Mapitio ya magazeti katika Tv mbalimbali Aprili Mosi, 2015
Tume ya Binadamu na Utawala Bora: Kuuawa kwa Askari na kujeruhiwa WanaCUF


BoT Auction today: 10.08% a 7-year Fixed Rate Treasure Bond


Machi 30, 2015: Tamko la Jukwaa la Wakristo kuhusiana na Muswada wa Mahakama ya Kadhi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sisi, Maaskofu kutoka TEC, CCT na CPCT tumekutana leo tarehe Machi 30, 2015hapa Dodoma ili kuomba kwa pamoja juu ya mgawanyiko unaodhihirika wa dini za Kikristo na Kiislamu kutokana na muswada wa Mahakama ya Kadhi. Maaskofu tuliokutana hapa hatuna hasira na wala hatuongozwi na hasira wala mihemko katika kufikia maamuzi tunayofanya kama ambavyo wengine wanavyotutafsiri. Tunafikia maamuzi yetu baada ya maombi na sala na tunasukumwa na upendo kwa wananchi ili kujenga taifa lenye umoja, amani, utulivu na maelewano.
Pia tumekuja kufuatilia kwa kina Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964. Muswada huu unapendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi  ambao utawasilishwa Bungeni April 01, 2015kwa hati ya dharura na hivyo kuufanya umma wa Watanzania kutokujua maudhui yaliyomo katika muswada huo wakati bado hoja zetu za msingi tulizopeleka kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge na kwa Waziri Mkuu hazijajibiwa.
Tangu tulipokutana Machi 10, 2015 ambako tulitoa tamko letu kuhusiana na Mahakama ya Kadhi na Katiba Inayopendekezwa, tumekuwa tukiendelea kutafakari juu ya yale tuliyokuwa tumesema katika matamko yetu mbalimbali na jinsi amani na utulivu wa nchi yetu vinavyoendelea kumomonyoka siku zinavyokwenda.
Kwanza tumeshangazwa na tabia ya viongozi wa serikali ya kuitisha na kuendesha mikutano wanayodai ni ya viongozi wa dini lakini isiyo rasmi. Machi 03, 2015 Waziri Mkuu aliitisha mkutano kupitia Mchungaji mmoja ambapo hakuna hata kiongozi mmoja wa taasisi au Kanisa aliyeshiriki. Jambo la kushangaza ni kile kilichotokea Machi 28, 2015 ambapo Mhe. Rais alishiriki kikao cha kikundi ambacho sio rasmi yaani Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam. Tunasema kamati hiyo siyo rasmi kwa sababu haina baraka za viongozi wa ngazi za juu wa kidini wa Mkoa huo na haina mwongozo wa kazi zake. Mikutano ya jinsi hii kati ya serikali na wale ambao imewaona kuwa ndio viongozi wa dini sio sahihi kwani viongozi wa dini wana taratibu zao za kualikwa au kuwakilishwa katika mikutano na viongozi wa serikali au wa dini au madhehebu mengine. Tunawashauri wanaohutubia na wanaoshiriki mikutano hii wajue kwamba washiriki hawana uwezo wa kuamua au kukubaliana na jambo lolote kwa niaba ya viongozi wao wa juu na pia viongozi husika wa serikali wasifurahi kwamba ujumbe wao umewafikia viongozi wa dini kwani hao washiriki sio wawakilishi rasmi na hawana uwezo wa kutoa maamuzi au kukubaliana juu ya jambo fulani la kitaifa.
Pili, tumekuwa tukifuatilia kwa karibu juu ya muswada wa Mahakama ya Kadhi na tumebainisha dhahiri kwamba kile tulichokuwa tunasema kitatokea kimeaanza kutokea bayana. Yale yaliyotokea kwenye semina kuhusu Mahakama ya Kadhi kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMachi 29, 2015 ambao ni wasomi, ni ishara ndogo sana ya kile kitakachotokea maeneo yote ya nchi yetu. SERIKALI KWA NIA MOJA NA KWA SABABU TUSIZOZIJUA INAANZISHA VITA VYA KIDINI KATI YA WATANZANIA WAKRISTO NA WAISLAMU. Tunashangazwa kuona jinsi serikali inavyonuia jambo hili ovu litakaloleta balaa kwa nchi yetu wakati huu wa kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa na baadaye Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kutokana na mambo hayo makuu mawili hapo juu, sisi Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo Tanzania tunatamka kama ifuatavyo :
  1. Matamshi ya Mhe. Rais akihutubia aliyowaita viongozi wa dini tarehe Machi 28, 2015 kuwa Mahakama ya Kadhi ni ya Waislamu wenyewe na serikali haitajihusisha wala kugharamia yanakinzana na kile kinachoendelea bungeni na nchini. Hapa tunajiuliza, endapo maneno ya Rais ni kweli, mbona Bunge linaendelea kujadili kitu ambacho serikali haitajihusisha wala kukigharimia ? Kwa mantiki hiyo, tunamtaka Mhe. Rais aagize muswada huu uondolewe Bungeni na usijadiliwe tena kwa kuwa Utafiti wa Tume ya kurekebisha sheria ulishaonyesha madhara ya uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi. Vinginevyo, kuendelea kujadiliwa kwa muswada huu maana yake ni kwamba serikali inajihusisha na itagharimia mahakama hiyo.
  2. Serikali ijue kuwa endapo Wabunge wa dini za Kikristo na Kiislamu watapigana na kisha baadaye wananchi nao wakafanya hivyo katika maeneo yao, SERIKALI ITAKUWA NDIYO CHANZO CHA MAPIGANO HAYO. Kama tulivyotamka hapo juu, kuhusiana na jambo hili tunamtaka Mhe. Rais aiepushe nchi yetu na kuingizwa kwenye mapigano ya kidini ambayo kuyadhibiti itakuwa vigumu sana (tafadhali rejea kinachoendelea huko Nigeria). Pia tunamwomba Mhe. Rais akumbuke na kutafakari kile kilichotokea na kinachotokea nchi ya Afrika ya Kati kati ya kundi la Seleka (Waislam) na kundi la Anti Balaka (Wakristo).
  3. Tunaamini kuwa viongozi wa serikali wanafahamu viongozi rasmi wa dini na madhehebu ya dini. Kwa mantiki hiyo tunawashauri viongozi wa serikali waache kabisa kutumia vikundi visivyo rasmi kualika mikutano wanayodhani kuwa itakubalika na waumini wa dini hizo. Mikutano yote ya jinsi hiyo itakayoitishwa ni batili na maamuzi yake hatuyatambui na hatutayatambua.
  4. Bado Maaskofu tunasimamia Tamko letu la Machi 10, 2015 na tunawahimiza Wakristo wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga Kura na zaidi wajitokeze kwenda kupiga kura yaHAPANA wakati wa kura ya maoni kwani Katiba inayopendekezwa ilifikia hapo kwa njia ya ubabe, ilikosa uadilifu na mbaya zaidi ni RUSHWA YA AHADI YA MAHAKAMA YA KADHI ya iliyotolewa na Waziri Mkuu kwa Waislamu wakati wa kupitisha Katiba Inayopendekezwa. Tunafanya hivyo kwa dhamiri safi kwa sababu ya imani yetu na kwamba sisi ni raia wa nchi hii na tuna haki ya kueleza mawazo yetu bila woga kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inavyotupa haki.
  5. Mwisho tunawaomba Wakristo wote waendelee kufunga na kuomba kwa ajili ya utulivu na amani ya nchi yetu.
Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla,wala hapati dawa .’Mithali 29 :1
Imetolewa na
image2

Hotuba ya Rais Kikwete UN kuhusu ajira na kazi za utu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: [email protected]
Website : www.ikulu.go.tz   
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kuna Umuhimu mkubwa wa kuweka suala la Ajira  katika  ajenda   ya maendeleo,  mipango na progamu ya Mataifa yote duniani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York wakati wa ufunguzi wa Mkutano  unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu  (Achieving sustainable development through employment creation and decent work).
Rais Kikwete amesema tatizo la ajira lina pande mbili, kwanza linaweza kutumika vizuri pale  wawekezaji wanapokuja  barani Afrika, wanaweza kupata nguvu kazi iliyopo tayari,  ikiwa inakidhi matakwa ya kazi na pili ni changamoto kubwa pale ambapo ajira hazipatikani kwa kundi kubwa la vijana ambao wanaongezeka kila mwaka.
"Hivyo ni muhimu ukuzaji wa ajira kuwa kipengele muhimu katika ajenda ya maendeleo, mipango na programu mbalimbali katika Mataifa yote" Rais amesema na kuelezea kuwa pamoja na ukweli uliopo kuwa nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania, zimeonyesha hali nzuri ya uchumi kwa miongo miwili mpaka mitatu iliyopita, na kuonyesha kuwa bara la Afrika ni moja ya mabara yanayokua kwa kasi kiuchumi duniani, bado bara linakabiliwa na tatizo kubwa la ajira.
"Natarajia  tutabadilishana mawazo ya jinsi gani Afrika inaweza kutatua tatizo hili na pia kupata mawazo ya nini kifanyike kuweza kuvutia wawekezaji zaidi". Rais amesema.
"Pia nitapenda kupata mawazo na ikiwezekana kuunga mkono katika kusaidia vijana wetu katika suala la kujiajiri" ameongeza na kusema suala hili linahitaji programu maalum na miradi.
Rais Kikwete amezungumzia suala la ajira barani Afrika kuwa la kutia mashaka na hivyo kuhitaji hatua za haraka. Takwimu zinaonesha kuwa Afrika ilitengeneza ajira 37 million  pekee kwa kipindi cha muongo uliopita, kati ya hizi asilimia 28 zilikuwa ajira zenye utu, na wakati huo huo inakadiriwa kuwa, soko la ajira barani Afrika linapokea watu milioni 122 katika ajira mpya kila mwaka.
"Hii inatisha sana kwa vile karibu watu 200 barani Afrika ni wake wenye miaka 15 na 24 na kwamba idadi hii itaongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2045"
Rais amefafanua na kuonyesha wasiwasi wake kwamba bara la Afrika litakumbwa na idadi kubwa ya ukosefu wa ajira, na kibaya zaidi idadi kubwa kuwa ya vijana.

.............Mwisho.............
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
New York - USA
31 Aprili, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiondoka baada ya yeye kuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano unaozungumzia jinsi ya kupata Maendeleo endelevu kwa kukuza ajira na kazi zenye utu (Achieving sustainable development through employment creation and decent work) tarehe 30 Aprili, 2015 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani. 

Al-Shabab suspected in killing of Kampala attack prosecutor Joan Kagezi

Joan Kagezi

KAMPALA, Uganda (AP) — Ugandan police said on Tuesday they are investigating whether the killing of a prosecutor in Kampala late Monday was carried out by Somalia's Islamic extremist group al-Shabab.

Joan Kagezi, a prosecutor in the ongoing trial of about a dozen men facing terror charges, appears to have been the victim of a targeted assassination, Patrick Onyango, a police spokesman in the Ugandan capital, said Tuesday.

There are many possible suspects, including al-Shabab, but it is too soon to make any arrests, he said.

"We cannot rule out al-Shabab ... because that's the major case that she was handling," he said, referring to the trial in Uganda of suspects accused of being involved in the July 2010 bombings here in which more than 70 people were killed while watching a soccer World Cup final on TV.

The U.S. Embassy in Uganda condemned the prosecutor's killing in a statement Tuesday that described Kagezi as a "heroine in the forefront of the fight against crime and terrorism."

"The United States reiterates its support for the Ugandan government's efforts to combat international terrorism, in which Joan Kagezi played a leading role," the statement said. "We stand in solidarity with Ugandans and the Ugandan government as they seek to bring to justice the perpetrators of this heinous crime."

Onyango said Kagezi was shot twice by gunmen after she left her car — in which she was traveling with two of her children on the way home from work — to buy groceries in a Kampala suburb. After shooting her twice in the head and neck, the gunmen fled on a motorcycle during heavy vehicular traffic, he said, citing eyewitness accounts.

The killing has shocked Uganda amid repeated warnings that al-Shabab is plotting fresh attacks in Uganda.

The latest warning, issued last week by the U.S. Embassy, said there was a terrorist threat against locations in Kampala where foreigners often congregate.

Uganda has contributed troops toward an African Union peacekeeping mission in Somalia, the reason al-Shabab cited for carrying out the 2010 attacks.

[video] "Mmejenga shule halafu baadaye mnakuja kujenga maabara, utafikiri hamkuchora ramani!' - "Sugu" BungeniMbunge wa Singida Mhe. Tundu Lissu asema anashangazwa na wanaopinga kuanzishwa kwa mfuko wa Vijana katika Mswada wa Baraza la Vijana.

Akichangia katika mswada huo, Joseph Mbilinyi "Sugu", Mbunge wa Mbeya Mjini alitoa mchango wake kwa kufananisha linaloendelea sawa na ujenzi wa maabara ulioanza mwaka jana katika shule zilizojengwa miaka 15 iliyopita.

Ally Kiba kuangusha show tamasha la Mwana Dar Live chini ya Vodacom TanzaniaMsanii wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na jinsi anavyojiandaa kuwapagawisha mashabiki wake katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka. Wengine katika picha kushoto Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu” na Kiongozi wa kikundi cha Warriors Damian Darada (kulia).Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwatambulisha wasanii wa muziki watakaotumbuiza katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Kiongozi wa kikundi cha Warriors Damian Darada, Mkurugenzi Mtendaji wa On Point Solution Bahati Singh ambao ni wakala wa kinywaji cha Vita Malt Nchini na Meneja Mkuu wa ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho.Meneja Mkuu wa ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili toka kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwatambulisha wasanii wa muziki watakaotumbuiza katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka, kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa On Point Solution Bahati Singh ambao ni wakala wa kinywaji cha Vita Malt Nchini na watatu toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu na Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri "Msaga Sumu"Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka wakionesha mshikamano kwa kushikana mikono pamoja na waandaaji na wadhamini kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo.

Taarifa ya Polisi kuhusu mabadiliko kwa makamanda


31st March 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.

Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu. Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.

Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence Ngonjani. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.
Aidha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ferdinand Mtui aliyekuwa mkuu wa operesheni maalum polisi makao makuu ameenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma.

Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frasser Kashai amehamishiwa Polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Mwombeji. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kihenya Kihenya amehamishiwa polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kati Ilala, Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Satta.

Kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi, mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Kauli ya Gwajima baada ya kuachiwa kwa dhamana

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiingizwa katika gari wakati akitoka katika hospitali ya TMJ na kupelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kupewa dhamana ambapo alitakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kati April 2.
- Asha Bani

Taarifa na: KAROLI VINSENT

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) ni sawa na sikio la kufa ambalo alisikii dawa, baada ya leo kuibuka na kusema haogopi kulitetea tamko lililotolewa na jukwaa la kikristo nchini ambalo linawahamasisha waumini wa dini hiyo kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba, ambapo amesema atalipinga hata kama serikali ikimwekea vikwazo vya aina yoyote.

Kauli kiongozi wa huyo wa Kiroho ameitoa muda huu kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ambapo alipojisalimisha ili kuhojiwa kwa mara ya mwisho baada ya kutoka kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam alipolazwa kutokana na kuugua gafla wakati akiwa kwenye mahojiano na Jeshi la polisi wiki iliyopita.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni na ameachiwa kwa dhamana na jeshi hilo huku akitakiwa kufika katika kituo kikuu cha polisi april 02, 2015 kwa ajili ya kuendelea na mahojiano na jeshi la polisi huku waumani wake kijitokeza na kumpokea Askofu wao. Ambapo amesema hawezi kutishika wala kuyumbika kutokana na vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea wakristo hapa nchini ambao wamewekewa Katiba anayoiita ni mbovu.

“Mimi nimetoka kwa amani nashukuru sana Mungu animeponya salama, ila nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao wanakandamizwa na mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi,”
amesema Askofu Gwajima.

Askofu Gwajima ameongeza kuwa kwa kuwataka viongozi wenzake kuheshimu tamko la Jukwaa la Kikristo na hata yeye mwenyewe amesema ataliheshimu sana.

“Nawaamomba viongozi wa dini wenzangu tuliheshimu tamko hili la kikristo, na endapo tukiwa tofauti tutakuwa tunakwenda tofauti na tunajivunjia heshima kwa jamii ambapo tulionekana kuwa na msimamo mmoja wakati tukilitoa na mimi mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho” 
ameongeza Gwajima.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu afya yake amesema hawezi kuzungumzia afya yake, akawataka waandishi kutoendelea kumuuliza huku akiwataka waumini wake kushangilia kwa ushindi waliupata anadai umetokana na nguvu ya Mungu.

Kabla ya kulazwa katika Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika Hospitali ya Polisi Kurasini na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo yeye na wafuasi wake waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo kuna daktari wake maalumu.


Askofu Gwajima akiwa katika wheelchair.

WhatsApp Call now officially open to all, no invites required, just update to v 2.12.19 - here is the link


The WhatsApp calling feature is working. It opens seamlesly, no questions asked, no invites needed, no hacks required. You only need to update the app to version 2.12.19, which you can find hosted on APK Mirror or on WhatsApp's website.

Once you download the apk file and install it (make sure you have Unknown Sources enabled in your phone's Security Settings to be able to do so), you'll open WhatsApp and the app's UI will have switched over to the new one with the Calls functionality enabled.

Over at the AndroidPolice blog, Rita El Khoury (hat off for the tip) has explored this and noted:

  1. You can initiate a new call to any contact while chatting with them or browsing the list of Contacts, but if their version of WhatsApp is still not compatible, you'll get a warning. 
  2. If you try to call someone who is offline at the moment, you'll hear the phone ring but no one answers and the person will be notified with a missed call the next time they are connected.
  3. While on a call, WhatsApp lets you switch to speakerphone mode and mute your microphone should you need that, and a notification shows up with the duration and the option to hang up. But keep in mind that there no longer is an option to place a network call to a contact when you're inside the app, so you will have to remember to head out to your phone's contact list to do so.

Alleged Tanzanian-Zanzibari ‘Jihadi bride’ stopped on way to Somalia was a medical student, topped high school

Three female suspects whose identities were revealed in court by police yesterday have shattered the long-held notion that Kenyans seeking to join Al-Shabaab are generally from poor or disadvantaged backgrounds.

The young women from Mombasa are accused of trying to cross into Somalia to marry Al-Shabaab militants. Khadija Abubakar Abdulkadir, Maryam Said Aboud and Ummul Khayr Sadir Abdulla were arrested in El Wak town.

The three well-educated women from middle- class families are alleged to have joined Al- Shabaab last September, after being lured by a Syrian female contact through the Internet.

Police claim the three hoped to reach Syria and join Islamic State, a terror group so brutal that even Al-Qaeda’s leader, Ayman al-Zawahiri, disowned it.

The suspects were remanded for 20 days to allow police complete investigations.

Relatives watched in disbelief yesterday as the State unveiled three women in Mombasa it accuses of trying to cross into Somali to join Al-Shabaab and become 'jihadi brides'.

More disturbing to relatives, friends and the security/intelligence community in Coast where two of them are from middle-class families and are all well-educated.

According to reports, Khadija Abubakar Abdulkadir, Maryam Said Aboud and Ummul Khayr Sadir Abdulla joined Al-Shabaab in September last year, after linking up with the group on the internet. They were lured to join the militant group in Somalia by a Syrian female contact.

They were promised marriage to Islamic fighters in Somalia, eventually ending up as widows of Islamic holy fighters in Syria where they hoped to reach through Turkey after flying from Mogadishu.

A State report suggests Umul Khayr, who wore a red shawl in court yesterday, was the mastermind of the recruitment.

Their cellphones and two laptop computers were reportedly seized by police during the arrest after they alighted from a bus in El Wak town on Friday from Nairobi.

The report also claims Ummul Khayr confessed during interrogation by detectives that she was recruited by an Abdulla Ibl Zubeir through a telephone contact in Somalia.

Yesterday, she told relatives that "somebody was supposed to pick us", before the group was arrested in El Wak in Mandera county.

They were unable to connect with Abdulla, whom Kenyan investigators suspect was in Mandera and the alleged Syrian contact.

Intelligence sources indicate Maryam was born in 1990 and was a top student at Burhani Secondary School in Malindi where she scored a grade B in 2008 before proceeding to Kenyatta University. She graduated in 2012 with a bachelor's degree in Commerce.

Khadija was pursuing a bachelor's degree in Pharmacy at the Thika campus of Mount Kenya University after scoring a grade B at Tawir Secondary School in Malindi in 2012, according to a report by police and relatives.

But Mount Kenya University (MKU) has since denied that Khadija is a student at the university. The university's head of corporate communication, identified as Dr Bureti, said the student by the name Khadija was not a student at the institution.

Following the State's request, Senior Resident Magistrate Irene Ruguru allowed police to detain the three girls for 20 days to allow for investigations, which detectives say will extend to Zanzibar, Sudan and Somalia.

Relatives divulged very little about their social lives while the women displayed little emotion in the dock.

The Standard established that one of the suspects made frantic efforts to have her mother erase certain numbers from her cellphone while another wanted her room to be cleared of some documents.

One suspect maintained police arrested them in a group of six women, a claim The Standard could not establish amid reports some of the women travelling with them could have been undercover agents.

It was difficult to ascertain whether the women had displayed any sense of grievance at school or work station although Fatma Said, a sister to Maryam Said, told The Standard she (Maryam) "had complained about low pay at the hospital where she worked and expressed desire to look for a better job".

Ummul Khayr from Zanzibar studies medicine at International University of Africa in Khartoum, according to State documents and Sadir Abdalla Said, who turned up at the Mombasa law courts claiming to be her father.

"She was a third-year student of medicine at the International University of Africa in Khartoum," Sadir Abdalla Said, who alleged he had flown from Oman where he claims to work but a detective indicated the parents of the Zanzibari suspect "are both university lecturers in Sudan".

Sadir claimed he last met Ummul Khayr in Zanzibar in August, last year, and disclosed the woman visited him in Oman in 2011.

Salma Ahmed, Maryam's mother, said her daughter left their Malindi home on March 22 "after asking for permission to go for an interview in Nairobi."

She did not state what interview she was going for but her sister indicated Maryam was disaffected with her low-paying job in a Malindi hospital.

Salma said she spoke with her daughter after she allegedly reached Nairobi the next day but lost contact after her (Maryam's) phone went off after March 25.

Amina Abdulla Aziz, who said she is Khadija's mother, told The Standard she left their home in Malindi by bus on March 20 allegedly to resume studies at the Thika university campus.

Khadija's sister Fatuma said the family lost contact with her on March 24 after her cellphone went dead.

[update] Tanzia! Dk Aleck Che-Mponda aaga dunia

Dr. Aleck H. Che-Mponda
Dk. Aleck H. Che-Mponda

MAZIKO ya mwasisi wa Tanzania People’s Party (TPP), Dk. Aleck Che-Mponda (80), aliyefariki dunia Machi 30, mwaka huu katika hospitali ya Massana jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani ya mifupa, yatafanyika Aprili 7, mwaka huu kijijini kwao Manda wilayani Ludewa, Njombe.
Akizungumzia taratibu za mazishi jana nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach jijini Dar es Salaam mdogo wa marehemu, Bernard Mponda alisema hivi sasa wanaendelea na taratibu za mazishi ikiwa ni pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya kuusafirisha mwili huo kwenda Ludewa.
Alisema kwa sasa msiba upo nyumbani kwa marehemu na watoto wa marehemu wanategemewa kufika nchini kuanzia leo wakitokea Marekani, na kwamba ibada ya kumuaga marehemu itafanywa Jumatatu ijayo katika Kanisa la Mtakatifu Albano lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Aliongeza ibada ya kuaga mwili huo itafanywa Jumatatu saa nne asubuhi kanisani hapo na kisha safari ya kuelekea Manda itaanza na maziko yatafanywa Jumanne kikijini kwao.

Dada Chemi Che-Mponda, binti wa Dk Aleck Che-Mponda, mwanasiasa maarufu na mmoja wa waasisi wa mageuzi ya vyama vingi nchini Tanzania, ametaarifu kupitia blogu yake kuhusu msiba wa kuondokewa kwa baba yake Mzazi

Wadau, ninasikitika kutangaza kifo cha Baba yangu mzazi, Dr. Aleck H. Che-Mponda, kilichotokea katika hospitali ya Massana mjini Dar es Salaam, jana jioni (March 30, 2015). Mipango ya mazishi inafanyika. Alikuwa anumwa ugonjwa wa Saratani (Cancer ya Mifupa).

Habari ziwafikie ndugu na marafiki wote popote walipo.

Rest in eternal peace, Dr. Aleck H. Che-Mponda (1935-2015)

Dk Che-Mponda alianzisha Tanzania Peoples Party (TPP). Pia, alifanya utafiti muhimu kuhusu mgogoro kati ya Malawi na Tanzania kuhusu Ziwa linalopakana na nchi hizo mwaka 1971 kwa ajili ya PhD yake katika Chuo Kikuu cha Howard, ''The Malawi-Tanzania Border and Territorial Disputes, 1968: A case study of Boundary and Territorial Imperatives in the new Africa".0

Maoni ya Malisa na Mtatiro baada ya Makonda kumtaka Gwajima kwa mahojiano

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akimjulia hali Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aliyelazwa Hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu baada ya kupata mshituko katika mahojiano na polisi akituhumiwa kutoa lugha isiyofaa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
Dotto Mwaibale

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa amemwandikia Gwajima barua akimwita ofisi kwake, jana mchana alimtembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali kiongozi huyo lakini akasisitiza kuwa nia yake bado ipo palepale.

“Nilimtaka leo aripoti ofisini kwangu lakini kwa bahati mbaya anaugua na amelazwa. Nitakwenda kumuona ili nijue hali yake ikoje,” alisema Makonda kabla ya kufunga safari kwenda hospitali alikolazwa.

Alisema pia atataka kiongozi huyo wa kiroho amweleze anavyoelewa maana ya uhuru wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba, usajili wa taasisi yake na katiba ya taasisi hiyo.

“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.

Baada ya kauli hiyo, mijadala kadhaa iliendelea katika mitandao ya kijamii hususani Facebook na Twitter ambapo baadhi ya wananchi walitoa maoni yao wakishangaa na kuhoji uhalali wa DC kutaka kuhoji masuala ambayo yako chini ya mamlaka nyingine kisheria. Yafuatayo ni moja ya maoni hayo yaliyoandikwa kwenye kurasa zao za Facebook.

JULIUS MTATIRO...

YA GWAJIMA vs PENGO
“Polisi wanamuhoji mtuhumiwa ili waone kama ana kosa la kumshitaki au la, hapohapo Mkuu wa Wilaya husika naye anamuandikia barua kumtaka aripoti kuhojiwa na Mkuu wa Wilaya.
Hakuna Sheria wala Kanuni inayompa mamlaka Mkuu wa Wilaya kujihusisha na upepelezi au ufuatiliaji wa makosa ya jinai. Ni kupoteza muda tu kwa wakuu wa wilaya wanapojaribu kuwaita watuhumiwa wakawahoji, labda pia ni kutojua nini kimewaweka kwenye zile ofisi.
Pamoja na mimi kutokukubaliana na ujengaji hoja wa matusi uliotumiwa na Mchungaji GWAJIMA kumfikishia ujumbe Kadinali Pengo, namshauri Gwajima asiitikie wito huu wa rafiki yangu, mdogo wangu na kijana mwenzangu DC wa Kinondoni, PAUL MAKONDA, na DC hatakuwa na cha kufanya.
Wakuu wa wilaya wanahitaji mafunzo zaidi juu ya kazi yao vinginevyo nyadhifa hizi zifutwe tubaki na wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri. Kwa sababu wakuu wa wilaya wamekosa kazi, sasa wameanza kujishughulisha na upepelezi wa makosa ya jinai. Sina mbavu hapa....”

GODLISTEN J MALISA...

MAKONDA ACHANA NA GWAJIMA, SHUGHULIKA NA YANAYOKUHUSU.!
“Nimecheka sana baada ya kuamka na kukuta Habari kwenye media kuwa eti Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndg.Paul Makonda amemtaka Askofu Gwajima akaripoti kwake haraka iwezekanavyo mara tu baada ya kutoka Hospitali kwa ajili ya mahojiano.
Hahahaah hiki ni kituko cha mwaka. Mahojiano gani Makonda anataka kumfanyia Askofu Gwajima? Kwamba Makonda nae amekuwa Afisa Upelelezi wa jeshi la Polisi au?
Navyoelewa ni kuwa swala la Gwajima ni Criminal Defamation. Ndio maana Jamhuri ikaingilia suala hilo. Na kwa utaratibu wa criminal case ni kuwa Polisi wanafanya upelelezi wao then State Prosecutor anasimama mahakamani dhidi ya mtuhumiwa.
Sheria zote na machapisho yote ya kisheria yanazohusika na Defamation cases kwa nchi yetu (Defamation Law in Tanzania; Leading Statutes, Cases &Materials) hakuna hata moja inayotoa mandate kwa Mkuu wa Wilaya kufanya upelelezi au kuhoji.
Sheria ya Kanuni za Adhabu Tanzania (Penal Code) haitoa mandate hiyo. Wala sheria ya Magazeti (Newspapers Act, 1976), wala sheria ya utangazaji (Broadicasting services Act, 1993, wala sheria ya mwenendo wa makosa ya madai (Civil Procedure Code, 1966) wala Sheria ya Ushahidi (The Tanzania Evidence Act, 1966).
Hizi zote ni sheria zinazodeal na defamation na hakuna hata moja iliyogrant mandate kwa mkuu wa wilaya kuhoji wala kupeleleza. Wala hakuna sheria kati ya hizo nilizozitaja inayosema "Polisi wakishafanya upelelezi Mkuu wa wilaya amuite mlalamikiwa ili ajiridhishe"
Sasa najiuliza logic ya Makonda kumuita Gwajima kwa mahojiano ni nini? Kwamba anadhani yeye ana nguvu kuliko Polisi? Kwamba anadhani Polisi hawawezi kufanya upelelezi kwa ustadi mkubwa kama yeye? Kwamba haamini upelelezi unaofanywa na jeshi la Polisi?
Kweli ujinga ni kipaji. Yani kabla hata Polisi hawajamaliza upelezi wao wewe ushakurupuka unataka Gwajima akuone? Akuone ili iweje? Kama ni kuhojiwa ameshahojiwa na Polisi na kama atapatikana na kesi ya kujibu atapelekwa Mahakamani. Sasa wewe unataka akuone ili iweje? Aje akuombee toba au?
Nadhani Polisi wamzuie huyu "DC wa miezi 6", maana anaweza kuharibu upelelezi unaoendelea kwa kutafuta "cheap popularity".
Sijawahi kusikia popote duniani, DC anaingilia kesi ambayo upelelezi wake haujakamilika. Hata upelelezi ukikamilika kesi haipelekwi kwa DC inapelekwa mahakamani. Sasa huyu Makonda kapata wapi "kiherehere" cha kumuita Askofu Gwajima.
Au labda anataka kutubu? Lakini hata kama anataka kutubu angesubiri kwanza Gwajima atoke hospitali, kisha amuite waongee. Sio kuandika mitandaoni na kutangaza kwenye vyombo vya habari eti Gwajima akitoka amuone.
Gwajima yupo ICU, wewe unatangaza kwenye media eti akitoka akuone.. hii ni akili au matope? Unadhani huko ICU Gwajima anasoma blogu na kusikiliza "Radio Mbao" kama ulivyozitumia kutoa agizo lako? Acha "akili ndogo" kijana.!
Wakati fulani Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freeman Mbowe aliwahi kusema wakuu wa wilaya hawana kazi ndio maana muda mwingi wanatumika kisiasa au kuingilia mambo yasiyowahusu. Mbowe alisema wakuu wa wilaya wana kazi mbili tu kubwa "Kufungisha ndoa na kuandaa vyeti vya vizazi na vifo."
Hii ya vizazi na vifo kwa sasa inafanywa na RITA, so kwa mujibu wa Mbowe wakuu wa wilaya wamebaki na kazi moja kubwa ambayo ni KUFUNGISHA NDOA. Sasa najiuliza hivi Kinondoni hakuna watu wanaofunga tena ndoa zao Bomani ili Mkuu wa wilaya apate kazi za kufanya? Maana Makonda anaonekana hana kazi ndio maana anaanza kuingilia hadi mambo ya kisheria ambayo hayajui kabisa. Yani kwenye sheria "this guy is typical tabularasa/layman"
Nashauri kama Makonda hana kazi ya kufanya ashughulike na usafi wa mazingira maana manispaa ya Kinondoni bado usafi hauridhishi, asimamie halmashauri izibue mitaro ya maji taka, na kuzuia manyanyaso kwa wafanyabiadhara wadogo. Haya masuala ya kisheria aachane nayo maana hayamhusu kabisa na hayawezi.!
Wasalaam,”

"Waumini waamue wanavyoona inafaa bila kushinikizwa" - Kikwete


Hotuba ya Rais Kikwete kwa Viongozi wa Dini

Why's Kenya represented by Chinese at Venice Biennale? Read this...

  • The following article has been adopted from the NPR "as is"
In The Shame In Venice 2, Kenyan artist Michael Soi protests the makeup of his country's pavilion at the Biennale.Courtesy of Michael Soi

There's something sketchy at this year's Venice Biennale — the international art exhibition sometimes dubbed the Olympics of the contemporary art world.

When you come to the Kenyan pavilion, almost all of the artists will be ... Chinese.

The Biennale, one of the oldest and most important exhibitions of contemporary art in the world, takes place in Venice every two years. Thirty countries, including the U.S., have a permanent slot.

About 50 other countries have applied for their own exhibition space, called a pavilion. The East African country of Kenya hosted its first pavilion in 2013 and plans to host another this year, featuring mainly Chinese nationals. None of them have apparently ever been to Africa or reference it in their work.

The controversial roster — including contemporary artists Qin FengShi Jinsong,Li ZhanyangLan Zheng HuiLi Gang, and others — has provoked outrage among Kenyan bloggers and artists. It's also provoked a sense of deja vu — the same thing happened in 2013. Kenya's first-ever pavilion was also overwhelmingly Chinese.

"I was a member of the jury for the last Biennale in 2013 and the Kenyan Pavilion was shambolic," writes Olabisi Silva on Facebook. The founder and director of the Centre for Contemporary Art in Lagos, Nigeria, wrote that the Kenyan pavilion was "full of Chinese and Italian artists with some [Kenyan artists] in a dark room."

"A frightening manifestation of neocolonialism vulgarly presented as multiculturalism," wrote Wenny Teo in a critique of the 2013 exhibit, "to be avoided like the plague."

In Nairobi, where the Kenyan contemporary art scene is gaining traction with serious art buyers, the news is being felt not just as an artistic flop but as a colossal missed opportunity. "It's a kick in the stomach," says Sylvia Gichia, director ofKuona Trust, an artist's collective and residency program in Nairobi. Organizations like hers work hard to bring Nairobi's artistic renaissance to a global audience via art fairs and art auctions.

Needless to say she is dismayed that the 370,000 art lovers who visit the Biennale will see none of the work that's driving the contemporary Kenyan scene. "What," Gichia asks, "do the Chinese have to do with visual arts in Kenya?"

Nobody in Kenya's government will answer that question. (Calls and texts to the personal cellphone of Nairobi's minister of culture, Hassan Wario, went unanswered.) In most countries, the government either selects the artists or assigns that duty to a private gallery. In Kenya, the government apparently played no role other than to fob off the job to an Italian curator, Paola Poponi.

Poponi cannot say she has ever set foot in Kenya, but her official title is "commissioner" of the Kenyan pavilion, the same title she held in 2013. She defended the choice of artists, in an email liberal with capitalizations, saying that the Kenyan pavilion ably expressed the international theme of this 56th Biennale, which is All The World's Futures.

Poponi wrote, "Talking about art FROM ANOTHER PART OF THE WORLD during an art exhibition can be useful for KENYA, always more able to create its OWN IDENTITY." She said that art should not be constrained by geography and explained in a follow-up email that "MEETING THE REST OF THE WORLD" would enable Kenyan artists to analyze their own experiences "more deeply." 


But if Poponi's goal is to expand the vision of Kenyan artists and have them "meet" the rest of the world, what better way than to invite Kenyans to the Biennale exhibition?

Poponi wrote back to say that the pavilion does feature Kenyans. Two of them. The one ethnic Kenyan in this pavilion — Yvonne Amolo, who has won awards for her film about racism — lives in Switzerland and has no connection to the contemporary Kenyan art scene.

The other Kenyan citizen is a 72-year-old Italian-born painter, sculptor and real estate magnate who has lived in the Kenyan coastal town of Malindi for nearly a half a century. Armando Tanzini sits at the heart of this controversy, because he's the only artist whose work has appeared in both the 2013 and 2015 Kenyan pavilions.

On his Facebook page, Tanzini describes what he is all about:

"I love Africa, I love it with its endless qualities and its anful defects, I love it because it's innocent and poor, I love it like I love all my neighbors, also the rich one, but the poor — uncomfortable — are signals. Why don't we turn our head to this forgotten world placed under Equator? Why don't we try to help them to make concrete the huge richness of their land and their souls? Not as missionaries, but as smart and sincere managers, ready to give and receive. I've been working with them for 30 years, testing several irrational economies such as tourism, agriculture, handcraft, estate activities and so on. I discovered that only magic of creativity could face those economic appalling emergencies, especially in artistic and scientific fields."

I sat down with Tanzini last week in a cafe in Nairobi to understand how the pavilion had come to be. He spoke proudly of the art workshops he holds for Kenyan children at his exclusive beachfront lodge. He described with awe his adopted hometown, Malindi, where he first bought property in the late '60s. That was long before the town would become known as Kenya's "Little Italy" for its palatial Italian resorts frequented by Formula One racers and celebrity politicians.

Tanzini, a prominent figure in this Italian scene, doesn't mingle much with Kenya's contemporary artists. But when I asked him about the controversy around Kenya's pavilion, he explained that if not for his efforts, Kenya would not have any pavilion at all.

"The government of Kenya, they don't know about this important exhibition, the Biennale," he says. "I try several times to help them to understand."

Finally, in 2013, with the government's approval, he paid hundreds of thousands of dollars to get Kenya a pavilion and organize the show. This year he says it wasn't solely his money. He had other private sponsors. But again, no funding was forthcoming from Kenya's government. "Unfortunately, if I want to bring Africa, or Kenya, I must compromise in some way," he said. "Compromise because we have no[t] the money."


Tanzini wouldn't elaborate on what this compromise was, or where the additional money had come from, or if the commercially successful Chinese artists in the pavilion were invited because they, too, could also pay their own way.

But if you were tasked with organizing a show in Venice and you wanted to find artists with the money and incentive to chip in on the sizable entrance fee, you would do well to look to the Chinese. Davide Quadrio, a curator of Chinese contemporary art at Arthub Asia in Shanghai, says he knows "many artists" that "buy their introduction to Venice. And they don't even care about the venue anymore. Or the credibility of the show."

The reason, he explains, is the outsized value of the Venice imprimatur to domestic Chinese collectors. Chinese artists can sell their work for more money if they can say they've shown in the prestigious biennial exhibition.

"Somehow Venice became a sort of brand for many organizations in China to position their artist inside China," he says. "The value that Venice represents in contemporary art for China? Is actually the China market."

That doesn't make Kenyan artists feel any better. Even Tanzini admits that he feels "guilty" and "sad" because he would like to bring other Kenyan artists than himself.

When I asked him which artists he would have liked to bring, I expected him to name a leading Nairobi-based artist like Peterson Kamwathi or Sam Hopkins orMiriam Kyambi.

Instead, he gestured to his young Kenyan secretary, Sarah, sitting next to him on the couch. (Moments earlier, while Tanzini had been using the restroom, she had told me that she wasn't an artist but had quite enjoyed participating in some of Tanzini's workshops.) "She has such talent," Tanzini insisted. She does "amazing work with rubber."

A petition circulating on Change.org, titled Renounce Kenya's fraudulent Representation at 56 Venice Biennial 2015, proclaims that "a group of well connected persons, who lack neither the intellectual nor creative capacity to represent Kenya's contemporary art to the international arena, are posturing to the world as the Kenyan Pavilion at the 56th Venice Biennial in Italy."

The Biennale would not respond to requests for comment. When the exhibition opens on May 9, participants will have to contend with Kenyan protesters, who say they'd rather have no pavilion at all than one that doesn't represent their country. Novelist Binyavanga Wainaina told me that "we have people there, watching out for it, watching out to document it."

He was quick to point out that his issue is not with the Biennale nor with Tanzini but with Kenya's Ministry of Culture — and Kenya's dismissive attitude toward the arts.

"That this parody could happen two years ago was already far from excusable," Wainaina said. That it would happen a second time, without government comment, he says, is "farcical."

Mapitio ya magazeti katika Tv mbalimbali Machi 31, 2015

Ufafanuzi wa Polisi kuhusu silaha zinazomhusu Gwajima
Leo tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe 29/03/2015. Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za Short Gun.

Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:

Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha kwamba silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat Gwajima. Kuhusu risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima anamiliki Bunduki aina ya Short Gun yenye namba 102837 ambayo inatumia risasi za aina ya hizo zilizokamatwa.

Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea. Aidha watu hao pia wanahojiwa kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi zilizotajwa hapo juu wakati wao sio wamiliki halali za silaha hiyo na risasi hizo na idadi iliyotajwa kwa mujibu wa sheria.

Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi litapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
S. H. KOVA,
DAR ES SALAAM.

Various job opportunities in Tanzania at Etihad Airways


Please click on the highlighted job title for details.

TitleDepartmentCityCountryDate Added Date Added

Airport Duty ManagerAirport OperationsDar es SalaamTANZANIA19 March 2015

Airport ManagerAirport OperationsDar es SalaamTANZANIA19 March 2015
Airport Operations OfficerAirport OperationsDar es SalaamTANZANIA19 March 2015
Driver/MessengerGlobal SalesDar es SalaamTANZANIA1 March 2015
Marketing CoordinatorGlobal SalesDar es SalaamTANZANIA1 March 2015
Office CoordinatorGlobal SalesDar es SalaamTANZANIA1 March 2015
Reservation and Ticketing AgentGlobal SalesDar es SalaamTANZANIA1 March 2015
Reservation and Ticketing SupervisorGlobal SalesDar es SalaamTANZANIA1 March 2015
Sales RepresentativeGlobal SalesDar es SalaamTANZANIA1 March 2015
Sales Support AdministratorGlobal SalesDar es SalaamTANZANIA1 March 2015
At the time of publishing this ad, application deadline for these jobs was marked for April 17th, 2015.