Mambo 7 yatakayokufanya uzungumzwe vizuri


Moja ya kipimo cha mafanikio ya mtu katika maisha yake ni kusemwa vizuri na watu kwa kuwa hiyo ndiyo ishara ya upendo walionao kwake. Je, kama ungeombwa kuorodhesha tabia zako ambazo unafikiri zinaweza kuwafanya watu wakuseme vizuri ungeweza kuandika ngapi? Je, unaweza vile vile kuandika zile ambazo zinaweza kukufanya usemwe vibaya? Kama hujawahi kufanya hivyo hebu jaribu siku moja.

Je, unajua jinsi unavyosemwa na watu katika jamii? Wanakusema vizuri au vibaya? Hili ni moja kati ya changamoto zinazotukabili katika maisha kwa kuwa watu huwa hawapendi kuwambia wenzao uso kwa uso tabia zao nzuri au mbaya. Hupenda kusema mahali ambapo mhusika hayupo. Mara nyingi maelezo ya jinsi jamii inavyowaona watu hutolewa siku ya mazishi yao.

Moja ya kipimo cha mafanikio ya mtu katika maisha yake ni kusemwa vizuri na watu kwa kuwa hiyo ndiyo ishara ya upendo walionao kwake. Je, kama ungeombwa kuorodhesha tabia zako ambazo unafikiri zinaweza kuwafanya watu wakuseme vizuri ungeweza kuandika ngapi? Je, unaweza vile vile kuandika zile ambazo zinaweza kukufanya usemwe vibaya? Kama hujawahi kufanya hivyo hebu jaribu siku moja.

Kwa kuwa kila mmoja wetu anapenda kupendwa, kuthaminiwa na kusemwa vizuri tunakabiliwa na swali moja kubwa. Tufanye nini katika maisha ili tuwe na mvuto na upendo kwa watu na tusemwe vizuri jamii?

Kuna mambo mengi mema tunayoweza kufanya ili tuwe na mvuto na sifa nzuri kwa watu na kuwafanya watuseme vizuri. Jambo la kwanza ambalo ni muhimu kuliko yote ni kujenga ujamaa na udugu au urafiki ambao huleta maelewano na ushirikiano. Mara nyingi nimewahi kusikia mtu akisema, “Amenipita bila kunisalimu!” Anayesema hivyo huwa hafikirii kuwa na yeye pia ana makosa kwa sababu amemtazama mtu huyo akipita hadi akatoweka bila kumsalimu. Wote wana makosa.

Huenda yule aliyesemwa na mwenzake naye amesemwa hivi, “Nimepita ananitazama tu bila kunisalimu! “Fanya juhudi kila mara uwe wa kwanza kujenga mazingira ya maelewano.

Katika makala hii tutataja mambo saba miongoni mwa mengi ambayo wanafalsafa husema yanasaidia kumfanya mtu aelewane na watu. Haya yalibuniwa na mjasiriamali maarufu huko Marekani Benjamin Fairless.


Jizoeze kuwa na tabia na mwenendo unaopendwa na watu


Hayati Shaaban Robert aliwahi kusema, “Tabia nzuri ni vazi analotakiwa mtu kulivaa kila anapotoka hadharani “Binadamu anapaswa kuwa na tabia nzuri katika jamii ili akubalike na kupendwa. Tabia nzuri hujumuisha mambo mbalimbali kama vile ucheshi, wema, huruma, heshima, uadilifu, ukarimu au upole.


Kuwa wa kwanza kuweka mazingira yanayojenga ujamaa na udugu


Watu husema, “Hali gani ndiyo mwanzo wa kujuana.” Kuwa na tabia ya kujitambulisha na kuwatambua watu wengine na kuwasalimu kwa majina yao kila mnapokutana. Salamu ya ucheshi na tabasamu huwa njia ya haraka ya kujenga uelewano na ushirikiano. Hali hii hujenga msingi wa mazungumzo na kutendeana wema.


Kukubali kuwa kuna tofauti na upungufu baina ya binadamu


Katika kuishi na kujenga uhusiano na watu hatuna budi kutambua kuwa binadamu hutofautiana katika utimilifu wa tabia, huwa ana haki ya kukosea na kila mmoja huwa ana haki ya kutofautiana na wengine. Kwa kanuni hizi za kibinadamu, kila tunapojaribu kujenga urafiki na maelewano tusiwachukie au kuwanyanyapaa watu kwa kuwa wanapendelea mambo yanayotofautia na yale tunayoyapenda sisi, mradi hayahusiani na uhalifu.

Hata hivyo, siyo lazima sisi tupende yale wanayoyapenda wengine bali tusiwachukie kutokana na yale wanayoyapenda. Tena vyema tukumbuke kuwa watu huwa hawapendi kuambiwa wamekosa. Wala tusihangaike kuwafanya watu wabadili tabia zao ziwe kama zetu ili kuwafanya marafiki zetu. Tukumbuke kuwa watu wote tukiwa na tabia zinazofanana dunia itapooza.

Tusiwapime watu ubora wao kwa mtazamo hasiTunapochunguza ubora wa watu katika kujenga urafiki tusiwachunguze sifa zao kwa mtazamo hasi bali tutumie mtazamo chanya. Kwa mfano watu wawili wanaweza kutaja sifa za mtu mmoja wakatofautia tu kwa sababu mmoja amezitazama kwa mtazamo chanya na hasi. Kwa mfano, mtu mwenye mtazamo chanya atasema, “Fulani ni mpole sana. Anapoongea na wageni huwasikiliza kwa makini bila kuwakatiza mpaka wanapofika mwisho. Kisha ndipo yeye hutoa maoni yake.” Mwenye mtazamo hasi husema hivi,” Fulani ni mtu asiye mcheshi. Hapendi wageni na wanapokuwa wakiongea yeye hukereka akanyamaza kimya na kuwaacha waongee pekee yao.

Tujifunze kutoa takrima ya mazungumzoHakuna kitu ambacho humfanya mtu ajihisi ameheshimiwa kama anapopewa nafasi ya kusema na akasikilizwa. Kama utataka kuwa na marafiki wengi hasa miongoni mwa watu wa hali ya kawaida, hautawafurahisha zaidi kuliko kuwapa nafasi ya kuongea na wewe ukawasikiliza huku akiwafurahia na kuwawekea mazingira yatakayo wafanya awe huru kuongea.

Kila wakati wafanye watu wajihisi wako katika hadhi ya juuMoja katika tabia mbaya tunapofanya jitihada ya kujenga urafiki na ushirikiano ni kujifanya watu wakuone uko juu kuliko wao. Jenga tabia ya kuzungumza na watu huku ukiwafanya wajione mko sawa na unawaheshimu na kuwathamini. Tabia hii huwafanya wakuone unawajali na kufanya upendo wao kwako uchanue.

Wakati mambo yanapoharibika, usiwalaumu wengine


Katika maisha kila siku kila tatizo linapotokea tumezoea kumtafuta wa kumlaumu. Mara nyingi tunawasikia watu wakisema, “Isingekuwa fulani nisingekuwa hivi! “Hakuna jambo linaloharibu upendo kama kulaumiana. Ili uwe na maelewano mazuri na watu epuka kabisa kutupia lawama mtu au watu. Tunapokuwa na tabia nzuri na upendo kwa watu tunakuwa wepesi kubebeka. Lakini tunapokuwa na tabia mbaya na mwenendo usiopendeza katika jamii watu wanasita kutupatia vyeo au wadhifa katika maisha. Kwa hakika tunakuwa wazito wala hatubebeki kwa urahisi.

Be a great writer, presenter: The 3 parts of a powerful speech


Step 1: Prepare
 • What kind of speech is this?
 • Who is your audience?
 • What do you want your audience to feel?
 • What’s your overarching point of view on the topic?
Step 2: Organize
 • An Attention-Getting Introduction
 • A Preview
 • Points 1 Through 3: Make your case. 
 • A Recap
 • Hold Q&A before you wrap up 
 • The Closer: It’s almost over—but not quite
Step 3: Present With Passion
 • Don’t just stand up there
These points are explained in a short, concise and to the point article at themuse.com

Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Agosti 8, 2016
CUF kufa kifo cha mende?

CHAMA cha Wananchi (CUF) ni kama kipo kuzimu. Kimelegea, kimechuja na kwa sasa kimegota, --- limechapisha gazeti tando la MwanaHALISI Online.

CUF ya Prof. Ibrahim Lipumba, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa kabla ya kujiweka pembeni, si hii inayoongozwa na Twaha Taslima ambaye amebeba mikoba ya uenyekiti kwa ‘dharura’.

Wapo wanaochekelea kuiona CUF ya sasa ikikosa miguu ya kusimama, ikipoteza mvuto na mvumo wake katika siasa za nchi hii.

Wapo wanaotamani CUF ifutike leo, kesho, wapo wanaovutiwa na mwenendo wa kuchechemea wa CUF kwa sasa lakini pia wapo wanaotamani Taslima awe mwenyekiti wa taifa wa chama hicho. Si kwa wema, isipokuwa ni kwa imani kwamba, Taslima ndio njia sahihi ya kuzima nuru ya CUF kwenye uwanja wa siasa nchini. Dalili hizo zipo wazi, tangu Taslima aingie madarakani chama hicho hakijulikani kinafanya nini, kina mipango gani na kina mwelekeo upi? Chama hicho kwa upande wa Bara ni kama kimebemendwa.

CUF inayovuma ni ile ya Zanzibar chini ya Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho. Kwa sasa unapozungumzia CUF unazungumzia Zanzibar. CUF ya Bara ipo ziiii! Sababu ni kwamba, CUF ya Bara baada ya Prof. Lipumba haijapata mbadala, anayeshika mikoba yake hana sifa, uwezo, ubunifu na hata uono wa kisiasa.

CUF ya Bara kwa sasa inajifichwa kwenye kwapa la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Inategemea huruma ya matamko ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha NCCR-Mageuzi ili kusikika.

CUF ya Taslima imepoa, haina harakati kama zile zilizokuwa zikifanywa na Prof. Lipumba. Watendaji wa CUF kwa sasa wanaishi kwa majungu. Baadhi yao wana fikra finyu kuhusu mwelekeo wa chama hicho. Unapozungumza nao hawaoneshi mwelekeo wa chama hicho, wanachojali ni kwamba ‘wapo huru’.

Prof. Lipumba alijiuzulu Agosti mwaka jana kwa madai kuwa, viongozi wenzake wanne kutoka UKAWA  kumkaribisha ndani ya umoja huo Edward Lowassa na kisha kumteuwa kuwa mgombea wake wa urais. Ndipo Taslima akatwaa nafasi hiyo kwa muda. Kinachofanyika ndani ya chama hicho hakieleweki, mwelekeo wa CUF unatia mashaka.

Taslima ana utofauti mkubwa na Prof. Lipumba kwenye siasa za ushindani katika nchi hii, ni kwa kuwa Prof. Lipumba alikuwa na uwezo wa kuchambua na kuandika mambo ya kijamii, kiuchumi na kisasa jambo ambalo halipo kwa kaimu mwenyekiti wa sasa (Taslima). Prof. Lipumba ana ushawishi mkubwa na kwa watu wengi tofauti na Taslima ambaye mpaka sasa sehemu kubwa ya Watanzania hawamjui, hawajawahi kumuona na pia uwezo wake hauonekani.

Kwa bahati mbaya Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu (Bara) hana uwezo wa kuhuisha harakati za CUF.

Lipo la kujifunza kwa CHADEMA wakati walipoamua kumtwaa Lowassa ambaye alikuwa amechafuka kutokana na kauli zao za awali.

Tathimni ndani ya CHADEMA zilionesha kuwa Lowassa bado ‘keki’ kwa taifa. Licha ya baadhi ya viongozi wa chama hicho kutotaka kumpokea lakini alijiunga na chama hicho hivyo kuwa mwiba kwa CCM. CHADEMA ilisoma alama za nyakati na kwa kuwa, lengo la siasa ni mafanikio, ilimtwaa Lowassa ambaye mafanikio yake ndani ya CHADEMA na UKAWA hakuna anayeweza kubeza. CHADEMA ilimpoteza Dk. Willibrod Slaa kwa kuwa, thamani yake mbele ya Lowassa ilikuwa ndogo.

Turudi CUF, thamani ya Taslima ni kubwa kuliko Prof. Lipumba katika mazingira ya sasa? Sihitaji jibu.

Bila shaka, uamuzi wa kukurupuka, uliojaa chuki, husda na ujinga uliotamalaki unaweza kuizika CUF.

Pamoja na kutangaza nia ya kuitaka nafasi ya uenyekiti, lakini kwa sasa Taslima sio mtu sahihi kwa nafasi hiyo vinginevyo chama hicho kitakufa kifo cha mende.

Taarifa ya habari ChannelTEN Agosti 7, 2016


IRS warns of surge in: Automated phone scam calls; Fake tax pays using cards

IRS Warns Taxpayers of Summer Surge in Automated Phone Scam Calls; Requests for Fake Tax Payments Using iTunes Gift Cards

WASHINGTON — The Internal Revenue Service today warned taxpayers to stay vigilant against an increase of IRS impersonation scams in the form of automated calls and new tactics from scammers demanding tax payments on iTunes and other gift cards.

The IRS has seen an increase in “robo-calls” where scammers leave urgent callback requests through the phone telling taxpayers to call back to settle their “tax bill.” These fake calls generally claim to be the last warning before legal action is taken. Once the victim calls back, the scammers may threaten to arrest, deport or revoke the driver’s license of the victim if they don’t agree to pay.

“It used to be that most of these bogus calls would come from a live-person. Scammers are evolving and using more and more automated calls in an effort to reach the largest number of victims possible,” said IRS Commissioner John Koskinen. “Taxpayers should remain alert for this summer surge of phone scams, and watch for clear warning signs as these scammers change tactics.”

In the latest trend, IRS impersonators are demanding payments on iTunes and other gift cards. The IRS reminds taxpayers that any request to settle a tax bill by putting money on any form of gift card is a clear indication of a scam.

Some examples of the varied tactics seen this year are:
 • Demanding payment for a “Federal Student Tax.” See IR-2016-81.
 • Demanding immediate tax payment for taxes owed on an iTunes or other type of gift card
 • Soliciting W-2 information from payroll and human resources professionals. See IR-2016-34.
 • “Verifying” tax return information over the phone. See IR-2016-40.
 • Pretending to be from the tax preparation industry. See IR-2016-28
Since these bogus calls can take many forms and scammers are constantly changing their strategies, knowing the telltale signs is the best way to avoid becoming a victim.

The IRS will never:
 • Call to demand immediate payment over the phone, nor will the agency call about taxes owed without first having mailed you a bill.
 • Threaten to immediately bring in local police or other law-enforcement groups to have you arrested for not paying.
 • Demand that you pay taxes without giving you the opportunity to question or appeal the amount they say you owe.
 • Require you to use a specific payment method for your taxes, such as a prepaid debit card, gift card or wire transfer.
 • Ask for credit or debit card numbers over the phone.
If you get a phone call from someone claiming to be from the IRS and asking for money and you don’t owe taxes, here’s what you should do:
 • Do not give out any information. Hang up immediately.
 • Contact TIGTA to report the call. Use their “IRS Impersonation Scam Reporting” web page or call 800-366-4484.
 • Report it to the Federal Trade Commission. Use the “FTC Complaint Assistant” on FTC.gov. Please add “IRS Telephone Scam” in the notes.
 • If you think you might owe taxes, call the IRS directly at 800-829-1040.

Sabodo azungumzia taarifa za matrilioni ya kujenga Dodoma


Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo ameitaka Serikali kuwachangisha wananchi ili kupata fedha za kuhamishia makao makuu ya Serikali mjini Dodoma, limeandika gazeti la  MWANANCHI.

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.
“Nataka niweke suala hili vizuri, sina fedha za aina hiyo popote pale. Ninazo mali kadhaa lakini sina fedha zote hizo. Watu wengi wanakuja kwangu, wanakuja hapa, nipe pesa, nipe pesa, hakuna pesa hapa,” 
alisema Sabodo na kuongeza: 
“Mimi ni kama kichocheo tu, kama ndimu unatia kwenye soda. Nilichosema ni kutafuta juhudi kutoka kwa kampuni za India na Singapore kufanikisha ujenzi wa makao makuu ya Dodoma, lakini sina kiasi chote hicho cha fedha,” alisema.
Juma moja lililopita, gazeti la serikali, HABARI LEO lilichapisha habari ifuagayo...

MFANYABIASHARA maarufu, Mustapha Jaffer Sabodo ametangaza kutoa dola za Marekani bilioni 5 (Sh trilioni 10) kwa ajili ya kuwekeza mkoani Dodoma, ikiwa ni njia ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda mkoani humo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Sabodo alisema atawekeza kiasi hicho cha fedha, iwapo serikali yote itahamia mkoani humo, itakuwa ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye alitamani kuona mkoa huo unakuwa makao makuu ya nchi.

Alisema alichofanya Rais Magufuli, kimewashinda marais wengine waliomtangulia, hivyo yeye kama mfanyabiashara na mtu mwenye mapenzi makubwa kwa nchi yake, lazima aunge mkono hatua hiyo ya Serikali kuhamia Dodoma ambayo aliita ‘Azimio la Dodoma’.
“Niliposikia anatangaza kwenye televisheni ya taifa kwamba Serikali itahamia Dodoma, ilikuwa mara yangu ya kwanza baada ya miaka mingi kupita, nilitabasamu moyoni, jambo ambalo lilinitokea miaka 10 ya kwanza ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere. “Leo nimesikia kutoka kwako nimeona ile roho ya Nyerere imezaliwa tena. “Kwa hiyo natangaza kuunga mkono Azimo la Dodoma kwa kuwekeza dola za Marekani bilioni 5, ambazo zitatumika kwa ajili ya uwekezaji mkubwa katika huduma mbalimbali za jamii mkoani humo,” alisema Sabodo.
Sabodo alisema atatoa fedha hizo ili zitumike kuwekeza kwenye viwanda kama vya mvinyo, viwanda vya kusindika mihogo na viwanda vingine ambavyo vitahitajika katika mkoa huo.

Alisema kuwepo kwa huduma hizo mkoani Dodoma, kutasaidia kuufanya mji huo kukidhi matakwa ya watumishi wa umma watakaohamia huko.

Mfanyabiashara huyo aliongeza kuwa atafanya uwekezaji mkubwa huo kwa sababu lengo lake ni kuona mji wa Dodoma, unaungana na miji ya jirani kama Mpwapwa, Kondoa na Manyoni ili kutoa fursa ya kupanua huduma mbalimbali katika makao makuu hayo ya nchi.

Sabodo alisema kwamba juhudi zake za kuwekeza katika huduma za jamii kama shule, pia ataziendeleza katika mkoa huo kwa kuhakikisha kwamba zinajengwa shule kadhaa za kisasa, ambazo zitamudu mahitaji ya watu wa eneo hilo.

Kwa upande wa huduma ya afya, Sabodo alisema atatumia umaarufu wake kuwashawishi wamiliki wa Hospitali ya kimataifa ya Apollo ya India ili waje nchini wakashirikiane naye kujenga hospitali ya kisasa, ambayo itakuwa inatoa huduma za kisasa mkoani humo.
“Mnaifahamu hospitali ya Apollo ni wawekezaji wakubwa katika huduma za afya, kwa kusukumwa na hatua hii ya Rais nitaongea nao tushirikiane katika kujenga huduma za jamii katika mji huo,” alisema Sabodo.
Pia alisema atawashawishi wawekezaji wengine kutoka nchi za India, Singapore na kwingineko kuja kuwekeza katika mji huo wa Dodoma katika sekta ya viwanda, kuhakikisha kwamba azma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda inatimia.

Sabodo ambaye alisema wazi kuwa utendaji wa Rais Magufuli, umemvutia kutokana na hatua yake ya kupiga vita rushwa, alitangaza kuwa kuanzia sasa hatatoa tena msaada kwa vyama vya upinzani kama ambavyo amefanya miaka ya nyuma kama njia ya kuimarisha demokrasia nchini.
“Huko nyuma nilikuwa nawapa CHADEMA fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuimarisha demokrasia, sasa natangaza tena kwamba sitawapa tena fedha, niwape za nini wakati Rais aliyeko madarakani anafanya kazi ambayo ndio nilikuwa naipigania? alihoji Sabodo.
Sabodo ni mfanyabiashara wa kitanzania mwenye asili ya Kihindi ambaye alizaliwa mkoani Lindi. Katika maisha yake amekuwa anafanya biashara katika nchi za Kenya, Ufaransa, India, Sudan na Zimbabwe.

Pamoja na biashara zake, Sabodo amekuwa anajihusisha kuchangia katika miradi ya maendeleo ya huduma za jamii, uimarishaji wa demokrasia nchini na pia alishiriki kutunisha mfuko wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa kuanzisha bahati nasibu.

Masomo ya sayansi Form I - IV; Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala, ni lazima - WaziriSERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine, limeripoti gazeti la HABARI LEO.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Tanga na Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na nne.

Alisema hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.

Alisema kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi, wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.

Hatua hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana wanachagua kusoma masomo ya sanaa.

Alisema ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo ya sayansi.
"Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,” alisema Profesa Ndalichako.
Alisema Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri kupitia elimu waliyopata.

Aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumzia kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.

Alisema pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao kutoka nje yakaongezeka.

Katibu wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya mazingira ilivyo nchini.

Alisema ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba yenye vifaa na walimu wa kutosha.

Alisema iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Walimu washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.

Pamoja na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa kufundisha maeneo hayo.

Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Brazil yaonesha nia kuwekeza Tanzania kuzalisha umeme wa maji na mabaki ya miwa

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente, wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Na Veronica Simba

Serikali ya Brazil imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia maji na mabaki ya miwa. Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente, alipomtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake na kufanya mazungumzo naye.

Balozi Puente alimweleza Profesa Muhongo kuwa nchi yake inao ujuzi na uzoefu wa kutosha katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali hususan maji.

Alisema, Brazil ingependa kuchangia kufanikisha azma ya Rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
“Kutekeleza mchakato wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda, unahitaji umeme mwingi unaotokana na vyanzo mbalimbali. Ni bahati nzuri kwamba Tanzania inazo njia za kufanikisha azma hiyo,” alisema.
Alisema kuwa, nchini Brazil, kuna Kampuni kubwa zenye uzoefu wa muda mrefu unaofikia miaka 20 hadi 40 katika kazi hiyo, ambazo huzalisha umeme wa maji nchini mwao na hata nje ya nchi.

Pia, alitaja eneo jingine ambalo nchi yake ina nia ya kuwekeza kuwa ni uzalishaji wa umeme unaotumia mabaki ya miwa ambayo aliielezea kuwa chanzo kizuri cha nishati safi.

Balozi Puente alisisitiza kuwa, Brazil ikiwa ni nchi inayozalisha miwa kwa kiwango kikubwa duniani, itasaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati kwa kuzalisha umeme unaotokana na mabaki ya miwa kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Kwa upande wake, Waziri Muhongo, akimjibu Balozi Puente, alikiri kuwa kuwa Brazil ina ujuzi, uzoefu na uwezo mkubwa hususan katika maeneo ambayo Balozi aliyataja na hivyo akamwambia nchi hiyo inakaribishwa kuwekeza Tanzania kwa kufuata masharti na utaratibu uliowekwa na Serikali.

Akizungumzia zaidi kuhusu utaratibu wa uwekezaji, Waziri Muhongo alieleza kwamba Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara yake, inabadilisha utaratibu wa kupokea wawekezaji katika sekta husika.

Alisema, kunaandaliwa utaratibu maalum utakaokuwa wa wazi na kuruhusu ushindani kwa wenye nia ya kuwekeza kwa malengo ya kupunguza au kuondoa kabisa mazingira ya rushwa na muda mrefu unaotumika katika majadiliano pasipo sababu za msingi.

Profesa Muhongo alifafanua zaidi kwamba, Serikali itaweka mazingira mazuri zaidi ya ushindani kwa kuandaa maelezo ambayo pamoja na mambo mengine yatabainisha aina mbalimbali za vyanzo vya umeme vilivyopo nchini pamoja na maeneo vilipo.

Alisema, Kampuni zenye nia ya kuwekeza zitakaribishwa kupendekeza viwango vya bei vitakavyotumika kuuza umeme utakaozalishwa na zitashindanishwa, ambapo washindi wachache watachaguliwa kwa ajili ya majadiliano kabla ya kuingia mkataba wa uwekezaji husika.
“Kwa hivyo, tunaandaa kabrasha maalum litakalokuwa na maelezo husika na litakuwa tayari mwezi wa Septemba mwaka huu. Kabrasha hilo lenye maelezo litatumika kama mwongozo wa ushindanishaji maombi mbalimbali ya uwekezaji hususan katika kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kwa uwazi,” alisisitiza.
Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na gesi asilia, makaa ya mawe, maji, jua, upepo, jotoardhi, mawimbi ya bahari pamoja na nishati mbadala. Waziri Muhongo alisema kuwa maelezo hayo maalum yatasambazwa kwa wadau mbalimbali wa sekta husika wakiwemo wale wote wenye nia ya kuwekeza ikiwa ni pamoja nan chi ya Brazil kupitia Ubalozi wake hapa nchini.
“Kwa kutumia Kabrasha hilo maalum lenye maelezo husika, wewe Balozi utaweza kuwashawishi wafanyabiashara kutoka nchini kwako kutoa mapendekezo ya uwekezaji ambayo yana vigezo vyote muhimu vinavyoshawishi wapate fursa husika za uwekezaji katika sekta ya nishati,” Profesa Muhongo alimweleza Balozi Puente.
Kuhusu Mradi mkubwa wa ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, ambao pia Brazil imeonesha nia kuwa ingependa kuwekeza kwa kushirikiana na Tanzania; Profesa Muhongo alisema Serikali itaweza kulisemea hilo baada ya kipindi cha miezi takribani 45 kupita, ambapo mambo yote ya kisheria kuhusu Mradi huo yanatarajiwa kuwa yamekamilika.

Aidha, Profesa Muhongo alitumia fursa hiyo kuomba nafasi za masomo nchini Brazil kwa wanafunzi wa kitanzania katika ngazi za Shahada za Uzamili na Uzamivu katika sekta ya Nishati hususan Mafuta na Gesi, kwa kuzingatia kuwa Brazil imeendelea sana katika sekta hiyo.
“Ninyi mnazo Taasisi bora kabisa za Utafiti duniani. Mnafanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali.”
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, Brazil ni miongoni mwa nchi Tano (5) bora duniani zinazozalisha umeme kwa kutumia nishati jadidifu kwa sababu umeme mwingi wanaozalisha unatokana na maji, kutoka katika Mito mikubwa waliyonayo.


Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (Kushoto), akisaini Kitabu cha Wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), alipomtembelea Waziri na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika uwekezaji kwenye sekta ya nishati.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Carlos Alfonso Puente (kulia), wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala ya uwekezaji katika sekta za nishati na madini. Wengine pichani ni Maafisa wa Wizara waliohudhuria mkutano huo.

Serikali kutumia mataruma ya Kongolo kujengea reli ya kisasa

Waziri Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akikata moja ya kifaa kinachotumika kujengea reli wakati alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, Kongorl Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.
Serikali imesema itatumia kiwanda cha Kongolo cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kilichopo Mbeya kuzalisha mataruma yatakayotumika kwenye ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) inayotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni ili kupunguza gharama.

Hayo ameyasema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipotembelea kiwanda hicho kuona utendaji kazi na uzalishaji unaopatikana na kuiagiza kamati maalumu ya ujenzi wa reli hiyo kutembelea kiwandani hapo kuangalia uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hicho.

Profesa Mbarawa amesema Serikali ina dhamira ya kufufua viwanda hapa nchini ili kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania na kuifikisha nchi katika uchumi wa kati kupitia mapinduzi ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
"Nitahakikisha mkandarasi atakeyejenga reli hii anatumia mataruma yatakayozalishwa katika kiwanda hiki, badala ya kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nchi za nje", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa kwa kutumia kiwanda hicho Serikali itaokoa pesa ambazo zitaisaidia TAZARA kujiongezea mapato yatakayotokana na matengenezo ya mataruma na kupanua wigo wa kibiashara kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amekagua maabara ya kupima viwango na ubora wa kokoto na nondo kilichopo kiwandani hapo na kutoa mwezi mmoja kwa TAZARA kupata cheti cha ukaguzi kutoka Shirika La Viwango (TBS), ili iweze kurasimishwa rasmi.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa kuzalisha mataruma katika kiwanda cha Kongolo cha TAZARA-Mbeya Eng. Boniface Phiri amesema kuwa fursa ya kuwa sehemu ya mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa itaongeza uzalishaji wa kiwanda na kukuza pato la Mamlaka. "Kwa kushirikiana na wenzetu tutaongeza vifaa ili tuweze kuzalisha kwa wingi na ubora unaotakiwa katika mradi huu", amesema Eng. Phiri.

Kiwanda cha Kongolo ni kiwanda pekee katika nchi za Afrika na kati kinachozalisha mataruma kwa ajili ya reli na kina uwezo wa kuzalisha mataruma elfu ishirini na nne kwa mwaka. Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua miundombinu ya reli, barabara na mawasiliano mkoani Mbeya.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kushoto) akitoa maelekezo kwa Afisa Mfawidhi Kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw.Denis Daudi, wakati alipokagua huduma za mabasi katika kituo cha nane nane Mkoani Mbeya.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili Kushoto), akikagua moja ya kifaa kinachotumika kwenye Reli wakati alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA), Kongoro Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishiriki kuweka zege kwenye mashine ya kutengenezea mataruma ya Reli wakati alipotembelea kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, Kongoro Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia Mkoa wa Tanzania Bw. Fuadi Abdallah wakati alipokagua Mtambo wa kupimia ubora wa vifaa vya ujenzi katika Kiwanda hicho.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua moja ya kifaa cha kutengenezea Mataluma wakati alipokagua kiwanda cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, Kongoro Qwarre kilichopo Mkoani Mbeya.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na Watendaji na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara yake (hawapo pichani) wakati alipokutana nao Mkoani Mbeya.

Watendaji na wafanyakazi wa taasisi zilizopo chini ya Wizara yake wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati alipozungumza nao Mkoani Mbeya.