Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Agosti 23, 2016


Baraka wa BukobaWadau Blog amshukuru Mungu kwa sikukuu ya kuzaliwa


Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, Aug. 23.

Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. Ni neema ambayo sistahili. Napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana, niitumie kwa mambo mema; Nizingatie wajibu wa kuvitumia kikamilifu vipaji alivyonipa Mungu kwa manufaa ya wanadamu.

Siwezi kujivunia chochote nilichoweza kufanya, bali ni kumshukuru Mungu na kuendelea kumtegemea na kila ninaposherehekea kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa kwangu, fikra zinanituma kufananisha mchango wangu Kimkoa na Kitaifa sawa na ule wa watu maarufu; Ukweli ni kwamba ninajitahidi lakini mchango wangu bado ni hafifu sana. Mengi nimefanya kupitia Bukobawadau Blog Media ninachoweza kusema ni kwamba changamoto ni kubwa sana!
I will always praise God!
----

Baraka,

wavuti.com inaungana nawe katika kumpa Mungu shukurani kwa zawadi hii ya uhai na afya pamoja na mafanikio tele.

wavuti.com inajivunia ushirikiano wako katika tasnia ya kublogu.

wavuti.com inakuombea maisha marefu yaliyojaa afya njema, mafanikio mengi na baraka tele!

How to sustain desire; Revive a long-term relationship


Report indicates that Tanzania is among Africa's Top 10 Investment Destinations

Tanzania was among the leading investment destinations in Africa in 2015, the recently published 2016 African Economic Outlook (AEO) indicates.

The AEO presents the current state of economic and social development in Africa and projects the outlook for the coming two years. 

The AEO is a product of collaborative work by three international partners: the African Development Bank (AfDB), the OECD Development Centre and the United Nations Development Programme (UNDP). 

The top 10 African investment destinations in 2015 were: 
 1. Egypt (USD10.2b) 
 2. Mozambique (USD4.7b) 
 3. Morocco (USD4.2b) 
 4. South Africa (USD3.6b) 
 5. Ghana (USD2.5b) 
 6. Democratic Republic of the Congo (USD2.5b)
 7.  Zambia (USD2.4b) 
 8. Tanzania (USD2.3b) 
 9. Ethiopia (USD2.1b) 
 10. Guinea (USD1.9b) and 
 11. Kenya (USD1.9b) 
In East Africa, Tanzania (USD2.3b) and Uganda (USD1.3b) received stable investments in 2015 despite their lack of significant resources, according to the report.

Read more at: tanzaniainvest.com

Orodha ya waajri wanaotakiwa kuwasilisha taarifa za "Watumishi Hewa" ifikapo Agosti 26

Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora imetoa orodha ya majina ya Taasisi ambazo hazijawasilisha Taarifa ya Watumishi Hewa katika Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora. Serikali imetoa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha ambayo ni 26 Agosti, 2016.

Mara baada ya tarehe hiyo, Ofisi ya Rais -Utumishi itawasilisha taarifa rasmi ya watumishi hewa kwa Mheshimiwa Rais ikiwa na orodha na majina ya Taasisi ambazo zimewasilisha taarifa ya watumishi hewa na na zile ambazo hazijawasilisha taarifa hizo.

Ifuatyo ndio orodha ya Taasisi hizo:-

Namba za simu za RMOs kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko na kero za huduma

UTOAJI WA MALALAMIKO NA KERO JUU YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI PAMOJA NA MASUALA YA JINSIA, WAZEE NA WATOTO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007). Takribani kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi katika kupata huduma za afya.

Wasimamizi wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. Mhe Waziri amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.

Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: [email protected]

“Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.

MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)


IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016

Mabadiliko ya nyakati: Mwasisi wa "sungusungu" wakati huo na sasa...


Taarifa ya Polisi Dar: Kukamatwa silaha; Kuuawa majambazi; Sare za UKUTA


KUUAWA MAJAMBAZI HATARI 03 JIJINI DAR WAPATIKANA NA RISASI 300 ZA SMG NA MAGAZINE 10


KUKAMATWA KWA BASTOLA AINA YA BWOWNING NA RISASI 06

Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 22.08.2016 03:45 hrs huko maeneo ya Mabibo Loyola, kata ya Mabibo (W) Magomeni kikundi cha Ulinzi shirikishi wa eneo hilo wakiwa kazini waliona kundi la watu kati ya watu watatu hadi wanne wakiwa wanatembea.

Baada ya kuwaona waliwatilia shaka na kuwasimamisha iliwaweze kuwahoji. Hata hivyo katika mahojiano watuhumiwa wengine walifanikiwa kukimbia ambapo mtuhumiwa mmoja mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (20 – 25) alikamatwa.

Baada ya mtu huyo kukamatwa alianza kuwatishia kuwa atawaua huku akitamka maneno ya kiislam akisema ”Taqbir” na “Allah Huaqbar “ ghafla mtu huyo aliingiza mkono mfukoni na kutoaa kitambaa cha kufuta jasho na kukitupa chini ambapo bomu lililipuka. Kuona hivyo ulinzi shirikishi walikimbia na mtu huyo kuanza kukimbia huku akiwa na begi mgongoni. Hata hivyo mmoja kati ya hao ulinzi shirikishi alimpiga mtuhumiwa huyo rungu kichwani eneo la kisogoni, pamoja na kupigwa rungu kichwani mtu huyo aliendelea kukimbia na alitupa begi chini na kuendelea kukimbia. Ulinzi shirikishi nao waliendelea kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata ambapo wananchi walijitokeza na kumpiga hadi kufa kisha kumchoma moto. Askari polisi baada ya kupata taarifa hizo, walifika eneo la tukio ambapo ulifanyika upekuzi katika begi hilo na kukutwa magazine 10 za SMG zikiwa na jumla ya risasi 300.

Hadi sasa askari wapo eneo la tukio wakifanya upekuzi katika nyumba mbalimbali kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao inasadikiwa bado wapo eneo hilo. Msako mkali unaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao waliokimbia.

KUUAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI KATIKA MAJIBIZANO YA ANA KWA ANA

Katika tukio lingine tarehe 21.08.2016, saa 21:30hrs usiku huko Tandika Mtaa wa Chiwanda nyumba no. 08 Mkoa wa Temeke, Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam kilifanikiwa kuwaua majambazi wawili katika majibizano ya risasi ya ana kwa ana.

Tukio hilo lilitokea katika maeneo hayo ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna kundi la majambazi wanataka kuvamia nyumba hiyo.

Mara baada ya kupokea taarifa hizo Askari walifika eneo la nyumba hiyo kabla ya majambazi hao hawajaanza kupora ambao idadi yao walikuwa watano wakiwa na pikipiki mbili ambazo hazikusomeka namba.

Baada ya majambazi hayo kugundua kuwa wanafuatiliwa majambazi hayo walianza kuwafyatulia askari risasi ambazo hazikuleta madhara, ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili wanaume umri kati ya miaka (25 – 30), ambao walifariki dunia papo hapo na wengine watatu walifanikiwa kutoroka.

Katika upekuzi mmoja wa majambazi hao alikutwa na bastola moja aina ya Browining ikiwa na risasi 06 namba zake zikiwa zimefutwa. Jitihada za kuwatafuta majambazi waliokimbia unafanyika na upelelezi unaendelea.


KUPATIKANA KWA SARE AINA YA FULANA ZENYE MANENO YA UCHOCHEZI ZIKIWA NA ALAMA YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 20/08/2016 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye maneno ‘UKUTA’ fulana 6 za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’.

Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA KWA KOSA LA WIZI WA GARI

Mnamo tarehe 09.08.2016 saa 18:00hrs jioni huko Masasi Mjini kwenye gereji ya magari, Kikosi Maalum cha Kupambana na wizi wa Magari cha Polisi Kanda maalum cha Dar Es salaam kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa OMARY GILLIAD OMARY (35) kazi dereva kwa wizi wa gari. Mtuhumiwa alikamatwa kwa wizi wa gari No: T.612 AUJ aina ya Toyota Hiace mali ya mlalamikaji KAISARI MWALIMU YUSUFU (26) Mfanyabiashara mkazi wa Sinza.

Gari hilo iliyoibiwa tarehe 25.06.2016 likiwa limeegeshwa nyumbani kwa mlalamikaji maeneo ya Sinza ambapo mtuhumiwa alichukua gari hilo kwa nia ya kufanya kazi.

Baada ya mtuhumiwa kupewa gari hilo aliipeleka mafichoni Masasi Mjini mkoani Mtwara ambapo Kikosi cha Kupambana na Wizi wa Magari Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar Es salaam kilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa pamoja na kielelezo gari. Mtuhumiwa anahojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani kujibu shutma inayomkabili dhidi yake.

KINARA MWIZI WA VIFAA VYA MAGARI AKAMATWA AKIWA NA VIFAA MBALIMBALI VYA MAGARI

Kikosi maalum cha kupambana na wizi wa magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa hatari anayejihusisha na wizi wa magari na viafaa vyake. Mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 01/08/2016 majira ya saa 08:30 usiku, maeneo ya amani mtaa wa kongo askari wakiwa doria walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye SALUMU S/O ISSA @HASSANI (43) Mkazi wa mbagala akiwa na (1).SIDE MIRROR 12 (2). SITE MIRROR 11(3) CAMP BAMPA 24 (3).PLATE SIDE MIRROR 44 (4) VITASA28 (5).SIDE LAMP 11 (6).INDICATOR 17 vifaa hivyo Vyote vikiwa ni mali za wizi akiwa ameviiba na baada ya kumhoji alikiri kuhusika na wizi huo. Mtuhumiwa huyo atapelekwa mahakamani wakati wowote upelelezi utakapokamilika.

TAARIFA YA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM YA D’SALAAM KUANZIA TAREHE 21.08.2016 HADI TAREHE 22.08.2016.

Taarifa ya Kikosi cha Usalama barabarani Kanda Maalum ya D’salaam ya ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 21.08.2016 hadi tarehe 22.08.2016 ni kama ifuatavyo:-
 1. Idadi ya magari yaliyokamatwa 5,346
 2. Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa 216
 3. Daladala zilizokamatwa 1,121
 4. Magari mengine (binafsi na malori) 225
 5. Jumla ya Makosa yaliyokamatwa 20,562
Jumla ya fedha za Tozo zilizopatikana TSH 161,750,000/=

S.N.SIRRO – CP
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Taarifa ya COSTECH ya Kongamano la tano la kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu

TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

ISO 9001: 2008 CERTIFIED


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu waandishi wa habari, tumewaiteni kuwaeleza kuwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imeandaa Kongamano la tano la kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Kongamano hili ni fursa kwa wataalam wakiwemo watafiti, wabunifu, watunga sera pamoja na wajasiriamali kukutana na kujadili na kuelezea mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu katika kufikia taifa la viwanda. Kongamano la mwaka huu litafanyika kwa muda wa siku tatu, ukumbi wa Kisenga jengo la LAPF Kijitonyama, jijini Dar es salaam, kuanzia tarehe 23 hadi 25 Agost, 2016.

Kupitia kongamano hilo ambalo siku ya ufunguzi mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, wadau watatoa mchango wao wa namna sayansi, teknolojia na ubunifu vitakavyochangia kufikia uchumi wa viwanda katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ambayo ni mshauri mkuu wa serikali kwa mambo yote ya sayansi na teknolojia, imeratibu na kuhamasisha tafiti kulingana
na vipaumbele vya taifa hasa; kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, viwanda, mazingira, nishati, TEHAMA na sayansi ya jamii.

Tafiti katika vipaumbele hivyo, yametoa matokeo chanya yanayodhihirisha uthubutu wa kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Watafiti watapata fursa ya kuwasilisha matokeo ya miradi kumi na mitano iliyofadhiliwa kwa pamoja kati ya serikali za Afrika ya Kusini na Tanzania tangu mwaka 2013ambapo kila nchi ilichangia zaidi ya shilingi milioni mia tano. Matokeo ya tafiti hizi yanatupatia fursa ya kuwashirikisha watanzania ili wafahamu kinachoendelea katika Nyanja ya utafiti.

Baadhi ya matokeo ya tafiti yatakayowasilishwa kwenye kongamano hilo, ni pamoja na teknolojia ya kuongeza thamani na usindikaji wa ngozi. Teknolojia hiyo iliyogunduliwa chini ya COSTECH, mpaka sasa imewezesha kujengwa kiwanda kidogo cha ngozi Morogoro kwa ajili ya mafunzo. Mafunzo yatatolewa kwa wakurugenzi wa wilaya zote 136 nchini lengo ni kushirikiana na serikali kuwa na kiwanda cha ngozi kila wilaya.

Kabla ya teknolojia hii, kati ya ngozi milioni 8 zinazozalishwa kwa mwaka, ni asilimia 40 pekee zilikuwa na ubora. Tekonolojia hii itaongeza thamani ya ngozi mbichi za ng’ombe, mbuzi na kondoo na kufikia shilingi bilioni 89.5. Ngozi hizo zikisindikwa zitakuwa na thamani ya shilingi bilioni 300 kwa mwaka. Viwanda hivyo vikikamilika vitatengeneza bidhaa kama viatu, mabegi n.k vyenye thamani ya shilingi trilioni 3 kila mwaka.

Matarajio yetu ni kuwa kila kiwanda kitaajiri wafanyakazi rasmi 100 na wengine 500 wasio rasmi, hivyo wilaya zote zitaweza kutoa ajira kwa watu 81,600.

Ndugu waandishi wa habari, wasilisho lingine litakuwa la ugunduzi wa chanjo ya kuku yenye uwezo wa zaidi ya asilimia 80 kudhibiti magonjwa matatu ya kideli, ndui na mafua kwa kuku. Chanjo hii ipo katika hatua za mwisho kukamilika na kinajengwa kiwanda Morogoro kwa ajili ya kutengeneza chanjo hiyo. Tanzania kuna jumla ya kuku milioni 60 kulingana na takwimu za wizara ya kilimo hivyo endapo utatokea ugonjwa wa mlipuko na chanjo hiyo ikatumika, tutaokoa jumla ya kuku milioni 48 wenye sawa na thamani ya shilingi bilioni 2.8.

Tume pia imefadhili utafiti kwenye kilimo cha pamba ili kuongeza uzalishaji na kuwezesha viwanda vya nguo kupata mali ghafi ya kutosha. Awali mkulima angeweza kuvuna wastani wa kilo 800 kwa ekari moja lakini kwa kutumia kilimo cha kitaalam na mbegu zilizofanyiwa utafiti ataweza kuvuna wastani wa kilo 1,100 ikiwa ni ongezeko la kilo 300. Bei elekezi ya pamba ni shilingi 1,000 kwa kilo hivyo endapo mbegu mpya hii itaingizwa sokoni, mkulima atakuwa na ongezeko la shilingi laki 3 kwa kila ekari moja.

Tume imefadhili utafiti wa kilimo cha mpunga katika kituo cha utafiti cha kilimo Dakawa. Wataalam wamegundua mfumo wa kilimo shadidi ambacho kupunguza matumizi ya mbegu kwa asilimia 80 ambapo awali ekari moja ilipandwa kilo 18 lakini sasa ni kilo 3 tu zinatosha kupanda shamba la ekari moja. Uzalishaji utaongezeka ambapo awali mkulima alivuna magunia 15 kwa ekari moja lakini sasa atavuna magunia 32.

Utafiti pia umefanywa kwenye kilimo cha mihogo na kugundua aina mbili za mbegu ambazo ni Kiroba kwa kanda ya kusini na Mkombozi kwa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini. Mbegu hizi ni kinzani kwa magonjwa ya batobato na michirizi kahawia ambayo yanashambulia mihogo ya asili na kuzorotesha uzalishaji. Mbegu hizi za kisasa hutoa mavuno mengi. Jumla ya mbegu milioni moja zilitolewa kwa vikundi vya wakulima katika mikoa ya Mtwara na Mwanza. Wakulima wameongeza kipato kutokana na uzalishaji kuongezeka. Habari njema zaidi ni kuwa kiwanda cha kutengeneza wanga utokanao na mhogo kitajengwa Mtwara au Lindi.

Ndugu waandishi wa habari, kuwa na taifa la viwanda ni lazima uzalishaji wa malighafi uongezeke mara dufu. Tume ya Sayansi na Teknolojia imefadhili utengenezaji wa mashine ya kuchakata mkonge. Mpaka sasa mashine imetengenezwa na ipo kwenye majaribio ya ndani. Mashine ina uwezo wa kuchakata majani ya mkonge 3,300 kwa siku. Mashine hii ni kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo ambao wamekuwa wakitumia njia za zamani kuchakata mkonge. Mwezi Novemba itaanza kutumika kwa wakulima ambapo kwa kutumia mashine hii watapata nyuzi zenye ubora unaotakiwa.

Tume imejikita katika kuhawilisha teknolojia mpya kama vile teknolojia za kisasa zinazotumika kuendeshea mitambo viwandani (mechanotronics), teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani (drones), na teknolojia nyinginezo zinazotolewa kwa sasa

Ili nchi yetu iwe ya uchumi wa kati, katika sekta ya uendelezaji, uhawilishaji na ubiasharisha wa teknolojia, mambo kadhaa yanatakiwa kufanyika ikiwa ni pamoja na:

Kuanzisha na kuimarisha atamizi, kama ambavyo Tume ilivyoanzisha na kuimarisha atamizi ya DTBi. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 atamizi imeanzisha kampuni 40 ambazo zimezalisha ajira kwa takribani vijana 300 na ajira zisizo za moja kwa moja (indirect) 8,500 kwa mwaka. Atamizi hii inazalisha takribani dola milioni 1.5 kutokana na waatamizi kuuza huduma zao

Aidha, Atamizi hii imezalisha, kulea na kubiasharisha bunifu mbalimbali kutoka kwa vijana hususani katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama vile mifumo bora na rahisi wa ulipaji kodi za serikali za mitaa, ulipaji huduma za maji na umeme, udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, usikilizaji wa kipindi cha Bunge kupitia simu ya mkononi, ulipaji tiketi za mabasi kupitia simu ya mkononi.

Tangu mwaka 2010 mpaka sasa, serikali imeboresha uwezo wa watafiti 517, kwa kugharamia gharama za masomo kwa ngazi za shahada za uzamili na uzamivu. Kati ya hao, 445 wamehitimu masomo yao na sasa wamerejea katika vituo vyao vya kazi ili kuendelea kulitumikia taifa kupitia utafiti.

Ndugu waandishi wa habari, hayo ni baadhi tu ya mafanikio ambayo tume imeyapata. Malengo ya tume ni kuhakikisha inaendelea kutoa ushauri wenye tija kwa serikali kutokana na matokeo ya sayansi, teknolojia na ubunifu. Karibuni sana katika kongamono hilo.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Dr. Hassan Mshinda
Mkurugenzi Mkuu
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
22/08/2016

Call for application: Afya Bora Fellowship


Read more: afyaboraconsortium.org

Customer complaints about Vodacom Tanzania "scam"

update: The tweet quoted below indicates that Vodacom is now aware of this.


wavuti.com via the contact box received the following message...

Hi,

I made a payment of 30,000/ TShs using M-pesa (ref number/ muhamala - 3h585y6u9y ) for traffic fine (car number T638 CVW ) on 6th of August to wrong account number 221188 instead of 1607310659 .

I report the issue the next day on 7th of August to Voda , they advice me to talk to Maxcom of which i did. Maxcom customer service said they will return the money as soon as possible but refuse to give me time frame. "to me it was shocking or rather sound fishy"

After two days i called them again they said the same thing that the money will be returned i just have to wait and again no time was given and when i asked the customer service personnel become annoyed or even upset with my curiosity, instead of helping me with explanation of why there is no time period of solving a problem like this.

After a week i called them again i got different personnel and different advice that i have to ask Voda to report the problem to them of which i did , Luckily i got a good responds from Voda customer service personnel Emanuel Moshi that Maxcom are just avoiding their responsibilities and he is going to do as they wish to stop the excuses, the Voda personnel wrote the report about my issue to Maxcom and send me a reference number (CSR159140506) informing me that i will be notified just after they have resolve the issue.

After 4 days they send me a massage said I have to call 0764700200 to resolve my issue of which i did, but again i was told by Maxcom the money have been send to Voda and its on their system i should contact them.

Today is Monday 22/08/2016 i have called Voda to check if the money is on their system but they said there isn't any money i should check with Maxicom. I called Maxcom, and the customer service personnel Lady took my report as if i am reporting for the first time and she offer me an apology for the delay and that she will process the return of my payment as soon as possible and again no time frame .

I ask myself if this happens to me with all the follow ups , how many people are affected by this scam , how much money are people loosing and Maxcom benefit on peoples mistake.

This issue is bigger than its sound, the customer service don't give you the time frame for your money to be returned of which is very strange , they make you call them on the number which is not free to do the follow up, and all the time you call them is as if you reporting the matter for the first time, they take the details afresh and give you the same answer.

Do the Maths; if 30,000/ TSh is small to you that soon you will give up to follow up , TO THEM IT ISN'T .

Assume the lowest number possible to do mistake per day is 10 people on 30,000/TSh category and let us forget about other payment above or lower 30,000/TSh which are many as well.

30,000/TSh x 10 = 300,000/ TSh per Day

300,000/TSh x 30 = 9,000,000/ TSh per Month

9,000,000/TSh x 12 = 108,000,000/ TSh per Year

NOTE: The amount above is the lowest possible Yearly

Imagine this amount of money someone is making without a sweat and not even the Government collecting Tax from it because they don't know about the scam or can not trace the refund to customer if truly happens and most victims of this calculated scam are not reporting it cause they don't know where to start and where to report it, this is the problem of ELECTRONIC PAYMENTS.

But if citizen and the authorities are educated about this issue well we will be able to stop this big company to ripping off its customers in daylight.

PLEASE: Forward this information to all social media to alert good Tanzania citizens and its good Government authority about this scam.

Regards,
E. R. M. | email withheld

Taarifa ya habari ChannelTEN Agosti 22, 2016[video] Vurugu iliyovunja mkutano wa CUF

WM Majaliwa: Kama tuna mtumishi anaiba dawa, ni muuaji; Fuatilieni na kuwachukulia hatuaWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwachukulia hatua watumishi wote wa sekta ya afya wanaojihusisha na wizi wa dawa.
“Fuatilieni na kuwachukulia hatua watumishi wa Zahanati wanaoiba dawa. Hawa hawana nafasi ya kuendelea kufanya kazi kwa sababu ni wauaji,” alisema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo juzi jioni (Jumamosi, Agosti 20, 2016) wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Katavi mara baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Alisema kila kiongozi kwenye eneo lake ahakikishe dawa zinazopelekwa na Serikali kwa ajili ya kuwahudumia wananchi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Pia ameitaka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kujenga duka la dawa mkoani Katavi kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa dawa katika mkoa huu pamoja na mikoa jirani.

Wakati huo huo Waziri Mkuu aliwataka Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata na Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada waende wakasome kama wanahitaji kuendelea kuwa na wadhifa huo. Alisema Mratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata ni lazima awe na shahada ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utolewaji wa elimu katika shule za sekondari na msingi.

Kwa upande wa walimu wakuu katika shule za msingi, Waziri Mkuu alisema ni lazima wawe na diploma, hivyo aliwataka walimu wakuu wote wasiokuwa na diploma kwenda kusoma kabla hawajaondolewa kwenye wadhifa huo.

Alisema Serikali imetenga zaidi ya sh. bilioni tano kwa mwezi ambazo ni posho ya madaraka, ambapo Waratibu Elimu Kata wanapewa sh 250,000 kwa mwezi huku Wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu katika shule za msingi wanapewa sh. 200,000.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga alisema mkoa umeendelea kuongeza bajeti ya dawa ili kuhakikisha dawa zinapatikana katika ngazi zote za kutolea huduma.

“Mwaka 2012 bajeti ya dawa na vifaa tiba ilikuwa sh. Milioni 558 ambayo ilitosheleza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa asilimia 70. Katika bajeti ya mwaka 2016/2017 mkoa umetengewa jumla ya sh bilioni 1.3 ambayo tunaamini itamaliza tatizo la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba,”alisema
Mkuu huyo wa mkoa alisema mfumo mpya wa usambazaji dawa kupitia MSD umesaidia dawa, vifaa tiba na vitendanishi kupelekwa moja kwa moja hadi katika ngazi ya zahanati hali iliyosaidia dawa kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kwa asilimia 100.

Mapema jana Waziri Mkuu alifanya ziara katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambapo alisema Serikali itahakikisha hospitali hiyo inaongezewa huduma zaidi kwa sababu ni ya wilaya ila inahudumia wagonjwa wa mkoa wote.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, AGOSTI 21, 2016.


Mkurugenzi Usalama wa Taifa astaafu; Wajue waliowahi kuongoza UwT

Rashid Othman
MKURUGENZI Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othman, amestaafu rasmi -- linaripoti gazeti la MTANZANIA.

Othman, aliteuliwa kushika wadhifa huo na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Agosti 20, 2006, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mtangulizi wake Apson Mwang’onda aliyestaafu Agosti 21, mwaka 2006 kwa mujibu wa sheria.

Kigogo huyo wa Usalama wa Taifa, aliyeapishwa kushika nafasi hiyo Agosti 21, 2006 amehudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka 10.

Chanzo cha kuaminika kililiambia MTANZANIA kuwa, Othman alistaafu Agosti 19, mwaka huu na nafasi yake kwa sasa inakaimiwa na Mkurugenzi wa Mambo ya Ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa, George Madafa.

Chanzo cha kuaminika kililiambia MTANZANIA kuwa Othman, anatajwa kuwa ni mtu aliyefanikiwa kuimarisha ulinzi pamoja na kuwa na maofisa wenye kuzingatia maadili ya kazi.
“Tunajua kuna wakati Idara iliyumba kidogo lakini kwa kipindi cha Othman tutamkumba kwa mambo mengi ikiwemo kurudisha nidhamu kwa maofisa nchi nzima. Ilifika wakati wengine walikuwa hawana maadili ya kazi lakini kwa sasa tunajivunia Othman na kwa hakika anakwenda kupumzika lakini tutamkumbuka,” kilisema chanzo chetu.
Waliowahi kuongoza usalama

Kwa miaka kadhaa Idara hiyo iliongozwa na vigogo kadhaa waliobobea katika masuala la Ulinzi na Usalama wakiwamo; Emir Mzena, Lawrance Gama, Hans Kitine ambapo alipoondoka nafasi hiyo ilikamatwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga.

Mbali na hao nafasi hiyo ilishikiliwa pia na Imran Kombe na Apson Mwang’onda hadi sasa Rashid Othman akisubiri mrithi wa nafasi yake kwa majaliwa ya Rais Dk. Magufuli, ambaye ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi wa nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria.

Hii ndiyo Usalama

Katika mchakato wa mageuzi ambayo yamefanyika kwenye Katiba ya mwaka 1977, mfumo wa sheria na siasa za nchi, taasisi za dola zimejikuta zikiwa nyuma wakati vuguvugu la mageuzi likienda mbele.

Moja ya tasisisi zilizokumbwa na fukuto hilo ni Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ambayo hapo awali chini ya utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, ilikuwa ni taasisi ambayo haikutambulika kisheria kutokana na muundo wake kuwa wa siri na wa gizani.

Matokeo ya utendaji wa idara hiyo uliiletea sifa ya kuogopwa na kuonekana ni chombo cha majungu, chuki na wauaji wa wananchi wenye misimamo tofauti na watawala serikalini.

Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wakiwa katika muundo wa kiraia ni wanajeshi na idara hiyo ni chombo nyeti katika uhai wa dola..

Chombo hicho hufanya kazi kwa taratibu za idara zote za usalama wa taifa na huwa hakiingiliwa na mtu yeyote kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kwa hapa nchini mageuzi ya mwaka 1992 yaliyoanzisha mfumo wa vyama vingi na mabadiliko mengine ya kisheria na Katiba, yalisababisha kuundwa kisheria kwa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kutambulika rasmi kisheria hapa nchini kulianza mwaka 1996, baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Sheria ya Usalama wa Taifa Na.5 ya mwaka 1996 na kutambulika rasmi kwa jina la Tanzania Intelligence and Security Services (TISS).

Pamoja na hali hiyo imenyang’anywa mamlaka ya kukamata wahalifu ingawa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere idara hiyo ilikuwa na mamlaka hayo chini ya ‘Detention Order’ yaani sheria ya kumuweka mtu kizuizini.

Taarifa kuhusu mazoezi yanayofanywa na polisi


Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi.

Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Waziri Nchemba azungumzia kulipua UKUTA


BAVICHA yalaani upotoshwaji kuhusu UKUTA[video] UVCCM yatangaza kuandamana nchi nzima Agosti 31