Uganda defends decision to abandon Kenya for Tanzania in oil pipeline construction

The government of Uganda defended its decision to construct an oil pipe line through Tanzania, breaking its silence on why it had abandoned an earlier plan to build it through Kenya.

Ugandan legislators on Tuesday questioned why government had abandoned an earlier plan to construct the oil pipeline from Lake Albert to Kenya's Lamu Port.

The pipeline will now be built through Tanzania'a Tanga Port.

"The government changed to Tanzania because it's cheaper than using Kenya's route to Lamu Port," Dozith Abeinomugisha, the assistant commissioner in charge of oil refinery in the Energy ministry, said.

Abeinomugisha said the Kenyan route would delay the project, as it lacks existing roads coupled with the fact that it is always affected by monsoon winds for up to three months annually.

The 1,400km pipeline will connect Uganda's western region, near Hoima – where big oil reserves have been discovered – with Tanzania's port of Tanga.

The project is expected to cost about $4 billion and create 15,000 jobs.

National Level Implications of Implementing the SDGs in Tanzania


This study investigated the progress towards formulating, adopting and implementing Sustainable Development Goals (SDGs) in Tanzania. The 15 years of implementation of the Millennium Development Goals (MDGs) in Tanzania proved that the country still needs to do more to eradicate poverty. Inadequate budgetary resources had been one of the major hurdles encountered during MDGs implementation. The present study reveals that dependence on traditional sources of financing had been the major reason for the country’s failure to effectively finance its development agenda.0

It is therefore recommended that the government explores non-traditional revenue sources for financing of the SDGs such as public-private partnerships (PPPs). Integrating and mainstreaming the SDGs in Tanzania’s national planning process can only be effective by strengthening the capacities of all key players identified in the planning process. Thus, the government and other important stakeholders should develop the capacities of the local government officials and allocate sufficient financial resources for effective mainstreaming and integration of the SDGs
to the grassroots level.

Author: Oswald Mashindano, Solomon Baregu

Kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya Tanzania leo Julai 22, 2016

USA rolls out "STEPS", a program to help it's citizens traveling abroad stay safe


The Smart Traveler Enrollment Program (STEP) is a free service to allow U.S. citizens and nationals traveling abroad to enroll their trip with the nearest U.S. Embassy or Consulate.
 • Receive important information from the Embassy about safety conditions in your destination country, helping you make informed decisions about your travel plans.
 • Help the U.S. Embassy contact you in an emergency, whether natural disaster, civil unrest, or family emergency.
 • Help family and friends get in touch with you in an emergency.
Find out more here: https://step.state.gov/step

You can send requests now to have your Twitter account verified


On Tuesday, July 19th, Twitter announced that it has created an online application process (click here to start) for Twitter accounts to receive verified status.
Verified accounts on Twitter allow people to identify key individuals and organizations on Twitter as authentic, and are denoted by a blue badge icon. An account may be verified if it is determined to be of public interest. Typically this includes accounts maintained by public figures and organizations in music, TV, film, fashion, government, politics, religion, journalism, media, sports, business, and other key interest areas.
AndroidPolice notes that:
There are several account requirements before you can even submit a request. For example, you need to have a profile picture, a verified phone number, a verified email, a birth date (for personal accounts), and so on. When submitting a request, you'll need to supply at least two links that help verify your identity and noteworthiness. You will also be asked to upload a photo ID (Twitter says it may ask for this, but it's on the form).
After the application is submitted, Twitter will reach out via email to respond. Presumably you have to be at least somewhat of a known quantity on the internet to get the blue badge. If you are denied, you can try again 30 days later.

Wasifu wa Dk Magufuli, mtarajiwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha MapinduziWASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI


MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM

1.0. MAISHA

Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke na watoto saba. Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.

Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora za jamii na kero zao zinaondoka.

2.0. ELIMU NA MAFUNZO


Rais Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera. Mwaka 1977 alihamia shule ya sekondari ya Lake iliyopo Mkoani Mwanza na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa .

Mwaka 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati. Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la kujenga Taifa kikosi cha Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi 1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni, Arusha. Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.

Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza ya Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati. Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988. Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Salford cha Uingereza. Mwaka 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.

3.0. UZOEFU WA NDANI YA SERIKALI

Baada ya kuhitimu masomo yake ya Stashahada ya Ualimu, mwaka 1982 hadi 1983 Dkt. Magufuli alikuwa Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Sengerema iliyopo Mkoani Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1989 alijiunga na Chama Cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza, ambapo alifanya kazi kama Mkemia Mkuu hadi mwaka 1995.

Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoa wa Kagera. Baada ya Uchaguzi, Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2000. Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki lakini mara hii akipita bila kupingwa. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara ya Ujenzi hadi mwaka 2005.

Mwaka 2005 Rais Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki, kwa mara nyingine akipita bila kupingwa. Baada ya uchaguzi, Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi hadi hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya nne kuwa Mbunge lakini, kufuatia mgawanyo wa majimbo uliofanyika, mara hii katika Jimbo jipya la Chato. Baada ya uchaguzi, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Wakati akiwa Mbunge na Waziri, Dkt. Magufuli amefanya shughuli na kushika nyadhifa kadhaa ndani na nje ya nchi. Mwaka 2014, Dkt. Magufuli alishiriki katika Bunge Maalum la Kutunga Katiba Mpya akiwa ni Mjumbe wa Bunge hilo. Aidha, wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).

Tarehe 25 Oktoba, 2015 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tarehe 5 Novemba, 2015 aliapishwa kushika rasmi wadhifa huo.

4.0. UZOEFU WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

Rais Dkt. Magufuli alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. Amekuwa Mwanachama mwaminifu na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

Sambamba na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Dkt. Magufuli mara zote alijitoa kukitetea Chama na kuhakikisha kinapata ushindi. Alishiriki kikamilifu kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM katika Chaguzi Ndogo zilizofayika katika majimbo ya Busanda, Biharamulo Magharibi na Igunga na kupata ushindi. Katika Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 11 – 12 Novemba mwaka 2012, Dkt. Magufuli alikuwa miongoni mwa Mawaziri wachache waliopata fursa ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya Mwaka 2010 – 2015. Alielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani, hususan katika sekta ya miundombinu.

Tarehe 11 mwezi Julai, 2015 Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ulimchagua na kumteua Dkt. Magufuli kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliinadi vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015) na kukiwezesha Chama kupata ushindi mkubwa. Tarehe 25 Oktoba, 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nafasi hiyo imemwezesha kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

5.0. UFANISI KATIKA UONGOZI

Dkt. Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu, aliye na hofu ya Mungu, mkweli, mtekelezaji wa ahadi, mwadilifu, shupavu, mahiri, mbunifu, mtafiti, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge. Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma, rushwa, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile. Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoyaamini.

Katika nyadhifa zote alizopata kutumikia alifanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Amejidhihirisha na kujipambanua kuwa ni mfuatiliaji na msimamizi wa sheria. Akiwa Mwalimu Sengerema Sekondari aliwezesha wanafunzi wote wa darasa lake kufaulu masomo ya Hesabu na Kemia aliyokuwa akiyafundisha. Akiwa Mkemia Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Nyanza alisimamia vyema ubora wa uzalishaji wa mafuta ya Pamba na kuifanya Kampuni ya Nyanza kuwa mzalishaji mzuri wa mafuta ya Pamba.

Akiwa Waziri wa Ujenzi anakumbukwa kwa kubuni na kusanifu miradi ya ujenzi wa barabara, kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati uliopangwa. Uwezo wake katika kubuni na kusanifu miradi ya barabara uliigwa na nchi majirani, ikiwemo Kenya. Ameondoka Wizara ya Ujenzi akiwa amesimamia ujenzi wa zaidi ya Kilometa 17,000 za barabara za lami, madaraja makubwa zaidi ya 14 na madaraja madogo madogo zaidi ya 7,000 na vivuko. Aidha, alisimamia vizuri taasisi mbalimbali za Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu na Wakadiriaji Majengo.

Dkt. Magufuli pia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuweka kumbukumbu ya kazi zake. Akiwa Wizara ya Ujenzi aliweza kutaja majina ya barabara zilizojengwa au zilizokuwa katika hatua za ujenzi, urefu wake, majina ya wakandarasi pamoja na gharama za ujenzi bila kusoma mahali popote. Wakati wa Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa alimwita “Askari wa Mwavuli”.

Akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisimamia upimaji wa ardhi za vijiji na viwanja vya makazi, na kushughulikia migogoro mingi ya ardhi iliyowahusu wananchi wa maisha ya chini. Wakati akiwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi alikuwa maarufu wa kutambua na kutaja idadi ya mifugo, kama vile samaki, ng√≥mbe, mbuzi, kondoo, kuku, mbwa n.k. Kitendo cha kukamata meli ya kichina iliyokuwa ikivua samaki kwa wizi ndani ya Bahari Kuu ya Hindi eneo la Tanzania kilidhihirisha uzalendo kwa Taifa lake. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete alimpachika jina maarufu la “Tingatinga”.

Sifa hizi nzuri ameendelea nazo hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais. Katika miezi michache ya uongozi wake amethibitisha anatekeleza ahadi. Aliahidi kutoa elimu bila malipo na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Ameweza kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wasio waaminifu, wala rushwa, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa hakika Dkt. Magufuli anaakisi uongozi bora unaopaswa kuigwa na viongozi wengi Barani Afrika na Dunia.

6.0. DHIMA YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 – 2020) NA MALENGO YAKE MAHSUSI


Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 inazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne;- Kwanza kuondoa umaskini, Pili, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, Tatu, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, na Nne, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya Watanzania na mali zao.

Sambamba na kutekeleza mambo hayo makubwa manne, kipindi cha Kampeni na wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 Rais Dkt. Magufuli alitaja malengo mahsusi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Malengo hayo ni haya yafuatayo:
 • Kudumisha Muungano, Amani na Umoja wa Tanzania. Serikali haitamwonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga amani na mshikamano katika nchi. Hili alilidhihirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar, kwani Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu.
 • Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Viwanda vinalengwa ni vyenye kutumia nguvu kazi kubwa, malighafi za ndani ya nchi, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Nia ni kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini;
 • Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi, hususan miundombinu ya usafiri na nishati;
 • Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu, Afya na Maji. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinapatakana sio tu kwa urahisi bali pia kwa ubora unaostahili ili kukabiliana na maadui ujinga, umaskini na maradhi;
 • Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu ndani ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi, uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati;
 • Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi, ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili. Lengo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wote wa kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, ukusanyaji wa mapato ya Serikali na udhibiti wa matumizi ya Serikali nao utaimarishwa;
 • Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za binadamu. Jitihada za makusudi zitaelekezwa katika kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, dhuluma na uonevu wa aina yoyote. Aidha, maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatalindwa. Kwa upande mwingine, wananchi watahimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi;
 • Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu, ikiwemo wizi, ujambazi, tatizo la dawa za kulevya n.k.
 • Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema, mahusiano mema na Mataifa mengine duniani pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda;
 • Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo, sanaa, burudani na utamaduni, ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.
HITIMISHO

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kuwataka watanzania washiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira hii inakusudia kuwezesha Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati uaoongozwa na Viwanda ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Bodi ya KCU yavunjwa; Meneja afutwa kazi

Kaimu Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa
Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera, Kagera Co operative Union 1990 LTD (KCU)pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho na Mrajisi Masidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera wamesimamishwa kazi kuanzia leo tarehe 21.07.2016 kwa tuhuma za ubadhilifu zaidi ya shilingi milioni 900 pamoja na kuingia mikataba yenye harufu ya rushwa iliyopelekea hasara kubwa kwa Chama hicho Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera.

Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akitangza rasmi kusimamishwa kwa Bodi ya KCU pamoja na Meneja Mkuu wa Chama hicho cha Ushirika alisema kuwa Bodi hiyo ikishirikiana na Meneja Mkuu Bw. Vedastus Ngaiza walitoa taarifa za uongo katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho wa mwezi Mei 2016 kuhusu deni wanalodaiwa na Benki ya CRDB.

Dkt. Rutabanzibwaalisema baada ya kutuma wakaguzi kutoka ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Wakaguzi hao walibaini kuwa taarifa waliyosomewa wananchama katika mkutano ilitaja kuwa deni lilikuwa Shilingi bilioni 2.8 kumbe haikuwa kweli kwani deni lilikuwa limepanda hadi shilinngi bilioni 3.15 Bodi na Meneja Mkuu walikuwa wamewadanganya wanachama wa chama hicho.

Pili, Wakaguzi hao waligundua kuwa shilingi Milioni 124 zilitumika katika malipo na hakukuwa na maelezo ya kutosheleza kuhusu malipo ya fedha hizo.

Tatu, KCU iliingia mikataba ya kukodisha majengo yake amabayo haikufuata bei ya soko kwa sasa, na mikataba hiyo ilifungwa kwa makubaliano ya miaka 10 jambo ambalo linapelekea Chama hicho kulipwa pango kwa bei ya chini kabisa isiyoendana na soko.

Nne, Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU kimekuwa kikinunua kahawa ya kiwango cha chini kabisa na kusababisha hasara kubwa. Tano, Chama cha KCU kilijiingiza kataika miradi isiyokuwa na tija kama mradi wa kununua maharage ambao ulikisababishia hasara kubwa Chama hicho.

Dkt. Rutabanzibwa alisema kuwa kutokana na sheria Na. 6 ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi wa Vyama vya Ushirika nchini Bodi ya KCU hakufanya kazi yake ipasavyo ya kukisimamia vizuri chama hicho Aidha, Bodi hiyo ilifanya vikao 12 kwa mwaka jana 2015 vikao ambavyo vinaonekana havikuwa na tija kwani pamoja na vikao hivyo vya Bodi kufanyika bado kulikuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha.

MAELEKEZO

Dkt. Ruatabazibwa baada ya kutaja ubadhirifu uliofanyika katika Chama Kikuu cha Ushirika KCU alisema kuwa Serikali imeamua kuchuka hatua zifuatazo;-

1. Kufuta Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Kagera KCU iliyoteuliwa mwaka 2014.

2. Kusitisha ajira ya Meneja Mkuu wa KCU Bw. Vedastus Ngaiza mpaka hapo uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha utakapokamilika.

3. Kusitisha nafasi ya Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Bw. Nestory Shorozi kwani ubadhirifu huo ulifanika yeye akiwepo bila kukishauri vizuri Chama hicho Kikuu cha Ushirika .

4. Akaunti zote za Chama cha Ushirika KCU kusimamishwa mara moja mpaka hapo utaratiibu mzuri utakapokuwa umewekwa .

KUNUSURU CHAMA

Dkt. Rutabanzibwa alisema kuwa katika kukinusuru Chama Kikuu cha KCU pia na kuendelea na Msimu wa manunuzi ya kahawa Serikali imefanya uteuzi mdogo wa Mrajisi Msaidizi Bw, Robert Makene Mtambo kutoka Ukerewe Mkoani Mwanza atakayeshikiria kwa muda nafasi ya Bw. Nestory Shorozi aliyekuwa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kagera.

Aidha mrajisi Msaidizi aliyeteuliwa Bw. Mtambo atakaimu nafasi ya Meneja Mkuu wa KCU iliyokuwa ikishikiliwa na Bw. Vedastus Ngaiza.

Katika kukaimu nafasi hiyo Bw. Mtambo atatakiwa kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama wa KCU ndani ya mwezi mmoja na katika mkutano huo atateuliwa Mwenyekiti ambaye atatakiwa kusoma taarifa halisi ya KCU iliyotakiwa kusomwa mwezi Mei 2016 katika Mkutano Mkuu.

Adha Dkt. Rutabanzibwa alisema Serikali haikukurupuka kuchukua hatua hiyo bali ilifanya uchunguzi wa kutosha ikiwa ni pamoja kuipa bodi nafasi ya kujieleza lakini haikutoa maelezo ya kutosha na badala ya kupunguza deni wao waliliongeza deni likapanda zaidi.

Pia Dkt. Rutabanzibwa aliviagiza vyombo vya uchunguzi kama TAKUKURU, Polisi na Usalama kuanza kulifanyia kazi suala hilo mara moja.

Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa alimalizia kwa kusema kuwa Serikali imeamua kulifanyia kazi suala la VyamaVikuu vya Ushirika nchini kwani vyama hivyo vimeonekana kuwa badala ya kuwasaidia wakulima vinawadidimiza ambapo alisema walianzia Mwanza, sasa Kagera, na wanaelekea Mikoa ya Geita, Simiyu, na Shinyanga.


Kaimu Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa (kulia) akiongea na waandishi wa habari mkoani Kagera mara baada ya kuwasilisha uamuzi wa Serikali

Jengo la Ofisi Kuu ya Chama cha Ushirika, KCU 1990 LTD Mkoani Kagera.

Jaribio la mapinduzi Uturuki: Uchambuzi - Kwa nini idara ya ushushushu ilishindwa kuyazuia
Julai 15 mwaka huu, serikali ya Uturuki ilinusurika kupinduliwa katika jaribio la mapinduzi liliyodumu kwa chini ya masaa 12. Tayari watu zaidi ya 60,000 aidha wamekamatwa, wamesimamishwa au wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusiana na jaribio hilo lililofeli.

Jaribio la mapinduzi lilitokeje?

Awali daraja kuu katika mkondo wa Bosphorous liliwekewa vizuizi na kundi la wanajeshi wakitumia vifaru, na wakati huohuo ndege za kivita zilikuwa zikiruka katika anga la mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara, huku milio ya bunduki ikisikika sehemu mbalimbali.

Baadaye, Waziri Mkuu Binali Yildrim, alitangaza kwamba kulikuwa na jaribio linaloendelea la kuipindua serikali.

Muda mfupi baadaye, kikundi cha wanajeshi kilitangaza kupitia radio ya taifa kuwa jeshi limechukua madaraka kutoka kwa Rais Recep Tayyip Erdogan ili kulinda demokrasia.

Kisha likafuatia tangazo la hali ya hatari (curfew), sheria za kijeshi (marshall law) na maandalizi ya katiba mpya.

Rais Erdogan ambaye alikuwa likizoni alifanikiwa kuwasihi wananchi waingie mtaani kupinga mapinduzi hayo. Alitoa wito huo kwa kutumia app ya Facetime ya iPhone na kuonyeshwa live kama inavyoonekana pichani chini.Katika usiku huo, vituo vya televisheni vilivamiwa na wanajeshi, milipuko kadhaa ilisikika sehemu mbalimbali za Ankara na Istanbul, abaadhi ya waandamaji walishambuliwa na wanajeshi na kuuawa au kujeruhiwa, jengo la bunge na ikulu zilishambuliwa, helikopta ya jeshi ilitunguliwa, na mnadhimu wa jeshi kuchukuliwa mateka.

Jaribio la mapinduzi liliishaje?

Ili jaribio hilo la mapinduzi lifanikiwe, wahusika walihitaji sapoti ya sehemu kubwa zaidi ya jeshi badala ya kikundi kidogo tu, na sapoti ya wananchi mtaani. Yote mawili hayakutokea. Kana kwamba hiyo haikutosha, vyama vya upinzani navyo vilijitokeza kulaani jaribio hilo.

Kufikia Jumamosi asubuhi - chini ya masaa 12 baada ya tangazo la mapinduzi - baadhi ya wanajeshi walioshiriki katika jaribio hilo walianza kujisalimisha.Kadhalika, polisi walifanikiwa kurejesha sehemu mbalimbali muhimu mikononi mwa dola kutoka kwa waasi. Kufikia Jumamosi mchana, mitaa ilikuwa imesheheni wananchi wakilaani jaribio hilo la mapinduzi na kuunga mkono serikali ya Erdogan.Kwanini jaribio hili la mapinduzi lilifeli?

 • Kwanza, jaribio hilo halikuwa na sapoti ya kutosha ndani ya jeshi la nchi hiyo. Kilichoonekana ni kikundi kidogo tu cha wanajeshi kilichojumisha wanajeshi wapya, pasipo uwepo wa viongozi waandamizi wa jeshi la nchi hiyo.
 • Pili, jaribio hilo halikuwa na spaoti ya wananchi. Mara baada ya Rais Erdogan kuwataka wananchi waingie mtaani kupambana na jaribio hilo, ikageuka kuwa mapambano kati ya wanajeshi na wananchi, kitu ambacho kwa vyovyote kingeathiri 'uhalali' wa mapinduzi hayo.
 • Tatu, wahusika wa jaribio hilo la mapinduzi kushindwa kudhibiti njia zote za mawasiliano kati ya viongozi wakuu wa serikali na wananchi, kwa mfano vituo vya televisheni na redio. Mwelekeo wa jaribio hilo la mapinduzi ulibadilika kwa kiasi kikubwa baada ya Rais Erdogan kuonekana kwenye kituo kimoja cha televisheni akiwataka wananchi waingie mtaani.
 • Nne, Uturuki ni taifa lenye asilimia kubwa ya watu wenye kipato cha kati na cha juu. Ni vigumu sana kwa taifa lenye wananchi wa aina hii kuunga mkono mapinduzi. Ni rahisi kwa mapinduzi kuungwa mkono katika nchi masikini ambapo mara nyingi 'chuki' dhidi ya serikali huwa kubwa.
Jaribio hilo la mapinduzi lilionekana kufeli bayana baada ya Rais Erdogan kurejea Instanbul na kuhutubia katika uwanja wa ndege wa Ataturk.Hali ikoje sasa?

Idadi halisi ya waliokamatwa, kusimamishwa kazi au kutimuliwa kazi na hatua nyingine zilizochukuliwa ni kama ifuatavyo:
 1. Watumishi 300 wa Wizara ya madini wametimuliwa. 
 2. Watumishi 184 wa Wizara ya Forodha wametimuliwa. 
 3. Waandamizi wanane wa Bunge wameondolewa. 
 4. Waturuki wote wanapaswa kuwa na nyaraka za ziada wanapofanya safari nje ya nchi. 
 5. Watumishi 86 wa taasisi ya udhibiti na usimamizi wa mabenki wametimuliwa. 
 6. Watumishi 51 wa Soko la Hisa wametimuliwa. 
 7. Majaji 140 wa Mahakama Kuu wametumiwa hati za kukamatwa. 
 8. Watumishi 15,200 wa Wizara ya Elimu wametimuliwa. 
 9. Vyombo vya habari 24 vimefutiwa hati za usajili. 
 10. Watu 429 wa taasisi ya umma ya masuala ya dini (Diyanet) wameondolewa. 
 11. Walimu binafsi 21,000 wamefutiwa leseni zao. 
 12. Watumishi 393 w Wizara ya Familia na Sera za Jamii wametimuliwa. 
 13. Watumishi 257 katika ofisi ya Waziri Mkuu wametimuliwa. 
 14. Wakuu (deans) 1577 wa vyuo vikuu wametakiwa kujiuzulu. 
 15. Magavana 33 wametimuliwa. 
 16. Watumishi 9,000 wa Wizara ya Mambo ya Ndani wametimuliwa. 
 17. Maafisa Usalama wa Taifa 180 wamesimamishwa kazi 
 18. Majaji 2,745wametimuliwa. 
 19. Watumishi wa umma milioni tatu wamezuwia kwenda likizo. 
 20. Mjadala kuhusu kurejeshwa kwa hukumu ya kifo umeanza, na Rais Erdogan ametanabaisha kuwa pindi bunge likiridhia kurejeshwa kwa hukumu hiyo basi wote waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi watahukumiwa kifo. 
 21. Maafisa 1,500 wa Wizara ya Fedha wametimuliwa. 
 22. Majenerali na maadmirali 85 ni miongoni mwa maelfu ya wanajeshi waliokwishakamatwa. Pia zaidi ya polisi 8,000 wamekamatwa, wametimuliwa au wamesismamishwa kazi. 
Mashushushu wa Uturuki walikuwa wapi wakati mapinduzi hayo ynaandaliwa na hadi yakakaribia kufanikiwa?

Makala hii inahusu hasa swali hilo hapo juu, kwa moja ya kazi kuu za Idara ya Usalama ya taifa lolote lile ni kutambua, kuzuwia na kudhibiti matishio ya usalama wa taifa, ikiwa ni pamoja na mapinduzi. Sasa wakati serikali ya Uturuki ikionekana kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi mbalimbali wa umma ikiwa ni pamoja na kuwakamata, kuwasimamisha kazi na kuwatimua, ni idadi ndogo tu ya maafisa usalama wa taifa waliochukuliwa hatua (angalia juu nilipoandika kwa maandishi mekundu).

Lakini swali kubwa zaidi ni kwamba je Idara ya Usalama wa Taifa ya nchi hiyo, MIT, haikufahamu kuhusu mipango ya kufanyika kwa mapinduzi hayo, na kwanini?

Turudi nyuma kidogo. Oktoba mwaka jana, mhadhiri wa chuo kikuu cha Haifa , Israel, Norman Bailey, alieleza kwa uhakika kuwa jeshi la Uturuki linaweza kuchukua madaraka ya nchi hiyo iwapo litaona nchi inaelekea kusikofaa.

Kadhalika, Machi mwaka huu, wachunguzi wa masuala ya usalama wa Russia walionya kuwa jeshi la Uturuki lilikuwa likijiimarisha kisiasa, na hivyo kujenga msingi wa mapinduzi.

Baadaye mwezi huohuo, Michael Rubin wa taasisi ya American Enterprise, aliuliza "je Uturuki itakumbwa na mapinduzi?" na akajibu kwamba "isiwe jambo la kushangaza iwapo jeshi la Uturuki litajaribu kumng'oa (Rais) Erdogan na kuwatupa jela watu wake wa karibu."

Machi 30, jarida linaloheshimika la Foreign Affairs lilichapisha makala ya Gonul Tol, Mkurugenzi mwanzilishi wa Taasisi ya Mashariki ya Kati, kituo cha stadi za Uturuki, alieleza kuwa nchi hiyo ilikuwa ikikabiliwa na mapinduzi.

Kadhalika, mwanzoni mwa mwezi huu, Joseph Fitsanakis wa tovuti ya IntelNews alizungumzia kuhusu hali tete iliyokuwa ikiikabili Uturuki na kutanabaisha kuwa hakuna nchi katika eneo hilo ambayo ilikuwa 'haijatulia' kama Uturuki.

Pia, wachambuzi wa taarifa za kiusalama wa Marekani walikuwa wakihofia kitambo kuhusu hali ya usalama nchini Uturuki. Swali lilibaki kuwa lini kungetoa jaribio la mapinduzi na lingeongozwa na nani.

Sasa, kama wataalamu hao mbalimbali wa masuala ya usalama waliokuwa wakitegemea 'vyanzo vya wazi vya taarifa za kishushushu' (open sources) waliweza kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa jaribio hilo la mapinduzi, inatarajiwa kuwa mashushushu wa Uturuki pia walikuwa na tahadhari hiyo.

Kwa kuangalia 'sintofahamu' iliyoikumba serikali ya Rais Erdogan wakati wa jaribio hilo la mapinduzi, yayumkinika kuhisi kuwa idara ya ushushushu ya nchi hiyo nayo ilikuwa katika 'sintofahamu' pia.

Na kuthibitisha kuwa taasisi hiyo haikuwa imejipanga vizuri, asuhuhi ya Julai 16 makao makuu yake yalishambuliwa na helikopta za jeshi pasipo upinzani wowote.

Wakati serikali ikikabiliwa na jaribio la mapinduzi, mkuu wa idara ya ushushushu ya nchi hiyo, Hakan Fidan, alikuwa mafichoni.Kuna sababu kuu tatu zinazoweza kueleza kwanini idara ya ushushushu ya nchi hiy, MIT, ilionekana kutokuwa na taarifa kuhusu jaribio hilo la mapinduzi na kushindwa kwake kulizuwia.
 • Kwanza, uwezo wa utendaji kazi wa taasisi hiyo ni duni, na kwa kiasi kikubwa umekuwa ukikuzwa na vyombo habari kuliko hali halisi. Taasisi hiyo inaelezwa kuwa yenyeurasimu mkubwa, yenye kutumia mbinu za kale, in uhaba mkubwa katika mtandao wake wa upatikanaji taarifa za kiusalama, sambamba na mapungufu katika uwezo wake kwenye uchambuzi wa taarifa za kiusalama.
 • Pili, kuchanganya siasa na taaluma ya ushushushu. Awali, taasisi hiyo ilikuwa ikijitegemea na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia taaluma na utaalam wa ushushushu. Hata hivyo, tangu Erdogan aingie madarakani mwaka 2003, taasisi hiyo imekuwa kama chobo cha kisiasa cha AKP, chama tawala chenye mrengo wa kulia kidogo kidini kinachoongozwa na Erdogan.
 • Tatu, kwa takriban muongo mzima sasa, MIT imekuwa 'bize' zaidi na changamoto za matishio ya usalama kwa Uturuki kutoka nje, yaani tishio la kikundi cha kigaidi cha ISIS, harakati za uhuru za Wakurdi na wapiganaji wao wa PKK, kuibuka kwa taifa lisilo rasmi la Rajava huko Syria, na hali tete ya usalama huko Iraki na Syria kwa ujumla. Changamoto hizo zimepeleka taasisi hiyo kuwekeza nguvu nyingi katika kukabiliana na matishio kutoka nje badala ya matishio ya kiusalama ya ndani ya nchi.


Kwa upande mwingine, kumekuwa na hisia kwamba huenda Erdogan alishirikiana na MIT kuruhusu wapinzani wa chama tawala na serikali ndani ya jeshi la nchi hiyo kufanya jaribio hilo la mapinduzi , lengo likiwa ni kuwa mapinduzi hayo yakishindikana (na lengo ni yashindikane) basi Erdogan awe na kila sababu na haki ya kuendesha taifa hilo kwa mkono wa chuma. Ikumbukwe kuwa kwa muda mrefu Erdogan amekuwa akifanya jitihada za kutaka taasisi ya urais wa nchi hiyo iwe ya kiutendaji kuliko sasa ambapo kinadharia mkuu wa serikali ni Waziri Mkuu.

Nimalizie makala hii kwa kuahidi kufanya uchambuzi mwingine kadri taarifa mbalimbali zitakavyopatikana. Kwa habari zaidi kuhusu masuala ya ushushushu, bonyeza hapo juu palioandikwa 'INTELIJENSIA,' sambamba na kusoma habari nyingine katika blogu hii.

Taarifa ya habari ChannelTEN Julai 21, 2016Taarifa Wizara ya Elimu kwa wenye maswali kuhusu waliorudishwa Stashahada maalumu UDom


Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM


Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais Dk. Ali Mohammed Shein, wakimuonyesha kiti cha kukaa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli, walipoingia ukumbini, kabla ya kuanza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete, katika ukumbi wa Sekretarieti, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.

Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016 pamoja na wajumbe wa mkutano huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais Dkt John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano unaotarajiwa kufanyika Julai 23,2016.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM,Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa Sekretarieti, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.


Mwenyekiti Mtarajiwa Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama na wafuasi wa chama cha CCM nje ya ukumbi wa ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mwenyekiti mtarajiwa,Rais Dkt Jonh Magufuli nje ya ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete

Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini.

Wajumbe wa mkutano huo wakijadiliana kabla ya kuaza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.


ajumbe wa mkutano huo wakijadiliana kabla ya kuaza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.


Mpango maalum kupima na kurasimisha ardhi kwenye maeneo yasiyopimwa Dar kuanza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Mozes Kusiluka
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeandaa mpango maalumu wa upimaji wa Ardhi na Urasimishaji wa maeneo yote yasiyopimwa katika jiji la Dar es Salaam ambapo viwanja zaidi ya laki tatu (300,000) vitapimwa na wamiliki wake kupewa Hati.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam kuhusu zoezi hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Mozes Kusiluka amesema kuwa Serikali imeamua kuja na mpango huo kwa sababu ya ukubwa wa jiji hilo na wingi wa watu ulioambatana na ujenzi wa makazi holela.
“Katika mwaka wa fedha 2016/2017 tumepanga kuwa na mpango maalum wa jiji la Dar es salaam ambapo wataalam wetu watakwenda, kuhakiki mipaka na kupima maeneo yote ambayo hayajapimwa na kutengeneza ramani zitakazoonyesha maeneo ya barabara na maeneo ya huduma nyingine kwa kushirikiana na wananchi husika.
Amesema kuwa baada ya zoezi la uhakiki Serikali itatoa hati za maeneo hayo na kusisitiza kuwa zoezi hilo litafanyika pia katika maeneo mengine ya miji mikubwa nchini yenye watu wengi ikiwemo jiji la Mwanza.

Dkt. Kusiluka amesisitiza kuwa urasimishaji utakuwa shirikishi kwa kuwahusisha watu wote wa maeneo yatakayopimwa na Serikali ambapo wananchi wenye nyumba watashirikiana na viongozi wa Serikali katika mitaa kupanga na kuimarisha mindombinu ya maeneo yao pamoja na kukubaliana maeneo ambayo barabara za mitaa zitapita, mitaro ya maji machafu, magari ya kupitishia huduma za dharula kama Zimamoto nay ale ya kubebea wagonjwa.
“Mpango wa urasimishaji ni Shirikishi, wataalam wa ardhi watakwenda kwenye maeneo yote yatakayopimwa hususan katika jiji la Dar es salaam na kukaa na wananchi wote,kupitia mipaka wakishirikiana na wananchi wote kwa uwazi ili zoezi hilo liwe na manufaa na tija kwa wananchi wote” Amesisitiza Dkt. Kusiluka. 
Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria zinazoisimamia sekta ya Ardhi nchini Tanzania bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya Wakulima na wafugaji, migogoro ya kijinai ya mtu mm kuvunja nyumba au kuvamia eneo la mtu bila idhini, migogoro ya mipaka kati ya majirani na ile inayosababishwa na wananchi kutokujua sheria.

Mbali na sababu hizo amebainisha kuwa idadi ya watu na matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali imekuwa ikiongezeka wakati ardhi ikibakia ileile jambo linaloifanya sekta hiyo kuja na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto hizo kupitia watalaam waliopo.

Amesema kuwa serikali imefanya mambo mbalimbali kuhakikisha kuwa inatatua kero za wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali kwa kuwatumia wataalam wake kupima na kupanga maeneo ya vijiji mbalimbali, kutoa elimu pia kuajiri wataalam wa masuala ya Ardhi katika Halmashauri zote nchini.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kupima maeneo yote ya ardhi nchini ambayo hayajapimwa kupitia mpango wa miaka 10.
 • Aron Msigwa –MAELEZO.

HoFundMe: Help fix water wells for children

Shallow water sources for a nearby school
My wife is currently in Tanzania, Morogoro in remote village. 

Morogoro is about 7 hours from Dar es Salam. The villages are another additional 3 hours from Morogoro town. She is currently working with communities that had cholera outbreak, one of them is still under quarantine. The villages she is currently working with lacks clean and safe water sources. 

Women have to walk 30 minutes to collect water from a stream, shown in the picture. The stream is shared with livestocks and was also a source for cholera outbreak in one of the villages. 

There are three communities that desperately need help (population:9000). 
 • The first community, she is asking for help to repair one of the boreholes and to install a water pump. 
 • The second community, a borehole was installed and was not finished. She is looking for funds to install a water pump as well. 
 • For the third community they need at least one water well. Raised funds will first be used to repair and install water pumps.
Please donate at: gofundme.com/2fjuepgs

My wife with community members

Waanzisha kampeni wakitaka MoDewji apewe hisa nyingi Simba SC

Habarini ndugu waandishi wa habari. 

Tukiwa kama mashabiki wa Simba hatujaridhishwa na hali ya timu yetu ni muda mrefu tunakuwa tunakosa makombe lakini wale viongozi wa Simba hawana lolote wanalofanya bora enzi za uongozi uliopita. Tunaomba mtoe katika vyombo vyenu tunataka Simba iende hatua nyingine. 

Tulijadiliana tukaona ndugu yetu MO anattaka kununua timu sasa kwanini tumnyime na hali ni mbaya. Tupeni msaada habari itoke.

Plz nisaidie: https://www.change.org/p/uongozi-wa-simba-tumfanye-mo-dewji-awe-mwenye-hisa-nyingi-simba

Mengi amtumia WM Majaliwa ujumbe mzito

Mengi akizungumza katika Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji kwa niaba ya TPSF.
Katika kufikia malengo ya Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025, Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi amemtumia Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ujumbe kupitia kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama, ujumbe ambao anaamini kama ukifanyiwa kazi Tanzania itaweza kufikia malengo yake kwa haraka zaidi.

Dkt. Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP alituma ujumbe huo kwa Waziri Mkuu wakati ufunguzi wa Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji ambalo linafanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, kongamano lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Alisema kuwa pamoja na serikali kufanya jitihada nyingi ili kuwashirikisha wananchi wake katika uwekezaji kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi lakini bado kuna changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza na zinahitaji kufanyiwa kazi.
"Serikali imekuwa ikitumia pesa kuwapeleka vijana kusoma nje lakini nikakutana na kijana mmoja akaniambia kasoma nje lakini bado hana ajira na alipelekwa kusomea digrii ya mambo ya mafuta na gesi.
"Nadhani ni vyema serikali ikabidili mwenendo wake na kuhakikisha vijana wote ambao wanapelekwa kusoma nje wakirudi nchini wapewe nafasi za kazi ili kulisaidia taifa kwa hiyo naomba utufikishie ujumbe kwa Waziri Mkuu ukienda Dodoma katika mkutano mkuu wa chama," alisema Dkt. Mengi.
Pia alisema nchi yetu imekuwa ikitegemea zaidi kilimo hivyo iwekeze katika kilimo na iache kuagiza nje bidhaa ambazo zinatengenezwa na vyakula ambavyo vinapatikana nchini lakini pia kuwapa vipaumbele wawekezaji wazawa na hata wanapokuja wageni ihakikishe na watanzania wanashiriki kikamilifu katika kuwekeza.
"Nchi yetu kwa miaka mingi tunajulikana kuwa tunafanya zaidi kilimo na nadhani hapa kunahitaji ushirikishwaji mkubwa wa Watanzania na tuache kulima nanasi na hapo hapo tunaagiza juisi ya nanasi nje. Ni muhimu Watanzania watambue kuwa nchi yao ni tajiri na wakishiriki kikamilifu itafika mbali," alisema Dk. Mengi.
Kwa upande wa Waziri Mhagama ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi alikiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lakini serikali inalifahamu hilo na wameanza kufanya mabadiliko ya sheria na sera wanazozitumia kwa sasa.
"Serikali inalifahamu jambo hilo kama kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ili kuwasaidia Watanzania kukuza uchumi wao na wa taifa, kwa sasa tumeanza kufanya mabadiliko kwa baadhi ya sheria na sera na tutaendelea kuangalia ni wapi kunahitajika mabadiliko ili kila jambo lifanyike kwa faida ya watanzania wote," alisema Waziri Mhagama.
Akielezea kongamano hilo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa alisema malengo ya kongamano ni kubadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa serikali na sekta binafsi lakini pia kushirikisha mashirika ya nje ya nchi ili kuweza kupata njia bora ambayo itakwenda kutumika katika kuwashikirikisha watanzania wote ili kila mmoja ashiriki kukuza uchumi wa taifa.


Waziri Mhagama akitoa hotuba katika kongamano hilo pamoja na kujibu baadhi ya hoja alizotoa Dkt. Mengi.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa akielezea malengo ya kongamano hilo la siku mbili.


Baadhi ya wageni waalikwa ambao wamehudhuria kongamano hilo la siku mbili.
Wageni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano.

 • Taarifa tumeshirikishw ana MoDewji blog