Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Agosti 9, 2016


Child narrates 5 tips on how to choose the right backpack for your child


Taarifa ya habari ChannelTEN Agosti 9, 2016DC bans use of mobile phones during working hours

Tarime District Commissioner Glorious Luoga has banned the use of mobile phones at the District Hospital during working hours -- reports The Daily News.

He issued the ban during a day-long meeting with workers of the hospital workers last week. He said the decision was aimed at improving service delivery at the hospital which serves hundreds of patients, particularly from poor families.
“The use of mobile phones is prohibited until further notice,” he declared, warning the workers to abstain from corrupt acts.
“Asking bribes from patients is a painful act.
I want you to change and provide quick services to patients,” he said. He said he would install a suggestion box at the hospital to receive public views in relation to services provided at the largest health facility.

Members of District Defence and Security Committee accompanied Luoga during his visit to the hospital.

Taarifa aliyoitoa NW Dk Kigwangalla kuhusu uhusiano na Juma Mwaka

Kuna baadhi ya magazeti na mitandao imekuwa ikiandika kuwa Dkt. Kigwangalla amesoma high school na aliyekuwa 'Tabibu', Ndg. Juma Mwaka, shule ya Kigoma Sekondari na kwamba walikuwa marafiki; hizi ni habari za uongo, za kupika zenye kupotosha ukweli ili kuwaaminisha watu kuwa 'wanajuana' na pengine wana ugomvi 'binafsi'.

Nimekuwa nikimpuuza kwa sababu sikuwa na haitotokea nikawa na nia mbaya dhidi ya mtanzania mwenzangu yeyote kwa sababu tu mimi nina dhamana ya uongozi. Sinaga tabia hiyo.

Uongo ukirudiwa rudiwa hubadilika na kuwa ukweli. Leo nimeamua, hapa chini, kukanusha ili watanzania pia mumpuuze, tuendelee kuimarisha huduma za tiba asili na tiba mbadala kutoka kwa matabibu wa kweli wanaofuata taratibu na siyo wasanii kama huyu. Uongo ama uzushi dhidi yangu mimi binafsi kamwe hautonirudisha nyuma mimi kama mtumishi wa umma. Lazima ifike mahali tujenge nchi ya watu 'serious' wanaofuata Sheria, Kanuni na Taratibu. Wanaoheshimu Serikali. Kwenye Afya za watanzania hatuwezi kuvumilia usanii, lazima tuwalinde walaji. Hili ni jukumu tulilopewa na Mhe. Rais. Tutasimamia Sheria ipasavyo. Hatutolegeza hata kidogo.
  1. Sikusoma 'high school' Kigoma Sekondari. Nimesoma O'level (form I - IV) Kigoma Sekondari. High School nilisoma Shinyanga Sekondari. Sikumbuki kusoma katika shule zote hizi mbili na mtu mwenye Jina Hilo. Kama alisoma Kigoma Sekondari labda mbele yangu ama nyuma yangu. Pia kipindi nasoma Kigoma Sekondari, hakukuwa na 'high school'.

  2. Ndg. Juma Mwaka hajawahi kuwa rafiki wala adui yangu. Sina ugomvi binafsi. Nafanya kazi ya kusimamia Sheria ya tiba asili na tiba mbadala ipasavyo.

  3. Naithamini tiba asili na tiba mbadala na Ndiyo maana nimeongoza Wizara ya Afya kufanya Mapinduzi makubwa kwenye eneo hili, ikiwemo kuweka utaratibu mzuri na rahisi zaidi wa kusajili watoa huduma, dawa zao, mazingira wanapotunzia dawa, wasaidizi wao, viwanda vyao, na pia kuweka mikakati ya uanzishwaji wa viwanda vya dawa za tiba asili na tiba mbadala sambamba na kufanyia utafiti dawa zao na kudhibiti ubora wa dawa zenyewe na dozi wanazowapa wateja.

  4. Muulizeni Ndg. Juma Mwaka anaposema ana ugomvi 'binafsi' na mimi, anamaanisha nini, ugomvi upi? Juu ya nini? Awape taarifa kamili. Mimi Sina ugomvi naye. Kwanza sikuwahi kumjua kabla ya ziara yangu ya kikazi pale Foreplan, ntakuwaje na ugomvi na mtu nisiyemjua? Si utakuwa ujuha huo?

  5. Mnaofuatilia suala hili mtakeni Ndg. Juma Mwaka awape majibu ya Msingi ya hoja za wakaguzi kutoka Wizara ya Afya. Mimi nilikuwa msimamizi nikiwapa nguvu wataalam wafanye kazi yao. Wataalamu walikuwepo, nao ana ugomvi nao 'binafsi'? Mwambieni awajibu kama dawa za tiba ya kisasa kukutwa kwenye eneo lake la kazi ilikuwa halali? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya maboksi 200 ya dawa? Alikuwa na vibali vya kutunza zaidi ya magunia 10 ya dawa za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa usajili? Alikuwa na uhalali wa kuendelea kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wateja wake wafuate dawa pale ili wasikatishe dozi? Tena kinyume na katazo la Baraza la tiba asili na tiba mbadala! Yeye yuko juu ya Serikali? Yuko juu ya Sheria? Ama anadhani anaweza kuidhihaki na kuiogofya Serikali?

  6.  Baada ya ziara yangu ya December 2015, ambapo sikutoa maelekezo ya kumfungia wala kumfutia kibali, niliwaelekeza Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala kuwa wawaite wawaelekeze matabibu wote wafuate Sheria, kanuni na taratibu. Waliitwa. Wakaelekezwa. Waungwana wakatii. Yeye hakutii, wakamfuta. Baada ya kufutiwa usajili, akaendelea kujitangaza na kutoa huduma, yeye ni nani?

  7. Kufanya haya ni kuvunja sheria za nchi. Na makosa haya yana adhabu zake. Sisi kama Serikali tumeagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Serikali ina mkono mrefu, itamkamata. Itamtia nguvuni na atafikishwa mahakamani. Ataenda kujitetea huko kuwa ana 'ugomvi binafsi' na Naibu Waziri Kigwangalla!
Mwisho, aende akafuatilie kisa cha mfanyabiashara wa kigiriki aliyesema ameiweka Serikali mfukoni - Mwalimu Nyerere alimfanya nini!

Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB.

Katuni: Soka la Bongo - Wakimataifa vs Wananiliu...


Katuni: Uzichaji za huyu mwanangu...


Rais wa Chama cha Hemophilia Tanzania Richard Minja ashiriki WFH 2016 World Congress


TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA HEMOPHILIA2016, MAREKANI

Kongamano la Kimataifa kuhusu ugonjwa wa Hemophilia limemalizika Orlando, nchini Marekani Julai 24-28, 2016. 

Hemophilia ni ugomjwa wa damu wa kurithi ambapo damu inakosa uwezo wakuganda pale mshipa unapodhurika. Huwapata zaidi watoto wa kiume.

Kongamano hilo lilikutanisha zaidi ya wadau 6,000 kutoka takribani nchi 130 duniani chini ya World Federation of Hemophilia (WFH). Malengo makuu yalikuwa kuboresha tiba na maisha ya wagojwa.

Pamoja na mambo mengine, kongamano ni jukwaa la kutambua jitihada zinazofanyika duniani kote hususani utafiti wa kupata tiba na uangalizi bora kwa wagonjwa. Hutengeneza jukwaa na mtandao kwa wagonjwa, wazazi/jamaa, madaktari bingwa, wahudumu, watengeneza sera na watafiti wa dawa na kujenga mahusiano na baraza la kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa washiriki toka sehemu mbalimbali duniani.

Moja ya mafanikio ni ugunduzi wa dawa (factors) zenye uwezo wa kufanya kazi mwilini kwa muda mrefu zaidi (longer half-life drugs) na hivyo maisha bora kwa wagonjwa. Pili ni upatikanaji wa misaada (donations) ya dawa kutoka makampuni yanayotengeneza dawa kwa nchi maskini. 

Ikumbukwe nchi hizi hazimudu kununua dawa kwa wagonjwa kutokana na bei yake kuwa kubwa. 

Tanzania imewakilishwa na Raisi wa Chama cha Hemophilia Tanzania Bw. Richard Minja.
Richard Minja at the Orlando, Florida summit

Uwanja wa ndege Dodoma kukamilika mwishoni mwa mwezi huu


Waziri Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na mafundi wanaokarabati na kufanya upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma wakati alipokikagua
Imeelezwa kuwa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma utakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti ili kuruhusu ndege za abiria sabini mpaka tisini kuweza kutua na kuruka na hivyo kurahisisha usafiri wa anga kwa ukanda wa kati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa baada ya kutembelea kiwanjani hapo kukagua hatua ya mwisho ya ujenzi iliyofikiwa ambapo amesema kasi ya Mkandarasi Chicco anayetekeleza kazi hiyo inaridhisha katika kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika kwa muda na kwa viwango vilivyokubalika.

Amesema mpaka sasa ni asilimia themanini ya kazi iliyotekelezwa kwa siku arobaini na tano tangia kuanza ukarabati hivyo kasi iliyotumika kwenye kiwanja hiki itatumika kwenye ujenzi wa viwanja vingine nchini.

"Tunaamini kabisa kwa kasi ya mkandarasi na msimamizi mtakamilisha ujenzi huu haraka na viwango tulivyokubaliana katika mkataba ili ndege kubwa zianze kutua na kuruka" amesema Prof. Mbarawa.

Naye Msimamizi wa ujenzi wa kiwanja hicho kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi Mbila Mdemu amesema kazi ya ukarabati na upanuzi inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa kuzingatia ubora na viwango na kukamilika kwa wakati

"Tulipewa kazi hii na tunaahidi kuwa itakamilika kama tulivyoelekezwa ili kuwapa wananchi wanaozunguka mikoa ya Dodoma na jirani fursa ya kutumia usafiri wa Anga", amesema Eng. Mdemu.

Ameongeza kuwa kazi zinazokamilishwa sasa ni kumalizia sehemu ya maegesho ya ndege na tabaka la mwisho kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege.

Mradi wa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Dodoma umegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa zaidi ya shilingi bilioni 11.8 na kukamilika kwake kutaongeza idadi ya safari za ndege zitakazosafirisha abiria wa mikoa ya kanda ya kati.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma kutoka kwa Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho, Mkoani Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa kutoka Eng. Guo Zhingjian wa kampuni ya Chicco inayojenga kiwanja hicho Mkoani Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa vitendo wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka kutoka kwenye katapila mara baada ya kukagua vifaa vya ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa mafundi wanaokarabati na kupanua kiwanja cha ndege cha Dodoma wakati alipokagua kiwanja hicho.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa mafundi wanaokarabati na kufanya upanuzi katika kiwanja cha ndege cha Dodoma wakati alipokagua kiwanja hicho.