Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Septemba 29, 2016
  • Shukurani ya magazeti iifikie timu ya MJENGWA BLOG

Taarifa kwa wafanyabiahara wa utalii kuhusu kusajili na kulipia ada ya leseni 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

WAFANYABIASHARA WA UTALII KUSAJILI NA KULIPIA ADA YA LESENI YA MWAKA 2016

Wizara ya Maliasili na Utalii inawakumbusha wafanya biashara za utalii wasiokuwa na leseni ya biashara hiyo inayotolewa kwa mujibu wa sheria ya Utalii Na. 29 ya Mwaka 2008 Vifungu Na.10 na 31, kuwa wanatakiwa kusajili na kulipia ada ya leseni kwa mwaka 2016 ifikapo tarehe 31 Oktoba, 2016.

Biashara za Utalii husika ni hizi zifuatazo:
1Kampuni za kusafirisha watalii10Vivutio vya kuuza bidhaa za urithi (Cultural heritage centres)
2Kampuni za uwindaji wa kitalii11Wajasiriamali wa utalii wa utamaduni (Cultural tourism enterprises)
3Wawindaji Bingwa12
Kampuni za kukodisha vifaa vya utalii

4Kampuni za kusafirisha watalii kwa ndege13Maeneo ya michezo ya burdani (Theme parks, wildlife forms. Zoo, snake parks etc)
5Kampuni za kusafirisha watalii kwa Maputo (hot air balloon)14Kampuni za kukodisha magari kwa watalii
6Kampuni za kusafirisha watalii kwa farasi15Kampuni za kukatisha tiketi za ndege
7Kampuni za kusafirisha watalii kwa boti16Wakala wa kutoa huduma kwa watalii (tourist handling agents)
8Kampuni za kupandisha watalii Milimani17Nyumba za huduma za malazi (hoteli, loji, kambi za kitalii)
9Kampuni za utalii wa michezo ya kusisimua (tourism adventure sports)18Maduka ya zawadi za kitalii (Curio Chops)
i. Wizara inachukua nafasi hii pia kusisitiza kwamba ni kosa linalostahili adhabu kisheria kufanya biashara ya utalii bila ya kusajili na kulipia ada ya leseni kwa mwaka husika.

ii. Vilevile, tunapenda kuwafahamisha kuwa maombi kwa ajili ya leseni ya kufanya biashara ya utalii kwa mwaka 2017 yameanza kupokelewa katika Ofisi zetu zilizopo Dare s Salaam, Arusha, Mwanza na Iringa.

iii. Orodha ya wafanyabiashara ya utalii waliosajiliwa na kulipia ada za leseni inapatikana katika tovuti ya Wizara (www.mnrt.go.tz), na katika ofisi za Wizara zilizotajwa hapo juu.

Angalizo: Umma unatahadharishwa kutofanya biashara na kampuni za biashara za utalii ambazo hazina Leseni ya Biashara ya Utalii ya mwaka 2016, kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria.

Imetolewa na:

KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Simu: +255 22 2864230

Barua pepe:[email protected]

Taarifa ya habari ChannelTEN Septemba 28, 2016Elected DSE New Board Members

Example fallback content: This browser does not support PDFs. Please download the PDF to view it: Download PDF.

Afariki akisaidiwa na mjamzito mwenziye kujifungua; DC aagiza kusimamishwa watumishi waliozembea

MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Said Mtanda ameagiza kusimamishwa kazi na kufanyika kwa vikao vya kisheria ili kuwafukuza kazi watumishi wawili wa idara ya afya wilayani humo kwa uzembe ambao ungesababisha kifo cha mama mjamzito.

Mtanda alitoa agizo hilo jana baada ya mjamzito Catherine Gideon (33), mkazi wa kijiji cha Kasu wilayani humo, kujifungua kwa kupewa msaada na baadhi ya wagonjwa waliokuwapo hapo, ikiwa ni pamoja na kusaidiwa kukata kitovu cha mtoto na mjamzito mwenzake aliyekuwapo hospitalini hapo.

Mzazi huyo alifikwa na mkasa huo katika hospitali teule ya wilaya juzi, alisema Mtanda, baada ya kukosa huduma kutoka kwa muuguzi wa zamu, Godfrey Lazaro na muuguzi msaidizi, Maria Msafiri.

Imedaiwa kuwa wauguzi hao hawakuwapo kazini tangu saa 4:00 usiku, alisema.

Akizungumza na Nipashe kwa simu jana, Mtanda alisema amelazimika kuchukua hatua za kinidhamu baada ya watumishi hao kushindwa kutekeleza wajibu wao licha ya kwamba walikuwa zamu ya usiku.

Alisema watumishi hao walirejea kazini saa 12 asubuhi na kukuta tayari wagonjwa wamemsaidia mzazi, hali iliyozua manung’uniko kutoka kwa wagonjwa dhidi ya watumishi hao.

Mtanda alisema ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuwaandikia barua ya kuwasimamisha kazi kuanzia jana na kuagiza vikao vya kisheria na nidhamu vianze kuketi kuanzia leo ili kubaini makosa yao na kuwatimua kazi kwa vile wilaya yake haipo tayari kuwalea "watumishi wa aina hiyo."

Kiongozi huyo wa serikali pia aliwaonya watumishi wote wa umma pamoja na sekta binafsi kutofanya mzaha katika majukumu yao huku akiwataka wale wanaoona wamechoka kazi, waachie ngazi.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mathias Abuya, alisema wanaendelea na vikao vya kisheria na watafukuzwa kazi ikiwa watathibitika kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na sheria za taaluma ya udaktari na afya ya binadamu.

Kunambi aeleza alivyomudu kuachana na dawa za kulevya

Verry Kunambi na mwanaye
Verry Kunambi na mwanaye
WATU wengi wamekuwa wakiwatenga waathirika wa dawa za kulevya na kuona kama ni watu wasiofaa katika jamii.

Kuendelea kupuuzwa kwa kundi la watu hawa kulisababisha kila kukicha idadi ya watu wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kuendelea kuongezeka.

Baada ya Serikali kuona nguvu kazi ya Taifa inazidi kupotea kwa sababu hii, iliamua kubuni mbinu mbalimbali kukabiliana nayo.

Serikali kwa kushirikiana na asasi mbalimbali zilianzisha mipango mikakati ya kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya ili kupunguza athari za kiafya ndani ya jamii pamoja na maambukizi ya Ukimwi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Verry Kunambi (50), ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa wanaotumia dawa za kulevya (TANPUD), anasema naye ni miongoni mwa walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Anasema TANPUD ilianza mwaka 2011 ambapo mwaka 2015 ilipata usajili wa kudumu ambapo malengo makubwa ni utetezi wa watumiaji dawa za kulevya ili waweze kuthaminiwa na kupata huduma muhimu ndani ya jamii.

Kunambi anasema alisoma Shule ya Msingi Ilala Boma na baada ya hapo alijiunga na Sekondari ya Lomwe iliyopo Usangi, Kilimanjaro.

Anasema mwaka 1987 – 1991 alijiunga na ubaharia na ndipo alipoanza kutumia dawa za kulevya akiwa Iran baada ya kukutana na kundi la vijana wengi wakitumia dawa hizo.

Anasema wamezaliwa watoto sita ambapo yeye ni mtoto pekee wa kiume katika familia ya Theresphory Kunambi na Catheline Bruno.

Kunambi anasema mama yake mzazi alifariki mwaka 1985 wakati yeye akiwa bado hajaanza kutumia dawa za kulevya.

Anasema Februari mwaka 1991 alirejea nchini ambapo alikuwa na fedha nyingi na ndipo matumizi ya dawa za kulevya yalivyoongezeka na alienda tena Pakistan kuchukua dawa hizo huku akishirikiana na mtandao wa wafanyabiashara wakubwa.
“Nilijiunga na mtandao wa wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ndipo nilipoenda zaidi ya mara mbili nje ya nchi kufuata mzigo,”anasema Kunambi.
Anasema mwaka 1998 aliishiwa fedha na ndipo alipojiingiza kwenye matumizi makubwa na kuanza kujidunga sindano.
“Katika kipindi hiki ndicho nilichokuwa nimezidiwa. Nilihama nyumbani kwa sababu familia yangu yote ilinitenga.
“Baba yangu alifuatilia nyendo zangu kwa karibu na kunipa ushauri mara kwa mara ili niachane na matumizi ya dawa hizo,”anasema Kunambi.
Anasema mwaka 2010 alipata elimu ya kuzuia dawa za kulevya na ilipofika mwaka 2011 alianza tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), na mwaka 2013 alimaliza tiba na ndipo alipopelekwa shule kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa kutoa elimu kwa wengine waweze kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Kunambi anasema mwaka 2013 alimuoa Edna Kunambi na walibahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Davis.
“Mke wangu alikuwa ni mlokole na kipindi chote cha uchumba alikuwa akifahamu kama mimi natumia dawa hizo na alikuwa akijitahidi kuniombea hadi Mungu alivyotoa kibali cha kuoana,” anasema Kunambi.
Kunambi anasema watumiaji wengi wa dawa za kulevya wanakumbana na changamoto ya kutengwa na jamii na kuonekana kama ni watu wasiofaa katika shughuli mbalimbali.

Anaishauri Serikali na jamii kwa ujumla kujitahidi kuendelea kuwapa ushauri na huduma za matibabu watumiaji wa dawa za kulevya ili waweze kuachana na matumizi hayo.

Anasema kuzidi kuwaacha wakihangaika peke yao kunazidi kuchangia ongezeko la matumizi hayo hapa nchini.
“Inasikitisha hadi leo kuna baadhi ya familia zimewatenga vijana wao kwa sababu tu eti wanatumia dawa za kulevya, jambo ambalo limekuwa likisababisha kundi hili kukosa elimu sahihi ya madhara ya matumizi ya dawa hizi na jinsi ya kujikinga,”anasema.
Anasema yeye binafsi alipokea ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu kuachana na matumizi ya dawa hizo na anashukuru Mungu hadi alipofikia ameweza kupata mafanikio makubwa ikiwamo kuwa tegemeo la familia yao.
“Nakumbuka wakati nimeingia kwenye matumizi makubwa ya dawa za kulevya dada zangu walikuwa wakiumia mno kwa sababu ni mtoto pekee wa kiume. Hali ile nikikumbuka nasikitika mno na sihitaji irudie tena kwenye familia nyingine,” anasema Kunambi.
Pia anaishauri serikali itunge sheria kali kwa waagizaji wa dawa hizo kwakuwa wao ndiyo wachochezi wa matumizi hayo hapa nchini.
  • Imeandikwa na CHRISTINA GAULUHANGA via MTANZANIA

SSRA yazungumzia hofu ya wananchi kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde.

Na Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA), imewataka Watanzania kuondoa hofu iliyojengeka kwenye jamii kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya kifedha.

Akizungumza katika warsha maalum ya siku moja ya waandishi wa habari, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa SSRA, Ansgar Mushi alisema kuwa mifuko hiyo haina hali mbaya kama wanavyodhani watu katika jamii kwani ina fedha za kutosha.

“Watanzania wamekuwa wakiambizana kuwa mifuko hii ina hali mbaya kifedha, napenda kuwahakikishia kuwa ina fedha za kutosha kwani tumekuwa tukifanya ukaguzi wa mara kwa mara. Katika kaguzi zetu za mara kwa mara hakuna mfuko tuliobaini kuwa una kasoro au upungufu wowote,” alisema Mushi.

Aidha, Mushi alisema kwa mwaka mifuko hiyo ya pensheni imekuwa ikikusanya jumla ya sh trilioni 1.692 wakati mfuko wa bima ya afya (NHIF) unakusanya sh bilioni 88.5 ambapo jumla ya makusanyo yote ni sh trilioni 1.78.

Kwa upande wa fao la kujitoa, Mushi alisema licha ya kutawaliwa na sintofahamu, fao hilo lilifutwa na Serikali kuanzia mwaka 2012 na kwa sasa SSRA imeanzisha mchakato wa kuratibu uanzishwaji wa fao la upotevu wa ajira.

Mushi alisema kuwa fao hilo lilipofutwa, bado kulikuwa na mifuko iliyoendelea kuruhusu kujitoa lakini kwa sasa wameamua waanzishe mchakato wa fao la kupoteza ajira, ambalo ni mahususi kwa ajili ya kuwanufaisha waathirika.

“Fao la Upotevu wa ajira litakuwa mahsusi kwa ajili ya wale waliopoteza ajira zao, huku wakiwa wamechangia mifuko ya hifadhi kwa kipindi cha miezi zaidi ya 18. Hawa watalipwa asilimia 33 ya mshahara wa mwisho kwa kipindi cha miezi 6,”

“Kipindi hicho cha miezi 6 kikiisha, mtu huyo kama hajapata ajira atawekwa katika hatua nyingine ambapo ataruhusiwa kuchukua nusu ya fedha alizochangia katika kipindi chake cha ajira,” alisema Mushi.

Akizungumzia wale waliopoteza ajira zao wakiwa hawajafikisha kipindi cha miezi 18, Mushi alisema kuwa wataruhusiwa kuchukua asilimia 100 ya fedha walizochangia kipindi chote walipokuwa kwenye ajira.

“Watu hao wataruhusiwa kuchukua fedha zao kwa asilimia 100 ambazo walichangia kipindi wakiwa waajiriwa. Hata hivyo, napenda kuwaambia Watanzania kuendelea kuichangia mifuko hiyo kwani ina manufaa zaidi nyakati za uzeeni baada ya kustaafu,” alisema Mushi.


Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Tathmini wa SSRA, Ansgar Mushi akitoa mada katika warsha hiyo.

Waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.

Waandishi wakiwa kwenye semina hiyo

Semina ikiendelea.

Waandishi wa habari wakichukua mambo kadhaa kwenye semina hiyo.

Wanahabari wakiwa makini katika semina hiyo.

Maswali yakiulizwa.

Taswira meza kuu katika semina hiyo.

Picha ya pamoja waandishi wa habari na maofisa wa SSRA.
Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062

Mfumo mpya wa kuhakiki uhalali wa bima za vyombo vya moto

Mamlaka ya Bima (TIRA) inakuletea mfumo wa kuhakiki bima za vyombo vya moto (gari, pikipiki, bajaj nk) yaani TIRA MIS. Jinsi ya kutumia mfumo huu wa kielectronik ni kama ifuatavyo:

1. Ujumbe Mfupi wa Simu ya Mkononi (SMS)


  • Andika neno STIKA acha nafasi
  • Andika Namba ya Stika i.e. STIKA 8091390 
  • Itume kwenda namba 15200

Utatozwa TSHS 100 kwa ujumbe. Baada ya muda utapokea ujumbe wenye taarifa za uhalali wa stika pamoja na bima ya chombo chako.

2. Tovuti ya https://mis.tira.go.tz

  • Bofya Hakiki Stika ya Bima|Validate Motor Insurance Sticker, kisha ingiza namba ya stika na bofya Hakiki|Validate.

Kama taarifa zako sio sahihi wasiliana na kampuni iliyokukatia bima au toa taarifa Polisi kuhusiana na aliyekuuzia bima hiyo.

EPUKA BIMA BANDIA, KATA BIMA HALALI KWA USALAMA WA CHOMBO CHAKO NA ABIRIA


[video] Hotuba ya Rais Magufuli ya kuzindua ndege za ATCL Bombardier Q400


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.