Urembo wa "kumaliza darasa la saba"

Wahitimu wa darasa la saba wakisoma risala kwa mgeni rasmi wa maafali ya 48 ya Shule ya Msingi Litisha wameiomba Serikali kuwasaidia upatikanaji wa maji shuleni hapo ili waepukane na adha ya kutafuta maji umbali mrefu.

Kivutio cha utalii mkoani Ruvuma: Jiwe la Mbuji


JIWE la Mbuji lililopo wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, ni miongoni mwa vivutio adimu na vya kipekee vilivyopo katika Bonde la Ziwa Nyasa ambalo linajumuisha mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Njombe.

Tayari Wizara ya Maliasili na Utalii imeliingiza Jiwe la Mbuji kwenye orodha ya vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Ruvuma ili hatimaye kazi ya kutangaza eneo hilo na vivutio vingine, iweze kufanyika kwa tija.

Neno Mbuji lina maana ya Kitu Kikubwa. Hivyo pengine, jiwe hilo kuitwa Mbuji, ilitokana na ukubwa wake usiokuwa wa kawaida. Jiwe hili lipo katika Kijiji cha Mbuji, Kata ya Mbuji. Kwa sasa limekuwa kivutio kwa wageni wa ndani na nje wanafika kutembelea wilaya ya Mbiga kwa shughuli zao mbalimbali, zikiwemo za kitalii.

Moja ya maajabu ya jiwe hili, ni ukubwa wake likilinganishwa na mawe yote yanayopatikana katika mkoa wa Ruvuma. Chini ya jiwe hili kuna vyanzo vingi vya maji. Ni vigumu kwa mtu yeyote kulipanda bila kwanza kuwaona wazee wa kimila wa eneo hili. Yeyote anayethubutu kulipanda bila kuwaona wazee hao, yanayomkuta anajua mwenyewe, lakini ukweli ni kwamba ni tayari juu yake. Ni vigumu kulizunguka jiwe hilo bila kufuata mila na desturi za Kabila la Wamatengo wanaoishi eneo hilo.

Kwa jamii ya Wamatengo, jiwe hili linaheshimika sana. Sehemu kubwa ya wananchi wanaoishi kuzunguka eneo lilipo jiwe hili hawajawahi kulipanda wala kulisogelea katika maisha yao yote kwa hofu ya kupoteza maisha.

Sixmund Ndunguru (90), ni mmoja wa wazee wa kimila wa Kabila la Wamatengo. Katika mazungumzo yake na FikraPevu anasema pamoja na mambo mengine kwamba ili kuweza kupanda jiwe hili, ni lazima mtu awe na mzee wa kimila wa kumwongoza, anayezifahamu vizuri mila na tamaduni za kabila hilo.

“Ninayafahamu maajabu ya jiwe la Mbuji tangu nikiwa na umri mdogo. Mandhari ya jiwe hili hayajabadilika wala kuharibiwa tangu nilipoanza kulifahamu,” Mzee Ndunguru anaanza masimulizi yake juu ya jiwe hili.

Anaendelea: “Mimea hii aina ya matete inayozunguka jiwe hili imekuwepo miaka mingi sana. Kwa mara ya kwanza, mimi mwenyewe nilipanda juu ya jiwe hili miaka ya 1940 nikiwa na baba yangu mzazi…kwa hiyo, mtu yeyote anaruhusiwa kupanda jiwe hili ilimradi azingatie maelekezo ya wazee wa kimila.”

Kwa kawaida, Wamatengo wanaamini kwamba katika jiwe hili lina viumbe vinavyoitwa Ibuuta ambavyo ni mfano wa binadamu. Viumbe hivyo vinaelezwa kuwa vifupi mno na vya ajabu. Inadaiwa kwamba wakati mwingine inapofika usiku viumbe hivyo huweza kuonekana. Hata hivyo, inaelezwa kwamba viumbe hivyo vifupi vinapatikana pia katika mataifa kadhaa duniani, lakini vikifahamika kwa majina tofauti.

Maliwato ya wanafunzi wilayani Namtumbo

Mkuu was Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge akikagua choo kinachotumiwa na wanafunzi was while ya msingi Sasawala wilaya ya Namtumbo. Choo hiki kimemsikitisha mkuu HuYo kwani kimejegwa kwa nyasi na ni kichafu ambapo zaidi ya wanafunzi 400 wanatumia. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma)

Malawi court jails Tanzanian to 10 years for child trafficking

The Chitipa magistrate court has sentenced a Tanzanian woman to 10 years imprisonment with hard labour for trafficking four children to her country -- reports NyasaTimes.

Her Malawian masterminder Daniel Simfukwe has been jailed for seven years on the offence.

Police prosecutor Reynard Chabwera told the court that Piri Mwamphasi, the convicted Tanzanian child trafficker even camped in a village in Chitipa looking for the children whom she wanted to work in farms in Tanzania.

Chabwera said Simfukwe is the one who was running around getting the children for Mwamphasi.

Over 70 children are yet to be brought back to Malawi after they were rescued in South Africa a few months ago.

Ikulu yahadharisha kuhusu barua ya kutapeli watu kwa kuwachangisha fedha

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuwatahadharisha kuwa kuna watu wametumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua kwa Kampuni Binafsi na Wakurugenzi Watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi 23/09/2016"

Mnataarifiwa kuwa barua hizo zilizotiwa saini na muhuri wa kughushi na ambazo hata maelezo yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa utapeli.

Yeyote aliyepokea barua hizo azipuuze na achukue hatua mara moja kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.

Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuueleza umma kuwa uendelee kupokea taarifa sahihi zinazotolewa kupitia vyombo vya habari na pale ambapo kuna mashaka juu ya taarifa zenye nembo ya Ikulu wasisite kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu zilizotajwa katika anuani ya mawasiliano hapo juu.

Tafadhari atakayepata ujumbe huu umtaarifu na mwenzake.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Septemba, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN Septemba 17, 2016


Kujitoa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii - Mambo 10 muhimu kuyaelewa

Kujitoa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ni sawa na Mkulima kula Mbegu

 • Mambo 10 muhimu kuyaelewa kuhusu Hifadhi ya Jamii
Upo mjadala unaoendelea na kufukuta kuhusu uamuzi wa Serikali kupeleka Muswada wa Sheria Bungeni kufanya marekebisho katika Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Muswada huo sijauona na haujawekwa hadharani. Hata hivyo, lililopenyezeka katika vyombo vya habari ni taarifa ya azma hiyo ya Serikali iliyotamkwa katika kikao cha Serikali na wadau kuwa Muswada huo utafuta FAO LA KUJITOA.

Nimefuatilia mjadala huo na kuisoma barua ya wazi ya vyama vya wafanyakazi kwa umma ikilaani vikali nia hiyo ya Serikali na muswada. Nikasikia na kusoma tena kauli mbalimbali za Serikali na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuhusu azma hiyo na mambo mengine mengi yanayoambatana na muswada unaondaliwa. Kwa maelezo hayo, muswada huo una mambo mengi zaidi ya kinachoitwa fao la kujitoa. Aidha, maelezo yao ni kuwa muswada wenyewe haujakamilika isipokuwa ni hatua ya maoni tu.

Ninachokiona kwa haraka haraka ni kuwepo kwa ombwe la taarifa katika suala hili jambo linalofanya mjadala wenyewe kwenda harijojo. Ombwe hili litafanya hata muswada wenyewe ukitolewa tushindwe kuujadili vizuri na kwa nafasi. Kwa sababu hiyo, nimejitolea kuchokoza mjadala kwa kuyaweka bayana mambo 10 ya msingi ya kuyaelewa kuhusu hifadhi ya jamii kama ninavyoyainisha hapa chini.
 1. Ipo tofauti kati ya dhana mbili 'AKIBA YA WAFANYAKAZI' na 'HIFADHI YA JAMII' yaani Provident Scheme na Social Security. Provident Scheme inakupa tu jumla ya fedha wewe na mwajiri mliyochangia siku ya kustaafu na mnaachana kimoja. Social Security inahusisha mnyumbuliko wa mafao ikiwemo malipo ya kila mwezi baada ya kustaafu, matibabu kwa mtu na mwenza, gharama za maziko na malipo kwa mjane na kusomeshewa watoto. Kutokana na uchanga wa mifuko hii, mafao bado yanatofautiana kati ya mfuko na mfuko hatimaye mbeleni mafao yanapaswa kufanana katika mifuko yote.

 2. Hifadhi ya Jamii ni Haki ya Kikatiba na si suala la hiyari. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa kila mtu anahaki ya kupata hifadhi. Aidha Hifadhi ni Haki ya Binadamu katika Tamko la Haki za Binadamu na Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani. Haki hiyo inaambatana na wajibu kwa Serikali, Mwajiri na Mfanyakazi. Serikali kusimamia na kuhakikisha Haki hiyo inatolewa na kupatikana, Mwajiri kumchangia Mfanyakazi na Mfanyakazi kuchangia kwa mujibu wa Sheria.

 3. Hakuna kitu kinachoitwa FAO LA KUJITOA kulikuwepo na KUJITOA KWENYE MAFAO. Kwa kuwa mifuko iliyopo iliundwa kwa sheria tofauti kwa nyakati tofauti, baadhi ya mifuko ilikuwa bubu kuhusu kipengele cha kukataza kujitoa hali iliyofanya watu kujitoa bila kukataliwa. Hivyo hakuna FAO LA KUJITOA lililofutwa na hakuna Mfuko wowote wenye fao hilo. Kilichofanyika ni kuoanisha Sheria mbali mbali za Mfuko na kuwa na Sheria moja kurahisisha udhibiti na usimamizi ambapo katika Sheria hiyo ya 2012 imetamka bayana kutokuwepo na kujitoa kuziba ombwe lililoachwa na sheria mbalimbali.

 4. Hifadhi ya Jamii ni KINGA si AKIBA. Hifadhi ya Jamii ni sawa na bima ya kumkinga mfanyakazi na mwanachama dhidi ya majanga yanayoweza kumpata na kumpotezea uwezo wake wa kuzalisha na kujikimu. Majanga hayo ni kama kustaafu,kupata vilema na kamwe si mfuko wa akiba na mikopo, chama cha kuweka na kukopa au upatu. Hivyo michango yako katika hifadhi ya jamii haiwezi kuwa mbadala wa wewe kujiwekea akiba na kuwekeza sehemu ya kipato chako inayobaki kwako baada ya kukatwa mchango wako usiovuka asilimia 10 ya mshahara wako(kwa wale wafanyakazi). Kushindwa kwako kuweka akiba hakuhalalishi kugeuza Mfuko wako wa Hifadhi ya Jamii kuwa ni Benki. Hoja ni kuongeza tija na hatimaye mishahara/kipato na kujenga utamaduni wa kuweka akiba (culture of saving).

 5. Michango yetu kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni MBEGU ambayo mavuno yake yanatokana namna tunavyoendelea kuyapalilia na kunyunyuzia dawa kwa kuendelea kuchangia. Huwezi kupanda leo na kuvuna kabla ya mazao kukomaa au msimu wa mavuno kufika. KUJITOA KWENYE MAFAO NI SAWA NA MKULIMA KULA MBEGU.

 6. Unapostaafu au kwa sababu yoyote unapolazimika kuhifadhiwa na jamii kwa kupewa kinga una uwezo wa kutumia zaidi ya ulichochangia. Hifadhi ya jamii hutoa kinga kwa kadiri ya uhitaji na si kwa kadiri ya mchango pekee. Hii inatokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa upande mmoja na muendelezo wa mitiririko ya michango kwa wale ambao bado wako katika umri wa kuchangia. Mafao yako wewe baada ya kuchukua kiinua mgongo yataendelea kulipwa na wale ambao bado wanachangia. Hivyo, kuruhusu watu kujitoa ni kumomonyoa nguzo ya Hifadhi ya Jamii ya vijana na wanaojiweza kuwafaa wazee na wasiojiweza. Ndivyo ilivyo duniani kote.

 7. Skimu za Hifadhi ya Jamii tofauti na iliyokuwa skimu ya mifuko ya Akiba ya Wafanyakazi inapaswa kugusa wananchi wote kwa kuwa ni haki ya kikatiba na si wafanyakazi pekee. Inapaswa kugusa wasiojiweza,wasio na ajira, waliojiajiri,wakulima, wanamichezo na wengine walioko kwenye sekta isiyo rasmi. Tuendako kila mtanzania anapaswa kuwa mwanachama wa hifadhi ya jamii kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea ambako namba yako ya uanachama wa hifadhi ya jamii ndio kitambulisho chako kikuu. Hivyo hoja ya kujitoa katika mfuko ulipwe ukajiajiri haijitoshelezi. Huko tuendako hata ukijiajiri hatimaye itakuwa ni lazima uchangie hifadhi ya jamii kama ilivyo lazima sasa kulipa kodi alimradi una kipato kiwe cha kuajiriwa au kujiajiri. Kujiunga katika hifadhi ya jamii kwa wasio waajiriwa katika sekta rasmi ni hiyari tu kwa sasa katika kipindi cha mpito.

 8. Tanzania imeingia katika skimu hii mwanzoni mwa miaka ya 2000 tulipobadilisha mifuko iliyokuwapo. Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (NPF) ukawa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) ukabadilika kutoka kuwa mfuko wa Mashirika ya Umma tu na kuwa mfuko wa kila mtu, na Serikali kuunda PSPF, LAPF nk. Sisi Tanzania ndio tumeianza safari ya kuelekea kwenye hifadhi ya jamii na bado hatujafikia huko. Katika muda mfupi manufaa yameanza kuonekana kadri uwezo wa mifuko unavyoongezeka na kupata faida. Leo tuna bima ya afya, fao la ulemavu kazini, fao la kujifungua, fao la elimu, fao la afya vijijini nk. Huko tuendako, mafao haya yatafanana katika mifuko yote na upo uwezekano wa mifuko yote ya sasa kuunganishwa na kuwa mmoja. Hatuwezi kufika huko ikiwa wanachama wataruhusiwa kujitoa kila wanapojisikia kufanya hivyo maana itaathiri uimara wa mifuko.

 9. Kama ilivyo kanuni ya msingi kwa sheria yoyote, katika kila sheria lazima kuwepo na mazingatio (exceptions). Zipo aina ya sekta au kazi ambazo kwa mazingira yake ya asili ya shuruba zake hakuna mfanyakazi anayeweza kuhimili kuwa na uwezo wa kufanya kazi hizo hadi miaka 55. Aina hizi za kazi humfanya mfanyakazi apoteze uwezo wake wa kufanya kazi na kuchangia kutokana na sababu za kiafya (na)au ulemavu. Lazima sheria itambue watu wa aina hii na kazi za aina hii ili kuwawezesha hawa kuanza kunufaika na hifadhi ya jamii kabla ya umri wa kisheria uliowekwa wa kuchangia kwa miaka 15 au kupata mafao ya kiinua mgongo kabla ya miaka 55 kwa hiyari na 60 kwa lazima. Hawa wanahitajika kuwekewa FAO lao (si kujitoa) mahsusi la kuwahifadhi, kuwasitiri na kuwakinga dhidi ya kudhalilika na kufadhaika katika jamii. Hawa wanahitaji hifadhi. Mjadala wetu wafaa kuelekezwa hapo tunapojadili kuhusu marekebisho ya Sheria. Pia tujadili pendekezo la fao la kukosa ajira na ikiwezekana kama tunaweza kutumia michango yetu kama dhamana kukopea nyumba, kujisomesha nk na si kujitoa. Tusipoteze lengo kwa kile alichokisema Mwl. Nyerere, 'Tukipoteza muda mwingi kugawana KIBABA tutapoteza wasaa wa kugawana PISHI'.

 10. Mimi na wewe hatuiujui kesho yetu wala hatuna uhakika wa msaada wa ndugu zetu na rafiki zetu pale tutakapofikwa na uzee au janga. Hifadhi ya Jamii ndio mbeleko yetu ya kujishikizia. Mimi na wewe na wengi wetu ambao ndio wafanyakazi wengi wa Tanzania ambao hatujachangia mifuko kwa zaidi ya miaka 15 kuweza kustahili mafao ya pensheni tuna maslahi gani na kujitoa kwenye mafao? Hao viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wanaotutia hamasa mbona wote umri wao umeshakwenda na wamekaa mkao wa kufaidika na pensheni? Tukumbuke Ujana Ukuta na Fainali Uzeeni.
Inawezekana kabisa sijatoa majawabu na ieleweke haikuwa lengo langu. Lengo langu ni kuchokoza tu mjadala. Tujadili.

---
Ndugu Kibaja Kariongo ni mdau wa harakati za wafanyakazi

President Buhari apologizes for plagiarizing President Obama's speech


LAGOS, Nigeria (AP) — Nigeria's President Muhammadu Buhari has apologized for plagiarizing President Barack Obama's 2008 victory speech and says he will punish those responsible. The two leaders are set to meet next week in New York.

Adeola Akinremi in her Friday column for ThisDay newspaper denounced "the moral problem of plagiarism on a day Mr. President launched a campaign to demand honesty and integrity."

Several sentences were almost identical to Obama's in a speech Buhari made Sept. 8 launching his campaign "Change Begins With Me."

Buhari said, "We must resist the temptation to fall back on the same partisanship, pettiness and immaturity that have poisoned our country for so long."

Obama said, "Let us resist the temptation to fall back on the same partisanship and pettiness and immaturity that has poisoned our politics for so long."

On Friday, the White House said Obama has scheduled a meeting with Buhari on Tuesday on the sidelines of the U.N. General Assembly session.

They are expected to talk about continued U.S. support for security and economic changes in Nigeria, Africa's largest economy and most populous country, as well the government's efforts to counter the Islamic extremist group Boko Haram.

The White House also said that Obama, in his final appearance before the U.N. session, plans to promote trade between the U.S. and Africa on Wednesday, attending a summit with some 200 U.S. and African CEOs and African heads of state.