WhatsApp adds option to invite people to group chat via links


The popular messaging app, WhatsApp has added the ability to invite someone to join a group chat with a link. Any WhatsApp administrator who has joined the beta program (go to Google Play and become a beta tester for this app) have this option in the latest release (or download the APK version 2.16.281) which lets you share the link directly using a QR code or NFC tag in this new beta changes. The admin can later revoke a link ultimately denying ability for anyone to join the chat.

To try it out, go to add a new participant to your chat goup, you will have a new "invite to group via link" option at the top of your contacts list. Tap on it to open a new screen with the unique link to your chat, which you can share via WhatsApp or copy & share using another app, or revoke.


Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Septemba 28, 2016[video] Rais Magufuli alipozuru kitengo cha ukaguzi wa makontena bandarini Dar, Septemba 26, 2016


[video] Kauli ya Prof. Lipumba kuhusu barua aliyoandika kujiuzulu CUF


[video] Baraza Kuu la CUF likisoma uamuzi wa kumfuta uachama Prof. Lipumba


MAAZIMIO NA MAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LILILOKUTANA KWENYE MAKAO MAKUU YA CHAMA, MJINI ZANZIBAR


TAREHE 27 SEPTEMBA, 2016

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) limekutana leo, Jumanne, tarehe 27 Septemba, 2016 katika kikao cha dharura kilichofanyika Makao Makuu ya Chama, mjini Zanzibar na ambacho kiliitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 80 (1). Wajumbe 43 kati ya wajumbe 53 wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa walihudhuria kikao hicho.

Agenda tatu zilizotayarishwa na kuwasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa zilijadiliwa na kufanyiwa maamuzi ambazo ni:
  1. Kujadili barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya tarehe 23/09/2016;
  2. Kupokea na kujadili mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba kutokana na hujuma alizozifanya tarehe 24/09/2016 Afisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam;
  3. Kumjadili na Kumhoji Prof. Ibrahim Lipumba mbele ya kikao na kumchukulia hatua za kinidhamu.
Baada ya mjadala wa kina wa agenda hizo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio na maamuzi yafuatayo:

KUHUSU BARUA YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YA TAREHE 23/09/2016:

1. Baraza Kuu limeukataa ushauri, msimamo na mwongozo wa Msajili wa Vyama vya Siasa alioutoa kupitia barua yake ya tarehe 23/09/2016 kwa sababu Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act, No. 5 of 1992) – Sura ya 258 haimpi mamlaka wala uwezo wowote kutoa ushauri, msimamo au mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusiana na maamuzi ya vikao vya Chama na kwa kulitambua hilo ndiyo maana katika matamko yake yote aliyoyatoa, Msajili huyo ameshindwa kutaja kifungu gani cha sheria hiyo kinampa uwezo huo.

2. Baraza Kuu limesikitishwa sana na kitendo cha Jaji Francis Mutungi kujishushia hadhi, kujifedhehesha na kujivunjia heshima mbele ya macho ya jamii ndani na nje ya nchi, yeye na Ofisi anayoiongoza kwa kuvunja sheria na kudharau maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UAMUZI wa tarehe 9/5/2005 wa Jaji T.B. Mihayo katika kesi ya Emmanuel Nyenyemela na Magnus Msambila v/s Registrar of Political Parties & Others (Civil Case No. 6 of 2003) ambapo Jaji Mihayo aliamua kwamba:
“… I do not see anywhere in the Political Parties Act where the Registrar has power to bless or condemn meetings of political parties or decisions that they make.”
Tafsiri yake ikiwa ni kwamba, “… Sioni popote katika Sheria ya Vyama vya Siasa ambapo Msajili ana madaraka ya kubariki au kupinga vikao vya vyama vya siasa ay maamuzi ambayo vikao hivyo vinafanya.”

3. Baraza Kuu limemuagiza Katibu Mkuu wa Chama kumjibu kwa maandishi na kwa kina Msajili wa Vyama vya Siasa na kumueleza maamuzi ya Baraza hilo ambalo kikatiba ndilo lenye madaraka ya kusimamia uendeshaji wa Chama kwamba halitambui ushauri, msimamo na mwongozo huo na limeutupilia mbali kwa kukosa kwake mantiki, hoja na pia kukosa nguvu za kisheria.

4. Baraza Kuu linamtanabahisha Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba atabeba dhamana kwa yote yaliyofanywa na yatakayofanywa na Prof. Ibrahim Lipumba na kikundi chake cha wahuni ambacho kilivamia Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam tarehe 24 Septemba, 2016 na kupiga watu na kufanya uharibifu wa mali kutokana na tamko lake hilo ambalo halina msingi wa kisheria.

KUHUSU MASHTAKA DHIDI YA PROF. IBRAHIM LIPUMBA KUTOKANA NA HUJUMA ALIZOZIFANYA TAREHE 24/09/2016 AFISI KUU YA CHAMA, BUGURUNI, DAR ES SALAAM:

1. Baraza Kuu limepokea mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba yaliyoandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 108 (1) ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia nidhamu ya Chama katika ngazi ya Taifa na kuyawasilisha mapendekezo yake mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

2. Baraza Kuu limeridhika kwamba Kamati ya Utendaji ya Taifa imefuata masharti yote ya Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014) katika kuanda mashtaka hayo kutokana na mtuhumiwa, Prof. Ibrahim Lipumba, kuvunja Katiba ya Chama, Ibara ya 12 inayohusu ‘Wajibu wa Mwanachama” hasa Ibara ndogo za 12 (6), 12(7) na 12(16).

KUHUSU KUMJADILI NA KUMHOJI PROF. IBRAHIM LIPUMBA MBELE YA KIKAO NA KUMCHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU:

1. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeridhika kwamba Kamati ya Utendaji ya Taifa ilimfikishia mtuhumiwa, Prof. Ibrahim Lipumba, barua ya wito (Kumb. Nam. CUFHQ/OKM/WM/2016/Vol.1/49 ya tarehe 24/09/2016) ambayo pia ilikuwa na maelezo ya tuhuma na kumtaka afike mbele ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichofanyika leo, tarehe 27 Septemba, 2016, mjini Zanzibar kuja kujieleza na kujitetea kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Katiba ya Chama kwa kuvunja masharti yanayohusu “Wajibu wa Mwanachama” Ibara ya 12(6), 12(7) na 12(16).

2. Baraza Kuu limesikitishwa na dharau iliyooneshwa na Prof. Ibrahim Lipumba dhidi ya kikao hiki ambacho ni chombo cha juu chenye mamlaka ya kusimamia uongozi wa Chama pamoja na kupelekewa wito wa kumtaka afike mbele yake. Kitendo hicho cha dharau kinaonesha tu jinsi gani heshima na uaminifu wa Prof. Ibrahim Lipumba kwa Chama ulivyoshuka.

3. Baraza Kuu limeridhika kwamba kwa kuwa Prof. Ibrahim Lipumba akiwa mtuhumiwa alichagua mwenyewe kudharau wito wa kufika kujieleza na kujitetea ambayo ni haki yake kama mwanachama kwa mujibu wa Ibara ya 11(6) ya Katiba ya Chama, halikuwa na sababu ya kutoendelea kumjadili na kuchukua hatua dhidi yake.

4. Baraza Kuu limeridhika na mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba kwamba kwa kitendo chake cha kuongoza na kusimamia kikundi cha wahuni kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam, siku ya Jumamosi, tarehe 24 Septemba, 2016 na watu hao aliowaongoza na kuwasimamia kupiga walinzi waliokuwepo, kuvunja na kuharibu mali za Chama na hivyo kuharibu heshima na taswira ya Chama mbele ya jamii ndani na nje kwamba amtenda makosa kinyume na “Wajibu wa Mwanachama” kama ilivyoelezwa kwenye Ibara ya 12(6), 12(7) na 12(16) za Katiba ya Chama.

5. Baada ya kuridhika na mashtaka hayo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limeamua kwa kutumia uwezo wake kwa mujibu wa Ibara ya 10 (1) (c) na kwa kura zote 43 za wajumbe wake waliohudhuria kumfukuza uanachama Prof. Ibrahim Lipumba, kuanzia tarehe ya leo, Jumanne, tarehe 27 Septemba, 2016.

6. Kwa maamuzi haya, Baraza Kuu linaweka bayana kwa wanachama wa CUF, Watanzania na mamlaka zote nchini kwamba kuanzia tarehe ya leo, Prof. Ibrahim Lipumba hana haki ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na shughuli zozote za Chama.

MWISHO:

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawapa pole wanachama wa CUF walioathirika kutokana hatua ya Msajili kuingilia mambo ya Chama kinyume na uwezo alio nao na pia kwa matendo ya kihuni yaliyofanywa na Prof. Ibrahim Lipumba na kikundi chake kuvamia Ofisi Kuu ya Chama. Wakati huo huo, Baraza Kuu linawapongeza wanachama wote kwa kusimama imara kukilinda Chama chao na linawahakikishia litasimamia wajibu wake wa kikatiba kukiongoza na kukilinda Chama hiki dhidi ya njama za maadui wa ndani na nje.

HAKI SAWA KWA WOTE

BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi)

27 Septemba, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN Septemba 26, 2016Mwinjilisti ampiga hadi kumuua bintiye kabla ya kujinyonga na kufa

Mwinjilisti wa Kanisa la African Inland Church (AICT), Charles Kazereng’wa (45), amejinyonga hadi kufa, baada ya kumuua mwanaye, Malita Charles (15) kwa kumpiga akimtuhumu kujihusisha na ufuska.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Rodson amelithibitishia gazeti hili kutokea kwa matukio hayo juzi jioni.

Hata hivyo, alisema kuwa asingeweza kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu alikuwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Geita.

Hata hivyo, habari za uhakika kutoka katika Kitongoji cha Elimu, Kijiji cha Kaseme kilichopo wilayani Geita ambako mwinjilisti huyo alikuwa akiishi na familia yake zinasema kuwa alichukua uamuzi wa kumwadhibu binti yake huyo aliyehitimu darasa la saba mwaka huu, baada ya kumkuta akizungumza na mwanamume ambaye hata hivyo hakufahamika.

Inaelezwa kuwa baada ya kumpiga, alimchukua na kwenda naye nyumbani na kumfungia ndani huku akiendelea kumwadhibu hadi alipofikwa na umauti.

Kwa mujibu wa shuhuda ambaye hakuwa tayari kutajwa jina gazetini, baada ya mwinjilisti huyo kubaini kuwa amemuua mwanaye, alichukua uamuzi wa kukimbia umbali ya kilometa moja na kujitundika mtini kwa kamba iliyomnyonga hadi kufa.

Kamanda Mponjoli, alisema kuwa uchunguzi wa Polisi na wa madaktari unaendelea na kwamba utakapokamilika miili ya marehemu wote wawili itakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Aliitaka jamii kuwa makini wakati wa kuadhibu watoto kwa kuwa si wakati wote wanapaswa kupewa adhabu kali na hatarishi kama vipigo vinavyoweza kuwasababishia umauti.

Wakati huohuo, baadhi ya wakazi wa Kata ya Kaseme wanaomfahamu mwinjilisti huyo walieleza kwa nyakati tofauti kushangazwa na hatua aliyoichukua kwa sababu hakuwa na tabia ya uhalifu wa aina yoyote wala ukatili.

Masaga Makanika na Magesa Masai kila mmoja kwa wakati wake alisema kuwa mwinjilisti huyo alikuwa ni muumini mzuri wa dini asiye na rekodi mbaya ya matukio ya kiuhalifu na kwamba hatua alizochukua zimewaacha na maswali mengi huku wakifikiri kuwa pengine ni mipango ya Mungu au majaribu ya shetani.
  • Source: Habari Leo

Copy: Judgment of The Court of Appeal - DPP vs Zombe, Bageni, Mabula, Makele et al

IN THE COURT OF APPEAL OF TANZANIA
AT DAR ES SALAAM
(CORAM:LUANDA, J.A., MJASIRI, J.A. And KAIJAGE, J.A.)
CRIMINAL APPEAL NO.358 OF 2013
DIRECTOR OF PUBLIC PROSECUTIONS .……………………….………. APPELLANT

Air Tanzania a second Bombardier Q400 aircraft to its fleet


Sept 27, 2016: Bombardier Commercial Aircraft has delivered two Q400 turboprops to Tanzanian Government Flight Agency and these dual-lavatory configuration aircraft will be operated by Air Tanzania.

“As we look to expand operations and increase our route network across Tanzania and the African continent, the technologically advanced Q400 aircraft is a key component in our growth strategy,” said Leonard Chamuriho, Permanent Secretary, Ministry of Transport, Works and Communication, Tanzania.

“Its ability to operate at challenging airfields, combined with its fuel efficiency, excellent reliability and comfortable passenger amenities, make it a valuable addition to our fleet.”

“The Q400 aircraft is showcased very well in Africa where it has proven itself to be extremely efficient and continues to maintain strong market share in its class,” said Jean-Paul Boutibou, vice president, Sales – Middle East and Africa, Bombardier Commercial Aircraft.

The delivery of the two aircraft increases the fleet of Q Series turboprops in Africa to approximately 125 aircraft including 40 Q400 aircraft.

Designed as a modern, 21st-century turboprop, the Q400 aircraft is the most recent development in the Q Series family of aircraft. It provides unmatched performance, operational flexibility and passenger comfort.

In addition to the standard single-class configuration, Q400 aircraft are available with an optional dual-class interior for enhanced passenger comfort; in an optional extra-capacity configuration offering up to 90 seats for higher-density markets; and in a cargo-passenger combi configuration.

Thanks to its combination of turboprop attributes, jet-like features, industry-leading passenger experience and environmental footprint, the Q400 aircraft is exceptionally versatile and can be adapted to a variety of business models.

By offering a 30 percent reduction in fuel burn over the jets it often replaces, the Q400 aircraft radically reduces carbon emissions and increases cost efficiency.

Bombardier’s commercial aircraft presence in Africa includes a Regional Support Office (RSO) and spare parts depot, co-located in Johannesburg, South Africa as well as Authorized Service Facilities in South Africa and Ethiopia.

Bombardier has recorded firm orders for a total of 565 Q400 aircraft. [Source: stattimes.com]

Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.

Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikipata Saluti ya maji (Water Canon Salutation) mara tu baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.

n11: Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.

Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na nahoda wa John Kuipers aliyeeendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na kuiwasilisha salama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.

Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akikagua Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.


Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakitelemka baada ya kuikagua Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. 

Waliochaguliwa kujiunga vyuo vikuu mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2016/2017

Chuo Kikuu Cha Mwalimu Nyerere <<bonyeza Hapa>>

Chuo Kikuu Cha UDSM, DUCE na MUCE <<bonyeza Hapa>>

Chuo Kikuu Cha Tumaini Makumira <<Bonyeza Hapa>>

Chuo Kikuu Cha UDom <<bonyeza Hapa>>

Chuo Kikuu Cha IFM <<Bonyeza Hapa>>

Chuo Kikuu Marian << Bonyeza Hapa>>

Chuo Kikuu CBE << Bonyeza Hapa>>

Tumaini - Mbeya << Bonyeza Hapa>> & <<Hapa>>

Chuo Kikuu MUM << Bonyeza Hapa>>

Chuo MUM (Diploma) <<Bonyeza Hapa>>

Chuo - Stella Maris << Bonyeza Hapa>>

Chuo- Kampala - KU << Bonyeza Hapa>>

Mkuu wa Wilaya amsimamisha kazi Meneja wa Mamlaka ya maji na kuteua kaimu

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akizungumza wakati wa kikao cha Kumng'oa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na salama Wilyani humo
Na Mathias Canal, Dodoma

Kushindwa kusimamia miundombinu ya maji na kupelekea kuwa na ugumu wa upatikanaji maji kwa kiwango kinachotakiwa ni miongoni mwa kadhia zilizopingwa wakati wa kampeni na Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ambaye ndiye Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuahidi kuchagua wasaidizi watakaosimamia na kulimaliza jambo hilo mara baada ya kuingia madarakani.

Kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wakitupa lawama kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambao wamesababisha kudorora kwa uchumi na kuchagiza ugumu wa maisha kutokana na umbali wanaotumia kutafuta maji, huduma za afya sambamba na umbali wa shule za Sekondari na Msingi.

Kutokana na kadhia ya upatikanaji hafifu wa maji safi na salama Wilayani Kongwa imepelekea kukalia kuti kavu kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na Salama Wilayani humo Ndg Kisha Bonga kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo ikiwemo kusababisha wafanyakazi wa Mamlaka ya maji kufikia maamuzi ya kuandamana.

Maandamano ya Wafanyakazi hao yalifanyika siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita yaliyoanzia Ofisi za Mamlaka ya Maji safi hadi ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa wakiwa wamegoma kufanya kazi kutokana na kuchelewa kulipwa mishahara yao.

Katika malalamiko ya wafanyakazi hao yaliyopelekea kugoma kufanya kazi yanachagizwa na kudai mishahara ya zaidi ya miezi nane sasa (8) ikiwa ni muda wenye ishara ya kutolipwa mishahara yao tangu mwaka 2016 ulipochomoza mwanzoni mwa Januari mwaka huu.

Katika malalamiko yao pia wamemlalamikia Meneja huyo wa Mamlaka ya maji Ndg Kisha Bonga kwa kutumia lugha zisizo na staha kwa kuwataka waache kazi wale wote wanaoshindwa kuishi pasina kulipwa mshahara jambo ambalo linawafedhehesha watumishi hao.

Hata hivyo DC Ndejembi akizungumza na wafanyakazi hao aliwataka kwa umoja wao kurejea Ofisini kwao na kuendelea na kazi huku akiahidi kulivalia njuga jambo hilo kwa kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ili wajue tatizo limeanzia wapi na kwa namna gani linaweza kutatuliwa.

Katika kutaka kutatua mgogoro huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi alizuru katika ofisi ya Meneja wa Mamlaka ya maji kama alivyotoa taarifa kuwa angefika kukutana nae kwa pamoja washirikiane namna ya kutatua kadhia hiyo lakini Meneja huyo aliondoka na hakurejea tena tena jambo lililomlazimu kufanya kikao na wafanya kazi hao kwa kuanza kuomba kusomewa Mapato na matumizi ili kupata ahueni ya mahali pa kuanzia.

Mamlaka ya maji safi na salama Wilayani Kongwa inakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na moja (11,000,000) kwa mwezi fedha ambazo zingeweza kabisa kuwalipa wafanyakazi wote ambao kwa kila mwezi malipo ya mishahara yao haizidi milioni tano 5,000,000 hivyo kushindwa kufanya malipo hayo Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa huo ni uvivu na uzembe katika utendaji.

Fundi Mkuu wa Bomba Wilayani humo pamoja na Mkurugenzi huyo hawajawahi kupitisha hata mwezi mmoja bila kupata malipo ya mshahara wao jambo ambalo limemshangaza Mkuu wa Wilaya hiyo na hatimaye kufikia maamuzi ya kumsimamisha kazi Meneja wa Mamlaka ya Maji Ndg Kisha Bonga kwa kupungua ufanisi wake katika utendaji.

Kutokana na maamuzi hayo Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhandisi Ngusa Izengo wamemteua Mhandisi Hamisi Ally kuwa kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji ili kusukuma gurudumu la utendaji kazi kusonga mbele.

Mara baada ya kukaimu nafasi hiyo Mhandisi Ally aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi kutatua kero ya muda mrefu katika kata ya Chamkoroma kwa hujuma za wafanyabiashara wa maji kukata bomba na kuliunganisha ili wapate maji wao peke yao na hatimaye kuwauzia wananchi kwa shilingi mia nne kwa kila dumu la lita ishirini.
Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na salama WIlayani Kongwa wakizunguza na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Deogratius Ndejembi

Taarifa ya Ikulu - Rais, Waziri Mkuu watengua uteuzi wa Katibu Tawala Kagera, Mkurugenzi na Mhasibu wa Halmashauri Bukoba

Rais Dk. John Magufuli, Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakitazama mfano wa hundi hiyo

Rais Dk. John Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 545, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dk. John Magufuli akizungumza na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 545, Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dk. Aziz Mlima

Rais Dk. John Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo .

Rais Dk. John Magufuli akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya kupokea msaada wa fedha hizo.