AU Chair Mugabe welcomes proposal to name HQ after Nyerere; Pays tribute to Algeria for ending colonialism in Africa

ADDIS ABABA - New chairman of the African Union, Zimbabwean Head of State Robert Mugabe paid tribute to Algeria on Saturday in Addis Ababa for its role and contribution to the liberation of Africa from colonialism.

Mugabe who was speaking during the second and last day of the 24th Ordinary Summit of AU Heads of State and Government, paid tribute to several African countries which have contributed to the liberation of the continent from colonialism and "emphasized the role of Algeria who was on the frontline with the Africans. "

The AU chairman, speaking at the end of the session on the examination of peace and security issues, also welcomed the proposal to name the new headquarters of the AU Peace and Security Department after an African famous figure, late Julius Kambarage Nyerere (1922-1999), nicknamed "Mwalimu" (the teacher). He was President of Tanzania between 1964 and 1985.

Maandalizi ya kilele cha miaka 38 ya CCMKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mratibu wa Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Emmanuel Nchimbi, walipokuwa wakikagua mazoezi ya vijana wa Chipukizi wa CCM ya paredi na halaiki kwa ajili ya Maadhimisho ya Kilele cha Miaka 38 ya CCM, yatakayofanyika Kitaifa kesho kwenye Uwanja wa majiMaji mjini Songea.Vijana wa Chipukizi wa CCM waliopo katika mazoezi ya halaiki na paredi kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM mjini Songea, wakikipiga saluti wakati wa mazoezi ya mwisho leo kwenye uwanja wa MajimajiKijana wa Chipukizi wa CCM Mbaraka Ngonyani akionyesha umakini wake wakati akipiga saluti wakati wa mazoezi hayo ya mwisho leoKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa UVCCM Sixtus Mapunda wakitazama mazoezi ya mwisho ya Chipukizi haoMshika bendera ya CCM kwenye kikosi cha Bendera cha Gwaride la Umoja wa Vijana wa CCM, Sharif Mohammed na wenzake wakipita kwa ukakamavu mbele ya jukwaa kuu wakati wa mazoezi ya mwisho ya gwaride na halaiki kwa ajili ya Kilala cha Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yanayofanyika kesho Kitaifa kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani RuvumaVijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini SongeaVijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini SongeaVijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini SongeaVijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini SongeaVijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha mazoezi ya ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini SongeaVijana wa Chipukizi wakionyesha ohodari wao wa mazoezi ya 'kikomandoo' wakati wa mazoezi yao ya mwisho ya paredi na halaiki kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 38 ya CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini SongeaChipukizu hao wakiwa kwenye mazoezi ya halaikiMmoja wa Chipukizi wa CCM waliokuwa katika mazoezi hayo akisaidiwa baada ya kuanguka kutokana na mazoezi hayo ya mwisho kupamba moto. Alipata ahueni baada ya kupatiwa huduma ya kwanza. 

  • Taarifa-picha hii tumeshirikishwa na: Bashir Nkoromo

Prof. Muhongo akabidhi ofisi ya Uwaziri kwa Simbachawene

Waziri mpya wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati makabidhiano ya ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,leo jijini Dar es Salaam.
Waziri mpya wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati makabidhiano ya ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,leo jijini Dar es Salaam.

Waziri mpya wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akikabidhiwa rasmi nyaraka za ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo,leo jijini Dar es Salaam.
picha: Emmanuel Massaka via Michuzi BlogFeatured at the NPR: It's been a hard road to 12-Step for Zanzibar's heroin addicts


Could a 12-step program, with its Christian roots, help addicts recover in a conservative Muslim island in the Indian Ocean?

Suleiman Mauly was desperate to find out. He'd been using heroin in his native Zanzibar since age 17. The island nation is a key stop for heroin smuggled from Pakistan and Afghanistan to Europe. An estimated 7 percent of the 1 million inhabitants are heroin addicts.

Mauly had tried to get clean a couple of times. It didn't work. Then he discovered a 12-step program in Mombasa, Kenya.

He not only stopped using drugs, he made amends to friends and family he'd harmed as an addict.
"And before you make amends you have to search yourself, your feelings of guilt and resentment," says Mauly, now 34 and in recovery for 8 years. "It's a kind of Christian spiritual process." Indeed, the 12-step program, founded in Akron, Ohio, some 80 years ago, relies on Christian concepts: confession, redemption, submission to a higher power.
"People have difference experiences with the higher power," he says. "Some of them say it's Allah. Some of them, Jesus. For me, the power greater than myself was a program, a group and my family. And then later, I've started to understand how to rely on God." 
He is largely responsible for introducing the program to his country.

But the program's Christian connection turned out to be a sensitive topic in Zanzibar, where the mostly Muslim population has... Click here to continue reading.


Raha ya dafu huku ukibarizi upepo mwanana wa bahari...

Anafurahia dafu huku akibarizi katika upepo mwanana katika ufukwe maeneo ya Upanga Mashariki, pembezoni mwa Barack Obama Drive jijini Dar es Salaam kama alivyokutwa na kamera ya Mohamed Mambo mwishoni mwa wiki iliyotangulia (picha: DailyNews)

Rais Kikwete mkutanoni AU, Addis Ababa


Rais Jakaya Kikwete akipitia moja ya taarifa wakati akiwa kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa,Ethiopia leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe.


Rais Kikwete, Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika (kulia) wakikutana na marais wastaafu, Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini(Kushoto) na Joachim Chissano wa Msumbiji (wapili kushoto) wakati wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Ethiopia leo.


Rais Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.


Rais  Kikwete,Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika (wanne kushoto), Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki (kulia) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kukutana wakati wa mkutano wa wakuu wan chi wanachama wa AU unaofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.

Picha: Freddy Maro/IKULU

Bungeni: Taarifa maalumu kuhusu deni la Serikali la Sh 1,875,896,246,224/= kwa Mifuko ya Jamii

TAARIFA MAALUM KUHUSU DENI LA SH. 1,875,896,246,224.48 AMBALO SERIKALI INADAIWA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII


2.7.1
​Mheshimiwa Spika, tarehe 24 Oktoba, 2014, Kamati ilifanya kikao cha mashauriano kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gavana wa Benki Kuu, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Msajili wa Hazina na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

2.7.2
​Mheshimiwa Spika, Dhumuni la kikao hicho lilikuwa kujadili na kutafuta ufumbuzi juu ya hoja ya ukaguzi iliyoibuliwa kwenye Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusiana na ukaguzi kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma zinazoishia tarehe 30 Juni 2013. Kwa mujibu wa Taarifa hiyo na ukaguzi uliofanyika baadaye, mpaka kufikia tarehe 30 Septemba 2014 Serikali ilikuwa inadaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii jumla ya Sh.1, 875,896,246,224.48. Aidha, ilifahamika kuwa deni hilo halijumuishi deni la Serikali kwa PSPF la Sh. 7,066,530,000,000.00 ambalo lilianza mwaka 1999 baada ya PSPF kulipa mafao ya Wanachama ambao kisheria walistahili kulipwa lakini walikuwa hawachangii kwenye Mfuko huo.

2.7.3​
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa kulipwa kwanza kwa deni la Sh.1, 875,896,224.48 ili mifuko ya Hifadhi ya Jamii iweze kujiendesha bila matatizo, makubaliano yafuatayo yalifikiwa katika kikao hicho:-

a) Serikali kulipa kwanza asilimia 50 ya deni hilo kwa kutoa Hati fungani (Special Government Bond) ifikapo tarehe 14 Novemba, 2014 endapo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itasamehe kiasi cha tozo kilichojumuishwa katika deni hilo kinachotokana na malimbikizo ya madeni kwa miradi na mikopo ya Serikali.

b) Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kujadiliana na Bodi za Wadhamini kuhusu kuridhiwa kwa ombi la Serikali la kusamehewa na Mifuko hiyo kiasi cha tozo kilichojumuishwa kwenye deni hilo ili iweze kulipa sehemu ya deni hilo kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.

2.7.4​ 
Mheshimiwa Spika, Bodi za Wadhamini wa Mifuko hiyo ziliridhia kusamehe tozo hizo endapo Serikali ingetoa Hati Fungani hiyo tarehe 14 Novemba, 2014. Lakini cha kusikitisha Serikali haikutimiza ahadi yake na mpaka Kamati inawasilisha taarifa yake makubaliano hayo hayajatekelezwa na Mifuko imeendelea kuwa katika hali mbaya ya kifedha. Kamati inapendekeza kuwa Serikali itekeleze makubaliano hayo mara moja na bila kuchelewa na ukopaji holela wa Serikali kwa Mifuko wa Hifadhi ya Jamii
nchini ukome mara moja.

3.7 ​
Mapendekezo ya kuinusuru Mifuko ya Hifadhi ya Jamii isishindwe kutoa huduma kwa Wanachama wake na Wastaafu kutokana na Serikali kushindwa kuilipa Deni la Jumla ya Sh.1, 875,896,246,224.48.

​KWA KUWA, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inakabiliwa kupungukiwa uwezo wa Fedha za kujiendesha kutokana na Serikali kushindwa kulipa deni la Sh. 1,875,896,246,224.48 kama ilivyoainishwa kwenye Sehemu ya Pili ya Taarifa hii,

​NA KWA KUWA, Kamati imefanya kila linalowezekana kuwezesha deni hilo lilipwe kwa manufaa ya wanachama wa Mifuko hiyo na Wastaafu,

​HIVYO BASI, Kamati inaliomba Bunge lako Tukufu kuazimia Serikali ilipe deni hilo haraka iwezekanavyo ile kuinusuru Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika changamoto ya kushindwa kulipa mafao ya Wastaafu na kutoa huduma nyingine.

Zitto Kabwe

[video] Mahojiano ya Sporah na Dj Romy Jones wa Diamond

Diamond Platnumz' Official Dj Romy Jones akiongelea historia ya maisha yao na kazi zao.

Mamba washambulia wananchi kijiji cha Kafunjo

Ujumbe ufuatao unachapishwa kama ulivyopokelewa kwa njia ya anwani pepe:

Moja wapo ya matukio makubwa yaliyotokea ndani ya mwaka 2014 wilayani Karagwe, mkoani Kagera, ni idadi kubwa ya watu kufariki baada ya kuliwa na mamba katika kijiji cha Kafunjo, kata ya Kiruruma katika wilaya ya Karagwe. Na hivi majuzi tarehe 28.1.2015, mtoto moja amenusurika kifo baada ya kungatwa na mambo alipokuwa ameenda kuchota maji katika ziwa hilo.

Zaidi ya watu 5 wameliwa na idadi kubwa ya mifugo wakiwemo ngombe, mbuzi na nguruwe wmeliwa na mambakatika mwaka huu wa 2014. Idadi hii ni nyongeza ndogo tu ya watu waliokufa maji katika ziwa hili la kafunjo wakiwa ama wakifanya shughuri ya uvuvi, wakisafiri kwenda ngamo au wakiwa wa wameenda kuchota maji au kutafuta kuni.

Cha kusikitisha ni kuwa, viongozi wa eneo hili hawatowi taarifa za matukio haya, jambo linalowafanya wananchi katika eneo hilo kutojhesabu kuwa, wanayo serikali.
Akina mama na watoto ni kundi ambalo limeathirika sana na matatizo haya. Kijiji cha Kafunjo hakuna zahanati hivyo akina mama wotewanalazimika kusafiri mwendo mrefu hadi zahanati iliyoko katika kijiji cha Kamagambo. Hali hii inawafanya hasa akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano kukosa chanjo muhimu na tiba wanavyopaswa kupata.

Hali hii imesababisha kuwepo na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu hasa wenye kuwa na tatizo la kifafaa na ulemavu mwingine hasa wa viungo. Kijiji cha Kafunjo kina zaidi ya watu 185 wenye ilemavu wa aina mbali mbali na kwa sasa wanasaidiwa na shirika la KCBPR la kanisa la anglikana.

Kufuatia mamba kula watu huko Kafunjo, Radio fadeco imefanya ziara katika kijiji hicho kwa siku ya leo. Safari ya kuelekea kijiji cha Kafunjo imeanza mchana na kuhusisha mwandishi wa habari Vitus Mzare ambaye ni mwenyeji wa eneo hili na ameingooza teama ya radaio fadeco kutoka Kayanga.
Kijiji cha Kafunjo ni miongoni mwa vijiji vya kata ya Kiruruma. Ni kijiji mojawapo ya vijiji vinavyozunguka ziwa na Kafunjo. Barabara iendayo katika kijiji hiki ni nzuri kuanzia mji mdogo wa Nkwenda. Kabla ya kuingia kijiji cha Kafunjo unakaribishwa na beria mbili. Mmoja ikiwa ya wilaya ya Kyerwa na inayofuata ni ya wilaya ya Karagwe.

Safari yetu katika kijiji cha Kafunjo kiongoji cha Kirigite imetupeleka hadi kwa mzeeDeogratius Thomas ambaye siku za hivi karibuni amemuzika kijana wake ya miaka 13 baada ya kuliwa na mamba sehemu zake za mwili. Marehemu huyu amekuwa ni mtu wa 5 kuwawa na Mambo katika familia hii ambaue tumeikuta katika majonzi makubwa.

Safari ya radio fadeco katika kijiji cha Kafunjo imekua kufuatia taarifa zilizotolewa na Kijana Deus Faustine Kaijage ambaye baada ya kukerwa na matatizo yaliyomo, hasa ya watu kufariki kwa kuwawa na mamba, huku viongozi wakionekana kutogushwa na matatizo ya wananchi, kijana huyu aliamua kutafuta radio fadeco. Baada ya hatua kaada za kutuma ujumbe wa simu na wakati mwingine kupiga simu bila kupokelewa, kijana huyu aliamua kutumia mtandao wa facebook. Ndipo mkurgenzi wa radio fadeco alipokutana na ujumbe wake wa face book kama unavyosomeka:

Deus Faustin Deus Kaijage
3:04pm Dec 24

Ndg sekiku naitwa deus faustine niko kafunjo kata kiruruma nataka kukupa habari kwa undani.Ilikuwa 19/12/14 majira ya saa 2:30 asubuhi kama kawaida watoto walikuwa wamezoea kwenda kuoga kwenye ziwa kafunjo hapo ndipo mtoto aitwae arani kasana alipo shikwa na mamba wananchi wakaanza kumtafuta atimae hawakufanikiwa kumpata atimaye kwenda nyumbani kwa ajili ya matanga.

22/12/14 saa1:30 jioni akaokotwa na wavuvi wa dagaa akiwa ameliwa baadhi ya viungo vyake na ni mtu wa nne ndani ya mwaka huu.naomba unitafute nikuabalishe mengi kwa no.0683938249/0754096634.

Kitu gani kilimufanya kijana huyu kuwasiliana na radio fadeco kuhusu mkasa huu wa mamba ambao wamemaliza watu katika kijiji hiki cha kafunjo?
………………………….

Baada ya kufika katika kijiji cha Kafunjo, radio fadeco imeenda moja kwa moja hadi familia ya Mzee Deogratius Thomas aliyepoteza mtoto. Wananchi katika kijiji hiki wamefurika kuzungumza na wajumbe kutoka redio fadeco., na hapa ni baadhi ya mazungumzo katika famila hii.
Ninakuomba ufuatilie mkasa huu ili uweze kubaini kilio cha jamii hii ya Kafunjo. …….


...........
Maoni ya wasikilizaji kupitia mtandao wa facebook:
Wanasemaje kuhusu sakata la mamba kula watu Kafunjo pasipo hatua shaiki kuchululiwa na yeyote anayehusika:

Amos Amabilisi Augustine

January 30 at 6:05pm


Hakika Nyakati Za Mwisho Zimefika! Watu 16! Halafu Kumuua Mamba Mpaka Kibali, Fine Ni Ulinzi Wa mali Asili Lakn Itakuwa Asili Kwa Akina nan kama mama ze2 na wadogo zetu wanakufa? enyi wanasiasa wa karagwe kuweni serious bwana! halafu oo naomba kura na vitenge! 2fkie kipindi nanyi watawala mjiulize hawa wangekuwa ndugu zenu? najua mnipitia ukurasa wa mh. aliyepost japo hamkocomment! Mungu Azipumzshe Roho Za Wapendwa Wote

Thomson Rwakilomba

January 30 at 5:36am


poleni kwa matatizo watu wa Kafunjo, tayari wananchi wameishaonyesha nia ya dhati ya kutaka mabadiliko na tunayasubiri kwa hamu, wito wa kazi kwa wananchi hakuna hila pale penye wito wa fedha hawalazi damu, sina hakika bajeti zao zikoje na unaweza kukuta maliasili hawana hata risasi, je tunajua kupanga mipango yetu ya maendeleo kwa kushirikisha wananchi ili kujua kero halisi zao ili zitafutiwe rasilimali fedha ili zitumike kumaliza kero za msingi, kwa kifupi watanzania hatuthamini utu wetu na wengine bali tunathamini kupiga hela maana tunakoelekea watu wenye dhamana watasema ni wakati wa kupiga hela kujinufaishia na kila mtu atakufa na lwake, kwa sasa hakuna uzalendo, tukitaka uzalendo na tuwe na mstakabali mzuri wa maisha yetu tuiangalie vizuri sana 2015, tuchague viongozi makini na wenye uchungu na wanaofahamu kero zetu ili iwe rahisi kushugulikia kero muhimu kwa wananchi na baadae kuzigeuza kero na changamoto nyingine kuwa za maendeleo ili wananchi waweze kunufaika nazo, Kumbuka "uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi na uchungu wa Karagwe tunaujua sisi Wanyambo" tujipange tuzijue kero zetu na tuwape dhamana wenye uchungu watakaondoa kero hizo ili wananchi waishi kwa amani, Mungu ibarike karagwe na watu wake, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Elias Sanga

January 29 at 12:53pm


wa Kyerwa KageraTZ. Nimenufaika na matumizi ya Mkaa unaotengenezwa kwa mchanganyiko wa taka kavu zaMaharage, Nyasi kavu naUdongo. Uliobuniwa na kikundi cha KIMUKA-Kyerwa.

Elias Sanga

January 29 at 12:53pm


wa Kyerwa KageraTZ. Nimenufaika na matumizi ya Mkaa unaotengenezwa kwa mchanganyiko wa taka kavu zaMaharage, Nyasi kavu naUdongo. Uliobuniwa na kikundi cha KIMUKA-Kyerwa.

Odilo Maurice

January 29 at 6:45am


ufugaji mamba ni mbinu inayotumiwa na wakulima wengi hivyo serikali ingefa itenge eneo hilo kwa ajili ya mradi kama huu. mamba huitajika kwa ngozi yake kwa ajiri ya kutengenezea vitu k.v mikanda, mifuko ya kwekea pesa yaani wallets n.k pia nyama yake inauzwa bei ghari ktk nchi za magharibi, hivyo badala ya kero ktk eneo hilo inaweza kuwa baraka maana wafanyakazi katika kilimo hk weng wao watakuwa wana karagwe, ahsante Mh. Joseph wawezaendeleza na kudevelop hii proposal hadi kuleta mafanikio.

Mutabazi Rosette Dorothy

January 28 at 11:38pm


viongozi wetu inabidi wajali mahitaji yetu kwasababu watu wanapoteza maisha kulingana na kwamba viongozi wanachukulia mambo mengine kuwa ya kawaida wakati ni ya hatari hivyo basi matukio kama haya yashughulikiwe haraka iwezekanavyo make ttazidi kuwapoteza watu


Prisca Tinka

January 28 at 11:33pm


tunapenda sana iwe ivo ila kwa uamzi tunao utoa katika uchaguzi ndo utasaidia kuokoa maisha ya wana karagwe tujiulize wakati imetokea mwanzoni nini kilifanyika na sasa imejiyokeza tena

Odillo Severine
10:17pm Jan 28
Hongereni sana sisi huku kibosho tunaendelea vizuri na ni jambo la kumshukuru Mungu kwa hizo hatua za maendeleo yetu. REDIO FADECO mbona hatuipati online


# Mugishalove Kamuntu Pole sana ndugu wote waliousika kwa namna moja au nyingine, na usumbufu wa mamba hao. Mungu amlaze pema peponi mtoto aliyepoteza maisha. Bw. Joseph Sekiku, jamani hao wahusika wa malihasili wako wapi, serkali ya kijiji imefanya nn, diwani ameangaika na suala hili kwa kiasi gani, mbunge analijua hili au kwakuwa aliyekufa hajatimiza umri wa kupiga kula. Tukiliacha hili kwa mtindo we halinigusi, wala fsmilia yangu haiathiriki, Mungu atatuwajibisha hakika. Ndiyo, tunaweza kuwafuga mamba km tutachukua hatua kwanza yakuwafanya wasiwe tishio ya maisha ya watu, me naona hadui wa maisha yako suluisho la kwanza sio kumfuga. Naomba ndugu Sekiku , fuatilia maana selikari yote iko kayanga, wawe pia bila shaka huko kayanga muda mwingi, chukua atua wasaidie wanakafunjo, wape taharifa hz wahusika wa I dara ya malihasili, nina imani kuna litakalofanyika ili kuokoa maisha ya wat

Thomson Rwakilomba poleni kwa matatizo watu wa Kafunjo, tayari wananchi wameishaonyesha nia ya dhati ya kutaka mabadiliko na tunayasubiri kwa hamu, wito wa kazi kwa wananchi hakuna hila pale penye wito wa fedha hawalazi damu, sina hakika bajeti zao zikoje na unaweza kukuta maliasili hawana hata risasi, je tunajua kupanga mipango yetu ya maendeleo kwa kushirikisha wananchi ili kujua kero halisi zao ili zitafutiwe rasilimali fedha ili zitumike kumaliza kero za msingi, kwa kifupi watanzania hatuthamini utu wetu na wengine bali tunathamini kupiga hela maana tunakoelekea watu wenye dhamana watasema ni wakati wa kupiga hela kujinufaishia na kila mtu atakufa na lwake, kwa sasa hakuna uzalendo, tukitaka uzalendo na tuwe na mstakabali mzuri wa maisha yetu tuiangalie vizuri sana 2015, tuchague viongozi makini na wenye uchungu na wanaofahamu kero zetu ili iwe rahisi kushugulikia kero muhimu kwa wananchi na baadae kuzigeuza kero na changamoto nyingine kuwa za maendeleo ili wananchi waweze kunufaika nazo, Kumbuka "uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi na uchungu wa Karagwe tunaujua sisi Wanyambo" tujipange tuzijue kero zetu na tuwape dhamana wenye uchungu watakaondoa kero hizo ili wananchi waishi kwa amani, Mungu ibarike karagwe na watu wake, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.u wa kafunjo hasa watoto.

Amos Amabilisi Augustine Hakika Nyakati Za Mwisho Zimefika! Watu 16! Halafu Kumuua Mamba Mpaka Kibali, Fine Ni Ulinzi Wa mali Asili Lakn Itakuwa Asili Kwa Akina nan kama mama ze2 na wadogo zetu wanakufa? enyi wanasiasa wa karagwe kuweni serious bwana! halafu oo naomba kura na vitenge! 2fkie kipindi nanyi watawala mjiulize hawa wangekuwa ndugu zenu? najua mnipitia ukurasa wa mh. aliyepost japo hamkocomment! Mungu Azipumzshe Roho Za Wapendwa Wote

Zilipendwa: Usiingilie ugomvi wao - Mbaraka Mwinshehe

Marehemu Mbaraka Mwinshehe anakwambia, "wanapogombana mtu na mke wake ndani ya nyumba, usiingilie kati ugomvi wao, usiingilie kabisa..." kwa sababu "utakujapata balaa na kusingiziwa mengi, mwisho wake utapata lawama"....

"Hayo yashike kichwani, usijite kimbelembele..."

EU Statement following that of EU Heads of Mission in Tanzania

PRESS RELEASE

Brussels — The government decision of January 23rd to suspend the circulation of "The East African", a longestablished regional newspaper, gives rise to concerns about freedom of press in Tanzania.

It is the duty of the media to work within the law and to make every effort to adopt and a dhere to professional standards. But Press Freedom and freedom to express opinions are fundamental rights of the people, which call for circumspection and proportionality in the application of the law.

The Delegation of the European Union expresses its concern that modern media legislation in Tanzania, including on the citizens' Right to Information, has not yet been promulgated despite the longstanding requests of the media profession and the repeated commitments of the Government.

It is recalled that in October 2010 the EU's independent Election Observation Mission recommended expediting modernisation of the media laws, taking into account stakeholders' views.

The Delegation of the European Union calls upon the Government to make every effort to preserve the freedom of expression in Tanzania and it urges all stakeholders to prioritise constructive dialogue as the primary means to resolve differences.

It also reiterates its commitment to monitor, support promote and monitor media freedom as a shared value of the EU partnership with Tanzania.

The High Commission of Canada and Embassies of Norway and Switzerland associate themselves with this statement.

Copyright European Union, 1995-2015

Download Facebook Lite for Android to reduces app overhead


Facebook released Facebook Lite, a super lightweight version of its app directed at developing markets.

Currently, the app is only available officially in a few countries—Bangladesh, Nepal, Nigeria, South Africa, Sudan, Sri Lanka, Vietnam and Zimbabwe.

The app is just about 252KB only (as opposed to the 27MB that the main app can usually take up), so if you're on an older device, a slower network, or just don't want all the extra junk, Facebook Lite is probably exactly what you were looking for. 

Alternatively, if you don't like it, the mobile site is always a good alternative.

Download Facebook lite from: Google Play  or APK mirror.

Death Row Records co-founder involved in fatal hit-and-run

The attorney for Marion "Suge" Knight says his client plans to turn himself in to authorities after he accidentally ran over and killed a friend and injured another man as he fled attackers in Compton, Calif.

Authorities are investigating Thursday's incident as a homicide.

Los Angeles County sheriffs say it looks like Knight's pickup truck backed over the victims and then drove forward and struck them again.

The empty truck was found Thursday night in a Los Angeles parking lot.

Death Row Records was a leading rap label in the 1990s.

It was founded by Tracy "The D.O.C." Lynn Curry, Andre "Dr. Dre" Young, Marion "Suge" Knight and Richard Gilbert "Dick" Griffey.

It featured artists such as Dr. Dre, Tupac Shakur and Snoop Dogg.

Rais Salva Kirr alazwa hospitali baada ya kuugua ghafla

Rais wa Soudan Kusini, Salva Kirr, amelazwa hospitali baada ya kuugua ghafla, na kukimbizwa katika hospitali ya mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mashahidi wamesema kwamba rais Kiir, alianza kuvuja damu kutoka puani.

Hayo yanatokea baada ya rais Kiir kuanzisha mazungumzo Jumatano wiki hii na kiongozi wa waasi Riek Machar kujadili masuala kwa lengo la kukomesha vita viliyosababisha maafa makubwa ambavyo vimedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja nchini Sudan Kusini.

Pande hizi mbili bado hazijaafikiana kuhusu kuundwa kwa serikali ya mpito. Maelfu ya watu wamekufa na zaidi ya milioni wameyakimbia makazi yao tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwezi Desemba mwaka 2013.
Kabla ya kuugua, hapo jana Jumatano Kiir alifanya mazungumzo na kiongozi wa waasi Riek Machar ambapo alimtaka kupuuzilia mbali maswala yanayochochea machafuko ili kumaliza Machafuko hayo ambayo yamedumu zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Viongozi wa kikanda, wanakutana baadaye leo, kushinikiza pande zote kufikia makubaliano ili kumaliza vita.

Hata hivyo rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa (AFP) huenda amefuta ziara yake nchini Ethiopia kushiriki katika mkutano wa kilele wa marais na viongozi wa Afrika, na amejielekeza katika mji wa Gao, ambapo maandamano na vurugu dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa, MINUSMA yaliyosababisha vifo vya watu wengi. Hii ni mara ya kwanza rais huyo kujielekeza kaskazini mwa Mali tangu achaguliwe.

RFI Swahili

PAC yaishauri Serikali namna ya kuinusuru TTCL

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa mapendekezo ya kuinusuru Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kutokana na hali mbaya ya kampuni hiyo kifedha kwa sasa ambapo inaendeshwa kwa hasara huku ikiwa na madeni makubwa. PAC imetoa mapendekezo hayo katika taarifa yao kwa bunge ya mwaka juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mashirika ya umma iliyotolewa Januari 28 mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa ya PAC hali ya mapato na matumizi ya TTCL kwa mwaka 2012 ilipata hasara ya bilioni 20.883 huku kwa mwaka 2013 ikipata hasara ya bilioni 16.258. PAC ilisema majumuisho ya hasara ya TTCL kupata hasara kwa takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na hasara ambayo kwa mwaka 2013 ilifikia bilioni 334.48, jambo ambalo limeiondolea mvuto wa kukopeshwa na taasisi za fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.

"...Ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali," ilieleza taarifa hiyo ya PAC.

PAC iliongeza kuwa ukiacha madeni yaliopo pia TTCL inadaiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) jumla ya bilioni 25 hivyo kufanya jumla ya deni kufikia bilioni 101.6. Kamati hiyo ya bunge imesema kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa wa mawasiliano.

Katika mapendekezo ya PAC ili kuikwamua TTCL imeishauri Serikali kununua hisa asilimia 35 zinazomilikiwa na Bharti Airtel katika TTCL kwa gharama ndogo kwani Bharti Airtel haikutimiza kikamilifu masharti ya mkataba wa mauziano ya hisa hizo hapo awali kwani tangu inunue hisa hizo haijafanya uwekezaji katika Kampuni ya TTCL.

"...TTCL isamehewe deni la Serikali Sh. 76.6 bilioni na deni la TCRA Sh. 25 bilioni ambayo jumla yake ni Sh. 101.6 bilioni na fedha hizo zipelekwe kuongeza mtaji ili Kampuni itoke kwenye kuwa na mtaji hasi wa Sh. 87.896 bilioni na kuwa na mtaji chanya wa sh. 13.704 bilioni. Likifanyika hili basi Kampuni hiyo itaweza kukopesheka. Serikali ikamilishe taratibu zake za kuimilikisha TTCL Mkongo wa Taifa ili izidi kuuendeleza kwa ufanisi na kuongeza mapato ya TTCL," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo PAC imeshauri kuwa kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya muundo wa Kampuni ya TTCL kwani kwa sasa ina idadi kubwa ya wafanyakazi (1549) isiyoweza kuwalipa. Aidha, ilibainisha kuwa kwa sasa zinahitajika bilioni 32 kwa ajili ya kugharamia urekebishaji wa muundo wa Kampuni ili uendane na mahitaji ya utoaji wa huduma mbalimbali.

Mashirika mengine yenye hali mbaya kifedha na uendeshaji ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania, ATCL ambayo kwa sasa ina madeni makubwa huku ikiwa na ndege moja aina ya Dash 8–Q 300, Wafanyakazi 142 na Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

"Jamani mnaniua! Jamani mnaniua" Inasikika sauti katika video hii nyingine ya wafuasi wa CUF "walivyoshughulikiwa"

Hii ni video nyingine zaidi ya ile iliyopachikwa siku mbili zilizopita.

Majibu yao walipoulizwa na Mwalimu: Waziri wa Elimu ni nani?...


Is Tanzania ready for a female president?

What do we learn from the Tegeta Escrow Account in relation to Hon. Professor Anna Tibaijuka’s Political Profile?

Is Tanzania ready for a female president? What do we learn from the Tegeta Escrow Account in relation to Hon. Professor Anna Tibaijuka's Political Profile?

With the Tanzanian presidential elections fast approaching in October 2015, a game of political positioning, maneuvering and witch hunt to eliminate competition from a potential female front runner is unfolding.

Prof. Anna Tibaijuka, the Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development is being put under pressure to resign or be sacked from Government with the aim of weakening her politically ahead of the October 2015 elections. 

She is being linked to the ongoing Tegeta Escrow Account Controversy because of a donation she received on behalf of a charitable organization she founded — the Barbro Johansson Girls' Education Trust (Joha Trust) that advocates for quality girls' education in Tanzania and Africa and operates model secondary schools for poor girls, mostly orphans. 

The Joha Trust board of trustees through the chairman Mr Salmon Odunga, a retired Permanent Secretary, and the patron Ambassador Paul Rupia , also a retired Head of the Tanzania Civil Service during the Mwinyi Administration, has reacted angrily to claims that Tibaijuka received the Escrow money un-procedurally and scoffed at calls for her resignation from Government. 

In a press statement signed by the two officials, the Trust is appealing to President Kikwete to reject calls to sack Tibaijuka since no law has been broken and that the money donated by a local businessman has been utilized properly for furtherance of girls education. 

"It is our hope that his Excellency the President will assess this matter with wisdom and care in view of its far-reaching implications," the statement says. 

Controversy arose after a prominent Tanzanian businessman James Rugemalira of VIP Enginerring and Marketing , who sold his shares in the Tegeta Power Plant, made a donation of US$ 1 million to Joha Trust.
The funds were received by Tibaijuka on behalf of the board transparently through a bank account that she was instructed to open at Rugemalira’s Mkombozi Bank as condition for the grant. Rugemalira indicated he would not be bothered with interbank transfers. Tibaijuka did not use any funds for personal gain confirmed the statement of the Board of Trustees.

However, her detractors are arguing that by receiving the money she contravened the Leadership Code of Ethics Act that states that any gift whose value is more than US$ 33 must be surrendered by the receiving official to his/her employer.

The board maintains that the donation was given to the school and it was never a personal gift to Tibaijuka and therefore the question of breaking the law does not arise.

The Joha Trust board is adamant that it is a common practice in Tanzania for leaders to receive donations on behalf of their respective communities, charities or the needy, be it in cash or kind. There has never been a case before where this was questioned. Why should the Tibaijuka donation be treated differently and selectively they argue. The kind of controversy generated is therefore being interpreted as nothing more than political opportunism, malice and propaganda fueled especially from her own ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) members who fear her in the internecine party nomination process. 

They say the move to censure Tibaijuka and punish people selectively for common practice would also dampen the spirit of the trustees and many other leaders who struggle to mobilize resources for development in a young nation. The board says in the absence of a law to guide voluntary donations, they do not question the source of funds.It’s our custom to receive donations in good faith, be they large or small, cash or in kind,’’ said the Trust in the statement.

After the bank had assured that Rugemalira had paid all taxes for his funds, they say they received his donation happily and with gratitude.

“Until the government informs us that the funds were illicit, we remain grateful to Rugemalira for his generous support to our cause of girls education”.

They say since the founding of the Trust, Joha has never interpreted a donation given to a trustee on its behalf as a personal gift to the trustee.

“It would be an unfortunate precedent to interpret donations received by public officials for onward
transmission to their respective constituencies or stakeholders as their personal gifts,’’ said the statement.

Tibaijuka, who is currently the Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development in Tanzania, is the first African woman ever elected by the UN General Assembly as Under‐Secretary‐General of a United Nations programme. She is the former Executive Director of the United Nations Human Settlements Development Programme known as UN‐HABITAT, the organization she run for ten years between 2000 to 2010 and raised it from obscurity to great prominence and financial stability. Architect of slum upgrading programmes in a number of Africa countries, she also founded the World Urban Forum a premier UN conference on cities and sustainable urbanization. 

Her carrier at the UN culminated with her winning the 2009 Gothernburg Award for Sustainable Development that is equated to a “Nobel Prize in the Environment”. She was also Director General of the United Nations Office at Nairobi – UNON‐ between 2006 to 2009. In that capacity she skillfully managed the behind the scenes peace process in Kenya during the Kofi Annan negotiations after the 2008 post‐election violence. It should be remembered that in 2004, by then, the British Prime Minister, choose Professor Anna Tibaijuka as a member of 17 prominent people to form the Commission for Africa to define challenges facing Africa and to provide a clear recommendations on how to support the changes to reduce poverty. Her excellent performance on the Commission is always recalled and quoted. 

As minister of lands, she has turned around a ministry that was marred with corruption and mismanagement in a maze that forms the Tanzanian bureaucracy. She is credited for her visionary and steadfast leadership style forging strategic policies to secure long term public interests in large scale land allocations for foreign investors. Since coming to office she introduced the policy of land for equity deals, whereby the government would retain at least a 25 per cent share in expansive land based investments such as farms and forests. She was invited to present this new land tenure vision for Africa into the 2013 G8 preparatory meetings held at Lancester House in London by Prime Minister David Cameron. 

Although Tibaijuka has not yet declared her candidature, if women can have a chance, she is considered by many as a front runner to replace President Kikwete who retires next year. Her opponents fear her because they feel since she returned into the country from the UN, her political carrier has progressed meteorically. In the 2010 elections she contested and defeated a former Minister for CCM parliamentary seat primaries and thereafter went through unopposed. Subsequently, President Jakaya Kikwete is said to have favored and promoted her to top positions not only in his cabinet but more important in the ruling Party hierarchy.

Although a non party cadre, Kikwete nominated Tibaijuka for election into the powerful Central Committee of CCM by the National Executive Committee. She won with a landslide despite being a novice. It would seem that success has now come to haunt her and is the main factor behind the current vendetta against her.

Prior to her political and United Nations portfolios, Tibaijuka was a Professor of Economics at the University of Dar es Salaam and is the author of various books and research papers.

She was an active member of the civil society and in 1994 she founded the Tanzanian National Women’s Council, BAWATA, an independent non‐party affiliated organization fighting for women’s economic and social rights.

In 1996 she founded Barbro Johannson Girls’ Education Trust (Joha Trust) that advocates for quality girls’ education in Tanzania and Africa and operates a model secondary school for poor girls, mostly orphans.

This is the organization now at the centre of the current controversy that is threatening to mar her political standing and an outstanding international reputation.

By
Nicholas Mararo
Nuvision Media Ltd, Kenya
17 December 2014

Mtanzania Jumanne Tevez afanyiwa ukatili Afrika Kusini

  • Akatwakatwa sehemu za siri, ajeruhiwa vibaya mgongoni, tumboni na kwenye jicho

MFANYABIASHARA aliyefahamika kwa jina la Jumanne Tevez, mkazi wa Dar es Salaam, amefanyiwa unyama baada ya kudaiwa kukatwa uume wake na wenzake.
Habari za uhakika kutoka chanzo chetu cha habari zilisema kuwa Tevez, amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu.

Chanzo chetu hicho ambacho kipo karibu na familia ya mfanyabiashara huyo, kilieleza kuwa taratibu zinafanywa ili mke wake pamoja na kaka yake waweze kusafiri kwa ajili ya kwenda kumchukua.
“Hizo taarifa ni za kweli kabisa na hivi ninavyokuambia mke wake na kaka yake wanatarajia kuondoka kesho ili wakamchukue. Amelazwa katika hospitali moja huko Afrika Kusini na hali yake si mbaya sana.

“Yule jamaa kama unavyojua alikuwa mtu wa dili wa muda mrefu, hivyo inawezekana alitofautina na wenzake ndio maana wakamfanyia kitu mbaya, si unajua hawa jama wa poda (dawa za kulevya), humalizana wenyewe tu,” 
kilisema chanzo hicho kilipozungumza na Uhuru, jana.

Habari zilizoandikwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimuonyesha mfanyabiashara huyo akiwa amevuliwa nguo zote huku akiwa amefungwa kamba mikononi na miguuni.

Tevez, anadaiwa kufanyiwa unyama huo baada ya kuwadhulumu wafanyabiashara wenzake wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Habari zinadai kuwa, mfanyabiashara huyo alifanyiwa unyama huo, Afrika Kusini baada ya kubainika kuficha dawa hizo.

Mfanyabiashara huyo anadaiwa kuficha mzigo aliopewa kutoka Afrika Kusini kuuleta Tanzania na kwamba baada ya kufika nchini, aliwaeleza wenzake kuwa mzigo huo umepotea.

Maelezo hayo yalionekana kuwaudhi waliompa mzigo huo, ndipo walipomuita Afrika Kusini, ambako baada ya kufika, waliamua kumfanyia unyama huo.

Picha mbalimbali zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zinamuonyesha Tevez, akiwa na jeraha mgongoni, tumboni na jicho lake la mkono wa kushoto.

Mfanyabiashara huyo alijipatia umaarufu mkubwa jijini Dar es Salaam, baada ya kufunga ndoa na msanii maarufu wa muziki wa taarab, Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ ama jike la Simba.
Katika nyimbo mbalimbali alizokuwa akiimba, Isha anasikika akimtaja mwenza wake huyo wa zamani waliyetengana.

Akizungumza kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini, mmoja wa marafiki wa Tevez, alisema amepata taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, alisema baada ya kusoma habari hizo na kuona picha, alimpigia simu rafiki mwingine wa karibu wa mfanyabiashara huyo, ambaye naye alikuwa hajapata taarifa kamili.

“Ninachoweza kukueleza ni kwamba habari hizi nimeziona pamoja na picha kwenye mitandao ya kijamii, nimejaribu kufuatilia kwa rafiki yake mwingine, ambaye yupo karibu naye sana, lakini hakunieleza ipasavyo mkasa huo.
“Hadi sasa kwa kweli tupo njia panda, inawezekana ni kweli, lakini bado hizi taarifa rasmi kutoka kwa familia wanazificha sasa subiri tuone. Cha kusikitisha zaidi baadhi ya watu wanasema amevuta (kufariki dunia), lakini yote hayo hatujathibitishiwa,” 
alisema.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilisema haijapata taarifa za kuteswa kwa mfanyabiashara huyo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema wizara haina taarifa hiyo na kwamba wataendelea kuzifuatilia kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi, Godfrey Nzoa, hakuweza kupatika kuzungumzia suala hilo kwani simu yake ya mkononi ilikuwa haipo hewani muda wote.


Ripoti ya PAC kuhusu hesabu zilizokaguliwa FY 2013


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


BUNGE LA TANZANIA
________________

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
_______________

TAARIFA YA MWAKA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU
ZA SERIKALI KUHUSU HESABU ZILIZOKAGULIWA ZA SERIKALI KUU NA MASHIRIKA YA UMMA KWA MWAKA WA FEDHA ULIOISHIA JUNI 30, 2013
_______________________

(Imeandaliwa kwa kuzingatia Kanuni ya120 na kuwasilishwa Bungeni kwa
mujibu wa Kanuni ya 114 (15) ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007)Imetayarishwa na:
IDARA YA KAMATI ZA BUNGE
OFISI YA BUNGE
S.L.P 941
DODOMA                                                                                                    28 JANUARI 2015


YALIYOMO
SEHEMU YA KWANZA

1.0
Utangulizi
1
1.1
Maelezo ya awali
1
1.2
Majukumu ya kikanuni ya Kamati
2
1.3
Miongozo iliyotumika katika utekelezaji wa shughuli za Kamati
3
SEHEMU YA PILI

2.0
Uchambuzi wa Taarifa za Ukaguzi Maalum na Taarifa za Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013

5
2.1
Taarifa ya awali kuhusu ukaguzi maalum wa misamaha ya kodi
5
2.2
Matokeo ya ukaguzi maalum wa fedha za ushuru wa mauzo nje ya nchi na ruzuku ya serikali kwa zao la korosho katika mkoa wa mtwara katika kipindi cha 2006/07 hadi 2010/11
10
2.3
Ukaguzi maalum wa ujenzi wa jengo la kumbi za watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere dar es salaam (jnia) katika kipindi cha 2006 hadi 2012
16
2.4
Ukaguzi maalum wa kuthibitisha iwapo kulikuwa na tija katika matumizi ya shilingi bilioni 9 na milioni 600 katika vikao mbalimbali vya mabaraza ya wafanyakazi, manunuzi na matangazo katika mamlaka ya bandari tanzania (TPA) kwa mwaka wa fedha 2011/2012
21
2.5
Taarifa maalum kuhusu matokeo ya ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na hatma ya hisa za Serikali katika benki hiyo
252.6
Taarifa maalum ya Kamati kuhusu Hali ya kifedha na kiutendaji ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
32
2.7
Taarifa maalum kuhusu Deni la Sh. 1,875,896,246,224.48 ambalo Serikali inadaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
35
2.8
Taarifa maalum kuhusu Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL)
36
2.9
Hoja za Ukaguzi kuhusu dosari katika umiliki wa Nyumba za Mashirika ya Umma
38
2.10
Taarifa maalum kuhusu gharama halisi zinazotumika katika kutangaza Hotuba za  bajeti kwenye magazeti baada ya kusomwa bungeni
40

2.11
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Tathmini ya zoezi la Ubinafsishaji
41
SEHEMU YA TATU

4.0
Mapendekezo ya Kamati
42
SEHEMU YA NNE

5.0
Hitimisho
53SEHEMU YA KWANZA
________________

1.0      UTANGULIZI
1.1  Miongozo ya Uwasilishwaji wa Taarifa
        Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kukushukuru kwa kunipa fursa ya kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, pamoja na mambo mengine, maoni na mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma. Maoni na Mapendekezo yanatokana na uchambuzi wa kina wa Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013, Taarifa za Kaguzi Maalum mbalimbali zilizofanywa na CAG na Taarifa ya Msajili wa Hazina (The Treasury Notes) kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2012 pamoja na Ziara za ukaguzi wa ufanisi katika baadhi ya miradi inayotekelezwa na Serikali Kuu pamoja na Mashirika ya Umma.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)   inaanza kufanya kazi zake baada ya Kupokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kama inavyoeleweka aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ndugu. Ludovick Utouh amestaafu Utumishi wa Umma hivi karibuni. Kamati inampongeza kwa dhati kwa kazi kubwa na nzuri aliyofanya ya kuimarisha usimamizi na uwajibikaji wa fedha za Umma, ni ukweli ulio wazi kuwa Ndugu Utouh ameandika historia kubwa katika dhana nzima ya usimamizi wa fedha za Umma katika Nchi, hii kwa Niaba ya Kamati, tunampongeza na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe maisha marefu na yenye baraka kwa kazi iliyotukuka kwa Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, Kamati inampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumteua Profesa Mussa Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Kamati inamaamini kuwa Profesa Mussa Assad akiwa ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya fedha atafanya kazi zake kwa weledi na uadilifu mkubwa. Tangu ateuliwe, Kamati imepata ushirikiano mkubwa wa Profesa Assad na Ofisi nzima ya Taifa ya Ukaguzi, Kamati itaendeleza ushirikiano huo kwa manufaa ya usimamizi imara wa fedha za Umma katika Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, Kwa namna ya pekee, Kamati inapenda kumpongeza Ndugu Lawrence Mafuru ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Msajili wa Hazina nafasi ambayo tangu mwaka 2009 imekuwa ikikaimiwa na watendaji mbalimbali wa Serikali, hali ambayo ilikwamisha ufanisi wa Ofisi hiyo muhimu kwa Taifa. Ni imani ya Kamati kuwa Ndugu Lawrence Mafuru atatumia uzoefu wake alioupata kwenye sekta binafsi kuchochea fursa za mabadiliko ya kimaendeleo katika Mashirika ya umma na uwekezaji wa umma (Public Investment).
1.2  Majukumu ya kikanuni ya Kamati
        Mheshimiwa Spika, Kamati hii kwa kuzingatia Nyongeza ya Nane chini ya Kanuni ya 115 (2) fasili Ndogo ya 11 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2007, ina majukumu ya kikanuni yafuatayo;
a)  Kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Wizara za Serikali na Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
b) Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyokwishatolewa na Kamati yenye lengo la kuondoa matatizo hayo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Wizara za Serikali na Mashirika ya Umma; na
c)  Kutoa mapendekezo na ushauri kwa Wizara za Serikali na Mashirika ya Umma kuhusu matumizi mazuri ya fedha za umma.
d) Kutathmini ufanisi wa Mashirika ya Umma;
e)  Kufuatilia utekelezwaji wa Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.
1.3  Miongozo iliyotumika katika utekelezaji wa shughuli za Kamati
        Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma imetumia nyenzo zifuatazo:-
a)  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake;
b) Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Mwaka 2007 na maboresho yaliyofanyika kwenye Nyongeza ya Nane;
c)   Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2012;
d)  Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Mashirika ya Umma kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2012;
e) Taarifa za Kaguzi Maalum mbalimbali zilizofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
f)   Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004, Sheria ya Fedha za Umma ya Mwaka 2001 na Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008;
g)  Taarifa za Mhasibu Mkuu wa Serikali kuhusu mapato na matumizi ya kila Fungu pamoja na Taarifa ya Mhakiki Mali wa Serikali kuhusu usimamizi wa mali za Serikali;
h) Taarifa za Msajili wa Hazina kama Mwenye hisa Mkuu katika Mashirika yote ambapo Serikali imewekeza;
i) Taarifa za Hesabu zilizokaguliwa za kila Fungu na Shirika kwa Mwaka wa Fedha unaojadiliwa ikiambatanishwa na majibu ya hoja za Ukaguzi kutoka katika Manejimenti ya kila Fungu na Shirika husika;
j) Taarifa za kitafiti kutoka maeneo mbalimbali juu ya mambo yanayogusa majukumu ya Kamati na;
k) Ziara za Ukaguzi wa Ufanisi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali Kuu pamoja na mashirika ya Umma.
1.4  Mheshimiwa Spika, Taarifa hii ina Sehemu Nne yaani, Sehemu ya Kwanza ni utangulizi, Sehemu ya Pili ni Uchambuzi wa Taarifa za Ukaguzi Maalum mbalimbali na Taarifa za Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013, Sehemu ya Tatu ni Maoni na Mapendekezo ya Kamati, Sehemu ya Nne ni Hitimisho.
  
SEHEMU YA PILI
______________

2.0    UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA KAGUZI MAALUM MBALIMBALI NA TAARIFA ZA HESABU ZILIZOKAGULIWA ZA SERIKALI KUU NA MASHIRKA YA UMMA KWA MWAKA WA FEDHA UNAOISHIA JUNI 30, 2013
2.1    TAARIFA YA AWALI KUHUSU UKAGUZI MAALUM WA MISAMAHA YA KODI;
2.1.1 Mheshimiwa Spika, Misamaha ya kodi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilikuwa ni asilimia tatu (3%) ya Pato la Taifa (GDP). Kwa miaka mitatu ya nyuma 2010/2011 hadi 2012/2013 misamaha ya kodi ilikuwa na wastani wa asilimia 3.33 ya Pato la Taifa. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 mapato yaliyopotea (lost revenue) kutokana na misamaha ya kodi yalikuwa asilimia 4.3 ya pato la Taifa kiasi ambacho ndio cha kiwango cha juu kabisa katika miaka 5 iliyopita. Aidha, kwa nchi ya Kenya misamaha ya kodi ni asilimia 1 ya pato la Taifa. Hadi kufikia Juni 30, 2013 misamaha ya kodi iliyokuwa imetolewa ilikuwa na thamani ya Sh. 1.5 trilioni. Hata hivyo, kufikia mwezi Juni 2014, misamaha hii iliongezeka kwa takribani asilimia 22.6 mpaka kufikia Sh. 1.8 trilioni.
2.1.2 Mheshimiwa Spika, Ukubwa wa mapato yanayopotea kutokana na misamaha ya kodi mwaka hadi mwaka uliipa mashaka Kamati kama Sheria zinazosimamia utoaji na matumizi ya misamaha ya kodi zinafuatwa, kiwango cha mapato tunayoacha au kusamehe ni sahihi na malengo yaliyokusudiwa yanatimia. Kwa lengo la kuthibitisha hayo na kuishauri Serikali juu ya namna bora ya kusimamia matumizi ya misamaha ya kodi kwa manufaa ya nchi, Kamati ilikubaliana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuanza utaratibu wa kufanya Ukaguzi Maalum wa Misamaha ya Kodi kila mwaka kuanzia mwaka wa fedha wa 2012/2013.
2.1.3 Mheshimiwa Spika, Katika kikao chake cha tarehe 2/4/2013 Kamati pia iliagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ianishe Sheria zote zinazosababisha uvujaji wa mapato ya Serikali kutokana na misamaha ya kodi na kupeleka mapendekezo Serikalini ili Bunge liweze kufanyia marekebisho. Aidha, Mamlaka ya Mapato bado haijakamilisha mchakato wa marekebisho ya Sheria husika.
2.1.4 Mheshimiwa Spika, Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alianza kufanya Ukaguzi maalum wa Misamaha ya Kodi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013 mnamo mwezi Februari, 2014 na kuwasilisha kwenye Kamati Ripoti ya Matokeo ya Awali ya Ukaguzi huo tarehe 23 Januari, 2015 kupitia barua Na. FA.249/309/01/55. Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, ukaguzi huo unaotarajiwa kukamilika hivi karibuni ulihusisha misamaha ya kodi iliyotolewa kwa Makampuni ya Madini, Taasisi za Kijeshi, Maduka yanayouza bidhaa zilizosamehewa kodi katika viwanja vya ndege (Aiport Duty Free Shops), Wawekezaji wenye Vyeti vya kupatiwa motisha kutoka TIC, Wawekezaji kwenye EPZ (Export Processing Zones), Misheni za kidiplomasia na Umoja wa Mataifa, Watumishi wa Serikali, Mashirika ya Dini na Mashirika ya hisani ya Jamii.
2.1.5 Mheshimiwa Spika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, katika Ripoti ya awali aliyoiwasilisha kwa Kamati amebaini yafuatayo;
a)      Ukiukwaji wa maelekezo ya Serikali uliosababisha hasara ya Sh. 22,325,178,728 kufuatia kuhamishwa kwa mafuta yenye msamaha wa kodi kutoka kwa Makampuni ya Madini kwenda kwa Wakandarasi mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ripoti hiyo, M/S Geita Gold Mines na Resolute Tanzania Limited walihamisha mafuta yaliyosamehewa kodi yenye thamani ya Sh.22,325,178,728 kwenda kwa Wakandarasi mbalimbali (M/S Geita Gold Mines - Sh. 22,305,069,488 na Resolute Tanzania Limited - Sh. 20,109,240). Uhamishaji huo ulikuwa ni kinyume na Tangazo la Serikali Na. 480 la tarehe 25 Oktoba 2002 lililoelekeza kusitisha msamaha wa kodi pale ambapo mafuta yaliyosamehewa kodi yatatumika kwa matumizi tofauti na yaliyokusudiwa au yatahamishiwa, kuuzwa au kupewa mtu mwingine ambaye hana haki ya kupewa msamaha huo.
b)      Matumizi ya misamaha ya kodi kwa malengo tofauti na yaliyokusudiwa na kusababisha upotevu wa mapato ya Sh. 392,701,602.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 na 2012/2013 Kampuni ya Kiliwarrior Expeditions Ltd ya Arusha iliyokuwa na cheti (Na.030863) cha kupatiwa motisha kutoka TIC iliagiza magari 28 na kusamehewa kodi yenye thamani ya Sh. 465,235,220.10. Ukaguzi maalum umebaini kuwa Kampuni hiyo inamiliki magari mawili tu ambapo moja lina namba za usajili T 721 AFM lililonunuliwa tarehe 10/01/2005 na na lingine lina namba za usajili T 461 AUU lililonunuliwa tarehe 30/04/2008 . Aidha, magari hayo si kati ya yale magari 28 yaliyoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi.
Mheshimiwa Spika, Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato (Arusha) ilikiri kuwa baadhi ya magari hayo yalisajiliwa na TRA na yanatumiwa na watu binafsi ambao hawakuwa na haki ya kupewa msamaha wa kodi. Pamoja na TRA kufanikiwa kuwakamata wamiliki wa magari 5 kati ya 28 na kurejesha kodi iliyosamehewa kimakosa ya Sh. 72,533,618, Kamati ilishangazwa na kitendo cha TRA kutositisha usajili wa magari hayo ilhali ikijua kabisa wamiliki hao wapya hawastahili kupewa msamaha wa kodi. Kamati inashawishika kuamini kuwa baadhi ya Maafisa wa TRA walikula njama na wamiliki hao wapya wa magari kwa maslahi binafsi katika kusajili magari hayo au kuna udhaifu mkubwa katika mifumo ya udhibiti matumizi mabaya ya misamaha ya kodi.
c)       Misamaha ya kodi iliyotolewa kwa Kampuni isiyostahili yenye thamani ya Sh.53,399,565.
Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Kilemakyaro Mountain Lodge Limited ilipewa msamaha wa kodi kwa ajili ya mradi wa ujenzi na upanuzi wa hoteli kadhaa katika kiwanja No. 2531 kilichopo katika kijiji cha Changarawe wilayani Karatu, Arusha. Ukaguzi Maalum umebaini kuwa Kampuni hiyo iliagiza magari 3 kwa kutumia msamaha huo wa kodi na magari hayo yalipata msamaha wa kodi wenye thamani ya Sh.72,641,972.80 (BMW X5 - Sh.39,145,405.60; Toyota Land Cruiser Prado - Sh.14,254,160.40; na Hyundai Santa -Sh.19,242,406.80).
Mheshimiwa Spika, Wakaguzi walipoenda kukagua mradi huo, hawakukuta gari hata moja ingawa Menejimenti ya Kampuni iliweza kuthibitisha ununuzi wa gari moja tu (Hyundai Santa mpya) na hawakuwa na taarifa ya ununuzi wa hayo magari mengine. Kwa maana hiyo, Serikali ilipoteza mapato ya Sh.53,399,569 kwa kusamehe kodi ya uagizaji wa BMW X5 na Toyota Land Cruiser Prado kwa pamoja.
Mheshimiwa Spika, mapungufu ya aina hii yanaashiria kuwepo dalili za nyaraka kugushiwa katika kuwezesha msamaha wa kodi kutolewa kwa mtu au Kampuni isiyostahili.
d)      Utoaji wa misamaha ya kodi isiyo na ukomo kwa ajili utekelezaji wa miradi ya ukarabati na upanuzi wa makampuni mbalimbali ulioikosesha Serikali mapato ya Sh. 63,213,537,216.70 katika mwaka wa ukaguzi.
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi umebaini kuwa misamaha ya kodi iliyotolewa kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa uwekezaji uliokwishafanyika imeongezeka kutoka Sh. 34,205,432,788.50 kwa mwaka 2011/2012 hadi Sh. 63,213,537,216.70 kwa mwaka 2012/2013 ambalo ni ongezeko la asilimia 84.81. Kukosekana kwa ukomo wa muda, kiasi na aina ya vifaa vinavyopewa msamaha wa kodi kumetengeneza mianya kwa baadhi ya wawekezaji kufaidika na misamaha ya kodi isiyo na ukomo kwa kuwa ukarabati na upanuzi endelevu wa miradi ya makampuni. Kamati inaona si sahihi kuendelea kutoa misamaha ya kodi kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa miradi ambayo ilifaidika na misamaha hiyo wakati inaanzishwa na kuiendelea kuikosesha Serikali mapato kwa muda mrefu.
e)      Misamaha ya kodi ya Sh. 13,081,104,878 iliyotolewa kwa kuzingatia maombi yasiyo na nyaraka za kutosha.
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi umebani uwepo wa misamaha ya kodi ya Sh.13,081,104,878 iliyotolewa kwa wawekezaji mbalimbali bila kuwepo kwa nyaraka zinazohitajika. Nyaraka zilizokosekana ni pamoja na kibali za msamaha wa kodi kutoka Hazina, kibali kutoka Wizara mama, Taarifa ya matumizi yanayoendelea ya misamaha ya kodi kibali cha ujenzi, Taarifa za ukaguzi wa kushitukiza. Hii ni kinyume na taratibu za uandaaji na usimamizi wa matumizi ya misamaha ya kodi ambazo zinaitaka Mamlaka ya Mapato kuhakikisha maombi yote ya misamaha ya kodi hayashughulikiwa mpaka zinapowasilisha nyaraka zinazohitaji kisheria.
f)            Kufungwa kwa duka la bidhaa zilizosamehewa kodi bila kuwasilisha TRA Hesabu za matumizi ya misamaha ya kodi kulikoisababishia Serikali hasara ya Sh.3, 824,547,526.
Mheshimiwa Spika, Kampuni ya M/s Conti- Africa Ltd katika miaka ya 2011/2012 na 2012/2013 ilipewa msamaha wa kodi wenye thamani ya Sh.3, 824,547,526 kwa ajili ya bidhaa zitakazouzwa kwenye duka la Jeshi huko Arusha. Hata hivyo, Wakaguzi walipoenda Arusha hawakulikuta duka hilo na Menejimenti ya TRA (Arusha) iliwathibitishia Wakaguzi kuwa Kampuni hiyo ilifunga biashara hiyo muda mrefu.
Mheshimiwa Spika, Kamati haikufurahishwa na kitendo cha Kampuni hiyo kufunga biashara bila kuwasilisha TRA hesabu za misamaha ya kodi na TRA kutofuatilia kama msamaha wa kodi uliotolewa unatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Ni wazi kwamba, TRA kutofanya ufuatiliaji kunatoa fursa ka bidhaa zilizosamehewa kodi kupelekwa kwenye maduka yasiyo ya kijeshi na kuikosesha mapato Serikali.


2.2    MATOKEO YA UKAGUZI MAALUM WA FEDHA ZA USHURU WA MAUZO NJE YA NCHI NA RUZUKU YA SERIKALI KWA ZAO LA KOROSHO KATIKA MKOA WA MTWARA KATIKA KIPINDI CHA 2006/07 HADI 2010/11
         Mheshimiwa Spika, iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mtwara mnamo mwezi Mei 2011 ziliomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi maalum kwa lengo la kuthibitisha yafuatayo:-
a)       Ni sababu gani fedha za ruzuku, pamoja na ushuru wa korosho ghafi hazipelekwi kwenye Halmashauri zinazolima zao hilo ili Halmashauri hizo ziweze kupanga matumizi ya fedha hizo kama ilivyo kwa fedha zingine za Halmashauri hizo.
b)      Kwa kiwango gani Wakurugenzi wa Halmashauri wanaruhusiwa katika kuidhinisha malipo ya fedha za ruzuku pamoja na ushuru wa mauzo ya korosho ghafi.
c)       Ni kwa kiwango gani maafisa wa ngazi za Mkoa na Bodi ya Korosho wamezingatia taratibu za udhibiti wa fedha za ruzuku na ushuru wa mauzo ya korosho ghafi ili zitumike kwa mujibu wa malengo yaliyokusudiwa.
d)      Ni kwa idhini ya nani Halmashauri ziliruhusiwa kutumia fedha zaidi ya magao wake.
2.2.1 Mheshimiwa Spika, katika kuthibitisha sababu za ruzuku pamoja na ushuru wa korosho ghafi kutopelekwa kwenye Halmashauri zinazolima zao hilo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amebaini kuwa Sheria Na.21 ya 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2006 iliyokuwa ikielekeza kuwa fedha za makusanyo ya ushuru wa usafirishaji korosho ghafi nje ya nchi kupelekwa Halmashauri zinazolima korosho ilifutwa na Bunge na kutungwa Sheria mpya Na.18 ya mwaka 2009. Aidha, Sheria Na.18 ya mwaka 2009 ilifanyiwa marekebisho na Sheria ya fedha ya mwaka 2010 kwa kuingizwa kifungu Na.17A kinachotoza ‘Export Levy’ na kuelekeza asilimia 65 (65%) ya ‘Export Levy’ hiyo ipelekwe kwenye Mfuko wa kuendeleza zao la Korosho na asilimia 35 (35%) ibakie Hazina kwenye Mfuko mkuu wa Serikali.
         Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo maboresho ya Sheria yaliyofanywa na Bunge yanaelekeza fedha hizo kufikia walengwa kupitia Mfuko wa kuendeleza zao la Korosho na sio kupitia Halmashauri zenye wakulima wa zao la korosho.
2.2.2 Mheshimiwa Spika, kimsingi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amethibitisha ushiriki wa Watendaji Wakuu wa Halmashauri katika kuidhinisha malipo ya fedha za ruzuku na ushuru wa korosho ghafi ingawa ukaguzi wake ulibaini mapungufu yafuatayo;
a)      Hasara ya Shs.223,815,000 inayotokana na malipo kwa pembejeo ambazo hazikupokelewa
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi umebaini kuwa Kampuni za Mukpar Tanzania Ltd na Equatorial Africa Ltd zililipwa na Bodi ya Korosho Shs.223,815,000 zaidi ya fedha ambazo walipaswa kulipwa kama utaratibu wa ulipaji wa asilimia 50 ungefuatwa katika msimu wa 2009/10. Kimsingi utaratibu huu unaelekeza kuwa Bodi ya Korosho humlipa Mzabuni asilimia 50 ya bei ya pembejeo baada ya kupata nyaraka zinazothibitisha kuwa Vyama vya Msingi vimelipa asilimia 50 ya bei ya pembejeo.
Mheshimiwa Spika, ukaguzi umebaini utaratibu huo haukufuatwa na kilichofanyika ni Mfuko wa Pembejeo wa Wilaya ya Masasi kupita Katibu wa Mfuko huo (Afisa Kilimo wa Wialaya ya Masasi) kutoa vibali vya kugushi vya malipo kwa Bodi ya Korosho kwa kigezo kuwa Mfuko umepokea pembejeo zote kutoka kwa Mukpar Tanzania Ltd na Vyama vya msingi vimeshalipa asilimia 50 ya bei ya pembejeo. Hivyo, kusababisha Bodi ya Korosho kuilipa kimakosa Mukpar Shs. 292,375,000 pamoja na usafiri Shs.2,880,000 (lita 24000*Shs120).
Mheshimiwa Spika, Kamati ilipomuhoji Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho alithibitisha kutopokelewa kwa pembejeo hizo mpaka sasa na hakuna juhudu zozote zilizofanyika kuokoa fedha hizo. Aidha, mpaka sasa si Mukpar (T) Ltd wala Afisa Kilimo wa Wilaya ambaye amechukuliwa hatua za kinidhamu au za kisheria.
b)      Malipo ya pembejeo pasipo viambatanisho Shs. 184,564,500
Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Pembejeo wa Wilaya ya Tandahimba (MPEWATA) unadaiwa kiasi cha Shs. 184,564,500 na makampuni ya Bytrade Tanzania (Shs. 154,564,500) na Mega Generics Limited (Shs. 30,000,000). Kampuni hizo zililipwa kiasi cha Shs. 262,132,500 (asilimia 50 ya Shs. 524,265,000) na Bodi ya Korosho kinyume cha utaratibu unaoelekeza Bodi kulipa asilimia 50 ya bei ya pembejeo baada ya kupata nyaraka zinazothibitisha kuwa Vyama vya Msingi vimelipa asilimia 50 ya bei ya pembejeo.  Malipo ya Shs. 262,132,500 yalifanywa bila uthibitisho wa malipo ya Vyama vya Msingi kufanyika, hadi wakati wa Kamati inahoji Menejimenti ya Bodi ya Korosho pembejeo zenye thamani ya Sh.154, 564,500 zilizolipiwa ruzuku zilikuwa hazijapelekwa kwa wakulima na hazijulikani zilipo na hakuna hatua za kisheria wala za kinidhamu zilizochukuliwa kwa waliohusika. 
2.2.3 Mheshimiwa Spika, katika kukagua hali ya udhibiti wa fedha za ruzuku na ushuru wa mauzo ya korosho ghafi ili zitumike kwa mujibu wa malengo yaliyokusudiwa, Ukaguzi umebaini yafuatayo:-
a)      Matumizi ya fedha za ruzuku na ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kuendeshea shughuli za ofisi Shs. 1,075,046,004
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi umebaini kuwa kiasi cha Shs.1,075,046,004 kilitumiwa na Bodi ya Korosho kulipia matumizi mbalimbali ya Ofisi ikiwemo mishahara, gharama za matengenezo, bili za umeme n.k. ikiwa ni kinyume na maelekezo ya sheria inayotaka fedha hizo zitumike kwa ajili ya kuendeleza zao la korosho. Fedha hizo ni nje ya fedha za usimamizi.  Aidha, Kamati ilipoihoji Menejimenti ya Bodi ya Korosho ilishindwa kuthibitisha kuwa fedha hizo ni mgao wao na haikuweza kuwasilisha kibali cha kutumia fedha hizo.
Jedwali 1: Mchanganuo wa fedha zilizotumika kulipia madai mbalimbali ya Ofisi
Mwaka
Jumla ya Matumizi
Fedha za Usimamizi
Ziada ya fedha iliyotumika
2006/07
2007/08
2008/09
2009/10
2010/11
382,676,430
115,496,912
365,365,153
315,845,456
285,662,053
50,000,000
100,000,000
80,000,000
80,000,000
80,000,000
332,676,430
15,496,912
285,365,153
235,845,456
205,662,053

1,465,046,004
390,000,000
1,075,046,004

b)   Kukosekana kwa uthibitisho wa matumizi ya marejesho ya mikopo ya Ruzuku Shs. 345,958,266 katika Bodi ya Korosho
Mheshimiwa Spika, Katika msimu wa mwaka 2006/2007, kiasi cha Shs.345, 958,266 kilirejeshwa Bodi ya Korosho kutoka Halmashauri za Wilaya mbalimbali kwa ajili ya kuanzisha Mfuko (Revolving Fund). Aidha, mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo haukupatikana wakati wa ukaguzi maalum. Hata, Kamati ilipohoji Menejimenti ya Bodi ya Korosho haikuweza kuthibitisha matumizi ya fedha hizo.Jedwali 2: Marejesho ya Mikopo ya ruzuku kwa Wilaya za Mtwara
Halmashauri
Deni (Mgao) Shs
Marejesho Shs.
Bakaa Shs.
Mtwara (M)
55,275,380
25,372,940
29,902,440
Mtwara (V)
139,891490
40,433,736
99,457,754
Tandahimba
380,125,059
162,151,590
217,973,469
Newala
183,807,909
100,000,000
83,807,909
Masasi
349,620,950
18,000,000
331,620,950
JUMLA
1,108,788
345,958,266
762,762,522

c)    Deni la Pembejeo Shs.762,762,522
Mheshimiwa Spika, Halmashauri za Manispaa ya Mtwara, Wilaya ya Mtwara, Tandahimba, Newala na Masasi zilipelekewa pembejeo zenye thamani ya Sh.1,108,720,788 ambapo fedha hizo zilitakiwa kurudishwa Bodi ya Korosho kwa ajili ya kuanzisha Mfuko Endelevu wa Pembejeo (Revolving Fund). Halmashauri zilizotajwa hapo juu zilikiri kupokea pembejeo hizo na kuzikopesha kwa Vyama vya Msingi/wadau mbalimbali wa zao la Korosho. Ukaguzi ulibaini kuwa Halmashauri zote za Wilaya zimegoma kurejesha fedha hizo Bodi ya Korosho kwa maelezo kwamba ni fedha halali za Halmashauri hizo kwa mujibu wa sheria Na.9 ya mwaka 1982.
Mheshimiwa Spika, mpaka ukaguzi huu maalum unakamilika, kiasi cha Shs.762,762,522 kilikuwa hakijakusanywa kutoka kwa Vyama vya Msingi/wadau mbalimbali waliokopeshwa pembejeo kama jedwali hapa chini linavyoonyesha:
Jedwali 3: Marejesho ya Mikopo ya Pembejeo kwa Halmashauri za Mtwara
HALMASHAURI
DENI (MGAO)
MAREJESHO
BAKAA
MTWARA (M)
55,275,380
25,372,940
29,902,440
MTWARA (V)
139,891,490
40,433,736
99,457,754
TANDAHIMBA
380,125,059
162,151,590
217,973,469
NEWALA
183,807,909
100,000,000
83,807,909
MASASI
349,620,950
18,000,000
331,620,950
JUMLA
1,108,720,788
345,958,266
762,762,522

d)   Ruzuku kulipia Pembejeo ambazo hazikuombwa na wakulima
Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka 2011/2012, Wakulima wa Halmashauri ya Newala walipeleka mahitaji yao ya pembejeo (dawa aina ya Sulphur ya unga) kwa ajili ya zao la korosho. Badala yake, Halmashauri ilipelekewa pembejeo aina ya Falcon (Sulphur ya maji) ambayo ndiyo ilikuwa kwenye ruzuku na hivyo kusababisha migogoro na wakulima ambao waligoma kutumia pembejeo aina ya Falcon na hivyo kulazimika kujinunulia pembejeo aina ya Sulphur kutoka kampuni ya Abbasi Tanzania LTD ambayo haikuwa kwenye mfumo wa ruzuku.
Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, Ukaguzi maalum umebaini kuwa dawa zote zinafanya kazi moja na kuwa Sulphur ya unga ina madhara kwenye udongo.  Hivyo, ni wazi kuwa elimu ya kutosha haitolewi kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya baadhi ya pembejeo na hivyo kufanya wakulima waone wanahujumiwa kwa kutopelekewa aina za pembejeo walizoomba. Hata hivyo, Kamati haikuweza kupata taarifa ya matokeo ya utafiti uliofanywa kuthibitisha kutofaa kwa matumizi ya dawa aina ya sulphur ya unga.

e)    Kutozingatiwa kwa mapendekezo ya wakulima
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi huu maalum umebaini kuwa Bodi ya Korosho imekuwa haizingatii maelekezo ya wakulima na hivyo kuamua kuwapelekea pembejeo wanazoona wao zinafaa.  Hali hii imekuwa ikisababisha migogoro isiyokuwa ya lazima baina ya wakulima na Bodi ya Korosho kupitia Vyama vyao vya Msingi.
f)     Kukosekana kwa Taarifa na nyaraka mbalimbali
Mheshimiwa Spika, Bodi ya Korosho ilitoa maelekezo kwa wadau wa zao la korosho katika ngazi mbalimbali kuhusu namna ya kutunza na kuandaa taarifa ya matumizi ya fedha za pembejeo ikionyesha orodha ya wakulima walionufaika na pembejeo za ruzuku. Pamoja na kuwepo kwa maelekezo hayo, Halmashauri za Wilaya ya Tandahimba, Nanyumbu, Masasi, Mtwara (M) na Mtwara (V) hazijawahi kuandaa Taarifa hizo na hakuna barua yoyote kutoka Bodi ya Korosho ya kuwataka wadau wa zao la korosho kuandaa na kuwasilisha taarifa hizo. Hali hii inaleta wasiwasi kama Bodi ya Korosho inafanya kazi ya usimamizi kama inavyotakiwa ili kuhakikisha wakulima wananufaika na pembejeo za ruzuku.
2.3    UKAGUZI MAALUM WA UJENZI WA JENGO LA KUMBI ZA WATU MASHUHURI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM (JNIA) KATIKA KIPINDI CHA 2006 HADI 2012
         Mheshimiwa Spika, Baada ya uchambuzi wa kina wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi Maalum wa Ujenzi wa jengo la kumbi za watu mashuhuri katika Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, ilibainika kuwa mnamo mwaka 2007, Serikali ya Tanzania kupitia iliyokuwa Wizara ya Miundombinu waliingia mkataba na Kampuni ya China Songangol International Limited (CSIL) ili kufanikisha Miradi kumi na moja ya uwekezaji na uendelezaji katika Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
Mheshimiwa Spika, Baada ya kusainiwa kwa [1]makubaliano (MOU) baina ya wadau hao wawili (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na China Sonangol International Limited, CSIL) ilikubaliwa kwamba awamu ya kwanza ya mradi ihusishe miradi mitatu ambayo ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la wageni wa kitaifa, makubaliano ambayo yalisainiwa tarehe 28 Februari, 2007. Baada ya Ukaguzi maalum, maeneo yafuatayo yaligundulika kuwa na dosari kutokana na ujenzi wa jengo hilo;
2.3.1 Ujenzi kuanza kufanyika bila kupata kibali cha Baraza la Mawaziri
         Mheshimiwa Spika, Katika kupitia Hati za makubaliano baina ya Wizara ya Miundombinu, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Kampuni ya CSIL, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini kuwa Wizara ya Miundombinu iliandaa rasimu ya Waraka na kuuwasilisha kwenye Baraza la Mawaziri kuomba kibali cha Serikali kuendelea na utekelezaji wa ujenzi wa jengo la wageni wa kitaifa (State Recepetion Building) kwa njia ya ubia kwa kushirikiana na CSIL.

Mheshimiwa Spika, katika ukaguzi maalum uliofanyika, ilibainika kuwa kulikuwa na mapungufu katika Waraka husika kwani haukuwa umesainiwa na Waziri wa Miundombinu, haukuwa na tarehe ikionyesha uliandaliwa lini na pia haukuwa na namba ya kuonyesha ni waraka namba ngapi na zaidi hapakuwepo na uthibitisho iwapo Waheshimiwa Mawaziri waliridhia kwa hatua zaidi za kumshauri Mheshimiwa Rais ili kuagiza ujenzi wa jengo hilo.

         Mheshimiwa Spika, Kamati itahitaji kupata maelezo ya kina ya Serikali iwapo mchakato wa kuruhusu ujenzi wa jengo hilo ulipitia taratibu zote za kupata idhini ya Baraza la Mawaziri ikizingatiwa kuwa Kampuni ya CSIL baadaye ilishindwa kutekeleza majukumu yake ya kimkataba ikiwamo uendelezaji wa eneo la Terminal three katika Uwanja wa JNIA.
2.3.2 Mkanganyiko kuhusu mchango wa Serikali katika ujenzi wa jengo hilo.   
         Mheshimiwa Spika, Dosari kubwa nyingine iliyobainika na CAG kuhusu ujenzi wa Jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa JNIA ni kuhusu kiasi cha gharama ambacho Serikali ilichangia katika ujenzi husika. Mkanganyiko wa gharama za Serikali katika ujenzi huo ulitokana na taarifa za awali kuonyesha kuwa Serikali ilichangia kiasi cha Dola za Kimarekani milioni mbili (sawa na Shilingi bilioni tatu za kitanzania).
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum baada ya kupitia na kuchambua nyaraka mbalimbali za mikataba na manunuzi ilithibitisha kuwa gharama za mchango wa Serikali katika Jengo la kumbi za watu Mashuhuri kwa kazi zilizofanyika ulikuwa ni Shilingi 869,485,164 na sio bilioni tatu (3,000,000,000). Hivyo basi, ni muhimu Serikali ikalifahamisha bunge lako tukufu utata wa gharama hizo ulitokana na jambo gani.
2.3.3   Mapungufu kuhusu gharama halisi za ujenzi wa jengo la watu Mashuhuri katika JNIA
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi uliofanyika bado unadhihirisha kwamba gharama halisi za Ujenzi wa Jengo la watu Mashuhuri katika Uwanja wa Julius Nyerere zina mkanganyiko. Katika Ukaguzi wao, Wakaguzi walishindwa kupata nyaraka wala vielelezo vyovyote vilivyomo kwenye majalada ya Ofisi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na yale ya Kiwanja cha JNIA ikiwamo Mkataba kwa ajli ya kuonyesha gharama halisi za ujenzi wa jengo hilo. Kilichopatakina kwa wakaguzi ni “Offer of Grant for VIP Lounge” yenye thamani ya RMB 27,980,000 ambazo ni sawa na Sh.5, 335,359,318.

Mheshimiwa Spika, tafsiri ya kukosekana mikataba hapo juu inaashiria kwamba Mkandarasi (M/s Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd) pamoja na Mfadhili (M/s China International Fund Limited) hawakukabidhi nyaraka za ujenzi Serikalini na hivyo kushindwa kufahamu gharama halisi iliyolipwa na Mfadhili huyo.

Mheshimiwa Spika, ili kupata thamani halisi ya ujenzi wa Jengo hilo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa barua ya tarehe 3/04/2014 yenye kumb. Na. AB/235/280/08 aliiagiza Wizara ya Uchukuzi iwasiliane na Mthamini Mkuu wa Majengo ya Serikali ili kufanya tathmini ya gharama halisi za ujenzi wa Jengo hilo. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mthamini Mkuu wa Majengo ya Serikali, hadi kufikia Mwezi Mei, 2014 gharama za Ujenzi wa Jengo hilo ilikuwa ni sawa na Sh.3,072,000,000 na mchango wa Serikali kwa shughuli zisizohusu ujenzi wa Jengo ulikuwa jumla ya Sh.869,485,164 tu.

Mheshimiwa Spika, Katika mikutano mbalimbali ya Bunge lako tukufu mwaka 2011 na 2012, Serikali ilitoa tamko kuwa Jengo la Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam lilijengwa kwa jumla ya Shilingi 12 bilioni, tofauti ya Shilingi bilioni 9 kutoka gharama iliyoainishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali.

2.3.4 Kukiukwa kwa Sheria ya Manunuzi kulikofanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA)

Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum ulibaini kuwa manunuzi ya jumla ya Sh.916, 917,145 yaliofanywa na TAA yalifanywa kinyume na kifungu namba 45 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma (Public Procurement Act) Na. 21 ya mwaka 2004. Kifungu husika kinaitaka Mamlaka ya Ununuzi kuainisha manunuzi yote yanayotarajiwa kufanywa katika mwaka husika katika Mpango wa Manunuzi wa mwaka (Annual Procurement Plan).

Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum ulithibitisha kuwa manunuzi ya jumla ya Sh.916, 917,145 hayakuwamo kwenye mpango wa manunuzi wa mwaka katika miaka iliyohusisha Ukaguzi maalum 2009 hadi 2011. Athari ya jambo kama hilo kufanyika ni kuwa manunuzi hayo yalifanywa pasipo kuwepo kwenye bajeti wala Mpango wa Manunuzi na vilevile kutokupata idhini ya Bodi ya Zabuni au ya Ushauri ya Wizara. Kwa namna nyingine, uamuzi huo usiokuwa wa kisheria ulisababisha kutotekelezwa kwa shughuli zingine za TAA zilizokuwepo kwenye mpango ili kutoa nafasi kwa manunuzi haya yasiyokuwepo kwenye mpango kufanyika.

2.3.5 Malipo yaliofanywa bila kuwepo na ushindani wa bei

Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum umebainisha kuwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ilifanya Malipo ya kiasi cha Sh.283,803,729 kwa watoa huduma mbalimbali bila kufanya ushindani wa bei ambao ungesaidia kupata bei nafuu ya huduma na vifaa ili kuokoa fedha za Umma kama inavyoelekezwa na Kanuni ya manunuzi ya Umma Na. 68 (4-5) ya mwaka 2005.

Mheshimiwa Spika, Athari inayotokana na maamuzi ya kutoshindanisha bei ili kupata huduma au vifaa ni kukosekana kwa uthibitisho wa thamani ya fedha katika manunuzi hayo. Hivyo, kutoshindanisha bei wakati wa manunuzi ya huduma na vifaa kulisababisha TAA kuwa na matumizi yasiokuwa na gharama nafuu kwa kipindi chote cha ujenzi wa jengo hilo.

2.3.6 Malipo yaliofanyika bila kufuata taratibu za Manunuzi

Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum ulipitia nyaraka mbalimbali ili kubaini iwapo mchakato wa manunuzi wakati wa ujenzi wa Jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ulifuata utaratibu. Katika Ukaguzi huu, ilibainika kuwa manunuzi yanayofikia kiasi cha Sh.737, 240,842 yaliyofanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam hayakufuta mchakato wa manunuzi.

Mheshimiwa Spika, kukiukwa kwa Sheria ya Manunuzi kunatoa taswira kuwa Watumishi wasiokuwa waaminifu walitumia mwanya huo kununua vifaa na huduma zilizo juu ya kiwango cha malipo ya kawaida kwa manufaa yao binafsi. Aidha, kukiukwa kwa Sheria hiyo kulisababisha uwepo wa matumizi mabaya ya fedha za TAA.

2.3.7 Mali, Vifaa na Samani kutothaminishwa na kuwekewa alama za utambuzi
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum umebaini kuwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) haina uthibitisho wowote wa hati za kupokelea mali, vifaa na samani husika (Delivery notes) unaonyesha kupokelewa kutoka kwa Mfadhili (China Sonangol International Limited, CSIL).
Mheshimiwa Spika, Kutokana na dosari zilizojitokeza kuhusiana na makabidhiano ya jengo na mali zilizopo, ni dhahiri kuwa kumekuwepo na mifumo dhaifu iliyosababisha kutokuwepo kwa makabidhiano rasmi ya Jengo hilo kutoka kwa Mfadhili. Uwezekano wa mali kuibwa, kuhamishwa, kuuzwa, kupotea au kubadilishwa ni mkubwa na zaidi mali hizo zitashindwa kujumuishwa katika Hesabu za mwaka za Mamlaka kinyume na utaratibu wa kimataifa wa Taarifa za Hesabu ( IFRS).
2.4    UKAGUZI MAALUM WA KUTHIBITISHA IWAPO KULIKUWA NA TIJA KATIKA MATUMIZI YA SHILINGI BILIONI 9 NA MILIONI 600 KATIKA VIKAO MBALIMBALI VYA MABARAZA YA WAFANYAKAZI, MANUNUZI NA MATANGAZO KATIKA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA) KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012
Mheshimiwa Spika, Ukaguzi maalum wa matumizi ya zaidi ya Sh. 9,600,000,000 yaliokuwa yamefanywa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) uliombwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) baada ya kuchambua na kujadili Taarifa ya Hesabu za Mamlaka kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 212.
Mheshimiwa Spika, baada ya kujadili kwa kina Taarifa husika, Kamati ilimuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya Ukaguzi maalum wa matumizi hayo ili kuona iwapo yalikuwa sahihi na kama TPA na Taifa lilipata tija kwa matumizi husika. Aidha, Ukaguzi maalum ulibaini mambo yafuatayo;
2.4.1 Matumizi ya Shilingi 684,705, 237 yalitumika bila kuwa na uhusiano na Vikao vya Wafanyakazi.
Mheshimiwa Spika, baada ya Ukaguzi maalum na baada ya CAG kupokea majibu ya hoja za ukaguzi kutoka kwa Bodi ya TPA, ilibainika kuwa kuna matumizi ya Sh.684, 705,237 yaliofanyika lakini hayakuwa na uhusiano wowote na vikao vya wafanyakazi kama ilivyokuwa imetaarifiwa na Menejimenti ya TPA.
Mheshimiwa Spika, matumizi ya fedha hizo kwa kazi isiyokusudiwa yanadhidhirisha uwepo wa mianya kwa watumishi wasiokuwa waaminifu kujipatia fedha za Umma bila ya kuzingatia Sheria na Miongozo ya matumizi ya fedha. Hadi tunapowasilisha Taarifa hii, Mamlaka ya Bandari Tanzania haijatoa uthibitisho wa namna fedha hizo zilivyotumika.
2.4.2   Kutopatikana kwa nyaraka za matumizi ya Sh. 384,199,742.40 zinazodaiwa kutumika kwa matangazo
Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia Ukaguzi maalum na mahojiano na Kamati, ilibainika kuwa TPA wamekuwa wakifanya matangazo mbalimbali kwa njia ya redio, televisheni, magazeti na vipeperushi. Hata hivyo, katika uhakiki wa matumizi husika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alishindwa kupata nyaraka za kuthibitisha matumizi ya jumla ya Sh. 384,199,742.40 ambazo TPA walidai kuwa zilitumika kwa matangazo.
Mheshimiwa Spika, kutopatikana kwa uthibitisho wa nyaraka za matumizi ya fedha hizi ni kiashiria kingine cha udhaifu katika usimamizi wa fedha za Umma uliopo katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Aidha, jambo hili pia ni kiashiria cha matumizi mabaya ya fedha za Umma na ubadhirifu.
2.4.3 Malipo ya viwango vipya vya Fedha za kujikimu TZS 62,825,725.97 (Perdiem) bila kupata kibali cha Msajili wa Hazina
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Msajili wa Hazina, na kwa kuzingatia maelekezo ya Ofisi hiyo yenye jukumu la kusimamia utendaji wa Mashirika ya Umma, Mashirika yote ya Umma yana wajibu wa kupata kibali cha Msajili wa Hazina kabla ya kuanza kulipa viwango vipya vya mishahara na posho za kujikimu.
Mheshimiwa Spika, matokeo ya Ukaguzi maalum yamebainisha kuwa Bodi ya TPA iliidhinisha na kuanza kulipa Malipo na viwango vipya vya posho ya safari ya kujikimu kwa watumishi wake bila ya kupata kibali cha Msajili wa Hazina jambo ambalo ni kinyume na Sheria. Kwa mwaka husika wa Ukaguzi, Jumla ya Sh. 62,825,725.97 zililipwa kwa Watumishi wa TPA kinyume na utaratibu na matakwa ya Sheria.
Jedwali 4: Viwango vya Posho za kujikimu kwa Watumishi wa TPA (Ndani ya Nchi)
Ngazi ya Mshahara
Kiwango cha Posho (Kabla ya Mabadiliko)
Kiwango cha Posho (Baada ya Mabadiliko)
TPSS 4
270,000
500,000
TPSS 3
270,000
400,000
TPSS 1-2
217,000
320,000
TPGS 7-8
164,000
215,000
TPGS 3-6
118,000
156,000
TPOS 4
94,000
125,000
TPGS 1-2
94,000
125,000
TPOS 1-3
94,000
125,000

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiwa imepewa Jukumu la kikanuni la kusimamia matumizi ya fedha za Umma, katika Kikao chake cha tarehe 15 Januari, 2015 ilipokutana na Bodi na Menejimenti ya TPA iliagiza fedha hizo zote zilizolipwa kwa wahusika kinyume na utaratibu na kabla ya kibali cha Msajili wa Hazina (kilichotoka Januari, 2015) zirejeshwe mara moja. Ni imani ya Kamati kuwa hii itakuwa njia bora ya kudhibiti Bodi na Menejimenti za Mashirika ya Umma zinazokiuka miongozo ya Msajili wa Hazina katika masuala ya viwango vya mishahara na posho za kujikimu.
2.4.4 Manunuzi ya dharula yenye thamani ya Tshs. 6,355,500,000, Dola za Kimarekani 810,000 na Euro 13,915
Mheshimiwa Spika,[2]kifungu 42 (a) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za mwaka 2005 G.N No.97 kinawataka Maafisa masuhuli katika Taasisi za Umma kuhakikisha kuwa wanafanya maoteo ya manunuzi ya dharula yanayoweza kutokea katika mwaka husika wa fedha katika Taasisi zao na kisha kuainisha njia za ununuzi zitakazotumiwa ili kuhakikisha kuwa tija inapatikana katika manunuzi husika.
Mheshimiwa Spika, Kamati ilishtushwa na manunuzi yenye thamani kubwa ya zaidi ya Shilingi Bilioni 8 za kitanzania kufanywa kwa njia ya dharula katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Kufuatia hoja hii ya Ukaguzi na kwa kuzingatia [3]kifungu 42(1) (c) ya GN No. 97 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPA) ya mwaka 2004, Mamlaka ya Bandari ilitakiwa kupata kibali cha Mlipaji Mkuu wa Serikali (Paymaster General) ili kuhalalisha udharula wa manunuzi yaliofanyika.
Mheshimiwa Spika, Tarehe 6 Machi, 2013 kupitia barua yenye kumbukumbu Na.PPRA/AE/106/C/20 Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma ilimwandikia Mlipaji Mkuu wa Serikali ikimshauri kuwa ni vema manunuzi haya ya dharula yaliofanywa na TPA yakafanyiwa Ukaguzi maalum kutokana na utata uliopo. Ni kwa msingi huo hadi leo hii, Mlipaji Mkuu wa Serikali hajatoa kibali cha kuruhusu idhini ya uhalali wa manunuzi husika.
Mheshimiwa Spika, katika eneo hili la manunuzi ya dharula na tena yenye thamani kubwa kama ilivyotajwa hapo juu, ni dhahiri kuwa fedha za Umma zimetumika vibaya kwa baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu kutengeneza udharula usiokuwepo ili wajipatie fedha kwa njia ya udanganyifu. Ukaguzi maalum umebainisha kuwa mambo yanayoitwa ya  [4]dharula yaliohusisha manunuzi hayo ni ya muda mrefu na ya kihistoria ikiwa ni pamoja na msongamano wa mizigo bandarini, ufanisi mdogo wa Kampuni ya TITCS na pia kutumia fedha kwa dharula wakati manunuzi husika yalipangwa katika mpango wa mwaka wa manunuzi wa Shirika.
Mheshimiwa Spika, mapungufu katika uzingatiaji wa Sheria ya manunuzi kwa mujibu wa matokeo ya Ukaguzi maalum yamejitokeza pia katika maeneo ya ujenzi wa (a) gati namba 2 na 3 katika Bandari ya Dar es Salaam (b) Ujenzi wa magati katika [5]Bandari za mwambao wa ziwa Tanganyika ambapo imebainika kuwa Mkandarasi aliyepewa kazi hana uwezo wa kutosha na hivyo takribani Sh.5, 517,986,016 zipo hatarini kupotea iwapo hatua za haraka na za makusudi hazitachukuliwa na Serikali.
2.5    TAARIFA MAALUM KUHUSU MATOKEO YA UBINAFSISHAJI WA BENKI YA TAIFA YA BIASHARA (NBC) NA HATMA YA HISA ZA SERIKALI KATIKA BENKI HIYO
Mheshimiwa Spika, Kamati ina jukumu la kuangalia na kufuatilia uwekezaji unaofanywa na Serikali katika Mashirika mbalimbali ya Umma na Taasisi za kibiashara. Kamati hufanya kazi hii kwa karibu na Ofisi ya Msajili wa Hazina ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kujadili Taarifa ya Msajili wa Hazina (The Treasury Statement) kila mwaka inayobainisha kwa kina Uwekezaji wa Serikali, Dhamana za Serikali, Mikopo ya Serikali na pia Mapato yatokanayo na Uwekezaji husika.

Mheshimiwa Spika, katika Taarifa ya Msajili wa Hazina kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2013 pamoja na Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa husika, Kamati imebaini kuwa kuna uwezekano wa Serikali kupoteza hisa inazomiliki katika NBC iwapo jitihada za haraka hazitachukuliwa. Uchambuzi ufuatao wa Kamati kwa kuzingatia Taarifa nilizozieleza hapo awali unabainisha dosari za mchakato mzima wa kuuzwa kwa NBC na hatma ya uwekezaji wa hisa za Serikali.

2.5.1 Mchakato wa kuuzwa NBC

Mheshimiwa Spika, Baada ya kukamilika kwa marekebisho ya NBC kama ilivyoelekezwa na Baraza la Mawaziri kwa kuundwa kwa NMB Bank Ltd, NBC (1997) Ltd na NBC Holding Corporation, Serikali iliamuru mchakato wa mauzo ya hisa asilimia 70 ya hisa za NBC (1997) Ltd na NMB Ltd kwa Mwekezaji mahiri uanze. Mnamo mwaka 1998 NBC (1997) Ltd iliwekwa chini ya uangalizi wa iliyokuwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma (Public Corporations Act) ya mwaka 1992. Matangazo ya awamu ya kwanza ya kukaribisha zabuni za ununuzi wa hisa asilimia 70 za NBC yalianza kutolewa kuanzia tarehe 1 Agosti mpaka 30 Novemba, 1998.  Matangazo hayo yalitolewa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Hadi kufikia tarehe ya mwisho ya wasilisho la zabuni 30 Novemba, 1998, Taasisi nne ziliwasilisha zabuni zao. Taasisi zililikuwa zifuatazo:
a)       Stanbic (T) Limited;
b)      The Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA);
c)       First Adili Bancorp/Tanzanian Consortium; na
d)      Barclays Bank Plc (UK).

Mheshimiwa Spika, Tarehe 5 Disemba, 1998, Timu ya Wataalam wa Serikali (Divestiture Technical Team) kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ilifanya tathmini ya zabuni (Evaluation of technical bids). Kimsingi, katika tathmini hiyo, zabuni ya Barclays Bank Plc iliweza kupata alama za juu kwa wasilisho la kiufundi (technical bid), ingawa kwa upande wa wasilisho la kifedha (financial bid) lilikuwa na mapungufu mbalimbali ambayo yaliwasilishwa kwenye Kikao cha Makamishina wa PSRC (PSRC Commission) kwa taarifa na hatua zaidi. Makamishina wa PSRC baada ya kupitia Taarifa ya zabuni hiyo walielekeza zabuni hiyo itangazwe upya. Awamu ya pili ya zabuni ya ununuzi wa hisa asilimia 70 za NBC ilikuwa kwa njia ya barua za mwaliko wa wasilisho la zabuni kwa wazabuni 60 waliogawanyika katika makundi matatu. Makundi hayo ni:

a)       Wazabuni 8 waliowasilisha zabuni zao kwenye zabuni ya awali ya Novemba, 1998;
b)      Wazabuni 8 ambao walinunua “Information Memorandum/Bid Document” lakini hawakuwasilisha zabuni zao kwenye zabuni ya awali ya Novemba, 1998; na
c)       Wazabuni 48 Wawekezaji mahiri ambao hapo awali waliandikiwa barua ya mwaliko na Mhe. Waziri wa Fedha kupitia barua yake ya tarehe 30 Oktoba, 1998.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 29 Januari, 1999 ilikuwa ni tarehe ya mwisho ya kuwasilisha zabuni hii kulingana na barua ya mwaliko iliyotajwa hapo juu.  Hadi tarehe ya mwisho (29 Januari, 1999) ya wasilisho la zabuni, ni Taasisi nne tu ndizo zilizowasilisha zabuni zao. Taasisi hizo ni:
a)       Stanbic (T) Limited;
b)      ABSA Group of South Africa;
c)       First Adili Bancorp/Tanzanian Consortium; na
d)      Barclays Bank Plc (UK).

2.5.2   Kuuzwa kwa NBC kwa ABSA GROUP
Mheshimiwa Spika, ABSA Group Limited walishinda zabuni ya ununuzi wa asilimia 70 ya hisa za NBC kwa bei ya shilingi za Kitanzania billioni 15.0 ambazo zilikuwa ni sawa na Dola za Marekani millioni 21.834 kulingana na “exchange rate” ya tarehe ambayo makubaliano yalifikiwa, yaani tarehe 31 Machi 1999. Mazungumzo baina ya Serikali na ABSA juu ubinafsishaji wa NBC Ltd ikiwemo matakwa ya kisheria ya Benki Kuu juu ya hali ya kifedha/dhamana ya benki, mahitaji ya uwekezaji na bei ya mauzo yalifanyika kuanzia mwezi Februari, 1999.  Pande husika zilikubaliana kwamba Serikali itoe dhamana za shilingi za  Kitanzania billioni 28.7 wakati wa kufunga mauzo (yaani tarehe 31-3-2000) pamoja na guarantee ya kulipa any shortfall ili kufikisha mtaji wa Shillingi za Kitanzania billioni 7.8.

Mheshimiwa Spika, Serikali na ABSA walikubaliana kwamba Serikali italipa sehemu ya fedha za hiyo shortfall baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa mahesabu ya kufunga mauzo. Baada ya ukaguzi kufanyika, dhamana zilizotakiwa kuongezwa ndani ya benki ili kufikia mtaji wa shilingi za Kitanzania billioni 7.8 zilikuwa ni Shilingi za Kitanzania billioni 6.094.  ABSA Group walisaini mkataba wa awali wa mauzo tarehe 22 Julai, 1999 na kulipa Dola za Marekani 2,183,400 ambazo ni sawa na asilimia kumi (10%) ya bei ya manunuzi. Kwa mujibu wa makubaliano kiasi hicho kiliwekwa kwenye akaunti maalum (ESCROW ACCOUNT) ya ABSA Group iliyofunguliwa katika benki ya Standard Chartered hapa Tanzania.  

Mheshimiwa Spika, ABSA Group Limited walisaini mkataba wa mauzo tarehe 14 Disemba, 1999 na kwa mujibu wa makubaliano yaliyomo ndani ya mkataba huo, ABSA Group walilipa shillingi za Kitanzani billioni 12 kati ya shilingi billioni 15 (sawa na Dola za Marekani 14,999,630.86 kulingana na exchange rate ya Machi 31, 2000. Malipo hayo yalifanywa kwa njia ya bankers cheque iliyowasilishwa kwa Mwenyekiti wa NBC Ltd mnamo mwezi Machi 2000 wakati wa makabidhiano ya hisa. Cheque hiyo ilikuwa cleared na fedha kuingia kwenye account ya NBC iliyopo Chasemanhattan Bank USA mnamo tarehe 4 April 2000. Kiasi hicho cha Shilingi bilioni 12.0 kililipwa moja kwa moja NBC Ltd ili kujazia mtaji wa Benki na hivyo kuiwezesha NBC kukidhi masharti ya Benki Kuu ya Tanzania ya kupata leseni.  Kwa mujibu wa Mkataba wa mauzo, ABSA Group walitakiwa kulipa shillingi za Kitanzania billioni 3 iliyobakia katika awamu tatu; shillingi bilioni 1.0 ilitakiwa kulipwa Machi 2004; shillingi billioni 1.0 ilitakiwa kulipwa Machi 2005 na shillingi  billioni 1.0 ilitakiwa kulipwa Machi 2006. Kiasi chote cha shilingi bilioni 3.0 kililipwa Wizara ya Fedha kulingana na makubaliano.

2.5.3 Jukumu la Kuongeza Mtaji katika NBC
Mheshimiwa Spika, Serikali inamiliki asilimia thelathini (30%) ya hisa katika Benki ya NBC Limited.  Tatizo la mtaji wa NBC Limited, lilianza kujitokeza kuanzia mwaka wa fedha 2010, hali ambayo ilipelekea NBC kupewa notisi na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kupewa taarifa kuwa, ifikapo tarehe 30 Juni, 2012 iwe imeongeza mtaji wake ili kutokiuka Sheria inayoihitaji benki hiyo kuwa na uwiano wa mtaji usiopungua kiwango cha asilimia 12 (Capital Adequacy Ratio). Serikali ilikubaliana na wanahisa wengine yaani ABSA GROUP na International Finance Corporation kuiomba Benki Kuu ya Tanzania kutoa ruhusa kwa NBC Limited kuendesha shughuli zake katika hali hiyo ya upungufu wa mtaji hadi tarehe 30 Septemba, 2012 ili kutoa nafasi kwa wanahisa kutafuta utatuzi wa namna ya kuongeza Mtaji wa Benki hiyo.
Mheshimiwa Spika, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa ruhusa ya nyongeza ya muda wenye vipindi vya miezi mitatu hadi tarehe 31 Disemba, 2012 na kwa mara ya mwisho iliongeza muda wa ruhusa hiyo hadi tarehe 31 Machi, 2013. Katika ruhusa ya mwisho, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na kuruhusu Mwanahisa atakayeshindwa kutoa mtaji katika benki awe tayari kupunguziwa umiliki wa hisa zake“diluted” ili kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa kuongeza mtaji ifikapo tarehe 31 Machi, 2013.
Mheshimiwa Spika, Katika Kikao cha Wanahisa kilichofanyika tarehe 25 Machi 2013; Wanahisa, kwa kauli moja, walikubaliana kuongeza Mtaji wa Benki NBC 1999 Ltd kwa kulipia hisa za ziada 570,000 kwa bei ya shilingi 131,766.00 kwa kila hisa. Ikiwa ni sawa na mtaji uliotakiwa kuongezwa katika NBC ili kufikia kiwango kinachotakiwa na Benki Kuu ya Tanzania cha Shilingi za Kitanzania bilioni 75,049,620,000. Serikali ilitakiwa kutoa shilingi za Kitanzania bilioni 22.5 ikiwa ni asilimia 30 sawa na kiwango cha hisa inazomiliki.
Mheshimiwa Spika, Sababu zilizochangia kushuka kwa mtaji wa benki ya NBC 1999 Ltd na kuathiri ufanisi wake ni pamoja na utekelezaji na usimamiaji usio thabiti wa Utoaji wa Mikopo kwenye biashara ya Usafirishaji ambao uliigharimu benki kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 55 kutokana na wateja kutolipa mikopo hiyo. Mtaji wa benki ulipungua kutokana na utekelezaji wa Sera ya Benki Mama (ABSA) inayohusu utambuzi wa faida, ya “Group Retail Impairment Policy” ambayo ilichangia kupunguza faida ya benki NBC 1999 Ltd kwa kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 30.
Mheshimiwa Spika, Benki ilipata hasara kutokana na makosa ya kiuhasibu kwa kutumia mfumo (accounting system) uliosababisha kutambua mapato hewa kwa kupitia “interest suspense account” ndani ya utunzaji wa hesabu za benki. Hali hii iliongeza hasara ya shilingi za Kitanzania bilioni 36.8 baada ya mapato hayo hewa kuondolewa.Gharama kubwa katika kukarabati na kuboresha mtandao wa mawasiliano (IT Replatforming) kulisababisha benki NBC 1999 Ltd kuingia gharama ya shilingi za Kitanzania bilioni 26 ambazo zilirekodiwa kihasibu kama ``intangible assets’’ ambazo Benki Kuu ya Tanzania haizitambui katika kukokotoa mtaji halisi wa benki[6] (TIER 1 CAPITAL RATIO).
Mheshimiwa Spika, Baada ya Wanahisa kukaa kikao cha tarehe 25 Machi 2013 walikubaliana kuongeza mtaji kwa kununua hisa za ziada kabla ya tarehe 31 Machi 2013; IFC (ambao wanamiliki asilimia 15 ya hisa katika NBC) pamoja na ABSA (wanaomiliki asilimia 55 ya hisa katika NBC) waliahidi kulipia hisa zao za ziada ifikapo tarehe 28 Machi 2013. Kwa kuwa Serikali kwa wakati huo haikuwa imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 22.5 katika Bajeti yake kwa ajili ya kuongeza mtaji katika NBC; Serikali ilikubaliana na Barclays/ABSA kuwa ABSA wailipie Serikali kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 22.5 katika benki ya NBC 1999 Limited kama mkopo kwa Serikali.
Mheshimiwa Spika, Wakaguzi waliomba makubaliano hayo yaani “Memorundum of Understanding (MoU)” ya Serikali kukopeshwa kiasi hicho cha fedha na “call option agreement” lakini hayakuweza kupatikana kutoka kwa Msajiri wa Hazina. Hata hivyo Serikali itaendelea kumiliki asilimia 30 ya hisa katika NBC kabla ya tarehe 31 Machi 2015 kama itaweza kurudisha mkopo wa Barclays/ABSA (kwa maana nyingine kutekeleza ununuzi wa haki zake ambazo zilinunuliwa na Barclays/ABSA kwa kiingereza “to exercise her call option”). Serikali inalazimika kutekeleza ahadi hii kabla ya tarehe 31 Machi 2015 vinginevyo hisa za Serikali katika NBC zitapunguzwa (diluted).
Mheshimiwa Spika, Pia, wakaguzi walifanya kikao na maafisa kutoka kwa Msajili wa Hazina, Benki Kuu ya Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kujua ni lini Serikali italipa kiasi hicho lakini waliambiwa kuwa barua ya utekelezaji wa ahadi ya Serikali bado inapitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
2.6    TAARIFA MAALUM YA KAMATI KUHUSU HALI YA KIFEDHA NA KIUTENDAJI YA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA (TTCL)
2.6.1 Mheshimiwa Spika, tarehe 21 Januari 2015, Kamati ilifanya kikao cha mashauriano kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Msajili wa Hazina, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Menejiment ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Lengo la kikao hicho likiwa ni kutafuta namna bora ya kuikwamua TTCL kutoka katika hali mbaya ya kifedha na kiutendaji ili iweze kuhimili ushindani uliopo katika sekta ya mawasiliano nchini.
Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuelezea hali ya TTCL naomba nilikumbushe Bunge lako Tukufu kuwa TTCL ilianzishwa kwa Sheria ya Kampuni ya Simu Tanzania Na. 20 ya mwaka 1993 na kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni Na. 212, tarehe 31 Desemba 1993 baada ya kuvunjwa kwa lililokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania mwaka 1993. Hadi hivi sasa Hisa za TTCL zinamilikiwa na Serikali na Bharti Airtel Tanzania B.V kwa uwiano wa asilimia 65 na asilimia 35 sawia na hivi sasa kuna mazungumzo kati ya Serikali na Bharti Airtel juu ya Serikali kununua hisa asilimia 35 za Bharti Airtel ili imiliki asilimia 100 za TTCL.
2.6.2 Hali ya TTCL
a)       Mapato na matumizi ya Kampuni kwa mwaka 2013
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa, TTCL ilipata hasara ya Sh. 20.883 bilioni kwa mwaka 2012 na hasara ya Sh. 16.258 bilioni kwa mwaka 2013.
Jedwali 5: Mapato na matumizi ya TTCL

2013
Sh.
2012
Sh.
2013/2012
Variance
2013/2012
Variance
Revenue
93.613bn
92.443bn
1.170bn
1%
Direct Costs
(29.064bn)
(37.917bn)
(8.853bn)
-23%
Gross Profit
64.549bn
54.526bn
10.023bn
18%
Operating Costs – Cash related
(79.180bn)
(73.686bn)
5.494bn
7%
Profit/(Loss) After Tax
(16.258)
(20.883bn)
4.625bn
22%

b)      Majumuisho ya Hasara (Accummulated Losses)
Mheshimiwa Spika, kutokana na TTCL kupata hasara kwa muda mrefu, takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na jumuisho kubwa la hasara ambayo kwa mwaka 2013 imefikia jumla la Sh. 334.48 bilioni. Ukubwa wa hasara hii umeiondolea TTCL mvuto wa kukopeshwa na Taasisi za Fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.
c)       Hali ya kifedha
Mheshimiwa Spika, ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Aidha, tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali.
Mheshimiwa Spika, kukosekana kwa fedha za kutosha kuendesha Kampuni kumesababisha TTCL kushindwa kuboresha au kukarabati miundombinu inayoendelea kuchakaa. Hivi sasa karibu asilimia 50 ya miundombinu ya TTCL ni michakavu (obsolete) na inahitaji kubadilishwa na mitambo ya kisasa.
d)      Mizania Hasi (Deficit Shareholders Equity)
Mheshimiwa Spika, wingi wa hasara ikijumuishwa na uhaba wa uwekezaji umepelekea TTCL kuwa na mtaji hasi wa wanahisa (Negative shareholders Equity) ambapo mpaka kufikia mwaka 2013 TTCL imekuwa na mtaji hasi wa jumla ya Sh.87.896 bilioni. Hii ikitafsiriwa kitaalamu inamaanisha kuwa TTCL ni Kampuni muflisi.
Mheshimiwa Spika, mnamo mwaka 2005 Serikali iliipa TTCL mkopo wa jumla ya Dola za Marekani milioni 28 kwa ajili ya kulipa wafanyakazi waliostaafishwa, deni hilo halijalipwa mpaka sasa na limefikiwa jumla ya Sh. 76.6 bilioni pamoja na riba. Aidha, ukiacha deni hili TTCL inadaiwa na TCRA jumla ya Sh. 25 bilioni hivyo kufanya jumla ya deni kuwa Sh. 101.6 bilioni.
Mheshimiwa Spika, Kamati inaona kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa Kampuni hiyo ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa, ina wafanyakazi ( 1549) wanaotegemea ajira katika Kampuni hiyo na inatoa huduma ya internet kwa makampuni mengine ya simu nchini.

2.7    TAARIFA MAALUM KUHUSU DENI LA SH. 1,875,896,246,224.48 AMBALO SERIKALI INADAIWA NA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
2.7.1 Mheshimiwa Spika, tarehe 24 Oktoba, 2014, Kamati ilifanya kikao cha mashauriano kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gavana wa Benki Kuu, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Msajili wa Hazina na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
2.7.2 Mheshimiwa Spika, Dhumuni la kikao hicho lilikuwa kujadili na kutafuta ufumbuzi juu ya hoja ya ukaguzi iliyoibuliwa kwenye Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusiana na ukaguzi kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma zinazoishia tarehe 30 Juni 2013.  Kwa mujibu wa Taarifa hiyo na ukaguzi uliofanyika baadaye, mpaka kufikia tarehe 30 Septemba 2014 Serikali ilikuwa inadaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii jumla ya Sh.1, 875,896,246,224.48. Aidha, ilifahamika kuwa deni hilo halijumuishi deni la Serikali kwa PSPF la Sh. 7,066,530,000,000.00 ambalo lilianza mwaka 1999 baada ya PSPF kulipa mafao ya Wanachama ambao kisheria walistahili kulipwa lakini walikuwa hawachangii kwenye Mfuko huo.
2.7.3 Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa kulipwa kwanza kwa deni la Sh.1, 875,896,224.48 ili mifuko ya Hifadhi ya Jamii iweze kujiendesha bila matatizo, makubaliano yafuatayo yalifikiwa katika kikao hicho:-
a)       Serikali kulipa kwanza asilimia 50 ya deni hilo kwa kutoa Hati fungani (Special Government Bond) ifikapo tarehe 14 Novemba, 2014 endapo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itasamehe kiasi cha tozo kilichojumuishwa katika deni hilo kinachotokana na malimbikizo ya madeni kwa miradi na mikopo ya Serikali.
b)      Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kujadiliana na Bodi za Wadhamini kuhusu kuridhiwa kwa ombi la Serikali la kusamehewa na Mifuko hiyo kiasi cha tozo kilichojumuishwa kwenye deni hilo ili iweze kulipa sehemu ya deni hilo kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.
2.7.4 Mheshimiwa Spika, Bodi za Wadhamini wa Mifuko hiyo ziliridhia kusamehe tozo hizo endapo Serikali ingetoa Hati Fungani hiyo tarehe 14 Novemba, 2014. Lakini cha kusikitisha Serikali haikutimiza ahadi yake na mpaka Kamati inawasilisha taarifa yake makubaliano hayo hayajatekelezwa na Mifuko imeendelea kuwa katika hali mbaya ya kifedha. Kamati inapendekeza kuwa Serikali itekeleze makubaliano hayo mara moja na bila kuchelewa na ukopaji holela wa Serikali kwa Mifuko wa Hifadhi ya Jamii nchini ukome mara moja.
2.8    TAARIFA MAALUM KUHUSU KAMPUNI YA NDEGE YA TANZANIA (ATCL)
         Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.
2.8.1   Hali halisi ya ATCL kwa sasa
         Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Msajili wa Hazina kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2013 na kwa kuzingatia Taarifa ya Wizara ya Uchukuzi, imebainika kuwa ATCL kwa sasa ina Ndege moja tu aina ya Dash 8 – Q 300, Wafanyakazi 142 na Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam huku ikiwa na madeni makubwa kama itakavyofafanuliwa hapo baadae.
2.8.2   ATCL imefikaje hapo ilipo kifedha na kuwa na Madeni makubwa?
         Mheshimiwa Spika, baada ya kuvunjika kwa mkataba wa ubia baina ya SAA ana ATC, mnamo mwezi Machi 2008, Wizara ya Miundombinu kwa wakati huo iliingia katika makubaliano na Kampuni ya China Sonangol kuwa Kampuni hiyo ya China ingeleta ndege mpya 7  kwa ATCL ikiwamo Ndege 5 aina ya Airbus ambazo zingewasili  mwaka 2012 na 2013.
         Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Msajili wa Hazina na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, Wakati ATCL ikisubiri ndege hizo mpya, Kampuni ya China Sonangol iliitambulisha Kampuni ya Wallis Trading Inc kwa ATCL na kisha Kampuni hizi mbili (Wallis Trading Inc na ATCL) zikaingia mkataba wa Ukodishaji ndege aina ya Airbus 320 kwa kipindi cha miaka 6 kwa Malipo ya USD 370,000 kila mwezi.
         Mheshimiwa Spika, huu ndio ulikuwa mwanzo wa mwisho wa ATCL, kwani baada ya Ndege hiyo kuwasili ilifanya kazi kwa muda wa miezi sita tu na baadae ilifungiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kushindwa kutekeleza matakwa ya usafiri wa anga. Ndege hiyo ilipelekwa kwa matengenezo makubwa mwezi Julai, 2009 nchini Ufaransa na haijawahi kurudi hadi leo wakati ambapo Serikali kama mdhamini wa ATCL anadaiwa fedha nyingi na Kampuni ya Wallis.
         Mheshimiwa Spika, kutokana na deni la ATCL kwa Wallis linalofikia USD 42,459,316.12 hadi tarehe 31 Oktoba, 2011 na kufuatia majadiliano mbalimbali baina ya Serikali na Kampuni hiyo, Serikali imekwishalipa jumla ya USD 26,115,428.75 hadi sasa wakati bakaa inayodaiwa ni USD 23,996,327.82.
         Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa sana na upotevu huu wa fedha za Umma ambao umetokana na mkataba mbovu ulioingiwa na watumishi wa Umma wasiokuwa waaminifu na uchungu na  Taifa lao. Mabilioni ya fedha yanaoendelea kulipwa kwa Kampuni ya Wallis kwa huduma ya ndege iliyofanya kazi hapa nchini kwa miezi sita tu na kisha ndege hiyo kupelekwa Ufaransa kwa matengenezo ni fedheha kubwa kwa wazalendo wa Taifa letu. Aidha, Taarifa zinasema ndege hiyo ikiwa Ufaransa ilipakwa rangi na kukodishwa kwa Shirika la ndege la nchi ya Guinea wakati Serikali yetu ikiendelea kulipia tozo ya ukodishaji wa ndege husika.
         Mheshimiwa Spika, ni wakati sasa kwa Serikali kuamua kwa dhati kushughulikia suala la ATCL kwa mapana yake ikiwa ni pamoja na kuangalia uhalali wa kulipa deni la Wallis (ambalo lipo chini ya dhamana ya Serikali, hivyo ni fedha za Umma)  ambaye kimsingi naye alikiuka makubaliano ya Mkataba kwa kukodisha ndege iliyokuwa imekodishwa tayari kwa ATCL. Aidha, ni muhimu wahusika wa uingiaji wa mkataba husika wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke.
2.9    HOJA ZA UKAGUZI KUHUSU DOSARI KATIKA UMILIKI WA NYUMBA ZA MASHIRIKA
2.9.1 Bodi ya Sukari Tanzania
Mheshimiwa Spika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali tangu mwaka 2012 amekuwa akitoa hoja kuhusu nyumba ya Bodi ya Sukari inayokaliwa sasa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika.
Mheshimiwa Spika, Nyumba ya Bodi ya Sukari iliyopo kwenye Kiwanja Na. 482 Bray Road Masaki, Dar es Salaam ambayo anakaa Mhe. Stephen Wassira (Mb) haijarudishwa kwenye umiliki wa Bodi tangu February 12, 2008 kiongozi huyo alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Uratibu na Mahusiano. Juhudi za Bodi za kumuomba kiongozi huyo kurudisha nyumba hiyo na baadaye kuwasiliana na Katibu Mkuu Kiongozi kwa barua iliyoandikwa Disemba 2011 na kujibiwa Mwezi huo huo kwa ahadi kuwa nyumba hiyo ingerudishwa kwa Bodi ya Sukari hazikufanikiwa. Hivyo, mpaka Kamati inawasilisha Taarifa yake nyumba hiyo bado haijarudishwa.

         Mheshimiwa Spika, Kufuatia kutorudishwa kwa nyumba hiyo mpaka sasa, Kamati iliielekeza Bodi ya Sukari kumuandikia barua Waziri husika ili arudishe nyumba hiyo na Msajili wa Hazina kuhakikisha umiliki wa nyumba hiyo unabaki kwa Bodi ya Sukari. Hata hivyo, Kamati ilipata taarifa kutoka kwa Msajili wa Hazina kuwa kwa sasa Serikali ipo katika mchakato wa kuhamisha umiliki wa nyumba hiyo kutoka Bodi ya Sukari kwenda Wakala wa Majengo (TBA), kitendo ambacho kinafanyika bila kuihusisha Bodi ya Sukari wala Msajili wa Hazina kinadhihirisha uwepo wa mipango ya baadhi ya watumishi ndani ya Serikali kwa makusudi au kwa kushinikizwa wanataka kuhakikisha nyumba hiyo inabaki katika umiliki wa mtu binafsi. 
2.9.2 Bodi ya Korosho Tanzania
Mheshimiwa Mwenyekiti, Baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa National Agricultural Products Board (NAPB) au Cashewnut Authority of Tanzania (CATA) na kuundwa Bodi ya Korosho, hatua kadhaa zilichukuliwa za kubadilisha majina yaliyokuwepo kwenye hati miliki za viwanja na nyumba kutoka majina ya NAPB au CATA kuwa Bodi ya Korosho.
Mheshimiwa Spika, Kamati imepata taarifa kutoka kwa CAG kuwa Bodi ya Korosho ilinyang’anywa umiliki wa Nyumba iliyopo kwenye Kiwanja Na. 37 maeneo ya Ursino, Upanga Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG, Kiwanja hiko ambacho kilitakiwa kuhamishiwa kwenye umiliki wa Bodi ya Korosho, hapo awali tarehe 23 Januari 1967 kilisajiliwa kwa jina la National Agricultural Products Board kwa Hati Na. 9425. Miliki hiyo ilirejeshwa Ofisi ya Ardhi Kinondoni mnamo tarehe 13 Aprili, 2011. Ofisi hiyo iliandaa Hati nyingine kwa jina la Mohamed Said Hamad wa S.L.P 90164 Dar es Salaam. Hati husika ziliwasilishwa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi na kusainiwa tarehe 15 Aprili 2011 na baadaye kuwasilishwa Ofisi ya Msajili wa Hati na kusajiliwa kwa Hati Na. 98733.
Mheshimiwa Spika, Jambo la kushangaza tarehe 22 Juni, 2011 Ofisi ya Msajili wa Hati ilipokea nyaraka za uhamisho wa miliki hiyo kwenda kwa Ndugu Silvestry Francis Koka wa S.L.P 9014 Dar es Salaam. Baada ya uhamisho huo kufanyika, Mamlaka ya Korosho iliwasilisha nyaraka za zuio (caveat) mnamo tarehe 4 Mei 2012. Lengo likiwa ni kuzuia muamala wowote kuhusu miliki hiyo usifanyike. Aidha, Bodi ya Korosho Tanzania ilitoa taarifa kwa Ofisi ya Mkurugenzi Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili ifanye uchunguzi wa kina na kuwapata waliohusika kuhamisha na hatimaye kuuza kiwanja cha Bodi ya Korosho bila ridhaa ya mamlaka husika. Hivyo, kwa kuwa muamala uliofanyika una mazingira ya udanganyifu (fraud), Kamati inapenda kusisitiza uchunguzi wa DCI ukamilike haraka iwezekanavyo ili wahusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
2.10  TAARIFA MAALUM KUHUSU GHARAMA HALISI ZINAZOTUMIKA KATIKA KUTANGAZA BAJETI KWENYE MAGAZETI BAADA YA KUSOMWA BUNGENI
         Mheshimiwa Spika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amebaini kuwa fedha jumla ya Sh.2,545,517,366.79 zilitumika kwa kipindi cha miaka miwili kama gharama za machapisho ya hotuba za bajeti za Wizara 21 na Taasisi 5 kama ilivyoainishwa katika Jedwali hapa chini. Aidha, kati ya matumizi hayo, kiasi cha Sh.184,239,208 kilikuwa bado kulipwa hadi wakati wa ukaguzi huu na kilihusu machapisho ya hotuba za bajeti kwa vipindi vya 2011/2012 na 2012/2013.
Jedwali 6: Fedha zilizotumika kwa kipindi cha miaka miwili
Mwaka wa Fedha
Idadi ya Wizara
Idadi ya Taasisi
Kiasi kilicholipwa (Sh)
Kiasi bado kulipwa (Sh)
Jumla ya matumizi (Sh)

2011/2012
19
2
1,097,433,579.92
34,175,248.00
1,131,608,827.92

2012/2013
18
4
1,263,844,578.80
150,063,960.07
1,413,908,538.87

Jumla
21
5
2,361,278,158.72
184,239,208.07
2,545,517,366.79

Mheshimiwa Spika, kudhihirisha matumizi makubwa ya fedha zinazotumiwa na Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika kutangaza bajeti zao, Kamati ilibaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini peke yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilitumia jumla ya Sh. 211,547,952 kwa ajili ya kutangaza Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Mathalani mojawapo ya chombo cha habari kiitwacho Jambo Concepts Tanzania kililipwa jumla ya Sh. 49.01 milioni ndani ya siku moja kwa ajili ya kutangaza Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo siku ya tarehe 13 Juni 2013. Jambo la kujiuliza ni msingi upi Wizara iliutumia katika kulipia Kiasi kikubwa cha fedha kwa chombo cha habari kimoja kwa Tangazo la siku moja wakati kwa vyombo vingine vya habari vililipwa wastani wa Sh. 9 hadi 11 milioni kwa huduma ya aina hiyo.
Mheshimiwa Spika, huu ni ushahidi wa wazi kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha za Umma yenye taswira za upendeleo kwa baadhi ya Taasisi za Umma kutumia mwanya wa kutangaza Hotuba za Bajeti za Wizara kwa malengo yasiyo bayana na ni viashiria vya matumizi mabaya ya madaraka na kukosekana udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma.
2.11  TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU TATHMINI YA ZOEZI LA UBINAFSISHAJI
Mheshimiwa Spika, Mnamo mwaka 2012, iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilipendekeza kwa Bunge lako Tukufu na kisha kuridhiwa kama azimio la Bunge kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ifanye tathmini kuhusu zoezi zima la ubinafsishaji wa yaliokuwa Mashirika ya Umma ili kuangalia maeneo yapi zoezi husika lilifanikiwa na wapi halikufanikiwa ipasavyo.
Mheshimiwa Spika, Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Ofisi ya CAG imefanya zoezi hilo kwa Mashirika kumi yaliobinafsishwa na wamewasilisha taarifa hiyo mbele ya Kamati. Kamati ipo katika hatua za awali za kushughulikia Taarifa hiyo ambayo pia nitaiwasilisha Ofisini kwako kwa maelekezo zaidi.SEHEMU YA TATU
______________

3.0    MAPENDEKEZO YA KAMATI
3.1    Uwepo wa mapungufu mengi katika matumizi ya misamaha ya kodi katika mwaka wa fedha wa 2012/2013;
KWA KUWA, Misamaha ya kodi imeendelea kuongezeka kila mwaka na Taarifa ya awali ya ukaguzi wa misamaha hiyo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeonyesha mapungufu makubwa katika matumizi ya misamaha hiyo kama ilivyoanishwa kwenye Sehemu ya pili ya Taarifa hii,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo;
a)       Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha Kitengo cha kusimamia misamaha ya kodi ambacho kitakuwa na jukumu la kufuatilia matumizi ya misamaha ya kodi na kuwasiliana na Mamlaka zingine zenye jukumu la kutoa misamaha ya kodi.
b)      Mamlaka ya Mapato ianzishe utaratibu wa kuzikagua (Inspection and Monitoring Visits) mara kwa mara Kampuni zilizopewa misamaha ya kodi kwa lengo la kuhakikisha Kampuni hizo zinatekeleza matakwa ya Sheria na kuepusha hasara inayotokana na matumizi mabaya ya misamaha ya kodi. Aidha, TRA ihakikishe inaokoa kodi yenye thamani ya Sh.22,325,178,728 iliyopotea kutokana kukosekana kwa udhibiti na usimamizi mzuri wa matumizi wa misamaha ya kodi kwa kuitaka kampuni ya Geita Goldmines kulipa fedha hiyo pamoja na adhabu kali.
c)       Mamlaka ya Mapato iongeze udhibiti wa misamaha ya kodi inayotolewa kwa waagizaji wa magari ikiwa ni pamoja na kuhakikisha gari lililosamehewa kodi linasajiliwa kwa jina la muagizaji (importer). Aidha, TRA ihakikishe Kampuni ya Kiliwarrior Expeditions Ltd na Kampuni ya Kilemakyaro Mountain Lodge Limited zinarudisha haraka iwezekanavyo mapato yaliyopotea ya Sh. 392,701,602 na Sh.53,399,565 sawia kutokana na udangajifu uliofanyika katika uigizaji wa magari na Kampuni hizo zifutiwe mara moja msamaha wa kodi wa kuingiza magari nchini
d)      Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato ihakikishe inafanya uchunguzi na makampuni yanayodaiwa kodi kutokana na kutumia vibaya misamaha ya kodi yarudishe fedha hiyo na Maafisa wa Mamlaka ya mapato walioshiriki katika udanganyifu huo wachukuliwe hatua za kinidhamu na za kisheria.
e)       Mamlaka ya Mapato ihakikishe maduka ya bidhaa zilizosamehewa kodi na makampuni yenye misamaha ya kodi yanawasilisha hesabu zake zinazohusu misamaha ya kodi kabla ya kufunga biashara. Aidha, TRA ifanye uchunguzi kuhusiana na matumizi ya msamaha wa kodi uliotolewa kwa M/s Conti- Africa Ltd kabla na baada ya kufunga biashara yake na kuhakikisha mapato yaliyopotea ya Sh.3,824,547,526 yanarudishwa na Kampuni hiyo.
f)          Mamlaka ya Mapato ihakikishe Makampuni yaliyosamehewa kodi yanawasilisha Taarifa za Matumizi ya misamaha ya kodi kabla ya kupewa msamaha mwingine wa kodi.
g)       Mamlaka ya Mapato ihakikishe maombi yote ya misamaha ya kodi hayashughulikiwi mpaka ziwasilishwe nyaraka sahihi zinazohitajika kisheria.
h)      Menejimenti ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ianzishe mchakato wa kurekebisha Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997 ili kuondoa misamaha ya kodi kwa ukarabati au upanuzi wa miradi ya Makampuni yaliofaidika na misamaha hapo awali wakati wa uanzishwaji wake.

3.2    Mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi maalum wa wa fedha za ushuru wa mauzo nje ya nchi na ruzuku ya Serikali kwa zao la korosho katika Mkoa wa Mtwara katika kipindi cha 2006/07 hadi 2010/11
3.2.1 KWA KUWA, Taarifa ya Ukaguzi maalum wa fedha za ushuru wa mauzo nje ya nchi na ruzuku ya Serikali kwa zao la korosho katika Mkoa wa Mtwara katika kipindi cha 2006/07 hadi 2010/11 imeonyesha kuwepo kwa mapungufu makubwa katika matumizi ya fedha hizo kama ilivyoanishwa kwenye Sehemu ya pili ya Taarifa hii,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo,
a)       Fedha za ruzuku na ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi Shs. 1,075,046,004 zilizotumika kulipia gharama za kuendesha ofisi kinyume na makusudio ya Sheria inayotaka fedha hizo zitumike kwa ajili ya kuendeleza zao la korosho.  Kwa mantiki hiyo Bodi ya Korosho inapaswa kuzirejesha fedha hizo kwenye akaunti ya pembejeo na zitumike kama Sheria inayoelekeza.
b)      Bodi ya Korosho itoe mchanganuo kuonesha marejesho ya mikopo iliyotolewa 2006/2007 ipatayo Shs. 345,958,266 yalivyotumika.
a)       Bodi ya Korosho kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ihakikishe inapeleka TAKUKURU maelezo kuhusu udanganyifu uliopelekea Kampuni ya Mukpar Tanzania Ltd kulipwa kimakosa Shs.223,815,000 ili uchunguzi uweze kufanyika. Aidha, Maafisa wa Bodi ya Korosho na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi watakaothibitika kushiriki kwenye udanganyifu huo wachukuliwe hatua za kinidhamu na za kisheria.
b)      Uagizaji wa pembejeo za korosho na hasa madawa ufanywe kwa mfumo wa uagizaji wa pamoja (Bulk Procurement) kwa zabuni itakayoendeshwa na Bodi ya korosho na wasambazaji wakubwa, wa kati na wadogo wanunue kutokana na zabuni hiyo na kusambaza kwa wakulima. Hii itaondoa ukiritimba wa uagizaji wa madawa na kushusha bei ambayo mkulima ananunua madawa na kuondoa kwa kiasi kikubwa rushwa iliyokithiri katika biashara ya madawa ya korosho.
c)       Bodi ya Korosho kama msimamzi na mlipaji wa fedha ihakikishe malipo yanafanyika baada ya Halmashauri husika kuthibitisha kutoa kibali na pia kupokea pembejeo ili kuepuka pembejeo zilizokwishalipiwa kutoletwa na wauzaji wa pembejeo hizo.
d)      Bodi ya Korosho pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(ARI) ziendelee kushirikiana na Maafisa Kilimo kutoa elimu kwa wakulima mara kwa mara kuhusiana  na matumizi ya madawa/pembejeo ili kuepuka migogoro ya wakulima kukataa kutumia pembejeo zilizolipiwa ruzuku.
e)       Bodi ya Korosho izingatie mapendekezo ya wakulima wakati wa kufanya mchakato wa kuagiza pembejeo ili kukidhi matakwa ya wakulima.
f)         Bodi ya Korosho na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ziendelee kufanya ukaguzi wa madawa mapema kabla hayajasambazwa kwa wakulima ili kuepuka usambazaji wa madawa yaliyokwisha muda wake wa matumizi.
g)       Halmashauri zihakikishe zinatunza kumbukumbu za malipo ya fedha za ruzuku na ushuru wa korosho ghafi ili kuwezesha uhakiki wa fedha hizo wakati wowote inapotakiwa.
h)      Halmashauri zifanye juhudi kuhakikisha kuwa fedha zote zinazohusu pembejeo zilizokopeshwa kwa wadau/Vyama vya Msingi katika msimu wa mwaka 2006/07, zinakusanywa na kupelekwa katika Mfuko wa Pembejeo wa Wilaya kama ilivyoamriwa na kikao cha RCC cha tarehe 26 Mei 2010 ili kuendelea kuwanufaisha wakulima wengine.
i)         Bodi ya Korosho izingatie mgawanyo wa fedha na matumizi ya kila Halmashauri, ili kila Halmashauri itumie kulingana na kiwango ilichotengewa.
j)         Bodi ya Korosho isihamishe fedha za Halmashauri moja kwenda Halmashauri nyingine bila kupata idhini ya Halmashaui yenye fedha husika.
3.2.2 KWA KUWA, Uzalishaji wa Korosho umeongezeka na kufikia takribani tani 200,000 kwa mwaka katika msimu uliokwisha na kwamba Tanzania inapoteza fedha za kigeni kwa wastani wa dola za kimarekani 110 milioni kwa mwaka katika kipindi cha miaka 5 iliyopita kutokana na kuendelea kuuza korosho ghafi nje ya nchi (The African Cashew Alliance Report 2014),
         HIVYO BASI, Kamati inapendekeza kuwa sehemu ya ushuru wa korosho (Export levy) unaopelekwa Hazina utumike kujenga Viwanda vya kubangua Korosho vya ngazi ya kati na ngazi ya chini ( vijijini) mpaka hapo nchi itakapoweza kubangua korosho yote nchini. Aidha, Viwanda vitakavyojengwa viendeshwe kwa ubia kati ya Serikali, Sekta Binafsi na Ushirika wa Wakulima.
3.3    Utata juu ya gharama halisi za Ujenzi wa Jengo la kumbi za Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
         KWA KUWA, Taarifa ya Ukaguzi maalum wa Ujenzi wa Jengo la kumbi za watu mashuhuri katika Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere imeonyesha kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za Umma na ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Manunuzi kama ilivyoanishwa kwenye Sehemu ya pili ya Taarifa hii,
         HIVYO BASI, Kamati inapendekeza Serikali kupitia vyombo vyake vya dola ikiwepo TAKUKURU kufanya uchunguzi wa jinai kwa walioshiriki kuipotezea Serikali zaidi ya Shilingi bilioni 9 na Wahusika wachukuliwe hatua za kisheria haraka iwezekenavyo.
3.4    Mapungufu yaliyojitokeza katika Ukaguzi Maalum wa Matumizi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
KWA KUWA, Taarifa ya Ukaguzi maalum wa matumizi mbalimbali ya fedha za Mamlaka ya Bandari Tanzania imeonyesha kuwepo na ukiukwaji mkubwa wa Sheria za Fedha, Sheria ya Manunuzi, usimamizi mbovu wa miradi ya Mamlaka, udhibiti mdogo katika matumizi ya fedha za Mamlaka na ubadhirifu katika malipo yanayofanywa kwa Wafanyakazi,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo:-
a)       Mamlaka ya Bandari Tanzania iongeze udhibiti katika matumizi yanayofanyika kwa ajili ya vikao vya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama zisizo za lazima na idadi ya vikao visivyo vya lazima. Aidha, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aendele kufuatilia kwa umakini matumizi yanayofanyika katika eneo hili kila mwaka.
b)      Mamlaka ya Bandari Tanzania ihakikishe inaboresha mfumo wa kielektroniki wa kutunza kumbukumbu ili kudhibiti suala la ukosefu wa kumbukumbu na nyaraka. Aidha, Mamlaka ya Bandari iwasilishe kwa Wakaguzi nyaraka zinazothibitisha matumizi ya jumla ya Sh. 384,199,742.40 zinazodaiwa kutumika kwa matangazo tu.
c)       Mamlaka ya Bandari Tanzania izingatie matakwa ya Sheria zinazosimamia fedha kabla ya kuanza kufanya malipo ya aina mbalimbali hususan kwa wafanyakazi wake.
d)      Serikali ichukue hatua za haraka na za makusudi kuokoa jumla ya Sh.5,517,986,016 ambazo ni gharama ya ujenzi wa magati katika mwambao wa Ziwa Tanganyika ambapo imebainika kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imempa kazi ya ujenzi wa magati hayo Mkandarasi asiye na uwezo wa kifedha na sifa za kufanya ujenzi huo.
3.5    Mapendekezo mahsusi kuhusu ya kuikwamua Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na hatma ya Hisa za Serikali katika Benki hiyo
KWA KUWA, Serikali inaelekea kupoteza umiliki wa asilimia 25 za hisa katika NBC kama itashindwa kulipa Shilingi bilioni 22.5 kwa Barclays/ABSA kabla ya tarehe 15 Machi 2015,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo:-
a)       Gavana wa Benki Kuu, Msajili wa Hazina na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wafanye mapitio ya mchakato wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC na mikataba yote (Technical Assistance Agreement, Shareholding agreements, uwiano wa uongozi ndani ya NBC) iliyoingiwa hapo awali ili kuona kama kuna tija ya vifungu na makubaliano waliyomo katika mikataba hiyo kwa sasa ili waweze kuishauri Serikali hatua za kuchukua kuikwamua NBC na kulinda hisa za Serikali katika Benki hiyo.
b)      Baada ya Tathmini hiyo Serikali ihakikishe inalipa Shilingi bilioni 22.5 kwa Barclays/ABSA kabla ya tarehe 15 Machi 2015 ili kunusuru hisa zake kuchuliwa;
c)       Serikali baada ya kulipia hisa zake ifikiriye kuziuza kwa wananchi kama ilivyoainishwa kwenye mkataba kuwa baada ya kubinafsisha NBC hisa za Serikali zitauzwa kwa wananchi.
d)      Serikali kupitia NBC ihakikishe inawachukulia hatua za kisheria haraka iwezekanavyo Wafanyabiashara wote waliohusika na uchukuaji wa mikopo ya usafirishaji iliyopelekea NBC kupata hasara kubwa.


3.6    Mapendekezo ya Hatua mahsusi za kuikwamua Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
KWA KUWA, kuna umuhimu wa kuikwamua Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye sekta ya mawasiliano,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuikwamua TTCL:-
a)       Serikali kununua hisa asilimia 35 zinazomilikiwa na Bharti Airtel katika TTCL kwa gharama ndogo ikizingatiwa Bharti Airtel haikutimiza kikamilifu masharti ya mkataba wa mauziano ya hisa hizo hapo awali kwani tangu inunue hisa hizo haijafanya uwekezaji katika Kampuni ya TTCL.
b)      TTCL isamehewe deni la Serikali Sh. 76.6 bilioni na deni la TCRA Sh. 25 bilioni ambayo jumla yake ni Sh. 101.6 bilioni na fedha hizo zipelekwe kuongeza mtaji ili Kampuni itoke kwenye kuwa na mtaji hasi wa Sh. 87.896 bilioni na kuwa na mtaji chanya wa sh. 13.704 bilioni. Likifanyika hili basi Kampuni hiyo itaweza kukopesheka.
c)       Serikali ikamilishe taratibu zake za kuimilikisha TTCL Mkongo wa Taifa ili izidi kuuendeleza kwa ufanisi na kuongeza mapato ya TTCL.
d)      Kutokana na TTCL kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi (1549) isiyoweza kuwalipa kuna umuhimu wa kufanya Marekebisho ya Muundo wa Kampuni. Aidha, zinahitajika Sh. 32 bilioni kwa ajili ya kugharamia urekebishaji wa muundo wa Kampuni ili uendane na mahitaji ya utoaji wa huduma mbalimbali.
e)       Serikali itakapokamilisha umiliki wake kwa asilimia 100 iwekeze mtaji zaidi baada ya kufanya tathmini ya mahitaji ya Kampuni. Hatua hii ihusishe kuwezesha Watanzania kumiliki kampuni hii kupitia soko la Hisa la Dar es Salaam.
   
3.7    Mapendekezo ya kuinusuru Mifuko ya Hifadhi ya Jamii isishindwe kutoa huduma kwa Wanachama wake na Wastaafu kutokana na Serikali kushindwa kuilipa Deni la Jumla ya Sh.1, 875,896,246,224.48.
         KWA KUWA, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inakabiliwa kupungukiwa uwezo wa Fedha za kujiendesha kutokana na Serikali kushindwa kulipa deni la Sh. 1,875,896,246,224.48 kama ilivyoainishwa kwenye Sehemu ya Pili ya Taarifa hii,
         NA KWA KUWA, Kamati imefanya kila linalowezekana kuwezesha deni hilo lilipwe kwa manufaa ya wanachama wa Mifuko hiyo na Wastaafu,
         HIVYO BASI, Kamati inaliomba Bunge lako Tukufu kuazimia Serikali ilipe deni hilo haraka iwezekanavyo ile kuinusuru Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika changamoto ya kushindwa kulipa mafao ya Wastaafu na kutoa huduma nyingine.
3.8    Mapendekezo kuhusu deni la USD 23,996,327.82 ambalo ATCL inadaiwa na Wallis Trading Inc.
         KWA KUWA, Serikali haikunufaika na mkataba wa kukodisha ndege aina ya Airbus kutoka kwa Kampuni ya Wallis baada ya ndege hiyo kugundulika ni mbovu ndani ya miezi sita na kupelekwa kutengenezwa kwa muda mrefu,
         NA KWA KUWA, Serikali inaendelea kulipa tozo ya ukodishaji wa ndege hiyo ambayo haifanyika kazi,
         HIVYO BASI, Kamati inapendekeza yafuatayo;
a)      Serikali kuangalia uhalali wa kulipa deni la Wallis ambaye kimsingi naye alikiuka makubaliano ya Mkataba kwa kukodisha ndege iliyokuwa imekodishwa tayari kwa ATCL.
b)      Serikali ihakikishe inawafikisha kwenye vyombo vya Sheria ili haki itendeke kwa wahusika wa uingiaji wa mkataba huo unaoendelea kuipa hasara Serikali kwani hadi sasa hakuna kesi iliyopelekwa mahakamani mahususi kwa waliongia mkataba husika.

3.9  Mapendekezo kuhusu umiliki wa nyumba za Mashirika ya Umma
3.9.1   Bodi ya Sukari Tanzania
KWA KUWA, Nyumba iliyopo Kiwanja Na. 482 Bray Road Masaki, Dar es Salaam ni chanzo cha mapato ya Bodi ya Sukari na Uhamishaji wa umiliki wa nyumba hiyo kwenda TBA haukushirikisha Bodi husika,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza kwamba utwaaji wowote wa nyumba za Shirika lazima ufuate taratibu za kisheria ikiwemo maamuzi ya Bodi husika. Bunge liitake Serikali kufuata taratibu za kuichukua nyumba ya Bodi ya Sukari (iwapo ni kwa masalahi mapana ya Taifa) kuipeleka Wakala wa Nyumba ( TBA). Hatua hii pia ihusishe Bodi ya Sukari kulipwa thamani ya nyumba hiyo ili kukomesha mtindo wa Serikali kujichukulia nyumba za Mashirika ya Umma bila kufuata taratibu na kuzimilikisha kwa watu au Viongozi binafsi kama ilivyokwishatokea miaka ya nyuma.
3.9.2 Bodi ya Korosho Tanzania
KWA KUWA, Uuzaji wa Nyumba iliyopo kwenye Kiwanja Na. 37 maeneo ya Ursino, Kinondoni, Dar es Salaam una mazingira ya udanganyifu (Utapeli) wa kughushi nyaraka na matumizi  mabaya ya madaraka ambayo ni makosa ya jinai, 
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza Jeshi la Polisi likamilishe uchunguzi na kuwafikisha mahakamani waliohusika na uuzaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho na Msajili wa Hazina ahakikishe Bodi ya Korosho inapata hati miliki ya nyumba zake zote bila kuchelewa.
3.10 Mapendekezo Kuhusu Gharama za Matumizi ya Wizara na Taasisi zake kutangaza Hotuba za Bajeti
KWA KUWA, imebainika kuwa Wizara na Taasisi nyingi za Serikali zinatumia gharama kubwa kwa matangazo ya Hotuba za bajeti, NA KWA KUWA matangazo hayo hayalingani na tija ya gharama zilizotumika,
HIVYO BASI, Kamati inapendekeza kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, atoe kipaumbele maalum cha Ukaguzi kukagua matumizi husika na pia Maafisa masuhuli waagizwe kupunguza matumizi hayo yasiokuwa ya lazima kabla hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao. 

SEHEMU YA NNE
______________
4.0    Hitimisho
4.1    Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Kamati imeeleza kwa kina namna Kamati ilivyotekeleza majukumu yake ya msingi na mafanikio iliyopata katika utekelezaji wa majukumu yake. Pamoja na kuainisha mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza katika Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondoa mapungufu hayo kwa maendeleo ya Taifa.
4.2    Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi kwa uongozi wako makini ambao umeniwezesha mimi kuwasilisha Taarifa hii hapa Bungeni na kuiwezesha Kamati yangu kutekeleza majukumu yake bila vikwazo kwa kutoa maelekezo na miongozo thabiti pale Kamati ilipohitaji msaada wako.
4.3    Mheshimiwa Spika, ninapenda kuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Uongozi kwa jinsi tulivyoshirikiana katika kuweka mikakati mbalimbali ya uendeshaji wa Bunge na Kamati zake.
4.4    Mheshimiwa Spika, nawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kwa kutekeleza majukumu ya Kamati hii kwa moyo na uadilifu mkubwa. Aidha nawapongeza kwa kushiriki kikamilifu katika kuboresha mijadala, maoni na mapendekezo ya Kamati na kunipa heshima ya kuiwasilisha Taarifa hii mbele ya Bunge lako tukufu. Mheshimiwa Spika, naomba kuwatambua Wajumbe hao kama ifuatavyo,
1)      Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, Mb                      -        Mwenyekiti
2)      Mhe. Deo Haule Filikunjombe, Mb             -        M/Mwenyekiti
3)      Mhe. Asha Mshimba Jecha, Mb                  -        Mjumbe
4)      Mhe. Dkt. Hadji H. Mponda, Mb                 -        Mjumbe
5)      Mhe. Hezekiah N. Chibulunje, Mb               -        Mjumbe
6)      Mhe. Gaudence C. Kayombo, Mb                -        Mjumbe
7)      Mhe. Abdul Jabir Marombwa, Mb              -        Mjumbe
8)      Mhe. Zaynab Matitu Vullu, Mb                   -        Mjumbe
9)      Mhe. Lucy Fidelis Owenya, Mb                   -        Mjumbe
10)  Mhe. Ester Nicholas Matiko, Mb                -        Mjumbe
11) Mhe. Deusiderius John Mipata, Mb            -        Mjumbe    
12) Mhe. Ali Keissy Mohamed, Mb                    -        Mjumbe
13) Mhe. Zainabu Rashid Kawawa, Mb             -        Mjumbe
14) Mhe. Kheri Ali Khamis, Mb                          -        Mjumbe
15) Mhe. Faida Mohamed Bakar, Mb                -        Mjumbe
16) Mhe. Ismail Aden Rage, Mb                         -        Mjumbe
17) Mhe. Modestus Dickson Kilufi, Mb             -        Mjumbe
18) Mhe. Kombo Khamis Kombo, Mb               -        Mjumbe
19) Mhe. Catherine V. Magige, Mb                    -        Mjumbe    
20) Mhe. Lolesia J. Bukwimba, Mb           -        Mjumbe
21) Mhe. Amina M. Mwidau, Mb                       -        Mjumbe

4.5    Mheshimiwa Spika, Napenda kumshukuru Katibu wa Bunge Dkt. Thomas D. Kashililah kwa ushauri wake kwa Kamati kwa kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu ya Kamati. Shukrani kwa Idara ya Kamati za Bunge kwa kuratibu shughuli za Kamati chini ya Makatibu wa Kamati ya PAC Ndugu. Mathew N. Kileo na Ndugu. Erick S. Maseke, pamoja na Waandishi wa Taarifa Rasmi za Bunge.
4.6    Mheshimiwa Spika,katika kutekeleza kazi zake, Kamati ilikuwa ikishirikiana na Wataalam kutoka Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali na Kamishna wa bajeti. Nawashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kuhakikisha Kamati hii inatekeleza majukumu yake vema.
4.7    Mheshimiwa Spika, Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Naomba kutoa Hoja.

Mhe. Zitto Z. Kabwe, Mb.
MWENYEKITI
KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
28 Januari, 2015[1] Makubaliano  ya awali yaliosainiwa tarehe 13 Machi, 2007
[2] Kanuni ya 42(a) ya Kanuni za Ukaguzi wa Umma za Mwaka 2005
[3] Regulation 42(1) (c) of GN 97 of the PPA , 2004
[4] Ukurasa wa 37 wa Kitabu cha Hoja za Ukaguzi Maalum uliofanywa na CAG kuhusu TPA
[5] Kipili, Kagunga, Lagosa and Sibwesa Jetties
[6] TIER 1 CAPITAL RATIO
Means the ratio of (a) Tier 1 capital, comprised of common stock and retained earnings, less goodwill or any other intangible assets to (b) risk weighted assets and off-balance sheet exposures as defined in terms of the BASLE PAPER