Taarifa ya Mnyika ya kusudio la kuurejesha mjadala Bungeni

WAZIRI MUHONGO, WAZIRI MKUU PINDA NA SPIKA MAKINDA WAJITOKEZE KUTOA MAELEZO JUU YA HATUA WALIZOCHUKUA KUHUSU UFISADI NA UDHAIFU KATIKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI; WASIPOFANYA HIVYO NITAUREJESHA MJADALA BUNGENI NOVEMBA 2014


Itakumbukwa kwamba tarehe 29 Aprili 2014 kupitia Hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Nishati na Madini (nimeambatisha nakala) juu ya mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara tajwa kwa mwaka 2014/2015 nilieleza ufisadi na udhaifu uliopo katika Wizara hiyo na mashirika yaliyo chini yake.

Kutokana na kukithiri kwa ufisadi na udhaifu huo nilipendekeza hatua zifuatazo ziweze kuchukuliwa katika Mkutano wa 15 wa Bunge uliokuwa ukiendelea wakati huo, nanukuu:

“Mosi, Spika aruhusu kabla ya mjadala huu kuendelea ziwekwe mezani nakala ya ripoti zote za

Utaratibu mpya na gharama za maegesho Mlimani City


CCM yaipongeza FRELIMO

Nape Nnauye

Na Bashir Nkoromo -- CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa furaha Chama cha FRELIMO kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu.

Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya FRELIMO, Filipe Nyusi ameibuka kidedea na sasa ndiye Rais Mteule wa Msumbiji ambaye baada ya kuapishwa atashika mikoba itaakayoachwa na Rais anayemaliza muda wake, Armando Gwebuza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao

Buriani Ben Kiko

Ben Kiko

Aliyekuwa mtangazaji maarufu wa habari wa SHIHATA (Shirika la Habari Tanzania) na RTD (Radio Tanzania Dar es Salaam ambalo sasa ni TBC yaani Shirika la Utangazaji la Taifa), bwana Ben Hamis Kikoromo al maaruf "Ben Kiko" ameaga dunia usiku wa leo katika hospital ya Taifa ya Muhimbili (Muhimbili National Hospital - MNH) alikokuwa akitibiwa figo.

Ben Kiko alihamishiwa katika hospitali ya jeshi ya Milambo, mkoani Tabora ambapo alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.

Mzee Kiko alijizolea umaarufu katika tasnia ya utangazaji wakati wa vita ya Kagera (Tanzania na Uganda) kutokana na taarifa zake za kusisimua wakati wa mapigano.

Mwaka 2012 mwanahabari huyo mkongwe alitunukiwa Tuzo ya Fanaka ya Maisha (Lifetime Achievement Award) kutokana na mchango wake katika uandishi wa habari.

Kabla mauti hayajamfika, Ben Kiko alikuwa akifanya kazi katika redio ya Voice of Tabora.

Apumzike pema!

Awafariji wote waliofikwa na msiba huu.

Ili kuokoa maisha ya Watanzania, Serikali isikwepe kulipa deni MSD

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
30 Oktoba 2014

Serikali isikwepe kulipa malimbikizo ya madeni MSD kuokoa maisha ya Watanzania!


Sikika imesikitishwa na tamko lililotolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kuhusiana na kushindwa kwa vituo vya huduma za afya kununua dawa MSD kutokana na kuongezeka kwa deni. Ni wazi kuwa waziri hajalipa tatizo hili uzito unaotakiwa na kutambua kuwa baadhi ya wagonjwa wanaweza kupoteza maisha kutokana na tatizo hili.

Sikika inatambua kuwa, mapato yatokanayo na uchangiaji katika huduma za afya ni moja tu ya vyanzo vinavyotumika katika kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini. Na pia inatambua kuwa chanzo hiki pekee hakiwezi kuziba pengo kubwa la ufinyu wa bajeti ya dawa na vifaa tiba muhimu ambao hauendani na mahitaji halisi. Kwa mfano, makadirio ya mahitaji ya dawa nchini kwa

Rejea: Taarifa ya CAG ya ukaguzi maalum wa IPTL wa akaunti ya Tegeta Escrow

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM WA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW
(UKAGUZI WA IPTL)


Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inapenda kuujulisha Umma kuwa Ukaguzi Maalum wa akaunti ya Tegeta Escrow ambao unafahamika kama Ukaguzi wa IPTL unaendelea na unaongozwa na Hadidu za Rejea (ToR) zilizotolewa na kisha kuridhiwa na Ofisi ya Bunge na Wizara ya Nishati na Madini.

Ukaguzi wa akaunti ya Tegeta Escrow uliombwa na Katibu wa Bunge na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini. Ukaguzi huu unalenga kufanya uchunguzi wa kina ambao utatoa taarifa kamili yenye kuonesha hali halisi kuhusu miamala (transactions) kwenye akaunti maalum ya Tegeta Escrow kisha kutoa taarifa kuhusiana na ukaguzi huo.

Kwa kuwa Hadidu za Rejea pekee haziwezi kuonesha ukubwa wa kazi bali utekelezaji wa kazi yenyewe ndio unaoweza kutoa taswira halisi, ni  vyema umma wa watanzania ukatambua kuwa

PAC yaahidi kuwalinda maafisa wa ofisi ya CAG waliotishiwa maisha na viongozi

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Public Accounts Committee - PAC) imesema itawalinda na kuwatetea maafisa wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General - CAG).

Uamuzi huo unatokana na taarifa za maafisa hao kutishiwa maisha na baadhi ya Viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma, zaidi ya shilingi bilioni 40.

Hatua hiyo ilielezwa katika mkutano uliofanyika mkoani Mwanza, wa majumuisho ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali ambayo iliwataka viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhudhuria mkutano huo ili kutoa majibu ya tuhuma hizo. Hata hivyo viongozi hao walipuuza agizo la kamati, hivyo kumlazimu Mwenyekiti kuuvunja mkutano huo.

Mjumbe wa kamati hiyo, Kange Lugora alisema kamati hiyo iliishauri wizara husika kushirikiana nao pamoja tangu mwanzo wa ziara yao katika majumuisho ya kamati hiyo ili kubaini yanayotendeka katika miradi ya maendeleo.

“Kitendo cha wizara kutoshiriki katika majumuisho ya kamati hii ni kuendelea kuhalalisha ubadhirifu unaoendelea kwenye halmashauri, tunaonyeshwa miradi hewa na serikali ngazi ya wizara ilipaswa wajionee wenyewe,” alisema.

Garden Avenue sasa ni Hamburg Avenue


Mtaa wa Garden ulioko jijini Dar es Salaam umebadilishwa jina na kuwa Hamburg Avenue.

Hafla ya kubadili jina hilo ilifanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, amesema uamuzi wa kubadili jina la mtaa huo limetokana na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania na jiji la Hamburg la nchini Ujerumani .

Kutokana na ushirikiano katika majiji hayo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kikosi cha zimamoto, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Philip Mwakyusa amesema Serikali ya Ujerumani itasaidia katika ujenzi wa mtambo wa kutengeneza mbolea kwa kutumia taka ngumu.

Polisi akamatwa kwa kumkata mfanyakazi wake vidole vinne

Steven Magessa (18) akizungumza na blog ya GSengo kusimulia masaibu yaliyomkuta.

ASKARI POLISI ASHIKIRIWA KWA KUMKATA MFANYAKAZI WAKE VIDOLE VINNE KWA PANGA KWA MADAI YA KUMWIBIA DEKI YA VIDEO NYUMBANI KWAKE.


JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake.

Tukio hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka huu katika kijiji cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la Igogo.

Akizungumza na G.SENGO BLOG kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari huyo kulikuja

Somo lenye maksi nyingi...


Peruzi "Shule Direct" bure kwenye app ya Internet.org

Kwenye picha maafisa wa Shule Direct (waliosimama) Bw. Fayaz Valli na Bi. Iku Lazaro wakiwa na ofisa wa Facebook Bw. Nahid Hirji (aliyekaa kushoto) na Bw. David Zacharia mwakilishi kutoka Tigo katika uzinduzi wa Internet.org

Taarifa kuhusu tetesi za uteuzi wa Konseli wa Heshima Uchina

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Hivi karibuni kumezuka taarifa za upotoshwaji zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali ya Tanzania imemteua Bw. Salaah, Mkurugenzi wa Home Shopping Centre, (pichani ) kuwa Konseli wa Heshima (Honorary Consul) kwenye mji wa Guangzhou kwenye Jimbo la Guandong.

Watoa taarifa hizo, hawakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yao zaidi ya kutoa picha mbalimbali za Bw.Salaah kutoka kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Taarifa hizo sio za kweli. 

Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za mahusiano ya kidiplomasia ya China, nafasi ya Konseli wa

How to minimize chances of a ticket when police stops youIn the USA, when pulled over by a police officer –

Do not move, do not look around, do not start digging for your paperwork.
 1. Pull over quickly and as far as safely possible
 2. Roll down your window completely (Not half way, not an inch so you can speak through the crack. All the way. Among other things, it will show that you have nothing to hide.)
 3. Turn on your overhead interior light (If it is not broad daylight out.)
 4. Put your hands on the steering wheel at 10 and 2
 5. Do not admit that you broke the law
 6. If asked for license and papers, announce your movements beforehand
 7. Sit still while waiting for the officer to return
 8. Do not say anything remarkable to the officer at the end of the stop
If the officer comes back with a ticket, do not argue with the officer. Do not declare, "I will see you in court!" Take the ticket, say Thank You. Signal that you are going re-enter the roadway, do so safely and go about your business. You do not want the officer to remember you. If you decide to fight the ticket, with or without an attorney, you may seek a plea deal of some sort. The officer will likely be consulted. An officer may be in court on a particular day with a stack of tickets. They probably can't all be tried due to time constraints. Some will get deals, some will not. You know who gets the deals? The harmless tickets where the driver did nothing to stick out in the officer's mind.

3 Steps for staying strong when things go wrongHappiness is not a goal; it’s the by-product of a life well lived. Deep down, you know this is true. And you also know it isn't always easy.

Life is hard sometimes. It’s impossible to live well without encountering struggle, and there are some seasons in our lives that are especially hard.

For Marc and me, one such season occurred in the fifteen months between September 2008 and December 2009. It was a period of profound loss, beginning when I lost my breadwinning job during the downturn in the economy. It was a scary and financially uncertain time for our family. Worry seeped into everyday life.

As we were learning to navigate our new reality, we were hit with a devastating loss: the death of a

Peroni Presents Deep Soulful House


Join the party this Friday at Peroni Nastro Azzurro Scene to be Seen at News Cafe; enjoy great music from DJ C-Note and DJ C-2 and great company!"

Uchaguzi Mkuu 1995 "siku ile kabisa sitaisahau na naamini ilikuwa ni hujuma" Jaji Ramadhani

Jaji Augustino Ramadhani
Augustino Ramadhani

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyosimamia uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo wa wa vyama vingi vya siasa wa mwaka 1995, Jaji Augustino Ramadhani, amesema kwamba uchaguzi huo katika jiji la Dar es Salaam ulihujumiwa.

Jaji Ramadhani alibainisha hayo katika mahojiano maalum na NIPASHE nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana, baada ya kuulizwa kile ambacho hatakisahau katika kipindi chake cha utumishi alipokuwa NEC.

“Kitu ambacho sitakisahau nilipokuwa makamu mwenyekiti wa NEC ni ule uchaguzi wa kwanza wa Multipartism (vyama vingi) Dar es Salaam, mwaka 1995,” alisema.

Jaji Ramadhan alisema wote waliokuwa katika tume hiyo hawatausahau uchaguzi huo kutokana na

Taarifa ya TRA ya yatokanayo na ziara ya ujumbe wa IMF

HABARI KWA UMMA

Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Wahitimisha Ziara yake Tanzania
Ujumbe wa wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ukiongozwa na Bw.Hervé Joly ulitembelea Tanzania kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 29 Oktoba 2014. Ujumbe wa IMF umefanya majadiliano ya tathmini ya kwanza ya Mpango wa Ushauri wa Sera za Uchumi (Policy Support Instrument -PSI) ulioidhinishwa na Bodi Tendaji ya IMF tarehe 16 Julai, 2014.

Ujumbe wa IMF ulikutana na Mhe. Mohamed Gharib Bilal , Makamu wa Rais wa Tanzania ,Mhe. Saada Mkuya Salum ,Waziri wa Fedha, Prof. Benno Ndulu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na maafisa waandamizi wa Serikali.

Wakati wa kuhitimisha ziara, Bw. Joly alitoa taarifa ifuatayo:

Daraja la kuunga Dar – Zanzibar laja

BAADA ya ndoto ya kuziunganisha pande mbili za katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni kwa daraja lenye umbali wa meta 680, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaangalia uwezekano wa kujenga daraja la kihistoria zaidi litakalounganisha Dar es Salaam na Zanzibar.

Kwa sasa, uongozi wa shirika hilo upo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania Bara na Unguja, kwa upande wa Zanzibar.

Umbali kati ya Dar es Salaam na Zanzibar ni kilometa 73.43, sawa na maili 45.62 hivyo kuwapo kwa

Bid to expel Shy Rose Bhanji from EALA flop

Bhanji defending herself before the Assembly yesterday. (John Mbanda)

Suspension of a member of the East African Legislative Assembly from Tanzanian, Shy Rose Bhanji, from the Assembly’s commission was last evening halted due to lack of quorum minutes before members could cast their votes.

The Assembly had shelved the first business on the order paper to debate a motion that sought to review the rules of procedure that had been interrupted in March to prioritise Bhanji’s suspension.

But just as members were readying themselves to vote by way of secret ballot after a three-hour debate, Ugandan MP Susan Nakawuki brought it to the attention of the Speaker that though the members in the Assembly were more than the required three quarters of the Assembly, Tanzania did not have a

Askari awekwa rumande kwa kumjeruhi raia

Na Kassian Nyandindi, Mbinga

JESHI la Polisi wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, limeingia katika kashfa mpya kufuatia askari wake wa usalama barabarani kumjeruhi mwendesha pikipiki kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kichwani, na kumsababishia jeraha ambalo lilisababisha dereva huyo kutokwa na damu nyingi.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 20 mwaka huu majira ya mchana, eneo la stendi ya magari ya abiria mjini hapa, ambapo askari huyo anayejulikana kwa jina la Msafiri Kilango, ndiye aliyefanya kitendo hicho kwa kumchoma kichwani dereva wa pikipiki aitwaye Erick Shonga.

Ajali mbaya ArushaPicha (juu na chini) za ajali mbaya iliyotokea jioni ya leo huko Tengeru kuelekea Usa River iliyolihusisha lori na gari dogo la abiria (Hiace) ambayo taarifa zinasema kuwa waliopona ni wawili (mtoto mdogo, na mtu mzima anayetajwa kuwa dereva bila kusema wa gari gani kati ya hayo).

Wanafunzi wa Kambangwa waendelea kunufaika na mradi wa kompyuta wa Vodacom na Samsung

Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakioneshwa na Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza moja ya progamu zinazopatikana katika Kompyuta zinazowawezesha kupata taarifa ya masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.

6 Ways to save when planning on big purchasesIf you live in the USA, big buys can bring big savings if you time them right.

Let's face it. Whether it's a new car, mattress or your dream swimming pool, you always have a major purchase on the horizon. The following tips can help you get the best deals on your big buys.

Looking to Move
Some experts say January is the best month to make an offer on a house because prices tend to be lower due to less competition. Springtime brings more buyers onto the market.

America's Department of State leads Partnership Opportunity delegation to Tanzania

The Secretary’s Office of Global Partnerships, in partnership with the Aspen Institute, the International Trade Center, and the Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), will lead a delegation of U.S. investors, entrepreneurs, and philanthropists to Tanzania as part of the Partnership Opportunity Delegations (PODs) initiative October 27-November 1.

Deputy Assistant Secretary of State for Public Affairs David Duckenfield will lead the State Department’s participation. The delegation will travel to Dar es Salaam, Bagamoyo, and Zanzibar to focus on the investment and entrepreneurship sector and explore investment and trade opportunities with Tanzanian firms and startups. During the POD, participants will engage government

Haya, Kashifa ya ufisadi NHIF

MFUKO wa Bima ya Afya (NHIF), umekumbwa na kashfa ya ufisadi ya kutumia zaidi ya sh. milioni 200 kununua gari jipya ambalo wamemkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.

Pia Bodi ya mfuko huo ambayo hupata fedha kutokana na michango ya wanachama wake, imetumia zaidi ya sh. bilioni mbili katika kipindi kisichozidi miezi sita badala ya mwaka mzima kama ilivyotengewa kwenye bajeti ya mfuko huo kwa mwaka huu wa fedha.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano, umebaini kuwa gari hilo lilinunuliwa kwa ajili ya matumizi ya Mkurugenzi wa Mfuko huo.

Gari hilo aina ya Nissan toleo jipya kabisa, lenye namba za usajili SU 39931, lilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Rashid Oktoba 11, mwaka huu, saa 9.15 na sasa limebadilishwa

Shirika la kijasusi latumia jina la gazeti kumnasa mshukiwa kwa kumtungia habari

Ingawaje ilifahamika kuwa Shirika la ujasusi la Marekani, FBI, lilitumia 'spyware' kuchunguza watu, siku ya Jumatatu ya wiki hii ndipo shirika moja la habari la nchini humu, Seattle Times, liliponabahi ya kuwa FBI walitumia jina lake kama chambo kutuma habari ya bandia, ili kupata taarifa za mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka na hatimaye kumkamata.

FBI walifahamu kuwa kutumia ujumbe wa barua pepe wenye ahadi za fedha nyingi almaaruf, Nigeria scam, wasingefanikiwa kwa hiyo walihakikisa wanaandika ujumbe ambao mtumiwaji atavutiwa na kubofya linki ili kusoma zaidi, bila ya kufahamu kuwa link hiyo ilikuwa bandia na habari yenyewe isiyo ya kweli.

Mathalan, walitumia tovuti ya mtandao wa kijamii, MySpace na chambo cha habari ya hatari ya

State of Freedom of the Press 2014 in Tanzania

2014 Scores
 • Press Status: Partly Free
 • Press Freedom Score (0 = best, 100 = worst): 55
 • Legal Environment (0 = best, 30 = worst): 18
 • Political Environment (0 = best, 40 = worst): 22
 • Economic Environment (0 = best, 30 = worst): 15
Throughout 2013, as Tanzania's increasingly unpopular ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party confronted the growing influence of the main opposition Chadema party, threats and attacks against journalists increased across the country, casting a pall over critical reporting in the run-up to parliamentary elections scheduled for 2015. In addition, press freedom was restricted by a number of anti-press laws that remained on the books despite challenges from media associations.

Although the constitution provides for freedom of speech, at least 17 laws encourage self-censorship and limit the ability of the media to function effectively. The most notorious and widely enforced of these laws is the 1976 Newspaper Registration Act, which empowers authorities to ban publications "in the interest of peace and good order." In July 2012, the Information Ministry had banned the Swahili-language weekly MwanaHalisi indefinitely on vague charges of sedition and false reporting for

Haya, PAC yaipa TanTrade saa 48 kuhusu yaliko magari 5, pikipiki 8 za Serikali

MAKUCHA ya Bunge, kupitia Kamati yake ya Hesabu za Serikali (PAC) imeendelea kufichua maovu katika idara za Serikali na Mashirika ya Umma, safari hii ikiwa zamu ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TanTrade) iliyopewa saa 48 kuwaanika wahusika wa magari matano na pikipiki nane zilizoyeyuka katika mazingira ya kutatanisha.

Mali hizo za umma, zinatajwa kununuliwa na iliyokuwa Bodi ya Biashara ya Nje (BET, sasa TanTrade) na kusajiliwa kwa namba za Serikali (STK), lakini bila maelezo yoyote, zimegeuzwa na kusajiliwa kwa namba binafsi. Maagizo hayo yalitolewa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe wakati kamati hiyo ikikagua hesabu za mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Mamlaka hiyo mwaka 2012, ilipokuwa BET, wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Nyerere, maarufu kama Sabasaba,

Ushauri wa biashara unazoweza kufanya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio. Kwa wiki chache zilizopita kulikuwa na makala ya ushauri kwa wanafunzi wanaoanza Chuo Kikuu, pia tumewahi kuweka makala za ushauri kwa wahitimu wa vyuo vikuu. Leo tutatoa ushauri mwingine kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo yao ya vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu.

Kabla ya kuingia kwenye ushauri huo kwanza tupate maoni ya msomaji mwenzetu:
Habari za kazi, ninakupongeza kwa makala nzuri na za kuelemisha, ninaombi moja kwako utoe makala ya biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaweza kufanya huku anaendelea kusoma?
Hayo ndio yalikuwa maoni ya msomaji mwenzetu aliyetaka kujua ni biashara gani au ujasiriamali gani mwanafunzi wa Chuo anaweza kufanya.

Kuna maswali matatu muhimu ya kujiuliza katika swala hili:-

Swali la kwanza, je inawezekana kufanya biashara au ujasiriamali ukiwa Mwanafunzi wa Chuo?

Gharama za kulala Muhimbili sasa ni 5,000/= kwa siku

(picha: wavuti.weebly.com)

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imepandisha gharama za huduma hospitalini hapo na sasa mgonjwa atakayelazwa atalazimika kulipa Sh5,000 kwa siku.

Gharama hizo zitalipwa kwa wagonjwa wote wa rufaa, ilisema taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Marina Njelekela na kusambazwa kwenye vyombo vya habari.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa gharama mpya zilianza kutumika Oktoba 17, mwaka huu. Hata hivyo, taarifa hiyo haikufafanua uamuzi wa kupandisha gharama hizo.

Alipofuatwa ili kutolea ufafanuzi mabadiliko hayo, Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Algaesha

Kontena laangukia daladala na kulipondaLori la mizigo ambalo limefunga tela limeangukia daladala (aina ya Hiace yenye namba za usajili T769 AFP) lililokuwa katika kituo cha mabasi katika eneo la Jet-Lumo.

Daladala hilo lilikuwa limeegeshwa katika kituo cha Kona, mwisho wa lami likisubiri abiria na mara semi-trailer ilipokuwa ikikunja kona, kontena lililokuwa limepakiwa lililiangukia daladala hiyo.

Haijafahamika ikiwa ajali hiyo ilisababisha majuhi ama vifo.

Juhudi za gari la kunyanyua makontena zilishindwa kuzaa matunda kutokana na kuzidiwa na uzito wa kontena ambalo kila likinyanyuliwa lilizidi kushuka chini na kuiponda bodi ya Hiace.

Taarifa ya DAWASCO ya kukatwa maji Dar es SalaamDawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Alhamisi na Iijumaa ya tarehe 30 na 31 Octoba 2014, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Chambezi, Bagamoyo.

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji;
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na

Rais Kikwete aondoka Vietnam kurejea Tanzania

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014.

Msanii aliyekamatwa na dawa za kulevya apelekwa Segerea

Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chidi Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.

Chid Benz, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata Kei’ ili avae vizuri nguo.

Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo

Africa Diaspora Marketplace III launched at the Tanzanian Embassy in USA

Jeffrey L. Jackson, Senior Private Sector Advisor, USAID speaking about the launch of ADM III. 

The Embassy of Tanzania in Washington, DC hosted the launch of the African Diaspora Marketplace III (ADMIII), on October 27th 2014. ADM is an opportunity for African diaspora members who are involved in businesses in their home country to acquire a grant from the United States Agency for International Development (USAID), which works together with Western Union and Homestrings to provide grants and technical support to these businesses. The Marketplace was initiated in 2009 in

Taarifa ya Wizara kuhusu habari iliyochapishwa na gazeti la Jamhuri

TAARIFA RASMI

Katika gazeti la Jamhuri la Jumanne Agosti 19 – 25, 2014 ISSN No. 1821-8156 Toleo No. 150, zilichapishwa taarifa potofu zenye kichwa cha habari; 

KASHFA IKULU;
 • Nyalandu atumia Leseni ya Rais kuua wanyamapori 704 bure,
 • Watakaouawa wamo pia tembo 8, chui 8, Simba 8, ndege,
 • Wauaji ni Wamarekani marafiki wa Waziri wa Maliasili.
I. Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwafahamisha Umma kuwa, tuhuma hizi si za kweli. Tuhuma hizi zimetolewa na watu wenye nia ovu na zimelenga kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na kumchafua mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu, kumshushia Heshima, kumdhalilisha kwa umma ili kumpunguzia dhamira, malengo na kasi ya kupambana na ujangili.

Ukweli ni kwamba Familia ya Freidkin ilipewa Leseni Maalum/Leseni ya Rais (Special

Tanzania: "la kutambua ndoa za jinsia moja, hilo tumekataa"SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.

“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata Katiba yetu

Karibu Festival kupambwa na Jhikoman, Zawose, Maembe, Prof. Jay, Barnaba...

Msemaji wa tamasha la Karibu Music Festival, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.

Wapo pia Prof. Jay, Barnaba, Shilole

Na Andrew Chale

WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari

Haya, Vigogo wa dawa za kulevya wauza mali na "kutoweka"

SIKU chache baada ya kunaswa kwa watuhumiwa wanaotajwa kuwa ni vinara wa kusafirisha na kuingiza dawa za kulevya nchini, hali imeanza kuwa tete kwa vigogo wengine wa biashara hiyo.
Baadhi ya vigogo wakiwemo wafanyabiashara wakubwa nchini, wameanza kukimbia nje ya nchi kukwepa mkono wa sheria, huku wengine wakisubiri hali itulie ndipo wajitokeze.

Hatua hiyo inatokana na askari wa Kikosi Maalumu cha Kudhibiti Dawa za Kulevya kuendelea kuwasaka vinara wa biashara hiyo kimya kimya, ikiwa ni mkakati wa kusambaratisha mtandao wa biashara hiyo haramu nchini.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikosi hicho, zinasema kuwa operesheni hiyo imekuwa ikifanyika kwa usiri mkubwa, kiasi cha mamlaka zingine kutofahamu kinachoendelea.

Bomu lategwa TBC na jirani na wanapokaa Polisi; JWTZ yatliegua

Bomu lenyewe kama linavoonekana katika picha.

Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo Mshangano cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.

Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji na watu wasiojulikana lilitegwa hatua zinazokadiriwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwa mujibu wa wataalamu wa

Walipoteza cheti cha NECTA kulipia 100,000/= wapate nakala

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA), limeanzisha utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa gharama ya sh. 100,000.

Utaratibu huo utawanufaisha watahiniwa waliohitimu kuanzia mwaka 2008, ambao vyeti vyao viliwekwa picha.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema hatua hiyo itapunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa sababu mbalimbali.

Taarifa kwa viongozi kuhusu urejeshaji fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni


Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inawataarifu Viongozi wote wa Umma nchini kwamba tarehe ya mwisho ya kurejesha Fomu za kutolea TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI ya viongozi kwa Kamishna wa Maadili kwa mwaka huu ni tarehe 31/12/2014. 

Fomu hizo za kutolea tamko zimeanza kutolewa na zinapatikana katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu Dar es Salaam na katika ofisi za Kanda za Mashariki Kibaha, Arusha, Dodoma, Tabora, Mwanza, Mbeya na Mtwara. Pia Fomu hizo zinapatikana katika Tovuti ya

Ushauri kwa wanaoanza Elimu ya Juu mwaka huu

Mwezi huu wa octoba wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu hapa Tanzania wameanza kuripoti kwenye vyuo walivyopangiwa. Awali ya yote nichukue nafasi hii kuwapongeza wale wote ambao wamepata nafasi ya kuendelea na elimu hii ya juu. Iwe ni kwa nafasi ya cheti, stashahada au hata shahada kuna kazi kubwa umeifanya huko nyuma na sasa unaingia kwenye ngazi nyingine ya elimu.

Leo naomba nichukue muda wako kidogo kukupa ushauri ambao unaweza kuwa msaada mkubwa sana kwako kama utaufuata. Ushauri nitakaokupa hapa sio namna gani ya kusoma maana naamini kwa miaka zaidi ya kumi uliyokaa kwenye mfumo wa elimu, unajua ni jinsi gani ukisoma utafaulu na jinsi gani ukisoma utafeli. Hivyo endeleza mbinu zilizokusaidia nyuma na ziboreshe zaidi ili uweze kupata ufaulu mzuri.

Ushauri mkubwa nitakaokupa hapa ni kuhusu mafanikio na uchumi.

Mpaka sasa umeshaimbiwa sana wimbo huu kwamba nenda shule, soma kwa bidii, pata ufaulu mzuri,

Statoil scholarship for Master Programme in Energy and Petroleum

Background

Since 2011 the University of Dar es Salaam (UDSM), specifically the Department of Chemical and Mining Engineering, the Norwegian University of Science and Technology (NTNU) of Norway and the Angolan University of Agostinho Netto are collaborating under the ANTHEI project to train professionals for petroleum engineering and geosciences at Masters level. Already three batches of a total of 28 Tanzanian students have been enrolled under the program. In this program the students spend one year in Norway for class work and another year at the University of Dar es salaam and the industry for project work and thesis. While in Tanzania the students are under the responsibility of the Tanzanian project coordinator at the University of Dar es Salaam with the support of local professors, NTNU Professors and Statoil Professionals. Statoil is a Norwegian oil Company already engaged in petroleum activities in Tanzania.

Under the same scheme, another batch of 10 students will be granted scholarship next year (2015) to undertake M.Sc. in Petroleum Engineering and in Petroleum Geosciences.  The scholarship covers subsistence allowance (stipend), travel grant to and fro, tuition, insurance and stationeries. The certificate will be issued by NTNU.

M.Sc. Petroleum Engineering and M.Sc. in Petroleum Geosciences

Rais Kikwete ziarani nchini Vietnam


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong, katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo Jumatatu Oktoba 27, 2014.

Job opportunity at Sikika for a Head of Finance

SIKIKA is a non-governmental organization that advocates for quality health services for all Tanzanians. The organization works to ensure equitable and affordable quality health care services through social accountability monitoring of health systems at all government levels. For more information about Sikika please visit us at www.sikika.or.tz

Sikika is seeking to recruit a Head of Finance who will be reporting to the Executive Director, with the following responsibilities; For more details, click here to read more…

Title: Head of Finance

Work Station: Dar es Saalam

Reports to: Executive Director

If you are interested and satisfy the above requirements you are encouraged to send your application only by e-mail to: [email protected]

Application Deadline: November 10, 2014

Shiriki na fuatilia masuala ya Katiba via ukurasa Facebook


Taarifa rasmi ya Serikali kuhusu uvumi wa mgonjwa wa Ebola Kilimanjaro

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA MKOANI KILIMANJARO

Utangulizi

Mnamo tarehe 22 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu mwanaume ana umri wa miaka 37, na mkazi wa Dar es salaam (Kimara ) ambaye alikwenda Kilimanjaro tarehe 20 Oktoba 2014 katika kijiji cha Kirua kwa ajili ya kusalimia ndugu. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali ( 38.2 0c), maumivu ya Misuli, kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na maumivu ya koo na kupoteza hamu ya kula.

Mgonjwa huyu anatibiwa katika Kituo cha Afya Shirimatunda, Kilimanjaro kuanzia tarehe 22.10.2014 ambako yupo hapo hadi sasa. Mgonjwa huyu kikazi ni “Land Surveyor” na hufanya kazi zake nchini na nje ya nchi ikiwemo nchi ya Senegali. Mnamo siku za karibuni alikwenda nchini Senegali kwa kazi za mkataba na kurejea nchini mwanzoni wa Oktoba 2014. Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na

Powering Africa - Tanzania's 2014-2025 energy reform roadmap to success

Web1_0.png

Tanzania’s 2014-2025 energy reform roadmap to success

The Ministry of Energy and Minerals has published an Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap for 2014 to 2025

DAR ES SALAAM, Tanzania, October 27, 2014/African Press Organization (APO)/ -- In its recent Investment Policy Review the OECD cited energy in Tanzania as a “critical bottleneck” and that the problem of reliable energy was the top barrier to doing business in Tanzania. This view was echoed during the Tanzania panel at the Africa Energy Forum in Istanbul in June at which TANESCO and EWURA specifically addressed this point. (www.energynet.co.uk/fr/event/powering-africa-tanzania)

It’s clear that project developers are keen to participate and that a multitude of funds are available to

Maelezo ya Waziri kuhusu huduma dhoofu hospitalini na deni la Serikali kwa MSD

Kuna taarifa katika vyombo vya habari iliyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA, kwamba serikali haijalipa kiasi cha shilingi bilioni 90 kwa bohari kuu ya dawa na kusababishia ukosefu dawa katika baadhi ya hospitali.

Ni kweli bohari kuu ya dawa imepungukiwa fedha za kununulia dawa, lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma kabisa kama inavyoelezwa. Kiasi cha pesa kinachotajwa si kigeni na serikali imekua ikitoa kiasi cha fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari ya dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza dawa.

Katika kukabiliana na hali hii hospitali zote kupitia waganga wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa kupeleka asilimia 50 ya mapato yanayotokana na uchangiaji kwenda bohari kuu ya dawa.

Taarifa kwa vyombo habari kuhusu ukosefu wa dawa na vifaa tiba

TAMKO LA SIKIKA KUHUSU UKOSEFU WA DAWA NA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI, VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI ZA UMMA NCHINI.


Sikika imesikitishwa na taarifa za hivi karibuni zinazoeleza kuwa na uhaba wa dawa na vifaa tiba muhimu katika vituo vya kutolea huduma vya umma nchini. Upungufu huu unasemekana kuathiri zaidi wananchi wasio na bima za afya.

Matatizo yanayosababishwa na uhaba wa dawa ni makubwa, kwani sio tu yanatishia uhakika wa huduma kwa mgonjwa anapokuwa katika kituo cha huduma za afya lakini pia yanapunguza ari ya kufanya kazi kwa watoa huduma. Aidha, matatizo haya pia yanaathiri ustawi wa jamii na mfumo wa huduma za afya nchini. Hali hii imeathiri wananchi wengi hasa wale wasio katika mfumo wa bima za afya na wale wenye bima zenye wigo mdogo.

Mfanyabiahara ajiua kwa kujifyatulia risasi

Timoth Mroki
Timoth Mroki
Na Mroki Mroki

MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo la Shams, jijini hapa.

Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari jingine katika eneo la Mbauda wakati akitokea katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.

Mmiliki wa KEAR Computer Training akamatwa kwa kuwatapeli Wanafunzi

MAKACHERO wa Jeshi la Polisi Nchini, wamemtia mbaroni mmiliki wa Kampuni ya KEAR Computer Training, Uttu Kingwande, kwa tuhuma za utapeli.

Kingwande anadaiwa kuwatapeli wanafunzi lukuki waliokuwa wakipata mafunzo ya kompyuta katika kituo chake alichokuwa amekifungua katika Shule ya Sekondari ya Mbeya.

Inadaiwa kuwa kituo hicho hakikuwa kimesajiliwa na hivyo alikuwa akijipatia pesa kiujacha ujanja.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, ambapo taarifa za kiuchunguzi

Siku umechelewa shule halafu "unamtaimu" Mwalimu wa zamu getini... we!

THE pupils (above) at Mgulani Primary School in Temeke, Dar es Salaam, peep from the entrance to the school as they either wait for the opportune moment to get inside after their mid-day recess or looking at another interesting spectacle. (Photo by Mohamed Mambo/DAILY NEWS)

Dawa zitapatikana vipi mahospitalini wakati MSD inaidai Serikali bilioni 90?

UHABA mkubwa wa dawa na vifaa tiba umezikumba hospitali nyingi nchini, zikiwemo za Muhimbili na Ocean Road, kutokana na serikali kudaiwa zaidi ya sh. bilioni 90 na Bohari Kuu ya Dawa, (MSD).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia masuala ya afya nchini la SIKIKA, Irenei Kiria, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hali hiyo inahatarisha maisha ya wananchi kwa kukosa matibabu.

Irene alisema kutokana na madeni hayo, MSD imesimamisha usambazaji wa dawa katika hospitali za serikali, zikiwemo za rufani na za wilaya, hasa za Mpwapwa na Kiteto, ambazo zinadaiwa mamilioni ya shilingi.

Eti huyu ni mwekezaji ama kuna utafiti unaendelea?

Nimepokea ujumbe na maelezo kupitia anwani pepe ambao nimeupachika hapo chini bila kubadili hat aiota moja.

Ujumbe huo umenisababisha niulize swali lililo kichwa cha habari hapo juu. Mtoa mada amegusia upande mmoja, nami nimegusia upande mwingine kuwa huenda huyu akawa anachagiza jambo kwa ajili ya kupata mwitikio wa mawazo na hisia tofauti za watu, utakaosaidia utafiti wake.

Inawezekana nawe una mtizamo wa tofauti.WAWEKEZAJI WA KIGENI WATUPIWE JICHO NA SHUGHULI ZAO
Je ! Huu ndio uwekezaji wenyewe ? Idara ya Uhamiaji mpo wapi ?
ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki ! 

Baadhi ya wawekezaji wa kigeni au pengine watumishi raia wa kigeni wamekuwa
wakivunja sheria za nchi kwa kujiingiza au kufanya shughuli zisizo katika miktaba yao
 ya kazi,au nje ya vibali vyao vya kufanyakazi hapa nchini Tanzania,lakini uvunjwaji wa sheria za nchi unaofanywa na wageni hawa unasaidiwa na sisi wenyewe kwa kuzingatia
zile mila zetu na misemo ya ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki.Matokeo yake tumekuwa na wachoma mahindi mtaani kutoka china,wabeba zege pia,
Kumradhi pengine makahaba au changudoa kwenye madangulo ya siri.
tunaweza kuwa na wakaanga samaki, walinzi "Kolokoloni" kutoka Thailand na Bangladesh,
inawekana kabisa tunao hapa nchini wapishi na tour guider kutoka nchi za ulaya !
Kwa mtindo na utamaduni wetu huu wa ah! wache "WAGENI WA MUNGU " wajitafutie ridhiki   tutajikuta tunao akina mama ntilie wakigeni.
Tunajiuliza wale wawekezaji wanajiusha na biashara za mitumba au maduka ya nguo kariakoo hivi vibali aliwapa nani? yaani muuza mtumba na duka la sukari atoke china,Yemen,Bangladesh ulaya ! hii kweli inaingia akilini kwa watanzania?
Sasa wawekezaji hawa kigeni wanafanya shughuli hizi mcha wa jua kali tena kweupe
Mkondo wa sheria ya nchi unavunjwa walinzi wa sheria wako wapi?
Wizara zinazohusika amlioni hili au ndio ah! TUWAACHE WAGENI WA MUNGU wajitafutie ridhiki ?  Watanzania ukarimu ni jadi yetu ! misemo hii haifanani kabisa
na ukiwikaji wa sheria za uhamiaji na ajira za nchi, kwani katu kwame uruma na
haki havikai pamoja.

Ushauri wa Amani kwa Lady Jaydee

Lady Jaydee (picha: Nairobi Wire)

Siku chache zilizopita mwanamziki maarufu wa Tanzania Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jaydee aliweka ujumbe kwenye mtandao wa facebook kwamba hayuko kwenye kipindi ambacho anaweza kutunga nyimbo. Ujumbe huo ulisomeka kama ifuatavyo;
Hiki ni kipindi ambacho siwezi kutunga/kuandika nyimbo, sina hisia zozote na nikilazimisha hazitakuwa nzuri.

Huwa nakaa hata miaka 3 au 5 pengine mwezi mmoja au miwili au 6 , yaani huwa haitabiriki, pale inapotokea tu ndio huwa. 

Natumaini jibu hili ni muafaka na litawaridhisha walio uliza, Poleni kwa kusubiri, i wish ningeweza
Niliona linaweza kuwa tukio la kawaida kwake na hivyo sikufikiri sana kuhusu hilo mpaka nilipokutana na rafiki yangu siku chache baadae. Rafiki yangu huyu ni mwandishi na nilitaka kujua anaendeleaje kwenye uandishi, nae akanijibu hayupo kwenye wakati mzuri wa kuandika, yaani hajisikii kuandika na hata akijisukuma haoni kama anaandika kitu kizuri. Hapa niliona kuna tatizo na hivyo kuona umuhimu wa kutoa ushauri kwa watu hawa na kwako pia kama unakutana na hali kama hizi kwenye kazi zako.

Tatizo analopitia Jaydee, na huyo rafiki yangu, huenda na wewe pia linaitwa writer’s block. Yaani

Nakala ya makubaliano ya vyama vinavyounda UKAWA

Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CUF uliohudhuriwa na wafuasi wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Kutoka kushoto ni James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI, Prof Ibrahim Li[pumba wa chama cha Wananchi CUF, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Dk. Emmanuel Makaidi wa NLD wakionesha hati yao ya makubaliano waliyoisaini jana katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI, Prof Ibrahim Li[pumba wa chama cha Wananchi CUF, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Dk. Emmanuel Makaidi wa NLD wakionesha hati yao ya makubaliano waliyoisaini jana katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam

Pichani ni viongozi wa juu wa vyama vinne vya siasa nchini Tanzania vilivyoingia makubaliano ya ushirikiano wa shughuli mbalimbali za siasa Oktoba 26, 2014.

Miongoni mwa mambo hayo ni kusimamisha wagombea wa pamoja katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani, Wawakilishi na Rais katika uchaguzi ujao.


“Ushindi wa CCM uchaguzi ujao hauepukiki” asema Dk Shein mkutanoni Kibandamaiti

Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein akionesha Katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la Katiba kwa wananchi na wanachama wa CCM zanzibar katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja leo jioni.

Umati mkubwa wa wananchi waliofurika katikauwanja wa Demokrasia kibandamaiti mjini
unguja wakiwa katika mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Makamo Mwenyekitiwa
CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali mohamed
Shein.
(picha: Ramadhan Othman, Ikulu.)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar wasikubali kugawiwa kutokana na mchakato wa Katiba unaoendelea

Akihutubia maelfu ya wana CCM na wananchi wa Zanzibar katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti mjini Unguja, Dk. Shein alisema wananchi wote waliridhia na kushiriki mchakato huo hivyo hakuna sababu ya kugawanyika baada ya Bunge la Katiba kupendekeza Katiba Mpya.

Wito wa kuhudhuria mkutano wa 'kuzika' CCM

Ujumbe niliopokea kupitia anwani pepe unasema:

Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) unawatangazia Wananchi wote wazalendo wapenda nchi yao kuhudhuria katika mkutano mkubwa wa aina yake wenye lengo la kuizika CCM siku ya Jumapili katika viwanja vya Jangwani kuanzia saa 8:00 mchana.

Njoo ushuhudie tukio muhimu la kihistoria ambapo Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vinavyounda UKAWA watakavyosaini makubaliano ya pamoja ya ushirikiano katika chaguzi zote zijazo kuelekea 2015. Njoo ujionee namna madalali wa nchi hii watakavyoumbuliwa na katiba yao feki kusasambuliwa!

Mkutano utaoneshwa moja kwa moja 'live' na kituo cha ITV.

Mpe taarifa hii na mwenzako.

Kuhusu majibizano ya risasi kati ya Mbunge na mwanaye

Polisi wakiwasili eneo la tukio katika ofisi za Faraja Trust Fund zinazomilikiwa na Mhe. Lucy Nkya ambako imeripotiwa kuwa milio ya risasi ilisikika jana asubuhi. (picha: Dunstan Shekidele)

Utata umeibuka, kufuatia tukio la mlio wa risasi linalodaiwa ni la majibizano kati ya Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Dk. Lucy Nkya na mtoto wake Jonas Nkya.

Kauli za kugongana zilizotolewa na pande mbili hizo, zimezua utata baada ya mtoto kusema bastola yake ilijifyatua, huku Mbunge akisema kishindo kilichosikika ni cha mlipuko wa mtungi wa jokofu.

Dk. Nkya ambaye aliwahi kuwa Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, aliiambia NIPASHE Jumapili kwa njia ya simu jana kuwa, wakati tukio hilo linatokea alikuwa nyumbani.

Alisema alipigiwa simu na Afisa Utawala wake, akimweleza kuhusu kishindo cha mlipuko

Tanzania to regulate mobile money services

Tanzania will establish a law to oversee mobile money and Internet banking transactions now being actively entered into by more than half of the country’s mobile phone subscribers. The number of active users of the services in Tanzania is set to increase from the current 55 per cent to 60 per cent of the population in 2015.

Kenya and Rwanda have recently enacted similar legislation to protect consumers against mobile money fraud, while Uganda is in the process of doing so.

Ministry of Finance sources said the National Payment Act will be tabled in parliament early next year for review to align it with new modes of settlement such as money transfers and mobile banking, which an estimated six million subscribers use to save.

CHADEMA yakamata askari 'wapelelezi' katika mkutano wake

Kadi ya mmoja wa waliokamatwa

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewabaini na kuwakamata polisi wawili  wa kituo cha polisi wilaya ya Geita, Ernest Silayo na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja waliokuwa kwenye mkutano wao wilayani Geita wakiwa wamevaa sare za chama hicho huku wakiwa na kadi za uanachama wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake CHADEMA, (BAWACHA), Kunti Yusuph alisema, askari hao wa kike na wa kiume walikamatwa na walinzi wa chama hicho (Red Brigedi) ambapo walinyang’anya simu zao za za kiganjani, vinasa sauti na kadi ya CHADEMA.

Yusuph alisema kuwa tukio hilo limeuthibitishia umma namna polisi wanavyotumika kufanya vurugu kwenye mikutano yao ikiwemo tukio la utupaji wa mabomu kwenye mkutano ya chama hicho iliyotokea jijini Arusha Juni mwaka jana na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa vibaya.

Taarifa ya NHIF kuhusu kupeleka huduma za Madaktari Mabingwa mikoani1.0 UTANGULIZI

Pamoja na kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama na wadau kwa maana ya kufungua ofisi mikoani, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za Madaktari Bingwa mikoani.

Mpango huu unawahusisha Madaktari Bingwa ambao ki-ukweli ni wachache kutoka katika hospitali zifuatazo:-

 • Hospitali ya Taifa ya Muhimbili;
 • Taasisi ya Mifupa MOI;
 • Hospitali ya Bugando.
Madaktari Bingwa hao wanafanya kazi katika hospitali za mikoa kwa kushirikiana na madaktari waliopo huko mikoani. Madaktari hao ni mabingwa wa:-

Simba haiachani na sare msimu huu?

Kikosi cha Tanzania Prison kilichohceza na Simba leo jioni.

Kikosi cha Simba kilichochuana vikali na timu ya Tanzania Prison uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jana jioni.
(picha: Rashid Mkwinda)

Timu ya kandanda ya Simba ya Jijini Dar es Salaam jana iliondoka kwa sare ya magoli na maafande wa Magereza Tanzania Prison.

Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kujipatia bao katika dakika ya pili ya mchezo baada ya Emmanuel Okwi kutikisa wavu kwa njia ya adhabu ndogo.Adhabu hiyo ilitokana na mchezaji wa Prison Lugano Mwangama kumfanyia madhambi mlinzi wa Simba Ramadhani Singano.

Yanga warushiana makonde na Stand United kisa uchafu

Wachezaji Yanga wakikabiliana na mashabiki wa Stand United,katikati ya nguzo mbili yupo kocha wa Yanga Maximo. (picha: Kadama Malunde-Malunde1 blog)

Jana jioni wakati wa mchezo wa soka wa ligi Vodacom 2014/2015 kati ya timu ya Yanga na Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga ilitokea vururu kipindi cha mapumziko baada ya wachezaji wa Yanga wakiongozwa na kocha wao Marxio Maximo kupanda Jukwaa Kuu wakidai kuwa vyumba vya kubadilishia nguo vilivyoko uwanjani ni vichafu na hivyo walihitaji kutumia vyumba vilivyoko Jukwaa Kuu, kitendo ambacho kilipingwa na mashabikiwa Stand United.

Hapo ndipo vurugu zikaanza,wachezaji wa Yanga wakirushiana makonde na mashabiki wa Stand United. Hali hiyo ilisababisha Kocha wa Yanga Maximo kuingilia kati huku naye akinusurika kuchapwa makonde na mashabiki, na kulazimika kukabiliana nao huku wakimrushia chupa za maji.Mapendekezo ya Mwalimu wa Madereva kuhusu ajali za barabaraniMimi ni dereva na pia ni Mwalimu wa madereva “Drivers Instructor ”. Napenda kutoa maoni yangu na mapendekezo kuhusu ajali barabarani kama ifuatavyo:-

Nimefanya uchunguzi kwa muda wa miaka mitatu kwa madereva tofauti, wa malori makubwa , mabasi makubwa na madogo (daladala), tax pick up za kukodi, malaori ya mchanga, madereva wa Serikali, madereva wa Waheshimiwa Wabunge na bajaji. Kwa makundi yote haya ukiondoa Madereva wa Serikali kinachowafanya madereva hawa kuendesha magari bila kujijali wao wenyewe, abiria na watembea kwa miguu kwa kuendesha mwendo kasi bila ya kujiwekea tahadhari ya chochote barabarani.

Madereva karibu asilimia 92 hawana ajira ya kudumu wala mikataba inayoainisha malipo na maslahi yao, hivyo malipo yao ni kutokana na safari wanaozifanya na idadi ya tripu, hali hiyo inawalazimu madereva kama wa bus wakimbie ili ajitahidi azipite gari zilizomtangulia bila kujali madhara yanayoweza kumkuta endapo atapata ajali. Unaweza kukuta madereva wengine mfukoni hawana hata shilingi elfu kumi (10,000/=) ambayo inaweza kuwa ya thadhari ya kumuona dokta kwa hatua ya huduma ya kwanza endapo atapata ajali. Hali hii inasikitisha sana kulingana na thamani ya gari analoliendesha , uhakika wa

Kilichotokea katika uchaguzi wa Zanzibar 2010

Baada ya gazeti moja lilichapisha habari kuhusu nafasi ya *Mzee Nassoro Moyo kwenye uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2010, Josephat Charo wa DW alizungumza na mwanasiasa huyo, hasa kupata ufafanuzi wa madai kuwa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa tayari kwa lolote lakini siyo kutangazwa mgombea wa kilichokuwa chama cha upinzani, CUF, kama mshindi wa urais kwenye uchaguzi huo.

Katika mahojiano haya, Mzee Moyo kwanza anaelezea vipi aliweza kumshawishi mgombea wa CUF, Seif Sharif Hamad, akubali ushindi wa mpinzani wake mgombea wa CCM na rais wa sasa wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza pleya ifuatayo:*Mzee Nassoro Moyo alikuwa mjumbe kwenye Baraza la kwanza la Mapinduzi la Zanzibar chini ya Marehemu Abeid Karume, Waziri wa Sheria wa Muungano, Waziri wa Elimu wa Zanzibar na sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano.

Mwandishi wa habari wa Mtanzania, Elias Msuya akifanya mahojiano ya Mzee Hassan Nassor Moyo nyumbani kwake Fuoni.
Mwandishi wa habari wa Mtanzania, Elias Msuya akifanya mahojiano ya Muasisi wa Muungano na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mzee Hassan Nassor Moyo nyumbani kwake Fuoni.

Hivi karibuni Bunge Maalum la Katiba limekabidhi rasimu ya Katiba inayopendekezwa kwa rais Jakaya Kikwete na rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Hata hivyo rasimu hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti huku makada wa CCM wakiiunga mkono na wapinzani wakiipinga.

Kwa upande wa Zanzibar, siyo wapinzani tu wanaoipinga, bali hata wana CCM wanaojitaja kuwa na uchungu wa visiwa hivyo.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni mjini Zanzibar, mwanasiasa mkongwe aliyeshiriki Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 Hassan Nassor Moyo anasema Katiba hiyo inapingana na Mapinduzi ya Zanzibar hivyo haikubaliki.

Swali: Katiba inayopendekezwa imepiotishwa na sasa inapigiwa debe kuelekea kwenye kura ya maoni. Nini nafasi ya Zanzibar katika Katiba hiyo?

Kauli ya Shy-Rose Bhanji kuhusu taarifa za kutia aibu

Tuhuma:

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EAC), Shyrose Bhanji kazua balaa kwenye kikao cha Bunge hilo mjini Kigali jana na leo! Walioandika trh 8 kwenda Brussels kwenye Bunge la EU members wote wa Tume yao na Wenyeviti wa Kamati. Wakiwa safarini kwenda ndani ya ndege sijuwi kukosa ile lishe aliyoizoea? Akawa anakunywa kama kichaa! Crews wakamzuia kuwa kwakuwa ndege ni ya mchana asinywe kupitiliza. Akaanza kutukana crews matusi yote unayoyajua!

Akawaambia hawajuwi kama yeye ni mbunge wa EAC? Akaanza kufanya fujo ndani ya ndege, akachukua chupa akapasua! Hapa security ndani ya ndege wakamkamata na kumtia pingu! Maneno yakawa yanamtoka ovyo. Wenzie walipojaribu kumtuliza wa kutoka Rwanda na mwingine Uganda (names withheld) akawageukia, tukana hadi marais wao hya kutosha! Hapo walikuwa juu ya anga ya Cairo.

Ebola-free Dallas Nurse Nina Pham meets Pres. Obama


The Ebola-free nurse Nina Pham visited U.S. President Obama after being cleared of deadly virus.

The 26-year-old was released from the hospital on Friday, eight days after she arrived at the National Institutes of Health in Bethesda, Md., and paid a visit to President Barack Obama in the Oval Office before her trip back to Texas. 

Pham contracted the disease while caring for America's 'Patient Zero', Thomas Eric Duncan, who died October 8, 2014.Taarifa: China, Tanzania zasaini mkataba wa mabilioni ya uwekezaji

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China leo, Alhamisi, Oktoba 23, 2014, zimetiliana saini Hati za Makubaliano (Memorandum of Undestanding) ambako taasisi za China zitawekeza mabilioni ya dola za Marekani katika uchumi wa Tanzania.

Shughuli hiyo ya utiaji saini imekuwa sehemu ya Mkutano wa Tatu wa Uwekezaji Kati ya Tanzania na China uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Nyumba ya Kufikia Wageni wa Serikali ya Diaoyutai mjini Beijing, China.

Aidha, utiaji saini huo ambao utaziwezesha taasisi kadhaa za Tanzania kunufaika na mitaji na uwekezaji kutoka China ulikuwa sehemu ya ziara rasmi ya Kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping. Rais Kikwete ameshuhudia shughuli hiyo ya utiaji saini.