Kwa wanaotaka kuuza au kununua kitabu cha ushushushu


Kitabu kuhusu taaluma ya uafisa usalama wa taifa (ushushushu) sasa kipo jijini Dar tayari kwa kusambazwa kwenye maduka ya vitabu sehemu mbalimbali nchini Tanzania.

Ninapenda kutumia fursa hii kuwakaribisha watu wenye maduka ya vitabu au wenye maduka ya baidhaa nyingine ambao wangependa kununua kitabu hiki kwa jumla kwa bei ya sh 8,000 kwa kopi kisha wao kukiuza kwa bei watakayojipangia wao.Pia fursa hii ni kwa wenye vibanda vya kuuza magazeti au wachuuzi wa bidhaa za mkononi.

Kila mnunuzi atapatiwa kipeperushi cha bure cha "kinapatikana hapa"Kwa manunuzi ya jumla ya kitabu wasiliana nami kwa barua pepe [email protected] au kwa Tanzania, namba 0754682554 au 0767216401 (jina la mhusika ni JOHN)

Kwa manunuzi ya rejareja, kwa sasa kitabu kinapatikana katika maduka ya vitabu yafuatayo (orodha hii ni endelevu, maduka mengine ya vitabu yatazidi kutangazwa baadaye)

Dar es Salaam
  • Mlimani Bookshop, Kariakoo 0754269042
  • General Booksellers, Mkwepu Str 0787368252
  • Zai Bookshop, Kariakoo 0754292532
  • Elite Bookstore, Mbezi Beach Tangi Bovu 
  • near Goba Road 0754767336
Moshi
  • APE Book, Rindi Lane, Opposite I&M Bank 0754767336
Mwanza
  • Gunda Bookshop near NHC Regional Office, Bantu Str Kemondo 0753969421
  • Victoria Bookshop, along Bantu Street, Kemondo 0755375034
Tanga
  • Hafat Bookshop, Barabara ya Saba, 0767216403
Musoma
  • Nyambusi Bookshop Opposite NMB Bank Main Branch, 0767578565

Taarifa ya habari ChannelTEN Agosti 5, 2016Waziri aagiza gereza la Iringa Mjini lihame

Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa pili kushoto wakisalimiana kwa furaha na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abeid Kiponza huku waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Mwigulu Nchemba na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto) wakiangua kicheko
Na MatukiodaimaBlog

Viiongozi wa dini wajionea maendeleo ya ujenzi wa JNIA Terminal 3

Viongozi wa dini wanaounda Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakiomba dua kuombea ujenzi wa Uwanja wa Jengo la Tatu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walipofanya ziara ya siku moja kutembelea jengo hilo Dar es Salaam jana.
Na Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imesema inatarajia kujenga njia ya pili ya kurukia ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya kubainika uwanja njia ya sasa haitatosha ifikapo mwaka 2025.

Tayari mamlaka hiyo imeshaanza kufanya mchakato wa kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuanza kujenga njia ya pili ya kurukia ndege.

Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam jana waliotembelea mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Ramadhan Maleta alisema, wataalamu walifanya utafiti na kubaini kuwa kufikia 2025 njia moja inayotumika sasa haitatosha kwa kuwa mahitaji yatakuwa yameongezeka.

Maleta alisema, pia Serikali iko katika mchakato wa kutafuta pesa kwa ajili ya kufanya maboresho ya jengo la abiria (terminal II), maboresho ambayo yatafanyika kuanzia mwakani.

“Maboresho ya jengo la terminal II yataanza mwakani, kwa sasa Serikali iko katika mchakato wa kutafuta pesa kwa ajili ya kufanya maboresho hayo ili tuweze kutoa huduma bora,” alisema Maleta.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema, mradi huo ni muhimu zaidi kwa kuwa utazidi kuimarisha heshima ya Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.

Pia alisema jengo hilo likikamilika kwa wakati litawasaidia Watanzania na pia litaongeza idadi ya ndege kubwa kutua nchini.

Alisema ujenzi wa jengo hilo ni ishara tosha kuwa Serikali inafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi wake maendeleo, na kwamba kamati hiyo itashirikiana na Serikali si tu katika kuhamasisha masuala ya amani bali hata maendeleo.

Katibu wa Kamati hiyo, Padri John Solomon alisema, kikubwa kilichowafanya kutembelea mradi huo ni kutaka kuona juhudi za Serikali kuhakikisha Tanzania inakuwa na uwanja mkubwa wa kisasa.

Mbali na ziara hiyo, kamati hiyo pia ilitumia nafasi hiyo kufanya maombi na duoa kwa ajili ya mradi huo ili uweze kukamilika salama bila kutokea kwa tatizo la aina yoyote ambalo linaweza kukwamisha.

Akitoa ufafanuzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Mradi huo, Mohammed Millanga alisema, ujenzi wa jengo hilo litakalohudumia abiria milioni sita kwa mwaka unatarajiwa kukamilika Desemba mwakani.

Alisema hadi sasa mradi huo ambao ulikuwa utekelezwe kwa awamu mbili kwa sasa awamu hizo zinatekelezwa kwa pamoja na umekamilika kwa asilimia 45.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Mohamed Milanga akitoa maelezo kwa viongozi hao wa dini waliotembelea uwanja huo Dar es Salaam jana.


Mwonekano wa uwanja huo unaojengwa.


Mwonekano wa chumba cha wasafiri katika jengo hilo.


Baadhi ya wakandarasi wa ujenzi huo.


Askofu, Stephen Mang'ano wa Kanisa la Menonite (kushoto), akiongoza maombi ya kuombea ujenzi wa uwanja huo.


Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Ramadhan Maleta (wa pili kulia), akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo mbele ya viongozi wa dini wanaounda Kamati ya Amani.


Meneja wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Wolffgang Marschick akizungumza na viongozi hao wa dini.


Viongozi hao wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kukamilisha ziara yao.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com-simu namba 0712-727062)