Nimesitisha kuweka taarifa mpya kwenye blogu ya wavuti.com

Kwa muda mrefu nimekuwa nikihudumia jamii ya Watanzania kwa kuweka taarifa mbalimbali hasa zinazohusu kujiendeleza, kujifunza, kujipatia maarifa na zaidi sana nafasi za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu pamoja na nafasi za ajira.

Nilifanya hivi kwa kupenda mwenyewe.

Kutokana na sababu zisizozuilika kwa sasa, nasitisha kuweka taarifa zote kwenye blogu hii kwa muda usiojulikana.

Asanteni kwa ushirikiano wenu kipindi hiki chote.

Nakutakieni kila la heri!

Subi Nukta.
Mei 3, 2018.