wavuti.com itaadimika

Nashukuru kwa kila mmoja aliyetembelea blogu hii ilipoanzishwa ikiwa nukta77.com hadi sasa wavuti.com

Watembeleaji wa mara kwa mara wa blogu hii mmekuwa marafiki zangu kwa namna mbalimbali. Mnakumbuka vyema kwa jinsi nilivyojitahidi kuhakikisha habari za uhakika zinapatikana kwa wakati, mpaka hapo nilipojaaliwa kupata mtoto na kushindwa kumudu kuendelea kufanya hivyo, kutokana na ukweli kuwa kipaumbele kilibadilika.

Ni kwa sababu hiyo tena, ninalazimika kupunguza zaidi idadi ya kasi ya machapisho hapa kutokana na ajira yangu (ambayo ndiyo chanzo cha kipato kinachoniwezesha si tu kutimiza mahitaji muhimu ya familia, bali pia kuniwezesha kulipia na kuendesha blogu hii kwa 'hobby') kunihitaji zaidi. Sheria za kazi zimebadilika na siwezi kutumia muda wa kazi kufanya shughuli binafsi.

Hivyo basi, kutokana na maelezo hayo, natangaza rasmi kuwa wavuti.com haitakuwa "active" tena, machapisho yatakuwa adimu kwa kuwa nitaendelea tu kuweka taarifa muhimu pale tu ninapopata wasaa wa ziada nje na baada ya majukumu ya ajira na familia. 

Kwa taarifa hii, nakutakieni usomaji mwema wa blogu na tovuti nyingine za habari kwa ajili ya kujua yaliyojiri ndani ya Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi, pale suala linapohusu Tanzania au kugusa maisha ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Wasalaam,
Subi

Mkuu wa Wilaya afunga Chuo cha Ualimu na kuamuru wanafunzi warejeshewe ada

MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deogratius Ndejembi amekifunga Chuo cha Ualimu cha Nkuruma kilichopo Mkoka na kuagiza uongozi wa chuo kurudisha fedha zote za ada walizolipa wanafunzi ili ziwasaidie kulipia vyuo vingine.

Alitoa agizo hilo wakati wa mkutano na wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo hicho kuhusu kutafuta suluhu ya mgogoro ambao ulianza Septemba 16, mwaka huu. Chuo hicho kilidahili wanafunzi 77 kwa lengo la kuwafundisha ualimu, walipofika wakaambiwa wanasoma masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

“Baadaye wakaambiwa wanabadilishiwa masomo sasa wanasoma Maendeleo ya Jamii, hii yote wamefanya kwa kuwa chuo hakina usajili wowote.Ada wamechukua na hakuna kinachoendelea,” alisema Ndejembi.

Ndejembi alifikia hatua ya kukifunga chuo kutokana na wanafunzi kugoma kufanya mitihani ya chuo ya kumaliza mwaka wa masomo kwa madai chuo hakitambuliwi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Alisema kukifungia chuo pekee haitoshi wanatakiwa kurudisha fedha zote za ada walizolipwa na wanafunzi katika mwaka huo wa masomo uliopita ili kuwasaidia kulipa vyuo vingine.

“Kuwarudishia fedha sio mwisho wa jambo hili kwa sababu mmepotezewa muda wenu na haki yenu ,mmeonewa, mmedhulumiwa kwa kusema hivyo namwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya na timu yake kuwakamata sasa hivi na wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria ili haki iweze kutendeka,” alisema.

Amewataja wanaotakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kuwa ni mmiliki wa chuo, Mathew Nkurlu, Msajili wa Chuo, Yohana Michael, Mhasibu Elieth Ruben, wakufunzi Pendael Petro na Christopher Mabatian.

Ndejembi alitaja sababu za kuagiza wakamatwe viongozi hao wa chuo ni kuwa walihusika kushiriki katika kufanya udanganyifu na kuwatapeli wanafunzi hao huku wakijua kinachoendelea.

Aidha, alisema serikali itawasaidia katika utaratibu wa kupata vyuo vingine kwa wale wenye sifa za kujiunga na vyuo katika kozi ambayo walianza kusoma.

Alisema kama ikitokea chuo hakina fedha za kuwarudishia wanafunzi, majengo yao yatatumika kama dhamana ya ada kwa vyuo ambavyo vitawapokea wanafunzi hao. Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, Mhoja Matando aliishukuru serikali kwa kuwasaidia kujua hatma ya kutimiza

Taarifa ya habari ChannelTEN Oktoba 10, 2016


The best way to sleep on a flight according to a posture expert


Ikiwezekana nakatupa kapaspoti kabisa...


Taarifa ya uteuzi wa Balozi Sefue na Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Dimplomasia