Saturday, November 1, 2025

Jinsi ya kuwasiliana na walioko Tanzania kwa kutumia Google Voice ama VoIP

Kama uko Marekani au Canada, unaweza ku-install Google Voice na kuitumia kupiga simu kwenye namba ya mtu moja kwa moja aliyeko Tanzania.

Natoa maelekezo kwa wanaotumia simu za Android (sina iPhone hivyo sijui kama mtiririko wa maelezo unafanana) 

  1. Install Google Voice (https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.apps.googlevoice
  2. Open na kufuata maelekezo ya kujiandikisha na kupata namba ya bure
  3. Bonyeza hamburger menu (mistari mitatu juu kushoto) 
  4. Bonyeza "Credit" 
  5. Bonyeza nukta tatu (three dots) juu kulia 
  6. Bonyeza Add Credit chagua na fuata maelekezo 
  7. Rudi kwenye Google Voice na piga namba kutoka kwenye contact list yako au kwa kutumia dial pad

Angalizo: Kama utapiga kwa kutumia Google Voice na isitoe mlio wa kuita simu, kata kisha jaribu kupiga tena na tena, eventually itaita namba unayoipigia. Unapaswa kuendelea kukata na kujaribu tena na tena.

Kama huwezi kutumia Google Voice, jaribu mbadala wa VoIP nyingine, unaweza kujaribu zilizoorodheshwa: https://www.voiprates.info (direct link ya kulinganisha gharama za kupiga simu Tanzania kwenye simu za mkononi ni: https://www.voiprates.info/?company=&country=Tanzania&type=%CE%9A%CE%B9%CE%BD%CE%B7%CF%84%CF%8C&currency=USD)

Kwa wanaotumia Starlink na kutaka roaming, ni muhimu kufuata maelekezo kuepuka kukatiwa huduma kama utatumia katika nchi ambayo haijaruhusiwa bado, "Using Starlink Roam in a unauthorized country different from your shipping address (marked "Coming Soon" or "Waitlist) may cause your service to be restricted immediately. (Starlink - What happens if I use Roam service in a different country than where I activated?)"