Get this FREE eBook by Leo Babauta: The One Skill


Get yourself an eBook by Leo Babauta (of ZenHabits)!

On marking his 41 years of wonderful life that he’s lived, and as a birthday present to all of us, Leo published a free ebook: The One Skill: How Mastering the Art of Letting Go Will Change Your Life.

He started this tradition of giving people gifts on his birthday, to celebrate the fact of being alive and last year he gave away Little Book of Contentment.

The One Skill book is about learning the skill of letting go, and how that will help you with problems in

Tanzania dismisses Rwandan publication as "baseless"

We have just received statement made by one of the Rwandan publication claiming that the Commander of the FDLR, the Rwandan rebels operating in Eastern Democratic Republic of Congo is visiting Tanzania and that he is scheduled to meet Tanzanian top government officials.

The Government wishes to clarify that the government is not aware of such claim of the visit of the said FDLR Commandant and that it has no intention to host any of the rebel.

It is unfortunate that the Rwandan publication decided to fabricate a story to meet their own interest and the Tanzanian should ignore whatever messages published in their online version of the Rwanda Today publication.
--- Statement quoted from Tanzanian Government blog

Oprah, Magic, Mayweather Jr., De La Hoya for possible Clippers bid

(image source: MSNBC)

A day after Sterling was banned for life from the National Basketball Association, several luminaries from sports and show business, Oprah Winfrey among them, signaled interest on Tuesday and Wednesday in buying the Los Angeles Clippers as the NBA set a first meeting to weigh removing Donald Sterling as

Bajeti ya Serikali 2014/2015: Shilingi trilioni 19.7/=Serikali imepanga kutumia Sh trilioni 19. 7 katika mwaka wa fedha 2014/2015, kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo, tofauti na Sh trilioni 18.2 ya mwaka huu wa fedha unaoishia Juni 30.

Katika fedha hizo, matumizi ya kawaida yamepangwa kuwa Sh trilioni 14.2, ambapo kati ya hizo Sh trilioni 5.1 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali, taasisi na wakala wake.

Aidha Sh trilioni 4.4 zimetengwa kwa ajili ya Mfuko Mkuu wa Serikali na Sh trilioni 4.4 kwa ajili ya matumizi mengine.

Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akiwasilisha Mpango wa

Korti yaombwa imsomee mashitaka nyumbani Mkurugenzi wa MSD

Upande wa mashitaka katika kesi ya kuingiza nchini vipimo bandia vya kupima virusi vya UKIMWI (HIV), umeiomba Mahakama kwenda kumsomea mashitaka nyumbani Mkurugenzi wa Operesheni Kanda ya Kaskazini wa Bohari ya Dawa (MSD), Sylvester Matandiko.

Wakili kutoka Taasisisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Leonard, Swai alitoa ombi hilo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kuwa mshitakiwa huyo anaumwa kiharusi.

Mbali na Matandiko, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, ambaye

EAC Extra Ordinary Summit: Leaders direct on political federation

R-L: Presidents Yoweri Museveni (Uganda), Uhuru Kenyatta (Kenya), Jakaya Kikwete (Tanzania)
R-L: Presidents Yoweri Museveni (Uganda), Uhuru Kenyatta (Kenya), Jakaya Kikwete (Tanzania) (photo: Freddy Maro of State House, Tanzania)

The 12th Extra Ordinary summit in Arusha, Tanzania was graced by Presidents Yoweri Museveni, Jakaya Kikwete and Uhuru Kenyatta of Uganda, Tanzania and Kenya respectively.

Burundi was represented by its First Vice President, Prosper Bazombaza, while Rwanda, its Prime Minister, Dr. Pierre Damien Habumuremye.

With the heads of state deciding to hold two Extra Ordinary Summits annually – in April and November –

Facebook introduces anonymous login and updated loginFacebook users can have a little more option with the introduction of an anonymous, single-click login in to apps using Facebook without sending personal information to the developer.
 • Anonymous Login: An easy way for people to try an app without sharing any of their personal information from Facebook.
 • Facebook Login: A new version that gives people the option to pick and choose what information apps get.
 • A Redesigned App Control Panel: A central place for people to see and manage the apps they use.
The new system is currently being tested with a few developers like Flipboard. You'll see the option to login anonymously below the typical Facebook login. You can choose later to allow more personal information to be shared from your account. Click here to go to Facebook's Newsroom page for more

Ufafanuzi wa Serikali kuhusu tuzo aliyotunukiwa Jaji Warioba

Rais Kikwete akimtunuku Nishani, Daraja la Kwanza, ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia alikuwa Mwenyekiti Tume ya kurekebisha Katiba Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano, Ikulu jijini Dar es Salaam Aprili 25, 2014. (picha, maelezo: Freddy Maro, IKULU)
Rais Kikwete akimtunuku Nishani,  Daraja la Kwanza,  ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia alikuwa Mwenyekiti Tume ya kurekebisha Katiba Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano, Ikulu jijini Dar es Salaam Aprili 25, 2014. (picha, maelezo: Freddy Maro, IKULU)

Na Magreth Kinabo, Habari - Maelezo -- Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene amesema Jaji Joseph Warioba alitunukiwa tuzo ya muungano iliyotukuka kwa kuwa alistahili kupewa kama viongozi wengine na kuwa kitendo si kumkejeli kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti hivi karibuni.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu suala

[audio] Jussa akihutubia wananchi Kibanda Maiti, Unguja

Na SwahiliVilla blog — Mjumbe Wa Bunge Maalumu la Katiba, Ismail Jussa amehutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) huko Kibanda Maiti mjini Unguja, Zanzibar.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na viongozi wa vyama vya siasa Tanzania kama vile Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Wilbrod Slaa wa CHADEMA, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.

UKAWA wafanya mkutano Kibanda Maiti, Unguja


Viongozi wa Wajumbe wa kundi la UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ndani ya Bunge Malaum la Katiba, wamehutubia maelfu ya watu waliohudhuria mkutano wao katika viwanja vya Kibanda Maiti mjini Unguja, Zanzibar jioni ya leo.

Aidha, katika mkutano huo katika mkutano ilielezwa kuwa ushirikiano wa UKAWA sasa siyo katika katiba pekee bali utakuwa mpaka Bungeni ambapo wanatarajia kuivunja Serikali ya sasa kivuli na kuunda nyingine yenye wajumbe mchanganyiko kutoka katika vyama mbalimbali.

Kwa mujibu wa Katibu wa UKAWA ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, mkutano mwingine wa UKAWA unatarajiwa kufanyika Pemba hapo kesho kabla ya mikutano kama hiyo kuendelea katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara/Tanganyika kama vile Dar es Salaam, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Iringa, Arusha n.k.

Mtatiro amesema lengo la mikutano hiyo ni kuwaelimisha wananchi juu ya hatua yao ya kuondoka Bungeni na kususia vikao vya Bunge Maalum la Katiba na kile wanachoamini kinapaswa kufanyika.ITV video: Mahojiano ya Jaji Warioba katika kipindi cha Dakika 45

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba ameongea na ITV kupitia kipindi cha Dakika 45 na kutoa ufafanuzi muhimu kuhusu mambo muhimu juu ya uundwaji wa katiba mpya.

Video iliyopachikwa hapo chini ni sehemu ya kwanza ya mazungumzo hayo.
 • Ikiwa unashindwa kutizama video za Youtube, unaweza kutizama video hii pia kupitia Dropbox
 • Pleya yenye audio ya mazungumzo imepachikwa kwa wasioweza kufungua video.Taarifa ya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi REA

TAARIFA KWA UMMA


UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA).

Waziri wa nishati na madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (Mb) ameteua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoka Taasisi zisizo za kiserikali (NGO), Sekta Binafsi na washiriki wa Maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014.

Majina ya wajumbe walioteuliwa na Taasisi wanazoziwakilisha ni kama ifuatavyo:-

Lost legacy: The untold story of Dar es SalaamMr Mejah Mbuya hops off his bike outside a building that seems to be unoccupied. “There used to be a plaque around here somewhere,” he murmurs, searching in vain. The building is in central Dar es Salaam, Tanzania’s steamy port city and commercial capital, and looks like many of the other older buildings in the area, in need of repair and dwarfed by proliferating high rises. “Anyway,” Mr Mbuya says, “this is the former head office of Frelimo.”

The Mozambique Liberation Front, or Frelimo, was founded in Dar es Salaam in June 1962. The movement used Dar es Salaam as its home base for 13 years, until Mozambique achieved independence in 1975.

Mr Mbuya is the co-founder of a unique tour company called Afri Roots. Along with safaris and treks, it also

Taarifa ya mabadiliko ya anuani ya ofisi - Utumishi wa Umma

MABADILIKO YA ANUANI YA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake kuwa anuani yake imebadilika hivyo kuanzia sasa mawasiliano yafanyike kwa kutumia anuani ifuatayo;

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
UTUMISHI HOUSE
8 BARABARA YA KIVUKONI
11404 DAR ES SALAAM


au

Mtihani mpya wa BRN kwa Kidato cha Nne

Wanafunzi wa Kidato cha Nne, watafanya mitihani miwili ya Taifa mwaka huu, baada ya kuongezwa mtihani wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), ambao utatumika kuwapima walivyojiandaa na Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Sekondari.

Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Paulina Mkonongo, alitangaza utaratibu huo jana na kufafanua kwamba lengo ni kubaini wanaohitaji msaada kabla ya mtihani wa mwisho, ili kuboresha taaluma darasani. 
 
Kwa mujibu wa Paulina, mtihani huo wa BRN, utafanyika kwa masomo machache lakini yanayosomwa na

Ajitoa uhai kwa simanzi ya kumkumbuka mkewe

Richard Kijazi, mkazi wa jijini Dar es Salaam, amejinyonga huku akiacha ujumbe unaodai kuwa amemkumbuka mkewe aliyefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema kuwa mwanaume huyo alikutwa amejinyonga chooni juzi saa 10:00 jioni maeneo ya Kijichi huku akiwa ameacha ujumbe wa

The porters on Mount Kilimanjaro

(photo source: www.schwartzphoto.com)

[...] the highest mountain in Africa, Tanzania's Kilimanjaro, which ranks second in National Geographic’s “Top Ten Climbs” list, attracts more than 40,000 visitors each year. But one surely doesn’t climb Kilimanjaro alone.

For every climb, which can take at least five days, three local workers also come along to provide guidance and to carry food and equipment. The industry employs thousands of guides, cooks and porters. It also generates roughly $50 million in revenue every year and pays more than double the average local wage -- an aspect that can be a double-edged sword.

Kilimanjaro's “network of tour operators, porters and guides makes it one of the best-organized mountain hikes in Africa,” according to a 2013 World Bank report, which estimates that the $50 million in revenue generated every year supports 400 guides, 500 cooks and 10,000 porters and contributes roughly 13 percent of the country’s overall gross domestic product.

Analysts suggest that $13 million of the revenue is used to... Click here to continue reading

Taarifa ya EWURA ya kufuta leseni za makampuni 9

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Whole Sale Licenses) kwa Kampuni tisa (9) zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini.

Uamzi huo umefanywa leo (29.4.204) katika kikao chache cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, Bw. Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa

Kitimtim! “Bandarini wasema gazeti la JAMHURI ni mkombozi”

 • Nguvu za ajabu alizokuwa nazo zaanza kuyeyuka, alalamika Kikwete hamsaidii
 • Marafiki zake wamtaka asimsingizie Rais, wasema amejiharibia mwenyewe
 • Ashinikizwa awarejeshe kazini aliowafukuza kibabe, wafanyakazi washangilia
 • Aanza kuogopa kivuli chake, ajitolea ‘photocopy’, adai wanaomsaliti anao TPA
 • Mtawa asema asihusishwe na Kipande, bandarini wasema JAMHURI mkombozi
 • Mwakyembe aweweseka, adai Lowassa, Profesa Tibaijuka hawamtakii mema

Nguvu za ajabu alizokuwa nazo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (58), zimeanza kuyeyuka kwa kasi baada ya GazetiJAMHURI kuchapisha mfululizo maovu anayotenda kwa kutumia wadhifa wake.

Vyanzo vya kuaminika vilivyopo karibu na Kipande, vinasema kwa sasa

Diamond aahidi makubwa Mtwara

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, Diamond Platinum akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na Tamasha la Heels & Ties litakalofanyika makonde beach Mtwara na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Wateja wanaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda namba 0754 980 769. na kupata punguzo la asilimia 20%. Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, Diamond Platinum akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na Tamasha la Heels & Ties litakalofanyika makonde beach Mtwara na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Wateja wanaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda namba 0754 980 769. na kupata punguzo la asilimia 20%. Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa

Dar es Salaam Aprili 30, 2014 ... Nyota wa muziki wa Bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika, Rais wa wasafi kama wengi wanavyomuita, Diamond Platnum, Dangote ameahidi makubwa kwa mashabiki wake wote wa Mkoa wa Mtwara kuhusu show ya aina yake inayotarajiwa kufanyika katika umbi wa Makonde Club mjini Mtwara siku ya ijumaa tarehe 2 mwezi huu.

Msanii huyo aliyeafanikiwa kujizolea mamilioni ya mashabiki wa muziki wa Bongo flava atasindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu - 'Beautiful Onyinye' au Madame kama

Rais Kikwete apokea ujumbe wa Rais wa Burundi kutoka kwa mjumbe maalum

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Sheikh Mohamed Rukara, Mjumbe Maalum wa Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunzinza, alipofika na ujumbe wake kuwasilisha ujumbe huo Ikulu jijini Dar es Salaam leo April 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Sheikh Mohamed Rukara, Mjumbe Maalum wa Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunzinza, alipofika na ujumbe wake kuwasilisha ujumbe huo Ikulu jijini Dar es  Salaam leo April 29, 2014

Rais Kikwete akutana na viongozi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo April 29, 2014. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif S. Rashid
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 29, 2014. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Seif S. Rashid

Letter from our reader: Global Education Crisis

As a newly appointed Global Youth Ambassador for A World at School, I want to call attention to the 57 million children around the world are currently being denied their human right to an education.

500 other young advocates for global education join me in this call to action. Together, we make up the Global Youth Ambassadors group – launched on April 1, by the United Nations Secretary-General Bank Ki Moon and the United Nations Special Envoy for Global Education Gordon Brown.

I have once worked with Twaweza in Uwezo Unit, the unit that deals with the quality of education in primary schools. At Twaweza I discovered that pupils in our primary schools are not learning. This motivated to join

Rais Kikwete azindua Mkoba Private Equity Fund

Rais Dkt jakaya Mrisho Kikwete akihutubia akizindua rasmi rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam leo April 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia akizindua rasmi rasmi mpango wa Mkoba Private Equity Fund katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam leo April 29, 2014

Mama Misheli Singoye kuzikwa kesho

Misheli Singoye

Mama mzazi wa Mtangazaji wa Television ya Taifa (TBC1), Angella Michael Msangi, Marehemu Mama Misheli Singoye anatazikwa kesho Jumatano, Aprili 30, 2014 ambapo ibada itaanza saa tatu asubuhi katika Kanisa la Pentekoste, Kigamboni na baada ya hapo safari ya kuelekea kwenye maziko Zinga kwa Awadhi, Bagamoyo Pwani.

Marehemu Mama Misheli Singoye alifariki Aprili 26, 2014 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Tangazo la Wizara kuhusu maombi ya kujiunga na Kozi za Afya

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa katika vyuo vinavyoendeshwa na Wizara ya Afya kwa mwaka wa masomo 2014/2015.


1. Kozi zinazotangazwa ni:
A.     Kozi za ngazi ya Stashahada (Ordinary Diploma Programmes):
 1.                   Stashahada ya Afya ya Mazingira (Ordinary Diploma in Environmental Health Sciences)
 2.                        Stashahada ya Uzoeza viungo (Ordinary Diploma in Physiotherapy )
 3.                        Stashahada ya Teknologia ya Viungo Bandia vya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Dental Laboratory Technology)
 4.                        Stashahada ya Teknologia ya Maabara za Afya ya Binadamu (Ordinary Diploma in Health Laboratory Technology)
 5.                        Stashahada ya Optometria (Ordinary Diploma in Optometry)
 6.                        Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Binadamu (Ordinary Diploma in Clinical Medicine)
 7.                        Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Clinical Dentistry)
 8.                        Stashahada ya Uuguzi (Ordinary Diploma in Nursing)
B.     Kozi za ngazi ya Cheti (Technician Certificate Programme)

Call for Artists: Bagamoyo International Festival of Arts & Culture


TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)


THE 33RD BAGAMOYO INTERNATIONAL FESTIVAL OF ARTS AND CULTURE


22 – 28 SEPTEMBER, 2014


CALL FOR ARTISTS


Dear Artists,

We would like to invite you (individual artist/groups) to apply for the participation and performance in the 33th Bagamoyo International Festival of Arts and Culture which will take place at the institute (TaSUBa - Bagamoyo) from 22 - 28 September 2014.

The aim of this festival is to support and expose activities of the artists, encourage cooperation and friendship of both local and international artists, promote mutual cultural exchange, share experiences

Mitizamo ya Watanzania wa Marekani kuhusu Muungano

Pleya iliyopachikwa hapo chini ina audio ya maoni ya Watanzania waishio Marekani wakielezea mitizamo yao kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Watanzania hao walikuwa wakizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano zilizofanyika siku ya Jumamosi, Aprili 26 katika ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC.wavuti.com imeshirikishwa post hii na SwahiliVilla blog.

Tafakuri ya ujenzi wa Taifa imara na nidhamu

Tafakuri na Shaaban Y.

Kuongoza na kutawala, ni jukumu la serikali. Kutawala ni kama kulinda, kutotawanya, kukusanya na kutoruhusu kutawanyika. 

Kulinda binadamu dhidi ya uharibifu na uovu ni jukumu la serikali. Kulinda na kuhifadhi ubinadamu ni jukumu la serikali. Kuongoza ni kuonyesha njia ni wapi taifa linapaswa kuelekea kwahiyo kiongozi ni lazima aweze kutawala na kuongoza kwa pamoja. Serikali haiwezi kukamilika pasipo kuwa na vitu hivyo vyote viwili. Kimoja ikiwa ni dira na kingine kukusanya na kulinda. Ili serikali ifanye kazi vizuri ni lazima iwe na uwezo huo. Lazima ikusanye, ilinde na iongoze.

Mfano mzuri wa kutawala na kuongoza ni mfano wa kondoo na mchungaji. Mchungaji ni lazima akusanye

Scholarship for Tanzanians from the Government of Mauritius

The Government of the Republic of Mauritius is offering scholarships for undergraduate studies in public tertiary education institutions in Mauritius.

Applications are invited from qualified Tanzanians to apply for undergraduate programs tenable in the Republic of Mauritius for 2014/2015 academic year in the following areas of specializations:-

Dakika 15 za Kijiwe cha Ughaibuni (No. 60)

Vodacom yawaunganisha Buhigwe na mtandao wa simu

 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiuzindua rasmi mnara wa Vodacom kuashiria kuanza kupatikana huduma za kampuni hiyo ya simu nchini katika kijiji cha Bukuba kilichopo Buhigwe mkoani Kigoma. Katikati ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.

 • Vodacom yawafikia wakazi 17,000 wa Bukuba
 • DC azindua huduma, kilimo, ufugaji kuboreka
 • Ataka wakulima, wafugaji kuitumia M-pesa kujikomboa
Zaidi ya wakazi 17,000 wa kijiji cha Bukuba wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kunufaika na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi za mtandao wa Vodacom baada ya kampuni hiyo kuzindua rasmi huduma zake kijijini hapo.

KIuzinduliwa kwa huduma za Vodacom kijijini hapo kunawapa nafais wakazi hao walio pembezoni mwa

Kielelezo kwenye 'lift' katika moja ya hospitali Tanzania


Jenerali Ulimwengu: Kama Dunia hii ni kijiji, nafasi ya Afrika ipi?

Kama kweli dunia hii imekuwa ni kijiji cha ulimwengu, je sisi tunajikuta wapi katika mipangilio ya kijiji hicho?
Tumepangiwa maskani yetu yawe wapi katika kijiji hicho na majukumu yetu ni yapi?
 1. Je, katika kijiji hicho Afrika ndiyo ofisi kuu ya utawala wa kijiji chetu?
 2. Je, sisi tumo ndani ya maabara ya kijiji tukifanya utafiti wa mbinu mpya za kuinua uzalishaji?
 3. Je, Afrika ni maktaba ambamo watoto na watu wazima wanajisomea ili kuongeza ujuzi wao au kujiburudisha kwa hadithi tamu? Je, katika mipangilio ya kijiji hicho sisi ndio wazalishaji wa chakula cha kulisha kijiji kizima?
 4. Ama, niliuliza, Afrika ndiko unapatikana msalani wa kijiji hicho, ambako kila mwanakijiji ana uhuru wa kwenda kujisaidia baada ya kuwa amekula na kushiba?
Sikupata jibu kutoka kwa wakuu wetu waliokuwa wakibadilisha ndege kwa ndege, wakikimbilia wapi sijui, kueneza injili ya ‘utandawazi’ na ‘kijiji cha dunia’.

Imenukuliwa kutoka kwenye makala ya Jenerali Ulimwengu, "Kama alivyosema Chachage, tu wahanga wa ‘collective imbecilisation’.." iliyochapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema.

Zanzibar AllStarz: Wimbo wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania - Golden Group

Pres. Kikwete to launch new private equity fund

President Jakaya Kikwete is expected to officiate a conference on investing in Africa’s future and the role of the private sector in Dar es Salaam this Tuesday.

The conference, jointly organised by Mkoba Private Equity Fund, which the President will officially launch at the conference, and UONGOZI Institute, aims to highlight the challenges and opportunities of investing in Africa, and the role that business and entrepreneurs can play to deliver on Africa’s promise.

“Given the crucial role the private sector plays in the development process, the conference will gather high level representatives from multiple sectors to discuss and promote productive investment and

[video] Elephant rescued after poison dart attack

A 4-ton African elephant was left to slowly rot from the inside after cruel poachers shot it with a poisoned arrow.

After being safely tranquillised, the medical team from the David Sheldrick Wildlife Trust and Kenyan Wildlife Service cut open a huge abscess on the elephant's side, before removing dead muscle tissue and extracting the arrow. The vets then cleaned and packed the wound with green clay, a substance believed to have strong antibacterial properties.

Awakening from the anaesthetic, the elephant rose from its slumber, fit enough to return to the herd.

Watch the video below...

Job opportunities for Tutorial Assistants at SUA

The Management of Sokoine University of Agriculture (SUA) invites qualified Tanzanians to apply for positions of Tutorial Assistants (TA’s) (<35 yrs of age) and Assistant Lecturers (<45 years). 

Applicants are advised to note that the minimum GPA of 3.8 or an average of B for unclassified degrees such as that of Veterinary and Medical graduates at undergraduate level applies for TA’s and 3.5 at BSc/BA level or equivalent (i.e. an average of B for Veterinary and Medical graduates) and a good Masters degree is applicable for those with postgraduate qualifications. 

Only registered Veterinarians will be considered for interviews.

Pres. Museveni is now on Twitter; And 1386 Tanzanians liked his update on Facebook regarding Tanzania

President Yoweri Museveni on Tuesday April 23, sent out his first tweet ever since joining the social media platform, Twitter -- Official Uganda's State House website reports.

Using his Twitter handle @KagutaMuseveni, the President saluted Kyambogo University science students for making a vehicle that uses ethanol instead of petroleum.

“I send my first tweet to salute Ugandan science students; they modified this

Askari sita wa Usalama Barabarani wafukuzwa kazi

Askari sita wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika wilaya za Rungwe na Mbeya waliofahamika kwa majina Coplo Johnson, PC Raymond, PC Simona, PC Shaaban, PC Kajolo na Sajini Hezron, wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kushawishi, kuomba na kupokea rushwa, blogu ya Mbeya Yetu imeripoti.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amenukuliwa akisema kuwa askari hao walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi na Hukumu kutolewa Aprili 24 mwaka huu na adhabu yao ikawa ni kufukuzwa kazi.

Aidha, askari wengine waliofukuzwa kazi hivi karibuni ni pamoja na PC James Kagomba aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la wizi wa kutumia silaha.

WP Prisca Kilwai anayekabiliwa na kesi ya wizi wa mtoto.

DC Marcelino Venance Na. 8084, PC Juma Idd Na. 3117 na askari mgambo MG Jackson Mwakalobo waliohukumiwa kifungo cha mwaka 1 kwa kosa la kusababisha kifo cha Dentho Kajigili, aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Ivumwe, Mbeya.

Akamatwa kuhusiana na vifo vya watoto 3 katika hoteli ya Landmark

Tukio la kusikitisha la vifo vya watoto watatu wenye umri wa miaka 6, 9 na 10 lililotokea hapo jana Jumapili, Aprili 27, 2014 majira ya saa 11 jioni katika bwawa la kuogelea la hoteli ya Landmark ya Mbezi Beachi jijini Dar es Slaam limesababisha kukamatwa kwa mfanyabiashara Mboka David (44) mkazi wa Kijitonyama -- aFikra Pevu imeripoti.

Habari zilizopatikana jana kutoka kwa kwa marafiki kupitia mawasiliano ya simu zilifahamisha kuwa watoto hao waliokumbwa na masaibu hayo walichukuliwa bila ya kutoa taarifa kwa wazazi wao na kupelekwa katika hoteli hiyo kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya kutimiza mwaka mmoja wa kuzaliwa ya mtoto mwingine.

Watoto hao walipoteza uhai walipozama katika bwawa hilo kwa kushindwa kuokolewa pale walipopiga kelele kuomba msaada.

Wanafunzi wafunzwa usalama na afya mahala pa kazi na barabarani

Mfanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Ammy Mlay akipima uelewa wanafunzi kuhusu amsula ya uslama na afya mahala pa kazi wakati wa semina ya mafunzo ya usalama mahala pa kazi na usalama barabarani iliyoandaliwa na kampuni ya Vodacom kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Msasani na Mbuyuni mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Oyster Bay jijini Dra es salaam. Semina hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Happy Paul (kushoto) na Ammy Mlay wakiwaonesha wanafunzi (hawapo pichani)kanuni ya lazima namba nne na sita ya usalama kazini kwa wafanyakazi wa Vodacom ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wafanyakazi wakati wote wanakuwa salama na wenye afya wanapotimiza majumu yao.Vodacom kwa ksuhirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni mwishoni mwa wiki waliendesha semina ya masuala ya afya na usalama kazini kwa wanafunzi wa shule za msingi Oyster Bay, Mbuyuni na Msasani.


* Mafunzo hayo yametolewa na kampuni ya Vodacom na kikosi Maaalum cha usalama barabarani Wilaya ya Kinondoni kwa shule za msingi Msasani, Mbuyuni na Oysterbay.

Dar es Salaam -- Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Kanda ya mkoa wa Kinondoni wamewapatia mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi wa shule za msingi Msasani, Mbuyuni na Oysterbay zote za wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa Vodacom wao wametoa mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa

NEC, ZEC embark on comprehensive capacity building


cid:image002.png@01CCE7DC.B5181EE0

    
NEC, ZEC embark on comprehensive capacity building
Bagamoyo, Monday 28 April 2014: Twenty (20) senior staff from the National Electoral Commission (NEC) and the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) will undergo a two-week train-the-facilitator programme based on the internationally renowned BRIDGE at the Oceanic Bay hotel in Bagamoyo. The training is expected to usher the two electoral management bodies (EMBs) in a new era of improved professional conduct of elections through the use of own staff to conduct BRIDGE or any other electronic training for both short term and long term professional development.  
BRIDGE stands for “Building Resources for Democracy, Governance and Elections” and

Mambo Yamebadilika - Chindo

[audio] Hotuba ya Rais Kikwete ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania

Iliyopachikwa hapo chini ni audio yenye hotuba ya alichokizungumza Rais Kikwete siku ya Ijumaa, Aprili 25, 2014 katika ukumbi wa PTA kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.Shukurani za rekodi na online upload ya audio hii zimwendee Hussein Momieh Hamis.

Pres. Obama on racist comment attributed LA Clippers Owner, Sterling


At a press conference in Kuala Lumpur, Malaysia, on Sunday, US President Barack Obama is quoted as saying the following regarding the controversy surrounding the racist comments (click here to listen to the audio) attributed to Los Angeles Clippers owner Donald Sterling:

 • “The owner is reported to have said some incredibly offensive racist statements that were published. I don’t think I have to interpret those statements for you; they kind of speak for themselves,”
 • “When people — when ignorant folks want to advertise their ignorance you don’t really have to do anything, you just let them talk. And that’s what happened here.”
 • “Obviously, the NBA is a league that is beloved by fans all across the country,” Obama said. “It’s got an awful lot of African American players. It’s steeped in African American culture. And I suspect that the NBA is going to be deeply concerned in resolving this.”
 • “The United States continues to wrestle with a legacy of race and slavery and segregation that’s still there — the vestiges of discrimination.
 • “We’ve made enormous strides, but you’re going to continue to see this percolate up every so often,” he added. “And I think that we just have to be clear and steady in denouncing it, teaching our children differently, but also remaining hopeful that part of why some statements like this stand out so much is because there had been — there has been this shift in how we view ourselves.”

Rais Kikwete azindua rasmi Kituo cha Magonjwa ya Moyo Muhimbili

Rais Jakaya Kikwete akiongea na mmoja wa wagonjwa watoto waliofanyiwa upasuaji kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo April 27, 2014

Rais Kikwete na Rais Mstaafu wa Namibia, Sam Nujoma Ikulu leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtembeza katika sehemu mbalimbali za Ikulu na Rais Mstaafu wa Namibia Mhe. Sam Nujoma aliyemtembelea leo April 27, 2014. Mhe Nujoma alikuwa ni mmoja wa watu mashuhuri waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano hapo jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtembeza katika sehemu mbalimbali za Ikulu na Rais Mstaafu wa Namibia Mhe. Sam Nujoma aliyemtembelea leo April 27, 2014.
Mhe Nujoma alikuwa ni mmoja wa watu mashuhuri waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano hapo jana.

Record heroin bust off Indian ocean near Kenya, Tanzania

HMAS Darwin's ridged hull inflatable boats, with members of the boarding party team embarked, approach the suspicious dhow to conduct a boarding.
HMAS Darwin’s ridged hull inflatable boats, with members of the boarding party team embarked, approach the suspicious dhow to conduct a boarding.

by Combined Maritime Forces

Australian warship HMAS Darwin, operating under the command of a Royal Navy Commodore and his British team has made the largest ever seizure of heroin from a dhow at sea.

The record breaking 1,032 kilograms haul, with an estimated UK street value in excess of 140 million pounds, was discovered onboard a dhow in the Indian Ocean 30 miles off the East African coast, near to Kenya and Tanzania.

HMAS Darwin’s crew found the dhow, a type of vessel common to the Middle East and Indian Ocean, on

Nigeria: Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania

Kikundi cha ngoma za asili cha Abuja Nigeria kikitoa burudani ya ngoma katika tafrija kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika hoteli ya Serena jijini Abuja.
Kikundi cha ngoma za asili cha Abuja Nigeria kikitoa burudani ya ngoma katika tafrija kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika hoteli ya Serena jijini Abuja.
Na: Geofrey Tengeneza – Abuja Nigeria

Jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wa Nigeria kwa ujumla, wameombwa kuja kuwekeza kwa ujumla na kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali vinavyopatikana nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay katika maadhimisho ya miaka hamsini 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi wa

Washington, DC: Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania

Ubunifu: Miaka 50 Ya Muungano wa Tanzania, Washington DC.
Ubunifu: Miaka 50 Ya Muungano wa Tanzania, Washington DC.

Mhe. Mwigulu Nchemba akikata Utepe Kuashiria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC zimefunguliwa rasmi. Kulia Kwake ni Balozi Libereta Mulamula na Kulia Kwake ni Waziri anayeshughulikia Muungano-Zanzibar Mhe. Mwinyihaji Makame.
Mhe. Mwigulu Nchemba akikata utepe kuashiria kuwa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano, Washington DC zimefunguliwa rasmi. Kulia  kwake ni Balozi Liberata Mulamula na kushoto kwake ni Waziri anayeshughulikia Muungano-Zanzibar, Mhe. Mwinyihaji Makame.

[audio] Kauli ya Makamu wa Rais Zanzibar, Maalim Seif kuhusu Muungano

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kujumuika katika Mkesha wa Muungano.Kulia kwake ni mwenyeji wake Wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi/. (picha: Tz Govt. Blog).

*Audio imepachikwa chini baada ya maelezo yafuatayo yalivyoandikwa na Hassan Hamad wa Ofisi ya Makamu wa Rais (OMKR)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Watanzania wana kila sababu ya kusherehekea miaka 50 ya Muungano kutokana na mafanikio yaliyopatikana.

Alitaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja kuimarika kwa hali ya usalama, ushirikiano na

Switzerland: Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania


Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Mhe. Modest Mero, akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya watu wa China-Geneva, Liu Jieyi katika tafrija maalum ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa ILO hii leo na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo balozi huyo China UN mjini Geneva, Balozi wa Kenya, Balozi wa Afrika Kusini, Balozi wa Togo, Balozi wa Botswana, Balozi wa Cameroon, Balozi wa Rwanda, wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na Watanzania waishio Switzerland. Kushoto ni Mke wa balozi huyo Rose Mero.

Mbeya: Hofu ya ‘ushirikina’ yakwamisha vita dhidi ya mimba kwa wanafunzi

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini.

Na Mwandishi wa TheHabari -- VITISHO na hofu ya vitendo vya ushirikina imebainika kuwa vikwanzo vya mapambano ya baadhi ya watu wanaowatia mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya.

Kauli hiyo ilitolewa juzi mjini hapa na baadhi ya wanakijiji kutoka katika baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela walipofanya mahojiano kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi alipotembelea vijiji hivyo.

Akizungumza mkazi wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Maria Kolneri alisema baadhi ya

Manyara: Vodacom yaisaidia Shule ya Barazani

Wanafunzi wa shule ya msingi Barazani iliyoko wilayani Mbulu mkoani Manyara wakiimba kwaya wakati wa tukio la makabidhiano ya jengo la darasa lililojengwa kwa msaada na Vodacom Foundation.

NW Dk Mahanga afungua Kongamano la Afya na Usalama katika matumizi ya kemikali sehemu za kazi ndogo


Washiriki wakijiandikisha nje ya ukumbi kabla ya kuanza kwa kongamano la afya na usalama katika matumizi ya kemikali sehemu za kazi
Naibu waziri wa Kazi na Ajira Dk Makongoro Mahanga amefungua kongamano la afya na usalama katika matumizi ya kemikali sehemu za kazi ndogo. Akitoa hotuba yake Naibu Waziri huyo amesema inatakiwa elimu na maelekezo mazuri yatolewe kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa kuhusu matumizi ya kemikali na usalama wa matumizi wa kemikali hizo.

Naibu waziri wa Kazi na Ajira aliongeza kwa kusema ripoti ya shirika la kazi duniani (ILO) ya mwaka 2004 inaonyesha kwamba, Duniani kote magonjwa yanayotokana na kemikali nii kwa kupitia njia ya

LIVE ONLINE NOW: Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano


Matangazo ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yalirushwa moja kwa moja online kupitia ikulu.go.tz  kutoka kwenye viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.

Usiku wa kuamkia leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alietunuku nishani na tuzo kwa viongozi mbalimbali wa Kitaifa na watumishi wa umma wapatao 86 waliotoa mchango wao katika kuulinda na kuudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka 50.

Zilizopachikwa hapa ni baadhi ya picha za waliotunukiwa zikifuatwa na picha za mkesha wa Muungano na zile zilizopigwa kutoka kiwanjani tarehe 26 Aprili 2014.

Mama Maria Nyerere akipokea nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano (Order) kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere.

Muungano 50 Celebrations Washington DC: Kilimanjaro Stars vs Zanzibar Heroes! Kombe uwanjani, Nyama choma...

KILIMANJARO STARS YAIHOFIA ZANZIBAR HEROES,

YAAGIZA MGANGA TOKA PANGANI!

NANI KUIBUKA KIDEDEA?

RATIBA KAMILI YA JUMAPILI HII HAPA...

null

Kingunge akerwa na kauli dhidi ya Jaji Warioba; Vikao vya Bunge la Katiba vyaahirishwa hadi Agosti 5

Mwanasiasa mkongwe na Mjumbe wa Bunge wa Bunge Maalumu, Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema si halali kumshambulia aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko, Jaji Joseph Warioba na ameonya wanaotoa lugha chafu dhidi yake, wasitumie Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama kinga yao.

Amesema CCM ni chama chenye adabu tangu kilipoanzishwa na mtu anayekitumia vibaya, kumshambulia  arioba au mjumbe mwingine yeyote, anakitukana chama kinachoongoza Serikali na wanachama wote:
“Mimi sitakubali na si halali kumshambulia Warioba au mjumbe mwingine yeyote binafsi, na tunapofanya hayo tusitumie kama ni msimamo wa CCM,”
alisema Kingunge jana bungeni mjini hapa alipokuwa akichangia mjadala wa Rasimu ya Katiba kuhusu Sura

Celebrating 50th Anniversay of Tanzania, China ties

BEIJING, April 26 (Xinhua) -- Chinese President Xi Jinping and his Tanzanian counterpart Jakaya Kikwete have exchanged messages of congratulations to mark the 50th anniversary of the establishment of diplomatic ties between the two countries.

Xi said China and Tanzania, which are all weather friends, have maintained unbreakable traditional friendship.

Since the establishment of bilateral ties 50 years ago, both sides have always respected, trusted and

[picha] Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress azuru ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress akikaribishwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh siku ya Alhamisi April 24, 2014 alipotembelea Ubalozi huo na kujitambulisha kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani)

Mahafali ya Pili Chuo cha Mafunzo ya Jinsia Tanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro (kushoto) akiwahutubia wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.

Na Thehabari.com, Dar es Salaam — MAHAFALI ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) yamefanyika Aprili 24, 2014 jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo hicho eneo la Mabibo. Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 9 wamehitimu mafunzo ya njinsia ngazi ya cheti.

Akizungumza kabla ya kuwatunuku vyeti, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro alikipongeza chuo hicho kwa kuendelea kutoa mafunzo ya jinsia nchini kwa ngazi mbalimbali jambo

LIVE ONLINE NOW! Rais Kikwete anazungumza ukumbini PTA

 Rais Jakaya Kikwete akiongea na Taifa kupitia mkutano wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwenye ukumbi wa PTA, Dar es Salaam

Matangazo ya moja kwa moja muda huu yamesitishwa baada ya Rais kumaliza hotuba yake aliyoitoa katika ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.

Matangazo yalikuwa yanarushwa moja kwa moja online kupitia: ikulu.go.tz

Wafanyakazi Vodacom waadhimisha Siku ya Malaria Duniani

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, Bw. Erick Mfinanga (kulia) na Bi. Farida Rashid (kushoto) wakionyesha vyandarua walivyokabidhiwa katika semina maalumu ya ugonjwa wa malaria na matumizi bora ya vyandarua kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kama sehemu ya kuadhimisha siku ya malaria duniani. Semina hiyo ilitolewa kwa ushirikiano wa Chuo hicho katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mbeya: Wanavijiji walaumiana kuhusu kudhibiti mimba kwa wanafunzi

Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Willson Mwamunyila (katikati) pamoja na wanakijiji wenzake wakizungumza na mwandishi wa habari hii.


WANAVIJIJI wa vijiji vya Shibolya, Usoha Njiapanda, Simambwe, Ikhoho na Ilembo Usafwa vyote vya wilayani Mbeya Vijijini wametupiana lawama kuhusiana na baadhi ya wazazi na viongozi wa vijiji kuwa wakifumbia macho watu wanaotuhumiwa kuwatia mimba wanafunzi wa msingi na sekondari na

UNHWA kuisaidia NIMR kugundua dawa kwa kutumia mimea

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea Kusini Bw. Young Woo Jin na ujumbe wake na uongozi wa NIMR walipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam

Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Tanzania (NIMR), imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea Kusini ambapo kampuni hiyo itaisaidia NIMR teknolojia mpya ya kufanya ugunduzi wa dawa za binadamu kwa kutumia mimea.

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam pembezoni mwa kongamano la 28 la kisayansi la NIMR, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dk. Mwele

MIsa ya kumbukumbu ya marehemu Joachim B. L. Kirambata

Joachim B. L. Kirambata enzi za uhai wake
Joachim Bwanampini Lebabu Kirambata enzi za uhai wake (02/02/1945 - 04/05/2103)

Tarehe 04/05/2014 umetimiza mwaka mmoja kamili tangu Mwenyezi Mungu akuite.

Ilikuwa siku ya majonzi makuu katika familia yetu siku kifo kilipotokea katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Unakumbukwa sana na familia yako, mkeo bi. Mary Kiarambata, Watoto wako Lilian, Joseph Filbert,

Washington DC: Maandalizi ya Sherehe za Miaka 50 ya Muungano

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akizungumzia maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya Muungano ofisini kwake Washington DC Jumatano, Aprili 23, 2014.
(picha: Sunday Shomari)


wavuti.com imeshirikishwa taarifa hii na Kwanza Production

Rais anakemea “wanasiasa wanaomtukana Nyerere na Karume” amekaa kimya matusi kwa Jaji Warioba na kauli za Lukuvi

NI dhahiri sasa kuwa mjadala wa Katiba mpya, hususan kipengele cha muundo wa Muungano, unaelekea kulipeleka taifa mahali pabaya. Japokuwa dalili za Bunge Maalumu la Katiba linaweza kuishia kuwa jukumu ghali kwa walipakodi masikini, hasa baada ya kusikika madai ya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kuwa posho ya shilingi 300,000 kwa siku haitoshi, lakini Watanzania wengi walikuwa na imani kwamba ‘upepo huo mbaya’ ungepita na hali ingekuwa shwari.

Hata hivyo, kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali inavyozidi kuwa mbaya. Kinacholeta wasiwasi zaidi

Mchango wa Maria Sarungi-Tsehai katika Bunge la Katiba

Mchango wangu wa kimaandishi kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba - 24 Aprili 2014

Mh. Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii nichangie kwa maandishi mjadala unaoendelea bungeni kuhusu sura ya 1 na ya 6 na kuhusu mwenendo mzima wa Bunge lako tukufu.

Mh Mwenyekiti, tokea tumefika Dodoma zaidi ya siku 70 tumeweza kushuhudia mengi, katika huu mchakato wa kujadili rasimu ya pili ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunamaliza siku rasmi tulizopangiwa bila kufanya maamuzi yoyote kuhusiana na Rasimu na bila muafaka.

Mh. Mwenyekiti, tunamaliza siku hizi 70, tukiwa tumegawanyika na kuparanganyika katika makundi, na

Not calling MPs ‘Honourable’, Kenyans risk KSh2M fine, jail

Kenyans risk being jailed for 12 months or paying Sh2 million for failing to refer to an MP as ‘Honorable’ when addressing him or her.
A proposed law seeking to bring order in addressing public officials in State functions prescribes tougher penalties for those who break the rule.

The same applies to those who fail to refer to the President as ‘Your Excellency, the Speaker as ‘The Right Honourable Speaker of Parliament’ and a judge of the Supreme Court ‘Your Lordship’.

The Order of Precedence Bill, 2014 prepared by Eldas MP Adan Keynan said the titles will promote the

Huduma ya kusajili kampuni, NGO

Anjoa Company Limited: Tonatoa huduma ya kusaidia kusajili makampuni, NGOs.

Pia, tunatoa business consutancy services kama vile:

- Company secretarial services
- Company registration,
- NGO registration
- Finance and Account consultancy,
- Loan software applications,
- Write-ups eg. project proposal ect.
- Social science research training and advice (Including academic research)

Tupo jijini Dar es Salaam

Wasiliana nasi kwa namba +255 (0) 759 692 024 au +255 (0) 688 510 564 au tuandikie kupitia: anjoa_li[email protected]

Karibu tukuhudumie.

[infographic] Treating Both Sides of Cyberbullying

The explosive growth of social media in recent years has enabled a lot new opportunities for kids and tennagers to turn to bullying online. The following infographic takes an in-depth look at cyberbullying statistics, as well as how to help treat the bullied and the bully.

Cyberbullying
Source: SocialWorkDegreeGuide.com

Serikali kudhibiti wasichana waendao China

Serikali imesema iko katika mikakati kuhakikisha inadhibiti vitendo vya wasichana kwenda China bila sababu maalumu ikiwa ni njia ya kudhibiti vitendo vya watoto wa kike kujihusisha kwa biashara ya ukahaba nchini humo, liliripoti gazeti la HabariLeo.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Ubalozi wa China nchini, zimeamua kuchukua hatua hiyo.

Sanjari na kulenga kuzuia wanaokwenda nchini humo bila shughuli zinazoeleweka, mkakati huo pia utashughulikia walioko nchini humo wakifanyishwa vitendo hivyo, warejee nchini. 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa

Bagamoyo International Festival of Arts and Culture


Ukiamua kupata fedha za kutosha, Inawezekana!
Kuna hii biashara ya mahindi ya kuchoma (maarufu kama gobo). Unaweza kulima kwa kutumia mtaji kidogo na kupata sarafu za kutosha.  Angalia mchanganuo ufuatao: kukodi shamba ekari moja wastani wa  tsh 50,000/=, kulima 30,000/=, kupalilia 30,000/=, mbolea mifuko mi-3, tsh 150,000/=, madawa wastani tsh 50,000/=; Jumla kuu ni tsh. 310,000/=. Gharama hii hauitoi mara moja bali ni kidogo kidogo kutegemea

[audio] Maelezo ya hatua wanayochukua "Tanzania Kwanza" nje ya Bunge

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaounda kundi la 'Tanzania Kwanza' wamezungumza na Waandishi wa habari leo na kuelezea mipango na mikakati watakayoichukua wakiwa nje ya vikao vya Bunge hilo.

 Tafadhali bofya kitufe cha pleya iliyopachikwa hapo chini, yenye audio kutoka 'Habari Maelezo,' ili kusikiliza.

Rais Kikwete azindua, Mnyika akata utepe wa ujenzi wa hospitali ya MUHAS, Mloganzila

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mkasi Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Mhe. John Mnyika ili na yeye akate utepe na viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 24, 2014. 
(picha hii na zilizopachikwa hapo chini ni kutoka IKULU)

[video] Jaji Warioba akionya kauli zinazoligusa Jeshi

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume na ufumbuzi wake kwa kutumia korodani za wanyama na vyakula asilia

KORODANI ZA MBUZI, KORODANI ZA KUKU NA DAWA YA JIKO KATIKA KUPONYA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

Korodani za jogoo
Korodani za jogoo

Ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa kwa ufasaha.

Tatizo hili linawakabili mamilioni ya wanaume duniani na limekuwa na athari nyingi kama vile kuvunjika kwa mahusiano na hata ndoa.

Mwanaume mwenye tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume anakuwa hana uwezo wa kumtosheleza mwanamke kwenye tendo la ndoa.

DALILI ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:-

[audio] Mchango wa Kadari Singo Bungeni kuhusu uraia-pacha

Mhe. Kadali Lincoln Singo
Mhe. Kadari Lincoln Singo


wavuti.com imeshirikishwa post hii na SwahiliVilla blog, shukurani.

Scholarships for International Undergraduate Students 2015 from Japan's Government

Japan's Ministry of Education, Culture, Sports, Science and Technology(MEXT) offers scholarships to international students who wish to study at Japanese universities as undergraduate students under the Japanese Government (MEXT) Scholarship Program for 2015.

Those who wish to study in Japan as an undergraduate student must choose a field of major from (1) Social Sciences and Humanities  (2) Natural Sciences

Please click here for details.

Mabingwa wa soka, Azam FC wavuna 75M kutoka Vodacom

Meneja Uhusiano wa Nje Vodacom Tanzania, Salum Mwalimu akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Pamoja naye katika picha, wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura na Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom, Ibrahim Kaude.

* Timu yenye nidhamu kuvuna 16M

Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imetangaza kuipatia timu ya Azam FC kitita cha Sh 75 kama zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka bingwa wa ligi msimu wa 2013/2014.

Mwaka jana Bingwa wa Ligi Kuu Vodacom ambapo ilikuwa timu ya Yanga alizawadiwa kitita cha

Mjumbe azungumzia asili ya makabila ya Zanzibar

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Riziki Said Lulida, ameonya Watanzania kuacha kubaguana kwa misingi ya upande wa Muungano kwa kuwa wao ni ndugu wa damu.

Kwa mujibu wa Lulida, asilimia zaidi ya 95 ya Wazanzibari, wanatoka Tanzania Bara na walifika Zanzibar kabla ya Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa mwaka 1964.

Akichangia mjadala wa rasimu ya Katiba kuhusu sura ya kwanza na ya sita juzi, Lulida huku akitoa historia ya asili ya wenyeji wa Zanzibar, alisema hakuna

Twaweza: What do people really think of the constitution? Je, Watanzania wanaionaje katiba?

Mjadala katika Bunge la Katiba umejaa na ubishi na mgawanyiko, lakini Watanzania wameungana kutaka katiba yenye uwajibikaji zaidi kwa viongozi wa umma na mfumo wa utawala wenye uwazi zaidi. Miongoni mwa vifungu katika rasimu pili ya katiba ambavyo vinaungwa mkono na wananchi walau sita kati ya kumi ni:
 • Idadi kubwa ya Watanzania wanaunga mkono vifungu vinavyohusiana na haki ya wananchi kupata taarifa au habari, na kuongezeka kwa uwajibikaji na uwazi wa viongozi wa umma
 • Mapendekezo kwa ajili ya utaratibu wa kudhibiti na kuwajibisha wabunge na mgawanyo wa madaraka ili kuepuka migogoro ya kimaslahi yanaungwa mkono na wengi
Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la

Salam za Sherehe za Miaka 50 ya Muungano kutoka CCM-UK

CHAMA CHA MAPINDUZI - TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM

 
Website: ccmuk.org, Blog: ccmuk.org/blog, Facebook page: chama cha mapinduzi uingereza, twitter: CCMUK 1, Contacts Phone +44 74 04 863333, +447545 213515. E-mail – [email protected] Uongozi na Wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Uingereza (UNITED KINGDOM) pamoja Watanzania wanaoishi nchini Uingereza kwa pamoja wanajumuika na Watanzania wote katika kuadhimisha kilele cha sherehe za miaka hamsini (50) ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitazofanyika Tarehe 26 Aprili, 2014 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, na pia kuwaombea shamrashamra za amani na Utulivu katika Mkesha wa Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utakaofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Tanzania Bara na Viwanja vya Maisara, Zanzibar kuanzia saa 4:00 usiku wa tarehe 25 April 2014.

Vile vile Mwenyekiti wa CCM UK anayemaliza muda wake Ndugu Maina A Owino anapenda kutoa shukrani za