Askari wa JKT akutwa mferejini akiwa kalewa chakariKatika hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada ya kukutwa amelewa chakari na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa

Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.

Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.

Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu .

Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza

"Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare, sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja.

Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana maombi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa.

Ushauri wetu kwa askari wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ama chonde chonde ulevi noma.

Hongera Mwl. Ishengoma kwa kuhitimu masomo ya shahada ya Udaktari


Dk Nelson Ishengoma

Dk Nelson Ishengoma ametunukiwa shahada yake ya udaktari katika Mahafali ya Tano ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Chimwaga vilivyopo Chuoni hapo.

Hongera sana Mwalimu wangu na sasa mwanzo wa jina linaanza na Dk. Siyo kazi rahisi lakini Mungu ameweza kukusimamia na kukuongoza. Nakuombea kwa Mungu ufanikiwe zaidi na zaidi. 

Kutoka kwa mwanafunzi wako,  Josephat Lukaza

[video] Dakika 54 za mazungumzo na Rais Kikwete aliporudi kutoka kwenye matibabu

Polisi aliyemwua Michael Brown ajiuzulu

Michael Brown (kushoto); Darren Wilson (kulia)

Darren Wilson (28), askari polisi wa kituo cha Ferguson huko St. Louis nchini Marekani ambaye alimpiga risasi iliyomwua kijana wa asili ya Afrika, Michael Brown (18) takriban miezi minne iliyopita, ameacha kazi.

Uamuzi huo wa Wilson ulitanganzwa jana Jumamosi na mmoja wa mawakili wake, Neil Bruntrager ambaye amesema hatua hiyo inaanza mara moja. Kabla ya hapo, Wilson alikuwa katika likizo ya kikazi tangu Agosti 9.

"I, Darren Wilson, hereby resign my commission as a police officer with the City of Ferguson effective immediately. I have been told that my continued employment may put the residents and police officers of the City of Ferguson at risk, which is a circumstance that I cannot allow. For obvious reasons, I wanted to wait until the grand jury made their decision before I officially made my decision to resign. It was my hope to continue in police work, but the safety of other police officers and the community are of paramount importance to me. It is my hope that my resignation will allow the community to heal. I would like to thank all of my supporters and fellow officers throughout this process."

Hivi karibuni uamuzi uliotolewa baada ya miezi mitatu ya uchunguzi wa vielelezo vya sababu ya kifo cha Brown na kumwona Wilson hana mashitaka ya kujibu, uliamsha ghadhabu miongoni mwa wananchi na kuzua maandamano katika majimbo tofauti nchini Marekani ya kupinga uamuzi huo.

Mahakama yamfutia mashitaka ya mauaji Rais Mubarak

Mahakama Kuu nchini Misri jana Jumamosi ilimfutia mashitaka ya mauaji rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak, mashitaka ambayo yalikuwa yanamkabili awali yaa vifo vya waandamanaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya mwaka 2011 baada ya kujaribu kutaka kusalia tena madarakani huku akiwa ameongoza nchi hiyo kwa miaka 30.

Uamuzi huo umechochea hasira ya wapinzani wa Mubarak ambapo karibu watu 1,000 walikutana katikati mwa jiji la Cairo kupinga serikali.

Wizara ya afya imesema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki dunia wakati Polisi wa kutuliza ghasia nchini Misri wakijaribu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga uamuzi ya mahakama nchini humo.

Aidha mahakama imemwondolea rais huyo wa zamani mashataka ya rushwa, lakini ataendelea kubaki kizuizini kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka mitatu katika kesi nyingine ya rushwa.

Maaafisa wengine saba waliohudumu kwenye serikali ya Mubarak akiwemo waziri wa zamani wa mambo ya ndani anayeogopwa Habib al Adly pia wamefutiwa mashitaka ya mauaji ya watu 800 waliouawa katika mapinduzi hayo.

via RFI Swahili

WB pledges $1.2 B to improve EAC infrastructure and competitiveness

East African Community heads of state attend retreat | Coastweek
 Kenyan Deputy President William Ruto [second right], Vice President of Tanzania Mohamed Bilal [second left], Rwandan Prime Minister Anastase Murekezi [first right] and Burundian first Vice President Prosper Bazombaza display copies of the communique they signed during the 3rd East African Community (EAC) heads of state retreat on infrastructure development and financing in Nairobi. The five Member States of the EAC on Saturday endorsed a ten-year infrastructure development plan that will require 100 billion U.S. dollars to implement. XINHUA PHOTO - FRED MUTUNE
The World Bank said today that it will provide $1.2 billion to support infrastructure development and improve the competitiveness of the East African Community (EAC) states.
In addition, through IFC and MIGA, the World Bank Group will provide additional resources for regional infrastructure through market-driven private sector financing and guarantees.

The financing will contribute to the EAC states’ planned investments in the next three to seven years. This support is additional to large ongoing individual country programs.

“We are partnering with the EAC governments, other development partners and the private sector to invest in regional infrastructure and to help deepen policy integration and reduce barriers to trade in the EAC,” said Philippe Dongier, World Bank Country Director for Burundi, Tanzania and Uganda, during the EAC Heads of State retreat in Nairobi. “We are preparing investments to revive the region’s inland waterways on Lakes Victoria and Tanganyika, and to enhance the capacity and efficiency of the two main EAC ports on the Indian ocean: Dar-es-Salaam in Tanzania, and Mombasa in Kenya. We will also invest in specific transport links to better connect landlocked countries (Burundi, Rwanda, Uganda and South Sudan) to the Northern and Central corridors, this way improving these countries’ access to the ports of Mombasa and Dar-es-Salaam.”

The retreat on Infrastructure Development and Finance focused on policies and reforms necessary to strengthen regional integration through enhanced efficiency of infrastructure investment and financing.

Working with private sector partners, IFC is already investing more than $1.0 billion annually in Sub-Saharan African infrastructure to spur economic growth and improve living standards,” said Oumar Seydi, IFC Director for Eastern and Southern Africa. “IFC intends to do more to support ports, power, rail, transport, and other key infrastructure projects in the East African Community in the years ahead.

The World Bank Group’s investments and support to reforms anticipate the boom of extractives in the region and will facilitate easier movement of people, goods and capital. The Bank Group will continue to support the EAC efforts in removing barriers to agriculture trade and selected services. This is expected to deliver real benefits to farmers, traders, youth and women in the region.

The retreat was officially opened by Kenya’s Deputy President William Ruto. Participants include the EAC Heads of State or their representatives, ministers, chief executives of development banks and regional economic communities, high commissioners, ambassadors and private sector leaders.

World Bank Group portfolio in the EAC

The World Bank is already supporting the EAC’s regional integration agenda with investments of $2.3 million in 17 regional projects in priority sectors. These include roads, railways, energy, information and communications technologies, finance, trade, health, agriculture, livestock development and health.

IFC presently has a portfolio of over $1 billion in EAC countries. Project support sectors include agribusiness, finance, infrastructure, manufacturing, services, and telecommunications. IFC’s infrastructure portfolio in East Africa includes investments in Kenya Power and Lighting, Thika Power and Gulf Power in Kenya; and the Bujagali Hydropower Project and Umeme in Uganda.

MIGA’s portfolio in the EAC includes 11 projects, amounting to a gross exposure of $550 million. MIGA’s support for the energy sector is particularly noteworthy and includes guarantees for the Gulf, Thika, Triumph, and OrPower 4 independent power producers in Kenya; KivuWatt Ltd. in Rwanda; and Bujagali and Umeme in Uganda.

The Bank Group is also using its knowledge resources and experience to assist the EAC member countries in analytical work and policy reforms that are critical to unleashing the region’s growth potential and increasing its global competitiveness in trade and investment.

Mkurugenzi wa Stanbic asimamishwa kazi na kurejeshwa nchini kwao

Vikao vya Bunge ambavyo vilijikita kikubwa katika kujadili kashfa ya fedha za akaunti ya BoT – Tegeta escrow vilikamilika jana kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa hotuba ya kuhitimisha vikao vya Bunge hilo.

Pinda ni mmoja wa viongozi wa Serikali waliotajwa katika kashfa hiyo na kushutumiwa vikali.

Michango ya Wabunge imetoa taswira ya kugawanyika katika makundi mawili makubwa ambapo kundi la moja linashinikiza kuwa wale wote ambao wametajwa katika ripoti wanapaswa kuwajibika ama kuwajibishwa huku kundi jingine likitetea kuwa waliotajwa katika ripoti ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) hawastahili kuwajibika wala kuwajibishwa kwa kuwa hawakutajwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Kundi hilo linaituhumu PAC kuwa imefanya uchambuzi wa baadhi ya mambo yasiyokuwemo kwenye ripoti ya CAG.

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akitoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ya PAC, alisema kwamba watu walionufaika na fedha za kampuni ya kuzalisha na kusambaza umeme ya IPTL na wale waliotoa na kupokea, hawakukatwa kodi na hivyo Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza taratibu ya kukusanya kodi kwa waliokwepa, huku akitoa mpaka tarehe 31 ya mwezi Desemba, kwamba wote walionufaika na fedha za IPTL wawe wameanza kulipa kodi.

Bunge liliarifiwa hiyo juzi kuwa tayari Benki ya Stanbic imechukua hatua ya kumsimamisha Mkurugenzi Mtendaji wake nchini Tanzania na kumrejesha kwao nchini Uganda.

Benki hizo zilizohusika katika kashfa hii, zimetakiwa kutoa taarifa leo Bungeni ya hatua ambazo zimechukua dhidi ya watu ambao walifanikisha ama kunufaika na fedha za IPTL.

Baada ya Wabunge kuwasilisha michango yao Mwenyekiti wa PAC alijibu baadhi ya hoja za Wabunge zilizotokana na mapendekezo ya Kamati hiyo (maazimio hayo unaweza kuyasoma kwa kubofya) na Waziri Mkuu alichukua nafasi ya kuchanganua mjadala mzima tangu ulivyoanza hadi kufikia na kuhitimisha kwa kuliahirisha Bunge (hotuba yake unaweza kuisoma kwa kubofya hapa) hadi Januari 27 mwakani.

Pole Ansbert Ngurumo kwa kuondokewa na malaika wako, Asiimwe!

Ni wakati mgumu sana katika maisha yangu. Si jambo jepesi kufiwa na mtoto. Nafarijika kwa maneno ya wote walionitumia salaam za rambirambi. Hapa chini, najaribu tu kufanya jambo gumu na zito - kuwashirikisha, kwa njia ya tanzia, WASIFU wa binti yangu Asiimwe aliyefariki ghafla mwanzoni mwa mwezi huu:

Asiimwe Wilhelmina alizaliwa tarehe 12/10/2002 katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam. Ni mtoto wa tatu, na binti wa pili, katika familia ya Bwana na Bibi Ngurumo.

Babu yake mzaa baba (aliyefariki dunia Mei 15 mwaka huu), Ta Theogenes Ngaiza, ndiye alimpatia jina Asiimwe, maana yake Mungu Ashukuriwe. Katika ubatizo, bibi yake mzaa mama akampatia jina Wilhelmina, lake mwenyewe. Akawa somo wake.

Hadi mwaka jana 2013, Asiimwe alikuwa anasomea katika Shule ya St. Aloysius Girls ya Dar es Salaam. Mwaka huu 2014 mwanzoni, alihamishiwa katika Shule ya St. Joseph Model English Medium, Rutabo, katika darasa la nne.

Jumatatu ya tarehe 10/11/2014 alipaswa kufanya mtihani wa taifa wa Darasa la Nne. Kwa miezi kadhaa kabla na baada ya kuhamia Rutabo, amekuwa katika mafundisho ya Komunyo ya Kwanza, ambayo alitarajia kupokea tarehe 15/11/2014.

Tarehe 06/11/2014 asubuhi, akiwa katika ibada ya misa kwenye Kanisa la Parokia ya Rutabo, alionekana kupepesuka. Kabla hajaanguka chini, Sista Mlezi alimdaka na kumtoa nje, akamkabidhi kwa walimu wamhudumie.

Walimu waliamua kumpeleka Hospitali ya Ndolage, akapimwa na kugundulika ana Malaria kali na upungufu wa sukari mwilini. Walimlaza na kutoa taarifa kwangu, baba yake.

Kabla ya kuwasili hospitalini, kwa kuwa nilikuwa mbali kidogo, Muleba Mjini, nilipiga simu nyumbani, nikashauri mgonjwa apelekewe chai, kwani nilikuwa nimeelezwa na walezi wake kwamba Asiimwe alipaswa kuwekewa drip ya dawa, lakini mishipa ya damu ilikuwa haipatikani.

Wauguzi walihisi hali hiyo ilitokana na kushuka kwa sukari, na ilihitajika sukari ya nyongeza mwilini ama kwa kunywa chai au glucose au kitu chochote chenye sukari.

Shangazi yake mkubwa aitwaye Francisca, aliandaa na kupeleka chai kwa mgonjwa. Kadiri ya simulizi la shangazi yake, alipowasili alikuta mgonjwa anazungumza, wakasalimiana huku, kadiri ya maelezo ya wauguzi, ameshawekewa drip ya quinine iliyochanganywa na glucose.

Nilipowasili hospitalini baadaye, nilikuta Asiimwe anamalizia drip ya pili ya quinine, na hakunitambua, kwani alionekana kuwa katika usingizi na uchovu mkali. Sote tuliokuwapo tulihisi ni uchovu uliotokana na ukali wa dawa.

Mnamo saa nane (8) usiku wa kuamkia tarehe 07/11/2014, Asiimwe alikata roho akiwa na drip ya tatu ambayo hakuweza kuimalizia.

Taarifa ya kifo chake, kwa mujibu wa daktari, inasema Asiimwe alifariki dunia kutokana na upungufu mkubwa wa sukari mwilini, ujulikanao kama hypoglycemia.

Sista mmoja aliyeishi na Asiimwe kwa karibu, na ambaye alikuwa mwalimu wake wa dini, alimweleza Asiimwe kama mtoto mwenye Sifa ya. Kimalaika. Alipenda sana ibada. Na hata alipotimiza miaka 12, mwezi uliopita, aliomba nimpatie zawadi. Alichagua anunuliwe Biblia Takatifu, ndogo.

Kwa maelezo ya Sista huyu, hiki kilikuwa kitendo kisicho cha kawaida kwa mtoto mdogo kuomba zawadi ya Biblia kutoka kwa mzazi katika siku yake ya kuzaliwa, kwani hata watu wazima wengi hawana, na hawasomi, Biblia; wala wasingechagua Biblia kama zawadi kwenye siku muhimu za maisha yao.

Asiimwe alibahatika kuwa mmoja wa watoto waliokwenda kuhiji Nyakijoga, Mugana, wiki chache zilizopita. Kwa maelezo ya Sista Mlezi, Asiimwe hakuwa kwenye orodha ya awali ya mahujaji kutoka shule hiyo.

Alipata fursa hiyo baada ya mwanafunzi mmoja kushindwa kwenda kwa sababu za kiafya. Sista akampendekeza Asiimwe ajaze nafasi hiyo.

Katika salaam za pole kwangu baba mzazi, Sista Mlezi alisema pamoja na kwamba alilia sana baada ya kupata taarifa za kifo cha Asiimwe, anaamini kwamba Mungu aliamua kumchukua mtoto huyu mapema ili aungane naye kabisa mbinguni, kabla ya muungano wa kiroho katika Ekaristi Takatifu aliyopaswa kupokea katikati ya mwezi huu.

Alisema, "Asiimwe alikuwa mtoto mwema sana mbele yetu na mbele ya Mungu. Mungu ameamua kumchukua mapema ili asichafuke. Amekuwa mwakilishi, na atakuwa mwombezi wa familia, mbele ya Mungu. Asiimwe alikuwa Malaika. Amewahi kabla ya Komunyo, ili aungane na Mungu kabisa."

Miongoni mwa watu walionipa pole na kuzungumza nami kuwa simu mara baada ya kupata taarifa za kifo cha Asiimwe, ni Mwenyekiti wa IPP, Dk. Reginald Mengi, ambaye alisema maneno haya ya faraja:

"Asiimwe alikuwa mtoto wako, lakini alikuwa mtoto wa Mungu zaidi. Mungu alikupa Zawadi hii ukae nayo kwa miaka 12 tu, halafu ameichukua. Usinung'unike, msikate tamaa wala msikufuru; bali kama yasemavyo maandiko, Mshukuruni Mungu kwa kila jambo."

Asiimwe alizaliwa, akabatizwa na akalelewa katika imani Katoliki; na amezikwa katika imani yake hiyo. Alikuwa mtoto mwenye upendo wa pekee kwa kila mtu aliyekutana naye.

Uso wake ulijaa tabasamu. Alikuwa na huruma ya wazi. Siku moja nilipomtembelea shuleni na kutoa pesa ya matumizi kwa ajili yake, aliniuliza kwa upendo na tabasamu usoni, "mbona hujamwachia Sista pesa yoyote? Mpe na yeye, ananitunza vizuri." Kwa ombi hili la Asiimwe, nilimpatia Sista kiasi kidogo cha pesa nilichokuwa nacho!

Alikuwa mchangamfu, mcheshi na mwenye utani kwa watoto wenzake na watu wazima. Mnamo Septemba 02, 2014, nilialikwa kwenye adhimisho la misa ya Shukrani ya Padri Denis Muchunguzi parokiani Rutabo.

Katika hafla iliyofanyika mbele ya Kanisa kwenye viwanja vya Shule ya akina Asiimwe, mtangazaji alinitaka nicheze ngoma ya Kihaya iliyokuwa inapigwa. Nilipoingia tu uwanjani na kuanza kucheza na Ndugu Diocles Rutabana, kama ilivyokuwa imetangazwa, nikistuka kuona Asiimwe akiwa mbele yangu, anacheza ngoma hiyo pamoja nami.

Ndiyo ilikuwa siku ya mwisho niliyomuona akiwa mzima! Kumbe alikuwa ananiaga. Aliniaga kwa tabasamu, kwa furaha!

Tulimlaza salama kwenye makao ya milele, katika makaburi ya familia ya babu zake, Kyamawa, Rwanda, Kamachumu, tarehe 09/11/2014.

Naandika haya kwa masikitiko na uchungu mkubwa sana. Napata kumbukumbu zinazoumiza moyo wangu. Siwezi kuendelea!

Kwa niaba ya familia, nawashukuru wote walioshiriki kumlea, kumfundisha na kumhudumia kwa njia na nyakati mbalimbali katika maisha yake mafupi ya miaka 12 na siku 24.

Nawashukuru pia kwa namna ya pekee wote waliotufariji kwa njia mbalimbali tangu tulipopatwa na msiba huu mzito.

Shukrani za pekee ziwaendee mapadri Faustine Mukyanuzi, Florence Rutaihwa na Johannes Rweyemamu, walioongoza ibada ya mazishi ya Asiimwe; Padri Evodius Mwijage aliyeadhimisha misa ya kuanua matanga, wote walioshirikiana nasi na wanaoendelea kutufariji katika kipindi hiki kigumu.

Katika Ibada ya Misa ya mazishi yake, Padri Mukyanuzi, Paroko wa Rutabo, alisema kwamba katika umri mdogo aliokuwa Asiimwe, ni dhahiri kwamba hakuwa na makosa makubwa mbele ya Mungu.

Akasema misa hiyo, pamoja na kumkumbuka marehemu, itumike kuombea wazazi na familia. Zilitolewa Misa 129 kwa nia hiyo.

Hata hivyo, kwa imani zetu, tunamwombea Asiimwe huko alikotangulia, Mungu amjalie pumziko jema na raha ya milele. Pengo lake haliwezi kuzibwa kamwe.

Tulimpenda sana, lakini Mungu amempenda zaidi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe!

Kwa heri, Malaika wangu, Asiimwe!

---
  • Wasifu wa Asiimwe umeandikwa na Ansbert Ngurumo na kuchapishwa hapa wavuti.com kutoka kwenye blogu yake.

Picha: Pinda, Mbowe, Lukuvi, Wassira, Mwandosya ...ndivyo siasa ilivyoWaziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene

Mawaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (kulia) na Stephen Wasira (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bugeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (kulia) akizungumza na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mjini Dodoma Novemba 29, 2014. 

Picha zote: Ofisi ya Waziri Mkuu

Maazimio ya Bunge kuhusu hoja ya PAC ya akaunti ya Tegeta escrow na IPTLMAAZIMIO YA BUNGE KUHUSU HOJA YA TAARIFA MAALUM YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA ‘ESCROW’ YA TEGETA PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL
_____________________________________


1. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi Maalum wa Malipo yaliyofanyika katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (‘CAG’) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (‘TAKUKURU’) imeonesha kwamba kwamba Harbinder Singh Sethi, James Rugemalira (VIP), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (‘TANESCO’) walihusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda kwa makampuni ya Pan African Power Solutions Ltd. (‘PAP’), na VIP Engineering & Marketing (‘VIP’);

KWA KUWA, kwa sababu ya kuhusika kwa watu hao na miamala iliyofanyika kwenye Akaunti ya Escrow imeliingizia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha za umma zinazotokana na kutokulipwa kwa kodi mbali mbali za Serikali na kushindwa kwa TANESCO kukokotoa upya kiwango cha malipo ya gharama za uwekezaji (‘capacity charges’) wa IPTL;

KWA KUWA, mabilioni ya fedha yaliyotolewa kwenye Akaunti ya Escrow yametumika kuwapa kile kinachoonekana kuwa ni rushwa baadhi ya viongozi na maafisa wa serikali kama vile Mawaziri, Majaji, Wabunge, Wenyeviti wa Kamati za Bunge, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi.

NA KWA KUWA, vitendo vilivyofanywa na watu hawa vinaashiria makosa mbali mbali ya jinai kama vile uzembe, wizi, ubadhirifu, kutakatisha fedha haramu, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na kupokea mali ya wizi;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na Taarifa Maalum ya Kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbali mbali unaoendelea;

2. KWA KUWA, vitendo vya kijinai wanavyhohusishwa navyo viongozi wa umma na maafisa wa ngazi za juu serikalini vinakiuka pia maadili ya viongozi wa umma na kuwanyima viongozi na maafisa hao uhalali wa kuendelea kushikilia nafasi za mamlaka katika uongozi wa umma;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wawajibishwe, kwa kuishauri mamlaka yao ya uteuzi kutengua uteuzi wao;

3. KWA KUWA, katika watu walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO;

NA KWA KUWA, Bunge na/au Kamati zake za Kudumu zina uwezo na mamlaka, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, ya kuwawajibisha viongozi hawa wa Kamati kwa kuwavua nyadhifa zao;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka, na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao Wenyeviti tajwa wa Kamati husika za Kudumu za Bunge;

4. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba katika watu waliotajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania;

KWA KUWA, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (‘Katiba’) imeweka utaratibu mahsusi wa kushughulikia nidhamu ya Majaji;

KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamtaka Rais kuunda Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Majaji;

NA KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamruhusu Rais kumsimamisha kazi Jaji au Majaji husika wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania;

5. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. ilishiriki kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwa njia haramu kutoka katika Akaunti ya Escrow na kupelekwa katika akaunti zilizofunguliwa na PAP katika benki hiyo;

KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba akaunti za PAP katika Stanbic Bank Tanzania Ltd. zimekwishafungwa baada ya fedha zote zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow kumalizika na Akaunti ya ya VIP katika Mkombozi Commercial Bank imebakiza kiasi fulani cha fedha;

NA KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba kuna uwezekano fedha zilizotolewa kutoka kwenye akaunti za PAP na VIP zilipelekwa katika benki nyingine;

NA KWA KUWA, vitendo vya Stanbic Bank (Tanzania) Ltd., na benki nyingine kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwenye Akaunti ya Escrow ni vitendo vya jinai kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi ziitaje Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. na benki nyingine yoyote itakayogundulika, kufuatia uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu (institutions of money laundering concern);

6. KWA KUWA, vitendo vya wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, hujuma ya uchumi na ufisadi vimeongezeka, kushamiri na kushirikisha viongozi wa kisiasa na maafisa wa serikali pamoja na wafanya biashara wakubwa;

KWA KUWA, kwa mujibu wa sheria iliyoiunda, TAKUKURU inashughulikia vitendo vya aina zote za rushwa zikiwemo rushwa ndogo ndogo (petty corruption) na rushwa kubwa na ufisadi (grand corruption) na matumizi mabaya ya madaraka;

NA KWA KUWA, kwa sababu ya majukumu yake mapana kisheria, TAKUKURU inaelekea kuelemewa katika vita ya kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa letu kiuchumi, kijamii na kisiasa;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Serikali iandae na kuwasilisha Muswada wa marekebisho ya Sheria iliyoiunda TAKUKURU kwa lengo la kuanzisha taasisi mahsusi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa;

7. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha jinsi ambavyo TANESCO imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kulipa gharama za umeme unaozalishwa na IPTL na hivyo kuathiri hali ya kifedha ya Shirika hilo;

KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba TANESCO itaendelea kulipa fedha nyingi kwa ajili ya gharama za umeme huo wa IPTL;

HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo.

8. KWA KUWA, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya TANESCO na makampuni binafsi ya kufua umeme imeisababishia TANESCO hasara ya mabilioni ya fedha na hivyo kutishia uhai wake wa kifedha;

KWA KUWA, Bunge lilikwishaazimia kwamba serikali iwasilishe mikataba husika Bungeni au kwenye Kamati zake kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza vyema wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri serikali;

NA KWA KUWA, Serikali haijatekeleza Azimio hilo la Bunge hadi sasa;

HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali itekeleze Azimio husika la Bunge mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti Serikali iwasilishe taarifa ya utekelezaji wa mapitio ya mikataba ya umeme.

Imewasilishwa leo hii tarehe 28 Novemba, 2014.

------------------------------------------------------
ZITTO ZUBERI KABWE (MB)
MWENYEKITI
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI

Taarifa ya punguzo la 40% ya matibabu kwa Watanzania

Konseli Mkuu, Bw. Omar Mjenga wa Konseli Kuu ya Dubai kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani iliyopo Dubai (Iranian Hospital Dubai), wakiweka saini makubaliano ya pamoja ambayo yatatoa punguzo la asilimia 40 ya matibabu kwa Mtanzania yeyote yule atakayetibiwa katika hospitali hiyo. Makubaliano hayo yamewekwa saini katika hospitali ya Irani iliyopo Dubai, maeneo ya Jumeirah.


Konseli Mkuu Omar Mjenga wa Tanzania, Dubai pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani, Dubai wakionyesha makubaliano mara baada ya kumaliza kutiliana saini.


Je, media imesimamia misingi kwenye kashfa ya 'Tegeta escrow'

Vyombo vya habari na dhima katika kashfa mbalimbali mfano, akaunti ya Tegeta escrow.
  • Je, vimesimamia misingi ya kiuandishi?
  • Je, umma umefaidikaje na taarifa hizi?
  • Je, taaluma ya habari imetenda na inatenda ndivyo?
Kwa mchanganuo wa ufafanuzi kuhusu hayo, ungana na Mohamed Khelef akiongoza 'meza duara' ya DW katika pleya iliyopachikwa hapo chini.

Hotuba ya Waziri Mkuu, Pinda ya kuhitimisha Mkutano wa Bunge


HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA 16 NA 17 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 29 NOVEMBA, 2014


I:          UTANGULIZI 
                                   
a)              Masuala ya jumla

Mheshimiwa Spika,
1.            Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Kumi na Sita na Kumi na Saba wa Bunge lako Tukufu.  Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

Mheshimiwa Spika,
2.             Mkutano huu ulijumuisha kujadili kazi kubwa zifuatazo:

Kwanza: Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/2016;

Pili:                 Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 [The Tax Administration Bill, 2014];

Tatu:              Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani wa Mwaka 2014 [The Value Added Tax Bill, 2014];

Nne:               Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2014 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2014]; na
Tano:             Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014, [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2014].

Aidha, ni hivi mapema leo Miswada 11 ya Sheria ya Serikali kuhusu mambo mbalimbali ilisomwa kwa mara ya kwanza.

Mheshimiwa Spika,
3.            Nitumie nafasi hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki katika Kamati ya Mipango hapa Bungeni kwa kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa na Serikali kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2015/2016. Maoni na Ushauri tuliopokea kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge tutauzingatia wakati wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2015/2016. Vilevile, niwashukuru kwa kujadili na kupitisha Miswada ya Sheria niliyoitaja hivi punde.

b)            Maswali
Mheshimiwa Spika,
4.            Katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya kawaida na yale ya Papo Papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Jumla ya maswali 241 ya msingi na 662 ya nyongeza yameulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali.  Aidha, Maswali 18 ya msingi na 13 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.c)         Kauli za Mawaziri
Mheshimiwa Spika,
5.            Waheshimiwa Wabunge watakumbuka kuwa tarehe 17 Novemba, 2014 nilipata fursa ya kutoa Kauli ya Serikali kuhusu Mgogoro kati ya Wakulima na Wafugaji Wilayani Kiteto. Aidha, baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri walipata nafasi ya kutoa Kauli mbalimbali za Serikali kama ifuatavyo:

i)          Kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu taarifa zilizotolewa na Vyombo vya Habari za shutuma dhidi ya Serikali za China na Tanzania kujihusisha na Biashara Haramu ya Pembe za Ndovu na ile inayohusu Kuridhia Mkataba wa Umoja wa Afrika kuhusu Demokrasia, Uchaguzi na Utawala wa Mwaka 2007;
ii)         Kauli ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu Hali ya Dawa Nchini na Matibabu ya Saratani Nchini; na

iii)        Kauli ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kuhusu Mwenendo wa Soko la Nafaka na Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo.

Maazimio

Mheshimiwa Spika,
6.            Tarehe 7 Novemba, 2014  Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kujadili na kupitisha Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa  Anne  Semamba Makinda (Mb.), Spika wa Bunge la Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  kwa  kuchaguliwa kuwa  Rais  wa Mabunge  ya  Nchi  Wanachama  wa Jumuiya ya  Maendeleo  ya  Kusini  mwa  Afrika (SADC-PF). Aidha, katika Mkutano huu Waheshimiwa Wabunge walipata pia fursa ya kujadili na kuridhia Maazimio mengine yafuatayo:

i)             Azimio la Bunge kuhusu Itifaki ya Kuanzishwa kwa Tume ya Utafiti wa Afya, Jumuiya ya Afrika Mashariki;

ii)            Azimio la Bunge la Kufuta na Kusamehe Madai au Hasara itokanayo na Upotevu wa Fedha na Vifaa vya Serikali kwa Kipindi Kilichoishia tarehe 30 Juni, 2011;          
iii)        Azimio la Bunge la kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Kiulinzi [The East African Protocol on Cooperation in Defence Affairs]; na

iv)        Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Uzuiaji wa Vitendo Haramu dhidi ya Usalama wa Miundombinu ya Kudumu iliyojengwa chini ya Bahari katika Mwambao wa Bara ya Mwaka 1988 [The Protocol for the Suppression of Unlawful Acts Against the Safety of Fixed Platforms located on the Continental Shelf – SUA, 1988].
           
e)         Taarifa Maalum za Kamati
Mheshimiwa Spika,
7.            Mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, Waheshimiwa Wabunge walipokea Taarifa Maalum ya Kamati ya Hesabu za Serikali (Public Accounts Committee - PAC) Kuhusiana na Miamala iliyofanyika katika Akaunti ya “ESCROW” ya TEGETA pamoja na umiliki wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Mheshimiwa Spika,
8.            Naomba nitumie fursa hii, kwanza kukushukuru wewe Mheshimiwa Spika kwa kuruhusu Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha Taarifa hii Maalum kwenye Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Aidha, niwashukuru Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati kwa uchambuzi wao wa kina na Mapendekezo yao kama yalivyowasilishwa katika Mkutano huu. Nitumie fursa hii pia kuwashukuru Waheshimiwa Mawaziri waliozungumza kwa niaba ya Serikali nzima kutoa maelezo yaliyolenga kutoa ufafanuzi wa hali halisi ya suala hili la Akaunti ya ESCROW ya TEGETA na pia kujibu baadhi ya Hoja za Kamati.

HAPA AMEONGELEA MASUALA YA ESCROW ACCOUNT.

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

a)            Maandalizi ya Kupiga Kura tarehe 14 Desemba, 2014
Mheshimiwa Spika,
9.             Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara unatarajiwa kufanyika tarehe 14 Desemba, 2014. Uchaguzi huo ni wa kawaida na unahusisha Uchaguzi wa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji, Mitaa, Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa. Taarifa nilizonazo ni kwamba hadi sasa maandalizi ya Msingi kuwezesha Uchaguzi huo kufanyika yamekamilika.

Mheshimiwa Spika,
10.         Ili kuhakikisha kuwa Uchaguzi huo unafanikiwa, maandalizi ya Kanuni za Uchaguzi yalifanyika kupitia Vikao vya Wadau mbalimbali ili kupata maoni, mapendekezo na ushauri ambao umesaidia katika kuboresha Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Wadau walioshirikishwa ni pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu; Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Asasi Zisizo za Kiserikali (AZAKI).

b)            Uandaaji wa Kanuni za Uchaguzi za Mwaka 2014
Mheshimiwa Spika,
11.         Katika maandalizi ya awali, orodha ya Vijiji, Mitaa na Vitongoji iliandaliwa na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali la tarehe 22 Agosti, 2014 lenye Tangazo la Serikali Namba 300 kwa Halmashauri za Miji na Tangazo Namba 301 kwa Halmashauri za Wilaya. Orodha hiyo imejumuisha Kata, Vijiji na Mitaa. Katika Uchaguzi wa mwaka huu, jumla ya Vijiji 12,443, Vitongoji 64,616 na Mitaa 3,741 vitahusika kwenye Uchaguzi.

Mheshimiwa Spika,
12.         Ili kufanikisha Uchaguzi huo, Serikali imekwishaandaa na kuchapisha Vipeperushi, Fomu za Wagombea, Rejesta ya Wapiga Kura, karatasi za kuonyesha Vituo vya Kupigia Kura, Mabango na Matangazo mengine kuhusu Elimu kwa Mpiga Kura. Tayari vifaa hivyo vimepelekwa Mikoani na vingine vinaendelea kupelekwa. Aidha, Masanduku ya Kupigia Kura yameshanunuliwa na tayari yameshasambazwa katika Mikoa yote Tanzania Bara.

Mheshimiwa Spika,
13.         Kwa vile siku zilizobakia kufikia tarehe ya Kupiga Kura ni chache, natoa Wito kwa Wananchi ambao hawajajiandikisha katika Rejesta ya Wapiga Kura wafanye hivyo bila kukosa. Aidha, Viongozi wa Vyama vya Siasa wawahimize Wanachama wao na Wananchi kwa ujumla wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na hatimaye wajitokeze siku ya Kupiga Kura. Aidha, Wasimamizi wa Uchaguzi wahakikishe vifaa vya Uchaguzi vinafika kwenye maeneo yao kwa wakati.

Mheshimiwa Spika,
14.         Napenda nitumie nafasi hii kutoa Rai kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa waendeshe kampeni kwa amani na kuepuka maneno ya uchochezi, kubaguana kwa misingi ya ukabila, rangi, udini ama hali ya mtu mambo ambayo yanaweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani. Aidha, nawaomba Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wanachama wao, wakishapiga kura wasiendelee kukaa katika Vituo vya Kupigia Kura, bali watawanyike na kusubiri muda wa matokeo.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika,
15.         Leo nimeona nizungumzie masuala muhimu yanayochangia kusukuma Gurudumu letu la Maendeleo. Kabla sijahitimisha hotuba yangu, naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru wote waliosaidia kufanikisha Mkutano huu. Kipekee nikushukuru wewe Mheshimiwa Spika, pamoja na Naibu Spika kwa kutuongoza vizuri.  Niwashukuru Wenyeviti wa Bunge kwa kazi nzuri ya kuongoza vikao vya Bunge lako Tukufu.  Aidha, niwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge kwa kazi nzuri na kwa michango mbalimbali wakati wa Mkutano huu.

Mheshimiwa Spika,
16.         Naomba pia nimshukuru Katibu wa Bunge na Wasaidizi wake wote pamoja na Wataalam wote wa Serikali na Taasisi zake ikijumuisha Taasisi za Sekta Binafsi, kwa misaada ya Kitaalam na huduma mbalimbali za kufanikisha Mkutano huu. Niwashukuru pia Waandishi wa Habari kwa kazi nzuri walizofanya kuhakikisha kuwa taarifa za majadiliano na maamuzi mbalimbali ya hapa Bungeni zinawafikia Wananchi. Niwashukuru Madereva kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuwasafirisha kwa usalama Waheshimiwa Wabunge, Viongozi mbalimbali, Wataalam na Wasaidizi wote walioshiriki katika Mkutano huu.

Mheshimiwa Spika,
17.         Nimalizie kwa kuwatakia wote safari njema mnaporejea kwenye maeneo yenu ya kazi na katika majimbo yenuAidha, niwatakie mapumziko mema ya Sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya wa 2015. Ninaamini kwamba, Mwenyezi Mungu atatulinda na kutuvusha salama sote kama tulivyo hadi kuuona Mwaka Mpya wa 2015.  Baada ya kusema hayo, naomba sasa kutoa Hoja kwamba, Bunge lako Tukufu liahirishwe hadi tarehe 27 Januari, 2015 saa 3:00 Asubuhi litakapokutana katika Mkutano wa 18 kwenye Ukumbi huu hapa Dodoma.

Mheshimiwa Spika,
18.         Naomba kutoa Hoja.

Tangazo la msiba wa Kepteni Kaluse aliyefariki katika ajali ya helikopta Dar

Mrakibu wa Polisi-Captain Kidai Senzala Kaluse enzi za uhai wake. 

Familia ya Mzee Senzala Kaluse wa Kimara Mwisho Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao KIDAI SENZALA KALUSE kilichotokea Novemba 29, 2014 Saa 4 asubuhi kwa ajali ya ndege aina ya helkopta huko Kipunguni B, Moshi Bar, Dar es Salaam.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa baba yake Mzee Kaluse huko Kimara Mwisho.

Habari ziwafikie, Ukoo wote wa Warutu, Ukoo wa Kaluse, Ukoo wa Mroki, Familia yote ya Timothy Nathan, Ukoo wa Kajiru na Taluka, Wakamba wote wa Ugweno Msangeni, Bibi wa Marehemu Mary Nathan wa Kinyenze- Morogoro, Familia ya Tarimo ya Ukonga Mombasa, Omary Msuya wa Moshi, Abdalh Mgonja wa Gonja Maore, Hosea wa Arusha.

Taarifa pia ziwafike maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Kikosi cha Polisi Anga, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

Misa ya kuaga Mwili wa Marehemu itafanyika mnyumbani kwao kuanzia Saa 6:00 kabla ya safari ya kuelekea Gonja Maore, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kuanza na mazishi yatafanyika Jumatatu Kijijini Kwao Gonja Maore.

Mawasiliano zaidi: Mroki Mroki- +255 717002303. 

MATAYO 5: 4 HERI WENYE HUZUNI; MAANA WAO WATAFARIJIKA

  • Taarifa hii imewasilishwa wavuti.com na Mroki Mroki/Father Kidevu blogTAARIFA

Marubani watatu wa polisi pamoja na rubani mmoja wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliyetambuliwa kwa jina la Joseph Alfayo wamekufa baada ya helkopta waliyoruka nayo katika ukaguzi wa kawaida kuanguka.

Helkopta hiyo namba 5H- TWA ni mali ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Ajali hiyo imetokea leo saa 4 asubuhi maeneo ya Ukonga Moshi Bar.

Akizungumza katika eneo la tukio, Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kamishna Suleiman Kova alisema, chanzo cha helkopta hiyo kuanguka bado hakijajulikana na uchunguzi kujua chanzo unaendelea.

Aliwataja wengine waliokufa ukiachia Alfayo kuwa ni Mrakibu wa Polisi Kapteni Gidai Sindano, Mkaguzi wa Polisi Inspekta Simba Muta na askari PC Josu Selisina.
Rais Kikwete arejea Tanzania baada ya matibabu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014.
(picha: Ikulu)

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani.

Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake.
"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," 
alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.

Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."

Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.

Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Rais Bw. Morris Mbena baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bw. Rashid Othman baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana kwa furaha na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Mama Maria Nyerere akiongea na Mama Salma Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya Rais Kikwete kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Dua ilisomwa na viongozi mbalimbali wa dini baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza kuongea na wanahabari mara tu alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabuRais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia kwa furaha wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliyeongoza mapokezi hayo ya Ikulu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa kwa furaha na mwanaye Khalfani baada ya kuwasili nyumbani salamaChronology of key events since IPTL signed a MOU with TANESCO

The Citizen brings you a chronology of key events since Independent Power Tanzania Limited (IPTL) signed a memorandum of understanding with Tanzania Electric Supply Company (Tanesco)  20 years ago:
1994 – Drought leads to power shortages as hydro catchment areas run dry.   Tanesco invites emergency solutions, eventually settling for two turbines financed by foreign aid.  A joint venture known as Independent Power Tanzania Ltd is set up between Mechmar Corporation of Malaysia (70 per cent) and VIPEM of Tanzania (30 per cent).
August 1994 – IPTL signs an MoU to provide electricity under an independent power project arrangement as a “fast track” measure, but a “medium to long-term solution” is proposed in November.
November 1994-June 1995 –  IPTL starts negotiations with Tanesco through KTA Tenaga Sdn Bhd (Malaysia-engineering), Fieldstone Private Capital Group (USA-finance), Long and Co. and Clyde and Co. (UK-legal affairs).
May-June 1995 – IPTL and Tanesco sign a 20-year power purchasing agreement to build and run a 100 megawatt slow-speed diesel (SSD) power plant in Tegeta, Dar es Salaam, at the cost of $163.5 million, including an engineering procurement and construction contract (EPC) worth $126.39 million, and with a “reference tariff” of $4.2 million per month plus 3.25 US cents per kWh of electricity actually produced.   The final tariff will depend on actual costs incurred.
February 1995-January 1996 – Without informing Tanesco, IPTL negotiates with Wärtsila to build a cheaper medium-speed diesel (MSD) plant.
Wärtsilä’s EPC bid increases by 33 per cent, from $85.7 million to $114.2 million, even though the scope of the project falls considerably.
February 1997 – EPC contract signed.
May 1997 – Mechmar/IPTL obtain a $105 million loan from Sime Bank and Bank Bumiputra. In September 1997, Tanesco requests full documentation on actual costs incurred in order to negotiate final power purchase tariffs.
IPTL produces the EPC at the end of February 1998.
April 1998 – Tanesco issues notice of default to IPTL for unilateral substitution of MSD facility.
April-October 1998 –  Tanesco attempts unsuccessfully to negotiate a lower tariff reflecting the “actual, verifiable and prudently incurred cost” to IPTL of building an MSD plant — as opposed to the contracted SSD plant.
November 1998 – Tanesco requests arbitration before the International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID) after IPTL fails to justify the cost structure and payments, including $6.4 million payments to Omni Technical Management Establishment and Prime Consolidated Establishment.
November 1999 – IPTL takes Tanesco to court, claiming interim payments of $3.6 million a month.
IPTL wins the case in March 2000, but execution of the ruling is stayed pending Tanesco’s appeal.
May 2000 – Two Tanzanian officials sign affidavits claiming they were offered bribes by IPTL director James Rugemalira. A third admits accepting a bribe.
February 2001 – ISCID finds that IPTL was overpriced by $23.5 million, but that the contract still stands since Tanesco was aware of the switch from SSD to MSD.
July 2001 – The Minister for Energy and Minerals announces that IPTL will start generating 100MW of electricity in October 2001, and that the Songas natural gas project will start in September.
January 15, 2002 – IPTL starts supplying power to the national grid for 13 US cents per unit.
March 1, 2002 – VIPEM petitions the High Court of Tanzania to wind up IPTL.
2006 – Tanesco disputes the capacity charges charged by IPTL, forcing the two sides to seek arbitration at the ICSID. Following the dispute, both IPTL and Tanesco agree to open an escrow account at the Bank of Tanzania (BoT), pending the determination of the arbitration.
2008 – Mechmar, a Malaysia-based company, which owns 70 per cent of IPTL, is placed under receivership because it defaulted on a loan it borrowed to buy the Tegeta power plants. Standard Chartered Bank Hong Kong gets an order from the High Court of Malaysia, which gives the bank the power to take over the management and operations of Mechmar, including IPTL.
2009 – The High Court of Tanzania places IPTL under a receiver manager (RITA) following the 2002 winding up petition filed by Mr Rugemalira.
2010 – The Malaysian High Court and later on British Virgin Islands High court revoke an attempt to sell Mechmar’s 70 per cent stake in IPTL to a company called Piper Link. The company, registered in the British Virgin Islands, is forced to surrender the share certificates by a British Virgin Islands court. Interestingly, Piper Link was represented by Mr Harbinder Singh Sethi, according to a report compiled by former Tanesco Chief Legal Counsel Godwin Ngwilimi.
2010 – Mr Sethi comes to Tanzania, and claims that he had bought 70 per cent of IPTL from the Malaysian company.  He attempts to take over the management of the company, but fails because of the winding up petition filed by Mr Rugemalira, the minority shareholder, who owns 30 per cent of IPTL.
September 2013 –  Mr Rugemalira finally agrees to sell his 30 per cent stake to Mr Sethi’s company called PAP for $75 million. He is paid an advance of $7 million on the condition that he withdraws his winding up petition filed at the High Court of Tanzania. Mr Rugemalira withdraw the petition, which paves the way for the consent judgment issued by Mr Justice John Utamwa in September.
October 2013 – PAP’s lays claim to the escrow monies start, but faces legal hurdles. BoT raises concerns, including the allegation that PAP had not registered the purported sale of the 70 per cent stake with the Business Regulatory and Licencing Authority (Brela). BoT also demands proof that PAP lawfully acquired 70 per cent of IPTL as it claims.
October 2013 – PAP presents documents to Tanzania Revenue Authority (TRA) that show that Mechmar sold its 70 per cent stake to Piper Link  for Sh6 million ($3,663). The documents further show that two weeks after the purported transfer of shares, the British Virgin Island company sold those share to PAP at the price for $300,000 (Sh500 million).
November/December 2013 – BoT transfers escrow funds to PAP’s accounts at Stanbic Bank after clearance from the Attorney General’s office as well as the Ministry of Energy and Minerals.
February, 2014 – ICSID rules that Tanesco was indeed overcharged by IPTL. The arbitrator orders the two parties to re-calculate the tariff and report back to the court in May 2014 so that a decision is made. At that time, the escrow account had already been emptied and officially closed.
March 2104 – Parliament’s Public Accounts Committee, directs the Controller and Auditor General to launch an investigation into the process leading to the irregular withdrawal of money from the escrow account.
  • SOURCE: The Citizen, 24 November 2014