Taarifa ya Habari Channel TEN Juni 30, 2015Namtafuta Mama Kaboga (Vaileth Johnson) au Kaboga mwanangu

Ujumbe huu umetumwa na mwenzetu kwenye barua pepe, tafadhali ikiwa una msaada wowote tuachie katika kisanduku cha maoni au ukurasa wa "contact

Namtafuta Mama Kaboga (Jina lake halisi ni VAILETH JOHNSON) au Kaboga mwenyewe. Huyu mama alikuwa akiishi Kurasini miaka ya 1998 hadi 2000, baadaye alihamia keko mwaka 2001 jirani na Gereza la Keko, na baadaye akahamia Keko Toroli miaka ya 2003, na Mwaka 2004 nikasikia amehamia Iringa Mfundi na mme wake amabye hata hivyo sikujua alikuwa akifanya kazi gani.

Mama huyu ni mzaliwa wa Tanga, Handeni na alikuwa na kaka yake ambaye jina lake pia sirikumbuki ila naye aliishi keko na mke wake.

Kwa nini namfafuta?
Namtafuta mama huyu kwa sababu, nilizaa naye mtoto wa kike na kila nilipotaka kuchukua mwanangu alikataa na wakati huo nilikuwa sijaoa, baadaye nilisafiri na kwenda nje ya nchi nikawa sina mawasiliano naye na hakuwa na mawasiliano - alipopata simu tuliendeleaa kuwasiliana na baadaye akabadilisha namba na tukawa hautuwezi tena kuwasiliana.

POPOTE ALIPO YEYE AU KABOGA NAOMBA ANITAFUTE kwa email: [email protected]

NIKO NCHINI SASA KWA MDA WA MIEZI MITATU HADI AUGUST NARUDI NJE.

Regards,
Patrick

Mbatia ajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga KuraMbunge wa kuteuliwa, Mhe. James Mbatia akiwasili katika kijiji cha Kirua Vunjo Magharibi na kupokelewa na msaidizi wake Hamis Hamis kwa ajili ya zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia BVR.Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. James Mbatia akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasil katika kijiji cha Kwamare kata ya Kirua Vunjo Magharibi Jimbo la Vunjo kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.Mbunge James Mbatia akitoa maelezo yake kwa mmoja wa maofisa wa zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kupita mfumo wa BVR.Mbunge James Mbatia akichukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la uandikishaji katika kijiji cha Kwamare kata ya Kirua Vunjo.Mhe. Mbatia akitia saini katika kifaa kimoja wapo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu.Mhe. Mbatia akiweka vidole gumba kwa ajili ya kuchukuliwa alama.

Afisa uandikisha akimkabidhi Mh Mbatia kitamburisho chake mara baada ya kumaliza zoezi la uandikishaji.Mhe. Mbatia akionesha kitamburisho maalumu kwa ajili ya zoezi la kupiga kura litakalofanyika hapo baadae mwezi oktoba.

Msaidizi wa Mh Mbatia ,Hamis Hamis akikabidhiwa kitamburisho chake mara baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
 • Tumeshirikishwa taariaf hii na Dixon Busagaga 

Wananchi wadai hawajafiwa na Mbunge wao

Sakata la Mbunge wa jimbo la Geita Marehemu Donald Kelvin Max kuzikwa jijini Dar es Salaam pasipo wananchi wake kupata fursa ya kuaga mwili wake limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wakazi wa jimbo la Geita Wilayani Geita, wakiwemo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, kukana kufiwa na mbunge wao kwa kile walichodai alikuwa mwakilishi wa eneo alikozikwa huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Geita kikidai hakuna kanuni zinazolazimisha mbunge kuzikwa kwenye jimbo lake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Malunde1 blog, ikiwa ni siku moja tangu mbunge wao kuzikwa, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wananchi huku wakionekana kukerwa na jambo hilo walidai kuwa, wanachojua mbunge wao yuko hai na iwapo angekuwa amefariki dunia angeletwa Geita kuagwa na wananchi wake.

Neema Steven Chozaile mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Geita alidai kuwa, kitendo kilichofanywa na chama cha mapinduzi cha kuruhusu mbunge wa Geita kuzikwa kimya kimya jijini Dar kimewafumbua macho wananchi na kwamba safari hii hawatafanya makosa katika kuchagua mwakilishi wao.
‘Tumepata fundisho kwamba tunapochagua mtu tuwe makini,tunayemtambua alipozaliwa,ni mtoto wa fulani maana haiwezekani mbunge wa Geita asiletwe hapa akaagwa na waliomchagua tena kwa kura nyingi, kama CCM wanaruka na helikopta kuhudhuria sherehe za mtia nia Monduli walishindwa kutumia usafiri huo kuleta maiti ya mbunge wetu akaagwa hapa kisha wakamzika watakapo, ndiyo maana tunasema huyo hakuwa mbunge wetu bali wa Dar alikozikwa’
alisema.

‘Mwaka 2010 niliamka alfajiri kwa ajili ya kuwahi foleni ili nimchague mbunge wangu Max,nikafanikiwa..nilivyosikia kwamba amekufa sikuamini ikanibidi nianze kutafuta msiba ulipo hadi mtaa wa Katoma wanakodai ni nyumbani kwake’
‘Lakini hakukuwa na dalili za msiba zaidi ya mikusanyiko ya wanaojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR,l akini wakati nikiendelea kuhangaika nijue msiba ulipo ndiyo nilipoelezwa msiba uko Dar na atazikwa huko..hii imetudhalilisha sana wakazi wa Geita’
alisema Fidelis Kanani mkazi wa Nyerere Road.

Zephania Mussa ambaye ni mkazi wa mtaa wa Nyanza Kalangalala mjini Geita, alisema 
‘Sisi Geita walishatudharau maana watu wa kuja ndiyo wanachukuwa uongozi,mfano marehemu Max alitudanganya ni mkazi wa Geita,tutamchagua tena nkwa kishindo tukiamini ni mwenzetu’‘Kitendo cha mbunge wetu kuzikwa nje ya hapa na bila kuagwa na waliomchagua kimetuuma sana na huu ndiyo mwisho kwa wanaGeita kuendelea kuwa shamba la bibi,kwa sasa mtu atakayekuja kutuomba ridhaa ya kutuongoza tutamtaka atupeleke nyumbani kwao,tujuwe ukoo wake na mpaka alipozikwa babu yake maana tulkijipanga tumzike mbunge wetu kwa heshima zote kumbe anazikwa Dar imeumiza sana nasoi tunasema waliomzika ndiyo waliomchagua wetu hajafa bado’
alisema Mussa.
‘Sisi kama Wanageita hili jambo limetuchanganya na ndiyo maana tunasema hatujafiwa na mbunge wafiwa ni wakazi wa Dar, haiwezekani mtu tuliyemwamini kama mwakilishi wetu azikwe kimyakimya sisi tuliopigwa mabomu ajili yake tusimuage na kwa nini azikwe huko,inamaana alitudanganya ni mkazi wa Geita ili hali sivyo?’
alihoji Lucas Charles mkazi wa mtaa wa Moringe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita Kamanda Alphonce Mawazo akitoa maoni yake alisema
‘Maoni yangu ni kwamba tumehadaiwa,mimi nilitoka mbeya kumzika mbunge wangu nikiwa sina shaka atazikwa Geita,kumbe tulichagua tulichagua mtalii na ndiyo maana alitelekeza jimbo kwa muda mrefu akiwa hajaanza kuugua maradhi yanayomsumbua. Mbunge ni lazima awe na uhusiano wa ardhi ya pale anapowakilisha awe na wajomba, dada, shangazi, babu zake, watu aliocheza nao utotoni,aliosoma nao,angalu awe anaguswa na damu ya pale, lakini sisi wana Geita tulichagua kwa ushabiki na hatukujua kwamba tulichagua mtalii’
Msiba huu umetufumbua macho na umetufundisha mambo mengi kwamba inatubidi tutambue kwamba Ubunge ni Uchifu na Chifu hawezi kutoka eneo jingine,lazima atoke eneo lilelile alilozaliwa maana kama mimi nilitegemea niwape pole ndugu zake ,mama, mke wake na ndiyo maana nikatoka Mbeya kuwahi mazishi harafu nikakuta hata harufu ya msiba hakuna’
‘Kwa kweli wana Geita tumejisikia vibaya na sisi wananchi tujifunzekwani na maendeleo hayaji kwa kuchagua mtu asiye mkazi,kwani angekuwa mkazi ningempa mkono wa pole shangazi yake lakini hakuwepo,nimekuja Dar napo sikufanikiwa maana sikujua hata msiba uko wapi,’
alisema Mawazo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo alidai kuwa, maiti ni ya familia ya Max na hakuna kanuni kwenye chama chao cha Mapinduzi (CCM) zinazowalazimishwa azikwe eneo alilokuwa akiliwakilisha kama Mbunge.
‘Anayehoji kwa nini Mbunge wao hakuzikwa Geita,mwambie kuwa maiti siyo ya ccm ni ya familia ambayo ndiyo ilitoa ratiba ya wapi azikwe,mi sidhani kama kuna sababu ya yeye kuzikwa Geita wakati kwao ni Dar es Salaam na ndugu zake wengine wamezikwa huko,kama wanasema walimchagua kwa kishindo na wanashangaa kuona hakuzikwa Geita waulize wakati anaumwa nani aliyekwenda kumsalimia kwa kishindo?’
alisema Musukuma.

Mbunge Max alifariki juni 23 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa zaidi ya mwaka mmoja akisumbuliwa na kansa ya Ubongo kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo alipatiwa matibabu nchini India kabla ya kurudishwa hapa nchini. Alikuwa mbunge wa jimbo la Geita tangu mwaka 2010 hadi mauti yanamkuta na amezikwa Juni 27, 2015 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 • Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Malunde 1

Rais Kikwete amteua Ngonyani kuwa Mkurugenzi Mtendaji STAMICO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico). Uteuzi huo umeanza Jumapili iliyopita, Juni 28, 2015.

Taarifa ya kuthibitisha uteuzi huo iliyotolewa Ikulu, Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) leo, Jumanne, Juni 30, 2015, inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Mhandisi Ngonyani alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Migodi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico. 

Mhandisi Edwin Ngonyani ni mhandisi wa migodini mwenye uzoefu wa muda mrefu wa sekta ya madini. Anayo shahada ya kwanza ya fani hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Zambia na shahada ya uzamili (MSC) kwenye fani hiyo hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Exeter, Camborne School, Uingereza.
Mhandisi Ngonyani amefanya kazi nzuri wakati anakaimu nafasi ya Ukurugenzi Mtendaji na kwa kumteua, Rais Kikwete ana imani kubwa kuwa ataendeleza kazi hiyo nzuri ya kuimarisha uwekezaji wa umma katika sekta hiyo ya madini kupitia Stamico.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

30 Juni, 2015

Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa hatia ya kumuua albino Henry Mwakajila

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).

Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso Kalonge (wakazi wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje), na Leonard Msalage Mwakisole na Hakimu Mselem Mwakalinga (wakazi wa Kiwira wilayani Rungwe).

Mshtakiwa wa nne, Mawazo Philemon Figomole, ameachiliwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasi na shaka kwamba alihusika katika mauaji hayo.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya mauaji yenye kumbukumbu Namb. KIW/IR/49/2008 na PI 5/2013, Jaji wa Mahakama Kuu Dk. Revila, amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka kwamba washtakiwa hao wanne walitenda kosa hilo na hivyo wanastahili adhabu hiyo.

Hii ni kesi ya saba ya mauaji ya albino kutolewa hukumu ambapo mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 15 wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa.

Ililezwa mahakamani hapo kwamba, mnamo Februari 5, 2008 majira ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni huko katika Kijiji cha Ilolo, Kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe, wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, washtakiwa hao walimteka nyara kijana Henry Mwakajila, ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Ukukwe na kisha kumuua.

Wakati wa mwenendo wa kesi, ilielezwa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwamba mshtakiwa wa kwanza Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga ambaye ni mganga wa jadi, mkazi wa Kijiji cha Mbembati, Wilaya ya Ileje, alikutwa na utumbo unaodhaniwa kuwa wa binadamu na ulipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ukathibitika kwamba ni utumbo wa marehemu Henry.

Mshtakiwa wa pili, Gerard Korosso Kalonge wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje alikutwa na vidole vinne na mifupa kumi (10) vyote vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu na baada ya uchunguzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali ilibainika kwamba ni viungo vya marehemu Henry Mwakajila.

Ilielezwa pia kwamba, washtakiwa Leonard Msalage Mwakisole, Mawazo Philemon Figomole na Hakimu Mselem Mwakalinga ndio waliodaiwa kumteka nyara mtoto huyo na kumuua, kisha kupeleka viungo kwa mganga wa kienyeji Asangalwisye Kayuni.

Mshtakiwa wa tano, Hakimu Mselem Mwakalinga, tayari alikwishahukumiwa kunyongwa katika kesi nyingine ya mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake.
Hukumu ya kesi hiyo namba 131/2012 ilitolewa Novemba 13, 2013 ambapo inaelezwa kwamba watuhumiwa walitenda kosa hilo Mei 19, 2011 katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Ingawa watuhumiwa walikuwa wanne, lakini Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya chini ya Jaji Samwel Karua iliwahukumu kunyongwa mpaka kufa mshtakiwa wa kwanza Hakimu Mwakalinga na mshtakiwa wa pili Daudi Mwasipasa kwa maelezo kwamba walihusika moja kwa moja na mauaji hayo ya kukusudia.

Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye alitiwa hatiani kutokana na kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji wakati mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela alitiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika katika mauaji hayo ingawa hakusika na kitendo hicho moja kwa moja, hivyo wote wawili walihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Hata hivyo, Myovela tayari alikwishahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria.

Inadaiwa kwamba, chanzo cha mauaji hayo ya John Mwankenja, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe, kilitokana na kiongozi huyo kufahamu kwamba hao ndio waliomuua mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila, hivyo aliuawa ili kupoteza ushahidi.

Taarifa ya CHADEMA kuhusiana na kuahirishwa zoezi la BVR Dar, Pwani

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO KUHUSU KUAHIRISHWA KWA MUDA WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA “BIOMETRIC VOTERS REGISTRATION” (BVR) KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NA MKOA WA PWANI


Kufuatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuutangazia umma kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura liliokuwa lianze tarehe 04/07/2015 kwa Jiji la Dar es Salaam na tarehe 25/06/2015 kwa mkoa wa Pwani kwamba limeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa tena; Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda Pwani (Mikoa ya Temeke, Kinondoni, Ilala na Pwani) kinaitaka Tume ifanye yafuatayo:

 1. Tume ya Uchaguzi itangaze tarehe ya kuanza zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani baada ya kuahirishwa ili kuwasaidia wananchi kujipanga kwa zoezi zima la uandikishaji.
 2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi izingatie mfumo wa kiuchumi na kimazingira uliopo katika mikoa hii unaowafanya watu wengi muda wa mchana kuwepo makazini/katika shughuli za kiuchumi. Na kupanga muda wakutosha kwa kuzingatia idadi ya wakazi. Hii ni pamoja na kuzingatia kuwa Jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani pekee, kwa takwimu za serikali, vina wapiga kura wapatao asilimia 15 ya wapiga kura wote nchini.
 3. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ihakikishe changamoto zote zilizotokea sehemu mbalimbali zinapatiwe ufumbuzi kabla ya zoezi halijaanza Dar es Salaam na Pwani. Changamoto hizi ni pamoja na; mashine kuwa mbovu, idadi ya mashine kutokukidhi mahitaji, idadi ya vituo kwenye kata kutoendana na idadi ya wanaotakiwa kujiandikisha, utaratibu wa kuchukua majina bila kuzingatia waliopanga mistari, na waandikishaji kutokuwa na uwezo thabiti wa kutumia mashine za uandikishaji. Uzoefu umeonyesha kuwa, changamoto hizi zimeendelea kujirudiarudia katika sehemu nyingi bila kutolewa ufumbuzi wa uhakika na Tume ya Uchaguzi.
 4. Tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweka wazi mbele ya umma kuwa Jeshi la Polisi halihusiki katika kupanga utaratibu wa BVR hali inayosababisha vurugu na ukosefu wa amani vituoni. Uzoefu uliopatikana wakati wa ziara za viongozi wakuu wa chama kukagua zoezi la BVR katika maeneo mbalimbali unaonesha kuwa maeneo yote ambayo polisi hawakuwepo vituoni wakati wa uandikishaji, utaratibu ulikwenda kwa utulivu lakini hali imekuwa tofauti kabisa kote ambako jeshi hilo limehusika kusimamia uandikishaji. Mf; Arusha Tunapeda kusisitiza kuwa; CHADEMA haitofumbia macho mikakati yoyote itakayoonekana ina dhamira ya kudhoofisha zoezi la uandikishaji ambayo itasababisha kuwanyima wananchi haki ya kikatiba ya kupiga kura, maana bila kujiandikisha mtu hawezi kupiga kura.

Mwisho, CHADEMA inapenda kuwahamasishwa wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la uandikishaji litakapoanza katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Asanteni!
IMETOLEWA NA
Mhe. MABERE N. MARANDO
MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA PWANI

Namtafuta "Mama Subi" alikuwa Muuguzi Mafinga Hospitali

Ujumbe huu umetumwa na mwenzetu kwenye barua pepe, tafadhali ikiwa una msaada wowote tuachie katika kisanduku cha maoni au ukurasa wa "contact

Kuna mtu namtafuta. Alikuwa staff nurse Mafinga hospital na akiishi Jones corner. In June 1984 alinipokea nyumbani kwake na nikamkuta pia mdogo wake wa kiume (whose name I can't remember) na sote tulikuwa tunaingia JKT Operation Nguvu Kazi. At that time she had a daughter nafikiri 3 to 5 years old called Subi (I guess it was short for Subilaga or Subira). Nikiwa jeshini wakati wa mafunzo ya kivita I got injured na nikalazwa Mafinga hospital kwa zaidi ya mwezi na wakati huo wote alikuwa hakosi kuja kunivisit wodini na quite often akiniletea chakula. Unfortunately, mara tu baada ya kuwa discharged nilihamishwa kambi na a few months later nikaondoka nchini.

Kwa nini namtafuta?
She was one person who happened to be extremely kind and generous and I have always wanted to meet her again, if only to say I wasn't that unthankful monster ambaye anatoweka bila shukrani.

Nilikuwa introduced kwake na family friends - Mr and Mrs Kihongo waliokuwa Mwanza in the '70s and '80s who felt I would be vulnerable as a young boy in a distant region and who, sadly, I can no longer trace.

I will be traversing the southern highlands this summer and so if she is anywhere within the area I would like to stop over and say thank you.

Kassim

Maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua moja ya nguzo za barabara za juu flyovers katika maingilio ya Daraja la Kigamboni. Katika eneo hilo kutajengwa barabara za juu ili kuruhusu magari kupita kwa urahisi wakati wa kuingia na kutoka katika daraja hilo.

Utapeli kwenye Mpesa kupigiwa simu umeingiziwa fedha kimakosa

Ujumbe huu umetumwa na rafiki kwenye kundi moja la WhatsApp tarehe 30 Juni 2015...

Ndugu zangu humu ndani.
Habari za jioni.
Naomba niwape mkasa wa leo. Ilibakia kidogo niibiwe ila nikastuka. Kuna utapeli wa Mpesa umeingia.

Kuna Dada kanipigia simu eti amekosea kutuma pesa kwangu. Akaniuliza umepokea ujumbe wa ongezeko la pesa, nikamwambia hapana. Akaniambia hapa ni vodacom kwani simu yako inashilingi ngapi kaka nikamueleza nakumbuka ni zaidi ya 120,000/- wakati tunaendelea kuongea mara msg ikaingia. Na akanieleza kaka angalia tena msg ukikuata ongezeko naomba unirudishie. Kweli kuangalia msg tu Vodacom ila maelezo ni ya Mpesa namba ya kawaida. Baada ya muda akanipigia kuwa alikosea akatuma 115,500/- anaomba nimrudishie nikamwambia subiri kidogo.

Wakati huo ni saa 12.45 leo jioni.

Nikampigia Meneja wa Vodacom rafiki yangu akanieleza, "una bahati sana. Leo ofisini kwangu nimepokea kesi 35 watu wametuma pesa kwa staili hiyo, wengine 750,000/-, 500,000/- mwenye pesa ndogo 250,000/- na akaniambia niwaeleze na wengine.

Nilipowapigia tena wakasema eti walipo mitambo ya Vodacom inamatatizo wakakata na simu.

Tafadhali kuwa muangalifu. Usiku mwema.

Orodha ya majina ya waliochaguliwa kujiugna Kidato cha Tano 2015

Kuna faili limepachikwa hapo chini au
au

TAARIFA KWA UMMA 


OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana 31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 na wavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 na wavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa na fursa ya mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI ya www.pmoralg.go.tz

Imetolewa na Katibu Mkuu, 
OWM-TAMISEMI


Mmoja akamatwa msituni na risasi 10, wawili watoroka

MTU mmoja amekamatwa ndani ya msitu wa Kata ya Kibindu aliyefahamika kwa jina la Ally Ayubu ambaye licha ya kukutwa na kisu pia alipopekuliwa alikutwa na risasi 10.

Katibu Mtendaji wa kijiji cha Kibindu, Juma Mgaza, amesema kuwa kukamatwa kwa mtu huyo kunatokana na taarifa zilizotolewa na mkulima mmoja baada ya kukutana na watu wasiofahamika katika kijiji hicho.

Kutokana na elimu waliyopewa wananchi na viongozi na Polisi, Mkulima huyo aliwaomba akatafuta Vocha ili apige simu kwa wenye Bodaboda waje wawasaidie, na walipobaini anawasiliana na uongozi, walimwambia wao wanatangulia kwa mguu asaidiwe mgonjwa, wakatokomea porini.

Uongozi wa Kijiji ulipofika na kumhoji, alisema yeye anaitwa, Ally Ayubu, mwenyeji wa mkoa wa Singida, ambapo alipopekuliwa alikutwa na risasi 10 ambazo hakutaja ni za bunduki aina gani, na mahindi mabichi yaliyovunjwa mashambani, na kuropoka kwamba kuna wenzake wawili wako porini wakiwa na bunduki moja.

Mgaza alisema baada ya Polisi wa kituo cha Pera kumchukua mtuhumiwa huyo na kuondoka naye hakukuwa na tukio lolote, na hakunamMwananchi yeyote aliyetoa taarifa ya kuibiwa chochote, isipokuwa mahindi waliyoyavunja na kula sababu ya njaa.
“Sina mwananchi yeyote katika Serikali yangu ya mji mdogo wa Madizi, ambaye amekamatwa na Polisi, kwa sababu mara baada ya kupata taarifa hizo, uongozi uliamua kupita kwa kila mjumbe wa mtaa kujua jambo hilo, lakini mtu yeyote ambaye alionekana kupotelewa na ndugu, isipokuwa wakulima waliorudi toka mashambani Njeura”
alisema Ahmad.

Taarifa ya Bryceson Mathias, Kibindu via Habari Mseto blog

Maoni ya KUB kuhusu Muswada wa Sheria ya Masoko ya Bidhaa 2015

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MASOKO YA BIDHAA YA MWAKA 2015 (COMMODITY EXCHANGE ACT,2015)

(Yanatolewa chini ya Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Bunge, toleo la mwaka 2013)


UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, muswada huu ulio mbele yetu kwa malengo yake kama utasimamiwa vyema ni mzuri kwani utaboresha mifumo ya mauzo ya mazao ya kilimo na bidhaa zingine kwa kadri mahitaji ya nguvu za soko yatakavyopelekea. Katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara ya mwaka 2014/15 alieleza dhamira na uhitaji wa kuwepo kwa mfumo huu wa soko la bidhaa. Kwani alieleza uwepo wa kitu kinachoitwa COWABAMA - (Collective Warehouse Marketing Systems) na kueleza kuwa huo ni mwendelezo wa kuanzisha Soko la Mazao na Bidhaa (Commodity Exchange Market).

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haina pingamizi na muswada huu wa Sheria ya Commodity Exchange kwani hili lilikuwa ni hitaji la wadau ambao wanashiriki katika mfumo mzima wa Stakabadhi za mazao Ghalani. Tunaamini kwa kiasi kikubwa wahusika katika mfumo huu wameshirikishwa kwa hatua zote za uandaaji wa muswada huu.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kulieleza Bunge lako ikiwa imefanya jitihada zozote za kuhakikisha kuwa elimu kwa umma hasa kwa wadau wote wa mfumo wa masoko ya bidhaa inatolewa. Sheria nyingi zinazoletwa katika Bunge hili zimekua zikilalamikiwa kutowafikia walengwa na hivyo utekelezaji wake siku zote umekua ukileta migogoro isiyoisha na mwishowe kusababisha hasara si tu kwa wazalishaji bali pia kwa watumiaji wa mwisho. Ni mikakati gani imewekwa ili kuhakikisha kuna utoaji elimu endelevu katika masuala ya masoko ya bidhaa?

Mheshimiwa Spika, hali ya miundombnu nchini hasa usafiri wa barabara na reli ambao ndio tegemezi kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa hasa za kilimo ni mbaya na isiyoridhisha. Sote ni mashahidi kuwa , pamoja na Serikali kujisifu kwa kuweka mtandao mkubwa wa barabara lakini barabara hizi hazijajengwa kwa ubora na ziinaleta changamoto kubwa za usafirishaji wa bidhaa hasa kipindi cha mvua. Leo tunapotaka kupitisha muswada huu wa masoko ya bidhaa, ni kwa kiasi gani tumeandaa mikakati ya kuimarisha miundombinu ili wauzaji na wanunuzi wa bidhaa wasipate hasara? ikiwa tutaendelea kuwa na miundombinu mibovu kama ilivyo sasa, ni dhahiri kuwa hata utekelezaji wa Sheria hii utakua mgumu na hivyo kuwa na Sheria bubu isiyoendana na mahitaji ya masoko ya bidhaa na hivyo kudidimiza uchumi badala ya kuinua uchumi .

Mheshimiwa Spika, maendeleo ya teknolojia katika masoko ya bidhaa ni mojawapo ya sababu zitakazoweza kufanikisha ama kufelisha utekelezaji wa Sheria hii. Ni kwa kiasi gani Serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na ukuaji wa teknolojia utakaomwezesha mtumiaji wa masoko ya Bidhaa ya Tanzania kuendana na mtumiaji wa masoko ya bidhaa mahali pengine duniani?

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuletwa kwa Sheria hii katika Bunge lako, ni dhahiri kuwa ili sheria hii iweze kutekelezwa kwa kiwango kinachotakikana, kanuni na miongozo yake ni lazima iwepo. Ikiwa Sheria hii italetwa na kanuni zitachelewa kutungwa, basi utekelezaji wake hautakua na maana yoyote na hivyo kuchangia kwa migogoro na migongano ya kisheria

MAPITIO YA MUSWADA

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 5 cha muswada kinachohusu malengo ya mdhibiti yanayohusiana na masoko ya bidhaa. Kambi Rasmi inapenda kupata taarifa ya kina kwani Mdhibiti ambaye ni CMSA yeye hana bidhaa bali bidhaa zinazotakiwa kuingia katika soko ambalo liko chini yake ziko chini ya mamlaka zingine ambazo zimeanzishwa kisheria na zinazo kanuni zake za uendeshaji; mamlaka hizo ni kama vile bodi ya Korosho, Bodi ya Kahawa, Bodi ya nafaka na Mazao mchanganyiko: Hivyo basi kwa kuangalia majukumu ya mdhibiti katika sheria hii ni dhahiri kuwa taasisi hizo hazitakuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria zilizozianzisha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi inaungana na wadau ambao wameliona tatizo hizo la kuziweka pembeni mamlaka na wakala za Serikali kama ambavyo baadhi yake zilivyoainishwa hapo juu, kwani kuna bidhaa ambazo zinatakiwa ziingie katika mfumo mzima au mnyororo wa uongezwaji wa thamani kabla ya kuwekwa katika soko la bidhaa. Na hapa Wizara mbalimbali zinahusika, na Waziri aliyetajwa ni Mmoja tu Waziri wa Fedha. Hii inaweza kukwamisha utekelezaji wa mfumo huu ambao tunaamini kuwa ni kwa faida ya wazalishaji wa bidhaa hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo kuhusiana na suala hilo la kutokutambuliwa na sheria kwa watendaji wengine wa Serikali ambao ni nguzo pia katika kuhakikisha bidhaa inauzwa, au wako karibu na wazalishaji.

Mheshimiwa Spika, katika kifungu cha 6 kinachohusu majukumu au kazi za mdhibiti, limetumika neno “Institutions” lakini neno hilo halijatolewa tafsiri, hivyo basi ni muhimu neno hilo likatolewa tafsiri yake ili kuondoa mkanganyiko kwa wadau wa Sheria hii.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 8(3) kinasema kwamba
“A company which is licensed as a commodity exchange shall not appoint any person to the position of Chief Executive Officer or Managing Director, senior management or the Board of Directors, change a substantial shareholder or change the organization structure without obtaining prior confirmation of the Authority”.

Mheshimiwa Spika, ni vyema Kambi Rasmi ya Upinzani ikapata maelezo ya kina kuhusiana na katazo hilo kwani kampuni pindi inaposajiliwa kwa mujibu wa sheria za makampuni sura ya 212, inakuwa na bodi yake na inakuwa na mamlaka kamili, na pia katika utendaji wake wa kazi bodi ndiyo yenye mamlaka ya kuteua nani awe ni mtendaji mkuu wa kampuni husika kwa vigezo walivyoweka wao.

Mheshimiwa Spika, Aidha, kulingana na mazingira ya kampuni ni jukumu la kampuni husika au wanahisa ambao ni wakurugenzi kuingiza mwanahisa au kumtoa kulingana na Articles of Association (makubaliano yao) zinavyosema. Sasa kitendo cha kuomba ruhusa kwanza kwa Mdhibiti wa Uendeshaji wa Soko la Bidhaa ni kuingilia mambo binafsi ya Kampuni husika. Tukumbuke kuwa Mtendaji Mkuu ni mwajiriwa na si mmiliki pale ambapo mmiliki akiona mtendaji mkuu hafanyikazi wala kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya wanahisa hivyo ni jukumu la Bodi ya wakurugenzi kuchukua maamuzi.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 3 na 4 cha muswada kinatoa ishara kama kwamba (makampuni yote) wale wote waliopata leseni “licensees” za soko la bidhaa ni mali ya Mamlaka, tukumbuke kwamba wadau wakuu wengi ni sekta binafsi hivyo kuiambia sekta binafsi isibadilishe mfumo wa utendaji kazi na watendaji wake, ni kuingilia masuala binafsi ya kampuni. Kambi Rasmi ya Upinzani inasema, Jambo hili halikubaliki kabisa na hivyo basi vifungu hivyo vifutwe kwa lengo la kuleta tija.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 9 (1) (b), (c) katika muswada bado vinaingilia mamlaka binafsi ya Kampuni na pia vinaweka ulinzi ambao utasababisha watendaji kujiona nao ni wamiliki na hivyo kuathiri utendaji kazi wao. Hoja ya Msingi ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani ingependa kuuliza ni kwanini ulinzi huo wa nafasi ya Mtendaji Mkuu hadi kuwekwa katika Sheria? Ni kweli kwamba haina ushindani pale wenye kampuni wanapotaka kufanya mabadiliko ya uongozi? Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kufuta vifungu hivyo vya ulinzi wa nafasi hiyo.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 67 cha muswada ambacho kinaelekeza kutumia maelezo ya kifungu cha 66(c ) cha sheria ya CAPITAL MARKET kuhusiana na tafsiri ya maneno ya mienendo mbalimbali ambayo hairuhusiwi kwenye biashara ya masoko ya bidhaa. Katika hilo Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kitendo cha kutumia rejea ya sheria nyingine “cross reference” ya sheria nyingine kwenye sheria hii ni uzembe, kwani sio mara zote mtumiaji wa sheria hii atakuwa katika nafasi ya kuwa na sheria nyingine ambayo inafanyiwa rejea.

Aidha, Mheshimiwa Spika, kifungu hicho hicho kimetumia maneno “manipulation, rigging Bucketing and Cornering” lakini kwa bahati mbaya katika kifungu cha 2 cha muswada kinachohusu tafsiri ya maneno, maneno hayo hayapo. Pia kwa kuwa tunatarajia sheria hii iwe toshelevu katika matumizi yake. Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuhakikisha kwamba kila kifungu katika sheria hii kijitosheleze badala ya kufanya rejea katika kifungu kingine cha sheria nyingine.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 70 cha muswada kinachohusu “liability to pay damages” kuwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia katika sehemu nzima ya XIII mbali ya kosa la kijinai kwa kosa husika pia atalazimika kufidia hasara iliyotokea katika manunuzi. Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kwamba kwa kuwa kitendo chochote cha kupanga kinachopelekea hasara kwa bidhaa hasa za kilimo. Maana yake ni kuhatarisha maisha ya mkulima, hivyo basi adhabu kali inatakiwa kutajwa kwenye sheria hii. Kwani adhabu ilivyowekwa katika muswada huu wa sheria haiko wazi ili kuwafanya wenye nia ovu kushtuka.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 82 cha muswada kinachohusu ulinzi “immunity” kuwa mamlaka, afisa au mtumishi yeyote hatahesabika ametenda kosa kwa kutenda au kutokutenda jambo na kupelekea hasara wakati akitimiza wajibu wake kwa nia njema, hadi pale itakapo bainika kuwa alikuwa ana nia mbaya.

Mheshimiwa Spika, kifungu hiki kama ambavyo kwa sheria nyingine zilizopita Kambi Rasmi ya Upinzani imekuwa haikubaliani na kifungu cha aina hii kwani kinahalalisha uzembe. Kwa sekta ya afya, uzembe wowote unagharimu maisha ya mtu na pia hapa tukiachia sheria kuwa na kifungu hiki, maana yake tunatoa mwanya wa kutokuwajibika na mwishowe ni hasara na inaweza leta athari kubwa kwa wanunuzi wa bidhaa na mara zote hasara inapelekwa kwa mzalishaji hasa mkulima kwa kuwa yeye ndiye mnyonge katika mfumo wa masoko ya bidhaa za kilimo. Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kifungu hiki kifutwe.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema hayo kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.

…………………………………

David Ernest Silinde (Mb)
K.n.y Waziri Kivuli- Wizara ya Fedha
29.06.2015Maoni ya KUB yanayohusu Muswada wa Sheria ya Benki ya Posta Tanzania

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA BENKI YA POSTA TANZANIA (KUFUTA NA KUWEKA MASHARTI YA MPITO), 2015 (THE TANZANIA POSTAL BANK {REPEAL AND TRANSITIONAL PROVISION} ACT, 2015)

(Yanatolewa chini ya Kanuni ya 86(6) ya kanuni za Bunge,Toleo la mwaka 2013)

Mheshimiwa Spika, awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu,Subhanahu wa Taala kwa kutujalia sote afya njema na kuendelea na kazi ya kulitumikia Taifa.

Pili nishukuru Chama changu cha CUF kwa uamuzi wake wa busara wa kunirejesha mimi kuwa Mgombea wa Jimbo la Mkanyageni na kama ukataji wa majimbo utaathiri Jimbo hilo, naamini chama pia kitafanya uamuzi wa hekima na busara kwa faida ya Chama wala sio matakwa binafsi ya yoyote.

Tatu nichukue nafasi hii kumpongeza Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif kwa ukomavu, uvumilivu na uhodari wake kisiasa na hata kama walimzuia kuingia katika Baraza, yeye alikwishafanya uamuzi mapema zaidi wa kutokwenda katika Baraza hilo maana hakuwa tayari kwenda kinyume na wajumbe wa Baraza kutoka CUF wakiwemo mawaziri. Uamuzi huo alioufanya mapema zaidi kuungana na Wawakilishi wake ndicho kilichomfanya Spika wa Baraza na wajumbe wa CCM kukasirika na kuchukua uamuzi wa chuki na kisasi ambao kwa waliokuwa hawajui wanadhani kuwa yeye alikuwa na shauku ya kwenda Barazani humo.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha CUF cha kususia baraza ni cha demokrasia popote pale Duniani kinachoonesha kutokukubaliana na jambo kwa njia ya kistaarabu. Kwa kuwa uchaguzi huru ni mchakato na unaanzia katika daftari la kuandikisha wapigakura, hivyo basi kitendo chochote cha kuwazuia au kutokuwaandikisha wapiga kura iwe Bara au Zanzibar ni jambo la hatari la kukiuka Demokrasia na kuufanya uchaguzi usiwe huru na wa haki.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaisihi,kuionya na kuitaka Serikali iwaandikishe watu wote wenye sifa katika daftari la wapiga kura kwa Bara au Zanzibar ili kufikisha makisio ya wapigakura milioni 24. Aidha

Haitakuwa uchaguzi huru na haki ikiwa idadi kubwa ya wapiga kura imeachwa kuandikishwa na kukoseshwa haki yao ya kikatiba.

Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa ni kwamba hali ya siasa Zanzibar imeshavurugwa na ilianzia pale vikosi vya ulinzi vilivyopewa silaha kuwapiga wananchi katika zoezi la kujiandikisha. Baya zaidi ni pale askari hao wanapovaa ki-ninja ili wasionekane nyuso zao na kuwachukua baadhi ya wananchi majumbani kwao usiku wa manane na kuwapiga na kuwatesa kisha kuwatupa mwituni wakiwa taaban.

Mheshimiwa Spika, vitendo hivi vinavyofanywa sasa Zanzibar haifai kuvinyamazia na ni lazima Serikali ya Jamhuri ya Muungano ichukue hatua madhubuti vinginevyo vinakaribisha machafuko yasiyo na ulazima-Mwanzo wa kutoweka kwa amani uanza taratibu na kama hatua zisipochukuliwa majuto yatakuwa ni mjukuu. Amani tayari imeanza kutoweka Zanzibar!!!

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini kwa umuhimu mkubwa ni kwamba UKAWA utatoa mgombea Urais mmoja na kuleta matumaini ya Watanzania na wanaojidanganya kuwa tutafarakana wanaota ndoto za mchana na watasubiri sana jambo hilo la kufarakana halitatokea.

Mheshimiwa Spika, muswada huu unaoletwa na Serikali kwa ajili ya kupitishwa una lengo la kufuta Sheria ya Benki ya Posta Tanzania, Sura 301 na kuweka masharti yatakayoiwezesha benki hiyo kusajiliwa na kuwa Kampuni, na pia kuweka masharti ya mpito kwa lengo la kuwezesha utekelezaji wa Sheria hii inayopendekezwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa maelezo ya Mheshimiwa Waziri aliyoyatoa katika Kamati ya Fedha, Uchumi Viwanda na Biashara ni kwamba Benki ya Posta ilikuwa inafanya kazi bila ya kukidhi matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo ni wazi Taasisi hiyo haikuwa na haina vigezo vya kuitwa Benki, hivyo basi Kambi Rasmi ya Upinzani inasema hata kama Serikali itabadili sheria ili ikidhi kigezo cha kuitwa benki kwa mujibu wa sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006. Ambacho ni kusajiliwa chini ya sheria ya makampuni Sura, 212, lakini bado kigezo cha mtaji kitaendelea kuwa ni tatizo katika kutimiza matakwa ya sheria ya Benki na taasisi za fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa umiliki wa benki hii tunaweza kusema ni kuwa taasisi hii inamilikiwa na Watanzania kwa asilimia mia moja (100%), kwa maana kwamba Serikali ya Tanzania inamiliki asilimia 86.4, Tanzania Zanzibar inamiliki asilimia 3.05, Shirika la Posta Tanzania asilimia 8.23 na Posta na Simu SACCOS asilimia 2.68. Kuhusu Zanzibar Kambi Rasmi ya Upinzani inazotaarifa kwamba inakusudia kuwekeza kiasi cha shilingi 950,000,000/- ili kuongeza hisa zake na kufikia asilimia 10 kutoka asilimia 3.05 za sasa.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo ni mtaji na mtaji unapatikana kwa wananchi kama utaratibu ulitumika kwa Serikali kupunguza hisa zake na kuwamilikisha wananchi, kabla ya kuziweka kwenye Soko la Hisa kwa sababu tahadhari kubwa ichukuliwe ili hisa hizo zikiachwa kwenye soko zisije kuchukuliwa na wageni wachache wenye fedha, na ile dhamira ya kuwa Benki ya watanzania ikatoweka na kuleta migogoro na Serikali kama ilivyofanywa na PSRC kwa makampuni mengine.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani kwa dhati kabisa inatoa pongezi kwa utawala na bodi ya wakurugenzi ya benki ya Posta Tanzania na hasa Mtendaji wake Mkuu kwa kuweza kuiondoa benki kutoka kwenye mtaji hasi wa shilingi milioni 78 mwaka 1992 hadi kuwa na mtaji chanya wa shilingi milioni 32,142 mwaka 2014. Hii ni kazi kubwa ukitilia maana na ushindani wa mabenki uliopo hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, katika kifungu cha 2 cha muswada kinachohusu tafsiri ya maneno “benki” limetolewa tafsiri kuwa ni Benki ya Posta Tanzania. Kambi Rasmi ya Upinzani inasema tafsiri hiyo ingeongezewa maneno kuwa ni Benki ya Posta Tanzania iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Benki na Taasisi za Fdha ya mwaka 2006.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza hivyo kwa kuwa toka mwanzo Benki hiyo ilikuwa inaitwa hivyo lakini haikuwa inakidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haipingani na hoja ya ubadilishwaji wa sheria ya uanzishwaji wa Benki ya Posta bali inasisitiza tena hitaji la mtaji, Serikali isikimbilie kutafuta wawekezaji toka nje ya nchi, madhara yake kimbilio hilo tumeliona kupitia Benki ya Biashara (NBC 1997 Ltd). Tunaamini wapo watanzania wenye fedha nyingi za kuwezesha kutimiza sharti la mtaji kwa mujibu wa sheria ya benki na taasisi za fedha ya mwaka 2006.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 6 cha muswada kinahusu kuhamisha wafanyakazi waliokuwa watumishi wa Benki ya posta na kuwa watumishi katika kampuni mpya. Jambo hili limeleta mgogoro sana na watanzania wengi ambao wana kesi zao mahakama za kazi kwa kiasi kikubwa ni kutokana na kampuni kubadilisha muundo wake. Ni maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwamba Serikali ihakikishe na kusimamia maslahi ya watumishi, pamoja na muswada huu wa sheria umetambua suala hilo ingekuwa ni vyema muswada ukaweka kifungu cha adhabu pale utawala wa benki utakapokiuka matakwa ya kifungu hiki.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapenda kutoa changamoto kwa watendaji wakuu wa mabenki yetu hasa (NMB, NBC, Dar es Salaam Community Commercial Bank, DTB, Akiba Commercial Bank na sasa TPB n.k) kwa nini hasa hazijitanui hadi nchi za jirani hata kama sio zaidi ya Bara letu la Afrika?

Mheshimiwa Spika, tulitarajia NMB kwa kuwa inamilikiwa na Waholanzi kwa asilimia kubwa kuwa itafungua tawi lake Uholanzi na katika Mataifa mengine ya Ulaya, lakini imekuwa ni kinyume badala yake wanachota faida ya hapa na kupeleka nje. Tusaidieni kueleza tatizo liko wapi? Kama wenzetu wa Kenya mabenki yao yanajaa Tanzania mabenki yetu kwanini hayana matawi Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Zimbabwe, DRC n.k.

Je, ni kweli tumekosa ubunifu na uthubutu kiasi hicho? Kama ni sheria kazi yetu kama wabunge ndio kazi tunayotakiwa kuifanya ili kuleta ustawi katika sekta ambazo sheria zinawazuia.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani,

Mheshimiwa Spika, Naomba kuwasilisha.

………………………

Mohamed Habib J. Mnyaa (Mb)
K.n.y Msemaji Mkuu-Kambi Rasmi ya Upinzani, Wizara ya Fedha
29.06.2015

Picha zinadhihirisha hatari ya usafirishaji aina hii huko Geita

Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambaba na watoto wadogo.Wakazi wa Mkoa wa Geita maeneo ya Buseresere na Katoro wapo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja kwenda jingine.

Mwakilishi wa kikundi cha usalama barabarani, Fungo Agustus ametutumia tukio hili ambapo magari madogo aina ya Pro Box yameingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa abiria hao. Abiria wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano mkubwa. 

Zifutazo ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji eneo la Buseresere.Aina nyingine ya gari dogo linalotumika kubebea abiriaMizigo na watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya gari hiloGari aina ya Pro Box ikiwa tayari kusafirisha abiriaTaarifa hii tumeshirikishwa na Dj Sek

Taarifa ya Habari ya asubuhi Channel TEN Juni 30, 2015


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Juni 30, 2015
Makulilo: Tofauti ya kuomba Masters, PhD kwa Ulaya na Marekani, Canada

Ukiachilia kujumuisha mambo yote ya jumla katika uombaji scholarship kama vile recommendation letters, sample writing, application nk, kuna utofauti uliopo ambao utakusaidia kufanya maamuzi ya wapi uombe.

a) Application Fee:


Vyuo vya ulaya havina Application Fee. Hili ni jambo muhimu sana, maana itakusaidia kuomba vyuo vingi bure. Gharama ni za kutuma documents kwa njia ya posta nk.

Kwa upande wa USA na Canada hii ni tofauti. Kwa kila chuo uombacho, unatakiwa kulipa si chini ya dola 50-100 kama fee. Hii kwa maisha ya Kitanzania ni hela kubwa ukizingatia unatakiwa uombe vyuo vingi ujiwekee uwezekano wa kupata.

b) Admission Exams

TOEFL au IELTS

Kwa upande wa Ulaya, wao wana mtihani mmoja wa English Proficiency. Unatakiwa kufanya aidha mtihani wa TOEFL (Test of English as Foreign Language) au IELTS (International English Language Testing System). Huo mtihani wa TOEFL ni wa kimarekani unafanyikia pale Chuo cha Mwalimu Nyerere kule Kigamboni, ambapo ada ya mtihani huo ni kama dola 185. Na mtihani wa IELTS ni wa waingereza na hufanyikia pale British Council ada yake ni kama laki nne hivi. Unatakiwa kufanya mtihani mmmoja kati ya hiyo miwili.

Kuna vyuo au nchi chache zinaruhusu applicants kuomba vyuo bila kuonesha cheti cha Kiingereza cha TOEFL au IELTS. Mfano, ukiomba vyuo vya Norway wao kupitia Quota Scheme scholarship applicants ambao wamesoma high school na university kwa lugha ya kiingereza hawana haja ya kuonesha/kufanya mitihani hiyo.

Ushauri wangu, usisubirie zali mpaka upate exemption hiyo. Maana ni vyuo vichache/nchi chache zenye kutoa exemption hiyo. Ukisubiria zali hiyo utasubiria muda mrefu kama ukikosa chuo husika. Ila ukifanya mtihani wa TOEFL au IELTS utakuwa umejiongezea wigo wa kuomba vyuo vingi, scholarships kibao ni LAZIMA uwe na requirement hii.

Kwa upande wa USA, vyuo vyote na scholarships zote ni lazima uoneshe cheti cha TOEFL au IELTS. Ila sharti lingine kwa USA, kwa kila chuo uombacho, ni lazima utumie original copy of test results. Na ni wenye kumiliki mtihani wa TOEFL yaani ETS ndio wenye mamlaka ya kutuma copy ya matokeo yako ya mtihani kwenye chuo uombacho. Na kwa kila chuo, copy ya cheti kimoja lazima ulipie dola 15 kwa kila copy. Hivyo ni gharama kwani ukiachilia kulipia application fee let's say dola 70, utalipia tena dola 15 ya TOEFL cheti kutumwa kwenye chuo. Kamwe hawachukui copy ya matokeo toka kwako.

GRE na GMAT

Ulaya wao hawana hii mitihani ya GRE na GMAT. Hii ni mitihani kama unataka kusoma USA only.

Mitihani hii ni kama ile matriculation enzi zile kuingia chuoni. GRE (Graduate Record Exam) ni kwa applicants ambao wanataka kusoma non-management programs. Na kwa GMAT (Graduate Management Admission Test) ni kwa wale wanaotaka kusoma Management Programs. Mitihani hii yote gharama yake ni kama dola 185 na inafanyikia pale kwa Mwalimu Nyerere, chuo kikuu.

Ukiachilia gharama ya mtihani, kwa kila copy moja utakayopata/utakayotuma kwenye chuo ni dola 27. Kumbuka chuo chochote huku hakichukui cheti/copy toka kwa applicant, all results should be sent from official owners of the exam, yaani ETS. Na hakuna chuo utakachopata iwe ni kwa masters au PhD bila ya GRE au GMAT exam.

Gharama unaiona: Kwa USA, kuna application fee kati ya dola 50-100 kutegemeana na chuo, kuna TOEFL, GRE, pamoja na gharama ya kila cheti/copy utakayotuma kwenye chuo. Hivyo gharama ya application ya chuo kimoja ni kama dola 100-120 kutegemeana na chuo, na bado unaweza kukosa kwani mwombaji sio wewe peke yako.

Hivyo kiushauri, huwa ni vyema mtu kuomba vyuo vingi vya ulaya sababu za gharama, na kama ukiomba USA basi viwe vichache unless lengo lako liwe ni lazima usome USA tu hivyo utaingia gharama hizo.

SHARE WITH YOUR FRIENDS

MAKULILO
[email protected]
www.makulilo.blogspot.com

WSD Postgraduate Training Fellowships

Postgraduate Training Fellowships for Women Scientists from Sub-Saharan Africa and Least Developed Countries (LDC) at Centres of Excellence in the South. The Fellowship is offered to women scientists to pursue postgraduate research in a field of the natural sciences.

Eligibility

 • Open to qualified women science graduates from countries in Sub-Saharan Africa and Least Developed Countries (see list below).
 • If applicants are over 40 years of age, they should include a brief explanation of why their research career has been delayed.
 • The minimum qualification is an MSc degree (or equivalent), or an outstanding BSc honours degree in the natural sciences, engineering or information technology disciplines (see list below).
 • Host institutions must be located in a developing country. This must be a different country from the applicant's home country.
 • Applicants must provide a preliminary acceptance letter from at least one host institute. The letter must be prepared based on the sample on page 10 and be signed by the head of department, potential host supervisor or postgraduate studies coordinator.
 • Students from eligible countries already enrolled on a PhD programme in their home country can apply for the sandwich option. This gives them access to expertise and resources that might not be available at the home institute.
 • Applicants already on site in the host country will not be considered eligible since this implies that they have already secured sufficient funding for their studies.
 • The applicant must be willing to return to her own country after completion of the fellowship.
 • Accompanying persons are not eligible for support. 

ELIGIBLE SCIENTIFIC FIELDS:

Agricultural Sciences; Structural, Cell and Molecular Biology; Biological Systems and Organisms; Medical and Health Sciences; Neurosciences; Chemical Sciences; Engineering Sciences; Information Technology; Astronomy, Space and Earth Sciences; Mathematical Sciences; Physics.

Please note that applications from students in the Basic (or 'pure') Sciences, such as Mathematics, Physics and Chemistry are encouraged.

ELIGIBLE COUNTRIES:

Afghanistan, Angola, Bangladesh, Benin, Bhutan, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Cambodia, Cameroon, Cape Verde, Central African Republic, Chad, Comoros Islands, Congo Dem. Rep., Congo Rep., Côte d'Ivoire, Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Haiti, Kenya, Kiribati, Lao People's Democratic Republic, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Maldives, Mali, Mauritania, Mauritius, Mozambique, Myanmar, Namibia, Nepal, Nigeria, Niger, Réunion, Rwanda, Samoa, Sao Tome and Principe, Senegal, Seychelles, Sierra Leone, Solomon Islands, Somalia, South Africa, South Sudan, Sudan, Swaziland, Tanzania, Timor-Leste, Togo, Tuvalu, Uganda, Western Sahara, Vanuatu, Yemen, Zambia, Zimbabwe.

Deadline for applications: 31 July 2015.

Call: Science Granting Councils Initiative in Sub-Saharan Africa

CALL FOR: EXPRESSIONS OF INTEREST

Deadline: July 22, 2015 by 00:00 (12:00 AM) (UTC-05:00) Eastern Time (US and Canada)

Eligibility: This initiative is open to Science Granting Councils in Eastern, Southern, Central, and West Africa.

Duration: 60 months

Budget: CA$13.9 million

Scope: ​This call aims to select organizations to participate in a 5-year Science Granting Councils Initiative in Sub-Saharan Africa to support research and evidence-based policies that will contribute to economic and social development.

The Initiative will support Science Granting Councils to
 • manage research
 • design and monitor research programs based on the use of robust science, technology, and innovation indicators
 • support knowledge exchange with the private sector
 • establish partnerships with each other and with other science system actors
 • Activities will include exchange and training, forums on evidence and best practices, online training, individualized on-site coaching, and collaborative research as requested by each participating Council.

The Initiative currently has funding for up to eight (8) Science Granting Councils. While the emphasis is on Eastern Africa; however the Initiative will include additional Councils from Southern, Central, and West Africa on request by countries. A further eight (8) Councils will be invited to participate in partnerships activities.

Documents
All additional questions should be addressed to [email protected]

​​This initiative is jointly funded by the UK Department for International Development (DFID), Canada's International Development Research Centre (IDRC), and South Africa's National Research Foundation (NRF).

Call for grants applications: IDRC Research Awards 2016

Deadline: August 06, 2015 by 16:00 (04:00 PM) (UTC-05:00) Eastern Time (US and Canada)

Eligibility: This call is open to Canadians, permanent residents of Canada, and citizens of developing countries pursuing a master’s or a doctoral degree at a recognized university OR who have completed a master's or doctoral degree at a recognized university. These research awards may be part of an academic requirement.

Other eligibility requirements include:
 • Your proposed research must focus on one or more developing countries.
 • Candidates cannot receive any other Canadian government scholarship, award, subsidy, bursary, or honorarium, or hold any federal government contract in support of a research/work project for the duration of the award.
 • If you are a non-Canadian residing, relocating, or studying in Canada and are recommended for an award, you will need a valid work permit before working at IDRC.
Duration: January to December 2016 (12 months). Based in Ottawa, Canada (Select placements may be located in one of IDRC's Regional Offices).

Budget: Salary for one year: CA$39,797-CA$46,070

Scope: For payroll purposes, awardees are considered as full-time employees of IDRC. Benefits include Employer contributions to Employment Insurance, Employer Health Tax, Canada Pension Plan, and paid vacation leave. Some travel and research expenses are also supported, up to a maximum of CA$15,000.

As a research award recipient, you will undertake a one-year paid program of research on the topic you submitted to the competition and receive hands-on experience in research management; grant administration; and the creation, dissemination, and use of knowledge from an international perspective.

Access the call document and frequently asked questions (FAQs):
All additional questions should be addressed to [email protected]

Mambo 5 unayolazimika kuyaacha ndipo ufanikiwe


Watu wenye mafanikio makubwa mara nyingi huwa ni watu ambao hawana tofauti kubwa sana na wewe. Huwa ni watu walewale ambao pengine tunakuwa nao na hata kupishana nao barabarani. Tofauti kubwa inayojitokeza kati ya watu hao na wewe ni namna wanavyofikiri na matendo yao wanayoyatenda kila siku. Matendo yao huwa yanaendana na mkabala na kile wanachokitaka maishani mwao na sio vinginevyo.

Kwa kuwa huwa wanajua wanachokitaka hujikuta ni watu wa kutenda na kuacha mambo ambayo wanahisi kwa namna yoyote ile yanaweza kuwarudisha nyuma. Kwa kifupi hawa huwa ni watu wanaoshikilia mambo wanayoona yanayowapa faida na mafanikio makubwa. Mambo yote ambayo ni mzigo kwao huwa hawayabebi. Hicho ndicho kitu ambacho hata wewe unachotakiwa kukifanya ili kufanikiwa zaidi.

Hutakiwi kung’ang’ania sana mambo ambayo hayawezi kukupa mafanikio katika maisha yako. Ili uweze kufanikiwa unalazimika kuyaacha mambo hayo mara moja. Mara nyingi umejikuta ukiwa ukikwama kutokana na wewe kuzidi kuwa king’ang’anizi kwa mambo hayo. Huu ni wakati wa kubadilika sasa. Kama ulikuwa hujui ama una kigugumizi juu ya hili, haya ndiyo mambo unayolazimika kuyaacha mara moja ili kuweza kufanikiwa:-

1. Acha kutegemea mafanikio ya haraka.

Mara nyingi hizi ndizo zimekuwa ndoto nyingi za watu wengi kutaka kuona mafanikio makubwa na ya haraka. Mafanikio yoyote huwa yanajengwa hatua kwa hatua. Tena kuna wakati huwa ni hatua za kutambaa mithili ya mtoto mdogo. Kama utategemea mafanikio ya haraka zaidi katika maisha yako hutayapata zaidi ya kujidanganya wewe mwenyewe. Acha kung’angania mafanikio ya haraka, utakwama. Jiwekee malengo kisha songa mbele.

2. Acha kuwa mtu wa visingizio.

Hili ni jabo mojawapo ambalo umekuwa ukiling’ang’ania mara kwa mara katika maisha yako. Umekuwa ni mtu wa visingizio kwa kudai kuwa huwezi kufanikiwa kwa sababu hukusoma, huna mtaji ama umetoka katika familia maskini. Kutokana na visingizio hivyo umekuwa huchukui hatua yoyote zaidi ya kuzidi kufanya maisha yako kuwa magumu. Ili uweze kufanikiwa, achana na kung’ang’ania visingizio kama mkombozi wako. Badala yake, chukua hatua juu ya maisha yako.

3. Acha kuogopa sana kushindwa.

Kushindwa ni hatua mojawapo muhimu ya kuweza kukufikisha kwenye njia halisi ya mafanikio. Unaposhindwa unakuwa unajifunza kutokana na makosa unayoyafanya na kisha kuendelea zaidi. Kama utaendelea kuogopa kujaribu mambo mapya kila siku kwa sababu ya kushindwa, tambua hutaweza kufanikisha mambo makubwa katika maisha yako. Ili uweze kufikia mafanikio makubwa hutakiwi kuogopa kushindwa kwa namna yeyote ile. Unatakiwa kuachana na woga huu mara moja ili kufikia mafanikio makubwa.

4. Acha kufanya kazi kutegemea pesa.

Kama utaendelea kufanya kazi na kuwaza pesa! Pesa Pesa!, hutaweza kufika mbali sana. Fanya kazi kwa lengo la kujifunza na kisha baada ya hapo pesa ndiyo ifuate. Ukiwa unafanya kazi kwa lengo la kupata pesa utajikuta unafanya mambo yako mengi sana chini ya ufanisi. Badili fikra zako na acha kung’ang’ania kufanya kazi kwa kutaka pesa tu. Ukitengeneza huduma iliyobora zaidi pesa kama pesa itake isitake itakufuata tu huko ulipo.

5. Acha kufikiria sana makosa yaliyopita.

Kwa kuendelea kufikiri sana makosa uliyoyafanya hiyo itakufanya uzidi kupoteza mwelekeo wa mafanikio yako. Njia sahihi ya kufanikiwa ni kuachana na kufikiria makosa hayo. Vinginevyo utakuwa unapoteza nguvu zako nyingi kun’gang’ania jambo ambalo haliwezi kukufikisha kwenye mafanikio ya kweli. Hili ni jambo mojawapo ambalo unatakiwa kuliacha mara moja ili uweze kufanikiwa.

Kwa vyovyote vile, kwa kadri unavyozidi kun’gang’ania mambo hayo ndivyo ambavyo unajikuta unazidi kuharibu maisha yako bila kujua. Ili kuweza kufanikiwa na kutimiza ndoto zako halisi ulizojiwekea, unatakiwa kushika wajibu mmoja tu. Huu ni wajibu wa kuweza kun’gang’ania mambo yatakayokusaidia na kubadili maisha yako kabisa. Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo unayotakiwa kuyaacha mara moaj ili uweze kufanikiwa.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YETU YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,
[email protected]

Imenukuliwa kutoka www.amkamtanzania.com

Cheka kidogo na methali za kisasa...


 1. Simba mwendapole = Huyo ni Sharobaro.

 2. Asiyefunzwa na Mamae = Ujue Mama hajapitia Ualimu.

 3. Zimwi likujualo = Lilikuona sehemu.

 4. Chelewa chelewa = Ukizikusanya utapata ufagio.

 5. Hakuna masika = Wakati wa kiangazi.

 6. Mpanda ngazi = Asiwe mwoga kuanguka.

 7. Dua la kuku = Bismilah Rahman Rahim. 

 8. Penye wengi = Pana ajali au tukio

 9. Ukiona vyaelea = Ujue ni vyepesi.

 10. Mwenye nguvu = Amekula ugali wa dona.

Kilimo bora cha pilipili hoho


Pilipili hoho ni moja ya mazao ya viungo ambalo hulimwa kwa wingi Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Mbeya na Iringa.

Zao hili hutumika kama kiungo kwenye vyakula mbalimbali kama vile vyama, viazi na ndizi. Vilevile hutumika katika kutengeneza kachumbari na kuweza kukaushwa na kusagwa ili kupata unga.

Viini lishe vinavyopatikana katika pilipili tamu au hoho ni Vitamini A,B,C na madini aina ya chokaa na chuma.

MAZINGIRA

Zao hili hukua vizuri kwenye hali ya hewa yenye joto la wastani (nyuzi joto 18 hadi 20) za Sentigredi, joto likizidi vichomozo, maua na matunda huanguka.

Huhitaji mwinuko wa kuanzia usawa wa bahari hadi mita 1,500 na mvua za wastani kiasi cha milimita 600 hadi 1500.

Udongo unaofaa kwa zao hili ni ule wenye rutuba, mboji nyingi, kina kirefu na usiotuamisha maji.

AINA

Kuna aina nyingi za pilipili hoho. Baadhi ya aina zinazostawishwa nchini ni California, Wonder, Emerald Giant, Sweet Neapotitan, Yolo Wonder, Pimiento na Keystone Resistant Giant. Aina zingine ni kama vile Ruby King, Ruby Giant, Libert Bell na Yolo Wonder B.

KUPANDA MBEGU

Mbegu zinaweza kupandwa moja kwa moja shambani au kuoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye kuhamishiwa shambani.

Kuotesha mbegu Kitaluni

Kabla ya kusia mbegu tengeneza tuta lenye upana wa mita moja. Urefu wa tuta utategemea eneo la shamba linalotarajiwa kupandwa. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha ndoo mbili au zaidi katika eneo la mita mraba moja. Changanya mbolea na udongo vizuri, kisha tengeneza vifereji vyenye nafasi ya sentimeta 10 hadi 15 kutoka kifereji hadi kingine. Kina cha kifereji kiwe sentimeta moja hadi tatu katika eneo hilo, kiasi hiki kitatoa miche ambayo itatosha kupandikiza katika eneo la mita mraba 100.

Baada ya kusia fukia kwa kutumia udongo laini au mbolea za asili zilizooza vizuri. Weka matandazo na kisha mwagilia maji. Endelea kumwagilia kitalu kila siku asubuhi na jioni hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku sita hadi 10. Mara zitakapoota ondoa matandazo. Endelea kumwagilia maji hadi wakati miche inakuwa tayari kwa kupandikizwa.

KUTAYARISHA SHAMBA

Tayarisha shamba vizuri mwezi mmoja kabla ya kupandikiza miche, katua ardhi katika kina cha kutosha sentimeta 30 kwenda chini, weka mbolea za asili kiasi cha tani 10 hadi 15 kwa hekta. Kiasi hiki ni sawa na debe moja kwa eneo la mita mraba moja changanya mbolea na udongo vizuri.

Ikiwa eneo hilo lina upungufu wa madini aina ya fosiforasi kama itakavyothibitishwa na wataalam, weka mbolea ya chokaa aina ya TSP. Kiasi kinachotakiwa ni kilo 200 kwa hekta. Lainisha udongo siku tatu au tano kabla ya kupandikiza miche.

KUPANDIKIZA MICHE

Miche huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki nne hadi 10. Wakati huu huwa na majani sita hadi manane na urefu wa sentimeta 10 hadi 15.

Pandikiza miche katika nafasi ya sentimeta 40 hadi 50 kutoka shimo hadi shimo na sentimeta 60 hadi 75 kati ya mstari na mstari. Ikiwa mbolea za asili hazikuwekwa wakati wa kutayarisha shamba, weka kiasi cha nusu kilo hadi moja katika kila shimo la kupandia.

Siku moja kabla ya kung’oa miche, mwagilia tuta ili kulainisha udongo. Ng’oa miche pamoja na udongo wake kisha pandikiza katika kina cha sentimita mbili zaidi kuliko ilivyokuwa kwenye kitalu. Pandikiza miche wakati wa asubuhi au jioni. Mara baada ya kupandikiza mwagilia maji ya kutosha.

KUTUNZA SHAMBA
 • Kuweka matandazo.
Tandaza nyasi kavu ili kuhifadhi unyevu ardhini, kuongeza rutuba ya udongo, kuzuia uotaji wa magugu, na mmmomonyoko wa ardhi.

 • Palizi.
Palilia shamba kila magugu yanapoota. Wakati wa kupalilia pandishia udongo kuzunguka shina ili kuifunika mizizi, na kuzuia mmea usiangushwe na upepo mkali.

 • Kumwagilia Maji.
Pilipili hoho hustawi vizuri iwapo zimepata maji ya kutosha. Hivyo umwagiliaji wa mara kwa mara hasa wakati wa kiangazi ni wa muhimu.

 • Kuweka Mbolea.
Zao hili huhitaji mbolea za kukuzia. Hizi ni kama mbolea ya S/A, CAN, Urea na mbolea ya mchanganyiko aina ya N.P.K Mbolea ya mchanganyiko (N.P.K) huwekwa wakati maua yanapoanza kutoka. Kiasi kinachowekwa ni gramu tisa hadi 10 (kijiko kimoja kikubwa) kwa kila mmea. Majuma manne baadaye weka CAN, S/A au Urea. Weka gramu sita (kijiko kidogo cha chai) kwa kila mche, kama utatumia CAN au S/A. ikiwa utatumia Urea, weka gramu tatu ( nusu kijiko cha chai) kwa kila mche).


Wadudu waharibifu na Magonjwa.
Wadudu.
 • Vidukari au wadudu Mafuta (Aphids).
Hivi ni vijidudu vidogo vyenye rangi nyeusi, kijani au kahawia. Hushambuliwa majani kwa kufyonza utomvu wake na kusababisha mmea kudumaa. Vidukari huzuiwa kwa kunyunyizia dawa kama vile Dimothoate au Selecron.

 • Mbawakau.
Ni wadudu wenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kahawia. Mabawa yao kwa nje ni magumu. Hushambulia shina karibu na usawa wa ardhi na kulifanya liwe na nundu.

Zuia wadudu hawa kwa kutumia mojawapo ya dawa zifuatazo; Carbaryl, au Dimecron.

 • Fukusi wa Pilipili (Pepper Weevil)
Mdudu huyu ni hatari sana kwa zao hili na mashambulizi kufanywa na funza wake wenye rangi nyeupe. Funza hawa hula sehemu ya ndani ya vichomozo na matunda machanga nan kusababisha kuanguka. Angamiza wadudu hawa kwa kutumia moja ya dawa zifuatazo; Actellic, Sumithion au Carbaryl.

 • Vithiripi (Thrips)
Hivi ni vijidudu vidogo vyenye rangi ya njano. Hushambulia majani na husababisha mmea kuwa na rangi nyeupe yenye kung’aa. Mmea pia kunyauka kuanzia kwenye ncha ya jani. Vijidudu hivi pia kueneza magonjwa yatokanayo na virusi.

Zuia vijidudu hivi kwa kutumia dawa kama vile;- Cyrmethrin, Sumicidin au Dimercon.

 • Sota (Cutworms)
Hawa hukata miche michanga karibu na usawa wa ardhi. Ili kuwazuia wadudu hawa, tumia dawa kama vile Carbaryl, Sumicidin au Ekalux. Nyunyizia mara baada ya kupandikiza.
 • Nzi Weupe (White flies).
Ni vidudu vidogo vyenye rangi nyeupe, na huonekana kama vumbi la unga vikiwa kwenye majani. Mmea ukitikiswa huruka.
Hushambulia mmea kwa kufyoza utomvu wake, na hueneza ugonjwa wa virusi unaosababisha kujikunja kwa majani.
Inzi weupe wanaweza kuzuiwa kwa kutumia Sumicidin, Sapa Diazinon au Diclorvos.

 • Utiriri Mwekundu (Red Spidermites)
Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi nyekundu au rangi ya machungwa yaliyoiva. Huonekana upande wa chini wa majani na hushambulia mmea kwa kufyonza utomvu wake.
Zuia utitiri kwa kutumia dawa kama vile Kelthane, Dimethoate na Diazinon.
Magonjwa

 • Magonjwa ya Virusi
Magonjwa haya hutokana na virusi. Husababisha majani kudumaa, kukunjamana, na kuwa na rangi ya njano. Ili kuzuia magonjwa haya, zingatia yafuatazo;-
- Panda aina ya pilipili zinazostahimili mashambulizi ya magonjwa haya.
- Ng’oa miche inayoonyesha dalili za magonjwa haya.
- Zuia wadudu wanaoeneza magonjwa ya virusi kwa kutumia dawa ya Kelthane 30 E, C, Dimethoate, Diazinon na Ekalux.
- Badilisha mazao. Baada ya kuvuna pilipili tamu, zao linalofuata lisiwe la jamii la zao hili kwa mfano nyanya na bilinganya.


 • Chule (Anthracnose)

Ugonjwa huu husababishwa na ukungu. Hushambulia matunda na kuyasababisha kuwa na makovu j ya mviringo yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kahawia. Zuia ugonjwa huu kwa kunyunyizia mojawapo ya dawa zifuatazo: Dithane - M 45, Topsini - M, Ridomol au Kocide,
 • Madoa Bakteria (Bacterial Leaf spot)
Ugonjwa huu husababishwa na viini vya vya bacteria. Hushambulia majani machanga j na baadaye matunda. Dalili j zake ni kuonekana kwa madoa ya njano kwenye majani na matunda.

Zuia ugonjwa huu hkwa kupanda mbegu zilizothibitishwa na wataalam.

 • Kuoza Mizizi (Root Rot)
Huu ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia mizizi na kusababisha kuoza. Mmea hunyauka na hatimaye hufa. Ugonjwa huu hupendelea sana hali ya unyevunyevu na joto jingi, hivyo zuia hali hii kwa kuepuka kupanda pilipili kwenye sehemu h inayotuamisha maji. Hali ikiwa mbaya, tumia dawa za ukungu kama vile Dithane M 45, Tpsin - M 70 au Ridomil.

 • Mnyauko Verticilium (Verticilim Wilt)
Huu pia ni ugonjwa unaoletwa na ukungu ambao hupatikana kwenye udongo. Hushambulia shina na kulisababisha libadilike rangi na kuwa ya kahawia. Baadaye mmea hunyauka na kufa. Unaweza kuzuia ugonjwa huu kwa kubadilisha mazao.

KUVUNA
 
Pilipili hoho huwa tayari kwa kuvunwa baada ya wiki 10 hadi 14 tangu kupandikiza miche. Uvunaji huendelea kwa muda wa wiki nane hadi 10. Muda wa kuvuna hutegemea aina na matumizi. Pilipili kwa ajili ya matumizi ya nyumbani huvunwa zingali na rangi yake ya kijani kibichi inayong’aa . zile za kisindika kiwandani huvunwa zikiwa zimekomaa na zenye rangi nyekundu. Matunda yakivunwa tangali machanga hunyauka kwa urahisi, kusinyaa na hupunguza wingi wa mazao. Wastani wa mavuno huwa kwa hekta ni tani 30 hadi 45.

Makala hii imenukuliwa kutoka kwenye tovuti ya DIRA YA MAFANIKIO. IMEADALIWA NA SAID MALOGO, MTAALAMU WAMASUALA YA KILIMO.
MAWASILIANO 0782 396 729

Taarifa ya maandamano ya amani Rombo kulaani udhalilishajiCristiano Ronaldo sells his image rights to Peter Lim


Portuguese and Real Madrid forward Cristiano Ronaldo announced on his website the he has sold his image rights to Valencia's owner, Peter Lim.

Lim, who is a close friend of Ronaldo's agent, Jorge Mendes, is a valuable link to Asian markets.

The deal is noteworthy, Marca adds, because image rights were a central part of negotiations when Ronaldo signed an extension with Real in 2013: "Image rights played a big role in Ronaldo's drawn-out contract negotiations with Real Madrid back in 2013. The eventual outcome was that the star regained control of over 50 percent of these rights, according to reports in the Portuguese media at the time."

Norfund's response to report "Irresponsible investment. Agrica’s broken development model in Tanzania"

OI_Report_Irresponsible_Investment.pdf

Cross-posted from MikaelBergius blog regarding the report above.

The Norwegian Investment Fund for Developing Countries (Norfund) has released a response to the report – “Irresponsible investment. Agrica’s broken development model in Tanzania” – released by The Oakland Institute on June 17th. The response can be found here (in Norwegian only). I have translated it below:

NORFUND RESPONSE TO OI REPORT

General Information:

Agrica is a 5000ha rice farm in the Kilombero Valley in Tanzania. The farm aims to produce more than 40,000 tons of rice per year. This significantly increases rice supply in Tanzania – a country currently unable to produce enough food to feed its own population.

Norfund has been one of the investors in Agrica since September 2010. The investment is part of Norfund’s strategy for developing sustainable agriculture in the LDCs in East Africa. Both shareholders and Agrica’s management aims to create value and improve living conditions for the population in the region, in addition to creating value for investors.

Establishing new agricultural projects in developing countries are always demanding. Agrica has, like all other businesses in this sector, faced challenges along the way. Norfund has, however, throughout the investment period followed Agrica’s work closely, and been impressed by the management’s knowledge and ability to follow international standards (IFC) in all environmental and social issues. This includes the necessary resettlement and measures to increase small farmers rice production through improved seeds and extension; ‘System of Rice Intensification program’ (SRI). The SRI program has so far reached 7,000 families and Agrica has bought some of the rice from farmers at market rates. By doubling or tripling production per hectare, the SRI program increases annual income and help reduce poverty in the area.

With its large production, Agrica contributes significantly to a more secure supply of rice in Tanzania. This project is an important investment for Norfund and contributes significantly to the country’s rice production and import substitution.

The allegations in the report:

The report from The Oakland Institute – “Irresponsible investment. Agrica’s broken development model in Tanzania” -was published on Wednesday, June 17th. The report critiques the use of aid funds in large-scale commercial farming, and accuses the project directly for:

1. Damaging / deteriorating living conditions for poor small farmers in the surrounding communities, mainly due to the required relocation of people to new homes and land areas and low compensation.

2. Forcing small-farmers to take up more debt than they can handle. It argued that “the outgrower scheme” has resulted in poor farmers struggling with debt repayment and are forced to sell their assets.

3. Polluting rivers, soils and wetland areas in the region resulting from the use of fertilizers and chemicals, and for threatening surrounding wetlands due to Agrica’s plans to expand the area under irrigation.

There is no cover for the title of the report or the above allegations. The report is based largely on interviews with 40 anonymous people (of more than 35,000 inhabitants) in the community.

A number of negative statements are presented. It is not possible to verify the accuracy of these allegations or follow up on complaints. No persons with scientific expertise have been responsible for the report. To Norfund’s knowledge, only students and Oakland Institute’s own staff have been involved.

The allegations are in stark contrast to Agrica’s thorough documentation of the relocation process. In a letter to The Oakland Institute, Agrica CEO, Carter Coleman, documents how IFC standards have been adhered to at all levels throughout the project. He explains how the resettlement process was structured so as to let the local community and affected individuals themselves decide where to move. The company also has an independent grievance committee where dissatisfied people can have their case reviewed. The concerns referred to in the report have not been raised there.

About SRI and the loan program: it is important to know that participation in the program has been voluntary and that Agrica has provided significant resources to establish this extension service which aims to assist smallholders in raising productivity and profits. Great amounts of illegal rice imports to Tanzania, however, have resulted in falling prices in the country. All rice farmers in Tanzania, including Agrica, have thus received lower earnings than expected during this period.

It is true that there were reports of a single case of contamination with chemicals in 2010. It was managed and addressed immediately and there have been no further complaints since then. Agrica can document that they are following IFC and FAO guidelines and have a clear strategy to control the use of chemicals. The plans to expand the area under irrigation have been thoroughly investigated by two different teams of experts, and the conclusions are that the planned expansion is in line with Tanzanian and international standards.

As we see it, small-scale farming is important, but Africa also needs a commercially efficient agricultural sector to achieve economic growth and get cheaper food. Large-scale farming can be sustainable if it is done the right way and use fertilizers and pesticides in a proper manner. It provides export earnings and / or reduced import costs, employment opportunities, and often market access for small farmers.

End of response

Bagamoyo: Msiba waisha baad ya "maiti" kupumua wakati akioshwa


Huko mjini Bagamoyo katika eneo lijukanalo kwa jina la Majani Mapana, mwanamama mmoja jana aliyetambulika kwa jina moja la Bi. Hatujuani aliyethibitishwa kuwa umauti umekuta, alipumua wakati wakimkosha na kwa matayarisho ya kuvikwa sanda.

Bi. Hatujuani aliugua kwa muda na kukimbizwa hosptilai ya wilaya Bagamoyo na baadaye kudhaniwa kuwa ama amepatwa na umauti wa muda mfupi au kupoteza fahamu lakini hospitalini hapo walithibitisha kuwa keshakufa. Mkasa huo ulitokea tarehe 28 Juni 2015 na wanandugu walishachukua maiti na matayarisho ya maziko yakiwa mbioni, turubai lilishafungwa,s anda tayari hadi Juni 29, 2015 wakimkosha maiti Bi. Hatu mwenye umri wa miaka 30, waliokuwa wakimkosha walishtuka maiti kuwa ana joto kali, anatoka jasho na anakunja na kukunjua mikono na miguu, lakini kusema wala kusimama hawezi!

Baada ya wanandugu kutangazia umma kuwa msiba hakuna tena bali tuna mgonjwa mahututi,
waliofika msibani na umati wa watu waligoma kuondoka mazikoni hadi kieleweke nini kilichozua mtihani huu tena katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
 • Taarifa kutoka kwa Msema Kweli

Facebook opens first African office in JohannesburgJOHANNESBURG, South-Africa, June 29, 2015/ -- 29 June 2015 – Facebook (NASDAQ:FB) (www.facebook.com) has opened its first office in Africa to further the company’s commitment to help businesses connect with people and grow locally and regionally. Based in Melrose Arch, Johannesburg, Facebook's newest business office will be headed by Ogilvy veteran, Nunu Ntshingila, the company's new Head of Africa.

Facebook is already an important part of how people and business connect in Africa. This office will support the significant growth in businesses and people using Facebook -- Facebook’s active user population in Africa has grown 20% to 120 million in June 2015 from 100 million in September 2014. More than 80% of these people access Facebook from their mobile phones.

“We are inspired by the incredible ways people and businesses in Africa use Facebook to connect. This momentum in Africa comes on top of strong advertiser partnerships and excellent adoption of our products across all regions. In Q1 2015, 52% of our total ad revenue came from outside the US and Canada. But we’re just getting started,” says Nicola Mendelsohn, VP, EMEA, Facebook.

“Mobile is not a trend; it’s the fastest development in communications we’ve ever seen. This couldn’t be more true in Africa – where so many people are mobile-only. This new office is a significant milestone for Facebook and our teams want to partner with businesses across the continent,” Mendelsohn adds.

“Africa is important to Facebook, and this office is a key part of our strategy to expand our investment and presence across EMEA. Facebook is already a central part of people’s lives in Africa, and with more than a billion people in Africa, we want to do more to help people and businesses connect.”

Helping businesses of all sizes to grow


“Our new African office will support our customers across the continent. We know that a one-size-fits-all approach won't work when it comes to building products and solutions that address diverse needs on the continent, which is why we are committed to creating solutions tailored to people, businesses and specifically for African markets,” says Ari Kesisoglu, Regional Director, MEA at Facebook.

Kesisoglu continued, “Our priority for the next few months is to continue the work we are already doing with some clients in this region. We will work more closely with businesses and agencies to understand the challenges, so that we can build solutions that help grow their business. People increasingly want to be connected to the world around them and desire information about new services and products to better their lives. At the same time, businesses need stronger, more flexible and less fragmented ways of reaching people in Sub Saharan Africa. Our mission will be to connect brands and consumers in Africa, creating value for all parties in the process.”

Adds Mendelsohn: “We are delighted we have a strong leadership team in place on the continent led by Nunu Ntshingila, our new Head of Africa. Nunu will join our team in September of this year and work with businesses and agencies across the region.” Nunu helped drive the creation of Ogilvy’s network in Sub Saharan Africa, which spans some 27 countries. A graduate of the University of Swaziland and Morgan State University in the US, Ntshingila has also held senior positions at Nike and the South African Tourism board.

Growth markets

Facebook will initially focus on growing its business in anchor countries in the major regions of Sub Saharan Africa: Kenya (East Africa), Nigeria (West Africa), and South Africa (Southern Africa). Other supported territories include Senegal, Ivory Coast, Ghana, Tanzania, Rwanda, Uganda, Zambia, Mozambique and Ethiopia.

Facebook will partner with governments, telecom operators, agencies and other stakeholders to deliver localised solutions to advertisers and users continent-wide. It will continue to focus on tailoring solutions, metrics and ad formats to the needs of customers and advertisers in the mobile-first, mobile-only African environment.

FOR MORE INFORMATION:

Janina Boezaart
Idea Engineers (on behalf of Facebook)
Tel: +27 72 281 2441
Email: [email protected]