Mzee amtuza 10,000/= Rais Magufuli baada ya kuamuru kituo cha mabasi na soko kuanza kazi bila kibali cha SUMATRA


Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za stendi ya mabasi ya abiria na soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. 

Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani ambako nako pia wana sehemu za biashara.


Rais Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo wakati akielezea changamoto za stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016


Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt. Magufuli kuhusiana na Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. 

Rais ameitaka SUMATRA ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu za biashara bila kuyatumia katika soko jipya wanadhibitiwa mara moja.


Wananchi wa Igunga wanalipuka kwa furaha na mzee huyu anatoa noti ya shilingi 10,000/- akitaka kumtuza Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua changamoto za stendi ya mabasi ya abiria na soko jipya zinazoikabili wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016


Rais Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele wa kiwango cha kwanza kutoka kwa uongozi wa wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016

Katuni: Thiwataki kabitha...Dodoma bila shurti


Maelekezo ya Zitto Kabwe kwa ACT Wazalendo baada ya kauli ya Rais MagufuliMaelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC ) kwa wanachama wote wa ACT Wazalendo ( KC/01/2016).


Tangu kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Utawala mpya umekuwa ukifanya kila juhudi kuminya uwezo wa Vyama vya Siasa kufanya Kazi zake kwa kisingizio kuwa huu ni wakati wa kufanya Kazi na kwamba Siasa zisubiri mwaka 2020.

Chama chetu kilipinga kwa nguvu zote uzuiaji huu wa shughuli za kisiasa kwani ni kinyume cha Katiba ya Nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa, sheria namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa Mara.

Mnamo tarehe 5 Juni 2016 Chama chetu kilifanya Mkutano wa Hadhara Mbagala jijini Dar Es Salaam na kutangaza Operesheni Linda Demokrasia. Lengo la Operesheni hiyo ( Tamko la Mbagala 2016 ) ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa Nchi ya kidemokrasia na kuepuka mwelekeo wa Utawala wa Imla ambao ni utawala wa kidikteta. Chama chetu asili ya uundwaji wake ni kupinga tabia za kidikteta tulizokumbana nazo ndani ya Vyama tulivyokuwamo.

Hivyo ilibidi tuwe mstari wa mbele kupinga dalili zozote za kuielekeza Nchi kwenye Uimla. Vyama unaweza kuunda utakapo, Nchi huwezi kuiunda ndio maana ni LAZIMA Sisi Kama wanachama wa Chama cha Wazalendo kupinga kwa nguvu zote kuminywa kwa Demokrasia na kuilinda kwa nguvu zetu zote.

Kufuatia Tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano kwamba shughuli za kisiasa zimezuiwa kwa niaba yenu nilitaka Vyama vyote vya Siasa nchini na wadau wengine wa demokrasia kuungana kwa pamoja kukataa Tamko hili ambalo linavunja Katiba ya Nchi ambayo Rais ameapa kuilinda na kuitetea. Wito wetu unanukuliwa hapa chini;

“Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita [ dhidi ya udikteta] pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria.”

Hata hivyo, hakuna Kiongozi wa Chama chochote kile ambaye aliona umuhimu wa kuunganisha nguvu na hivyo kujikuta kila Chama kinaendelea na operesheni zake.

Viongozi wetu akiwemo Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu walifanya juhudi zote kuwasiliana na watendaji wenzao wa Vyama vingine ili kufanya Kazi pamoja japo kwa uratibu lakini hatukupiga hatua yeyote ile.

Maelekezo Kwa Wanachama Wa Act­ wazalendo Juu Ya Kauli Ya Rais Magufuli Singida ­

Hivyo, Sisi sio sehemu ya operesheni yeyote ile iliyotangazwa na Chama kingine chochote kile isipokuwa Operesheni Linda Demokrasia ambayo sasa itaitwa Tamko la Mbagala la Juni 5, 2016.

Akiwa ziarani mkoani Singida, Rais amefafanua agizo lake la kuzuia mikutano ya kisiasa. Rais amesema kwamba hajazuia wabunge na madiwani kufanya mikutano ‘ KWENYE MAJIMBO YAO’. Kwanza Rais hana mamlaka ya kuruhusu au kuzuia Kazi za Wabunge na madiwani. Haya ni mamlaka ya KATIBA na sheria za Nchi. Hivyo ufafanuzi wake hauna maana yeyote ile.

Jambo la kushtusha ni agizo la Rais kwamba Wabunge hawana mamlaka ya kufanya mikutano nje ya majimbo yao. Hii ina maana hata Viongozi wa kisiasa ambao sio wabunge hawataruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa. Hii HAIKUBALIKI.

Anna Elisha Mghwira ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, anazuiwaje kufanya mikutano na wanachama wake nchini? Anazuiwaje kuongeza wanachama? Lakini mama Anna Mghwira aligombea Urais, kwanini asifanye mikutano kuwashukuru waliompa Kura japo hazikutosha?

Uchambuzi wa kitaalamu

Ni dhahiri Serikali ya Awamu ya Tano na sasa Chama tawala wameamua kubadili mwelekeo wa Nchi kisiasa ( kwa kubana uhuru wa kidemokrasia ) na kiuchumi ( kwa kuelekeza nguvu kwenye uchumi unaoelekezwa/endeshwa na dola ). Udhibiti wa Vyama vya Siasa ni moja ya hatua ya udhibiti wa jamii kwa ujumla wake.

Siku za usoni tutaona udhibiti wa waziwazi wa vyombo vya habari na kwa sasa tunaona namna Asasi za Kiraia ( CSOs) zilivyo kimya tofauti na miaka michache ya nyuma. Hizi zimejiweka kimya zenyewe na zitakazoinua sauti zitafuatiliwa na dola. Yote haya yanaturudisha nyuma katika katika kujenga Tanzania ya Kidemokrasia na yenye Maendeleo.

Utawala wowote ‘ regime ‘ hutaka kupata nguvu ya wananchi katika kujijengea uhalali. Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kuichukua vita dhidi ya ufisadi kama njia ya kujijengea uhalali na kwa kweli wananchi wengi waliochukizwa na vitendo vya kifisadi wanaunga mkono juhudi hizo.

Katika ziara yake ya Singida, Rais amenza kutumia maneno kama ‘ mabeberu ‘ na ‘ Maadili ya Mwalimu Nyerere ‘ maneno ambayo hayajawahi kutamkwa na kinywa chake. Hii inaonyesha kuwa Rais anaanza kukua/kukuzwa kiitikadi na hii itampa uhalali zaidi mbele ya jamii.

Hata Uamuzi wake wa kutekeleza maamuzi ya kuhamia Dodoma, na iwapo atatekeleza, itamjengea zaidi uhalali. Rais atautumia uhalali huu kujikita katika utawala na kuminya zaidi Demokrasia.

Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC )
  1. Chama cha ACT Wazalendo kiliundwa kwa madhumuni ya kurejesha Nchi kwenye misingi. Kupitia Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha tumeeleza misingi hiyo kwa kina. Naelekeza kwamba wanachama wote wa ACT Wazalendo wasome, kuelewa na kujadili Azimio la Tabora na kuchambua muktadha wake katika mazingira ya sasa ya Siasa za Nchi yetu.
  2. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo asione aibu kuunga mkono maamuzi yeyote ya Serikali au Chama kingine cha Siasa yanayoendana na Azimio la Tabora hususan vita dhidi ya ufisadi na kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi.
  3. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo akatae kwa namna anayoweza lakini kwa Amani mbinu zozote za kuminya Demokrasia nchini. Tamko la Mbagala la kulinda Demokrasia litumike kuongoza juhudi hizo. Chama chetu hakijatangaza maandamano na hivyo wanachama wetu wasiingie katika mambo hayo.
Hata hivyo kila mwanachama wa Chama chetu aandike barua kwa Rais Magufuli kwa namna anavyoona yeye kumtaka aache kuingiza Nchi kwenye utawala wa Imla. Chama chetu kina wanachama 431,120 wenye kadi. Ikulu ikipata barua 200,000 kutoka kila kona ya Nchi itafunguka macho.

Mwisho

Nawataka wanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo kukumbuka kuwa uasili wa Chama chetu ni kupinga kuburuzwa, ufisadi na Siasa za ujanja ujanja. Tujitahidi kwa nguvu zetu zote kutofanya yale ambayo Sisi tumeyakataa.

Viongozi wa kuchaguliwa kwenye vyombo vya uwakilishi Kama madiwani na wabunge wawe makini sana kutii Chama na misingi ya chama.

Tuwe mstari wa mbele kupinga ufisadi kwani rushwa ni adui wa Haki. Tuwe mstari wa mbele kutaka kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi. Sisi ndio Chama pekee chenye itikadi iliyo wazi. Tusiammie itikadi yetu popote tulipo na bila woga wala aibu.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama
30/7/2016

Photos: Mara river & sunset - Saadani, Bukoba, Geita, Bunda, Mwanza and lake Victoria @PMwihumbo

Saadani
Photos, courtesy of Pendo Mwihumbo, thank you for sharing (via Twitter)!

Geita
Bukoba
Mwanza
Mwanza
Mwanza
Mwanza

Lake Victoria
DNC 2016 speeches worthy watching again, and again

New Jersey Senator, Cory Anthony


U.S.A. First Lady, Michelle LaVaughn Robinson Obama, American lawyer and writer. 


Vermont Senator, Bernard "Bernie" Sanders, the longest-serving independent in U.S. A. congressional history.


U.S.A. 47th Vice President, Joseph Robinette "Joe" Biden Jr.


Michael Rubens Bloomberg, American business magnate, politician, and philanthropist. With a net worth of US$46.7 billion as of July 2016. The 6th richest person in the United States and the 8th richest in the world [Forbes].


Barack Hussein Obama II, The 44th President of the United States of America. The first African American to hold the high office.


Kareem Abdul-Jabbar, American retired professional basketball player. He owned eight playoff records and seven All-Star records. No player achieved as much individual and team success.


Khizr Khan, the father of a Muslim U.S. A. hero soldier, Capt. Humayun Khan who was killed in combat in Iraq.[video] Hotuba ya Rais Magufuli mkoani Singida


Mkuu wa Shule asimamishwa kazi kwa upotevu wa chakula cha wanafunzi


Taarifa ya habari ChannelTEN Julai 30, 2016


Kauli ya Wakili Kibatala baada ya Mkurugenzi kufukuzwa kazi na Rais Magufuli


Uganda, Tanzania pipeline: DRC, Burundi wants inclusion

THE government of the Democratic Republic of Congo (DRC) has shown willingness to use the Uganda-Tanzania Oil Pipeline set to be constructed in the country to transport crude oil from Kabale in Uganda to Tanga Port.

The Minister for Energy and Minerals, Prof Sospeter Muhongo, made the revelation in Dar es Salaam yesterday when opening a one-day meeting of ministerial Permanent Secretaries and Regional Commissioners from regions set to be involved in the course of the construction of the pipeline. Prof Muhongo said he was today expected to meet with the responsible minister from Congo to discuss how they would be involved in the project.

According to Mr Muhongo, Burundi is also expected to use the pipeline. He noted that the move by the government of DR Congo and Burundi to use the pipeline would be proper as the two countries would continue using the pipeline once Uganda Oil transport deal comes to an end.

He said the pipeline would also be used to transport oil from South Sudan. “The pipeline would be useful in the course of transporting oil from Lake Tanganyika if the search for oil in the lake is successful,” he said.

Meanwhile, the minister sounded a strong warning to residents against invading the lands that would be involved in the course of the construction of the pipeline. He said those who have invaded and others intending to do so should immediately pave the way as the government would not entertain anybody once construction starts.

“Those intending to invade should immediately stop as they would lose their money putting up houses and other infrastructure on land that would be used to construct the pipeline,” he said, tasking the RCs of the concerned regions to monitor the invaders.

He said research satellites would be used to establish those who would have invaded the construction lane land ahead of August, last year. “Those who will be found to have invaded the areas after August, last year - the start of the pipeline construction deal - will not be compensated,” he said.

He asked the RCs from the regions to be involved to provide the construction map of the pipeline in order to help abstain from unnecessary losses that they may incur in future. The pipeline to be constructed would pass through Kagera, Geita, Shinyanga, Dodoma, Manyara to Tanga.

He tasked the RCs to conduct awareness over the construction of the pipeline. In another development, Ugandans have started construction part of the project where they have provided 40 per cent shares of the project to five East African countries with each country holding eight per cent of the shares (150 million US-dollars).

Prof Muhongo said that plans were underway to involve private sectors to hold some shares (the eight per cent share for Tanzania) to supplement the government’s efforts in construction of the pipeline. Construction of the pipeline is scheduled to start in August, this year. It is expected to be completed before 2020.

This is how you get fined and/or land in jail in Tanzania if you disrespect the national flag


AS a way forward to restore national integrity, the Chief Government Printer, Mr Kassian Chibogoyo, has directed the Police Force to arrest anyone who will disrespect national emblems.

Government institutions that use worn-out or dirty national flags together with those who will be walking while the national flag is being raised or lowered shall face fines or an imprisonment term of not less than two years.
"National flags must be respected. We carried out a number of public education programmes on the importance of respecting the national flag. I now direct the Police Force to arrest all those who will be walking when the national flag is raised or lowered because it is against the National Emblems Act of 1971.
It is clearly stated that anyone who disrespects national emblems, including the national flag, will be fined, imprisoned for not less than two years or both punishments will be imposed," stated Mr Chibogoyo during a surprise visit to some of the government institutions with dirty or worn out national flags.
He said the operation is continuous. He directed government officials with improper national flags to change them immediately.

He, however, reminded on the timely raising and lowering of the national flag. Normally, the flag is raised at 6:00 am and lowered at 6:00 pm. Mr Chibogoyo also directed that the flags be bought at licensed institutions to avoid widespread mistakes by some private printers on getting the right colours when producing the national flags.
"For instance, most printers don't get it right on the blue colour on the flag. Instead they make it dark blue, which is legally wrong," he said. 
He noted that the Constitution states that it is only the president who has powers to modify the flag.
  • By Iddy Mwema, The Daily News

Africa after Apartheid: South Africa, race, and nation in Tanzania

The first page of the PDF of this article appears below.

Afr Aff (Lond) (2016)doi: 10.1093/afraf/adw042First published online: July 29, 2016
» Full Text (HTML) or Full Text (PDF)

CDA yatimua wapangaji ili ikarabati nyumba


Wakazi zaidi ya 100 leo wameondolewa kwa nguvu katika nyumba zinazomilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) baada ya kukaidi agizo la kuhama kwa hiari ili kupisha ukarabati.

Wamiliki hao waliondolewa na kampuni ya udalali ya Mvina, zoezi liloanza asubuhi leo chini ya usimamizi wa polisi waliokuwa na mabomu ya machozi na bunduki.

Awali wapangaji hao walipewa notisi ya kuhama kwa hiari ya siku 90 lakini baadaye wakaongezewa wiki moja iliyoisha leo.

Taarifa zinasema kuwa wapangaji ambao hawakuwepo wakati zoezi likiendelea, nyumba zao zilivunjwa milango na vifaa vyao kutolewa nje.

Baadhi ya wapangaji hao ambao hulipa kodi ya kati ya Sh 18,000 hadi 22,000 kwa mwezi kwa nyumba ya nyumba vitatu wanadaiwa madeni ya zaidi ya Sh 7 milioni.

Kwa mujibu wa CDA baada ya kukarabati huo wapangaji watakaokubali kuendelea kukaa katika nyumba hizo wataingia mkataba upya wa kupanga.


Jeshi la Polisi lamwita Mbowe


Freeman Mbowe via Twitter

Dodoma ni mbali kutoka wapi?

Taarifa ya Rais Magufuli ya kumtengua uongozini Mkurugenzi aliyeteuliwa majuzi


Agizo la Spika wa Bunge: Vikao vyote vya Kamati za Kudumu vifanyike Dodoma