia kukutoa kwenye umaskini ulionao.
 • Unaweza ukajifunza zaidi mafanikio kwa kutembelea BLOGU YA DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Imani ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,
E-mail; [email protected]
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com

Kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya Tanzania leo Juni 16, 2016FREE Chili Dog on Father's Day (June 19th) at Wienerschnitzel

More info at www.wienerschnitzel.com

Taarifa ya habari ChannelTEN Juni 15, 2016


Singo Africa: Home Business Technology & Consulting


Africa public and private organizations have heavily invested on computer desktop/laptop workstations, tablets, wide and local area networks, servers and storages etc. with promise that thing will change for better. However, over decades considerably only few have earned optimal return on their technological investments.

Singo Africa Limited is bringing world class experience by focusing on adding value and stimulate competitiveness to its Africa business partners' through their existing as well as to be acquired new technologies and business services.

Our Services

We strive to provide an excellent service in terms of quality of work, timely delivery, professional behavior, customer service and value for money.

We are primarily focusing on all business process automations and consulting on:-
 • Manufacturing, logistics and supply chain.
 • Microfinance, i.e. SACCOs, VICOBA, Agri-Coop societies, Micro-Credit etc.
Please visit www.singo.co.tz for detailed information.


Uber now in Dar es Salaam...


Following the success of Uber in many other cities, Uber is excited to launch its ride-sharing platform to the people of Dar es Salaam.

Uber’s innovative platform connects drivers with riders in real time, at the touch of a button. Whether you’re a local heading out with friends, in the city on business or exploring its tourist sites, Uber provides an affordable, safe and reliable way to get across the city.

Dar es Salaam’s exciting, rapidly growing market makes it a perfect fit for Uber. The World Bank states that Tanzania’s GDP growth rate is estimated at 6.8% for 2017 and the country is maintaining a low rate of inflation. Businesses are flourishing, with sectors such as transport, construction and financial services booming.

Alon Lits General Manager for Uber Sub-Saharan Africa said: “We are proud to launch Uber in Tanzania at such an exciting point in its growing economy. As the infrastructure of Dar es Salaam rapidly urbanises, so the demand for affordable, easy and flexible transport grows.”

He added, “We have set the standard for connecting people to world-class transport, moving millions of global citizens every day through our offering of affordable and reliable rides at the touch of a button. Our service complements existing transport options, so we can all work together to reduce traffic congestion and the environmental impact of transport in the city.”
 • Uber helps people get a ride at the push of a button - there’s no waiting on the street or walking through unfamiliar neighbourhoods to find a bus. It’s the most convenient way to get a safe, reliable and affordable ride.
 • No more street hails or waiting outside to find a ride. You can start the Uber app from anywhere and wait safely for your car to arrive. That means no standing on the street to hail a cab or struggling to find the nearest bus stop late at night.
 • Trips are no longer anonymous. When a driver accepts your request, you see his or her first name, photo, and license plate number. You can also check whether others have had a good experience with him or her. In addition, the driver can see your first name and rating. You can contact the driver—and vice versa— through the app if there is any confusion around pick-up details. 
 • Share your ETA and location. You can easily share your ride details, including the specific route and estimated time of arrival, with friends or family for extra peace of mind. They’ll receive a link where they can see in real time the name and photo of the driver, their vehicle, and where you are on the map until you arrive at your destination - and they can do all of this without having to download the Uber app themselves.
 • Feedback and ratings after every trip. After every ride, you and your drivers need to rate each other and provide feedback. Our safety team reviews this information and investigates any issues.
 • 24/7 Support. If something happens in a car, whether it’s a traffic accident or altercation between you and your driver, our customer support staff are ready to respond to any issues 24 hours a day, seven days a week.
 • Rapid Response. We have a dedicated Incident Response Team to answer any more urgent issues. If we receive a report that a driver or rider has acted dangerously or inappropriately, we suspend their account, preventing him or her from accessing the platform while we investigate.
 • Always on the map. Accountability is one of the things that makes riders feel safe in an Uber. We use GPS to keep a record of where a driver goes during the ride, allowing us to verify that the most efficient routes are being used, which creates accountability and a strong incentive for good behaviour.
 • Working with law enforcement. In cases where law enforcement provides us with valid legal process, we work to get them the facts, for example by providing trip logs. Again, transparency and accountability are at the heart of the Uber experience.
 • Pre-screening drivers. All drivers must undergo a screening process before they can use the Uber app.
Alon Lits added: “Uber is part of a broader global evolution in transportation. Dar es Salaam is a vibrant, thriving city with a growing youthful labour force that is ready to welcome and support our service. Together, in partnership with the current transport system in Dar es Salaam, we will shape the future of urban travel to benefit passengers, drivers and the environment. We are so excited to be launching here.”

Uber is celebrating its launch in Dar es Salaam by providing free rides. Tanzanians can try out the new service by accessing their complimentary rides on the Uber app. [via biztechafrica.com]
Alon Lits Meneja wa Uber Sub Saharan Afrika akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati alipotambulisha huduma mpya ya usafiri jijini Dar es salaam leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam linakuwa jiji la 475 kujiunga na mtandao unaokuwa wa Uber duniani. Kwa uzinduzi wa Uber, jukwaa la ubunifu wa kiteknolojia, Dar es Salaam inaungana na orodha ya vituo maarufu vya usafiri barani Afrika. Kufuatia mafanikio ya Uber katika nchi nyingi, Uber inayo furaha kuzindua jukwa la ushirika la abiria kwa watu wa Dar es Salaam.

Uber Dar es Salaam

Jukwaa la mtandao wa ubunifu la Uber, huwaunganisha madereva na wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe. Au ukiwa unatoka na marafiki kwenda mjini kibiashara, au kuangalia vivutio vya kitalii, Uber hutoa njia rahisi yenye unafuu kufika kila mahali.

Dar es Salaam Jiji linalokua kwa kasi kibiashara, linafanya iwe ni mahali sahihi kwa Uber. Taarifa za Benki ya Dunia zinasema kwamba Pato halisi la Tanzania (GDP) linakadiriwa kuwa 6.8% kwa mwaka 2017 na nchi imeweza kuhimili mfumuko wa bei. Biashara zinakua kwa kasi katika sekta za usafiri, ujenzi na fedha.

Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits anasema:
“Tunajivunia kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao uchumi wake unakua. Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya viwanda, hivyo huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa kuaminika.”
Akaongeza,
“Tumeweka viwango vya kuunganisha watu katika usafiri wenye kiwango cha juu duniani, kusafirisha mamilioni ya watu duniani kote kila siku kupitia huduma zetu za usafiri nafuu na za kuaminika kwa kubonyeza kitufe tu. Huduma zetu zinaenda sambamba na aina za usafiri uliopo, hivyo wote tunaweza kufanya kazi pamoja kupunguza foleni barabarani na kuboresha mazingira ya usafiri katika jiji.
Kwa nini Uber?

Uber husaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu kitufe-hakuna kusubiri barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa ajili kutafuta basi. Ni njia bora na karibu zaidi kupata usafiri salama, nafuu na wa kuaminika.

Kabla ya kuingia ndani ya gari
 • Hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri usafiri. Kwa usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo ukisubiri gari ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani kusubiri taksi au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu muda wa usiku. 
 • Safari hazina kificho. Mara dereva anapokubali ombia lako, unaona jina lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia kama kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea, dereva anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza kuwasiliana na dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama kuna mkanganyiko wowote kuhusu muda wa kukuchukua. 
Wakati wa Safari
 • Julisha mahali ulipo. Unaweza kuwajulisha ndugu na marafiki zako kwa furaha zaidi juu ya mipango ya safari yako kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na mahali ulipo, na muda unaotarajia kuwasili. Watapokea linki ambapo wataweza kuona muda kamili, jina na picha ya dereva, gari lake na mahali ulipo katika ramani hadi utakapowasili na wanaweza kufanya haya yote bila haja ya kupakua App ya Uber wao wenyewe. 
Baada ya Safari
 • Fanya mrejesho na toa alama kila baada ya safari. Baada ya kila safari, wewe na dereva wako mnahitaji kupeana alama na kufanya mrejesho. Timu yetu ya usalama hupitia taarifa hizi na kufanya uchunguzi juu ya kila jambo. 
 • Msaada masaa 24 kwa wiki. Endapo jambo litatokea ndani ya gari, kama ni ajali ya barabarani au kutoelewana kati yako na dereva, mfanyakazi wetu wa huduma kwa wateja yupo tayari kukusaidia kwa suala lolote masaa 24 kwa wiki. 
 • Msaada wa Haraka. Tuna timu mahiri inayoshughulika na matukio kujibu suala lolote linalohitaji ufumbuzi wa haraka. Tukipokea taarifa kuwa dereva au abiria amesababisha tukio la hatari au hayupo njia sahihi, tunafunga akaunti zao na kumzuia asiweze tena kuingia katika jukwaa la Uber wakati tukifanya uchunguzi.
Nyuma ya Pazia
 • Muda wote kwenye ramani. Kukubali kuwajibika ni moja ya mambo yanayofanya wasafiri kujisikia wako salama ndani ya Uber. Tunatumia teknolojia ya mawasiliano ya GPS kuweka taarifa za mahali madereva wanakotakiwa kwenda wakati wa safari, ili kutuwezesha kuthibitisha njia zinazotumika ni bora, kitu kichanachojenga uwajibikaji na ushawishi mkubwa kwa utendaji mzuri. 
 • Utendaji na mamlaka za sheria. Endapo mamlaka za kisheria zinatupa taratibu za kisheria, tunatafanya kazi kutafuta vielelezo, mfano kwa kutoa taarifa za safari. Hata hivyo uwazi na uwajibikaji upo katikati ya mafanikio ya Uber. 
 • Upimwaji wa madereva. Madereva wote lazma awapitie mchakato wa upimwaji kabla ya kuanza kutumia App ya Uber
Alon Lits ameongeza:
“Uber ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika Nyanja ya usafirishaji. Dar es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa ukiwa na vijana mahiri wenye nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari kutukaribisha na kusapoti huduma yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar es Salaam tunaweza kubadilisha sura ya usaifiri wa mjini kunufaisha abiria. Tuna furaha isiyo na kifani kwa uzinduzi huu.”
Uber inasherehekea uzinduzi mjini Accra kwa kutoa huduma ya bure ya usafiri. Waghana wanaweza kujaribu huduma mpya kwa kupata huduma ya bure kwa kuingia kwenye App ya Uber.

MAKUBALIANO (vigezo kwa usafiri wa bure) 
 • Ni lazima upakue App ya Uber na weka kificho cha promosheni MoveTanzania ili upokee usafiri wa bure 
 • Usafiri wa bure utapatikana kutoka Alhamisi Juni 16 saa 6 mchana mpaka Jumapili Juni 19 katikati ya usiku. 
 • Watumiaji watapata usafiri wa bure kwa safari sita tu na kila safari isizidi kiasi cha shs 12,000 
 • Usafiri wa bure utapatikana tu kwa safari zinazoanzia na kuishia maeneo ya Dar es Salaam yaliyopangwa.

Baadhi ya watendaji wa Kampuni ya Uber Ulaya na Afrika ikiwemo Tanzania wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Alon Lits katika mkutano huo.

Kuhusu Uber

Uber ni kampuni ya teknolojia inayowaunganisha wasafiri na madereva kwa kiasi cha kubonyeza kitufe. Hupatikana kwenye miji 475 katika nchi 73, jukwaa la Uber hujumuisha jinsi dunia inavyokwenda. Malengo ya Aber ni kubadilisha mtazamo wa watu jinsi wanavyokwenda duniani, kufanya kazi na kuishi. Inajihusisha kubadilisha jinsi watu wanavyoungana na familia zao, hivyo huleta uaminifu na ukaribu kwa kutoa nafasi katika mipango ya usafiri.

Taarifa ya CUF: Kauli ya Maalim Seif kuhusu maombi ya Prof. Lipumba kurejea uongozini


Waraka wa Edward Lowassa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP)

Kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP)

Salaam,

Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za kiitifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako.

Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukukifikishia ujumbe huu, yana uzito mkubwa na kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa kitaifa.

Msingi wa waraka wangu huu ni agizo ulilotoa wewe, Inspekta Jenerali wa Polisi la kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa na maandamano ya vyama vya upinzani.

Ni bahati mbaya kwamba wakati ukitoa maagizo hayo, nilikuwa niko nje ya nchi, ingawa kwa bahati njema, Watanzania wenye mapenzi mema na taifa lao waliopo hapa nchini na nje, walinifikishia taarifa juu ya agizo lako hilo.

IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanya hivyo ili kuweka rekodi sahihi, sambamba na kukosoa sababu ulizotoa kuwa nyuma ya agizo lako hilo.

Wakati nikiwa natafakari kwa mshangao agizo lako hilo, na baada ya kurejea nyumbani, nilipigwa na butwaa zaidi niliposikia Jeshi la Polisi tena katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, likiwazuia viongozi wetu wakuuna wa juu kitaifa kufanya mikutano ya hadhara.

Agizo hilo lilifuatiwa na tukio la kukamatwa, kushikiliwa na kuhojiwa kwa viongozi hao, akiwamo mwenyekiti wetu wa taifa, Freeman Mbowe (MB) huko Mwanza hivi majuzi.

Katika matukio hayo yote, Polisi mnadai kuwa na taarifa za kiintelijensia ambazo zinazonyesha kuwapo kwa uwezekano wa kutokea kwa vurugu kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya vyama vya siasa.

Madai haya ya polisi ambayo hata wewe binafsi umepata kuyatoa awali ulipoamua kwa sababu mnazojua ninyi wenyewe, kuminya haki za msingi na za kikatiba za vyama vya siasa kujumuika na kutimiza majukumu yao ya kisiasa hayana ukweli hata kidogo.

Si hivyo tu, uzoefu wa kihistoria unakinzana na kwenda kinyume kabisa na madai hayo, kwani yako matukio mengi ambayo yamethibitisha kwamba mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya upinzani, yakiwamo maandamano na hata mikutano imekuwa ikifanyika kwa amani.

Iko mifano mingi inayoonyesha kwamba, tumefanya shughuli mbalimbali za kisiasa kwa maana ya maandamano na mikutano ya hadhara kwa amani na pasipo kuwapo hata kwa ulinzi wa polisi.

Mifano ya namna hiyo ndiyo inayosababisha baadhi yetu si tu tupingane na maagizo yanayotoa mwelekeo wa kukandamizwa kwa uhuru wa kikatiba wa vyama vya siasa vya upinzani kujumuika bali kwenda mbali zaidi na kutilia shaka hata maagizo hayo na kuyaona kuwa na misukumo iliyojificha nyuma ya kichaka cha ‘sababu za kiintelejensia’.

Naandika waraka huu kwako nikiamini kwa dhati kabisa kwamba, kile kilichotokea Kenya hivi karibuni ambako mahakama ilitupilia mbali maagizo ya namna hii ya polisi kujaribu kuzuia haki ya kikatiba ya vyama vya upinzani kuandamana ndicho kinachoelekea kutokea hata hapa kwetu pia.

Si hilo tu, naamini wewe IGP ulifuatilia kile kilichotokea Uganda siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kutangazwa mshindi wa urais ambako chama kimoja cha siasa kiliitisha mkutano wa hadhara na kikamwapisha Besigye ambaye wao wanaamini ndiye aliyeshinda urais.

Waganda hao ambao wamekuwa wakiiamini kwamba mgombea wanayemuunga mkono ndiye aliyeshinda japo kura zake ziliibwa, waliruhusiwa kuandamana na kukutana kwa uhuru ingawa baadaye walikamatwa.

Ni jambo la kujifunza kwamba, Waganda hawa hawakuzuiwa na ‘kuwapo kwa taarifa za kiinteligensia’ licha ya kwamba walishtakiwa baadae.

Tunachojifunza hapa ni mamlaka za dola, kama lilivyo jeshi letu la polisi, kuheshimu na kulinda haki za raia na kuepuka hatari ya vyombo vyetu kujipa dhamana ya kuwaamulia wananchi masuala yao kwa kisingizio cha taarifa za kiintelijinsia.

Je, kwa maagizo ya namna hii, Inspekta Jenerali Mangu na wenzako polisi mnatuonaje sisi viongozi wa upinzani?

Je, mnafikiri pamoja na uzoefu wetu katika siasa na uongozi tunaweza tukawa mbumbumbu wa kutambua haki zetu au hata kushindwa kujua dhamana kubwa tuliyobeba ya kuwatumikia wananchi na taifa letu?

Je, IGP Mangu na wakuu wenzako wa Jeshi la Polisi mnapotoa maagizo ya namna hiyo hamuoni kwamba mnajenga taswira tu kwamba, malengo yenu ni kutafuta jinsi ya kutumia magari ya upupu yaliyoagizwa kwa pesa nyingi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana?

Je, mmeshindwa kujifunza kwamba, kama kulikuwa hakuna vurugu kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu pamoja na kuwapo kwa kila viashiria vilivyochochewa na taasisi za dola, wapinzani hatuna sababu hata moja ya kuwa chanzo cha vurugu za namna hiyo?

IGP Mangu, pengine ni busara nikakukumbusha kwamba, vyama hivi hivi vya upinzani chini ya mwavuli wa UKAWA viliwahi kuandamana kwa maelfu kutoka Buguruni yaliko makao makuu ya CUF hadi makao makuu ya CHADEMA Kinondoni kwa amani na kwa utulivu.

Je, hukumbuki kwamba katika maandamano hayo yaliyohusisha maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam, hakuna hata sindano ya wananchi iliyopotea wala mtu kukwaruzwa?

Hayo na mengine mengi ndiyo ambayo yamenifanya nitafakari sana na kukosa jibu naposikia polisi mkituzuia kwenda vijijini kuwashukuru wananchi kwa kutuheshimu na kutupiga kura zao.

Ni nini hicho kitakachoathiri amani na utulivu? Wanachama wa vyama vipi hao ambao eti watapingana kwa sababu sisi tumeamua kuwashukuru wananchi waliotuunga mkono kwa mamilioni?

IGP Mangu, nakuomba uyatafakari haya na kuliangalia upya agizo lako, ambalo yumkini haliitakii mema nchi yetu.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika.
Edward Ngoyai Lowassa

TCRA: Taarifa ya utekelezaji agizo la ukomo wa matumizi ya simu bandia

Rais Magufuli na viongozi wa dini katika futari iliyoandaliwa Ikulu

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' na wagemi wengine wakipakua chakula katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika foleni na wageni wake kwenda kuchukua chakula wakati wa kufuturu katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipongezwa na kaimu Mufti Sheikh Hamid Masoud Jongo baada ya kuongea machache katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Abdallah Mnyasi katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni mbalimbali katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Shamim Khan katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016. Kushoto ni Mke wa rais Mama Janeth Magufuli akifuatiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaliminia na wageni waliohudhuria futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016