USA fines airlines for lacking information about compensation for passenger flights bump, baggage damage or loss

WASHINGTON (AP) -- The government is fining four airlines for failing to have accurate notices explaining compensation for passengers who are bumped from flights or whose baggage is damaged or lost.

The Department of Transportation said Friday that it fined American Airlines $45,000, Southwest Airlines and Alaska Airlines $40,000 each, and United Airlines $35,000.

Under federal rules, airlines must explain potential compensation when they bump passengers from an oversold flight. Rules also generally bar airlines from limiting their liability when they lose, damage or delay a passenger's bag to less than $3,500.

The department said that during airport inspections, airline agents at gates or ticket counters didn't have the required notices or had outdated or inaccurate information.

Mwanamichezo mahiri adhihirisha hasira dhidi ubaguzi wakati ulipoimbwa wimbo wa Taifa


Ubaguzi wa rangi ya ngozi umeendelea kuwakera na kuwaudhi hata wasiobaguliwa, kutokana na athari wanazoziona kwa jamaa na marafiki zao.

Ni hivi majuzi tu mitando ya kijamii na vyombo vya habari vililipuka kwa gumzo mara mbili

Mara ya kwanza ilikuwa ni baada ya Mmarekani aliyeliletea taifa lake sifa kwenye michezo ya Olimpiki, Gabby Douglas kuandamwa kwa maneno ya kashifa, kejeli, dharau na kuudhi kwa kutokuweka mkono kifuani kama ishara ya kuheshimu na kulipenda taifa lake wakati wimbo huo ukiimbwa mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil mwaka huu.

Mara ya pili ilikuwa baada ya Mmarekani mwingine, Ryan Lochte aliyeshiriki Olimpiki izo hizo, kudanganya kuwa alishambuliwa na kuporwa katika moja ya vituo vya kuuzia mafuta nchini humo, kabla ya kugeuka na kukana kisha kuomba samahani baada ya watu kupaza sauti zao kuwa hili ni kosa kubwa lakini limepewa kisogo kutokana na rangi ya ngozi na jinsi ya mtu. 

Colin Kaepernick
Jana Ijumaa, mmoja wa wanamichezo maarufu wa mpira unaopendwa nchini Marekani "National Footbal League", Colin Kaepernick alidhihirisha hasira yake kwa kutokusimama kuonesha ishara ya heshima wakati wimbo wa taifa la nchi yake ulipokuwa ukiimbwa. Alipoulizwa sababu ya kutokufanya hivyo alisema:
"I am not going to stand up to show pride in a flag for a country that oppresses Black people and people of color," Kaepernick told NFL.com "To me, this is bigger than football and it would be selfish on my part to look the other way. There are bodies in the street and people getting paid leave and getting away with murder."
[...]
"This is not something that I am going to run by anybody," he said. "I am not looking for approval. I have to stand up for people that are oppressed. ... If they take football away, my endorsements from me, I know that I stood up for what is right."
Unaweza kusoma habari nzima: SBNation.com

Shughuli za kila siku za maisha ziwani Nyasa


Mtoto wa miaka 4 mkazi wa Manda katika wilaya ya Ludewa akiogelea katika ufukwe wa ziwa Nyasa kama alivyokutwa na mpigapicha wa MatukioDaimaBlog

Vikindu gun battles between police and bandits linked to revenge


FRESH revelations behind a wave of wild gun battles involving police officers and bandits unfolded yesterday with sources hinting that it is a calculated revenge mission.

[video] Magufuli: Leo ndiyo nimeshikana mkono na Mheshimiwa Lowassa


ITV na Radio One Stereo yawaaga rasmi Buhohela, Chacha, Gondwe


Anaomba msaada: Binti anayeongezeka kg 2 kila mwezi licha ya kubadili mlo afikia kilo 180


Rais mst. Mkapa na mkewe Anna washerehekea miaka 50 ya ndoa


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakikata keki katika hafla ya chakula cha mchana waliyoandaa baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN Agosti 27, 2016


Majadiliano ya kuhusu rasimu ya katiba inayopendekezwa kuunda TzUK Diaspora


Kwenye video zilizopachikwa hapa ni Abraham Sangiwa - Katibu Mkuu - Kamati ya Mpito - TANZUK inayoandaa utaratibu rafiki wa kuunda Jumuiya Shirikishi katika Kipindi Cha Majadiliano kuhusu Diaspora UK na Rasimu pendekezwa SEHEMU YA KWANZA, itakayoshirikisha kila Mwanadiaspora maeneo yote hapa nchini Uingereza - KARIBU.
Ujumbe wa Prof. Mbele kwa Polisi wa Tanzania Kuhusu UKUTA

Kwanza napenda kusema kuwa jamii yote inatambua kazi kubwa na muhimu inayofanywa na polisi katika kulinda usalama na mali za wananchi, pamoja na mazingira magumu na uhaba wa vitendea kazi unaowakabili polisi. Raia wema tunashukuru tunapoona polisi wakifanya doria mitaani, wakilinda sehemu muhimu kama mabenki, na kadhalika. Tunafurahi na kuwashangilia polisi wanapoweka mitego na kufanikiwa kuwanasa majambazi. Mioyo yetu inatulia tunapooa polisi wako kwenye mikutano wakilinda amani. Wakati wa kampeni mwaka jana, kwa mfano, tuliona polisi walivyokuwa wakilinda mikutano ya vyama vyote vilivyoshiriki kampeni. Hayo yote na mengine mengi ni ya kujivunia, na ni sherti tukumbushane.

Ninapenda kuongelea hali ya sasa inayotokana na azma ya CHADEMA kutangaza kuwa itafanya mikutano na maandamano nchi nzima kupinga kile wanachoita udikteta. Katika mazingira haya, tunawasikia viongozi wa CCM wakitoa vitisho dhidi ya kampeni hiyo inayoitwa UKUTA. Wanadai kuwa maandamano haya yanaashiria uvunjifu wa amani. Viongozi wa CCM wamefanikiwa kuliaminisha jeshi la polisi kuwa maandamano haya hayana nia njema bali kuharibu amani.
Napenda kusema kwamba hizi kauli za viongozi wa CCM ni za kijinga. Wananchi wanafahamu umuhimu wa amani. Ni wao ndio walinzi wakuu wa amani, kwa sababu wanajua kuwa wanaihitaji. Haijalishi kama wanachi hao ni wanaCCM au wapinzani. Haijalishi kama hawana chama. Wote tunataka amani.

Kauli za viongozi wa CCM kwamba CHADEMA wanataka kuharibu amani ya nchi hazina mashiko. Mheshimiwa Freeman Mbowe, mwenyekiti wa CHADEMA, ni mfanyabiashara. Hainiingii akili kuwa mfanyabiashara asipende amani, kwani amani ikivunjika, biashara zake hazitapona. Duniani kote, tunaona jinsi vibaka wanavyopora maduka na kuharibu biashara wakati amani inapovunjika. Hapa Marekani, kwa mfano, ikivunjika amani katika mji wowote, tunaona katika jinsi vibaka wanavyopora maduka na kuharibu biashara. Amani ikivunjika, wafanyabiashara ni waathirika wakuu.

Watanzania tunaposikia kauli za viongozi wa CCM tunapaswa kujiuliza: Je, ni kweli kwamba Mbowe anataka kuharibu amani? Kama ni kweli, basi Mbowe atakuwa ni mfanyabiashara wa ajabu, tofauti kabisa na wenzake, kama vile akina Bakhressa, Mohammed Dewji, Reginald Mengi, na wauza chipsi mayai mitaani. Muuza chipsi mayai anataka amani. Sembuse mfanyabiashara mwenye biashara kubwa na mali nyingi kama Mbowe?

Duniani kote wafanyabiashara, wawekezaji, na wajasiriamali wanaombea amani. Wawekezaji hawapeleki mitaji kwenye nchi isiyo na amani. Tanzania tunajivunia amani, na tunawaalika wawekezaji waje. Kama kuna mtu mwenye maslahi makubwa katika kuhifadhi amani, ni mwekezaji na mfanyabiashara. Propaganda za CCM kwamba Freeman Mbowe anataka kuhujumu amani ni ujinga.

Ninasikitika kwamba polisi wamerubuniwa na propaganda za kijinga za viongozi wa CCM. Matokeo yake tunayaona. Polisi wanakiuka wajibu wao wa kulinda amani katika mikutano na maandamano. Sheria ya vyama vya siasa inatamka wazi kuwa chama chochote hakiruhusiwi kutumia vyombo vya dola kuvitisha au kuvikandamiza vyama vingine. CCM inakiuka sheria hiyo, na inalitumia jeshi la polisi kinyume na sheria. Hili ni tatizo kubwa, na jeshi la polisi linawajibika kujirekebisha.

---
Prof. J. Mbele via HapaKwetu blog

Karibu nyumbani Simbu na pongezi kwa kutuwakilisha vyema Rio Olympics 2016Mwanariadha Mtanzania wa mbio ndefu, Alphonce Felix Simbu (24) jana amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam akitokea nchini Brazil kwenye michuano ya Kimataifa ya Olimpiki.

Simbu alitia fora kwa kushika nafasi ya 5 kwenye siku ya mwisho ya michuano ya Olimpiki katika mashindano ya marathon jijini Rio de Janeiro nchini Brazil kwa kutumia saa 2:11:15.Wafanyakazi NMB waung'arisha mji wa Moshi

Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo la njia mbili maarufu kama Double Road mjini Moshi leo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakivuka barabara tayari kuanza zoezi la kufanya usafi katika eneo la Double Road mjini Moshi leo.


Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakifanya usafi katika maeneo ya maduka yaliyopo eneo la Double Road mjini Moshi.Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi Emanuel Kishosha akiowaongoza wafanyakazi wenzake katika zoezi la kufanya usafi .


Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakiokota taka zilizokusanywa wakati wa zoezi la usafi lilofanyika katika eneo la Double Road mjini Moshi.Wafanyakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa na taka zilizokusanywa wakienda kuzitupa katika eneo la kusanyia takataka.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiendelea na usafi katikati ya barabara .

Meneja wa NMB tawi la Neslon Mandela Emanuel Kishosha akiwa amebeba taka mara baada ya kumaliza kuzikusanya wakati wa zoezi hilo la usafi.

Hivi ndivyo yalivyooonekana maeneo ambayo wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi walishiriki kuyafanyia usafi mjini Moshi hii leo.
  • Dixon Busagaga

Taarifa ya kusimamishwa kazi viongozi/watendaji 5 TPDC


4th Tanzania Oil and Gas Suppliers Conference


PRESS RELEASE 
 27TH Aug 2016
  • The 4th Tanzania Oil and Gas Suppliers Conference is set to welcome 200 delegates in 1st September this year.
  • The 4th Tanzania Oil and Gas Suppliers’ Conference kicks off in Dar on 1st September.
  • The 4th TOGSC to discuss opportunities in Tanzania helium gas on 1st September.
The 4th Tanzania Oil and Gas Suppliers’ Conference is taking place on the 1st September 2016 in Dar- Es- Salaam at Kilimanjaro Auditorium hall in (Bank of Tanzania) . Bringing together leading companies’ senior managers, representatives from related ministries, and renowned oil and gas industry experts.

In consideration of the developments, challenges and opportunities facing the oil and gas industry in meeting the growing energy needs of Tanzania region, the theme of the conference is “FURSA IN TANZANIA OIL PIPELINE, HELIUM & LNG PLANT”

Tanzania oil and gas suppliers conference will provide the opportunity to share opinions on current local content issues in the oil and gas industry including the recent agreements between president of Tanzania HE John Magufuli and President Of Uganda HE Yoweri Museveni to build a crude oil pipeline of 1,400km which will connect Uganda’s western region near Hoima District, where big oil reserves have been discovered, with Tanzania’s port of Tanga.

For the first time in Tanzania the conference will cover the subject on the discovery of the rare Helium Gas in large quantity in Tanzania which contains up to 10.6 percent helium, while the reserve is estimated to hold about 54 billion cubic feet of helium gas in total. And addressing the opportunities for Tanzanian owned and based companies to be part of its value chain as it is used in hospitals in MRI scanners, as well as in space craft, telescopes, and radiation monitors.

Apart from that the conference will also address about The future of liquefied natural gas (LNG) plant construction in Lindi by Tanzanian government, analyzing the Tanzanians entrepreneurs engagement in the LGN plant constructions as well as opportunities seen in this sectors, as Tanzania being holder of East Africa’s biggest natural gas reserves after Mozambique, with the ownership of 19,000 acres at Likong’o Mchinga in Lindi that pave the way for $30 billion LNG plant.

Around 200 delegates from more than 60 companies will take place in this conference, more than 20 speakers including leading experts, representatives of government bodies and directors of major oil and gas companies in Tanzania will discuss key issues in Tanzania oil pipeline, helium gas and future of the LNG plant.

Tanzania stakeholders are mainly advised to participate as the conference provide the suppliers with the opportunity to talk to colleagues, to gain more knowledge in oil and gas sectors, to get new information and technologies, expanding the opportunities for collaboration in the oil and gas sector both national and international.

The 4th Tanzania oil and gas suppliers conference is proudly sponsored and organized by 361 Degrees Tanzania

END

ABOUT TANZANIA OIL AND GAS SUPPLIERS CONFERENCE

Tanzania Oil and Gas Suppliers Conference (TOGSC) is a platform that bring together players from the value chain together with stakeholders from the government and the oil and gas industry to discuss and engage on the different opportunities and challenges in Tanzania. Incepted in 2013 with more than 100 delegates and exhibitors form leading oil and gas companies in Tanzania

This event provides an opportunity to Network, Engage, and Build knowledge and do business within the Neo Oil & Gas Industry in Tanzania. And aiming at being the ultimate link between the value chain and the stake holders in the oil and gas industry in Tanzania by empowering and building capacity, championing local content.

For more information visit www.togsc.com

Or contact : Maryam idrissa
Public relation officer
0652 345 451

[email protected]

Uchambuzi kuhusu uteuzi wa Dkt Kipilimba kuiongoza TISSTarehe 24 mwezi huu, Rais Dokta John Magufuli alimteua Dokta Modestus Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu (DGIS) wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Uteuzi huo umefanyika kufuatia kustaafu kwa mkurugenzi aliyemaliza muda wake, Othman Rashid.

Makala hii inajikita katika uchambuzi wa uteuzi huo kwa kuangalia changamoto na fursa zinazomkabili kiongozi huyo mkuu wa taasisi hiyo nyeti kabisa. Kwa mtizamo wangu, kama kuna kitu ambacho kinaweza kuzua maswali kuhusu uteuzi huo basi ni wadhifa wa Director of Risk Management alioshikilia Dokta Kipilimba huko nyuma alipokuwa mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania.

Sote twafahamu jinsi Benki Kuu yetu imekuwa ikiandamwa na matukio mfululizo ya ufisadi, kuanzia EPA hadi Tegeta Escrow. Kwa wadhifa wake katika taasisi hiyo, kuna uwezekano wa bosi huyo mpya wa mashushushu kuonekana ‘sehemu ya mfumo ulioshindwa kudhibiti ufisadi.’ Hata hivyo, utetezi unaweza kuwa huenda yeye alitekeleza majukumu yake vema lakini walio juu yake hawakuchukua hatua stahili.

Kadhalika, huko mtandaoni kuna ‘tuhuma’ kadhaa kuhusu Dokta Kipilimba, lakini itakuwa sio kumtendea haki yeye, blogu hii na mie mwenyewe kujadili tuhuma ambazo hazina ushahidi wowote. Ni muhimu kutambua kuwa Tanzania yetu licha ya kuwa kisiwa cha amani pia ni kisiwa cha majungu, uzandiki, fitna, umbeya na uzushi.

Changamoto kubwa kwa Dokta Kipilimba ni pamoja na kurejesha hadhi na heshima ya Idara ya Usalama wa Taifa. Katika miaka ya hivi karibuni, taasisi hiyo muhimu kabisa imekuwa ikishutumiwa kuwa inachangia ustawi wa ufisadi, ujangili, biashara ya madawa ya kulevya, nk.

Wanaoilaumu taasisi hiyo hawamaanishi kuwa watumishi wake wanahusika katika matukio hayo ya kihalifu as such bali kushindwa kwa Idara hiyo kukabiliana na kushamiri kwa matendo hayo ya kihalifu, ambayo kimsingi ni matishio kwa usalama wa taifa, na kazi kuu ya Idara hiyo ni kukabiliana na matishio kwa usalama wa taifa la Tanzania.

Ninaamini kuwa Dokta Kipilimba anafahamu kanuni muhimu kuhusu ufanisi au mapungufu ya idara ya usalama wa taifa popote pale duniani, kwamba “kushamiri kwa vitendo vinavyotishia usalama wa taifa lolote lile ni kisheria cha mapungufu ya idara ya usalama wa taifa ya nchi husika, na kudhibitiwa kwa vitendo vinavyotishia usalama wa taifa popote pale duniani ni kiashiria cha uimara wa idara ya usalama wa taifa ya nchi husika.”

Kwahiyo, kwa kuzingatia kanuni hiyo, kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya, ujangili, rushwa, na ufisadi mwingine ni viashiria vya mapungufu ya Idara yetu ya Usalama wa Taifa.

Changamoto nyingine kwa Dokta Kipilimba ni tuhuma za mara kwa mara dhidi taasisi hiyo muhimu kabisa kuwa katika utendaji kazi wake imegeuka kuwa kama ‘kitengo cha usalama cha chama tawala CCM.’ Idara hiyo imekuwa ikituhumiwa kuwa kwa kiasi kikubwa imeweka kando taaluma ya ushushushu (tradecraft) na kutekeleza majukumu yake kisiasa.

Madhara ya muda mfupi ya kasoro hiyo ni taasisi hiyo kujenga uhasama na vyama vya upinzani na kwa namna flani kupoteza heshima na uhalali wake. Lakini la kuogofya zaidi ni madhara ya muda mrefu, ambapo watu wanaoweza kuwa ni matishio kwa usalama wa taifa letu wanaweza kutumia ‘urafiki’ unaodaiwa kuwepo kati ya Idara ya Usalama wa Taifa na CCM, wakitambua bayana kuwa ‘Idara haina muda na makada wa chama tawala,’ na hatimaye kufanikiwa kutimiza azma zao ovu.

Baadhi ya watumishi wa zamani wa taasisi hiyo walijikuta matatizoni kwa vile tu walitekeleza majukumu yao dhidi ya wanasiasa wa chama tawala, na wakaishia kuonekana kama wahaini.

Changamoto nyingine kwa Dokta Kipilimba ni tuhuma zinazoikabili taasisi hiyo kuhusu mfumo wa ajira ambapo inadaiwa kuwa zimekuwa zikitolewa kwa upendeleo kwa ndugu na jamaa za ‘vigogo.’ Tatizo kubwa hapa ni kwamba utiifu wa ‘ndugu na jamaa hao wa vigogo’ haupo kwa taifa bali kwa vigogo hao waliowaingiza Idarani. Pengine sio vibaya kufikiria ‘utaratibu wa wazi’ katika ‘recruitment’ kama inavyofanywa na wenzetu wa CIA, NSA, MI5, MI6, HGCQ, nk wanaotangaza nafasi za ajira kwenye vyombo vya habari.

Pia kuna tatizo la baadhi ya maafisa usalama wa taifa ‘kujiumbua’ kwa makusudi kwa sababu wanazojua wao wenyewe, kubwa ikiwa kutaka sifa tu, au waogopwe ‘mtaani.’ Hii inaathiri sana ufanisi wa maafisa wa aina hiyo kwani ni vigumu kutekeleza majukumu yao ipasavyo pasi usiri.

Sambamba na hilo ni kasumba ya muda mrefu ambapo baadhi ya maafisa wa Idara hiyo waliopo kwenye vitengo mbalimbali kuwepo huko kwa muda mrefu mno kiasi cha kuathiri utendaji wao. Miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na ‘vituo muhimu’ na kwenye ofisi za balozi zetu nje ya nchi. Ikumbukwe kuwa unless afisa ametengeneza deep cover, uwepo wake kwa muda mrefu katika sehemu aliyokuwa ‘penetrated’ au kituo chake cha kazi kwingineko (mfano ubalozini) unaweza kupelekea ‘akaungua’ (burned).

Changamoto nyingine kubwa ni uwepo wa majasusi kibao nchini mwetu, hususan kutoka nchi moja jirani, huku wengi wa majasusi hao wakiwa wameajiriwa katika taasisi za umma na binafsi. Hili ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa wa Tanzania yetu.

Kwa upande fursa kwa Dokta Kipilimba, licha ya kuwa ‘mwenyeji’ katika taasisi hiyo muhimu, wasifu wake kitaaluma unamweka katika nafasi nzuri sana kukabiliana na changamoto za karne ya 21 ambayo imetawaliwa zaidi na teknolojia ya kisasa.

Dokta Kipilimba ni msomi aliyebobea kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na yayumkinika kuamini kuwa anaweza kutumia usomi wake kuibadilisha Idara yetu ya Usalama wa Taifa kwenda na wakati, kufanya kazi kama taasisi ya kishushushu ya karne ya 21, ambayo licha ya kutegemea HUMINT inaweza pia kutumia njia nyingine za kukusanya taarifa za kiusalama kwa kutumia teknolojia (GEOINT, MASINT, SIGINT, CYBINT, FININT na TECHINT kwa ujumla.

Fursa nyingine kwa Dokta Kipilimba ni matarajio ya sapoti ya kutosha kutoka kwa Rais Dokta Magufuli ambaye kama alivyoahidi wakati wa kampeni za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana, mapambano dhidi ya ufisadi yamepewa kipaumbe cha hali ya juu kabisa. Kama ‘sponsor’ na ‘consumer’ wa taarifa za kila siku usalama, inatarajiwa kuwa Dokta Magufuli atatekeleza ushauri wa Idara katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama wa taifa letu.

Dokta Kipilimba ana fursa ya kuleta mageuzi kwa Idara ya Usalama wa Taifa kwa kuangalia uwezekano wa kuwafikia watu walio nje ya taasisi hiyo, hasa pale uwezo wa Idara yetu unapokuwa limited. Nitoe mfano. Katika kupata taarifa mwafaka wa kudumu kuhusu, kwa mfano, mgogoro wa kisiasa huko Zanzibar, Idara inaweza ku-reach out wanazuoni wa historia ya taifa letu walipo ndani na nje ya nchi yetu.

Ikumbukwe kuwa sio rahisi kwa taasisi hiyo kuwa na maafisa au watoa habari katika kila eneo. Wenzetu wa nchi za Magharibi wamekuwa wakikabiliana na hali hiyo kwa kufanya kazi na ‘makandarasi’ (contractors), ambao of course, wamekidhi taratibu kama vile vetting.

Sambamba na hilo ni Idara hiyo kuangalia uwezekano wa kutumia hazina kubwa tu ya maafisa wake wa zamani, hususan wastaafu Ikumbukwe kuwa wengi wao ni watu wanaowindwa na ‘subjects’ mbalimbali wanaolenga kulihujumu taifa letu.

Nimalizie makala hii kwa kutoa pongezi za dhati kwa Dokta Kipilimba na Naibu wake (DDGIS) Robert Msalika, sambamba na kumtakia mapumziko mema Mkurugenzi mstaafu Othman, na kumkaribisha ‘uraiani.’
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI IDARA YETU YA USALAMA WA TAIFA