BENKI YA NMB YAKABIDHI PIKIPIKI TANO KWA JESHI LA POLISI – DODOMA

Benki ya NMB jana ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda kwa jeshi la polisi kwaajili ya kusaidia kazi za kila siku za jeshi hilo katika hafla iliyofanyika nje ya ukumbi wa St. Gasper katika mkutano wa maafisa wa polisi unaoendelea mjini hapa. Pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani – Mh Mathias Chikawe na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Tom Borgols, zina thamani ya shilingi Milioni 10.

 Waziri Chikawe alishukuru NMB kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi na hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo. “ Tunashukuru sana kwa hizi pikipiki, zitatusaidia sana kuboresha utendaji wa polisi, tutaendelea kuwa wadau wenu muhimu,” aliongeza Mh Chikawe.

Team ya NMB ipo Dodoma kwenye mkutano wa maofisa wa Polisi na kuonesha kuwa inawajali katika kipindi cha mkutano, NMB ina mabanda kadhaa ya maonyesho nje ya ukumbi wa St Gasper huku wakitoa huduma mbalimbali kama kutoa na kuweka fedha kupitia huduma ya NMB Wakala – huduma mpya inayoshirikisha mawakala wa MaxiMalipo, Kufungua akaunti kupitia Chap Chap Instant Account pamoja na elimu kwa ujumla juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.

[video] Ilivyokuwa sekeseke la maandamano ya CUF

Uliahidi mapato au makato Bro wa Tumia Fedha Federation alias TieFueFu?Ziara ya Maafisa Mawasiliano kwenye mradi wa gesi na hospitali ya Ligula


Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa Kitanda cha wagonjwa kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo jana, Januari 27, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa sanction mashine kwa muwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akitembeea katika eneo la mradi wa nyumba za wafanyakazi wa Mradi wa kuchakata Gesi Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant wakati wa ziara ya Maafisa Mawasiliano Serikalini Mkoani Mtwara. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa na Mkuu wa Kitengo Serikalini wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud (katikati).Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga(katikati) akitembelea katika katika eneo la Mradi wa kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant wakati wa ziara ya Maafisa Mawasilano Serikalini katika eneo a mradi huo Mkoani Mtwara


Mhandisi Jane wa TPDC akielezea jambo kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini walipofanya ziara ya kutembelea Mradi wa Kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant uliopo katika kijiji cha Madimba Mkoani Mtwara. Watatu kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba NkingaPichani ni Bomba ambalo litatumika kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi jijini Dar es Salaam.Mitambo iliyopo katika eneo la Mradi wa Kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant uliopo katika kijiji cha Madimba Mkoani Mtwara

  • Picha: Frank Shija na Hassan Silayo- WHVUM

Taarifa ya Mtatiro kuhusu kukamatwa kwa Prof. Lipumba, "et alia"


Prof. Lipumba akiwa katika gari la Polisi
(picha: Habari Mseto blog)

PROFESA LIPUMBA AKAMATWA NA POLISI KWA NGUVU!


Ndugu zangu, hivi punde nimeongea na Maharagande Mbarala na Bonifasia Mapunda na wamenijulisha kuwa, Profesa Lipumba na Manaibu Wakurugenzi wawili wa Chama Cha Wananchi CUF (Shaweji Mketo na Abdul Kambaya), pamoja na walinzi wa Profesa Lipumba, wamekamatwa na polisi. Pia, nimeongea na mhe. Joram Bashange, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, tayari yuko Central Police lakini hajaruhusiwa kuwaona viongozi. Mawakili wa CUF wanaelekea polisi pia.

KUMBUKIZI YA MWAKA 2001

Ukamataji huo uliotumia nguvu kubwa umetokea leo majira ya Mchana wilayani Temeke. Leo ni Januari 27 na ni siku yenye kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Wananchi CUF baada ya matukio ya mauaji yaliyofanyika tarehe na mwezi kama huu huko Zanzibar ambako wafuasi wa CUF zaidi ya 100 waliuawa kwa risasi na vyombo vya dola. Mauaji hayo yalifuatiwa na maandamano mbalimbali yakiwemo ya Dar Es Salaam yaliyoongozwa na Prof. Lipumba ambaye alivunjwa mkono, kuporwa saa yake ya thamani na polisi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

MAANDAMANO YA CUF KILA MWAKA:

Baada ya tukio hilo CUF imekuwa na utaratibu wa kuandamana kila mwaka (maandamano ya amani) ili kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya Januari 2001 na kuwaenzi waliopata ulemavu wa kudumu kutokana na kipigo cha vyombo vya dola. Mwaka jana 2014 mwezi kama huu Bendera za Chama cha Wananchi CUF zilipepea nusu mlingoti na pia maandamano yalifanywa maeneo kadhaa ya nchi na vyombo vya dola viliyalinda.

Mwaka huu nimeambiwa kuwa CUF ililijulisha jeshi la polisi juu ya maandamano ya leo kupitia barua ya Alhamisi, Tarehe 22 Januari 2014. Baada ya CUF kuandika barua hiyo, maandalizi ya maandamano na mkutano wa hadhara yaliendelea, ikiwemo kufanya matangazo kwenye wilaya za DSM, kukodi vifaa mbalimbali na hata kulipia matangazo LIVE kwenye redio kadhaa ili hotuba za viongozi ziweze kurushwa. Jeshi la polisi lilipokea barua hiyo tokea tarehe 22 Januari na likakaa kimya muda wote huo.

ZUIO LA POLISI:

Leo tarehe 27 Januari, maandamano yalipangwa kuanza saa 8 mchana kuanzia Temeke Mwisho kwenda hadi viwanja vya MBAGALA ZAKIEM ambako mkutano wa hadhara ungefanyika kuanzia saa 10.00 - 12.00 jioni. Cha ajabu ni kuwa, asubuhi ya leo ndipo Jeshi la Polisi limepeleka barua kwenye Ofisi Kuu za CUF Buguruni KUZUIA MAANDAMANO na MKUTANO WA HADHARA.
Barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar Es Salaam na Pwani inaeleza sababu kadhaa za zuio hilo:
1. Kwamba, maandamano ya CUF ya Mwezi Januari 2001 yaliyofanya vyombo vya dola vitumie nguvu na kuua raia hayakuwa halali na hivyo kuadhimisha siku hiyo mwaka huu ni haramu na kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.
2. Kwamba, Taarifa za kiintelijensia zinaonesha ati kuna watu wamepanga kufanya vurugu katika maandamano na mkutano huo.
3. Kwamba, kuna vitisho vya UGAIDI katika nchi yetu na hivyo maandamano hayo na mkutano huo vinaweza kuleta madhara ya magaidi kupenya na kutekeleza azma zao mbaya.
4. Sababu nyingine za kipuuzi, dhaifu na zisizo na maana.
Baada ya kupokea barua hiyo na kwa sababu wananchi na wapenzi wa CUF walikwishajikusanya kwa maelfu kwa ajili ya maandamano, ilimpasa Profesa Lipumba na viongozi waandamizi wa chama waweze kwenda hadi Temeke Mwisho ili kuahirisha maandamano hayo.

TEMEKE MWISHO:

Majira ya mchana leo, Profesa Lipumba aliongea na wanachama na wapenzi wa CUF waliojazana Temeke Mwisho karibu na Ofisi za CUF Wilaya na akaahirisha maandamano na mkutano (Usalama wa Taifa walikuwepo, Polisi walikuwepo kwa mamia na vyombo vya habari vilikuwepo). Baada ya kufanikiwa kuwatawanya wafuasi waliokuwa Temeke Mwisho, Profesa akajulishwa kuwa kule uwanjani Zakiem tayari kuna maelfu ya wafuasi, ikampasa yeye na viongozi waandamizi waingie katika magari na kuanza safari kwenda Zakiem kwa lengo la kuwatawanya wafuasi kwa amani kama alivyofanya kwa wale waliokusanyika Temeke Mwisho. Hapakuwa na wafuasi wa chama waliomfuata.

KUELEKEA MBAGALA ZAKIEM:

Wakiwa katika Magari yao na katika safari ya kwenda Mbagala Zakiem, wakazuiwa na magari zaidi ya 10 ya polisi walio tayari kwa mapambano. Profesa na viongozi wakawajulisha Polisi azma yao ya kwenda kutawanya wafuasi walioko Zakiem, baada ya mvutano mfupi Polisi hao waliwaruhusu waende Zakiem. Safari ya magari machache ikaendelea, bila wafuasi wanaotembea kwa miguu.
Walipofika mbele (Mtoni Mtongani - Round about) wakakuta BLOCK ya pili ya mamia ya Polisi wenye magari na silaha. Hawa nao wakawazuia wasiende ZAKIEM, wakati bado Profesa anawaelewesha, mabomu yakaanza kupigwa na viongozi kusambaratishwa kwa nguvu mno kama vile kulikuwa na jambo kubwa. Profesa amebebwa mzobemzobe akipigwa virungu na kutupwa kwenye DIFENDA ya polisi yeye, wakurugenzi wake na walinzi wake. Hivi sasa tuongeavyo wako CENTRAL POLICE na mie nilitoka tu kidogo Darasani ili kupiga simu na kusimuliwa tukio zima.

CHA KUSHANGAZA:

Wakati polisi wanazuia maandamano ya CUF kwa nguvu kubwa kiasi hiki, wanawapiga na kuwajeruhi viongozi wasio na hatia na ambao wamejishusha na kuahirisha maandamano na mkutano wao, Polisi haohao kila siku tunaona wanasimamia maandamano na mikutano ya Mwigulu Nchemba, Abdulrahman Kinana, Nape Nauye na viongozi chungu mbovu wa CCM.
Hata katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yanayotarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma, nimejulishwa kuwa kuna maandamano yamepangwa yakihusisha wana CCM mbalimbali katika wilaya za jirani ili kusheherekea sikukuu yao na kwamba Polisi watayalinda maandamano hayo ya CCM.

MASWALI YA KUJIULIZA:

Je, hizi taarifa za Kiintelijensia zinafanya kazi kwa mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu? Je, hao Magaidi wao wanavamia na kulipua mikutano ya vyama vya upinzani tu? Magaidi gani hawa ambao hawaendi kuvamia wezi wa fedha za umma ati wanakwenda kuvamia viongozi waadilifu wanaopigania haki sawa kwa wote na mabadiliko makubwa katika nchi yetu? Tunadhani matendo haya ya serikali na vyombo vyake dhidi ya vyama vya upinzani yanajenga mustakabali wa taifa? Yanajenga amani na upendo miongoni mwetu? Au yanazidisha chuki na uhasama na mgawanyiko/mpasuko katika taifa?
Kwa nini mamia ya askari wanaokwenda kupiga na kujeruhi viongozi wenye nia njema yasitumike kwenda kusaka majambazi walioua askari wetu pale Ikwiriri Rufiji? Kwa nini mamia ya askari hao yasiwasake majambazi walioteka mabasi ya abiria mkoani Arusha majuzi? Kwa nini mamia ya Askari hao yasijielekeze kuwasaka wauaji wa Albino na wazee wenye macho mekundu Shinyanga?

Kwa nini mamia ya askari hao wasipelekwe kuwasaka magaidi ambao tumegundua watakuja kutuvamia? Na mbona maguvu hayo ya polisi yasielekezwe kuwasaka wala rushwa wakubwa, wafadhili na wamiliki wa mitandao ya kuuza madawa ya kulevya, wezi wa fedha za umma na waharibifu wakuu wa Taifa hili?
Mbona taifa hili linaendeshwa kipuuzi namna hii? Mbona nchi yetu inapelekwa mbele kama vile kuwa Chama Cha Upinzani ni dhambi dhidi ya watawala wezi na mafisadi? Kwa nini basi CCM hao hao wakapigia debe kuanzishwe vyama vingi mwaka 1992? Sasa wanaogopa na kuweweseka kwa lipi?

(UKIONA SERIKALI INAOGOPA MAANDAMANO YA AMANI NA MKUTANO WA CHAMA KIMOJA TU HADI KUPIGA NA KUKAMATA VIONGOZI, JUA KWAMBA SERIKALI HIYO HAINA SIKU NYINGI MADARAKANI).

"Time will determine and judge each of us".

Julius Mtatiro,
27 Januari 2015,
Masomoni.

"Tanzania kuna wagonjwa wengi, wengine wanataka kuingia Ikulu"

Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) limesema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa taifa, ipo haja ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupimwa afya zao na kutangazwa kwa wananchi ili kuepuka kuwaweka wagonjwa madarakani.

Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba alisema hayo Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya uchaguzi wa marudio nchini Zambia kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Michael Satta wa chama cha Patriotic Front (PF).

Uchaguzi huo umefanyika kwa mara ya pili ambapo kabla ya Satta alitangulia Levy Mwanawasa aliyefariki akiwa katika nafasi ya urais Agosti mwaka 2008 na kusababsiha uchaguzi mdogo uliompa ushindi Rupiah Banda ambaye alishika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.

Kuhusu kupima afya za viongozi nchini, alisema Jukwaa hilo linapendekeza Tanzania kuitazama Zambia kama mfano na kuanza kujihami kwa baadaye licha ya kwamba hakuna anayepanga jambo kama hilo kutokea.

“Tanzania kuna wagonjwa wengi na wengine wanataka hata kuingia Ikulu …ni vyema afya zao zikapimwa na kutangazwa kwa wananchi ili kuepuka hatari ya kurudiarudia uchaguzi kama ambavyo imeikuta nchi ya Zambia,” alisema Kibamba.

Alisema ni wakati sasa kwa wagombea wote kujitathmini na kujipima kabla ya kupitishwa, kufanyiwa uchunguzi na kutambulika kuwa suala la afya za wagombea ni la kitaifa na si siri.

Kuhusu afya zitapimwaje alisema kwa Zambia Tume ya Uchaguzi nchini humo iliteua Wakala wa Afya kwa ajili ya kupima afya za wagombea na kwa hapa nchini ni vyema suala hilo likawa kama sharti ili kwa wale watakaoshindwa kutekeleza wakaachana na harakati hizo.

Alisema uchaguzi wa Zambia ulikuwa huru, haki na wa kuigwa na nchi mbalimbali za Afrika kwa kuwa ulifanyika kwa uwazi huku Tume ya Uchaguzi ya nchini humo ikifanya kazi kwa umahiri na kutoa elimu kwa raia kwa kiwango kikubwa.

Akizungumzia kuhusu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, alisema hakuna haja ya kuharakishwa na kufanyika Aprili, mwaka huu kwa kuwa maandalizi ya kutosha hayapo huku pia nakala za Katiba hiyo zikiwa hazijafikishwa kwa wananchi na kuweza kuisoma na kuielewa.

Alisema hadi sasa maandalizi ya uboreshwaji wa daftari la wapiga kura halijafanikiwa, pia upo mchakato wa vitambulisho vya Taifa unaoendelea na ambao haujaweza kusambaa mikoani tangu kuanza kwake ambapo ni vyema hatua ya Kura ya Maoni ikasimamishwa na kufanyika baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika.

  • HabariLeo

Barua ya Castro kwa Maradona yavuja! Asema bado haiamini Marekani

Fidel Castro, aliyekuwa akiiongoza Cuba tangu mapinduzi hadi mwaka 2006 alipong'atuka na kumwachia kiti kaka yake, Raúl, amekuwa mkimya tangu Marekani na Cuba zitangaze maazimio mapya ya kutafuta ukurasa mpya wenye matumaini baina ya nchi hizo mahasimu.

Leo, TeleSur, gazeti la Serikali ya nchi hiyo ya Kikomunisti ilichapisha sehemu ya barua (imeshaondolewa mtandaoni) ikisema kuwa iliandikwa na kiongozi huyo mstaafu mwanzoni mwa mwezi huu, kwenda kwa rafiki yake, mwanasoka mahiri, Diego Armando Maradona.

"I don't trust the politics of the United States and I've not said a word to them," "This doesn't mean, however, that I reject a peaceful outcome..." 

Barua hiyo ilinukuliwa pia na kituo cha Serikali cha runinga ikisema kuwa Castro amesisitiza kuwa Cuba itaendelea kulinda sera na misimamo yake ya kimapinduzi.

"We will always defend the cooperation and friendship with all of the world and our our political adversaries."

Castro hajabariki ukurasa mpya ulioanzishwa baina ya Marekani na Cuba ila amemtetea kaka yake, Raúl kuwa alifanya maamuzi kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na kulingana na maamuzi ya Bunge na Chama cha Kikomunisti cha Cuba.

Buy stuff from zulily.com at up to 70% off retail prices.

Blog Archive

Since February 1st, 2014