Kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya Tanzania leo Julai 20, 2016
Taarifa ya habari ChannelTEN Julai 19, 2016Global Health Fellows Program - Strategic Information and Monitoring & Evaluation Intern

Organization: Global Health Fellows Program
Country: United States of America
Closing date: 02 Aug 2016

Global Health Fellows Program - Family Planning Communications Intern

Organization: Global Health Fellows Program
Country: United States of America
Closing date: 02 Aug 2016

Heartland Alliance is looking for a Regional Director - Sub-Saharan Africa

Organization: Heartland Alliance
Country: United States of America
Closing date: 19 Aug 2016

"Malaria No More" Fall 2016 DC Advocacy & Communications Internship, USA

Organization: Malaria No More
Country: United States of America
Closing date: 12 Aug 2016

At Malaria No More, we envision a world where no child dies from a mosquito bite. We use our innovative partnerships and focused advocacy to elevate malaria on the global health agenda, create political will and mobilize the global resources required to achieve malaria eradication within a generation.

MNM's internship program offers full-time and part-time internships for 3 to 6 months at our office in Washington, DC. We welcome student interns, particularly those with an interest in public health or international development. Our internship is unpaid. We are currently recruiting for the Fall 2016 semester.

What do you gain as an intern?


An internship with MNM will give the intern a chance to work in a small, influential advocacy organization.

What will be the type of work you will do as an intern?
 • Compile research and write various Communications documents/briefs/projects, newsletters, blogs, etc.
 • Assist with the development of power-point presentations and support other admin tasks
 • Attend DC-based events/seminars on behalf of organization
 • Provide support in preparation of conference calls, meetings, etc., including drafting meeting minutes
 • Other duties as assigned
Are you eligible for an MNM internship?

To qualify for an MMV internship you must meet the following requirements:
 • Working towards or hold a university degree (undergraduate, Master’s or PhD)
 • Fluent in English
 • Interested in global health/ international development issues
 • Willing to think strategically, express ideas clearly both orally and in writing, and work independently and as part of a team
How to apply:

This is a competitive program and candidates will be selected on merit. If you fulfill the above- mentioned criteria, please apply with the subject line “DC Fall 2016 internship – your first, last name” and sending the following materials (see below) to: [email protected]
 1. A concise cover letter explaining why you would like to be considered
 2. Your CV
No telephone calls please.

Job: Programme Director - Plan, Tanzania

Organization: Plan
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 07 Aug 2016

The Organisation

Plan International is changing. We are responding to shifts in international development and humanitarian response to ensure we make a stand for all children’s rights, through a focus on girls and other disadvantaged children. As Plan International embarks on this ambitious and exciting process across our 70+ offices worldwide, we are introducing a number of new roles within the organisation.

Plan International is an independent child rights and humanitarian organisation committed to children living a life free of poverty, violence and injustice. We actively unite children, communities and other people who share our mission to make positive lasting changes in children’s and young people’s lives. We support children to gain the skills, knowledge and confidence they need to claim their rights to a fulfilling life, today and in the future. We place a specific focus on girls and women, who are most often left behind. We have been building powerful partnerships for children for more than 75 years, and are now active in more than 70 countries.

The Opportunity


The purpose of the project is to lead, manage and implement a maternal, newborn health, and sexual and reproductive health project in Rukwa, Tanzania, to improve access to family planning and health outcomes of vulnerable young mothers and their newborns in all 4 districts of this remote region. The budget for this project is approximately USD 10.3 million.

Reporting into the Country Director of Plan International Tanzania, the Programme Director will directly supervise four senior program and operational staff and oversee project coordinators. Key focus areas will include project management, reporting, project team management and partner relations.

The Person


You must possess significant experience in leading, managing and implementing large international development projects in community based maternal newborn health, health systems, adolescent programming, sexual and reproductive health rights and/ or community development.

A proven leader with people management skills, you should also be experienced in budgeting, financial management and foreign exchange risk management.

You must demonstrate knowledge about gender and development and be able to travel regularly within Tanzania, and internationally as required. You should be fluent in English and the ability to speak Swahili would be an advantage.

Type of Role:
5 year fixed term contract

Location: Program Country Office, Dar es Salaam, Tanzania

Salary: Circa $55,000 USD per annum + benefits

Reports to: Plan International Tanzania Country Director

Closing Date:
Sunday 7th August 2016

How to apply:

To apply for this position, please click on the link below: https://career012.successfactors.eu/sfcareer/jobreqcareer?jobId=14044&company=PlanInt&username

Tamko la Wizara kuhusu usambazaji, matumizi wa vilainishi vya tendo la ngono

TAMKO LA WIZARA KUHUSU MATUMIZI NA USAMBAZAJI WA VILAINISHI KWA AJILI YA UDHIBITI WA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali za mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU nchini ambazo zimepelekea kupungua kwa viwango vya maambukizi ya VVU kitaifa kutoka wastani wa asilimia 7 mwaka 2007-2008 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011-2012. Mafanikio haya yamefikiwa kutokana na ushirikiano wa karibu kati ya Wizara na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wale wa utekelezaji wa moja kwa moja wanaofanya kazi na mikoa yote Tanzania bara. Aidha kumekuwa na uitikiaji mzuri kutoka kwa wananchi katika utekelezaji wa afua hizo.

Sambamba na mafanikio haya, tafiti mbalimbali hapa nchini zimethibitisha kuwepo kwa kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU miongoni mwa makundi maalum yaliyo katika hatari zaidi ya maambukizi kuliko kiwango kilichopo miongoni mwa jamii ya kawaida. Makundi haya ni pamoja na Wanawake wanaofanya biashara ya ngono ambayo maambukizi ya VVU ni asilimia 26, Watu wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya (asilimia 36) na Wanaume wanaoshiriki ngono baina yao (asilimia 25). Aidha, makundi haya yamekuwa na muingiliano wa karibu sana na wana jamii ya kawaida, na hivyo kupelekea hatari ya kutofanya vizuri katika udhibiti wa maambukizi ya VVU nchini.

Hali hii ilisababisha kuwepo na umuhimu wa kuongeza nguvu katika afua mbalimbali za kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya VVU miongoni mwa makundi haya, pamoja na jamii ya kawaida ili kudhibiti VVU. Kwa mantiki hiyo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbali mbali walikubaliana mikakati mahsusi ya kutoa huduma bora na rafiki kwa watu wa makundi maalum kwa kuzingatia sheria, taratibu, mila na desturi za taifa letu.

Pamoja na nia njema na jitihada za pamoja baina ya Wizara na wadau katika mapambano dhidi ya UKIMWI, imebainika kwamba baadhi ya wadau wanaotekeleza shughuli za makundi maalum wamekuwa wakikiuka taratibu za kiutendaji hasa suala la kuihusisha Wizara na Mikoa husika wanakofanyia kazi kuhusu uanzishwaji na/au utekelezaji wa baadhi ya shughuli wanazozifanya. Aidha pia katika baadhi ya maeneo, wadau hao wamekuwa wakitekeleza shughuli ambazo ziko kinyume na makubaliano waliyoingia na Wizara ya Afya.

Miongoni mwa shughuli zinazokinzana na mila na desturi zetu ni pamoja na usambazaji wa vilainishi. Ni kweli kuwa Wizara imezuia usambazaji wa vilainishi na tayari tumewasiliana na wadau hao ambao wameahidi yafuatayo:
 • Kukusanya vilainishi vilivyokuwa vimesambazwa na kuhakikisha kuwa vinateketezwa
 • Imekubalika pia kuwa wadau kwa kushirikiana na Wizara watakaa pamoja na kuangalia endapo pana fedha ambazo zingetumika kununua vilainishi, basi fedha hizo ziweze kupangiwa matumizi stahiki kulingana na vipaumbele vya Wizara na taifa kwa ujumla.
Wizara inawapongeza na kuwashukuru wadau wote kwa jitihada za dhati zinazoendelea kutekelezwa na katika kusimamia kikamilifu miongozo inayotolewa na Wizara yenye lengo la udhibiti wa ugonjwa wa UKIMWI.

Imetolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
19 Julai 2016

AfDB yamwahidi Waziri Mpango kuwa itachangia Bajeti Kuu ya Serikali 2016/2017

Waziri Mpango (Mb) (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais AfDB, Dkt. Alberic Kacou (kushoto), Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Tania Kandiero (wa tatu kushoto), baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili
BENKI ya Maendeleo ya Afrika - AfDB, imeahidi kuchangia dola za Kimarekani milioni 200, sawa na shilingi bilioni 433.6/=, kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu, Dkt. Alberic Kacou, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Ofisini Kwake Jijini Dar es Salaam.

Makamu huyo wa Rais wa AfDB aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo, Tania Kandiero, amesema kuwa mchango huo umeongezeka kwa dola Milioni 50 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka jana ambapo Benki hiyo ilichangia Dola milioni 150.
"Misaada na mikopo inayotolewa na Benki yetu kwa serikali ya Tanzania imefikia dola za Kimarekani 1.9b hivi sasa" Alieleza Dkt. Kacou
Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika Bara la Afrika kupewa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mipango yake mahiri ya maendeleo inayokidhi vigezo na viwango vya taasisi hiyo.
"Tuna malengo matano ambapo tunataka kuwekeza katika sekta ya nishati, uzalishaji wa chakula, kuiendeleza kiviwanda, kuiunganisha na kuboresha maisha ya waafrika kwa ujumla" aliongeza Dkt. Kacou
Amepongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, kwa kusimamia vizuri nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kwamba uamuzi huo utaharakisha maendeleo ya nchi.

Akizungumza na ujumbe huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameshukuru uamuzi wa Benki hiyo wa kuongeza mchango wake katika Bajeti Kuu ya serikali kupitia mfuko mkuu wa Bajeti (GBS).

Amesema kuwa serikali imedhamiria kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge), pamoja na kununua ngege tatu za abiria ili kuboresha usafiri wa anga.
"Vilevile tumeamua katika Bajeti ya mwaka huu kununua meli mpya itakayo tumika kutoa huduma Ziwa Viktoria na kukarabati meli nyingine mbili ambapo moja iko Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Viktoria ili kuimarisha usafiri wa majini" Aliongeza Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amebainisha kuwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, serikali imejipanga kukuza sekta ya viwanda ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
"Mpango huo utakwenda sambamba na kuboresha sekta ya kilimo ili malighafi itakayozalishwa na wakulima, licha ya kuinua uchumi wa wakulima wetu, lakini pia viwanda vitapata malighafi ya kutosha" alisisitiza Dkt. Mpango.
Amerejea msimamo wa serikali kuwa haitakubali kupokea misaada inayoambatana na masharti magumu na isiyo na tija kwa nchi na kwamba jitihada zinazofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo nchini zinawekezwa kwa utaratibu mzuri ili ziweze kutumika kuleta maendeleo.
"Hatutakubali misaada isiyozingatia vipaumbele vyetu na ile inayohatarisha uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe" alieleza Dkt. Mpango.
Ameeleza kuwa uamuzi wa serikali wa kukusanya mapato yake ya ndani kwa kuwahimiza watu kulipa kodi na kubana matumizi yasiyo ya lazima umeanza kuleta matunda na kuongeza pia nidhamu ya matumizi ya pesa katika jamii.

Ameiahidi Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika - AfDB, kwamba fedha waliazoahidi kuzitoa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
 • Taarifa ya Benny Mwaipaja - WFM

Rais Mstaafu wa Kenya atembelea daraja la Mwalimu Nyerere Tanzania

Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioandamana kutembelea daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki ametembelea mabanda ya maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Katika tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amimweleza Mwakilishi huyo kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa hadi ifikapo 2020 iweze kufikisha maji kwa wananchi wote kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Kalobelo aliongeza kuwa hatua hiyo itaifanya Tanzania kufikisha maji kwa wakazi wa mijini kwa asilimia 95 na kwa wakazi wa vijijini kw asilimia 85.

Aidha, katika hatua nyingine, Mwakilishi huyo alitembelea barabara iliyopewa jina la Mwai Kibaki inayoanzia eneo la Morocco hadi njia panda ya Kawe jijini Dar es salaam pia alitembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.

Maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika mwaka huu yanayoendelea jijini Dar es salaam yanaongozwa na kaulimbiu inayosema “Kufikia lengo la Mendeleo Endelevu (SDGs) juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira.”
 • Taarifa hii (Picha/Maandishi) imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya serikali. Imeandaliwa na Eleuteri Mangi


Balozi wa Kenya nchini Tanzania Ali Chirau Mwakwere akimuonesha Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (wa pili kulia) eneo la daraja la Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es salaam.Katibu wa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati), Profesa Nick Wanjohi akifafanua jambo kwa mwakilishi huyo alipotembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.


Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Wiki ya Maji Afrika (Sylivester Matemu) wakati wa maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.


Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki akisalimia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo leo jiji Da es salaam.

Orodha ya majina ya wanafunzi wa SUA ambao (1) Hawajahakikiwa (2) Hawatalipwa na Bodi ya Mikopo

 1. Bofya maneno yafuatayo kufungua orodha ya wanafunzi SUA ambao hawajahakikiwa

 2. Bofya maneno yafuatayo kufungua kabrasha lenye Lorodha ya wanafunzi wa SUA ambao hawatalipwa na HESLB

Story Correction: South African climber dies on Mount Kilimanjaro

Wajawazito walazwa sakafuni katika jengo la CCM lililogeuzwa wodi

Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto akimpa pesa ya matumizi mzazi aliyejifungulia chini katika moja kati ya vyumba vya ofisi ya CCM kijiji cha Kihesa Mgagao jana ,wajawazito hao hulazwa chini kutokana na chumba kilichopo katika zanahati ya kijiji kutokuwa na uwezo wa kuhudumia wajawazito watatu
Na MatukiodaimaBlog 

WAJAWAZITO katika kituo zahanati ya Kihesa Mgagao wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wamekuwa wakilala chini katika godoro chini kwenye ofisi ya CCM kijiji cha Kihesa Mgagao kutokana na zahanati hiyo kukosa chumba kikubwa na vitanda vya kutosha.

Hata hivyo Zahanati hiyo imekuwa ikiwalaza pamoja wajawazito na wagonjwa wa kawaida hasa pindi wagonjwa wanaofika kutibiwa kuzidi wawili kwa siku.

Mwandishi wa mtandao huu wa MatukioDaimaBlog aliyefika zahanati hapo alishuhudia hali hiyo ya wajawazito hao kulazwa sakafuni baada ya chumba kidogo chenye vitanda viwili pekee cha kujifungulia kwenye Zahanati hiyo kuwa na wanawake wagonjwa wengine ambao walikuwa wajifungua.

Uongozi wa Zahanati hiyo umedai kuwa changamoto katika zanahati hiyo zipo nyingine ikiwemo ya ukosefu wa chumba cha kupumzika wagonjwa hali iliyowalazimu kuomba baadhi ya vyumba katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijiji cha Kihesa Mgagao ili vitumike kama wodi la kupumzisha wagonjwa na vyumba vya kujifugulia kwa wajawazito wanaofika Zahanati hiyo.

Pia ulisema hata hivyo wagonjwa hao wamekuwa wakilala gizani kutokana na kukosekana na taa za solla ama za kawaida kwa ajili ya matumizi na kuwa shughuli za kuwahudumia wagonjwa hao huwa ni shida kuzifanya gizani hivyo hulazimika kutumia tochi.

Alisema kimsingi zahanati hiyo iliyojengwa mwaka 2008 ndio ambayo inatumika kama kituo cha afya cha kata kutokana na ujenzi wa Kituo cha afya kutokamilika hivyo iwapo wajawazito watafika zaidi ya wawili kwa siku na wagonjwa wengine basi hulazimika wote kuchanganywa katika chumba kimoja kwenye jengo la CCM.

Pia alisema jingo hilo linalotumika kama wodi kiafya si salama kwa wagonjwa kwani halina mazingira mazuri ya kiafya huku suala la chombo cha kuchomea taka (Sterility)zinazotumika Zahanati hapo hakuna hivyo wamekuwa wakichoma kienyeji katika shimo la kawaida jambo ambalo ni hatari zaidi kiafya.

Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto ameahidi kuwasaidia ujenzi wa chumba kikubwa ambacho kitatumika kama wodi la wagonjwa na wajawazito wakati ujenzi wa kituo cha Afya ukiendelea .

Alisema kuwa amesikitishwa na hali hiyo ambayo aliiona katika Zanahati hiyo jana na kuwa ameutaka uongozi wa kijiji kuwasiliana na Halmashauri ili eneo lililopo liweze kutumika kuongeza jengo ambalo litatumika kama wodi

Wakati huo huo mbunge Mwamoto amekabidhi pesa za kununulia taa mbili zinazotumia nishati ya mwanga wa jua (solar) ambazo zitatumika wodini wakati huu ambao zoezi la kusogeza umeme wa Rea likiendelea na kuwa tayari amemuomba meneja wa TANESCO  mkoa kufika leo kutazama eneo hilo ili nguzo za umeme zilizoishia gereza la kihesa Mgagao zifiki kijijini hapo, na kuwa suala la vitanda ataendelea kulifanyia kazi.


Mama aliyejifungua akiwa amejipumzisha katika chumba cha ofisi ya CCM kwa kutandikiwa godoro sakafuni


Ofisi hiyo pia hutumika kama stoo


Zahanati ya Kihesa Mgagao


Jengo la CCM linalotumika kama wodi


Shimo la kuchomea taka


Mzazi akiwa amelala ndani ya jengo la CCM