Oh no! Samsung Galaxy Note7 inside Jeep SUV explode, burns the car


A Florida family got the shock of their lives over the holiday weekend when they discovered their Jeep engulfed in flames apparently after a phone left in the car exploded.

Nathan Dornacher and his wife Lydia Dornacher had returned home from a garage sale to unload a desk for their daughter Monday morning. Nathan left his Samsung Galaxy Note7 cell phone charging in the vehicle.

When he returned to the car to get the device, he couldn't believe what he saw.

“We were planning on grabbing the dog and [their 8-year-old daughter] and heading to Petco,” he wrote on Facebook. “I head back out to the car to grab my phone … and see flames.”

Fire had spread throughout the entire vehicle and black smoke billowed out of the torched SUV, photos of the incident showed.

St. Petersburg fire crews extinguished the fire. All that was left was metal, wires and ash.

“Not the barbecue I wanted on my day off,” Nathan Dornacher wrote.

The harrowing incident came just three days after Samsung recalled its Galaxy Note 7 smartphones in 10 countries after 35 incidents of the devices catching fire or exploding were confirmed.

Of the 35 prior incidents, 17 took place in the United States, with 17 others in Korea and one in Taiwan, Samsung said.

No injuries have been reported in relation to the recall.

After a thorough investigation, Samsung identified a “battery cell issue,” the company said in a September 2 statement.

In a question and answer section on its U.K. news portal, Samsung explained that “an overheating of the battery cell occurred when the anode-to-cathode came into contact, which is a very rare manufacturing process error.”

Customers who already bought the Note 7s could exchange them for new smartphones “as early as this week,” Samsung noted on its site, but a specific date was not mentioned.

“We are aware of the incident and we are working with Mr. Dornacher to investigate his case and ensure we do everything we can for him,” a Samsung spokesperson said in a statement to InsideEdition.com. “Consumer safety is Samsung’s highest priority. With regard to the Galaxy Note7, we are asking owners to take advantage of the Product Exchange Program announced on Friday of last week.

“The program offers Note7 owners the opportunity to exchange the phone for a new one. More details on the program can be found at http://www.samsung.com/us/note7exchange.”

Nathan Dornacher wrote on Thursday that Samsung has been very helpful since the incident.

“They are sending someone to review everything,” he wrote on Facebook. “We will not gain anything from this for the keyboard investigators out there. Yes we had insurance but very minimum and nothing to cover any of the recent work done [to the vehicle] no one’s fault but our own.

“We are not and have not asked for anything, we are not getting a lawyer, we will replace in time when we can afford it,” he continued. “All I want out of this is for everyone to take this recall seriously and if you didn't know about it please educate yourself before it's too late. I had the phone for 5 days and not having TV or a notification we did not know.

“We are safe no one was hurt all that matters to me.”


Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Septemba 9, 2016How to save on insurance: Whole life policy vs Term life insurance


Life insurance is important because it's a better way to love your family that ensure they’ll be taken care of if something happens to you.

According to EveryDollar post, research shows 64% of policyholders pay thousands more for life insurance than they have to each year. What are they doing wrong? They’re throwing money into a cash-value insurance policy.

People flock to one of the worst financial products out there, the cash-value policies, because they package insurance and savings together. The investment returns are very low, and your money is eaten away by big fees and commissions. Plus, if something happens to you, your family only gets the face value of your policy.

A Better and Less Expensive Plan for the Future is Term life insurance
  • Term life insurance is far less expensive, and you can invest the leftover money in growth stock mutual funds that you control. Here’s a good example.
  • Term life gives you the best mix of cost, coverage and control. So trade in that whole life policy for term life insurance! You can pick the right amount to take care of your family for a lower monthly price. Since you pay less, you can direct that leftover money toward investing or paying off debt.
Get more the app

Taarifa ya habari ChannelTEN Septemba 8, 2016Mushengezi: Tafakuri ya miaka 20 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania

Mengi yamesemwa katika miezi minane iliyopita juu ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli (JPM) katika ukusanyaji wa kodi.

Mara tu baada ya JPM kuchukua hatamu za uongozi tulishuhudia hatua mbalimbali zikichukuliwa baada ya Serikali hiyo ‘kugundua’ maeneo yaliyokuwa yanasababisha au kuchangia katika uvujaji wa mapato ya Serikali. Ghafla tukaambiwa juu ya makontena lukuki ya bidhaa zilizokuwa zimeondolewa kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam na maeneo mengine maalum ya kutunzia mizigo (ICDs) bila kulipiwa ushuru wa forodha na kodi nyingine.

Tuliambiwa pia juu ya meli nyingi zilizowahi kuwasili bandarini, zikateremsha mizigo na kuondoka bila kutozwa hata ‘ndululu’ na Mamlaka ya Bandari kama sheria na taratibu zinavyotaka. Viongozi wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) walivuliwa nyadhifa zao; na muda mfupi baadaye wengine kuteuliwa kushika nyadhifa hizo.

Baada ya hapo kuna kila dalili kwamba ufanisi wa taasisi hizo mbili umekuwa unaongezeka siku hadi siku. Kwa hiyo ni sahihi kabisa kupongeza hatua za awali zilizochukuliwa na Serikali na pia kupongeza viongozi wapya wa taasisi hizo. Hapo juu nimezungumzia juu ya Serikali ya JPM ‘kugundua’ maeneo yaliyokuwa yanasababisha au kuchangia uvujaji wa mapato. Si hilo tu. Serikali mpya ‘iligundua’ pia madudu mengi yaliyofanyika wakati wa Serikali zilizoongozwa na Jakaya Kikwete na watangulizi wake yaliyosababisha udumavu wa maendeleo ya nchi hii. Sina haja ya kuainisha hayo kwa kuwa yameandikwa sana.

Swali ambalo wengi wamejiuliza bila kupata majibu ni je, ni kweli kwamba Serikali iligundua hayo katika muda mfupi tangu iingie madarakani au JPM alipoingia ofisini alikuta majalada yenye taarifa mbalimbali za ‘madudu’ hayo, ambazo zilikuwa hazikufanyiwa kazi na mtangulizi wake na hivyo akaamua kuanza na kazi ya ‘kusafisha meza na makabati?

Au kwa kuwa JPM alikuwa kwenye serikali za awamu mbili zilizomtangulia alikuwa anafahamu ‘madudu’ hayo, lakini alishindwa kushawishi viongozi wa awamu hizo kuchukua hatua stahiki?

Bahati mbaya hata mimi, kama wengine, sina majibu ya maswali hayo. Itoshe kusema kwamba hata kama tumechelewa miaka 10 au 20, hatuna budi kufarijika kwamba angalau hatua zimeanza kuchukuliwa.

Hata hivyo, kama wengi tunavyojua, HAPA KAZI BADO, tena sana! Maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na kashfa mbalimbali zilizotikisa taifa hili wakati wa awamu zilizopita na bado hayajashughulikiwa. Vyombo vingi vya habari, hususan magazeti, havichoki kukumbusha viongozi (au watawala?) wetu juu ya ulazima wa kuchukua hatua stahiki juu ya maovu yote yaliyofanyika au yanayoendelea kufanyika, tena baadhi ya maovu hayo yakiwa mazito zaidi kuliko yale yaliyoshughulikiwa hadi sasa. Hiyo ni‘selective justice’ kwa wananchi ambao ndio waathiriwa wa maovu hayo. Au labda ni vema tuanze mchakato wa kujitazama kama Taifa, tuzungumze kwa uwazi yote yaliyotokea ya kuteteresha uchumi na mustakabali wa Taifa hili na hatimaye tufanye maridhiano na kusameheana kama walivyofanya wenzetu wa Afrika Kusini?

Kwa kuwa mada hii inajikita katika kuangalia machache ya hayo yaliyotokea katika TRA katika miaka 20 tangu ianze kufanya kazi Julai 1996 na uhusika wa viongozi katika kuathiri utendaji wake, nitaanza kwa kutoa mfano ‘ulio hai’ wa jipu ambalo nilitarajia kuwa miongoni mwa ‘majipu’ ya kwanza kutumbuliwa.

Kuna kampuni moja ambayo kwa takriban miaka 10 ilishikilia eneo moja nyeti la uchumi wa nchi yetu. Kampuni hiyo ilihodhi kwa kiasi cha kutisha biashara ya kuingiza bidhaa nchini kutoka nje bila kulipa kodi kwa thamani na viwango vinavyotakiwa. Si tu kwamba ilikuwa inaagiza bidhaa nyingi na kuziuza kwa bei nafuu, bali iliwalazimisha waagizaji wengine kupitisha bidhaa zao mikononi mwake kama walitaka kuendelea na biashara.

Wale waliokataa kutumia huduma ovu za kampuni hiyo walijikuta wakitozwa na TRA ushuru na kodi mbalimbali kwa viwango vinavyotakiwa au vya juu zaidi na hivyo kujikuta wakishindwa kuendelea na biashara.

Wale waliokubali kupitisha bidhaa zao kwenye kampuni hiyo, walifaidika na mtandao wake wa ufisadi kwa kulipa kodi kidogo au kutolipa kabisa na hivyo kuweza kuuza bidhaa zao sokoni kwa bei nafuu pia. Mengi yamesemwa na kuandikwa juu ya kampuni hiyo. Miongoni mwa hayo ni kwamba kampuni hiyo likuwa na mtandao mpana. Watumishi wa kampuni pamoja na viongozi wao walikuwa ‘hawagusiki’.

Aidha, kuna madai kwamba kampuni hiyo ilikuwa na ratiba maalumu ya kutembeza mgao wa fedha kwa wafadhili wake. Ilisemekana kwamba wale waliotaka mgao wao katika fedha za kigeni, kampuni ilitekeleza matakwa yao. Baadhi ya majengo mithili ya mahekalu na nyumba za kupanga, hususan ‘apartments’ tunazoona Dar es Salaam na kwingineko nchini yanasemekana kujengwa na fedha kutokana na bakhshish zilizolipwa na kampuni hiyo.

Mara tu baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, kampuni hiyo ilitangaza kuwa imefilisika! Sina taarifa yoyote kwamba Serikali mpya ililifahamu au inalifahamu hili na iwapo kuna hatua zilizochukuliwa au zilizoko mbioni kuchukuliwa juu ya kampuni hiyo ‘mufilisi’ na wote; na nina maana ya wote, waliohusika katika kashfa hii ya kampuni binafsi kutoza waagizaji wa bidhaa kodi na kuamua ni kiasi gani kiingie kwenye mfuko wa Serikali huku sehemu kubwa ikibaki kwake na mafisadi wengine walioitwa viongozi wa umma!

Iwapo iliweza kupitisha bandarini mizigo ya watu wengine kwa kulipa kodi kiduchu, ni dhahiri kwamba mizigo yake yenyewe ilikuwa inapita bila kulipiwa na kama ililipiwa, ni wao walioamua kiasi cha kulipa.

Kama nilivyogusia hapo juu, Juni mwaka huu TRA ilitimiza miaka 20 tangu ianze kazi rasmi. Historia inaonesha kwamba mwaka 1995, Serikali ilifanya uamuzi wa kuanzisha TRA. Uamuzi huo ulitokana na mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchambua Mfumo wa Mapato na Matumizi ya Serikali (MTEI COMMISSION) iliyoundwa na Mzee Mwinyi mwaka 1989.

Ni Tume hiyo hiyo liyopendekeza, pamoja na mambo mengine mengi, uanzishwaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Nilibahatika kuwa kwenye Sekretariati ya Tume ile kama nilivyobahatika kuwa mtu wa kwanza kuteuliwa na Serikali kuandaa uanzishwaji rasmi wa TRA baada ya sheria husika kupitishwa na Bunge.

Uamuzi wa kuondoa utawala na ukusanyaji wa kodi kutoka kwenye mfumo wa utumishi wa umma (civil service) ulikuwa na sababu mbili kuu.

Mosi, kutokana na uwezo mdogo wa kulipa watumishi wa umma vizuri na kuwapatia vitendea kazi vya kutosha, Serikali ilikubali pendekezo la Tume ile kuanzisha mamlaka inayojitegemea na kuipatia nyenzo za kutosha na pia kuwalipa watumishi wake vizuri kwa matumaini kwamba kwa kufanya hivyo, mamlaka hiyo ingeweza kukusanya kodi kwa ufanisi zaidi ili kuiwezesha Serikali kukidhi kwa kiasi kikubwa, matumizi ya Serikali.

Ilitarajiwa pia kuwa kwa kufanya hivyo, watumishi waliobaki kwenye mfumo wa kawaida wa utumishi nao wangeweza kuongezewa mishahara kadri mapato yalivyoongezeka ili nao wafanye kazi kwa ufanisi zaidi. Aidha, Tume ya Rais ilikuwa imeshauri kwamba mamlaka hiyo ingekuwa na uhuru zaidi wa kuajiri wataalamu kwa ajili ya kuongeza ufanisi, huku ikiwa pia na uhuru wa kuondoa watumishi wasiofaa kwa urahisi zaidi tofauti na serikalini ambako kulikuwa na urasimu.

Mara baada ya sheria hiyo namba 11 ya mwaka 1995 kuridhiwa na Rais mnano Julai 31, 1995, Bodi ya Wakurugenzi ya kwanza chini ya Gavana wa sasa wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu, iliundwa na kuanza kazi mara moja; mimi nikiwa Katibu wa Bodi hiyo. Miongoni mwa uamuzi muhimu wa kwanza wa Bodi ni ule wa kuacha, kwa kipindi cha mwaka wa kwanza, idara za kodi zilizokuwapo ziendelee na kazi chini ya mfumo na taratibu zilizokuwapo huku Bodi ikijikita kwenye kazi ya kuandaa mfumo na taratibu mpya ambazo zingeongoza chombo hicho kipya. Kwa maana nyingine, Bodi haikuona faida yoyote katika kurithi idara zilizokuwapo na taratibu na mifumo yake. Kufanya hivyo ingelikuwa ni sawa na kuweka mvinyo mpya katika chupa ya zamani. Kadri Bodi ilivyoendelea kutengeneza mifumo na taratibu mpya, ilifanya uamuzi muhimu ufuatayo:

Wafanyakazi wa chombo kipya (TRA) wangetokana na watumishi waliokuwa katika idara za kodi hizo hizo, yaani Idara ya Ushuru wa Forodha na Kodi ya Mauzo na Idara ya Kodi ya Mapato. Hata hivyo, iliamuriwa kuwa siyo wote wangechukuliwa. Ni wale tu ambao wangehakikiwa na kuonekana hawana matatizo ya kiutendaji na kimaadili ndio wangechukuliwa.

Kwa hiyo ulipofika wakati mwafaka na baada ya uchunguzi wa ndani, mamia ya watumishi katika idara hizo waliondolewa kazini kabla TRA haijazinduliwa rasmi. Kundi la pili la watumishi wa idara hizo liliondolewa baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na Bodi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali. Kwa maana hiyo, TRA ilipoanza kazi Julai mosi, 1996 ilianza kazi bila kuwa na ‘mzigo’ wa wafanyakazi ambao uadilifu wao ulikuwa wa shaka (doubtful integrity).

Wakuu wa idara zote katika TRA pamoja na manaibu wao, ikiwa ni pamoja na wale wa idara mpya za sheria, utumishi na fedha, ukaguzi wa ndani, utafiti na sera, n.k wangeajiriwa baada ya kudahiliwa na kuonekana wanafaa siyo tu katika utendaji kazi, bali pia kwa upande wa maadili.

Ili kuhakikisha kwamba chombo hicho kingeongozwa na watumishi wenye sifa hizo, iliamuriwa kwamba nafasi zote za wakuu wa idara na manaibu wao zingetangazwa na wale ambao wangefaulu wangefanya kazi kwa mkataba wa miaka mitatu mitatu ili kuhakikisha kwamba wanaendelea na sifa zilizowawezesha kuajiriwa.

Uamuzi mwingine muhimu uliofanywa na bodi kabla ya TRA kuanza kazi rasmi ni ule wa kuweka MASHARTI YA MAADILI (Code of Conduct) yaliyombana kila mfanyakazi. Kila mmoja alitakiwa kujaza fomu na kuorodhesha mali zake zote wakati wa kuingia TRA na kila mwaka baada ya hapo. Hii ilikuwa nguzo muhimu kuliko zote katika utendaji kazi wa watumishi wote. Nakumbuka kwamba kati ya mwaka 1996 na 2003 watumishi walio wengi waliheshimu na kufuata maadili ya kazi na hicho ndicho kilikuwa chanzo cha mafanikio tuliyoyashuhudia katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.

Hata hivyo, kama nilivyowahi kuandika mwaka 2006, nakisi katika maadili ya utumishi wa umma kwa ngazi zote iliwafanya watumishi wa TRA kuanza kulegea na hatimaye ‘kuanguka’ kwani katika mazingira kama hayo wasingeweza kuwa ‘watakatifu kumzidi Papa’.

Pamoja na hayo ni lazima nikiri kwamba hata kufifia kwa maadili ya watumishi wa umma katika Serikali nzima haukutokana na kukosa ‘code of conduct’. Viongozi wa juu hasa wale wa kisiasa walikuwa chanzo kikuu cha uozo katika utumishi wa umma. Nitatoa mifano michache ya mambo niliyoyashuhudia mimi binafsi.

Mwaka 1992 nikiwa Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya katika Idara ya Forodha tulifanikiwa kukamata kontena la futi 20 lililojaa dawa za kulevya. Enzi hizo kazi hiyo ilikuwa jukumu la Idara ya Forodha ingawa tulishirikiana na Jeshi la Polisi katika operesheni kubwa. Baada ya kukamatwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kontena hilo lilihifadhiwa kwenye bohari la Mamlaka ya Tumbaku Kurasini. Bohari lilifungwa na funguo kuwekwa katika mikono salama huku askari wa FFU wakililinda.

Siku konteina lilipofunguliwa kwa ajili ya Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi dhidi ya watuhumiwa wa kuliingiza nchini ili kuona vielelezo, iligundulika kwamba kontena lilikuwa limekatwa sehemu ya juu na dawa kuondolewa. Baada ya dawa kutolewa, sehemu iliyokatwa bati lake lilichomelewa upya. Hadi leo hakuna mtu yeyote aliyewahi kukamatwa kwa uhalifu huo uliofanyika ‘chini ya ulinzi wa FFU’.

Wakati tunapeleleza jinsi kontena hilo lilivyoingia nchini tulipata taarifa za kuaminika kuwa kontena la pili lilikuwa limeteremshwa kwenye Bandari ya Zanzibar.

Niliamua kwenda mwenyewe kufuatilia taarifa hizo. Baada ya kufanya kazi hiyo kwa siku kadhaa huku nikichunguza pia juu ya upatikanaji na matumizi ya dawa za kulevya Kisiwani humo, ilitolewa amri ‘kutoka juu’ kwamba niondoke Zanzibar katika muda wa saa tatu na nisirudi wakati wowote ‘bila kuomba na kupata kibali kutoka juu’.

Aliyenijulisha uamuzi huo wa Serikali alikuwa ni Waziri wa Fedha wa wakati huo. Ilikuja kufahamika kuwa ni vinara wa uingizaji wa dawa za kulevya ndio walijenga hoja iliyosababisha nifukuzwe mithili yaprohibited immigrant!

Mwaka 1993 nikiwa Kaimu Kamishna wa Upelelezi na Uzuiaji wa Magendo katika Idara hiyo hiyo niliamua kukagua viwanda vya wafanyabiashara waliokuwa wanaingiza walichoita mafuta ghafi ya kula ili kuhakiki iwapo walikuwa na mitambo ya kusindika mafuta hayo.

Nilitaka kufanya hivyo ili kulinda mapato ya Serikali kwa vile kwa muda mrefu mafuta ghafi yalikuwa hayatozwi ushuru wa forodha wala kodi ya mauzo. Tuliamini kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wanaingiza mafuta yaliyokuwa yamesindikwa, lakini ili kukwepa kulipa kodi waliamua kuyaingiza kama mafuta ghafi. Siku tulipokwenda kukagua kiwanda cha kwanza, tulicheleweshwa mlangoni wakati walinzi wakiwasiliana na wenye kiwanda.

Baada ya muda kupita huku tukisubiri, tuliitwa sehemu ya mapokezi ambako niliombwa kuzungumza na mtu aliyekuwa anasubiri kwenye ‘line’. Huyo hakuwa mwingine, bali Kamishna wangu ambaye aliniamuru kusitisha zoezi hilo (kazi hiyo) baada ya kupokea maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Tukio lingine katika mwaka huo huo ni pale nilipoamuriwa na kiongozi mwandamizi katika Wizara ya Fedha kuacha kufuatilia ulipwaji wa kodi kwenye kiasi kikubwa cha bia aina ya Stella Artois iliyokuwa imeingia nchini; na Waziri wa Fedha kuamua kwamba waingizaji wangelipa kodi husika kwa awamu (installments); uamuzi ambao ulikuwa kinyume cha sheria.

Kila mzigo mpya ulipofika nchini, kilitoka kibali kipya chenye masharti yale yale hata kama hakuna kodi iliyokwishakulipwa kwa mzigo uliotangulia. Nilipomwambia kiongozi huyo kuwa kufuatilia ulipwaji wa kodi hizo lilikuwa ni jukumu langu, alinitajia jina la mke wa kiongozi serikalini kuwa ndiye alikuwa anahusika na uingizwaji wa bidhaa hiyo. Nilipodadisi zaidi sababu za kunitaka nisitekeleze wajibu wangu, nilifukuzwa ofisini kwake na baada ya muda mfupi nilijikuta nashushwa cheo na kuhamishiwa mkoani Mwanza!

Hayo ni ya huko nyuma, lakini ni vielelezo vinavyothibitisha uhusika wa viongozi wa ngazi za juu serikalini na hata kwenye chama tawala katika kushuka kwa maadili ya watumishi wanaohusika na ukusanyaji kodi na wale wa umma kwa ujumla wao.

Mmomonyoko wa uadilifu katika utendaji kazi ndani ya TRA ulishika kasi baada ya Kamishna Mkuu wa kwanza kuondolewa kwa manufaa ya walafi. Hiyo ilikuwa mwaka 2003. Hata hivyo, mbegu za mmomonyoko huo zilianza kupandwa baada ya ujio wa Mwenyekiti wa Pili wa Bodi ya Wakurugenzi uliofuatiwa kwa karibu na mabadiliko ya mawaziri katika Wizara ya Fedha. Wote wawili walianza kukiuka misingi ya kazi iliyokuwa imewekwa na Bodi ya kwanza.

Misingi hiyo ndiyo ilikuwa nguzo ya ufanisi katika utendaji wa TRA kati ya mwaka 1996 na 2003. Pamoja na kwamba sheria iliyoanzisha TRA ilikuwa inatambua madaraka ya Waziri wa Fedha juu ya Bodi na watendaji wakuu wa TRA, mawaziri wa fedha waliokuwapo wakati TRA inaanzishwa hadi kuanza kufanya kazi waliheshimu mipaka ya kazi iliyokuwa imeainishwa kwa kuwa walikuwa wameidhinisha wenyewe. Mwenyekiti wa Bodi aliyeingia madarakani mwaka 1998 alitoka serikalini na alianza kulazimisha Bodi kubadili baadhi ya uamuzi wa Bodi ya kwanza. Alikuja na hoja za usawa wa jinsia na hata ukabila katika ajira bila kujali uwezo – na hilo lilianza kuathiri utendaji katika ukusanyaji mapato ya Serikali.

Aidha, alikiuka baadhi ya taratibu za kiutendaji kwa kushughulika na walipa kodi yeye mwenyewe huku akitoa maelekezo kwa Kamishna Mkuu juu ya viwango vya kodi vya kutoza wafanyabiashara hao. Kwa kufanya hivyo alikuwa anakiuka sheria ya TRA ambayo inakataza Bodi kuingilia kazi za ukadiriaji na ukusanyaji kodi.

Hakuishia hapo. Ilifika wakati akaanza kuongoza timu za wapelelezi wa kodi kufanya doria mchana na usiku ili kukamata bidhaa za magendo au wakwepakodi. Tuliomuonya juu ya ukiukwaji huo wa sheria ‘tulilipwa’ kama alivyoona inafaa.

Kwa ujumla, Mwenyekiti huyo alishirikiana na Waziri wa Fedha wa wakati huo katika kukanyaga msingi imara uliokuwa umejengwa na Bodi ya kwanza pamoja na Waziri aliyekuwapo wakati huo. Wote wawili walishirikiana kuweka viongozi waliotaka na ambao wangetii maagizo yao bila kuhoji. Wigo wa fungate hilo la viongozi wapya wa TRA na wale wa wizara liliendelea kupanuka hadi kwenye ngazi za juu za uongozi wa nchi, huku wakiingiza pia viongozi wa idara nyeti kama Takukuru na Usalama wa Taifa.

Kutokana hali hiyo, ilifika wakati ambako viongozi wa TRA walifanya wanalotaka wakijua kuwa hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuwauliza; achilia mbali kuwawajibisha. Matunda ya hali hiyo ni pamoja na madudu machache sana yaliyoibuliwa na Serikali mwanzo kabisa wa Awamu hii ya uongozi wa nchi hii.

Kwa hiyoTRA chini ya uongozi wake mpya inaposherehekea(?) kutimiza miaka 20 tangu ianze kazi rasmi inahitajika kuangalia misingi na sababu za mafanikio yake katika miaka ya kwanza ya uhai wake na kuiboresha kwa ajili ya kupata ufanisi zaidi.
  • Mushengezi Nyambele, kitaaluma ni Mwanasheria na Mtaalamu wa Kodi. Alishiriki kuanzisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwaka 1996 na kushika wadhifa wa Katibu wa Bodi na Mshauri Mkuu wa Sheria. Anapatikana kupitia simu: 0764 501 264

Mabadiliko bandarini

Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko amefanya mageuzi makubwa katika Bandari ya Dar es Salaam, sasa magari yanaruhusiwa kutolewa kwa saa 24.

Taarifa zilizolifikia JAMHURI zinasema Mhandisi Kakoko ametoa maelekezo mahususi kwa watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam kufanya kazi za wateja wote watakaofika Bandarini hapo kila siku kutoa mizigo yao hadi ziishe ndipo waende nyumbani.
“Ni kweli. Nimesema wafanyakazi wanaopitiliza muda wa kazi walipwe mafao ya ziada, ila kama kuna mfanyabiashara anayesubiri kutoa mzigo bandarini na amefika hapo hata kama amefika saa 5 usiku aweze kulipa ushuru na kuwezeshwa kuchukua mzigo wake,” Mhandisi Kakoko ameliambia JAMHURI.
Amesema amebaini wateja wengi walikata tamaa kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam, kutokana na kusumbuliwa hivyo ameamua kudhibiti usumbufu.

Katika kuthibitisha hilo, Idara ya Uhusiano ya Mamlaka ya Bandari imetoa Tangazo linaloeleza kuwa benki zenye matawi yake katika eneo la Bandari zitalazimika kufanya kazi hadi saa 6 usiku.
“Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwatangazia wateja wake, wadau, watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam na umma kwa ujumla kwamba; muda wa kulipia ankara za forodha katika ofisi za TRA na matawi ya benki ya CRDB na NMB yalipo ndani ya bandari sasa umeongezwa hadi saa sita (6) usiku ili kuongeza kasi ya utoaji wa magari bandarini.
“Tayari utaratibu huu umeshaanza kutumika na Mawakala wa Forodha wanashauriwa kutumia fursa hii kikamilifu. Endapo itaonekana kuna mahitaji ya huduma za Forodha na za kibenki baada ya saa sita usiku, muda huu utaongezwa.
“Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania inachukua fursa hii kuwashukuru wadau wote kwa ushirikiano wenu katika kuhakikisha bandari za Mamlaka zinatoa huduma zenye ufanisi na za gharama stahiki kwa watumiaji,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Habari kutoka kwa wafanyabiashara walioomba wasitajwe majina, zinasema wamefurahia utaratibu huo ila kabla ya kupongeza wanajipa muda kuona kama utaendelea au ni nguvu ya soda. Hadi sasa bandari imepewa lengo la kuzalisha Sh trilioni moja na kwa mwaka wa mapato ulioisha walifikia asilimia 68 ya lengo.

Bandari sasa imeanza kupata wateja baada kupiga marufuku mizigo ya wateja kwenda kwenye Bandari Kavu kabla ya eneo la Bandari kujaa mizigo, hali iliyokuwa inaongeza gharama za kusafirisha mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam kweni wenye ICDs walikuwa wanatumia mwanya huo kukamua wafanyabiashara.

Mwasisi wa TRA ‘ajilipua’ namna vigogo walivyovuruga na ufisadi wa viongozi waandamizi serikalini

Mmoja wa waasisi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mushengezi Nyambele,  hatimaye amejitokeza kueleza namna vigogo walivyoshiriki kuvuruga Mamlaka hiyo na vitendo vya ufisadi vilivyofanywa na baadhi ya viongozi waandamizi serikalini.

Nyambele ni Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi na Mshauri wa Sheria wa TRA wa kwanza.

Anaeleza matukio kadhaa yaliyofanywa na wakubwa serikalini, yakiwamo ya ukwepaji kodi, uptevu wa kontena zima lenye dawa za kulevya; na TRA ilivyoingiliwa na ukabila na upendeleo.

Juni 20, mwaka huu, TRA ilitimiza miaka 20 tangu ilipozinduliwa na Rais Benjamin Mkapa.

Nyambele ameliambia JAMHURI: “Ni lazima nikiri kwamba hata kufifia kwa maadili ya watumishi wa umma katika Serikali nzima hakukutokana na kukosa ‘code of conduct’.
“Viongozi wa juu, hasa wale wa kisiasa walikuwa chanzo kikuu cha uozo katika utumishi wa umma. Nitatoa mifano michache ya mambo niliyoyashuhudia mimi binafsi.”
Anarejea nyuma kidogo mwaka 1992 kabla ya kuanzishwa kwa TRA na kusema, mwaka huo akiwa Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya katika Idara ya Forodha walikamata kontena la futi 20 lililojaa dawa za kulevya.

Kwa sasa anasita kumtaja mtu au watu walioingiza dawa hizo na baadaye kuziiba kwa kukata kontena, lakini anasema ni watu wakubwa serikalini.
“Enzi hizo kazi hiyo ilikuwa jukumu la Idara ya Forodha ingawa tulishirikiana na Jeshi la Polisi katika operesheni kubwa.
“Baada ya kukamatwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kontena hilo lilihifadhiwa kwenye bohari la Mamlaka ya Tumbaku Kurasini. Bohari lilifungwa na funguo kuwekwa katika mikono salama huku askari wa FFU wakililinda.
“Siku kontena lilipofunguliwa kwa ajili ya Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi dhidi ya watuhumiwa wa kuliingiza nchini ili kuona vielelezo, iligundulika kwamba kontena lilikuwa limekatwa sehemu ya juu na dawa kuondolewa!
“Baada ya dawa kutolewa, sehemu iliyokatwa bati lake lilichomelewa upya. Hadi leo hakuna mtu yeyote aliyewahi kukamatwa kwa uhalifu huo uliofanyika ‘chini ya ulinzi wa FFU’”.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) wa wakati huo alikuwa Harun Mahundi; na Mkuu wa Upepekezi katika Jeshi hilo alikuwa Arthur Mwaitenda.

Anasema wakati wakipeleleza jinsi kontena hilo lilivyoingia nchini, walipata taarifa za kuaminika kuwa kontena la pili lilikuwa limeteremshwa kwenye Bandari ya Zanzibar.
“Niliamua kwenda mwenyewe kufuatilia taarifa hizo. Baada ya kufanya kazi hiyo kwa siku kadhaa huku nikichunguza pia juu ya upatikanaji na matumizi ya dawa za kulevya Kisiwani humo, ilitolewa amri ‘kutoka juu’ kwamba niondoke Zanzibar katika muda wa saa tatu na nisirudi wakati wowote ‘bila kuomba na kupata kibali kutoka juu’”.
Nyambele anasema aliyemjulisha uamuzi huo wa Serikali alikuwa ni Waziri wa Fedha wa wakati huo. Ingawa hamtaji kwa jina, Waziri wa Fedha kipindi hicho alikuwa Profesa Kighoma Malima.
“Ilikuja kufahamika kuwa ni vinara wa uingizaji wa dawa za kulevya ndio walijenga hoja iliyosababisha nifukuzwe mithili ya prohibited immigrant!,” anasema.
Katika tukio jingine, Nyambele anasema: 
“Mwaka 1993 nikiwa Kaimu Kamishna wa Upelelezi na Uzuiaji wa Magendo katika Idara hiyo hiyo niliamua kukagua viwanda vya wafanyabiashara waliokuwa wanaingiza walichoita mafuta ghafi ya kula ili kuhakiki iwapo walikuwa na mitambo ya kusindika mafuta hayo.
“Nilitaka kufanya hivyo ili kulinda mapato ya Serikali kwa vile kwa muda mrefu mafuta ghafi yalikuwa hayatozwi ushuru wa forodha wala kodi ya mauzo. Tuliamini kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wanaingiza mafuta yaliyokuwa yamesindikwa, lakini ili kukwepa kulipa kodi waliamua kuyaingiza kama mafuta ghafi.
“Siku tulipokwenda kukagua kiwanda cha kwanza, tulicheleweshwa mlangoni wakati walinzi wakiwasiliana na wenye kiwanda.
“Baada ya muda kupita huku tukisubiri, tuliitwa sehemu ya mapokezi ambako niliombwa kuzungumza na mtu aliyekuwa anasubiri kwenye ‘line’. Huyo hakuwa mwingine, bali Kamishna wangu ambaye aliniamuru kusitisha zoezi hilo (kazi hiyo) baada ya kupokea maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.”
Waziri Mkuu wa kipindi hicho alikuwa John Malecela.

Nyambele anakumbuka tukio jingine katika mwaka huo wa 1993 kwa kusema aliamuriwa na kiongozi mwandamizi katika Wizara ya Fedha kuacha kufuatilia ulipwaji wa kodi kwenye kiasi kikubwa cha bia aina ya Stella Artois iliyokuwa imeingia nchini.
“Waziri wa Fedha akaamua kwamba waingizaji wangelipa kodi husika kwa awamu (installments); uamuzi ambao ulikuwa kinyume cha sheria.
Kila mzigo mpya ulipofika nchini, kilitoka kibali kipya chenye masharti yale yale hata kama hakuna kodi iliyokwishakulipwa kwa mzigo uliotangulia. 
“Nilipomwambia kiongozi huyo kuwa kufuatilia ulipwaji wa kodi hizo lilikuwa ni jukumu langu, alinitajia jina la mke wa kiongozi serikalini kuwa ndiye alikuwa anahusika na uingizwaji wa bidhaa hiyo. Nilipodadisi zaidi sababu za kunitaka nisitekeleze wajibu wangu, nilifukuzwa ofisini kwake na baada ya muda mfupi nilijikuta nashushwa cheo na kuhamishiwa mkoani Mwanza!”
Ingawa Nyambele hawataji viongozi hao, rekodi zinaonesha kuwa Waziri wa Fedha mwaka huo alikuwa Profesa Kighoma Malima, Waziri Mkuu alikuwa Malecela, na Rais alikuwa Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Anaongeza:
 “Hayo ni ya huko nyuma, lakini ni vielelezo vinavyothibitisha uhusika wa viongozi wa ngazi za juu serikalini na hata kwenye chama tawala katika kushuka kwa maadili ya watumishi wanaohusika na ukusanyaji kodi na wale wa umma kwa ujumla wao.”
Anasema mmomonyoko wa uadilifu katika utendaji kazi ndani ya TRA ulishika kasi baada ya Kamishna Mkuu wa kwanza kuondolewa kwa manufaa ya aliowaita ‘walafi’.

Mwaka 2003 Kamishna Mkuu wa kwanza wa TRA Melkzedeck Sanare aliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Harry Kitillya, ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha.
“Mbegu za mmomonyoko huo zilianza kupandwa baada ya ujio wa Mwenyekiti wa Pili wa Bodi ya Wakurugenzi uliofuatiwa kwa karibu na mabadiliko ya mawaziri katika Wizara ya Fedha. Wote wawili (Mwenyekiti wa Bodi ya TRA na Waziri wa Fedha walianza kukiuka misingi ya kazi iliyokuwa imewekwa na Bodi ya kwanza.
“Misingi hiyo ndiyo ilikuwa nguzo ya ufanisi katika utendaji wa TRA kati ya mwaka 1996 na 2003. Pamoja na kwamba sheria iliyoanzisha TRA ilikuwa inatambua madaraka ya Waziri wa Fedha juu ya Bodi na watendaji wakuu wa TRA, mawaziri wa fedha waliokuwapo wakati TRA inaanzishwa hadi kuanza kufanya kazi waliheshimu mipaka ya kazi iliyokuwa imeainishwa kwa kuwa walikuwa wameidhinisha wenyewe.
“Mwenyekiti wa Bodi aliyeingia madarakani mwaka 1998 alitoka serikalini na alianza kulazimisha Bodi kubadili baadhi ya uamuzi wa Bodi ya kwanza. Alikuja na hoja za usawa wa jinsia na hata ukabila katika ajira bila kujali uwezo – na hilo lilianza kuathiri utendaji katika ukusanyaji mapato ya Serikali.
“Alikiuka baadhi ya taratibu za kiutendaji kwa kushughulika na walipa kodi yeye mwenyewe huku akitoa maelekezo kwa Kamishna Mkuu juu ya viwango vya kodi vya kutoza wafanyabiashara hao.
“Kwa kufanya hivyo alikuwa anakiuka sheria ya TRA ambayo inakataza Bodi kuingilia kazi za ukadiriaji na ukusanyaji kodi.
“Hakuishia hapo. Ilifika wakati akaanza kuongoza timu za wapelelezi wa kodi kufanya doria mchana na usiku ili kukamata bidhaa za magendo au wakwepa kodi. Tuliomuonya juu ya ukiukwaji huo wa sheria ‘tulilipwa’ kama alivyoona inafaa.
“Kwa ujumla, Mwenyekiti huyo alishirikiana na Waziri wa Fedha wa wakati huo katika kukanyaga msingi imara uliokuwa umejengwa na Bodi ya kwanza pamoja na Waziri aliyekuwapo wakati huo. Wote wawili walishirikiana kuweka viongozi waliotaka na ambao wangetii maagizo yao bila kuhoji. Wigo wa fungate hilo la viongozi wapya wa TRA na wale wa wizara liliendelea kupanuka hadi kwenye ngazi za juu za uongozi wa nchi, huku wakiingiza pia viongozi wa idara nyeti kama TAKUKURU (Taasisi ya Kuzuia Rushwa) na Usalama wa Taifa.
“Kutokana hali hiyo, ilifika wakati ambako viongozi wa TRA walifanya wanalotaka wakijua kuwa hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuwauliza; achilia mbali kuwawajibisha. Matunda ya hali hiyo ni pamoja na madudu machache sana yaliyoibuliwa na Serikali mwanzo kabisa wa Awamu hii ya uongozi wa nchi hii,” anasema Nyambele.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa Waziri wa Fedha anayetajwa kwa wakati huo ni Basil Mramba, aliyechukua nafasi hiyo kutoka kwa Daniel Yona. Mwenyekiti wa Bodi ya TRA wa pili alikuwa Dk. Enos Bukuku; ambaye pia kwa wakati huo alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu wa Mambo ya Uchumi.

Taarifa zaidi imechapishwa uk. 12&13 wa gazeti la hili la JAMHURI.

IGP Mangu kukabidhiwa uoenyekiti wa SARPCCO siku za usoni

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu anatarajia kukabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) katika mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Septemba, 2016 jijini Arusha. IGP Mangu atakabidhiwa uenyekiti huo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi ya Msumbiji ambapo atadumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa kamati tendaji za SARPCCO amabazo zitakutana Septemba 14 na 15 mwaka huu ili kuandaa ajenda na mapendekezo ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa wakuu wa Polisi ambao unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano huo mambo mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu yatajadiliwa ikiwemo uhalifu wa kuvuka mipaka, pamoja na kuweka mikakati na maazimio ya kufanya Oparesheni za pamoja zinazojumuisha nchi zinazounda shirikisho hilo.

Vilevile, mkutano huo utajadili kwa kina utekelezaji wa maazimio mbalimbali kupitia kamati tendaji za wakurugenzi wa upelelezi, kamati tendaji ya sheria, kamati tendaji ya mafunzo na kamati tendaji ya mtandao wa Polisi wanawake.

Aidha, suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo litajadiliwa katika mkutano huo.

SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika katika kukabiliana na uhalifu. Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Seychelles.

Imetolewa na:-

Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Rais aliyajua haya...? Msaada uliokataliwa na serikali + Nyumba za Magomeni Kota
TAARIFA KWA UMMA

MHESHIMIWA RAIS AJIONDOE KWENYE HILI LA KUHUJUMU MAMEYA WA UPINZANI.


Ndugu wananchi na wakazi wa *Manispaa ya Kinondoni*, nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuepushia mabalaa na kutujalia Afya njema.Hatuna la kumlipa zaidi ya kusema ahsante.

Leo nimeamua kuita vyombo vya habari ili kuhabarisha uma na watanzania wote kwa dhumuni moja tu, la kuelezea masikitiko yangu dhidi ya Utawala huu wa awamu ya tano, ambapo mimi Mstahiki Meya wa Kinondoni, nalazimika kwa namna moja kufanya nao kazi ya kuhudumia wananchi.

Naleta masikitiko yangu kwenu si kwa lengo la kuchochea hasira za watu bali kuonyesha, gilba, uzandiki, fitina na uchonganishi tunaokutana nao kutoka kwa viongozi wa serikali ya Awamu ya tano.

Ndugu wananchi lazma tuweke rekodi wazi ya kuwa mimi siyo mteuliwa bali mchaguliwa kutoka kwenye kundi kubwa la viongozi mliowachagua October 2015, hivyo mabosi wangu ni nyinyi na pakushtaki ni kwenu yani uma, ili mnitendee sawa na mapenzi yenu mliyonituma kuwaletea maendeo.

1. KWA MASIKITIKO SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, IMEANDIKA BARUA KUKATAA MANISPAA YA KINONDONI TUSIPEWE MSAADA WA MRADI KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKATAKA ZIWE MBOLEA, KUTOKA SERIKALI YA UJERUMANI, UNAOGHARIMU KIASI CHA SHILLINGI BILLIONI 3.2.

Kosa letu kubwa ni msaada kutoka wakati huu ambapo manispaa ya Kinondoni inashikiliwa na wapinzani (UKAWA) na kuonekana kwamba mradi huu ungetujenga binafsi na siyo CCM, kukataa huku ni kwa kuandikia barua wahisani hao kwamba mitambo na vitu vyote wanavyopanga kutuletea, vitozwe kodi, ambayo itagharimu kiasi cha sh millioni 900.

Ikumbukwe mradi huu ni msaada tu na siyo biashara na kwamba baada ya assembly ya mitambo, Wajerumani walikuwa wanaikabidhi manispaa ya Kinondoni ndani ya miezi 6, kitendo hiki siyo tu kutukwaza sisi kama wapinzani, ila kimewakwaza wahisani. Wahisani hao kutoka Ujerumani wamejitolea kutusaidia billioni 3.2, ukiongeza millioni 900, tafsiri yake tunawalazimisha watusaidie billioni 4.1, huo si uungwana hata kidogo.

Nani asiyejua mchakato wa mradi huu ulianza sikunyingi kabla ya wapinzani kuongoza manispaa ya Kinondoni, ila mradi umekuwa hai kipindi cha wa pinzani kwa sababu ya sifa yetu kubwa ya kutokuwa warasimu.

Ndugu wananchi hili limetusikitisha sana hasa kwa serikali hii inayo jipambanua ya kutetea wanyonge na HAPA KAZI TU.

Kushindwa kujua kuwa mradi huu ulikuwa unakuja kufanya mapinduzi makubwa ya hali ya USAFI si Kinondoni tu bali DAR ES SALAAM yote kama jiji..

Jiji letu lingekuwa safi na wananchi wangeondokana na michango ya takataka,sababu mradi huu ulikuwa umelenga kutoa magari ya taka kupita mtaani nakuzikusanya bure.

2. JUU YA UJIO WA MHESHIMIWA RAIS NDANI YA MANISPAA YA KINONDONI.

Nimeona nilitolee ufafanuzi hili suala baada ya kuona napigiwa sana na kutumiwa ujumbe kwa njia ya simu, watu wakitaka kujua ukweli wa mambo juu ya lililotokea siku ya 06-09-2016.

Siku hiyo niliomba Madiwani waliokuwa wana kikao cha kamati ya mipango miji kuja kujumuika nasi ingawa itifaki na mpangilio wa tukio ulikuwa kichama zaidi (Ki-ccm) kuliko kiserikali. Mimi mweneyeji kwenye manispaa yangu wakanikalisha nyuma siti ya tatu kutoka meza kuu, huku viongozi wa CCM kama Mwenyekiti wa Mkoa na wengine wakikaa mbele yangu.

Zaidi ni kwamba ujio huo wa Mheshimiwa Rais sikuwa nimetaarifiwa na taasisi yoyote ya Serikali, kuanzia Ikulu, Mkoa mpaka wilaya, isipokuwa niliona busara kwakuwa maandalizi yaliyoendelea yalifanyikia getini kwangu, si vyema kama muungwana kuacha kwenda kujumuika na Mheshimiwa Rais, isingeleta picha nzuri kwa kiongozi kama mimi.

Pili, kukosekana kwangu kwenye ratiba kusalimia au kuongea na Wananchi wangu wa Kinondoni pia nako kulinifanya nishangae zaidi; iweje mwenyeji nisiwepo kwenye ratiba hiyo huku watu mbalimbali wakipata fursa ya kuzungumza ama kusalimia watu wa Kinondoni.

Tatu, kupangwa kwa mtu maalumu wa kunitukana mimi mbele ya Rais ambaye amekiri kuwa alikutana na mkuu wa mkoa kwanza na kukubaliana kuwa ataongea huku tayari risala kwa niaba ya wahusika ikiwa imeshatolewa.

Nne, upotoshaji mkubwa uliofanywa na waziri Lukuvi; kwamba manispaa ionekane tulitesa wakazi hao na kuwatapeli bila ya msaada wowote, mpaka wao walipo amua kuja kuongea nao.

YOTE HAYA yalionyesha ni
namna gani viongozi hawa walijipanga kumpotosha Mheshimiwa Rais na kutosema kweli kwa dhumuni la kulaghai ama kuchafua taswira ya Manispaaa ya Kinondoni kwakuwa inaongozwa na wapinzani.

Kimsingi Waziri Lukuvi na Mkuu wa Mkoa walikuwa na kila sababu ya kuzuia nisipate japo dakika moja kusema ukweli juu ya mradi ule wa nyumba kongwe magomeni kota. Mradi ule ni sawa na miradi ya wilaya zingine Dar es salaam ambapo Temeke waliokuwa wapangaji waliondoka kwa hiari bila kulipwa chochote wakati Ilala mpaka sasa wapangaji na manispaa wapo mahakamani. Kinondoni pekee ndiyo ilikuwa imewalipa wapangaji wake pesa ya kodi ili kupisha ubomoaji.

Wakati huo wapangaji hao walikaa kwa muda wa miaka 10 bila ya umeme wala maji, baada ya Mahakama kuamuru kuwa yalikuwa ni makazi hatarishi.

Lakini Mheshimiwa Rais si kweli kwamba ardhi ile ilipangwa kuuzwa isipokuwa Mheshimiwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho kikwete alichukua baadhi ya madiwani na kuwapeleka Indonesia ziara ya kiserikali na baadaye wakaenda Romania, huko ndiko walipokuja na mwekezaji anayeitwa Blue Marine kutoka Romania, ambao walikubali kuwajengea wakazi hao 644 nyumba na kuwarudisha kama wapangaji huku wakitengeneza majengo mengine ya biashara, makao makuu mapya ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kuvunja Shule ya msingi pembeni ya magomeni kota ili kuijenga upya; Blue Marine walikwama kungoja saini ya waiziri wa Tamisemi tangu 2014.

Na kama Rais leo akiitisha documents hizo kutoka Tamisemi ataona mapendekeo ya mkataba kati ya manispaa ya Kinondoni na BLUE MARINE. Kusema ardhi ilikuwa imeuzwa ni upotoshwaji mkubwa uliofanywa na waziri Lukuvi huku akijua kuwa yeye akiwa Waziri awamu ya nne,chini ya Rais Kikwete tayari uwekezaji wa magomeni kota likua umesha anza, isipokuwa sheria inatutaka tumpe Waziri ili aweze kuidhinisha.

Waziri Lukuvi kusema kuwa mradi huu ulikuwa ni wa utapeli hatukomoi UKAWA bali tuna mshangaa kwa kumzushia shutuma hizo Rais kikwete, na akitaka kujua ukweli wa mradi hata pale Rais alipo mtuma aje afuatilie swala hilo.

Mheshimiwa Rais nilitaka nipate fursa nikueleze kuwa Mawaziri wote wa Ardhi walisha wahi kutaka kupora eneo hilo. Badala ya kukutana na Halmashauri akaona ni vema apate fursa ya kuitisha hati za Halmashauri na kuzifutilia mbali.

Mheshimiwa Rais kila mtu anaunga mkono juhudi za kuwasaidia wazee au wakazi wale wa nyumba kongwe ila kupotosha umma na kuliko fanywa na Waziri kulikuwa na lengo binafsi la kutaka kunufaika na mradi mpya utakao anzishwa.

Hasara kubwa iliyopatikana baada ya kufutwa hati za eneo hilo ni kwamba serikali za mitaa zimeondolewa maeneo ya uwekezaji ambayo yangesaidia kuimarisha makusanyo ya Halmashauri na kufanya serikali hizi za mitaa ziwe tegemezi baada ya kuporwa vyanzo vyake vya mapato. Baaada ya mwekezaji kujenga na kuwapatia makazi wapangaji wale palikuwa na kituo kikubwa cha uwekezaji kianzishwe.

Lakini si hilo tu; tayari benki ya dunia walikuwa wametoa fedha za kumpatia mkandarasi mshauri (consultant) GUff GMB kutoka ujerumani kiasi cha dola laki nne na themanini kutuandalia michoro ya jengo la utawala kwa ajili kuiwezesha Manispaa miongoni mwa majengo yaliyokuwa yanategemewa kutoka kwenye mradi wa viwanja hivyo vilivyo chukuliwa.

Mheshimiwa Rais nimalizie kuwa, ningepata walau dakika tatu ningekueleza jinsi Waziri wako Lukuvi alivyo hatari san, na Manispaa ya Kinondoni mpaka leo inaonja machungu yake aliyotusababishia kukosa kiasi cha shillingi zaidi billioni ya 12, ningekufafanulia na kukuomba utumie vyanzo vyako vya usalama kudhibitisha.

Nishukuru kuwa hata walichopanga pia kukifanikisha uliruka kiunzi baada ya kusema wakujenga bado haujaamua, tofauti ya Waziri Lukuvi kujiandaa na watu wake kupokea eneo hilo, imani yangu hata kama tumeporwa bado lipo salama sana, kuliko ungemkabidhi yeye ndiye achukue ardhi hiyo ili ekari mbili ajenge flats za hao 644, zingine wajanja wa mjini watumie kwa mambo yao.

Mwisho nataka kumwambia Mheshimiwa Rais ya kuwa Wabunge, Madiwani na Mameya tunakuja kwenye ziara zako tukijua ni ujio wa kiserikali, lakini kama kiongozi Mkuu wa nchi tunataka uwaonye viongozi wako waache kufanya ziara zako kuwa za kichama kuliko serikali.

Mheshimiwa Rais usishangae Ikafika muda usituone katika ziara zako zingine kama baadhi ya viongozi wa serikali kutaka kuchanganya uccm na ziara ya kiserikali; au kuona mtu kama mkuu wa Mkoa akiongea vijembe kuwa eti ni "mbabe wa vita"..ubabe dhidi ya nani? Na ni vita ipi? matusi yale mbele yako tafsiri itakuja kuwa unawatuma au kuwapanga mapema kutoa matusi na mipasho, sisi mameya tutaendelea kuwa ni waungwana.

Sisi Mameya wa upinzani tumefikia mwisho, Wabunge na Madiwani kwenye ziara zako, tukiona hatutambuliwi kama Viongozi wa Wananchi tuliochaguliwa,na wanachi badala yake nikuona fedheha za kuita makada wa CCM watutukane.

Yaani tulienda mbele za wananchi na kuwaomba kura kwa unyenye kevu, kama akitaka kuonyesha ubabe basi aje agombee kata ya ubungo.

"Tumepitia jando la kisiasa". Akiendelea kuwa kiongozi kwa kuteuliwa kamwe asijiongopee ni mbabe, atakuwa anajilisha upepo. Na hayo yote yanayoendelea kama yasipokemewa mapema ni wazi utakuwa unashiriki na wakuu wa mikoa na ma DC Kuhujumu upinzani.

Afia kisimani alimoingia kumwokoa mbuzi kwa ujira wa sh elfu sita

MKAZI wa Kijiji cha Kazibizyo Kata ya Ng’anzo, Wilayani Bukombe, Sebastian Lumbe (36), amefariki dunia kisimani alimoingia kumuokoa mbuzi kwa ujira wa Sh 6,000.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Misheni baada ya mbuzi huyo kutumbukia kwenye kisima kinachodaiwa kuwa na urefu wa futi 30.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Misheni, Antony Kuya alithibitisha kutokea tukio hilo.

Alisema baada ya mbuzi huyo kutumbukia kisimani, mmiliki wake, Marco Sylvester alitangaza ujira wa Sh 6,000 kwa mtu ambaye angefanikiwa kumtoa na ndipo Lumbe alipojitolea kuingia kisimani humo.

Alisema kabla ya Lumbe kuingia kisimani humo na kukutwa na mauti, walijitokeza watu wawili tofauti lakini kila walipoingia waligundua kisima hicho kilikuwa kirefu.

Kwa sababu hiyo walighairi hadi alipofika yeye na kujitosa.
“Baada ya kuingia kisimani alianza kupiga kelele za kuomba msaada.
“Watu waliokuwa karibu na kisima hicho walimtupia kamba lakini wakati anajaribu kuivuta kupanda ilikatika na akaanguka kurudi kisimani.
“Baadaye kijana mmoja, Leonard Mathayo aliingia kujaribu kumuokoa lakini wakati akiwa humo ndani alisema baada ya kukaribia kufika mwisho wa shimo alimkuta akitupa miguu.
“Alipoanza kumfunga kamba ili wamvute aliishiwa nguvu na kukosa hewa na hivyo ilimlazimu kuomba msaada kutoka nje,” alisema Kuya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo aliwaonya wananchi kuwa waangalifu na visima virefu kama hivyo kwa sababu ni hatari.

Article by P. Msekwa - Revisiting recommendations by the LRC on dual citizenship in Tanzania


THE ISSUE OF DUAL CITIZENSHIP IN TANZANIA : Revisiting recommendations by the Law Reform Commission


THE Daily News of Thursday, August 25, 2016; carried a news item concerning the official opening by the Zanzibar President, Dr Ali Mohamed Shein, of the annual meeting of members of the Tanzania Diaspora, which was being held in Zanzibar at the material time.

It was reported that “members of the Tanzania Diaspora reiterated their commitment of being good ambassadors abroad, including promoting investment opportunities, and working closely with the Government in changing the lives of their compatriots back home”.

It was further reported that several topics were scheduled for discussion, including the issue of dual citizenship, as well as the matter of giving Diaspora members the right to vote during general elections.

I am particularly interested in the issue of dual citizenship, for one specific reason; which is that I was still a member of the Law Reform Commission of Tanzania (LRCT), when that Commission made a thorough and extensive study of this matter in 2004, and submitted its recommendation to the Union Government on 12th May 2006, recommending its adoption.

But to date, no decision seems to have been taken on those recommendations.

That is the reason why, in this article, I am revisiting the findings of that study, plus the recommendations arising there from, for the benefit of our readers who may have a vested interest in this particular matter including, obviously, the Diaspora members themselves.

Furthermore, this revisit becomes even more relevant, in view of the Government statements which were made at the Diaspora forum both by President Shein, and the Minister for Foreign Affairs, Dr Augustine Mahiga.

The statements made on behalf of the Government. The Daily News reported as follows: “The issue of dual citizenship and the right to vote during general elections were some of the key questions discussed at the Diaspora forum.

But the Government Authorities asked members of the Diaspora to be patient, pointing out that both dual citizenship and the Diaspora’s right to vote at general elections are sensitive issues which are linked to the country’s Constitution.

We should avoid rushing into making decisions on them, to allow sufficient time for constructive discussions to take place, said both President Shein and Foreign Minister Dr Mahiga”.

Thus, in view of the ten years which have elapsed since the Law Reform Commission submitted its well considered recommendations to the Government, it is absolutely puzzling that the Government should be asking to be allowed “sufficient time for constructive discussions to take place”.

The big question is: are the ten years which have elapsed since the Government received the Law Commission recommendations on this matter, not enough time for that purpose? The Law Reform Commission’s study on dual citizenship.

In accordance with its mandate, which is “to take and keep under review all the laws of Tanzania for the purpose of their development and reform”; the Law Reform Commission of Tanzania undertook a comprehensive study on the project of the introduction of dual citizenship in Tanzania, within the framework of the citizenship law of the country.

This project commenced in June 2004, aimed at examining the current trend, at that time, in the development of the citizen laws of certain other countries which were changing their citizenship laws to accommodate dual citizenship; in order to see whether there was sufficient justification for updating the citizenship law of Tanzania in line with what was happening elsewhere in the world.

The decision to undertake this project was substantially prompted by the publication of a Report of the World Commission on the Social dimension of Globalisation, which was launched in March, 2004.

One of its recommendations strongly urged the adoption of dual citizenship by countries of the South, as one of the ways through which the nations of the South could equitably share the benefits of globalisation.

But it was also given additional credence by the widely expressed desire of many Tanzanians, both within and outside the country, that it was high time for Tanzania to seriously consider the adoption of the dual citizenship regime, as a way of minimizing the effects of the loss of highly skilled human resources resulting from the large number of highly qualified Tanzanians migrating to other countries of the world in search of greener pastures.

The scope of the study. The Commission’s study examined all possible factors in order to determine whether or not to adopt the dual citizenship regime.

The Commission made a thorough review of the current citizenship law, the immigration law, as well as other legislation which impacts on citizenship and related matters, such as the Constitution of the United Republic of Tanzania, the National Security Act, the Extradition Act, the Mutual Assistance in Criminal Matters Act, and the Prevention of Terrorism Act.

The study also examined the concept itself of dual citizenship, by making a comparative study of the citizenship laws of a number of African countries which have already adopted that regime, with a view to ascertaining the reasons and circumstances which led them to adopt the dual citizenship regime; plus the achievements and/or problems which have been encountered by those countries in operating the said regime.

The countries covered in this study include countries which have already adopted the dual citizenship legal regime, and those which, at that material time, were still actively considering the matter.

The countries studied were: Ghana, South Africa, Ethiopia, Mauritius, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Benin, Chad, Equatorial Guinea, Togo, Cote d’Ivoire, and India. Furthermore, because citizenship is a Union matter under our Constitution, the study covered both Tanzania Mainland and Tanzania Zanzibar.

The Commission’s Research findings. In the process of gathering the views and opinions of stakeholders, the Commission visited a total of seven regions in Tanzania Mainland, and two Regions in Zanzibar.

The Regions visited were Arusha, Mara, Mwanza, Tabora, Ruvuma, Iringa, Dar es Salaam, Unguja Central and Unguja South.

The key stakeholders who contributed their views at public as well as at private hearings included members of the general public, politicians, and members of the academia especially lawyers through their professional associations.

In giving their views, some of the stakeholders supported the introduction of dual citizenship without any reservations, but the majority suggested that its introduction should be subjected to certain specified restrictions.

For example, it was suggested that dual citizenship should be accorded only to Tanzanians who are citizens by birth, and not to those citizens belonging to other categories.

They contended that most Tanzanian citizens who acquired foreign citizenship did so primarily because it was necessitated by the need to improve their economic well being by working in the relevant foreign countries, while their allegiance to Tanzania remained intact.

They should therefore be allowed to retain the citizenship of origin. With regard to restrictions which should be imposed, it was suggested that Tanzanians with dual citizenship should not be allowed to participate actively in politics, or to hold high positions in Government.

Those who advanced this point of view suggested further that we should adopt the Indian model of dual citizenship, where such citizenship was granted only to persons who were described as “overseas citizens of India”, which meant persons of Indian origin who had acquired citizenship of another country.

The relevant Indian law provided that an overseas citizen of India is not entitled to the rights conferred upon ordinary citizens of India, and therefore had no right to equality of opportunity in matters of public employment, had no voting rights, and were not eligible to become members of the Indian Parliament.

But the Commission’s study identified many others who were totally against the introduction of dual citizenship, arguing that it would provide opportunities for bad people to endanger the security of the state by causing social and political conflicts of one kind or another.

In relation to this perceived danger, our Commission took note of the debates which took place in the South African Parliament in 1995, when that House was giving consideration to the Bill for the enactment of the South African Citizenship Act, 1995.

Historically, South Africa has always accepted the principle and practice of dual citizenship. Hence, in the debate on the above mentioned Bill (where this principle was apparently challenged), the Minister for Home Affairs, Dr Buthelezi, said the following: “The Government is appreciative of the fact that there are strong arguments against the principle of citizenship, which are based on considerations of the loyalty of such persons with dual citizenship.

However, the Government has no intention of legislating against dual citizenship. I am certain that the majority of South African citizens who also hold the citizenship of another country are as loyal and as respectful to the Republic of South Africa and its Constitution as our own citizens who hold no other citizenship. Consequently, this Bill contains no proposals that deviate from the present legal tolerance of dual citizenship”.

The Commission’s recommendations. The opening sentence of the Recommendations section of the Commission’s Report reads as follows: “The Commission has deliberated on the issue of dual citizenship by analysing both the advantages and disadvantages of this regime, and has come to the conclusion that the demand for dual citizenship deserves to be considered in a positive and forward-looking spirit . . .

The Commission is of the view that the current legal regime, which deprives certain Tanzanians of their citizenship, simply because they have acquired some foreign citizenship, is no longer beneficial to the country, for it is actually a loss of the country’s significant human resources”. Thereafter, the Commission makes the following recommendations:-

(i) That in the event that the dual citizenship legal regime is accepted, it should initially be applied to those Tanzanians who have lost their Tanzanian citizenship because of acquiring some foreign citizenship, by restoring to them their lost Tanzanian citizenship. Such restoration should be made on application by the concerned individuals, and considered on a case-by-case basis. The applicants should not be accepted in a rush and without thorough screening.

(ii) That there should be no automatic conferment of dual citizenship. It should rather be done by following appropriate procedures of application and consideration, which will be laid down in the relevant legislation, and the rules made under it.

(iii) With regard to the concerns that dual citizenship should not be allowed to participate actively in politics or to hold high positions in Government, the Commission was of the view that since the Union Parliament is empowered, under sub-article

(2) of article 5 of the Constitution of the Union Republic, to enact legislation imposing restrictions on a citizen from exercising the right to vote by reason of, among others, being a citizen of another state, this Constitutional provision can be used to achieve that particular objective.

The relevant law stipulates clearly that after receipt of the relevant Law Reform Commission Report by the Minister, he is expected to do the following: (a) to present the said Report to Parliament by laying it on the Table of the House, and (b) (unless, of course, the Government is unwilling to implement the recommendations of that Report), to prepare the necessary Bills to be submitted to Parliament for their enactment into law.

But, alas, as has been the case with many other Law Reform Commission recommendations, there has been no submission of the dual citizenship Report to Parliament; not even by taking the initial step of laying it on the Table of the House, in order to make it accessible to the general public!

Contacts: cell 0754767576. E-mail [email protected]

Government has cut spending, this adversely impacted our business - Nissan Tanzania

Dar es Salaam — Vehicle imports through the Dar es Salaam Port dropped by 10.8 per cent in the seven months of this year compared with a similar period in 2015.

Tanzania Revenue Authority (TRA) figures show 53,275 vehicles were imported through the port, down from 59,694 the similar period in 2015.
"We cannot give the exact reason for the decline," noted the TRA director for taxpayers services and education, Mr Richard Kayombo.
Mr Kayombo said the drop had nothing to do with the economy.

However, motor dealers have linked the fall to government cost-cutting measures as well as increases in import duty rates. "The government has cut spending including that on buying new vehicles. So, this has adversely impacted our business," said Nissan Tanzania commercial manager Ash Ramraj.
"Nissan accounts for 11.6 per cent of the market share and is committed to operating in Tanzania," he said.
It focuses selling more pick-up models, which are suitable for Tanzania, which will implement more infrastructure projects during the industrialisation process.

A showroom attendant said importers were discouraged by high import duty.
"The new excise tax law puts the charge on imported vehicles at Sh6.4 million and Sh6.7 million for some models --a departure from the previous duty of Sh3.4 million," he noted.
According to him, high taxes have raised the cost of importing vehicles significantly, with prices of some models going up by more than Sh3 million.

He cited an example of the Toyota Noah brand whose price jumped from Sh12 million last year to Sh15 million this year.

The situation has reduced demand, according to him.
"Business is bad as customers are not ready to buy big cars due to increased prices. They opt for small ones because they can afford."
Bad business

Conti-Car sales showroom salesman George Ochola said:
"If you look at what people are currently purchasing, you will realise that they are buying cars that were imported prior to the new tax was imposed on imports. So bad is the business that there is no reason of importing more of them because we have enough stock. Sales are sluggish."
He also attributed the decline in vehicle imports to efforts by the fifth phase government to deal with tax evaders.

Before President John Magufuli came to power, some vehicles were brought into the country illegally. This is no longer the case now.

He also said since the money circulation was low and the government had cut costs, owning cars did not figure high on the list of priorities of many Tanzanians.
"Vehicle sales have dropped terribly, from 50 units we sold last year," noted Mr Ochola.
He also said sales had fallen partly due to the increased competition.

Tanzania Freight Forwarders Association vice president Edward Urio attributed the drop in imports to the imposition of value-added tax (VAT) on goods in transit.
"VAT has scared away importers. They have opted to use other ports such as Mombasa, Beira and Durban in the region whose charges are relatively cheap," he said.
"The majority of Congolese and Zambian importers have opted to use other ports such as Mombasa and Durban after the introduction of a single customs territory."

To the DRC government, the single customs territory was an added advantage as it takes full advantage of tax collection but for traders it translates to profit loss and thus opting for other ports in the region, according to him.

Dar port authorities were quoted by a section of the local media as saying that Congo vehicle imports through the port had fallen by a half to 1,247 vehicles in the first two months of this year compared with a similar period last year.

Zambia's vehicle imports through the port decreased to 2,692 between January and February 2016 from 6,042 during a similar period last year.

According to Prof Samuel Wangwe of Repoa, if the drop is huge on consumer vehicles this is good for economy as it is more economical to use public transport as an alternative. But it is bad if the case is for productive vehicles.

He suggests that people be encouraged to import more productive vehicles to boost the country's economy.
  • via The Citizen

Two Private Universities sent warning letter for asking fees paid in forex

Two institutions of higher learning in the country, namely the Kampala International University (KIU) and the International Medical and Technological University (IMTU), had been slapped with warning letters for forcing local students to pay fees in foreign currency.

Deputy Minister for Education, Science and Technology, Engineer Stella Manyanya, informed the House here that the two institutions were warned after they were found to be charging Tanzanian students in United States dollars.

Eng Manyanya made the explanation in response to a basic question by Tumbatu MP, Mr Juma Othman Hija (CCM), who had complained over the tendency by some universities to charge fees in foreign currency, demanding to know whether the government had taken any action

. The deputy minister explained, however, that the varsities are allowed to make foreign students to make payments on foreign currencies, warning that the government will not hesitate to take actions against institutions forcing locals to pay in dollars and other currencies.

Section 48 (1) of the Universities General Regulations of 2013, according to the minister, prohibits the varsities from the practice while Section 48 (2) allows the institutions of higher learning to demand foreign students to make payments in other currencies.

She warned that any institution failing to abide to the regulations will face legal actions including warnings, suspension from operation and an order to stop them from admitting students.

Meanwhile, the government maintained yesterday that recruitment of employees at institutions such as the Tanzania Commission for Universities (TCU) and the National Council for Technical Education (NACTE) is based on qualification rather than where the employees come from.

Eng Manyanya made the explanation when responding to Uzini MP, Mr Salim Rehani, who had wanted to know how many Zanzibaris are employed at the two institutions.

The deputy minister pointed out that the recruitment of employees is based on competency, staff regulations and scheme of services, noting that all Tanzanians had the opportunity to get employed as long as they meet the criteria.
  • via DAILY NEWS

Chief Secretary: Malawi will never, and has never, at any time, acquiesced to Tanzania’s unwarranted and unjustified territorial claims

George Mkondiwa
Malawi government has informed all controlling officers to be on alert following a “propaganda” by the government of Tanzania to promote a new map showing that the east African country owns part of the Lake Malawi.

Chief Secretary George Mkondiwa has advised the officials to disregard the “half truth”s by Tanzania by rejecting use of any document bearing such misinformation.

The newly published map, which shows the boundaries of the country’s newly created regions, has reignited the ongoing dispute over the boundaries on Lake Malawi, which is potentially rich in oil and gas.

Malawi has since claimed that its boundaries with Tanzania have never changed and are as designated by colonialists the Anglo-Heligoland Treaty.

Government has also insisted that it has never accepted claims that Tanzania owns part of the lake.
“Malawi will never, and has never, at any time, acquiesced to Tanzania’s unwarranted and unjustified territorial claims,” Mkondiwa said.
Mkondiwa added:“Malawi government would like to call upon all officials in government ministries, departments, and agencies to be alert on this matter and to continue rejecting and refusing to use all such maps appearing in any form or media including calendars, diaries, official documentation or other documents for any purpose or business.”

Tanzania claimed it released the maps because new regions and districts had been created and it was therefore necessary to show the boundaries.


Malawi disputes Tanzania’s claim to half the lake – Africa’s third biggest.

It has accused Tanzania of raising tension by allegedly intimidating Malawian fishermen on the lake.

Malawi awarded oil exploration licences to foreign companies to search for oil in the lake, which Tanzania calls Lake Nyasa.

AfCHPR yapata Rais mpya baada ya jaji Augustino Ramadhani kung'atuka

Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR) imepata Rais mpya, Jaji Sylivian Ore kutoka Ivory Coast, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani aliyeitumikia Mahakama hiyo kwa miaka sita.

Katika kikao cha 42 kilichofanyika Arusha, majaji wanne walistaafu utumishi wao baada ya kuitumikia mahakama hiyo kwa miaka sita kila mmoja. Majaji hao ni Fatsah Ouguergouz (Algeria), Duncan Tambala (Malawi), Elsie Thompson (Nigeria) na Ramadhani.

Kikao hicho pia kiliwaapisha majaji wawili, Ntyan Ondo Mengue kutoka Cameroon na MarieTherese Mukamulisa wa Rwanda, waliochaguliwa kwenye mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Julai 13 hadi 15 mwaka huu, nchini Rwanda.

Mahakama hiyo inaundwa na majaji 11 ambao huchaguliwa kutoka katika kanda tano za Bara la Afrika, ambazo ni Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi na Kati na kwa sasa kuna nafasi mbili zilizobaki wazi ambazo zitajazwa Januari 2017 na majaji kutoka Kaskazini mwa Afrika.

Serikali haijashindwa kuongoza nchi - WM Majaliwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo macho, haijalala na haijashindwa kuongoza nchi bali imejipanga kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa.
"Serikali haijashindwa kuongoza nchi. Nataka niwahakikishie waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kwamba tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa na kazi hiyo imeanza kwa marekebisho makubwa kwa maeneo ambayo tunadhani yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa,” amesema.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, ambaye alitaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kunusuru mdororo wa uchumi uliopo nchini.

Bw. Mbowe alidai kwamba hali ya uchumi imeshuka na kwa mujibu wa taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) uagizaji wa bidhaa kutoka nje umepungua, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na sekta ya ujenzi imesimama hali inayoashiria kudorora kwa uchumi.

Kuhusu suala la kupungua kwa mizigo katika bandari na vituo vya forodha, Waziri Mkuu amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bahari umeshuka duniani kote kwa sababu ya kushuka kwa hali ya uchumi kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta na gesi.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema tayari wafanyabiashara wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameihakikishia Serikali kwamba mizigo yao yote itakuwa inapitia Bandari ya Dar es Salaam hasa kwa mkakati wa pamoja wa ujenzi wa reli ya standard gauge inayoanzia Dar es Salaam - Tabora - Isaka.

Wakati huo huo
Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuimarisha amani na ulinzi kwenye maeneo yote nchini na kwamba vyombo vya dola viko macho.
“Watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji watakamatwa popote walipo na kuchukuliwa hatua za kisheria,; amesema.
Amesema hatua hiyo inatokana na matukio ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni ambapo raia wasiokuwa na hatia na askari waliuawa katika maeneo ya Vikindu mkoani Pwani, Tanga na Mwanza. Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani

Katika swali lake, Bw. Ngonyani alitaka kujua ya Serikali kuhusu kukomesha mauaji hayo, yanayotokea kwa watu wasio na hatia pamoja na askari, ambapo Waziri Mkuu, alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi na familia, ambazo ndugu zao walipoteza maisha katika mauaji hayo.

Pia ametoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha wanawafichua watu ambao wanawatilia shaka na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili waweze kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, SEPTEMBA 8, 2016

Mkutano wa 17 wa dharura wa wakuu wa EAC Ikulu, Dar es Salaam, leo


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya Bw. Liberat Mfumukeko muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Sudan ya Kusini muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wa Burundi Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Nyamitwe muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016

Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akibadilishana mawili matatu na Rais Paul Kagame wa Rwanda muda mfupi kabla kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Rais Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Rutto akiwasili kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa dharula wa wakuu wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 8, 2016.

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Agosti 2016

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu fahirisi za bei za taifa kwa mwezi Agosti, 2016. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipindi cha mwezi Agosti Umepungua kwa asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 katika kipindi cha mwezi Julai 2016.

Hiyo inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioisha mwezi Agosti, 2016 imepunguwa ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Julaai 2016.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa NBS, Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Nchi zote za Afrika Mashariki kasi ya mfumuko wa bei imepuguwa katika kipindi cha mwezi Agost mwaka huu.

Alisema baadhi ya nchi hizio ni Kenya Mfumuko wa bei umepunguwa kwa asilimia 6.26 kutoka asilimia 6.36 katika kipindi cha mwezi Julai na Uganda bei imepunguwa kwa asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.1 kwa mei Julai Mwaka huu.

"Kupungua kwa mfumuko huo nhini kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali ya nchi," alisema Kwesigabo.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa z vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za Samaki kwa asilimia 701, Mafuta ya kupikia kwa asilimia 7.02 na mbogamboga kwa ailimia 6.9.

Pia bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupunga ni pamoja bei za Gesi kwa asilimia 22.8, Mafuta ya taa kwa asiimia 8.8, dezeli asilimia 9.8 na Petroli asilimia 15.8.

Aidha Fahilisi za bei ambacho hutumika kupima mabadiliko ya bei za huduma mbalimbali zimepungua kwa asilimia 103.28 kwa mwezi Agosti mwaka huu kutoka 103.50 katika kipindi cha mwez Agosti mwaka 2015.

Alisema kupungua kwa fahilisi za bei umechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula ambazo ni nafaka kwa asilimia 0.6, Unga wa muhogo asilimia 2.1, dagaa kwa asilimia 3 na mbogamboga asilimia 2.6.

Hata hivyo alisema thamani ya shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia sh.96 na senti 83 katika mwezi Agosti mwaka huu kutoka desemba 2015 ilivyokuwa sh.96 na sent 62 kwa mwezi Julai mwaka huu.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi umepunguwa kutoka asilimia 7.6 kwa mwezi Julai hadi kufikia asilimia 7 kwa Agosti mwaka huu.

  • Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062Tanzania inflation slows to 4.9 pct yr/yr in August


DAR ES SALAAM, Sept 8 (Reuters) - Tanzanian inflation edged down in August after food and fuel prices rose more slowly, the statistics office said on Thursday.

The state-run National Bureau of Statistics said inflation fell to 4.9 percent year-on-year last month from 5.1 percent in July. Month on month, the headline inflation rate was 0.2 percent in August.

Food and fuel prices are key drivers of inflation in east Africa's second-biggest economy.

"This is the first time this year that the annual headline inflation rate has decreased below 5 percent, which is the government's mid-term target for the inflation rate," Ephraim Kwesigabo, a director at National Bureau of Statistics, told a news conference.

The inflation rate for food and non-alcoholic beverages decreased to 7.0 percent from 7.6 percent in July, he said.

Tanzania changed the formula for calculating its annual headline inflation rate in February by reducing the weight of food in the basket of goods it uses. (Reporting by Fumbuka Ng'wanakilala; Editing by George Obulutsa and Toby Chopra)

Kauli ya Sirro kuhusu taarifa za kukamatwa watu kwenye nyumba za wageni

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani kupuuza taarifa za sauti zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni.
Taarifa hizo za uvumi zinazoendelea kuzagaa kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

Kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), mjambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.

Niwajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo, kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa. Sheria ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77 iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo. 

Sambamba na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu, kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale watakapomtilia mashaka mteja yeyete watoe taarifa kituo chochote cha polisi. 

Pia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la Dar Es salaam.

DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU

S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM