Kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya Tanzania leo Juni 23, 2016


Diallo amwomba radhi Dk Mwakyembe na kupiga marufuku gazeti la DIRA kusomwa StarTv

Wakati Mhariri wa Gazeti la Dira na mwenzake wako mahakamani kujibu mashitaka ya tuhuma za kuandika na kusambaza taarifa za uongo kwa lengo la kusababisha hofu nchini, uongozi wa StarTV umepiga marufuku gazeti hilo kusomwa asubuhi na kumwomba radhi Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe kwa usumbufu aliopata kwa kituo hicho cha runinga kulisoma gazeti hilo tata siku ya Jumatatu tarehe 20 Juni, 2016.

Taarifa kutoka ndani ya Sahara Media Group Ltd, wamiliki wa StarTv, zimesema msimamo huo ulichuliwa na kiongozi wao mkuu Anthony Diallo jana na taarifa hizo zimethibitishwa leo kwa njia ya simu na Dk. Mwakyembe.
"Ni kweli nimeongea na Diallo, nimeelewa changamoto za kuongoza watu wengi na nimepokea apology yao, jambo ambalo ni uungwana.
"Nimefarijika kuwa nao wametambua kuwa gazeti hilo halina viwango, hivyo hawatalisoma tena asubuhi", alisema Dk. Mwakyembe.
Wakati huohuo, Waziri huyo mwandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tano amesema maandalizi ya kufungua kesi ya kashifa dhidi ya mmiliki, mhariri, mchapishaji na wasambazaji wa taarifa za uongo za gazeti hilo yanaendelea vizuri.

Kuna mchezo mchafu unaendelea ziwa Natron?

(photo: viroola.com)
Mgogoro ulioibuka kati ya kampuni ya Wingert Windrose Safaris (Tanzania) Ltd (WWS) na Green Mile Safari Company Ltd (GM) unazidi kuibua maswali mengi baada ya kubainika kuwapo kwa mchezo mchafu ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mchezo huo mchafu umebainika kutokana na kughushiwa kwa ramani halali iliyotolewa kabla ya mwaka 2011 kwa lengo la kuwabeba wamiliki wa kampuni ya Green Mile Safari Company Ltd.

Bila kufuata taratibu, baadhi ya maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa nia ovu ya kumpotosha Waziri, walianza mbinu za kubadili ramani ya vitalu katika eneo la Ziwa Natron kwa nia ya kubadili jina la kitalu cha GM kutoka Lake Natron Game Control Area (GCA) North kwenda Lake Natron GCA East kwa kubadili ramani rasmi kuhalalisha nia yao hiyo.

Historia

Mnamo Septemba 6, 2011 Wizara iligawa vitalu na kuipatia kampuni ya Green Mile kitalu Lake Natron GCA North, na siku hiyo hiyo (Septemba 6, 2011) wakaigawia Wingert Windrose Safaris kitalu kiitwacho Lake Natron GCA North South.

Wizara ya Maliasili na Utalii, Februari, 2012 ilitangaza mgawanyo wa vitalu hivyo na kuonesha kwamba Wingert Windrose Safaris wamepewa vitalu vya Moyowosi GR (S) na Lake Natron GCA (N. South) wakati Green Miles Co. Ltd waligawiwa Selous GR MK1 na Lake Natron GCA North.

Tangazo hilo lilitolewa hadharani katika Maonesho ya Uwindaji ya Safari Club International (SCI) Hunting Show, Las Vegas, Marekani; ambalo pia liliambatana na taarifa ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige; tangazo ambalo haliwezi kubadilishwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori pekee.

Ilipofika Januari 3, 2013, takriban miezi 16 baada ya mgawanyo wa vitalu kufanyika, Wingert Windrose Safaris ikakuta kipeperushi cha Green Miles katika kongamano la uwindaji la Dallas Safari Club, lililofanyika Dallas, Marekani. Mkurugenzi Mtendaji wa Green Miles, Salum Awadh, alihudhuria kongamano hilo kama mgeni na si mshiriki, lakini alikuwa akigawa vipeperushi kwa wageni kutafuta biashara.

Katika vipeperushi hivyo alivyokuwa akigawa Salum Awadh wa Green Miles, kulikuwa na ramani inayonesha kuwa kitalu cha Wingert Windrose Safaris cha North South, lakini sasa kimepewa jina la Lake Natron GCA East, bila hata ya kuwapo mchakato wa kisheria wa kugawa upya ama kutangazwa kwa zabuni ya kugawa upya.

Maofisa wa Wingert Windrose Safaris walimkabili Salum Awadh katika kongamano hilo na kuhoji kuhusu ramani iliyopo katika vipeperushi vyake na akatoa jibu la kushitusha kwamba “Green Mile wamepata barua kutoka kwa Waziri wakijulishwa kwamba jina la kitalu walichogawiwa Green Mile cha Lake Natron GCA North limebadilishwa na kuitwa Lake Natron GCA East”.

Hakuweza kutoa ushahidi wowote wakati huo. Hata hivyo, Wingert Windrose Safaris inaendelea kusisitiza kwamba, mabadiliko ya majina ya vitalu hayawezi kubadili eneo kilipo kitalu, hata kingeitwa ‘Juma’ au ‘John’.

Ilibainika baadaye kwamba Green Miles walipewa barua na Mkurugenzi wa Wanyamapori Januari 7, 2013, siku chache baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Green Miles Salum Awadh kudai kwamba wamepewa barua na Wizara alipokuwa katika kongamano la uwindaji, Dallas Marekani.

Awali, hadi Januari 2013 kulikuwa na juhudi za kutaka kupatiwa ramani rasmi na Wizara, Wingert Windrose Safaris iligonga mwamba kupatiwa ramani ya kitalu chao cha Lake Natron GCA North South walichogawiwa Septemba 6, 2011. Ramani za vitalu vyote vya Wingert Windrose Safaris zilipatikana kutoka wizarani isipokuwa kile cha eneo la Lake Natron.

Maelezo ya utata wa Green Miles kujua uwepo wa barua hata kabla haijaandikwa na kuwa na ramani kabla hata ya kutolewa rasmi, kunayapa uzito madai ya Wingert Windrose Safaris kwamba kulikuwa na hila na nia ovu dhidi yao, na ndiyo sababu hasa ya kutotolewa kwa ramani rasmi kwa wakati ili kutoa nafasi kwa maofisa waovu wa wizara kughushi ramani halisi kuwabeba Green Miles.

Hata barua yenyewe ya Januari 7, 2013 iliyosainiwa na Profesa Jafari Kideghesho, ilikiri kuwa Green Miles walipewa kitalu kiitwacho Lake Natron GCA North, lakini barua hiyo ikaeleza kwamba jina hilo lilikosewa kutokana na jiografia ya eneo hilo na hivyo wizara imo katika mchakato wa kubadili jina la eneo hilo na kuwa Lake Natron GCA East na kwamba Waziri angeandika barua kujulisha kampuni husika, jambo ambalo halijafanyika na kwa hiyo hadi sasa hakuna mabadiliko rasmi yaliyofanyika zaidi ya kuwapo hila za kubadilisha.

Januari 25, 2013 Wingert Windrose Safaris ilikutana na Profesa Kideghesho na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI katika kongamano la kimataifa la Safari Club (SCI), lililofanyoka Reno, Marekani na wote walikana kufahamu chochote kuhusu mabadiliko ya mgawanyo wa vitalu wala majina katika eneo la Ziwa Natron; jambo ambalo linazidisha utata kwani inawezekana vipi mtu aliyesaini barua ya Januari 7, 2013 kukana kufahamu kilichoandikwa humo.
Mapema Februari 2011, ramani ya mgawanyo wa vitalu katika eneo la Ziwa Natron, ilipatikana kutoka TAWIRI Idara ya GIS inayoonesha wazi vitalu vilivyotangazwa Februari 2011 na Wizara.

AIBU KWA WIZARA

Mnamo Februari 14, 2013, maofisa wa Wizara wakiongozana na Naibu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, walikutana na maofisa wa Wingert Windrose Safaris, na kuonesha ramani kwenye projekta wakidai kwamba ramani hiyo ni ya Februari 2011 kabla ya kutangazwa vitalu.

Ramani hiyo ilikuwa katika mfumo wa ‘PDF’ file na maofisa wa Wingert Windrose Safaris walipobonyeza kwenye ‘properties’ katika ramani hiyo ilionesha kwamba imetengenezwa Februari 2013 na si 2011 kama walivyodai maofisa hao na hivyo kuwa aibu kubwa kubainika kuwa walighushi.

Kwanini ramani hiyo ilighushiwa na kurekebishwa kutoka ramani halisi ya mwaka 2011, ni maswali ambayo majibu yake wanayo wizara.

Kwa hiyo ni dhahiri kwamba Januari 2013; miezi 22 baada ya vitalu kutangazwa, baadhi ya maofisa waovu ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii, walijaribu kughushi ili kubadili majina ya vitalu Lake Natron GCA North kuwa East ili kuweza kuwapatia Green Miles Safaris kama inavyoonesha kwenye ramani iliyotolewa na TAWIRI.

Maofisa wa Wingert Windrose Safaris walikutana na Mkurugenzi wa Wanyamapori na maofisa wake katika ofisi za Wizara, jengo la Mpingo Mei 24, 2013 kujadili utata uliojitokeza na kwa mara nyingine inaoneshwa ramani iliyo katika mfumo wa ‘PDF file’ ikidaiwa kuwa imetengenezwa mwaka 2011, lakini baada ya kuingia kwenye ‘properties’ inaonesha tena imetengenezwa mwaka 2013.

Hatua zote hizo za kughushi zimethibitisha nia ovu ya maofisa wa Wizara kujaribu kupindisha ukweli kwa nia ya kuwafurahisha wamiliki wa Green Miles ambao baada ya kugawiwa kitalu chao cha Lake Natron GCA North, walitembelea eneo hilo na kutolipenda kutokana na kuwapo majabali ambayo yangewazuia kufanya uwindaji wa kufukuza wanyama kwa magari kama walivyozea japo kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu za uwindaji.
Video ifuatayo imeongezwa na mdau kwenye kisanduku cha maoni hapo chini....Dk Vincent Tarimo akielimisha kuhusu uvimbe katika njia ya uzazi - myoma, fibroids


Kitwanga arejea kutoka Israel: Nina nguvu na matumaini mapya


ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema yupo imara na amerejea nchini akiwa na matumaini mapya.

Pamoja na hali hiyo, amesema kuwa hivi sasa anajipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anaisaidia nchi pamoja na wapigakura wake na kuwa na maendeleo ya kweli na Jumatano ya Julai 29, ataripoti bungeni.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu, baada ya kurejea akitokea nchini Israel ambako alikwenda kwa shughuli zake binafsi.

Alisema licha ya mtihani uliomkuta, kwa sasa yupo imara kwa ajili ya kuwatumikia wapigakura wake kwa kuwawakilisha vema ndani ya Bunge.

“Niko imara kabisa na nina nguvu na matumaini mapya, nimeingia nchini jana (juzi) nikitokea nchini Israel ambako nilikuwa na shughuli zangu binafsi. Unajua mimi ni mtaalamu (wa mawasiliano) na wewe unajua kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya nini.

“Kifupi ninasema nilikwenda Israel kwa shughuli zangu binafsi kabisa ambazo kwa kipindi cha wiki tatu nilizokuwa huko nimefanya. Hata wanaosema nilikwenda kulia kwa Bwana nao ni mawazo yao, maana unajua ile ni nchi takatifu kutokana na historia yake,” alisema Kitwanga.

Alipoulizwa amepokeaje hatua ya kufutwa kwake kazi na Rais John Magufuli kwa kile kilichoelezwa ni ulevi, alisema kwa sasa hawezi kusemea jambo hilo kwani aliyemteua ndiye mwenye mamlaka ya kumwajibisha.

“Rais ni mtu mkubwa anaweza kufanya jambo lolote ili mradi havunji sheria, hata kilichotokea kwangu ni mamlaka yake halali, ingawa Mungu ndiye muweza wa kila jambo. Mimi ni Mkristo safi, nasi tumefundishwa kusamehe saba mara sabini na kusahau yaliyopita,” alisema.

Akieleza mikakati yake, Kitwanga alisema kuwa baada ya kuripoti bungeni wiki ijayo, atakuwa na ziara ya wiki tano ndani ya jimbo lake ambako atazungumza na wapigakura wake na kueleza yaliyomsibu hatua kwa hatua.

“Sitaki kuingia ndani sana ila mengine nitayasema nikiwa jimboni, lakini si kwa lengo la kubishana na mtu, na uzuri kila hatua ambayo nimepitia hata wapigakura wangu walikuwepo kwa uwakilishi wa madiwani wa Misungwi ambao walikuwa mjini Dodoma,” alisema.

Mei 21, mwaka huu, Rais Magufuli alimng’oa Kitwanga kuhudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutokana na madai ya ulevi, huku taarifa zaidi za ndani zikieleza kuwa alianza kushughulikiwa bila yeye mwenyewe kujua.

Pamoja na uamuzi huo wa Rais Magufuli, imeelezwa kuwa Kitwanga pamoja na timu yake walikuwa wakifuatiliwa nyendo zao na makachero.

Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili kuwa moja ya taarifa ambazo ziliwasilishwa kwa Rais Magufuli ndiyo iliyomlazimu kuchukua hatua hiyo.

“Unajua Kitwanga alikuwa akishughulikiwa muda mrefu bila yeye mwenyewe kujua, na hata kuondolewa kwake hadi sasa haamini. Wapo walioeleza kuwa baada ya kuwasilisha bajeti yake Mei 16, mwaka huu, alikwenda kulala Morogoro badala ya nyumbani kwake mjini Dodoma katika eneo la Sengia (Site11).

“Lakini pia inadaiwa kwamba kwa muda amekuwa halali nyumbani kwake na kwenda katika moja ya hoteli (jina linahifadhiwa) mjini Dodoma ambako hulewa hadi asubuhi jambo ambalo si la kweli, ni kama mkakati wa kumshughulikia na si hivyo tu hata baadaye zilitolewa taarifa kuwa yupo Morogoro ambako pia watu walimfuatilia kwa karibu, lakini kwa bahati nzuri hakuwepo.

“Tena si hilo tu, hata pia eti wanadai alilewa sana kwa kunywa Vodka hali ya kuwa hatumii kinywaji hicho na bila kujijua tangu usiku alipokuwa na madiwani wake yaani Mei 19, alikuwa akifuatiliwa na vyombo vya dola, tena walikuwa wakitumika wanawake ambao kama ndio walikuwa wakiandaa taarifa mbaya dhidi yake,” alisema mtoa habari wetu ambaye yupo karibu na mbunge huyo wa Misungwi.

Chanzo hicho cha habari kilisema kuwa pamoja na hali hiyo, wapo baadhi ya vigogo kutoka katika mashirika na taasisi nyeti za Serikali ambao walikuwa na vita ya kufa na kupona dhidi ya Kitwanga, hadi kufikia kufanya vikao vya siri vya kumshughulikia.

Kilisema kuwa mipango hiyo ilipangwa kwa ustadi mkubwa, na kwamba tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kuna baadhi ya watu walikuwa wakimfutilia kwa karibu wakiwemo ndani ya idara zilizokuwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

“Unajua huyu bwana alianza kushughulikiwa muda kidogo tangu siku ilipotolewa taarifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyoeleza kwamba naye hakujaza fomu ya maadili ya viongozi wa umma, yeye pamoja na mawaziri wenzake akiwemo Balozi Augustino Mahiga na January Makamba, ingawa nguvu kubwa ilikuwa kwake.

“Na tangu wakati huo haukupita muda kidogo likaibuka suala la Lugumi na kama unakumbuka hapo alikuwa na vita ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uhamiaji ambako kote huko kuna watu waliwajibishwa,” alisema mtoa habari wetu.

Pamoja na hali hiyo, katika kile ambacho kilikuwa kikiwatesa baadhi ya watu ndani ya Serikali, ni hatua ya ukaribu kati yake na Rais Magufuli ambao kuna wakati zilisambazwa video katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa na kiongozi huyo wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Katika video hiyo anaonekana Kitwanga akiwa na Rais Magufuli katika moja ya uwanja wa ndege ambako alikuwa akimuhamasisha achukue fomu ya kuwania urais, jambo ambalo alitekeleza baadaye na kufanikiwa kupita katika mchujo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk Yonazi atamka hatua anayotaka TSN ifikie


Dk Jim James Yonazi alitangazwa rasmi jana kupitia taarifa iliyotolewa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuwa ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) tangu Juni 18, 2016.

Dk Yonazi amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuona anaweza kumsaidia kazi kupitia kampuni hii ya magazeti na kusema amepokea uteuzi huo kwa moyo mkunjufu.

Ameahidi kufanya kazi kwa weledi, kama ambavyo Rais Magufuli amemtaka afanye kuongoza kampuni hii, inayozalisha magazeti ya HabariLeo, HabariLeo Jumapili, Daily News, Sunday News na SpotiLeo.

Alitoa mwito kwa wadau mbalimbali, kushirikiana na TSN kufanya magazeti ya serikali kuwa bora na yenye kuleta changamoto katika tasnia ya habari.

Alisema anatarajia kufanya kazi na watu mbalimbali na jambo ambalo anatamani kuona, ni ubunifu, habari za kweli na zinazokwenda na wakati.

Akieleza mtazamo wake kuhusu tasnia ya habari na mambo ambayo analenga kuyafanya baada ya uteuzi, Dk Yonazi alisema wananchi na hata dunia kwa ujumla, ina hamu ya habari za kutoka Tanzania.

Alisema panahitajika ubunifu na mikakati kuhakikisha magazeti ya TSN yanapeleka habari, siyo tu hapa nchini, bali pia kufikia nchi za nje kama ilivyo kwa mashirika ya habari ya kimataifa ya BBC na CNN.

Alisema wakati magazeti ya TSN sasa yanafika nchi za Afrika Mashariki, yanatakiwa kufika pia kwenye masoko ya kanda nyingine na nje ya Afrika.
“Tufike mahali, magazeti yawe kwenye viganja vyetu…ningependa sana kufikia hatua hii” 
alisema Dk Yonazi, akimaanisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususan simu, kutumiwa na wananchi wengi kupata habari.

Alisema anatamani hata watu wa mataifa mengine, waandike habari zao kutoka kwenye magazeti ya nchini hususani ya serikali.

DK YONAZI NI NANI?

Dk Yonazi ana Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Serikali Mtandao ya Chuo Kikuu Groningen cha Uholanzi na ana Shahada ya Uzamili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA ) na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Keele, Uingereza.

Amewahi kuwa mhadhiri mwandamizi, mtafiti na mshauri katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam. Pia amefanya utafiti katika masuala mbalimbali kuhusu uvumbuzi, mipango mikakati ya kiutawala katika Tehama.

Aidha, amebobea katika masuala ya mipango ya kiutawala katika Tehama, Uvumbuzi katika Utawala, Serikali Mtandao na Marekebisho ya Sekta ya Umma, Tehama katika Maendeleo na uvumbuzi katika Tehama. Vile vile amehusika katika mikakati mbalimbali ya Tehama hapa nchini na Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Pia amewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za kimataifa na za nchini katika ngazi za Umeneja na majukumu makubwa ya usimamizi wa kitaaluma. Dk Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Kompyuta katika chuo cha IFM, akisimamia maendeleo katika ugunduzi na ubunifu, iliyowezesha chuo hicho kufanya vizuri katika eneo hilo.

Amewahi kuwa mjumbe wa bodi kadhaa, ikiwamo Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyovunjwa na Rais Magufuli mwishoni mwa Aprili mwaka huu na Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Arusha. Pia ni mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Tehama katika Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) na Mratibu wa Kituo cha Tehama cha Utafiti na Ubunifu (CiRi). Source: Habarileo;Picha:FK Blog - 2014.

Rais Magufuli: You better leave! Kama unapataga hasara, kwa nini unaendelea kuwa hapa? Si ondoka?


Rais Magufuli ameitaka BoT kujiimarisha katika kusimamia maduka ya kubadili fedha za kigeni ambayo baadhi yake husafirisha fedha nje ya nchi na kutakatisha fedha haramu zikiwemo zinazotokana na dawa za kulevya.

Ametaka makampuni yanayowekeza kwenye madini kuondoka ikiwa kila mwaka kwa miaka nenda rudi, yanadai kuwa yanapata hasara lakini bado wanaendelea kuwepo. Amezitaka BoT na Hazina kushughulikia hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kumkaribisha aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Balozi wa China nchini Dkt Lu Younqing baada ya kuwa na mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na ujumbe wa Balozi wa China nchini Dkt Lu Younqing baada ya kuwa na mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa Benki kuu (BOT) jijini Dar es salaam Juni 22, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua Vitabu viwili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa Benki kuu (BOT) jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Magavana na Manaibu Magavana na menejimenti ya BOT kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Bodi ya wakurugenzi wa BOT kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN Juni 22, 2016Kamishna Kova aagwa rasmi kustaafu kazi ya utumishi wa umma


Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi.

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi

Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki.

Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki


Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi. 
 • Picha:Frank Geofray-PT

Call: Master’s Thesis Programme in knowledge exchange for food and nutrition security


Complex societal challenges such as food insecurity and malnutrition require new inclusive and innovative solutions. Such solutions can be created when tomorrow's experts and decision makers demonstrate high degree of professional expertise in their field of work. Moreover, they require transdisciplinary skills and experience in facilitating multi-stakeholder knowledge exchange and learning processes.

The aim of the Master’s Thesis Programme is to integrate Master students in ongoing food and nutrition security projects in the field of international research and development cooperation and to strengthen their analytical, theoretical and communicative skills. The Master’s Thesis Programme is designed to deliver theoretical and practical skills focusing on the food and nutrition security challenges in East Africa. To explore the real life beside their thematic content-related analysis, the participants will undertake fieldwork in the frame of different ongoing international projects in Kenya, Tanzania and Ethiopia. Thus, the participants will learn what multi-stakeholder knowledge exchange processes are, why they are needed and what their key elements are. Moreover, the students will get an insight of how to develop knowledge exchange strategies, engage different stakeholders in transdisciplinary research, design and facilitate successful knowledge exchange activities and use modern ICTs media to exchange knowledge and connect innovators.

The overall goal of the Master’s Thesis Programme is to qualify and link professionals and enable them to develop innovative and inclusive approaches for collaboration across boundaries of academia, politics and practice and to tackle growing societal challenges such as food insecurity and malnutrition.

The shape
 • Twelve months intensive Master Programme / July 2016 – July 2017
 • Workshops/trainings and participation at one international conference
 • Master’s Theses and at least one peer-reviewed article
The target group
 • Registered Master students at Kenyan, Tanzanian, Ethiopian or German universities with excellent performance in their current study
The thesis topics

HORTINLEA topics (open for application)
 1. Improving schoolchildren's nutrition and education through inclusive innovations
 2. Inter- and transdisciplinary knowledge integration into the disciplinary curricula of universities and educational organisations in East Africa
 3. Market trends and agricultural policies in Kenya - Opportunities and risks for smallholder AIV farmers
 4. Inclusive Horticultural Knowledge Exchange and Information Management Systems
 5. Monitoring and evaluating inter- and transdisciplinary food and nutrition security interventions in East Africa
 6. Integrating traditional and academic knowledge system approaches
Topics in collaboration with our partners
 1. Improving food and nutrition security through AIVs at Kakuma refugee camp (2 sub-topics)
 2. Improving food and nutrition security through traditional knowledge and food systems in Ethiopia (2 sub-topics)
 3. Improving food and nutrition security through traditional knowledge and food systems in Tanzania (2 sub-topics) 
HORTINLEA topics (closed for application)
 1. Finance for smallholder farmers in East Africa
 2. Using ICTs for exchanging horticultural knowledge and information
 3. Market Trends and Consumption of AIVs in the Upper Eastern Region of Kenya

Majibu ya Waziri kuhusu fidia na mafao kwa wafanyakazi wa migodini wanaoumia makazini


[video] Majibu ya Waziri kwa Ali Saleh ya sababu za Tanzania kufungua ubalozi Israel


[video] Mwijage: Watoto wa nyumbani hawawezi kuvaa mitumba

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, bwana Charles Mwijage amesema haoni sababu ya watanzania kuendelea kuvaa nguo za mitumba, na kuwataka wananchi na wadau wa biashara na viwanda kutowaombea watanzania ili waendelee kuvaa mitumba.


Tarehe ya Juni 20, 2016 Waziri Mwijage aliwajibu yafutayo, waliosema kuwa amepangiwa bajeti ndogo...

Taarifa kwa umma kuhusu matumizi ya majina ya kikoa cha .tz


TAARIFA KWA UMMA TOKA RAJISI YA DOT TZ

YAH: ELIMU KWA UMMA JUU YA MANUFAA YA MATUMIZI YA MAJINA YA KIKOA CHA DOT TZ (.TZ DOMAIN NAMES)

Tanzania Network Information Centre (tzNIC) au Rajisi ya dot tz ni kampuni inayoendesha na kusimamia rasilimali ya nchi (dot tz) kwa ajili mawasiliano kupitia mtandao wa Intaneti. tzNIC inapenda kuuarifu umma wa watanzania kuwa imetenga siku za Jumatatu (27 Juni 2016) na Jumanne (28 Juni 2016) kutoa elimu kwa umma juu ya kazi zake, manufaa ya matumizi ya majina ya kikoa cha dot tz (.tz domain names) na namna bora ya kuhama kutoka matumizi ya majina mengine ya vikoa kama dot com na dot org kwenda kikoa cha dot tz. Katika kipindi hicho tzNIC pia itapokea maoni mbalimbali juu ya uboreshaji wa huduma zake na nini kifanyike ili watanzania wengi wasajili na kutumia majina ya kikoa cha dot tz kwa ajili ya biashara zao, huduma zao na matumizi binafsi.

Tukio hili litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa tzNIC, Ghorofa ya 8, LAPF Millennium Towers, Kijitonyama, Dar es Salaam kuanzia saa 3 mpaka saa 10 jioni. Kabla ya tukio hili tzNIC itatoa maelezo ya utangulizi kupitia kipindi cha Jambo Tanzania (TBC) siku ya Ijumaa (24 Juni 2016) au Jumatatu (27 Juni 2016) asubuhi.

Kwa wale wa mikoani na watakaoshindwa kufika wanaweza kutupigia simu (022 2772659 au 022 2772660) au kutuandikia barua pepe kupitia [email protected]) au [email protected]

WOTE MNAKARIBISHWA

*************

Why use a .tz domain?

a) Identity
.tz brands your company/business/service with unique Tanzanian identity on the Internet. It is meant for all Tanzanians (people and entities).

b) Affordable and readily available
.tz domain fee is reasonably cheap and .tz domain space is not populated as compared to the rest

c) Credibility (Trust)
.tz has inbuilt credibility/trust due to company/business/service originality

d) Security
.tz domains are secure through DNSSEC and are managed based on Tanzania's legislations, policies and regulations.

e) Reaching out the world with equal competitive business powers
.tz domains provide global reach of customers with equal competitive powers (no one is small when it comes to business online)

f) Round the clock business operations
Business online over 24 hrs is possible with .tz domains

g) Favorable ranking with search engines
.tz domains have higher priority with most search engines when compared to .com and others.

h) Minimized cost of doing business or service provision
.tz enables one to do business or provide services online at a minimum cost compared to other means (e-commerce, e-business, etc)

i) Affordable electronic communication
.tz domains facilitate diminution of electronic communication costs

j) Local and affordable support
.tz support is available locally in both English and Swahili and as per local business environments.

Katuni: Funga mdomo...