Maelezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhusu matumizi ya mafuta lita 1,900

Athuman J. Kihamia
Athuman J. Kihamia
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Barua zote zitumwe kwa:
            Mkurugenzi wa Jiji,
            20 Barabara ya Boma,
Simu:

Nukushi:
+255 27 2548072/2503494 (Director)
+255 27 2544330 (General)
+255 27 2545768
             S. L. P.  3013,
             23101 ARUSHA,
Barua Pepe:  [email protected]
Tovuti:  www.arushacc.go.tz
Unapojibu tafadhali taja:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ndugu Athuman J. Kihamia anapenda kukanusha na kutoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu matumizi ya mafuta lita 1,900. Halmashauri ya Jiji la Arusha ina jumla ya Idara 13 na Vitengo 5. Idara ni Utawala, ujenzi, Fedha, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Maendeleo ya Jamii, Afya, Usafishaji na Mazingira,
Mipango miji, Mipango Takwimu na Ufuatiliaji na Maji.

Vitengo ni Ugavi, Ukaguzi wa Ndani, Sheria na Uchaguzi.

Katika Idara zote kuna jumla ya magari 48 mitambo 5 na wastani wa matumizi ya mafuta kwa Idara zote ni lita 18,900 kwa mwezi na Idara zenye matumizi makubwa ni ujenzi na usafishaji na mazingira hii inatokana na Idara hizi kutumia idadi kubwa ya malori na mitambo katika kutekeleza shughuli zake. Mafuta yanaweza kununuliwa kwenye vituo binafsi endapo itatokea dharura na GPSA inakosa mafuta na manunuzi yatafanywa kwa kuzingatia bei isiyozidi viwango vya GPSA.

Baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema wanasambaza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kutokana na juhudi mbalimbali ambazo Mkurugenzi amekuwa akizifanya za kutatua kero mbalimbali kwa kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima zikiwemo posho mbalimbali za watumishi na Waheshimiwa Madiwani. Fedha nyingi huelekezwa katika huduma mbalimbali za jamii kama vile afya na elimu.

Hata hivyo kumekuwepo baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu ambao wamejipanga kuchafua kila jambo jema linalofanywa na Mkurugenzi wa Jiji nia yao kuu ikiwa ni kumtoa kwenye lengo kuu la kuwahudumia wananchi bila ubaguzi wa aina yoyote, kusimamia miradi ya maendeleo na matumizi ya fedha zinazotokana na kodi za wananchi na ruzuku toka Serikali Kuu zilizokuwa zikitumika kinyume na utaratibu.

Aidha Mkurugenzi Kihamia amekuwa akipokea jumbe za vitisho na matusi kutoka kwa baadhi ya Madiwani lengo likiwa ni kudhoofisha juhudi anazozifanya za kuliweka Jiji katika mstari.

Tangu Mkurugenzi Kihamia alipoteuliwa amekuwa akisisitiza kufuatwa kwa kanuni, sheria, taratibu na miongozo na kuwachukulia hatua wale wote waliokwenda kinyume na utaratibu ikiwepo kurejeshwa posho zinazolipwa kinyume na taratibu kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na kufuta posho zisizokuwa za lazima zilizokuwa zikilipwa kwa Maafisa mbalimbali wa Jiji. Pia anatoa rai kwa watumishi wa Jiji wenye tabia yakutoa nyaraka za Serikali kinyume na sheria na kusambazwa katika mitandao ya jamii waache tabia hiyo kwani kosa la jinai na atakayegundulika atawajibika kwa mujibu wa sheria zilizopo. Ndugu Kihamia ameahidi kuwa kumchafua katika mitandao ya kijamii hakutapunguza dhamira yake ya kuwahudumia wananchi kwa weledi na uadilifu kwa kutenda haki bila kumwonea mtu yeyote.

Tangu alipofika Jiji la Arusha mwezi Julai 2016 Mkurugenzi hajawahi kuidhinisha mafuta, wala posho kwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya, wala kwa Mkuu wa Mkoa ambazo hazikuhusiani na shughuli za Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Hivyo wananchi wanaombwa kupuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli wowote na zina lengo la kumchafua Mkurugenzi huyu.

Frank R. Sanga
Afisa Tawala, Halmashauri ya Jiji
Arusha.

05 Oktoba 2016

fastjet orderd to compensate passengers following flight cancellations

Zanzibar — Aviation consumers' rights body has ordered FastJet, a budget airline, to compensate passengers for the inconvenience after canceling flights without notifications.

The airline canceled and rescheduled Dar-Mwanza and Dar-Mbeya flights on September 28 without notifying passengers.

The passengers later filed a complaint to Tanzania Civil Aviation Authority Consumer Consultative Council (TCA-CCC) which investigated the matter and established passengers' grievances.

TCAA-CCC Deputy Executive Secretary Debora Mligo said in a statement released today that the airline is supposed to pay the compensation according to the law of the land. Also "FastJet ticket sales should go concurrent with the number of seats available and should inform passengers when there are flight changes or cancellations--passenger has the right to be informed," Ms Mligo said.

The airline also was directed to educate their staff to use a customer-based language when addressing passengers during flight changes, delays and cancellations.

The body received complaints from stranded passengers on September 28 who were traveling between Dar-Mbeya and Dar-Mwanza that the airline rescheduled the flights without notifying them.

Also the passengers complained on harsh language used by the FastJet staff when addressing the issue and ignored them as though they have no right to know what was going on.

In May this year, Kisutu Magistrate Court ordered the airline to pay a passenger 30m/- as compensation after failing to inform him following a flight reschedule. The court also ordered the refund of customer's fare 43,000/- plus extra 339,000/- he spent on purchasing a ticket from another airline.

In February this year the airline was on spot after Kenya Civil Aviation Authority (KCAA) warned the airline against publication of misleading adverts which indicate ticket prices that are exclusive of taxes and fees in a bid to attract customers.

KCAA said failure to abide by existing aviation, consumer protection and competition laws could see the airlines fined or even have their licences revoked.

Moreover, Fastjet Africa recorded a 2016 first-half 15 million US dollars (about 30bn/-) net loss, reversed from a net profit of 6.4 million US dollars (13bn/-) for the year-end period. The first-half revenue rose slightly to 33.1 million US dollars (66bn/-) compared to 31.5 million US dollars (62bn/-) last year.
 • By Issa Yussuf , TheDaily News via AllAfrica

Job for a UK curriculum primary year 4 teacher - January 2017 - Tanzania

Job description

Position: Primary Year 4 Teacher

Required: January 2017

Curriculum: UK curriculum

Location: Tanzania

Experience Excellent NQT's considered.

School Vision / Ethos: This ambitious and expanding International school seeks to provide an international education of world class standards for international and local children using a British curriculum. They have a purpose-built school with some of the best sports facilities in Tanzania. This is a new school adding a year at a time, opening Grade 9 in 2017, following the IGCSE curriculum and two years later the IB diploma. They already have a reputation as a school with high standards in which all children make progress.

Tanzania is a stunning country in East Africa. This school located in the culturally diverse and thriving city of Dar es Salaam. Boasting bustling craft markets, restaurants and nearby beaches. Dar is a vibrant hub for further travel - the exotic Zanzibar is a cheap ferry ride away.

Requirements: Teachers with experience are preferred but excellent newly qualified teachers can be considered. You should have UK curriculum experience ideally however, other curriculum experience will still be considered. You need to be flexible and adaptable - Africa is not for everyone but for those with an adventurous spirit and an attitude of openness will thrive. You should be committed to your teaching and to nurturing inquisitive minds.

Package: Monthly salary after tax from approximately $1600 US per month (dependant on experience). *Please note cost of living is VERY LOW and you will likely save more than $1000 of your salary monthly. Accommodation allowance is provided and is usually in a 2 bed house or apartment (fully furnished and normally includes cleaner and gardener). You will receive International medical insurance. Tuition is free for up to 2 dependents.

Tanzania plants its first GMO research crop

Tanzania planted its first genetically modified maize research trials today under an initiative that is building a new model for advancing agricultural innovation through public-private partnerships.

The confined field trial, a pre-cursor to commercialization, will demonstrate the effectiveness and safety of a drought-tolerant GM maize hybrid developed by the Water Efficient Maize for Africa (WEMA) project.

Some 300 million Africans depend on maize as their main food source, but the crop is frequently harmed by drought, leading to hunger, poverty and human suffering. WEMA, a pioneering initiative that pools NGO, corporate and philanthropic resources, seeks to reduce crop failure by developing conventional and GM maize hybrids for smallholder farmers in sub-Saharan Africa.

“It's important that we develop drought-tolerant varieties to ensure food security,” said Dr. Kingstone Mashingaidze, a scientist with the National Agricultural Research Council of South Africa.

Under a royalty-free licensing agreement, seed companies in Tanzania, Kenya, South Africa and Uganda are already growing and selling drought-tolerant maize hybrids developed by WEMA to suit local conditions and branded as DroughtTEGOTM. Mozambique will introduce the TEGO brand seeds this year. The WEMA project has received commercial release approvals for more than 60 TEGO conventional hybrids across the five countries.

The TEGO hybrids caught on quickly as farmers growing the less-productive open-pollinated varieties saw their hybrid-cultivating neighbors reaping bigger harvests.

“I think the WEMA partnership is making a difference,” said Mark Edge, director of WEMA partnerships at Monsanto. “The TEGO hybrids’ improved performance provides a lot of promise and hope for smallholder farmers in Africa.”

The GM side has proven more challenging. Despite political constraints in Africa, WEMA moved forward with biotechnology because it “offered the promise to add still greater drought tolerance to the already improved [conventional] hybrids, resulting in an even more substantial gain for drought tolerant maize,” according to a case study authored by the WEMA partners. “Scientifically, the optimal approach was to use both techniques together.”

Seed companies in South Africa, which has a longer history with GM crops, were the first to take advantage of the royalty-free GM licensing agreement. They will begin selling royalty-free transgenic maize seeds with drought-tolerant and insect-resistant traits this year. Kenya is expected to follow suit in 2017.

Mozambique has approved field trials for drought-tolerant GM maize, which will begin either this planting season or next, pending issuance of a seed import permit.

Uganda has conducted numerous successful field trials, but since it lacks a national biosafety law, it has been unable to commercialize GM seeds for sale to farmers. “Eventually, biotech investment may be at risk there because there is no commercial path forward,” Edge said. “We may be getting close to that point. The horse has been led to water many times, but the horse is not drinking.”

That leaves Tanzania, which this week planted its first GM research crop — a drought-tolerant white maize. Pending the results, trials of an insect-resistant variety could begin next year.

“We have had successful meetings with local leaders, local government authorities, farmers and communities around the confined field trial (CFT) area,” said Philbert Nyinondi, coordinator of the Open Forum on Agricultural Biotechnology (OFAB) programming committee in Tanzania. “We must be transparent to maintain trust. We are informing them on the importance of the trial, and the process of bringing GM crops to commercialization.”

However, anti-GMO activists do not in support this agricultural advancement in Tanzania and have urged the public to protest the government’s issuance of the CFT permit.

Though WEMA, which is funded by the Bill & Melinda Gates Foundation, Howard G. Buffett Foundation and United States Agency for International Development (USAID), is providing a window of opportunity for the advancement of crop biotech in sub-Saharan Africa, “that window will close eventually,” Edge said.

“That’s the message the Africans need to hear,” he said. “They do not have unlimited time on this. No donor should have unlimited patience.”

A combination of altruism and business interests motivated Monsanto to participate in WEMA, which is led by the nonprofit African Agricultural Technology Foundation (AATF). Other partners are the International Maize and Wheat Improvement Center (CIMMYT) and the National Agricultural Research Systems (NARS) from the five participating sub-Saharan nations. AATF manages all the seeds.

In 2004-05, Monsanto offered to share its newly discovered drought-tolerant traits for humanitarian purposes. That proved a good match with the Gates foundation, whose officers had identified drought tolerance as one of the most important crop improvement goals for helping smallholder farmers in Africa.

WEMA was formed in 2008, introducing a new model for public-private partnerships (PPPs) in agriculture. Though the road has been rocky at times, the collaboration is providing tangible proof that public and private entities can work together for the public good.

“There needs to be a benefit for each member participating,” Edge said. “Otherwise you get platitudes, but no real action. There is such a strong desire across businesses, NGOs, government and Africans themselves. They want to find ways to do things better.”

He thinks more PPPs are likely as corporations strive to be socially responsible, and foundations and NGOs focus on creating systems and businesses that can sustain themselves through profitability.

“I think it’s a really good thing, and I’m hoping the case study with WEMA will help people understand what you need to do,” Edge said. “It’s not about perfection; it’s about success. There is a way to accomplish our common goals.”

By Joan Conrow via allianceforscience.cornell.edu

Taarifa ya serikali kuhusu kuteswa kwa Watanzania nchini Oman na Mashariki ya Kati

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijiji Dar es Salaam tarehe 05 Oktoba, 2016.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU TAARIFA ZA KUTESWA KWA WATANZANIA WANAOKWENDA KUFANYA KAZI OMAN NA NCHI NYINGINE ZA MASHARIKI YA KATI


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inachukua fursa hii leo kupeleka taarifa kwa Umma kupitia vyombo vya habari juu ya habari zilizochapishwa katika gazeti moja kuhusu mateso wanayopata Watanzania wanaofanya kazi za ndani nchini Oman ili kuondoa utata uliojitokeza kutokana na habari hiyo. Aidha, Wizara inapenda kutoa uelewa na ufafanuzi ili kupata ushirikiano kutoka kwa wananchi katika kukabiliana na changamoto wanazopata Watanzania nje ya nchi wakitafuta maslahi ya kiuchumi.

Ndugu Wanahabari,

Jana siku ya Jumanne tarehe 4 Oktoba 2016, Gazeti la Tanzania Mpya katika toleo lake Na.23 katika ukurasa wake wa mbele lilichapisha habari yenye kichwa cha maneno watanzania wateswa nchini Oman na kuwa wengine hunyofolewa figo zao na kupewa ndugu wa waajiri wenye mahitaji. Habari hii ambayo imeendelea ukurasa wa pili na watano imeambatana na picha ya Mheshimiwa Dr. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na hivyo kuwafanya wasomaji wengi kuamini kuwa taarifa ile imetolewa na Mheshimiwa Waziri.

Kitendo hiki cha kuchapisha habari hii na kutumia picha ya Mheshimiwa Waziri kimeleta usumbufu kwa mheshimiwa Waziri na pia kwa wasomaji kwani wengi wameamini kuwa taarifa ile imetolewa na Mhe. Waziri.

Wizara inapenda kuutangazia umma kwa ujumla kwamba Mheshimiwa Dr. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hausiki na taarifa hiyo na wala hakuwahi kuzungumza na mwandishi wa habari wa makala husika na kuwa yaliyomo kwenye taarifa hiyo ni maoni binafsi ya mwandishi na gazeti husika na kwa vyovyote vile hayawakilishi msimamo wa Mheshimiwa Waziri na Wizara anayoiongoza na serikali kwa ujumla.

Habari hii ni mfululizo wa uchapishaji wa habari zenye maudhui kama haya kwenye baadhi ya magazeti na mitandao ya kijamii ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kina na kuwa na taarifa sahihi kuhusu mada husika. Taarifa hizi zinaweza kuharibu uhusiano mzuri na wa kindugu uliopo baina ya Tanzania na Oman kati ya serikali na serikali na pia watu wake ambao wengi wana uhusiano wa damu

Ndugu Wanahabari,

Baada ya kusema hayo sasa naomba kutoa taarifa ya kina kuhusu suala zima la watanzania wanaokwenda kufanya kazi nchini Oman na nchi nyingine za mashariki ya kati na utaratibu ambao serikali imeweka katika kuratibu zoezi zima

Eneo la mashariki ya kati linaundwa na nchi za Oman , Saudi Arabia, Qatar, Bahrain, Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu ( Abu Dhabi, Dubai, Ajman, Al Ain, Fujairah, Ras Al Khaimah na Sharjah), Lebanon, Syria, Iran, Iraq, Yemen.

Nchi hizi kwa kiasi kikubwa ni tegemezi ya nguvu kazi kutoka nje ya eneo hili na hivyo kuwa soko kubwa la ajira kwa nchi mbalimbali, ajira hizi ni kuanzia watendaji wakuu, watendaji wa ngazi mbalimbali hadi wahudumu na watumishi wa majumbani
Kati ya nchi za mashariki ya kati Oman imekuwa na uhusiano wa karibu sana ambao ni wa kihistoria na kidamu, ambapo nusu ya familia za Oman asili yake ni Tanzania na hivyo kufanya kuwa na muingiliano wa karibu.

Kwa kuzingatia uhusiano huu Oman imekuwa ikipokea wafanyakazi mbalimbali kutoka Tanzania katika kada za madaktari, walimu, wauguzi, wahadhiri, wapishi, wahudumu katika masaluni ( nywele na kuchora Heena), madereva, wahudumu wa mashamba na bustani na watumishi wa nyumbani.
Kuanzia miaka ya 2010 wimbi la watanzania kwenda kufanya kazi Oman lilishika kasi na hivyo kuongeza idadi ya watanzania wanaoingia Oman kwa ajili ya kufanyakazi mbalimbali hasa majumbani ( Housemaids) , kufuatia wimbi hili ubalozi ulianza kupokea watanzania wanaolalamikia mazingira magumu ya kufanyia kazi, malalamiko yao yalihusu kufanya kazi masaa mengi, mshahara mdogo, kukosa mapumziko, kutoruhusiwa kutoka nje ya nyumba, kufanya kazi zaidi ya nyumba moja , kunyanyaswa kijinsia , kufanyishwa kazi ziadi ya kazi za Housemaid.

Katika mazungumzo na watumishi husika, ubalozi ulibaini kutokuwepo kwa utaratibu maalum wa kuratibu ajira zao kuja Oman, hivyo basi Ubalozi kwa kushirikiana na wadau wengine hapa Tanzania (Uhamiaji, Wizara ya Kazi, Wakala wa huduma za ajira Tanzania (TAESA) , Kamisheni ya kazi Zanzibar, Mamlaka ya viwanja vya ndege, Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa) vilianza utekelezaji wa utaratibu wa kufuatwa kwa wale wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi na hasa Oman.

Ndugu wanahabari

Chini ya utaratibu huu, Raia wa Oman mwenye nia ya kumwajiri mtanazania anapaswa kwenda Ubalozini na kujaza fomu ya kuomba kumwajiri mtanzania, baada ya fomu yake kuridhiwa na Ubalozi atapewa mkataba ambao atajaza na kuurudisha Ubalozi akiambatanisha nakala ya kitambulisho chake cha taifa, Uthibitisho wa makazi ( bili ya maji au umeme), nakala ya pasipoti ya mfanya kazi, hati ya kiapo na dhamana ya rial 100 .
Baada ya Ubalozi kuridhika na vielelezo vyake, ubalozi utapitisha mkataba na kumtaka mwajiri husika kuuwasilisha Tanzania kwa mtumishi husika ambae ataupokea na kuuwasilisha TAESA au kamisheni ya kazi ambao nao watamuhoji muhusika na kujiridhisha kuwa anaulewa wa kazi anayokwenda kufanya pamoja na masharti yake, wakijiridhisha watampa kibali ambacho ni barua ikimuomba kamishna wa uhamiaji amruhusu muhusika kusafiri nje ya nchi baada ya kutimiza utaratibu uliowekwa.

Ndugu wanahabari

Utekelezaji wa utaratibu huu umekuwa na mafanikio na pia changamoto, kwa kiasi kikubwa uratibu huu umeweza kupunguza matatizo waliyokuwa wanayapata ndugu zetu, kuongeza mshahara wao, kuwapatia haki ya kupumzika na mawasiliano na pia kuongeza uelewa wa watanzania juu ya haki zao na namna ya kuzipata pale zinapokiukwa.

Kufuatia kufanikiwa kwa utekelezaji wa utaratibu huu nchini Oman, serikali sasa imeanza kutumia utaratibu huu katika nchi yingine za mashariki ya kati

Pamoja na mafanikio kumekuwa na changamoto kama vile baadhi ya watu kukwepa kufuata utaratibu husika kwa kuwapitisha wahusika njia za panya, kughushi nyaraka husika, kuwepo kwa mawakala bubu na kuwa na tamaa ya kufanikiwa haraka, watanzania kutokuwa na ujuzi au uzoefu wa kazi wanayokwenda kuifanya, kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa maadili kama vile wizi, udanganyifu nk

Ndugu wanahabari


Ndugu wana habari, naomba nitumie nafasi hii pia kutoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya kunyang’anywa hati za kusafiria, huu ni utaratibu unaofuatwa na waajiri katika nchi zote za mashariki ya kati ambapo katika kipindi chote cha mkataba hati ya kusafiria huwekwa chini ya uangalizi wa mwajiri, utaratibu hufanyika kwa waajiri wa aina zote kwa maana ya taasisi ( Wizara, Idara, mashirika binafsi ) na watu binafsi, hivyo tunaomba ieleweke kuwa ni suala la utaratibu

Ndugu wanahabari

Katika kupambana na changamoto hizi serikali imejipanga kuimarisha udhibiti wa utekelezaji wa utaratibu huu kupitia vikao mbalimbali vya wadau. Vikao hivyo viliazimia Kuandaa mtaala wa kuongeza stadi na ujuzi kwa wanaokusudia kufanya kazi za Housemaid
 • Kuanza kutumia mawakala rasmi wa ajira walioandikishwa na mamlaka husika
 • Kuwepo mkataba wa ajira unaotambuliwa na Mamlaka za Nchi unayotaka kwenda. Kwa hapa nyumbani mamlaka zinazoweza kusaidia ni pamoja na Ofisi za Ubalozi za Nchi husika, Wakala wa Ajira Tanzania - TAESA (Tanzania Bara) au Kamisheni ya Kazi (Zanzibar); Mtanzania asikubali kuanza safari bila kupata mkataba na Kibali kutoka TAESA au Kamisheni ya Kazi. kila Ubalozi katika nchi za Mashariki ya Kati uandae mikataba ya kazi kutokana na muongozo uliokubaliwa na wadau wote.
Vilevile, kupitia kwenu wanahabari, tunatoa wito kwa watanzania wote, tuwe makini pale tunapopata fursa za kazi nje ya nchi. Kama nilivyosema hapo awali, ni muhimu kujiridhisha kwamba mambo yote ya msingi yanayohusiana na ajira hizo yamekaa sawa ikiwa ni pamoja na:
 • Kuzingatia na kufuata utaratibu uliowekwa na serikali, na wala mtanzania asikubali kuambiwa kuwa mktaba ataukuta huko anakokwenda au kusafiri kupitia nchi jirani kwenda kuanza kazi nje ya nchi,
 • wito kwa Taasisi zote zinazoratibu safari za Nje katika viwanja vya ndege au vituo vya mipakani kuhakikisha hawamruhusu mtu kusafiri nje kwa nia ya kufanya kazi bila kuwa na vibali husika.
 • Kutafuta msaada wa kupata uthibitisho kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki au Wizara ya Kazi kama kweli kazi uliyoahidiwa ipo- Wizara yetu itaweza kutumia Balozi zetu kuthibitisha;
 • Na pale unapokwenda Nje, ni muhimu kuhakikisha kwamba unajisajili kweye ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo katika nchi hizo au ubalozi wa Uingereza mahali ambapo hakuna Ubalozi wa Tanzania.
 • Kutokubali kuweka hati yako ya kusaifiria kama rehani kwasababu yoyote ile;
Katika kupata suluhisho la kudumu ikiwa ni pamoja na kuwasaidia Watanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi, Wizara kwa kushirikiana na wadau husika inaendelea na jitihada za kusaini Mikataba ya Ushirikiano katika Sekta ya Ajira na Kazi baina ya Serikali ya Tanzania na nchi hizo kama ule wa Tanzania na Qatar. Kusainiwa kwa mikataba hiyo sio tu kutasaidia kupata fursa za ajira katika nchi hizo bali kutailazimu Serikali ya nchi hizo kushirikiana na Wizara pindi raia wao watapokwenda kinyume na mikataba ya ajira iliyopo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 05 Oktoba 2016.


Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano, kutoka kulia ni Bw. Hangi Mgaka, Bw. Odilo Fidelis na Bw. Fred Maro.

Mkutano ukiendelea

Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Wadhamini CUF yapinga maamuzi ya juzi na kuionya CHADEMA

Bodi ya wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF), imegawanyika vipande viwili kutokana na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya chama hicho.

Kugawanyika kwa bodi hiyo kumekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wake, Abdallah Katau kutangaza kutomtambua Profesa Lipumba, huku baadhi ya wajumbe wakipinga tamko hilo wakiliita ni batili kwa mujibu wa katiba ya CUF.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wajumbe wenzake, mjumbe wa bodi ya chama hicho, Peter Malebo, alisema hawatambui tamko lililotolewa na mwenyekiti wao kwani bodi hiyo inajiandaa kuwakutanisha mwenyeki wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad ili kuweza kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

Alisema kutokana na hali hiyo, watakaa na wajumbe wenzao na kujadili suala hilo kabla ya kuwaita viongozi hao ikiwa ni pamoja na kujadili ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.
“Tutakaa na wajumbe wenzetu ili tuweze kujadiliana mgogoro wa viongozi wetu pamoja na kupitia maazimio ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ili tuweze kupata hoja ya kuwahoji kwenye kikao hicho.
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa chama chetu kinarudi kwenye hadhi yake kama ilivyokua awali kuliko hivi sasa ambapo kimegubikwa na mgogoro wa uongozi wa kitaifa,” alisema Malebo.
Alisema ikiwa watashindwa kupata mwafaka wataitisha Mkutano Mkuu wa dharura ili waweze kuwaeleza wajumbe wa mkutano huo hali ya chama na hatua za kuchukua.
“Kama mwafaka hautapatikana katika kikao hicho, tutalazimika kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu ambao pamoja na mambo mengine, tutawaeleza mgogoro wa viongozi wetu ili wajumbe waweze kutoa uamuzi,” alisema.
Alisema Bodi ya Wadhamini wa CUF inaundwa na wajumbe wanane ambapo kutoka upande wa bara ni watano na Zanzibar watatu.

Aliwataja wajumbe hao kuwa ni pamoja na Abdalah Katau, Peter Malebo, Ally Mbarouk, Amin Mrisha, Zacharia Kwangu, Yohana Mbelwa na Dk. Juma Muchi.

Alisema mpaka sasa bodi hiyo imegawanyika ambapo wajumbe kutoka Zanzibar wanamwunga mkono Maalim Seif huku wale wa bara wakimwunga mkono Profesa Lipumba hali inayozidi kupandisha joto ndani ya chama hicho.
“Kinachotutafuna ndani ya CUF ni ubaguzi unaoonyeshwa waziwazi kutoka kwa viongozi wa Zanzibar jambo ambalo limechangia kila mtu kuwa upande wake, lakini tutaitana na kujadiliana suala hili ili tuweze kupata mwafaka,” alisema.
Alisema bodi hiyo inafanya kazi ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo iliteuliwa mwaka 2011 na itamaliza muda wake, Desemba mwaka huu.

Atoa onyo CHADEMA

Katika hatua nyingine, Malebo aliwataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoingilia mgogoro huo kwa madai hauwahusu.

Alisema, kitendo cha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kujitokeza hadharani na kudai hamtambui Profesa Lipumba inaonyesha wazi kuwa ameshiriki kuongeza mgogoro ndani ya chama hicho.
“Mbowe haumhusu mgogoro wa viongozi wa CUF, huu ni mgogoro wa ndani ya chama, tunamshangaa kujitokeza hadharani na kudai hamtambui Lipumba, yeye ni nani ndani ya chama?, tunamuonya asirudie,” alisema.
Alisema, chama hicho kimejipanga kupambana na watu wanaoingilia mgogoro wao wakati si wanachama wa chama hicho, jambo ambalo limechangia kuendelea kuchochea vurugu hizo.

Taarifa ya habari ChannelTEN Oktoba 5, 2016


Mke wa Waziri aandika barua ya kuacha kazi ATCL baada ya kauli ya Rais Magufuli

MKE wa waziri mwandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tano (jina tunalihifadhi kwa sasa) aliyekuwa akifanya kazi Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ameacha kazi.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya shirika hilo vililiambia Nipashe jana kuwa mke huyo ambaye amedumu ATCL kwa zaidi ya miaka 20, aliandika barua ya kuacha kazi ghafla.

Kuacha kazi kwa mtumishi huyo (jina tunalihifadhi kwa sasa) kumekuja siku chache tangu Rais John Magufuli, bila kutaja jina, kusema anashangaa kuona wake wa baadhi ya mawaziri wake wanafanya kazi katika shirika ambalo halifanyi kazi vizuri.

Rais Magufuli aliyasema hayo Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizundua ndege mbili mpya ambazo zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya 'kulifufua' shirika hilo.

Car battery hydrogen sulfide fumes cause deaths of mom and daughter


[...] 

After a rigorous investigation, a medical examiner said Tuesday the deaths were caused by hydrogen sulfide intoxication, likely as the result of a defect in the car’s battery.

The colorless gas has a pungent odor and first responders were forced to retreat from the vehicle after they approached it and saw Lincoln and her daughter, who did not appear to be breathing.

In a release obtained by InsideEdition.com, the Orange-Osceola Medical Examiner's Office called the manner of death "unprecedented."
"While the source [of hydrogen sulfide] is most likely to be attributed to a malfunction of the battery, this remains to be confirmed. This case is unprecedented.
"Despite the large numbers of lead acid batteries in use worldwide, no other fatalities of this type have been reported. Similar batteries, under experimental conditions, have been shown to produce hydrogen sulfide gas," the statement read.
"The battery was not the original battery for the vehicle, [or] the correct battery and is believed to have malfunctioned," the statement said.
The statement also suggested the deaths were preventable.

Mcheza kikapu apata udhamini kusoma Marekani na kutakiwa aitangaze Tanzania


Na: Geofrey Tengeneza

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imemtaka kijana wa kitanzania ambaye pia ni mchezaji wa mpira wa kikapu Underson Simon (19) kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii nchini Marekani kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi kuitembelea Tanzania.

Underson ambaye ni tunda la kituo cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park cha jijini Dar es salaam amepata udhamini wa masomo kwenda kusoma shahada ya kwanza ya sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Georgia University kilichoko Atlanta Georgia nchini Marekani.

Akizungumza wakati wa kumuaga Underson ofisini kwake jijini Dar esalaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi mchezaji huyo anayechipukia wa mpira wa kikapu nchini anayechezea timu mpira wa kikapu ya vijana (Vijana Basketball Club) pamoja na kumtaka ajitahidi katika masomo yake, lakini pia amemtaka atumie fursa hiyo na ile ya kushiriki katika mashindano mbalimbali akiwa na timu yake ya chuo kikuu cha Georgia katika mchezo wa kikapu kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii.
“Peperusha vema bendera ya nchi yetu na tumia kila jukwaa utakalopata ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii duniani” alisema Bi Mdachi na kuongeza kuwa TTB inakusudia kuanza mchakato wa kumpa heshima ya kuwa Balozi wa heshima wa Utalii wa Tanzania.
Mkurugenzi huyo wa TTB alimkabidhi mchezaji huyo wa mpira wa kikapu nchini, bendera ya Taifa na vielelezo kadhaa vinavyoelezea utalii wa Tanzania ili visaidie kumjengea uelewa zaidi kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania.

Kwa upande wake kijana huyo Underson Simon alielezea kufurahishwa kwake kupata nafasi hiyo lakini pia kutambuliwa na TTB kama mmoja wa wanamichezo wa kitanzania wanaoweza kuvitangaza vema vivutio vyetu vya utalii nje ya nchi na hivyo kuchangia kukuza sekta ya utalii.

Naye mwalimu mwandamizi (kocha) wa mpira wa kikapu wa kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Bahati Mgunda amesema kituo chake kinajivunia mafanikio hayo ya mmoja wa wachezaji wao kupata ufadhili huo wa masomo ambao umetokana hasa na umahiri wake katika mchezo huo.

Simon ameondoka saa 9.00 alfajiri ya leo kwa shirika la ndege la Uturuki kuelekea nchini Marekani tayari kujiunga na chuo kikuu hicho cha Georgia.


Taarifa ya Ofisi ya takwimu ya aina ya wadadisi itakaowatambua na kuwatumia


Apply for TEDGlobal 2017 Fellowship to Attend TEDGlobal Conference in Tanzania


Location: Arusha, Tanzania.

Date: August 27 – 30, 2017.

Are you an inventor or filmmaker? A scientist or entrepreneur? Do you have a unique approach to your work that is worth sharing with the world? Could you benefit from the TED platform and the support of a dynamic global community of innovators? If yes, you should apply to be a TEDGlobal Fellow.

This year, TED is looking for new, extraordinary thinkers from around the world to join the Fellows program at the upcoming TEDGlobal 2017 conference in Arusha, Tanzania.Do you think you have what it takes?

The second major TED conference in Africa, TEDGlobal 2017 will focus on the challenges and opportunities facing the continent. All talented innovators in their fields – science, art, technology, entrepreneurship, film and beyond – are encouraged to apply to become a TED Fellow, especially those working on the African continent. If selected, you will attend the TEDGlobal 2017 conference, and participate in a Fellows only pre-conference designed especially to inspire, empower and support your work. Fellows will also deliver a TED talk at the conference, to be filmed and considered for publication on TED.com

TEDGlobal2017 themed: “Builders. Truth-Tellers. Catalysts.”

Twenty fellows will be selected to attend the TED Global conference to be held August 27-30, 2017. Participants will also have the opportunity to attend pre-conference programs with training by speakers.

Here is what you can expect at the TEDGLobal:
 • A four-day stage program
 • Entertainment
 • Simulcast lounge
 • Dinners, parties and tours
 • TED gift bag
 • TEDConnect
Eligibility:

TED look for different applicants than many other leadership-oriented programs. Instead of business people, professionals, policy wonks and government officials, the TED Fellows program focuses on doers, makers, inventors, advocates, filmmakers and photographers, musicians and artists, scientists, entrepreneurs, NGO heads, and human rights activists.

In addition to impressive accomplishment, fine character and a good heart are two very important traits we look for in a every potential TED Fellow. More than anything, this focus on character has defined the success of the TED Fellows program.

Application Process:

Apply online here. The online application includes answers to general questions, short essays and three references.

TEDGlobal 2017 will be an event not to be missed! Questions? Send a note to [email protected]

Visit Official Page

Job opportunities at MUHAS

Muhimbili University of Health and Allied Sciences

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES

Muhimbili University of Health and Allied Sciences is inviting applications from suitably qualified Tanzanias to be considered for employment to fill vacant posts listed hereunder for MUHAS Academic Medical Centre (MAMC) at University New Campus of Mloganzilla.

1. Medical Specialist II

Holder of Master of Medicine or its equaivalent in the respective field of specialization and a working experience of at least one year its attainement. The Candidate must be fully registered by the Medical Council of Tanganyika. Possession of PhD will bw an added advantage.

2. Medical Officer II

Holder of MD or their equivalent from a recognized Institution. Must have completed one year Internship and be registered by the Medical Council of Tanganyika as a Medical Officers

3. Nurse Specialist II

Holder of a Masters Degree in any of the Clinical Nursing/ Midwifery specialties from a recognized institution and is registered with Tanzania Nurse and Midwives Council.

4. Nursing Officer II

Holder of a Masters Degree in any of the Nursing/ Midwifery from a recognized institution plus successful completion of internship. Must be registered with Tanzania Nurse and Midwives Council.

5. Assistant Nursing Officer II

Holder of Diploma in Nursing from a recognized institution and is registered with Tanzania Nurse and Midwives Council.

6. Pharmacist II

Holder of a Degree in Pharmacy (B.Pharm) or equivalent from a recognized institution. In additional the candidate must have completed one year of internship and is registered by the Pharmacy Council of Tanzania.

7. Pharmaceutical Technician II

Holder of Diploma in Pharmacy of Pharmaceutical Management from any recognized institution. Must be registered by the Pharmacy Council of Tanzania.

8. Health Laboratory Scientist II

Holder of Bachellor Degree in Medical Laboratory Sciences or Bachelor of Science in Health Laboratory Sciences or equivalent qualification in relevant field from a recognized institution. Registration with competent professional board is mandatory.

9. Health Laboratory Technologist II

Holder of a Diploma in Medical Laboratory Sciences from any recognised Institution. Must be registered by the Health Laboratory Practitioners Council.

10. Radiographer II

Holder of a Diploma in Radiology from any recognized Institution. Must be registered by the Medical Radiology and Imaging Professionals Council as a Radiographer.

11. Medical Record Technician II

Holder of an ordianary Diploma in Medical in Records or its equaivalent from a recognized instution. Must have computer skills.

12. Health Attendant II

Having 1 year certificate in health related course with an Ordianry Secondary School education.

13. Accountant II

Holder of First Degree in Accountancy or equivalent

14. Drivers II

Holder of Form IV Certificate with passes in Kiswahili and English plus a clean valid Driving License at appropriate class and working experience of at least three (3) years in a similar position and must also posses Trade Test Grade II in Motor Vehicle Mechanics and Driving Certificate Grade II from a recognized Institution such as NIT or VETA

15. Senior Engineer II

Holder of RSc in Mechnaical Engineering, must have been registered as Professional Engineer by relevant ERB.

16. Personal Secretary II

Form IV Certificate with credit passes in Kiswahili and English, plus 80wpm shorthand and 50 wpm typing speed, tabulation and manuscript stage III, secretarial and office procedure stage II. Must have sufficient knowledge in computers in at least word processing spreadsheet, database, e-mails and internet. (Must have computer certificate). Possession of Diploma in Secretarial studies in mandatory.

GENERAL CONDITIONS FOR ALL POSTS:

Applicants must attach an up to date current Curriculum Vitae (CV) having reliable contact postal address, email address and telephone numbers.

Applicants should apply on the strengths of the information given in this advertisement.

The title of the position applied for should be written in the subject of the application letter and marked on the envelop.

Applicants must attach their detailed relevant certified copies of Academic certificates/ transcripts as follows:
 • Postgraduate Degree/ First Degree/ Advanced Diploma, Diploma/ Certificates
 • Form IV and Form VI National Examination Certificates
 • Computer Certificates where applicable
 • Professional Certificates from respective boards where applicable
 • one recent passport size picture and copy of birth certificate
Form IV and Form VI results slip are strictly not accepted. Presentation of forged academic certificates and other information in the CV will necessitate to legal action

Applicants should indicate three reputable referees with their reliable contacts

Certificates from foreign countries should be verified by Tanzania Commission for Universities (TCU) - (Degree Level) or National Accreditation Council for Technical Education (NACTE) -(Diploma Level) or National Examination Council of Tanzania (NECTA) - (Secondary Education).

Women are highly encouraged to apply

Only shortlisted candidates will be informed the date of the interview

APPLICATION LETTERS SHOULD BE POSTED OR HAND DELOIVERED TO THE FOLLOWING ADDRESS on or before 4.00pm on 17th October, 2016 (ie Deadline for receiving application)

THE DEPUTY VICE CHANCELLOR, HOSPITAL SERVICES, MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES – MUHAS,
P. O BOX 65001,
DAR ES SALAAM

Tanzania and Congo sign MoU for joint exploration of hydrocarbon in Lake Tanganyika

(Ecofin Agency) - The Democratic Republic of Congo and Tanzania have entered into a memorandum of understanding (MoU) to explore the petroleum potential of Lake Tanganyika together.

The agreement was signed in Dar es Salaam in the presence of Tanzanian President John Magufuli and Congolese President, Joseph Kabila.

“We have already discovered oil in the western parts of Lake Albert, and there’s a great possibility that there’s also oil in Lake Tanganyika, therefore, joint exploration is the way to go for mutual benefits,” Kabila said.

He added that they also deliberated on a joint partnership as regards the usage of the pipeline currently being built from Uganda to Tanzania to export Congo’s oil from Lake Albert.

East Africa is now been seen as a new hydrocarbon region, following major discoveries of oil in Uganda and natural gas in Tanzania and Mozambique.

In 2011, Tanzania granted oil and gas exploration rights for the northern side of Lake Tanganyika to a subsidiary of Total.

Tanzania also in February, announced that it had discovered 2.17 trillion cubic feet of possible natural gas deposits in an onshore field, increasing its total estimated recoverable natural gas reserves to over 57 tcf, Reuters reports.

By Anita Fatunji, ecofinagency.com

Tambwe: Kama niliwaudhi naomba wanisamehe


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe amewaomba wapenzi na mashabiki wa Simba kutomchukia na kumuona kama adui yao kwa sababu ya bao aliloifunga timu hiyo Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tambwe aliifungia Yanga bao ambalo lilizua utata mkubwa baada ya kudaiwa kabla hajafunga aliunawa mpira.

Bao hilo ndilo lilizua balaa kubwa katika mchezo huo ambapo mara tu baada ya kufunga ziliibuka vurugu kubwa zilizosababisha mashabiki wa Simba kuvunja viti zaidi ya 1,781, wakilipinga.

Hata hivyo baada ya kumalizika kwa mchezo huo mashabiki hao wa Simba waliendelea kulipinga bao hilo huku baadhi yao wakionekana kumchukia mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliibuka mfungaji bora.

Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe ambaye alijiunga na Yanga akitokea Simba, amewataka mashabiki hao kutomchukia na kumuona kama adui yao namba moja kwa sababu ya bao hilo.
Alisema yeye kazi yake ni kufunga haijalishi kafunga kwa njia gani hivyo amewataka mashabiki hao wa Simba kulijua hilo kisha waendelee kumuona kama ndugu yao.
“Binafsi sina uadui na Simba hata kidogo, ila nasikitika kuona baadhi yao wananichukia na kuniona kama adui yao kwa sababu ya bao langu, hakika hiyo siyo sawa.
“Katika mchezo wa soka kazi ya straika ni kufunga na haijalishi amefunga kwa staili gani kama niliwaudhi naomba wanisamehe, ila nawataka wajue kuwa kufunga ndiyo kazi yangu ambayo na nitaendelea kufunga kwa staili yoyote ile ili kuhakikisha naisaidia timu yangu kumaliza ligi kuu ikiwa katika nafasi nzuri na ikiwezekana kutwaa ubingwa,” alisema Tambwe.
Imeandikwa na Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam via GPL