Waziri Nchemba abaini Wachina haramu akifuatilia tukio la Mtanzania aliyepigwa na Wachina huko Geita

UPDATE, Julai 30, 2015:

POLISI WAMDANGANYA WAZIRI MWIGULU


MAOFISA wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Geita wamemdanganya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, kuhusu ukweli wa tukio la kushambuliwa kwa Masanja Shilomero (25) na mwajiri wake ambaye ni raia wa China.

Maofisa hao walimdanganya Waziri Mwigulu ambaye alikwenda mkoani Geita kufuatilia taarifa za kunyanyaswa kwa Masanja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyamitondo, Tarafa ya Butundwe wilayani Geita, kwa kuhofia kuwa akiujua ukweli atawatumbua.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vyake vya kuaminika vilivyo ndani ya jeshi hilo zimeeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya ya Geita (OC-CID), Samweli Kijanga, alikwenda eneo la mgodi akiwa ameambatana na baadhi ya makachero muda mfupi baada ya kuteswa na walinzi na kukutana na uongozi wa mgodi huo.

Julai 6, mwaka huu, Masanja alipigwa na mwajiri wake aliyetambuliwa kwa jina moja la Myo ambaye ni raia wa China baada ya kuomba kupandishiwa mshahara.

Baada ya kupigwa alikamatwa na polisi ambao walimpeleka mahakamani wakiwa wamemfungulia kesi yenye namba CC 278/2016 akituhumiwa kwa kosa la wizi wa mawe.

Tukio hilo lilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kumfikia Waziri Mwigulu ambaye alifika mkoani Geita Julai 27 na kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kabla ya eneo la mgodi lililo katika Kijiji cha Nyamahuna na baadaye alikwenda gerezani kukutana na Masanja.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Kachero Kijanga na timu yake walimkamata Masanja aliyekuwa amejeruhiwa kwa kipigo na kumweka korokoro ya kituo kidogo cha polisi ya Katoro na siku iliyofuata alifikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Katoro bila kufikishwa hospitali kwa ajili ya hati ya matibabu (PF3) wala kuchukuliwa maelezo kuhusu unyama aliofanyiwa.

Mmoja wa makachero waliopo mkoani Geita, amelieleza gazeti hili kuwa haiingii akilini kumuona Waziri akiwa na ujuzi wa kuhoji na kubaini dosari akiwazidi polisi ambao wamesomea kazi hiyo.
“Waziri kaja kahoji kwa dakika na kubaini kuna kosa la shambulio dhidi ya anayedaiwa kuteswa na Wachina, kwanini polisi wasigundue?
“Wao upelelezi uliishia kumpeleka mahabusu kwa maelezo ya mlalamikaji na hiyo ilikuwa baada ya OC-CID kukaa faragha na Wachina ambao ni wamiliki wa mgodi huo na walipomaliza kikao chao tulishuhudia kijana wa watu anakamatwa na ikaamuriwa asipewe PF3.
“Alikuwa ameumizwa sana lakini polisi hawakuona hilo wala haja ya kuita mashuhuda wa tukio na kuwahoji tofauti na waziri ambaye kwa muda mfupi aligundua uwepo wa Wachina zaidi ya 50 kinyume cha sheria, lakini tusimlaumu mkuu wa upelelezi maana tunasikia ni maagizo kutoka juu,” alisema polisi huyo.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baada ya polisi kupata taarifa kuwa Waziri Mwigulu atafika Geita kufuatilia suala hilo, Julai 27, majira ya alfajiri askari polisi wawili ambao majina yao tunayahifadhi kwa sasa wakiwa na Kachero Kijanga walikwenda Gereza la Geita kuomba kuchukua maelezo ya Masanja.

Kwamba polisi hawakuwa na kibali cha kumtoa Masanja gerezani hivyo waliruhusiwa kuchukua maelezo yake wakiwa ofisi za gereza ili kuepuka kutumbuliwa lakini ingetokea Waziri Mwigulu akaitisha jalada la uchunguzi lililofunguliwa dhidi ya Wachina hawakuwa nalo.

Polisi mwingine wa mkoani Geita aliyezungumza na gazeti hili (jina lake tunalihifadhi kwa sababu si msemaji) alieleza kuwa makachero hao walipotoka kuchukua maelezo ya Masanja gerezani ikiwa ni muda mfupi kabla ya waziri kufika, walikwenda kufungua jalada namba GE/RB/5498/2016 la shambulio la kudhuru mwili, mlalamikaji akiwa kijana huyo ambaye mbali na kuumizwa hakupatiwa hata fomu ya matibabu (PF3) na mlalamikiwa akiwa Myo.
“Waziri akiomba jalada hilo hata leo hawabaki kwa sababu litaonyesha ni lini limefunguliwa na atabaini kuwa Masanja alipelekwa gerezani akiwa hana PF3 ambalo nalo ni kosa,” alisema polisi huyo.
Alipoulizwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Ratson, kuhusu jambo hilo alisema hawezi kutoa taarifa kwa mtu ambaye hamfahamu licha ya kuelezwa mapema kuwa anazungumza na Gazeti la MTANZANIA.
“Mimi siwezi kuzungumza na mtu ambaye simfahamu kwa sababu taarifa nitakazotoa zina athari kwa jamii kama mna mwakilishi wenu huku mwambie aje kuniona ofisini,” alisema Afande Ratson kisha akakata simu.
Takribani wiki moja sasa kumekuwa na hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa Tanzania, Shilomero akiteswa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mwajiri wake ambaye ni raia wa China.


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi, kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyodaiwa kufanywa na raia wa China wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro, Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni Watanzania.

Takribani wiki moja sasa kumekuwa hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa Tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.

Ilimlazimu Waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani  ya Nchi kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa Watanzania.

Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la Mtanzania kuteswa na mwajiri wake, kipigo kilichosababisha kupoteza fahamu na siyo kifo.

Hatua za awali Waziri Nchemba alizozifanya ni kwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ya kushitakiwa na mwajiri wake kwa kosa la wizi lililosababishwa apigwe.

Katika mahojiano ya Waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo, Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye mhusika hasa wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na akiwapo gerezani.


Katika hali hiyo, ilimlazimu, Mhe. Mwigulu kwenda mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwa ajili ya kutambua waliofanya vitendo hivyo vya kinyama. Katika oparesheni hiyo, kijana aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini Watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na Mchina mmoja walioshirikiana kumpiga, kumtesa na kumjeruhi.


Kufuatia utambuzi huo na maelezo ya wahusika, Nchemba akaagiza wahusika wakamatwe mara moja na ameondoka nao kwa hatua zaidi za kisheria.Katika hali nyingine ya kusikitisha, Waziri Nchemba amebaini uwepo wa wahamiaji haramu raia wa China katika mgodi huo ambapo nyaraka za uhamiaji mkoa wa Geita zinaonesha raia 28 wenye vibali ndio waliruhusiwa kukaa kwenye mgodi huo, lakini katika operasheni ya kushitukiza aliyoifanya Mhe. Nchemba amebaini uwepo wa raia wa china zaidi ya 50 wanaoishi katika mgodi huo kinyume na sheria.Hivyo amemuagiza Mkuu wa Mkoa na timu yake ya uhamiaji kuhakikisha wote wasio na vibali wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.


Taarifa ya habari ChannelTEN Julai 27, 2016


Taarifa ya TRL ya ajali iliyohusisha basi la UDA na treni eneo la KAMATA Dar

Mtu mmoja afariki dunia baada ya basi la UDA kukigonga kichwa cha treni cha Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) katika makutano ya reli na barabara ya KAMATA saa 3:20 usiku jana Julai 26, 2016. Marehemu ametambuliwa kwa jina la Omari Abdallah Nyumba mkazi wa Mbagala.Aidha majeruhi 43 wa ajali hiyo walipelekwa hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo watatu kati yao ni mahututi.

Taarifa za awali za Kikosi cha Polisi Reli zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva Majuto Hamis wa basi hilo la UDA aina ya Hecher lenye namba za usajili T969 CVP kukaidi amri ya kusimama iliotolewa na Mfanyakazi wa TRL. Dereva huyo ni mmoja wa majeruhi ambaye amevunjika miguu na yuko chini ya ulinzi wa Polisi wa Reli akiwa wodini baada ya majeruhi wote kupatiwa huduma.

Kichwa cha treni kilichogongwa ni cha kazi za sogeza Namba 7317 kilikuwa kikitokea kituo kikuu cha treni cha Dar es Salaam.

Kikosi cha Polisi TRL wameahidi kutoa taarifa zaidi baadae hii leo kuhusu maendeleo ya majeruhi wa ajali hiyo.

Tokea uanze mwaka huu kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto hasa madereva wa pikipiki za bodaboda kutokuwa makini katika kuzitii sheria hizo zinazosimamia makutano ya reli na barabara.

Tokea kuanza kwa mwaka huu wa 2016 ajali nyingi zimeripotiwa hapa jijini Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Manyoni mkoani Singida zikihusisha vyombo hivyo.Wito unatolewa na Uongozi wa TRL kwa watumiaji wa vyombo vya moto boda boda, magari mkubwa na mabasi na wananchi kwa jumla kuzingatia sheria ili kuepuka madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na pia upotevu wa rasilimali muhimu ambazo kama zikitumiwa vizuri zitaboresha maisha ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Julai 27, 2016

DAR ES SALAAM

Orodha ya majina ya wadaiwa HESLB ambao hawajaanza kulipa

Tume ya Mikopo kwa ajili ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini imetoa kabrasha lenye orodha ya kwanza majina ya wanafunzi wanufaika wa mikopo ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao.

FIRST BATCH OF LOAN BENEFICIARIES WHO HAVE NOT STARTED TO REPAY THEIR LOANS


The Higher Education Students’ Loans Board (HESLB), hereby notifies all loan beneficiaries who are not servicing their loans and whose names appear herein that they have breached a contract as per the HESLB Act. No. 9 of 2004 (as amended) Section 19 (1).

These Loan Defaulters are further notified that according to HESLB Act No. 9 0f 2004 the Board, intends to take the following steps: -

(i) Shall be liable to legal action as per Section 19 (a) (1) of the HESLB Act.

(ii) Shall be subjected to additional monthly Penalty of 5% p.a. on the outstanding loans, over and above the 5% that was levied earlier.

(iii) Shall have his/her outstanding loan loaded with the cost of tracing that will be charged after being traced by the Board.

(iv) Shall be blacklisted and his/her information shall be submitted to the Credit Reference Bureaux, following which they shall be barred from access to credit facilities from all Financial Institutions.

(v) Shall be barred from securing Government scholarships or admission for Postgraduate studies in any Higher Learning Institution within and outside the country.

(vi) Their details shall be submitted to the Ministry of Home Affairs, Department of Immigration and all Embassies where they will be denied approval for travelling abroad.

All Loan Beneficiaries whose names have been published in the newspapers and on this website of the Board through http://olas.heslb.go.tz are required to repay their due loans immediately to avoid facing the above listed measures. Loans statements and other details of their due loans can be accessed by visiting HESLB Offices or writing to:

Acting Executive Director,
Higher Education Students’ Loans Board,
P.O. Box 76068
Dar es Salaam

Email: [email protected]

Rais Magufuli awaapisha M/Kiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu

Rais Magufuli na Mwenyekiti TSC, Oliva Joseph Mhaiki (kushoto) na Katibu TSC, Winfrida Gaspa Rutaindurwa (kulia) mara baada ya kuwaapisha katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Bw. Oliva Paul Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). 

Aidha, Rais Magufuli amemuapisha Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Julai 15 2016. Viongozi hao wanakuwa wa kwanza kuongoza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) tangu Tume hiyo ilipoundwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Namba 25 ya mwaka 2015 ikiwa na majukumu ya kusimamia na kuratibu masuala yanayohusu utumishi wa walimu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Oliva Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Winfrida Gaspa Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais Dkt. John Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo mara baada ya tukio la uapisho katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki mara baada ya tukio la uapisho wa Mwenyekiti huyo pamoja na Katibu wa Tume hiyo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki (watatu kutoka kushoto) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Winfrida Gaspa Rutaindurwa (watatu kutoka kulia) mara baada ya kuwaapisha. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo.Picha na IKULU

Serikali yamalizana na Bharti Airtel bilioni 14.9 ili iiache huru TTCL

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kulia) akizungumza kwenye mkutano wake na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema, Serikali imemalizana kimalipo na kampuni mbia wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) hivyo anataka kuiona TTCL ikizaliwa upya na kutoa ushindani wa hali ya juu katika soko la Mawasiliano nchini.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam. Akizungumza katika mkutano huo alisema serikali imefanya mengi katika kuiwezesha TTCL kuwepo na kuendelea kuhudumia Watanzania. "...Siku chache zilizopita, tumeilipa Bharti Airtel shilingi bilioni 14.9 na kuachana rasmi na kampuni hiyo," alisema Waziri Prof. Mbarawa.
"Ndugu Wafanyakazi, sasa ni wakati wa kufanya kazi. Hatuna tena muda wa kupoteza, muda tulionao ni wa kuwajibika, kuwatumikia Wananchi. Serikali inafanya kila jitihada kuwawezesha. Tunachotaka kwenu ni uadilifu, hatuna nafasi kwa wabadhirifu, wavivu na wanaovujisha siri za kampuni kwa washindani. Ni lazima mbadilike na mfanye kazi kwa juhudi kubwa sana, Wananchi waridhike," alisisitiza Prof. Mbarawa.
Awali akitoa taarifa fupi kwa Waziri, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema, kampuni hiyo inashukuru mchango mkubwa wa Serikali katika kuiwezesha ili kuendelea kutimiza vyema wajibu wake. "...Mhe Waziri, tunaishukuru sana Serikali na wewe binafsi kwa jitihada kubwa ambazo zimetufikisha hapa tulipo," alisema Dk. Kazaura katika taarifa yake.

Akitaja baadhi ya jitihada za Serikali, alisema imefanikisha kuiondosha Kampuni ya Bharti Airtel ndani ya TTCL, kuisamehe TTCL madeni ya takribani shilingi bilioni 100, Serikali kuipatia TTCL masafa ya Mawasiliano na kibali cha kutumia rasilimali zake kama dhamana ili kupata fedha za kufanikisha mipango na mikakati yake ya kibiashara.

Aidha Dk. Kazaura alisema, kutokana na mchango huu mkubwa wa Serikali, Kampuni hiyo imeongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi wake ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa huduma za 4G LTE ambazo hadi sasa zimesambaa katika maeneo 33 Jijini Dar Es Salaam huku mpango ukiwa ni kufikisha huduma hizo Jiji zima la Dar es salaam na mikoa mingine mitatu ifikapo mapema mwakani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete akizungumza katika mkutano huo alisema kampuni hiyo imejipanga kikamilifu katika kutoa huduma bora na za kiwango cha juu kabisa katika huduma za Mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta hiyo kwa weledi na ububifu wa hali ya juu.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza kwenye mkutano wake na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam wakiwa katika mkutano wao na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam wakiwa katika mkutano wao na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam wakiwa katika mkutano wao na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam wakiwa katika mkutano wao na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam wakiwa katika mkutano wao na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kulia) akizungumza kwenye mkutano wake na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam pamoja na maofisa kutoka wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano wakiwa katika mkutano wao na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Kampuni ya TTCL Makao makuu kabla ya kuzungumza na wafanyakazi.[/caption] [caption id="attachment_73749" align="alignnone" width="1000"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kushoto) akishirikishwa jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) katika ofisi za Kampuni ya TTCL Makao makuu kabla ya kuzungumza na wafanyakazi.

Askari FFU aliyemwua Daudi Mwangosi ahukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani
Na MatukiodaimaBlog, Iringa

MAHAKAMA kuu kanda ya Tanzania kanda ya Iringa imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa namba G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwaahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi. wakati akiwa katika majukumu yake ya kuchukua habari huku mke wa marehemu Mwangosi Itika Mwangosi akipongeza vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano mkubwa katika kufuatilia kesi hiyo.
"Mahakama inatambua uchungu wa familia iliyoupata kwa kifo cha marehemu Daudi Mwangosi ambaye aliuwawa pia marehemu aliuwawa kikatili ....siku zote adhabu inapaswa kulingana na kosa husika mahakama haiafiki maombi ya wakili wa upande wa utetezi kuomba mshtakiwa apewe adhabu ya kuachiwa huru kwa kuwa ni yatima ....mgongano wa hisia umeonekana katika kesi hii ila mahakama inampa adhabu ya kwenda jela miaka 15," alisema jaji Dkt Paul Kiwelo.
Akisoma shauri ya kesi hiyo kabla ya kutoa adhabu leo mahakamani hapo jaji Dkt Kiwelo aliwashukuru wazee wa baraza la mahakama kwa michango yao mkubwa mchango ulioisaidia mahakama hadi kufikia siku hiyo ya hukumu pia mawakili wote walioshiriki katika kesi hiyo.

"Suala la aina gani ya adhabu inafaa halikuwa rahisi sana kwani shauri hili upande wa jamhuri uliomba adhabu ya kufungwa maisha jela huku upande wa utetezi ukiomba mshitakiwa aachiwe huru kwa masharti ambayo mahakama ingeona yanafaa kutokana na kuwa na majukumu ya kulea wadogo zake na yeye kuwa yatima .....mahakama imetazama ukubwa wa kosa husika pia jamii ina mtazamo gani katika kesi hiyo lakini mahakama haitoi hukumu kwa mitazamo mbali mbali inatumia vifungu vya sheria suala la kutoa adhabu ni la kisheria si vinginevyo."

Jaji Dkt Kiwelo alisema kuwa adhabu haitolewi kwa ajili ya kulipiza kisasi ila inatolewa kama sehemu ya onyo na kuifanya jamii kutambua kuishi kwa kuheshimu misingi ya sheria kwani kuna mambo manne katika kesi yanatazamwa likiwemo la medhania ya kosa alilotenda na aina ya kosa pia maslahi ya jamii katika kosa husika.
"Naomba kusema mgongano wa hisia umeonekana katika kesi hii pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo bado mahakama haijayumbishwa na migogano hiyo .....mahakama haiitoi hukumu kwa kutazama ni kosa la kwanza wala mhusika hana rekodi mbaya ya makosa mahakama inaendeshwa kwa sheria ndugu wangefurahi kuona mtuhumiwa anafungwa hivyo siafiki maombi ya upande wa utetezi juu ya mkosaji naamini kabisa kwa kosa hili kumwachia kwa Masharti haki haitakuwa imetendeka."
Kwa mujibu wa sheria kuua bila kukusudia ni kosa kubwa sana ambapo adhabu yake huwa ni kufungwa jela maisha japo kila kosa huamuliwa kutokana na mazingira yake hivyo lazima upewe adhabu ambayo itakuwa funzo kwa wengine.
"Kuua si jambo dogo na mahakama hii kwa kuzingata vifungu vya sheria na pia mtuhumiwa umekaa mahabusu miaka minne inakuhukumu kwenda jela miaka 15 rufaa ipo wazi kwa asiyeridhika."
Akizungumza na wanahabari mara baada ya hukumu hiyo aliyekuwa wakili wa utetezi Lwezaula Kaijage alisema kuwa alisema kuwa yeye alikuwa ni wakili wake na kuwa kwa sasa hawezi kusema ni uamuzi gani ambao mteja wake anaweza kuchukua hadi hapo atakapowasiliana nae
"Nafikiri wote mlikuwepo mahakamani mmesikia kuwa amefungwa miaka 15 itabidi sasa mimi niende magereza kuzungumza nae ili nichukue sheria nione zinasemaje pia kuomba mwenendo mzima wa sheria kuona jinsi ulivyokwenda ili nione ni kitu gani ambacho labda mahakama ilielekezwa vibaya kabla ya kutoa hukumu hiyo kama nitaona kuna jipya basi tutakwenda kwenye rufaa."
Wakili wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki alisema kuwa katika hukumu hiyo mahakama kuu kanda ya Tanzania kanda ya Iringa imetenda haki pasipo kuegemea upande wowote na kuwa pamoja na nguvu kubwa ya polisi na jinsi ambavyo ushahidi uliokuwa umepelekwa kulenga kumnasua mwenzao ila mahakama hiyo imetumia ushahidi wa ungamo la mlinzi wa amani kutoa hukumu ambayo kimsingi haijaacha maswali kwa wananchi.

Wakili Shabakaki alisema kuwa kesi hiyo polisi waliifanya kama kesi ya nyani kumhukumu ngedele kwa kula mahindi kwani alisema aliyetenda kosa alikuwa ni askari ,mchunguzaji wa kesi hiyo ni askari hivyo katika mazingira hayo haikuwa rahisi kesi hiyo kufikia hukumu hiyo ila mahakama imetenda haki na kuwa wao kama watetezi wa haki za binadamu wataona ni hatua zipi za kuchukua baada ya mahakama kutenda haki.

Alisema pamoja na jukumu la polisi la ulinzi wa jamii ila polisi baadhi yao wameendelea kukiuka wajibu wao na kuogopwa zaidi na raia jambo ambalo si jema na kuwa nguvu kubwa iliyotumika siku zote wakati wa kesi hiyo ni kielelezo tosha kuwa polisi walikuwa wakitegemea mwisho wa siku mwenzao huyo kuachiwa huru.

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deo Nsokolo alisema kuwa wao kama UTPC wanapongeza mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa kwa kutenda haki katika kesi hiyo kwani alisema kuwa jeshi la polisi walipanda kuharibu kesi hiyo ila jaji kwa umakini wake ametoa adhabu.
" Sisi kama wanahabari tunajipongeza pia kwa hukumu hii kwanza kutiwa hatiani kwa mtuhumiwa na pili kufungwa jela miaka 15....... na ifahamike kuwa kesi hiyo ilikuwa ikiihusu serikali hivyo hukumu ya kesi hiyo imeingia katika rekodi ya dunia kuwa mwandishi aliuwawa na muuaji amefungwa miaka 15 jeshi la polisi Iringa kwa muda wote limekuwa likiwanyanyasa waandishi hivyo sisi kama viongozi wa wanahabari tutakwenda kuonana na viongozi wao wa juu."
Alisema kuwa yapo mambo ya msingi ambayo jeshi la polisi linapaswa kufanya ila si kwa kutumia nguvu kubwa kunyima uhuru wa vyombo vya habari hasa katika kesi hiyo ya Mwangosi .
"Polisi katika kesi nyingine wamekuwa wakiwasaidia wanahabari kupata picha kirahisi kwa watuhumiwa pindi wanapofikishwa mahakamani ila katika kesi hiyo wamekuwa wakimfunika mwenzao na kuzuia waandishi kupiga picha ila pamoja na yote hayo adhabu imetolewa pale pale"
Makamu Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile alisema kuwa polisi Iringa walitamani kuona kesi hiyo inaharibika na kama lisingelikuwa ungamo la mlinzi wa amani mtuhumiwa huyo alikuwa anaachiwa huru na ungamo chini ya mlinzi wa amani ni mahakama yenyewe hivyo ni wazi mahakama imeweza kutenda haki zaidi .
"Adhabu ni kumfanya mtu ajirekebisha na wapo waliotegemea kuwa muuaji wa Mwangosi nae ana hukumiwa kufa ila si haki binadamu ....lakini mtuhumiwa huyo wakati wote wa kesi hiyo hakupaswa kufikishwa mahakamani na polisi wenzake badala ya askari wa magareza ambao ndio wanawajibu wa kumpeleka mahakamani na mahabusu ila .....hata leo baada ya hukumu hatujui amepelekwa wapi maana wameondoka nae wao wenyewe ambao walitaka kesi ivurugike sasa sijui wanampeleka rumande ama gerezani au wamempeleka nyumbani kwanza kula chakula lakini naomba hili kuliacha hapo."
Bw Balile alisema kuwa kwa sasa wanaanzisha mchakato wa kufungua kesi ya madai kwa ajili ya familia ya Mwangosi na kuwa kujua ni mahakama ya ndani ama ya Afrika ambayo kesi hiyo itafunguliwa itajulikana baada ya kwenda kukaa na viongozi wenzake japo alisema haki yote itafikishwa kwa familia ya Mwangosi

Juzi Julai 25 mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa ilimkuta na hatia askari Simon katika kesi hiyo namba 45 ya mwaka 2013 ya mauaji ya bila kukusudia ya mwahabari Mwangosi aliyeuwawa kinyama Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi wakati chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) wakifanya uzinduzi wa matawi huku kukiwa na katazo la matukio ya mikutano ama mikusanyiko ya kisiasa kutokana na serikali kuongeza muda wa kuendelea na zoezi la senza ya watu na makazi.

Mjane wa marehemu Mwangosi Bi Itika Daudi Mwangosi alitoa pongezi nyingi kwa wanahabari kwa ushirikiano wao wakati wote wa kesi hiyo hadi ilipofikia mwisho .
" Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha salama siku hii ya leo .....na niishukuru mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa kwa kuweza kutenda haki pili ninawashukuru sana ninyi waandishi wa habari kwa umoja wenu ...nawashukuru sana tena sana zaidi ya sana hata kama mtu amekutendea wema gani Mungu alitupa neno moja tu la ahsante pia napenda kuwatia moyo msiogope songeni mbele Mungu yu paoja nanyi kama alivyowapigania hadi kufika leo atazidi kuwapigania zaidi teteeni kazi zenu elimisheni jamii vile mnavyoendelea kusaidia jamii ndivyo Mungu anavyowabariki daima sina neno la zaidi zaidi ya ahsante "
Marehemu Daudi Mwangosi aliuwawa kinyama Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakati wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kilipokuwa kikifanya mikutano ya ufunguzi wa matawi wakati kukiwa na zuio la mikutano hiyo kutokana na kuongezwa kwa muda wa senza ya watu na makazi .Ndugu wa Marehemu Daudi Mwangosi mama Mfugale kushoto akitoka mahakama kuu kanda ya Iringa akiwa na furaha baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa leo kwa askari aliyeuwa kufungwa jela miaka 15 Picha zote na MatukiodaimaBlogMjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akiwa katika foleni ya ukaguzi wa polisi ili kuingia mahakama kuu kanda ya Iringa leoMjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akiwa katika foleni ya ukaguzi wa polisiMjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akifurahi jambo na ndugu yake mzee Marko Mfugale mahakamani hapo leoMdogo na marehemu Mwangosi Bw Mecky Mwangosi kulia akisalimiana na Rais wa UTPC Deo Nsokolo kabla ya mahakama kuanza leoRais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Bw Deo Nsokolo akizungumza na wanahabari baada ya hukumu ya kesi ya mauwaji ya MwangosiWanahabari mkoa wa Iringa wakimsikiliza Bw Nsokolo leoWanahabari wakiwa nje ya viwanja vya mahakama baada ya kesi kumalizika

Mjane wa Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba akitoka mahakamani hapo huku akiwa na uso wa furaha baada ya hukumu kutolewa kwa muuaji kufungwa miaka 15 jelaMjane wa Mwangosi akiwa katika viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi akizungumza na wanahabari ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa umoja wao


Rais wa UTPC Deo Nsokolo akiwa na mtaalam wa IT Lukelo Mwaipopo leo nje ya mahakama kuu kanda ya Iringa