Mtikila aenda kortini kuomba aingzwe kwenye kesi ya IPTL vs Kafulila

MWENYEKITI wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila, ameomba kuunganishwa katika kesi ya madai inayomkabili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.

Awali, Kafulila akizungumza kwenye mjadala katika eneo la Urusi Mwanga mjini Kigoma jana, alisema Mchungaji Mtikila ameomba kuwa mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo huku Chama chake cha DP kikiwa mshitakiwa wa tatu.

Pia alisisitiza kuwa kamwe hakukurupuka kuibua kashfa hiyo ya ufisadi katika akaunti ya Escrow na

Maandamano Dar kupinga mauaji Mashariki ya Kati

TAASISI ya Hawzat-Imam-Swadiq (A.S), iliyopo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, imepanga kufanya maandamano kesho kupinga mauaji yanayoendelea Mashariki ya Kati dhidi ya Wapalestina.

Mkuu wa taasisi hiyo, Hemed Jalala, akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema wanapinga vikali mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina na kuamua kufanya maandamano yataanzia katika kituo cha daladala cha Ilala Boma hadi Kigogo uwanja wa Bibo kuanzia saa tatu asubuhi hadi sita mchana.
“Hadi sasa maelfu ya Wapalestina wamepoteza maisha, hivyo jamii na taifa kwa ujumla tunapaswa kushirikana na kuonyesha kuguswa na mauaji hayo, kwani waathirika ni

Taarifa rasmi iliyotolewa na Polisi kuhusu mabaki ya miili ya binadamu


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA

PRESS RELEASE

22/07/2014

WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU MAENEO YA BONDE LA MBWENI MPIJI ENEO LA BUNJU 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watu wanane na kuwahoji kuhusu tukio la kupatina kwa viungo vya binadamu vilivyogundulika katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji ambapo mifuko ya plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu yaligundulika. Polisi walipata taarifa 21/07/2014 jioni kutoka kwa wasamaria wema na ndipo jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP. Camilius Wambura walifika hapo majira ya saa 1.00 usiku.

Walipofika katika tukio waligundua mifuko ipatayo 85 mieusi yenye viungo vya aina mbali mbali vya

PPF na MSD wasaini mkataba wa “wekeza”; Wafanyakazi 400 wa MSD wajiunga PPF

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, wakiweka saini mkataba wa “Wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD, Keko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014. Chini ya Mkataba huo, zaidi wa wafanyakazi 400 wa MSD wamejiunga na PPF. 
Viongozi wa PPF na wenzao wa MSD, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa MSD waliokabidhiwa kadi za uanachama wa Mfuko huo, mara baada ya kutiliana saini mkataba ambapo MSD na PPF zimekubaliana kuanzisha mpango wa "Wekeza" ambapo wafanyakazi wa MSD sasa watakuwa wakichangia kwenye mfuko huo ili kujiwekea akiba na kujipatia mafao mbalimbali.

Rais Kikwete aandaa futari kwa wananchi Pemba, Zanzibar

Balozi Seif akibadilishana mawazo na  mmoja wa watoto walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete huk Wete, Pemba.

Na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ - Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu nchini kuendelea kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao kama inavyoagiza wakati wote.
Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili ya Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya Ikulu ya Serikali ya Muungano yaliyopo Mjini Wete Pemba.

Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa Waislam hupatikana katika mjumuisho wa

.