Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Septemba 22, 2016
The safest and dangerous countries across the globe for tourists (animated map video)

Mkuu wa Wilaya apiga marufuku bodaboda zaidi ya saa 6 usiku


Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na waendesha bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo na kupiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.

Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Muheza (DTO) Herbert Kazonde wakati wa mkutano huo. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.

Katibu wa Chama cha Waendesha Boda Boda wilayani Muheza, Francis Gerald akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto ambazo zinawakabili.
 • via blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Kilimanjaro Queens ilivyowasili mjini Bukoba baada ya kuweka historia ya kutwaa kombe la CECAFA

Imenukuliwa kutoka BukobaWadau blogMabingwa wapya wa Kombe la Chalenji la CECAFA, timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens, mara baada ya kutua hapa Mjini Bukoba leo asubuhi wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu na kuwapongeza kwa ushindi huo mkubwa walioupata kwa kuifunga Timu ya Kenya bao 2-1.

Timu hii inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kesho, Septemba 22, 2016 saa 7.00 mchana kwa ndege ya FastJet ikitokea Mwanza.

Mara baada ya kutua, itakwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya Courtyard iliyoko Sea View, Upanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambako watakuwako viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wale wa Serikali akiwamo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye.Bao mbili safi za winga Mwahamisi Omari jana ziliwapa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Kenya kwenye Fainali ya Mashindano ya CECAFA ya kugombea Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake iliyochezwa huko FUFA Technical Center, Njeru, Mjini Thika Nchini Uganda.

Bao hizo mbili za Mwanahamisi zilifungwa dakika za 26 na 45 na kuwafanya Kilimanjaro Queens waende Mapumziko wakiwa mbele 2-0.

Bao la Kenya, maarufu kama Harambee Starlets, lilifungwa Dakika ya 50 na Christine Nafula.
Kilimanjaro Queens ilitinga Fainali kwa kuwatoa Wenyeji Uganda 4-1 na Harambee Starlets kuibwaga Ethiopia 3-2.
Kilimanjaro Queens, chini ya Kocha Sebastian Nkoma, walitoka Kundi B pamoja na Rwanda na Ethiopia, na wao kufuzu kama Washindi wa Kundi baada ya Kura ya Shilingi kufuatia kulingana kila kitu na Ethiopia.

Here is a list, so far, of prominent Republicans voting for Hillary Clinton


Taarifa ya habari ChannelTEN Septemba 21, 2016


Orodha ya shule 43 za awali, msingi na sekondari zilizofutwa na Wizara ya Elimu

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imezifuta shule za awali, msingi na sekondari nchini zaidi ya 40, ambazo hazijasajiliwa kuanzia Julai mwaka jana.

Awali kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana, waligundua kuwepo kwa shule 35 zisizosajiliwa na kuzifuta, jambo lililofanya kutangaza shule zote ambazo hazijasajiliwa kujisalimisha ili kusajiliwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Usajili wa Shule katika wizara hiyo, Khadija Mcheka alisema Mei mwaka huu baada kuzipa miezi miwili shule ambazo hazijasajiliwa kufanya hivyo, walizifungia shule nyingine 12.

Mcheka alisema shule zinaweza kufutwa kwa sababu mbili zikiwamo zilizosajiliwa, lakini zikakiuka vigezo ambazo zikitimiza vigezo zinaweza kuomba upya usajili na kupewa.
“Lakini aina ya pili ni zile ambazo hazijasajiliwa na zinaendeshwa kinyume cha sheria ambazo nazo zikifuata taratibu zikatimiza vigezo zinaweza kupewa usajili,” alifafanua Kaimu Mkurugenzi wa Usajili wa Shule.
Alisema katika kipindi hicho mpaka Agosti mwaka huu baada ya tangazo la kuwataka kusajiliwa shule za awali nne, zile za awali na msingi 105 na sekondari 19, walifika wizarani kwa ajili ya kupata taratibu za usajili ambapo zipo zilizosajiliwa na nyingine kupewa vibali.

Alisema katika usajili, kuna wapo waliokidhi viwango na wengine waliopatiwa maelekezo na kupatiwa vibali vya kutumia majengo yaliyopo huku wengine wakipewa vibali vya kujenga majengo ya shule kabla ya kupata usajili.

Alisema kwa shule walizozifungia, waliwaandikia barua za kuwafungia na kuwataka kuhakikisha wanawatawanya wanafunzi katika shule zilizosajiliwa kwa gharama zao bila kuwaathiri wanafunzi.

Alitaja shule zilizofungiwa kwa kuendesha shughuli zake bila usajili kuwa ni shule za awali na msingi za

PWANI
 1. Must Lead
DAR ES SALAAM
 1. Brainstorm
 2. Pax
 3. Lassana
 4. Grace
 5. Rose Land
 6. Julius Raymod
 7. St Thomas
 8. Mary Mother of Mercy
 9. Noble Sinkonde
 10. Immaculate Heart of Mary
 11. St Columba
 12. Corner Stone
 13. Dancraig
 14. Mwalimu Edward Kalunga
 15. Edson Mwidunda
 16. Gisela
 17. Kingstar
 18. St Columba awali
 19. Bilal Muslim
 20. Thado
 21. Hocet
 22. Elishadai
 23. Lawrance Citizen
 24. Comrade
 25. Dar Elite Preparatory 
 26. Golden Hill Academy 
 27. Hekima
 28. Pwani Islamic
KAGERA
 1. St Kizito 
 2. Rwazi Encysloped 
PWANI
 1. Dancraig 
 2. Qunu
NJOMBE
 1. Hellen’s
ARUSHA
 1. Joseph
GEITA
 1. Samandito 
 2. Maguzu
Shule za Sekondari zilizofungiwa

DAR ES SALAAM
 1. Hananasif
 2. Elu
 3. Hocet
 4. Safina 
IRINGA
 1. Namnyaki
Shule ya Fountain Gate ya jijini Dar es Salaam imefungiwa kwa kuendesha bweni bila kibali.
“Baada ya kutoa tangazo kutokana na kubaini kuwapo shule nyingi zisizosajiliwa, wapo waliojitokeza na nyingine tumezifungia kutokana na kutokidhi viwango vya usajili lakini pia tunaamini wapo waliojificha wakiendelea kutoa huduma,” alisema Mcheka na kuwaagiza wakaguzi katika kanda na wilaya, kufanya ukaguzi na kutoa taarifa kwa zile ambazo hazijafungiwa na ikithibitika hazijasajiliwa, kuzifungia mara moja.
Alisema utaratibu uliopo kwa kuhakikisha shule zote zinasajiliwa kulingana na viwango stahili kwa lengo la kutoa elimu bora ni wakaguzi wa kanda, mikoa na wilaya kwa kushauriana na waratibu wa elimu katika kata, kuhakikisha shule yoyote inayochomoza, wanaifuatilia na kuwapa ushauri wa kufuata taratibu za usajili kwa kukidhi viwango stahili.

Alisema wamekuwa wakigundua kuwapo kwa shule, ambazo hazijasajiliwa kutokana na wakati wa mitihani idadi ya wanafunzi inazidi tofauti na walivyosajiliwa na kubainika kuwa wapo waliokuwa wakisoma katika shule, ambazo hazijasajiliwa wanawapeleka katika shule zilizosajiliwa.
“Kuna wenye shule ambazo hazijasajiliwa wakati wa mitihani wanakuja kuomba wanafunzi kufanya mitihani hivyo kuleta usumbufu wa kuwatawanya kwenye shule zilizosajiliwa na kwenda kuwakagua ili kuweza kusajiliwa,” alifafanua.
Msajili huyo alisema madhara yanayotokana na mwanafunzi kusoma shule ambazo hazijasajiliwa ni pamoja na haitajulikana mtoto anachosoma kwani haitajulikana mitaala wanayotumia kutokana na kukosa usajili, hivyo kushindwa kufanya mitihani. Pia mazingira ya shule na mpangilio wake, haitaendana na matakwa ya serikali ya kutoa elimu bora kwani mmiliki atafanya kile anachotaka.

Mei mwaka huu, wizara hiyo ilizipa miezi miwili hadi Julai 30, mwaka huu kuhakikisha shule zote ambazo hazijasajiliwa zinajisajili kabla ya serikali kuzifunga.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leonard Akwilapo alisema ifikapo Julai 30, mwaka huu, mmiliki wa shule itakayobainika kutosajiliwa ikiwemo zitakazokosa vigezo vya kusajiliwa, atapaswa kuhamisha wanafunzi waliopo kwa gharama zake.

Alipoulizwa ni shule ngapi ambazo zinajiendesha bila kusajiliwa, Kaimu Mkurugenzi Mcheka alisema tatizo kubwa lipo kwa shule za awali na msingi.

Taarifa ya Ikulu: Rais atengua uteuzi wa M/Kiti na kuvunja Bodi ya Udhamini LAPF

Prof. Hasa Mlawa
Prof. Hasa Mlawa

Msigwa (Mb) alikabidhi jimbo la Iringa Mjini madawati 537

MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi madawati 537 ambayo ameyatoa kwa ajili ya Jimbo la Iringa Mjini.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA

MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amekabidhi madawati 537 katika jimbo lake ili kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya kusoma katika mlundikano mkubwa huku baadhi yao wakiketi sakafuni.

Aidha Msigwa katika hotuba yake amewataka viongozi wa manispaa hiyo kuachana na tabia ya kuhujumu na kuiharibu miundombinu ya shule na badala yake wahakikishe wanatunza mali zote za serikali kwa lengo la kuwasaidia watoto wengine wa vizazi vijavyo waweze kusoma katika mazingira mazuri.
“Sipendi kuona wanafunzi wanaosoma katika shule za jimbo langu wanakaa chini. Kitendo hicho huwa kinaniumiza sana, ndiyo maana nimeamua kupambana kutafuta madawati ili kufanikisha azima yangu ya kukuza elimu kwa wanafunzi wa jimbo la Iringa Mjini,” alisema Msigwa
Naye Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe alisema kwa sasa hawana upungufu wa madawati hivyo hakutakuwa na changamoto ya mwanafunzi wake kujisomea wakiwa wamekaa sakafuni.

Madawati hayo 537 yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 60 na yatasambazwa katika Kata zote.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za Halmashauri hiyo wamesema kuwa tatizo la kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika baadhi ya shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri hiyo lilikuwa linasababishwa na wanafunzi wengine kujisomea wakiwa wameketi sakafuni pamoja na miundombinu isiyo rafiki kwao hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao.

Wanafunzi hao akiwemo Ayoub Joseph, Paul Kisige pamoja na Riziki Ismail walisema kwamba kitendo cha baadhi yao kujisomea wakiwa sakafuni kimesababisha kupunguza uwezo wa kufikiri, hivyo wamempongeza Mbunge Mch. Peter Msigwa kwa juhudi anazozifanya.
“Hapo mwanzoni kwa kweli hali ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu wanafunzi wengine walikuwa wanasoma wakiwa wanakaa chini na hii kiukweli inamwondolea kabisa uwezo wa kufanya vizuri mwanafunzi, lakini kutokana na agizo hili la Rais tumepata nafuu kubwa, na wanafunzi tuna imani tutaweza kufanya vizuri katika masomo yetu… na pia tunampongeza Mbunge wetu kwa juhudi zake za kutuletea madawati,” walisema wanafunzi hao.
Pia waliitaka serikali kutilia mkazo suala la nyumba za walimu na kuimarisha mambo ya msingi, kama kuongeza madarasa ili kuepuka mlundikano kwa wanafunzi.MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe

Mch. Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na Kimbe
haya ni baadhi ya madawati 537 aliyokabidhi Msingwa

Rebeca Gyumi wins UNICEF Social Change Award

On 20 September 2016, Rebeca Gyumi, a Tanzanian lawyer, activist, founder and Executive Director of the Msichana Initiative, receives The Social Change Award at the Global Awards Dinner, held in New York City, USA.
Global Goals Awards honour champions for women’s and girls’ rights

Inaugural awards ceremony organized by Project Everyone, UNICEF and Unilever

New York, 20 September, 2016 – Tanzanian Rebeca Gyumi, executive director of the Msichana Initiative in Tanzania, was honoured at the first annual Global Goals Awards in New York for her efforts to end child marriage in Tanzania.

“I would like to dedicate this award to all Tanzanian girls and every girl around the world who escaped child marriage in search of freedom. You are my true motivation,” she said.

Ms Gyumi, along with the Msichana Initiative, won a landmark court case in July that ended legal provisions permitting child marriage in the country. “Changing the law is one step towards ending child marriage. But it is just the beginning of a wider campaign to change these inhuman acts,” said Gyumi. “For child marriage to end, we need to work together.”

Ms Gyumi was honoured during a ceremony in New York along with a Syrian teen and Olympic swimmer who saved fellow refugees from drowning and an organization that brings health care to vulnerable girls and women in Pakistan.

The three honourees were recognized for their significant contributions to advancing the rights of girls and women. Leaders from business, government, and entertainment attended the ceremony. Also present were Chief International Correspondent for CNN Christiane Amanpour, entrepreneur Chris Anderson and Grammy Award winner and UNICEF Goodwill Ambassador Angélique Kidjo.

The Global Goal Awards are part of ongoing efforts to rally support for the Sustainable Development Goals (SDGs), a set of goals unanimously adopted by every country in the world to end poverty, protect the planet, and ensure prosperity for all by 2030.

The awards were curated by UNICEF with the 17 SDG Advocates forming the official judging panel.

Winners of the Global Goals Awards:
 • The Girl Award 
(to a girl or young woman for laudable work in creating progress for girls)
 • Winner: Yusra Mardini, Syria
Now in Germany, 18-year-old Yusra Mardini and her sister fled conflict in Syria in 2015. While traveling across the Aegean Sea their raft broke down and the sisters jumped into the water and helped guide the boat to safety, saving about 20 people on board. At the Rio Olympics Yusra was part of Refugee Olympic Team and used the opportunity to tell her story and raise awareness about the plight of refugees and migrants around the world. Yusra also won her heat in the butterfly.
 • The Social Change Award 
(to an individual who achieved significant social change for girls)

Winner: Rebeca Gyumi, Tanzania
Rebeca Gyumi is a lawyer, activist and the founder and executive director of the Msichana Initiative, a Tanzanian non-profit that advocates for girls rights and access to education. Rebeca and the Msichana Initiative won a landmark court case in July that ended legal provisions permitting child marriage in the country.
 • The Campaigner Award
(to an individual or organization improving the lives of girls and women)

Winner: DoctHERS, represented by Dr.Sara Saeed Khurram, Pakistan
The social enterprise DoctHERS matches trained junior female doctors in Pakistan with rural women and girls via telemedicine. DoctHERS reaches vulnerable girls and women with essential health care in Pakistan. The organization also provides employment opportunities for qualified female health professionals.

Download professional quality phtos of winners receiving the awards here http://uni.cf/2ckXrms

About UNICEF
UNICEF promotes the rights and wellbeing of every child, in everything we do. Together with our partners, we work in 190 countries and territories to translate that commitment into practical action, focusing special effort on reaching the most vulnerable and excluded children, to the benefit of all children, everywhere.

For more information about UNICEF and its work visit www.unicef.org

Follow us on Twitter and Facebook.

For further information and interview requests, please contact:

Usia Ledama, Communication Specialist, UNICEF Tanzania, Mobile: 255 682 911 534 / 0762 871830 ,Direct: 255 22 2196627 ; Email: [email protected]

Madereva waliotekwa DRC warejea Tanzania na kusimulia masaibu, almanusra ya kuuawa

Dereva Mbwana Said (kulia), akielezea jinsi walivyotekwa.
Na Dotto Mwaibale

MADEREVA 10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodhaniwa ni waasi Jamhuri ya Demokraia ya Congo (DRC) wamesema waliponea tundu la sindano kuuawa.

Kauli hiyo imetolewa na madereva hao katika hafla ya kuwapokelewa iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo jioni.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mbwana Said alisema analishukuru jeshi la Congo kwa jitihada kubwa walioifanya kwa ajili ya kuokoa maisha yao."
"Tunaishukuru serikali ya Congo kwa kutuokoa kwani tulikuwa katika wakati mgumu na leo kuungana tena na ndugu zetu" alisema Said.
Alisema walilazimia kutembea kwa muda mrefu huku risasi zikirindima kati ya majeshi ya serikali na waasi hao hadi walipofanikiwa kutuokowa kutoka kwenye mikono ya waasi hao.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba aliishukuru serikali ya Congo kwa jitihada iliyoifanya na kufanikiwa kuwaokoa madereva hao.

Balozi wa Congo nchini Jean Mutamba aliwataka madereva hao kuacha viza na nyaraka zao ubalozini pindi wanapo safiri na kurudi ili iwe rahisi kuwatambua pale wanapopata matatizo.
"Tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya na kutoa wito kuwa waendelee kusafiri kwa kufuata taratibu zilizopo," alisema Mutamba.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya Conco (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Afrika katika wizara hiyo, Balozi Samweli Shelukindo.

Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.

Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistic ambayo magari yake na madereva walitekwa, Azim Dewj (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapokea madereva hao.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisubiri kuchukua taarifa za kuwapokea madereva hao.

Madereva hao wakipokelewa uwanjani hapo.
Madereva hao wakiwa chumba cha mkutano cha uwanja huo wakati wa mapokezi yao.

Dereva Kumbuka Seleman (kulia), akisimulia jinsi alivyotoroka na kutoa taarifa ya kutekwa kwao.

Dereva Athuman Fadhili (kulia), akisimulia walivyookolewa na majeshi ya Congo na jinsi walivyojificha porini na kutembea umbali mrefu kwa kutambaa ambapo ilifika wakati waliomba bora wafe kuliko mateso waliyokuwa wakipata.

Hapa ni furaha ya kukutana na ndugu jamaa na wafanyakazi wenzao.

Picha ya pamoja na viongozi waliowapokea.

Ndugu, Jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzao wakiwa nje ya jengo la VIP uwanjani hapo wakisubiri kuwapokea.

Mapokezi yakiendelea.

Ni furaha ya kukutana na wapendwa wao.

Hapa dereva Mbwana Said akikumbatia na mjomba wake Kassim Salim katika hafla hiyo kwa Mbwana ilikuwa ni furaha na majonzi.

Mbwana Said (katikati), haamini macho yake baada ya kukutana na mke wake Mariam pamoja na mtoto wake Kauzari.
 • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com-simu namba 0712727062