Kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya Tanzania leo Julai 23, 2016

DC Polepole ataja Kata za wilaya ya Ubungo na kutoa namba ya mawasiliano

TANGAZO MUHIMU

Kwa Wakazi wa Kata za Makurumla, Mburahati, Manzese, Mabibo Sinza, Ubungo, Makuburi, Kimara, Mbezi, Msigani, Saranga, Goba, Kibamba na Kwembe. Ninyi ni wakaazi wa Wilaya Mpya ya Ubungo.

Kwa kila aliye na kero, ninapendekeza tuanze na zile kero sugu na kubwa kubwa na kama hakuna basi hata zile za kawaida. Kwa miezi miwili kutoka sasa Mimi na watumishi wenzangu wa Wilaya yetu, tutasikiliza na kuharakisha utatuzi au ushauri stahili.

Utolewaji wa Huduma kwa wananchi Wilayani Ubungo unazingatia Sera ya "Mlango Wazi". Serikali Ubungo inasema "Tuambie Ukweli ili tutende haki na wewe upate Haki yako"

Tafadhali na shime wana Ubungo, tujulishane ujumbe huu, ili ndani ya muda mfupi Ubungo iwe Wilaya ya Tofauti, itakuwa ngumu mwanzo ila itakuwa uhalisia mapema zaidi tukishirikiana.

Unaweza wasiliana nami moja kwa moja kupitia 0786146700 (nisipopokea tuma ujumbe mfupi-SMS) au kwa Mwezi huu wa Julai fika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Tutakuwepo kuwasikiliza na kuwahudumia.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano amenituma niwatumikie na kuwahudumia kama Mtumishi na Kiongozi wenu.

Humphrey Polepole
Mkuu wa Wilaya UBUNGO

Tanzania secure loan from Poland to finance $110 million tractor factory

Dar es Salaam — Tanzania has secured a $110-million soft loan from Poland to establish a tractor assembling factory that will enhance the agriculture sector, the government has confirmed.

The Permanent Secretary in the Ministry of Industry, Trade and Investment, Dr Adelhem Meru, said the factory, which is expected to be constructed in Kibaha, would take-off before the next financial year.

"The construction will start soon and we expect to produce about 2,400 tractors annually for local consumption and sell to other East African countries," he said at the Tanzania- Poland Business Forum that brought together various investors.

Dr Meru added that this will be one of the largest factories of its kind in East Africa.

"We expect that it will create between 150 and 200 jobs once production starts," he said.
 • via The Citizen

Kura kobisi wewe...


Kesi 12 za makosa ya kuhujumu uchumi zaiingizia serikali bilioni 29

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Mahakama Kuu chini ya kitengo kinachosimamia kesi za kuhujumu uchumi imetoa adhabu ya kifungo na kulipa faini ya shilingi bilioni 29 kwa watu 12 baada ya kutiwa hatiani.

Dk Mwakyembe alisema hayo jana kwenye mahojiano katika kipindi cha 360 kinachorushwa moja kwa moja, asubuhi siku za wiki na Televisheni ya Clouds.
“Tuna kesi 176 za kuhujumu uchumi tangu Juni mwaka jana hadi sasa. Kesi 13 zimekamilika, watu 12 wamehukumiwa vifungo vya jela na tunawadai Sh29 bilioni kwa hiyo kama mtu alikuwa na ‘kastore’ tutauza tupate hiyo pesa,” “Nchi ilipofikia tunataka tuachane na hizi tabia za udokozi unapopewa mamlaka ya kuhudumia umma.”
Alipoulizwa kuhusu mahakama ya mafisadi alisema: 
“Hatujaanzisha Mahakama, tumeanzisha divisheni (kitengo) ambacho kitasimamia kesi hizo kwa haraka na kwa weledi zaidi.”

[update] Congolese singer Koffi Olomide kicks his female dancer at Jomo Kenyatta International Airport

UPDATE: This is what transpired at the airport on artiste's return to Congo


Mbwa akimnusuru kifo mtu aliyeshambuliwa na chui huko Bunda

MTU mmoja, Makang’ha Mandazi (32), amenusurika kuuawa na chui aliyetoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuvamia makazi ya watu katika kijiji cha Kihumbu, kata ya Hunyari, wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Mandazi mkazi wa kijiji hicho, alinusurika kifo baada ya mnyama huyo kumvamia nyumbani kwake juzi saa 4:00 asubuhi na kuanza kushambuliwa huku akiwa ameangushwa chini, lakini akaokolewa na mbwa wake aliyemng’ata mkia mnyama huyo hatari.

Akizungumzia tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi kijijini hapo, Diwani wa Kata ya Hunyari, Magina Josephat, alisema lilitokea katika kijiji cha Kihumbu.
“Alinusurika kifo baada ya kuokolewa na mbwa wake aliyemng’ata mkia mnyama huyo, hali ambayo ilipelekea kumwachia na kuanza kushambuliana wanyama wenyewe na kutoa nafasi kwa majeruhi huyo kukimbia kuokoa maisha yake,” alisema.
Alisema wakati chui huyo kupambana na mbwa, wananchi walifika katika eneo la tukio na kuanza kumshambulia na kufanikiwa kumuua.

Josephat alisema Mandazi amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na amelazwa hospitalini kwa matibabu.

Diwani huyo alisema wanyama wakiwamo tembo wamekuwa wakitoka mara kwa mara katika hifadhi hiyo na kuleta mdhara kwa wananchi, pamoja kushambulia mazao ya wakulima mashambani mifugo yao.

Kufuatia hali hiyo aliiomba serikali kuwadhibiti wanyama hao na kuwasihi askari wa wanyamapori wanapopewa taarifa juu ya wanyama hao wawe wanawahi mapema kufika katika eneo la tukio ili kuokoa masiaha ya watu na mazao yao.

Ofisa Wanyamapori katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Marwa Kitende, alisema baada ya kupata taarifa hiyo walifika mapema katika eneo la tukio na kutoa mwongozo juu ya ulipaji fidia kwa mwananchi aliyejeruhiwa.

Alisema tayari wataalamu wanafanya uchunguzi wa kina kama mnyama huyo alikuwa na kichaa au la na kwamba ngozi yake kwa sababu ni nyara ya serikali imehifadhiwa sehemu maalumu na kuongeza kuwa wamekuwa wakifanya doria za mara kwa mara kwa ajili ya kudhibiti wanyama hao wanaotoka hifadhini.
 • NIPASHE

HESLB yatoa akaunti za kurejesha mikopo kwa wanufaika wote

Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao. Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho. Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.

Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao. Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao. Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.

Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:
 • A/C No. 2011100205 – NMB
 • A/C No. 01J1028467503 – CRDB
 • A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.

Imetolewa na:

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Imani anaainisha mambo 4 ya msingi kuyajua kabla hujaacha kazi kuuendea ujasiriamali

Inawezekana umechoshwa sana na kazi unayoifanya na una hamasa kubwa ya kutaka kuwa mjasiriamali kwa kujiajiri. Kama hayo ndiyo mawazo yako, kwanza hongera sana, kwani unachagua njia sahihi itakayokufikisha kwenye ndoto zako za kweli.

Nasema hivyo kwa sababu, watu wenye mafanikio makubwa duniani ni wajasiriamali na si vinginevyo. Lakini pamoja na kwamba umekuwa umechagua njia sahihi ya kukufikisha kwenye ndoto zako, ipo haja ya wewe kujua mambo ya msingi kwenye ujasiriamali kabla hujaingia huko.

Kwa kujua mambo hayo itakusaidia wewe kujiwekea misingi imara itakayokufanya usitetereke. Naamini kwa kusoma makala haya, itakusaidia usiwe na maamuzi ya kukurupuka ikiwa upo kazini na unataka kuachana na kazi yako na kuingia kwenye ujasiriamali moja kwa moja.

Sasa bila kupoteza muda, twende pamoja kujua mambo ya msingi unayotakiwa kujua kuhusu ujasiriamali, kabla hujaacha kazi.

1. Ujasiriamali unataka kujituma sana

Hakuna ubishi katika hili kama umemua kuwa mjasiriamali wa kweli ni lazima kujituma sana kila siku. Bila kufanya hivyo hutafika kilele cha mafanikio. Kuna wakati unatakiwa kufanya kazi kuliko kawaida ili kuweza kufikia kilele cha mafanikio yako.

Kama upo kazini na unataka kuingia kwenye ujasiriamali huku ukiamini utakuja kujiachia sana utakuwa unajipoteza. Hivyo, unachotakiwa kujua kama una mpango wa kuacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali, elewa unaingia kwenye kambi inayokutaka kujituma sana ili kuweza kufanikiwa.

Kujituma ni muhimu sana kwa mafanikio ya mjasiriamali yeyote.

2. Ujasiriamali hautakupa uhuru wote

Kama ilivyo kwa mwajiri wako kuna wakati anaweza kukubana, halikadhalika nao ujasiriamali uko hivyohivyo. Hata kama unafanya kazi ya kwako kuna mambo ambayo huwezi kuwa huru kwa asilimia zote, kwani ukifanya hivyo utapoteza mengi.

Kuna kipindi ambacho utatakiwa kuamka asubuhi na mapema. Pia kuna wakati itatakiwa kujinyima baadhi ya mambo ili kufikia mafanikio yako. Hiyo yote hutokea, kwani bila kufanya hivyo, utakaa sana kwa muda mrefu eneo moja bila kufanikiwa, kwa sababu utakuwa kama unazunguka tu.

3. Ujasiriamali unataka juhudi ya kujifunza kila siku

Ili uweze kuwa mjasiriamali bora na mwenye mafanikio ni lazima ukubali kujifunza kila siku. Kila wakati ubongo wako ni lazima upokee vitu vitakavyokusaidia kukubadilisha wewe ili ukubaliane na hali yoyote ya shindani.

Mjasiriamali wa kweli ni yule anayekubali kujifunza na kurekebisha udhaifu wake pale unapohitajika. Kujifunza huko hakuishii kwenye maandishi peke yake ila mpaka kwenye vitendo. Binafsi jiulize upo tayarii kujifunza kila siku? Kama ni ndiyo endelea na safari yako ya ujasiriamali bila kuchoka.

4. Hutakiwi kukata tamaa mapema

Unapoamua kuwa mjasirimali na kuchagua njia yako mwenyewe, kitu cha kimojawapo cha cha kukijua, ni kwamba hutakiwi kukata tamaa mapema. Kuna wakati mambo na mipango yako inakuwa inakwenda hovyo sana lakini unatakiwa kuvumilia bila kuchoka.

Ukiingia kwenye ujasiriamali halafu huku ukawa una roho ile ya kukata tamaa mapema hutafika popote. Kwa hiyo ingia kwenye ujasiriamali ukiwa tayari kwa lolote. Ikitokea hasara vumilia na kisha chukua jukumu la kuweza kusonga mbele bila kukata tamaa.

Hayo ndiyo mambo ya msingi unayaotakiwa kujifunza kabla hujaingia kwenye ujasiriamali. Chukua hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.

----

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email: [email protected]


Jinsi ya kutengeneza gauni la mtoto kutoka kwenye shati la mtu mzima/mkubwa
Unaweza pia kuweka nakshi na mifuko kama ilivyo kwenye video ifuatayo...


Taarifa ya habari ChannelTEN Julai 22, 2016Job: Project Manager - Maternal and Child Health, SolidarMed, Tanzania

Organization: SolidarMed
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 19 Aug 2016

Organisation: SolidarMed is a medium size Swiss NGO, dynamic, flexible and with a clear vision.

Project Information


SolidarMed has been strengthening the primary health care system of Ulanga District since 2010. The project now focuses on strengthening the supply side (service provision by skilled health staff at the health facilities in the district, including hospital, health centre, dispensaries), while scaling up the community health worker network. This Maternal, Neonatal and Child Health project is implemented by a dynamic local team and embedded into the overall SolidarMed country programme for Tanzania. It aims at generating and sharing lessons learnt and contributes to policy dialogue at different levels.

Country: Tanzania

Place of Assignment: Mahenge, Ulanga District, Morogoro Region

The position requires regular dislocations to the surrounding health facilities and Ifakara. (location of SolidarMed country office)

Start of duty: 
September/October 2016

Employment: 100 % (full time)

Contract type:
 Fixed term appointment: minimum of three years with the possibility of contract extension.

Key tasks and responsibilities

 • Overall management and coordination of the project, incl. planning, monitoring, budgeting, reporting
 • Act as technical advisor to partners (district health team) and build clinical capacity among local health staff (hospital, health centre, and dispensary) through training, coaching and mentoring, with a thematic focus on Maternal, Neonatal and Child Health.
 • Ensure the strategic and operational alignment of the two project components (community and facility level)
 • Contribute to the further development of the project
We are looking for
 • Medical doctor with an additional degree in Public Health, at least 3 years of work experience, incl. in low-resource settings, preferably in Sub-Saharan Africa
 • Clinical expertise in Maternal Neonatal and Child Health (obstetric and/or paediatric skills)
 • Interest in operational research, scientific exchange, knowledge sharing and data management; experience in this area would be an asset
 • Applied knowledge of project cycle management and team leading
 • Good writing and reporting skills (English)
 • Valid driving license
 • Personal flexibility and preparedness to live in a remote rural place with frequent dislocations to the rural health facilities
 • The position comes with a mix of managerial (planning, coordination, networking, reporting etc.) and clinical (mentoring, coaching, on the job teaching) tasks. We are looking for a hands-on person, socially competent, with clinical and public health competence, not afraid of organising and implementing.
Language Skills
 • Fluent English (written, spoken)
 • Basic Kiswahili. If not spoken: readiness to learn.
 • German would be an asset
We offer
 • A professionally run, innovate health program in a rural African setting
 • An attractive salary and benefit package commensurate with Swiss standards
 • Professional development opportunities and linkages with competence and research networks
 • Family posting in a rural but safe African setting; however no international or English medium school
 • A motivated team both in Tanzania and Switzerland
How to apply:

Application

Applications are accepted until 19th August 2016 in electronic format only.

Please email your CV and a short letter of motivation (reference “PM PHCU Tanzania” to: [email protected]

Please also mention how you heard about the job posting (if internet, please mention which site).

Only short-listed candidates will be contacted. For further information about the role and the project, email Dr. Karolin Pfeiffer: [email protected]

Address: [email protected]

Website: www.solidarmed.ch

Kagera University opening January 2017

THE official opening of the Karagwe University of Agriculture (KUA), which was scheduled to kick off in October, this year, has been re-scheduled to January, next year due to logistics problems, it has been disclosed.

The Karagwe Diocese under the Evangelical Lutheran Church (ELCT) is undertaking construction of the Karagwe University of Agriculture (KUA), which is expected to take the first intake of students in January, next year.

Bishop Benson Bagonza of the Karagwe Diocese told the ‘Daily News’, in an exclusive interview that the university would absorb about 300 students in the first intake pursuing degree courses in Agriculture, Livestock, Information Technology (IT) and Environmental Science.

“The construction works were being undertaken under three phases. Under Phase One, various activities were being implemented including construction of lecture halls. We are finalising plans to get registration from the central government to enable the university to kick off in January, next year,” he said.

According to Dr Bagonza, the total cost of the project was estimated to cost 14.5bn/- upon completion, making KUA the first university offering agriculture degrees in the Lake Zone regions of Mwanza, Kagera, Simiyu, Geita, Shinyanga and Mara.

“The aim of opening the university was to mitigate shortage of agricultural experts facing the nation. We hope the contribution will have an impact on the nation’s development,” he said.
 • via The Daily News