Taarifa ya msiba wa Bettisheba Ketang'enyi

Bettisheba Pole Ketang'enyi
Bettisheba Pole Ketang'enyi enzi ya uhai wake

Tunasikitika kutangaza kifo cha mama Betisheba Ketangenyi, mama yake Yvonne Matinyi, Felicia Simms, Fredderek Ketangenyi pia ni Dada yake na Rossie Musika, Neema Musika, Daudi Musika na Sijaona Musika, kilichotekea tarehe Septemba 30, 2015 katika hospitali ya NIH Maryland, Marekani.

Mipango ya kusafiri mwili wa marehemu inaendelea kwa mdogo wa marehemu Daudi Musika wa 3819 Gateway terrace Burtonsville MD 20866.

Unaweza kuwasiliana
 1. Frederick Ketangenyi 267 809 5124
 2. Felicia Simms 240 608 8686
 3. Rossie Musika 240 408 2693
 4. Neema Musika 571 991 9819
 5. Specioser Musika 571332 2215
 6. Sijaona Musika 202 487 8412

Are you or know someone suffering from BIID? This person became blind on purpose

Description of the video (cross-posted from YouTube):
For most people becoming blind would be a living nightmare - but for Jewel Shuping it was the fulfilment of a lifelong dream. Jewel, 30, from North Carolina, USA, has Body Integrity Identity Disorder (BIID), a condition in which able-bodied people believe they are meant to be disabled. Her need to lose her sight was so strong that in 2006 she decided to blind herself - by having a sympathetic psychologist pour DRAIN CLEANER into her eyes. As a young child she would spend hours staring at the sun in a bid to damage her eyes, acquiring her first white cane aged 18 and becoming fully fluent in braille by the age of 20. Tired of being secretive due to the stigma surrounding the condition, Jewel is now sharing her story to help raise public awareness of BIID and to encourage people with the condition to seek professional help.Atakachokifanya Magufuli endapo mauaji yatatokea baina ya wafugaji na wakulima


Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli (pichani) akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo, ameendelea na kampeni zake nchini kote za kuisaka Ikulu huku akiwaomba Watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.

Rais Kikwete akiwa UN aahidi Tanzania kubadili Sheria ya Ndoa na Sheria ya UrithiTanzania yatangaza hatua tano za kuendeleza haki za wanawake na usawa wa kijinsia

  - Yaahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kisera na kisheria
  - Miongoni mwa Sheria zitakazohusika ni Sheria ya Ndoa na Sheria ya Urithi
  - Ni katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu - SDG’s

Tanzania imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetetea na kuendelea haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa ya kufuta sheria zinazokandamiza wanawake na kutunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia, yote katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) mapya kwa manufaa ya wanawake wa Tanzania.

Miongoni mwa hatua hizo itakuwa ni pamoja na kufuta ama kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni ambavyo kwavyo vinaendeleza ubaguzi wa wanawake kama vile Sheria ya Ndoa, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake.
Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa Jumapili, Septemba 27, 2015 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipozungumza katika Mkutano wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Akinamama: Dhamira ya Kuchukua Hatua uliohudhuriwa na wakuu wa nchi mbali mbali duniani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani.

Rais Kikwete ameuambia mkutano huo ulioitishwa kwa pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Denmark, Mexico na Kenya kuwa hatua ya pili ambayo Tanzania inakusudia kuchukua ni kuridhia makubaliano yote ya kimataifa kuhusu haki za akinamama hasa Makubaliano ya Kimataifa Juu ya Kukomesha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake – Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against Women (CEDAW).

Hatua nyingine ambazo Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania itachukua katika miaka 15 ijayo ili kuhakikisha usawa wa kijinsia nchini ni zifuatazo:
 • Kuendeleza na kuunga mkono upatikanaji wa raslimali fedha zinazolenga kuongeza usawa wa kijinsia kwa mujibu wa Ajenda ya Kugharimia Maendeleo ya Addis Ababa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinatolewa pesa za kutekeleza mipango ya kitaifa na ya Serikali za mitaa za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.
 • Kuhakikisha utekelezaji wa uwakilishi wa uongozi wa asilimia 50-50 kati ya wanawake na wanaume katika nafasi zote za maamuzi kwenye ngazi zote.
 • Kupatikana na kutumiwa kwa data na habari za ukweli katika utunzi wa sera na utoaji maamuzi ya kukomesha ubaguzi wa kijinsia.
 • Kutunga na utekelezaji mfumo wa uwajibikaji na ufuatiliaji wa haki za kijinsia na haki za akinamama zilizokubaliwa kitaifa na kwenye ngazi ya Serikali za mitaa.
Rais Kikwete pia amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuhusu hatua za kisera na kisheria ambazo zimechukuliwa na Tanzania katika miaka ya karibuni kujenga usawa wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na marekebisho yake ya mwaka 2004 ambayo yanawapa akinamama nafasi na haki ya kupata, kushikilia, kutumia na kumiliki ardhi.

Hatua nyingine ni kuwapa wanawake nafasi za maamuzi na uongozi katika nyanja za kisiasa na maisha ya umma. Katika kutekeleza hilo, idadi ya wabunge wanawake imeongezeka kutoka asilimia 21.5 ya wabunge wote mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 34.5 mwaka huu, mawaziri wanawake wameongezeka kutoka sita mwaka 2005 hadi kufikia 26 mwaka huu na idadi ya majaji wanawake imeongezeka kutoka wanane mwaka 2005 hadi kufikia 41 mwaka huu.

Rais Kikwete amesema kuwa hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni kupunguza vifo vya wanawake wakati uzazi, kutunga Sheria dhidi ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto; kuanzishwa kwa uandaaji wa Bajeti inayotilia maanani mahitaji ya wanawake na kuongeza uwezekaji wa kiuchumi wa akinamama kupitia kuanzishwa kwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) yenye kulenga kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa akinamama wafanyao biashara ndogo ndogo na za kati.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

28 Septemba, 2015

Taarifa mpya 30.09.2015 ya Wizara kuhusu Mahujaji wa Tanzania nchini Saudi Arabia

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko makubwa imepokea majina mengine mawili ya Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kupelekea vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo kufikia watu saba (7) hadi sasa.

Majina ya Mahujaji hao ni Bw. Athumani Mateso Chaulana na Bw. Ahmed Said Bawazir ambao kupitia picha zao wametambulika kuwa wamefariki dunia.

Aidha, Wizara imepokea majina mapya 19 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao bado hawajaonekana. Itakumbukuwa kuwa tarehe 29 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji wa Tanzania ambao ni kati ya 50 ambao bado hawajaonekana. Kupatikana kwa majina hayo kunafanya idadi ya Mahujaji waliopotea na majina yao kutambulika kufikia 37.

Orodha ya majina mapya 19 ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-

1. Juma Bajuka
2. Masoud Juma
3. Issa Amir Faki
4. Juma Jecha Dabu
5. Nassor Mohammed Hemed
6. Mohamed Awadh Namongo
7. Juma Bakula
8. Said Habib
9. Hamis Juma Shamte
10. Khadija Hamad
11. Rahma Salim
12. Hadija Abdallah Sefu
13. Farida Khamis
14. Laila Manunga
15. Bi. Hawa Amrani Khamis
16. Saida Awadhi
17. Maimuna Seleman Ruwaly
18. Jalia Kassim Mashule
19. Nuru Omar Karama

Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kuonekana Mahujaji saba wakiwa hai. Mahujaji hao ni:-

1. Ali Abdulrahman (Abidina)
2. Abdallah Hassan Pande
3. Suleiman Ali Kidogoli
4. Mohammed Salum
5. Mwadini Hassan
6. Habiba Ramadhan Ali (Maulana)
7. Ramadhan Muhsin

Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Missionna Vikundi vya Mahujaji unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakiki picha za mahujaji waliofariki ili kubaini Mahujaji kutoka Tanzania.

Wizara inapenda kufafanua kuwa, orodha inayotolewa si kamili kwa maana kwamba inaweza kuongezeka kwa vile baadhi ya majina ya Mahujaji yaliwayowasilishwa Ubalozini na ndugu wa mahujaji waliopotea hayamo katika orodha hii. Pia Ubalozi unaendelea kuwasiliana na vikundi vilivyopeleka Mahujaji ili kuweza kupata taarifa kamili na sahihi ya jumla ya Mahujaji wote ambao hawaonekani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
30 Septemba, 2015

New! 2015/16 Annual WEF Global Competitiveness Index - Tanzania

The 2015/16 results of the World Economic Forum’s annual Global Competitiveness Index shows that Tanzania rose one place compared to 2014/15 i.e. from 121 to 120 of 140 countries.
Here are some screen-shots

Expand all pillars/Read more at: goo.gl/Zxd7Yf

You may also want to compare with the 2014 / 2015 report: goo.gl/Zxd7Yf

Taarifa ya CUF 29/09/2015 kwa umma


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Juzi, tarehe 27 Septemba, 2015 wakati anahutubia mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa matamko ambayo ni dhahiri yanaashiria kwamba yeye na chama chake hawako tayari kwa uchaguzi huru, wa haki na wa amani na badala yake wanajiandaa kusababisha shari na kutibua hali ya amani na utulivu uliopo.

Katika hotuba yake, Dk. Ali Mohamed Shein amenukuliwa akisema mambo mawili ambayo hayapaswi kuachiwa bila ya kutolewa kauli na chama chetu. Mambo hayo ni:
 1. Kwamba eti CCM wanazo taarifa kuwa CUF inaandaa wafuasi wake kufanya fujo kuanzia tarehe 24, 25 na 26 Oktoba, 2015 na kwamba Jeshi la Polisi limejizatiti kukabiliana na hali hiyo. Kauli hiiyo imekuwa ikirudiwa rudiwa kwa namna tofauti na Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi.
 2. Kwamba CUF mara hii kimekuwa kikisisitiza katika mikutano yake ya kampeni kwamba kitashinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa vyovyote vile, kwamba CCM wakitaka wasitake watatoa Serikali, na kwamba CCM wataipeleka weneywe Serikali Mtendeni (yaliko Makao Makuu ya CUF). Akasema kwa kauli hizo CUF kinaonekana wazi kwamba hakitokuwa tayari kukubali matokeo endapo kitashindwa.
Ni vyema tuweke bayana kwamba hatukustaajabishwa na matamko hayo ijapokuwa tumesikitishwa kumuona Mgombea huyo anatumia nafasi yake kuleta hali ya taharuki katika nchi na miongoni mwa raia pasina sababu yoyote. Tunaamini kauli hizo zinatokana na taarifa zisizo sahihi na ushauri mbaya anaopewa na wasaidizi wake ambao ndiyo wanaoonekana wana nia ya kusababisha vurugu pasina sababu wakati nchi yetu kwa kiasi kikubwa imetulia. Tunasema hatukustaajabishwa kwa sababu zifuatazo:
 1. Tamko kwamba eti CUF inaandaa wafuasi wake kufanya fujo kuanzia tarehe 24, 25 na 26 Oktoba, 2015 na kwamba Jeshi la Polisi limejizatiti kukabiliana na hali hiyo, sambamba na kauli za Balozi Seif Ali Iddi za kutisha watu mara kwa mara kupitia hotuba zake, linaonekana lina lengo la kuficha mipango miovu inayopangwa na viongozi wa Kamati ya Kampeni ya CCM la kutaka kuitia nchi katika taharuki katika siku za wiki ya mwisho ya kampeni kwa lengo la kuwatisha raia wema wasijitokeze kwenda kupiga kura tarehe 25 Oktoba. Tunazo taarifa kwamba miongoni mwa mambo yanayopangwa kwenye vikao vyao vya mikakati ni kwamba vikundi vya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi maalum na kupewa mafunzo ya kufanya hujuma dhidi ya raia wema wanaandaliwa kufanya fujo katika siku za mwishoni za kampeni wakisaidiwa na kile kikundi cha baadhi ya askari wa Vikosi Maalum vya SMZ wanaojifunika nyuso na kuvaa makachara. Lengo la mkakati huu ni kuwajaza hofu raia wema wasijitokeze kwenda kupiga kura. Ziko taarifa kuwa vijana hawa wanatafutiwa sare za CUF ili ionekane ni CUF wanaofanya fujo hizo. Kwa tamko hili la Dk. Ali Mohamed Shein ni wazi sasa kwamba mazingira yanaandaliwa ya kutafuta visingizio ili kuhalalisha mipango hiyo miovu.
 2. Sambamba na mkakati huo wa kutaka kuzua taharuki, tunazo taarifa pia kwamba kutokana na CCM kufikwa na maji ya shingo na kuonekana kuelemewa na uwezo wa Timu ya Kampeni ya CUF ambayo imepelekea mafanikio makubwa katika kampeni za CUF na mgombea wake, Maalim Seif Sharif Hamad, kuna mpango mwengine unaopangwa wa kutaka kuwakamata na kuwabambikizia kesi viongozi wa Timu ya Kampeni ya CUF na baadhi ya wagombea wa CUF wanaoonekana kuwa ndiyo wanaofanikisha kampeni za CUF zinazokimaliza CCM. Miongoni mwa wanaotajwa katika orodha ya kutaka kubambikiziwa kesi na kukamatwa ni Mwenyekiti wa Timu hiyo, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, na wajumbe wengine Mhe. Mansoor Yussuf Himid, Mhe. Ismail Jussa, na Mhe. Mohamed Ahmed Mugheiry (Eddy Riyami). Katika orodha hiyo, pia wanatajwa wagombea na wanaharakati kadhaa hususan wale waliohama CCM na kujiunga na CUF hivi karibuni ambao wanaonekana kukiweka CCM katika wakati mgumu kwenye majimbo yao. Wapo baadhi yao ambao tayari wamekamatwa katika siku za karibuni na kuhusishwa na tuhuma ambazo mtu anashangaa wakati wote walipokuwa CCM hawakuwahi kuhusishwa nazo. Miongoni mwa hao ni Khamis Jabu Mohamedambaye ni Mgombea wetu wa Udiwani katika Wadi ya Chumbuni, Abdi Seif ambaye ni Mgombea wetu wa Ubunge wa Jimbo la Shaurimoyo, na Ramadhani Abdulsatar Salehe ambaye ni Mgombea wetu wa Udiwani katika Wadi ya Kwahani.
 3. CUF inamtaka Dk. Ali Mohamed Shein, iwapo kweli anataka wananchi wa Zanzibar wamuamini kwamba ana dhati ya kuhakikisha amani na utulivu, awaeleze wananchi kwa nini hadi leo hajachukua hatua zozote za kuyafunga makambi ya vijana wa CCM yanayoendesha mafunzo ya kiharamia ambayo Maalim Seif Sharif Hamad alimuandikia rasmi na hata kumueleza ana kwa ana juu ya taarifa za kuwepo kwake. Makambi hayo ni pamoja na ile ya Tunguu (iliyopewa jina la SCENARIO ambayo ina vijana wapatao 900), Dunga (ina vijana 150), Welezo (ina vijana 200), na Amani CCM Mkoa (yenye vijana 300) huku kukitajwa mipango ya kufungua kambi nyengine kama hizo katika maeneo ya Kilombero, Pangatupu, Bumbwini na Makunduchi. Maalim Seif pia aliliarifu Jeshi la Polisi kuhusu taarifa za kuwepo makambi haya. CUF pia imechukua hatua ya kuiarifu jumuiya ya kimataifa juu kuwepo kwa makambi haya.
 4. CUF pia inataka ielezwe iwapo kweli Dk. Ali Mohamed Shein ana nia ya kuhakikisha amani na utulivu katika nchi yetu amechukua hatua gani dhidi ya matukio ambayo yamekuwa yakifanyika hadharani na yameandikwa kwenye magazeti mbali mbali na hata kuwepo kwa picha zake za video ya kuwepo kwa kikundi maalum kinachohusisha baadhi ya askari wa Vikosi vya SMZ ambavyo viko chini yake na ambao wamekuwa wakivaa makachara na kujifunika nyuso na kuhujumu watu mitaani hususan wakati wa uandikishaji wa wapiga kura wapya katika miezi ya Juni na Julai, mwaka huu. Matukio haya pia yameripotiwa na Maalim Seif kwake Dk. Shein na kwa Rais Jakaya Kikwete na pia CUF ikamuandikia rasmi Kamishna wa Polisi Zanzibar lakini hadi leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Matukio hayo yalifikia hatua mbaya tarehe 4 Julai, mwaka huu, kijijini Makunduchi pale watu wawili, Kheri Makame Hassan na Ramadhani Hija Hassan, walipopigwa risasi na kujeruhiwa vibaya. Tunashukuru kwamba jumuiya ya kimataifa imetuhakikishia kuwa inafuatilia matendo haya yote na kwamba wahusika watabeba dhima kwa yatakayotokea kulingana na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeiridhia.
 5. CUF inataka Dk. Ali Mohamed Shein pia aeleze iwapo yeye ni msimamizi wa amani na utulivu na anapenda uchaguzi huru na wa haki, ni kwa nini anakaa kimya wakati kikundi maalum cha askari wa Vikosi vya SMZ ambavyo viko chini yake wamekuwa wakiendesha zoezi maalum la kupita mitaani na barabarani, mjini na mashamba na kuzipachua na kuzichana picha za mgombea Urais wa CUF na wakati mwengine kubandika picha za Dk. Shein juu ya picha za Maalim Seif kinyume na Mwongozo wa Maadili ya Uchaguzi ambayo vyama vyote vya siasa, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vilisaini kwa pamoja? Haya yanafanyika huku askari wenyewe wa Vikosi wakikerwa na kutumiwa kisiasa kinyume na maadili ya kazi zao.
 6. Kuhusu kauli kwamba CUF mara hii kimekuwa kikisisitiza katika mikutano yake ya kampeni kwamba kitashinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa vyovyote vile, kwamba CCM wakitaka wasitake watatoa Serikali, na kwamba CCM wataipeleka weneywe Serikali Mtendeni na kwamba kwa kauli hizo CUF kinaonekana wazi kwamba hakitokuwa tayari kukubali matokeo endapo kitashindwa, hili ndiyo linavunja hadhi na muruwa wa Mgombea Urais wa CCM kuliko jambo jengine lolote na kumuonesha udhaifu wake. Waandishi wa habari na wananchi watakumbuka kuwa tarehe 23 Agosti, 2015 wakati Mgombea Urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alipokuwa anazungumza baada ya kuchukua fomu za uteuzi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) alitamka bayana kwamba iwapo uchaguzi utakuwa huru, wa haki na wazi, na yeye ikatokezea akashindwa basi atakubali matokeo na kumpongeza mshindi. Akatumia fursa hiyo kumtaka na Dk. Ali Mohamed Shein na yeye atoe kauli kama hiyo. Siku iliyofuata, tarehe 24 Agosti, Dk. Shein alichukua fomu na kuulizwa swali hilo, lakini waandishi wa habari na wananchi wote wakamsikia akisema kwamba, “Bado ni mapema kutoa kauli kama hiyo”. Hadi leo hajatoa kauli kwamba iwapo atashindwa ataheshimu na kukubali matokeo ya uchaguzi, atampongeza mshindi halali na atakabidhi madaraka kwa atakayepewa ridhaa na wananchi. Sasa hapo ni nani ambaye anaonesha dalili za kutokuwa tayari kukubali matokeo?
Hizi ni hoja za msingi ambazo tunamtarajia Mgombea Urais kupitia CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, azitolee ufafanuzi na nyengine zinahitaji hatua madhubuti kuchukuliwa ili tujue iwapo kweli anayoyasema kuhusu amani na utulivu yanatoka katika dhati ya nafsi yake au ni kauli zinazoficha dhamira nyengine ambayo hataki kuisema.

Kwa upande wetu, Chama Cha Wananchi (CUF) tunazichukulia kauli hizi kuwa ni dalili za kutapatapa kwa Mgombea Urais huyo na chama chake baada ya kubaini kwamba mambo yanawaendea kombo kutokana na mwamko mkubwa unaooneshwa na wananchi wa Zanzibar kumkataa yeye na chama chake. Wananchi wa Zanzibar wameamua kukipa talaka chama cha CCM baada ya kuchoshwa na ahadi za chama hicho zisizotimizwa miaka nenda miaka rudi. Sasa wameamua kuikumbatia fursa ya mabadiliko yanayowakilishwa na CUF na mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad.

Tunapenda kukinasihi Chama Cha Mapinduzi kwamba kisiwaingize Jeshi la Polisi katika mipango yao miovu wanayoipanga. Kwa hakika, hadi sasa Jeshi la Polisi limekuwa likifanya kazi nzuri ya kuhakikisha amani na utulivu katika kipindi chote cha kampeni. Na sisi CUF tumekuwa tukitoa mashirikiano ya hali ya juu ili kwa pamoja tuhakikishe nchi yetu inabaki salama na kwamba tunavuka katika kipindi hichi cha uchaguzi katika hali ya amani na utulivu. Hatudhani ni busara kwa viongozi wa CCM kula njama za kutaka kuturudisha kwenye vurugu na fujo.

CUF tunatoa wito kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama hapa nchini kuendelea kusimamia amani na utulivu wa nchi yetu pasina kuegemea upande wowote wa kisiasa na kuendelea kuwajengea imani wananchi wote kwa kukataa kuingizwa katika ubishani wa kisiasa wakati huu wa harakati za kampeni na hatua nyengine za uchaguzi. Sisi katika CUF tunawahakikishia mashirikiano yetu katika kufanikisha dhamira hiyo kama ambavyo tumekuwa tukifanya wakati wote.

Mwisho, tunamkumbusha Mgombea wa CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, kwamba alikabidhiwa uongozi wa nchi mwaka 2010 katika hali ya usalama wa hali ya juu na umoja wa kupigiwa mfano wa wananchi wa Zanzibar kutokana na kazi kubwa ya kuleta na kusimamia maridhiano iliyofanywa na mtangulizi wake, Dk. Amani Karume, akishirikiana na Maalim Seif Sharif Hamad. Tunamuomba na kumnasihi na yeye awe muungwana kwa kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki na utakaofanyika katika mazingira ya amani, usalama na maelewano, na pale wananchi wa Zanzibar watakapofanya maamuzi yao tarehe 25 Oktoba, 2015 basi ayaheshimu maamuzi hayo. Bila shaka, muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa utaendelea na unavihakikishia vyama vyote vya siasa vitakavyopata uwakilishi kwenye Baraza la Wawakilishi kuwa sehemu ya Serikali hiyo.

CUF tunalihakikishia Jeshi la Polisi na vyombo vyote vya ulinzi na usalama hapa nchini kwamba tutaendelea kuwa mfano katika kufuata sheria bila shuruti na kwamba tutaendelea kutoa mashirikiano kwao katika kuendelea kuitunza tunu ya amani na usalama katika nchi yetu. Tunawaomba na wao wasisite kuwasiliana na sisi kama ambavyo wamekuwa wakifanya kila inapoonekana kuna haja hiyo ili kwa pamoja tushirikiane kufanikisha uchaguzi huru, wa haki na wa amani. CUF tunaendelea kutoa wito kwa wanachama na wafuasi wetu na wananchi wote kwa ujumla kufuata sheria na pia maelekezo ya viongozi wetu katika kutunza amani na utulivu wakati wote wakijua kwamba tunaelekea katika ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
MKURUGENZI WA MAWASILIANO – TIMU YA KAMPENI YA CUF
ZANZIBAR – 29 SEPTEMBA, 2015

Kuhusu utalii wa Mfalme wa Falme za Kiarabu na kutorosha twiga kutoka Loliondo

SERIKALI imekanusha uvumi uliozagaa katika mitandao ya jamii wiki hii kuwa wanyama aina ya twiga wanatoroshwa kutoka pori tengefu la Loliondo na kupelekwa nje ya nchi.

Katibu Mkuu wa Wizara Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru (Pichani) ameziita habari hizo kuwa za uongo, uzushi na uchochezi.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Dkt. Meru alisema jambo hilo si la kweli na linalenga kuleta chuki dhidi ya serikali.

“Picha zile zimetolewa katika intaneti na kuelezwa kuwa ni za Tanzania, si kweli. Ni picha za kughushi,” alisema Dkt Meru.

Pia alibainisha kwamba twiga wa Tanzania wanatumika kama nembo ya taifa na hawaruhusiwi kuwindwa hata kidogo, “sasa kusema wamewindwa na kusafirishwa ni uzushi na upotoshaji.”

Alisema ukweli uliopo ni kwamba Kampuni ya Ortero Business Corporation iliyosajiliwa hapa nchini iliomba kibali cha kawaida cha uwindaji na kukubaliwa.

Kampuni hiyo ilipata vibali vya watu wanane vya uwindaji wa wanyama wakiwemo kongoni, ngiri, pofu, na swala pamoja na aina ya ndege mbalimbali. Kibali hakikuhusisha wanyama kama twiga, simba wala tembo.

Alisema kufuatia kibali hicho tarehe 25 Septemba, 2015 zilikuja ndege tatu aina ya CI 30 UAS, 312, na kupata kibali namba TCAA/5055/21294 ya mizigo; ndege ya abiria L6RJI iliyopata kibali namba TCAA/5055/21295 na ndege nyingine ya abiria A9HRM 767 iliyopata kibali namba TCAA/5055/21300.

Ndege hizo zilikuwa na Mohamed Sheikh Mohamed Bin Rashid, Mfalme toka Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu akiambatana na msafara wa watu 137 na kutua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Alisema ujumbe huo wa watu ulifuata taratibu za kuingia nchini na kupata vibali halali vikiwemo vya uhamiaji na baadaye walielekea Loliondo.

Miongoni mwa watu hao walikuwemo watazamaji, wafanyakazi wa ndege hizo, watoa huduma wa mfalme huyo miongoni mwa wengine.

Alisema vibali vya uwindaji huo vimeipatia serikali dola za kimarekani 41,400 sawa na Tshs milioni 85.

Kwa mujibu wa Dkt. Meru, baadhi ya watalii hao pamoja na mfalme huyo waliondoka Septemba 29, 2015 huku baadhi ya maofisa wake wakiwa bado hapa nchini kwa ajili ya kukamilisha utaratibu wa kuhakiki wanyama na ndege waliowindwa na malipo ya serikali.

Dkt. Meru alisema uwindaji huo ulisimamiwa na maofisa wa jeshi la polisi, usalama wa taifa, maofisa wa kuzuia wanyama wanaokatazwa kuwindwa, maofisa wa halmashauri ya Loliondo na maafisa wa wizara kitengo cha kuzuia ujangili.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Bw. Herman Keraryo utalii wa kuwinda ni moja ya vyanzo vikubwa vya mapato si kwa Tanzania tu bali na nchi nyingine duniani.

Kwa mwaka jana tu, utaliihuo uliingizia Wizara dola za Kimarekani milioni 18.

Alitaja faida nyingine kama kuwianisha idadi ya wanyama katika mapori na kuzuia ujangili.

WhatsApp becomes popular platform for trash talk in Tanzania’s 2015 election campaign


In Tanzania, WhatsApp has transformed political communication in the country.

“WhatsApp is a preferred tool of choice for propaganda, mudslinging, and negative messaging,” a digital media strategist tells Quartz, requesting anonymity in order to openly discuss how the platform is being used by political parties. The app is the go-to platform for “messaging you can’t say yourself that surrogates can do for you,” the strategist adds. In this way, WhatsApp networks are similar to Super PACs in the US, the officially unaffiliated groups that nonetheless raise money and cater directly for their chosen candidates’ whims.

Data in Tanzania on WhatsApp usage are scarce, but political operatives are flocking to the platform because it cuts across all demographics, unlike other social networks.

“People are sharing a lot of stuff but mostly they are using it to manipulate,”  “Taking screenshots to show that their opponents are [struggling],” Maxence Melo, co-founder of Jamii Forums, one of Tanzania’s most popular online platforms, tells Quartz.


Read Omar Mohamded's full post at qz.com/510899 

Taarifa ya CCM 29/09/2015 kwa umma


TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini. 

Kama ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani, zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa, tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye vitendo vya ufunjifu wa amani. 

Tukio la Tanga sio la kwanza. Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri. Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi. Lakini viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya taifa letu. 

Tunawasihi wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi. Wenzetu wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa. 

Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga. Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana. Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa. 

Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni. Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi. Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu. Katika mikutano ya kampeni, ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku mikutano ikiendelea.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na akasikika na watu wote. Mabadiliko wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya mgombea wao. 

Tunarudia kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM, na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa kura. Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo. Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi. 

Imetolewa na:
 
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
29.09.2015

Serikali yakanusha kukamatwa masanduku yenye karatasi zilizopigwa kura


Mndeme: Tanzania tuna migodi ya thamani kuliko dhahabu na gesi - II

TANZANIA TUNA MIGODI YA THAMANI KULIKO DHAHABU NA GESI

Sehemu ya Pili

Sehemu ya kwanza ya makala hii nilieleza kwa ufupi umuhim wa nchi zenye uchumi mdogo kama Tanzania kutazama namna ambavyo zinaweza kujiimarisha kiuchumi na kuboresha maisha na kipato cha watu wake kwa kutumia rasilimali au vitega uchumi vilivyo ndani ya uwezo wao. Msingi wa ushauri huu, ni ukweli kwamba, nchi zenye uchumi mdogo ziko katika mazingira magumu na yasiyo rafiki kuziwezesha kushindana kiuchumi na nchi zenye uchumi mkubwa. Niliahidi nitazungumzia mambo matatu au manne ambayo ninashawishika sisi kama nchi, tumeytatazama tu kama huduma na sio kama rasiliamali za uzalishaji mali. Nianze na la kwanza.

MGODI WA KWANZA: LUGHA YA KISWAHILI

Siku moja mwaka 2012 kipindi cha majira ya baridi nchii Ujerumani, nilisafiri kwa treni kutoka mji wa Aachen hadi Jiji la Bonn nikiongozana na mtanzania mwenzangu niliyekutana naye Uholanzi akiwa kwenye masomo ya shahada ya uzamivu. Nchi za wenzetu zina "viburi na unazi" kwenye matumizi ya lugha zao ndani ya mipaka ya nchi zao na raia wao hawababaishwi na lugha za mataifa mengine kirahisi bila kujali umaarufu wa lugha hizo. Kwa mfano: pamoja na kwamba treni za nchi nyingi za Ulaya zinafanya safari za kimataifa na zinabeba abiria wa nchi nyingi, lakini lugha inayotumika ndani ya treni hizo kutoa maelekezo ni za nchi inakotoka. Hivyo ukipanda treni ya Ujerumani kwenda nayo Uholanzi au Ufaransa, basi ujue kwamba humo ndani utakachokisikia muda wote (au kwa sehemu kubwa) ni Kijerumani pekee kama ilivyokua kwenye treni tuliyoipanda sisi.Jioni tukiwa njiani kutokea Bonn, tulianza kusikia maelezo ya mara kwa mara toka kwa wahudumu wa treni ile na kama kawaida hatukua twaelewa kinachoongelewa zaidi ya manano machache tuliyokua tumekariri na kuhisi kuna jambo lisilo la kawaida kuhusu ile safari. Baadaye kidogo treni ikasimama na abiria wote wakaanza kushuka. Tulipouliza abiria aliyekua pembeni yetu akatuambia kwamba ile treni haindelei na safari hivyo inatulazimu kushuka kwenye kituo kile na tusubiri treni nyingine ambayo ingefika baada ya muda mfupi. Vituo vya treni kwa wenzetu, ni vikubwa na vinachanganya sana ikichangiwa na matumizi ya lugha kwenye vibao vya maelekezo. Tukaanza kuulizana na mwenzangu ni kituo namba ngapi twatakiwa kwenda. Tulipojikuta tunafuata tu mkumbo wanapoelekea wengine bila kujua waendako, tuliamua kumuomba dada mmoja wa kijerumani aliyekua anatembea karibu na sisi atuelekeze tunapotakiwa kungoja treni nyingine.

Yule dada alitujibu swali letu kwa ukarimu sana (kitu ambacho sio kawaida kwa wenyeji wa nchi hizi ambazo unaweza kumuuliza mtu kitu akajifanya haelewi kingereza au akakuangalia tu na kukuacha). Zaidi sana, tulishangaa alipotujibu kwa KISWAHILI, "kama mwaelekea Aachen mwatakiwa kwenda upande wa pili namba 8". Tuliangaliana na mwenzangu kama watu waliomwagiwa maji ya baridi. Badala ya kufuata maelekezo yake, tulianza kumuuliza imekuaje anajua kiswahili na iwapo sio mjerumani. Dada yule alikua ni mjerumani wa asili kabisa na kakulia vijijini. Tukagundua kuwa, muda wote tuliokua twajimwaga tukijua hakuna anayetuelewa kwenye treni iliyojaa watu weupe, yeye alikua akitusikiliza. Tuliongea naye kwa muda wote tuliosubiri treni na hadi mwisho wa safari huku akitusimulia habari za Moroko, Sinza Mori, na mengine mengi kwani alikua ana miezi kama 3 tu tangu atoke Dar es Salaam alikokwenda kujifunza Kiswahili. Tangu siku ile, niliondoa mtazamo niliokua nao kwamba Kiswahili ni cha watanzania na nchi jirani. Niliondoa dhana kwamba kuna maeneo chaweza kuwa cha siri kama vile kuonge kisandawe na kiaangaza. Niligundua kuwa sina uhuru wa kukitumia kama lugha ya siri mahali popote kwa kigezo kwamba sio Tanzania au hakuna watu wenye rangi kama yangu. Zaidi ya yote, NILIANZA KUTAFAKARI UKUU NA NGUVU YA KISWAHILI.Kwa nini nakitazama Kiswahili kama Rasilimali?

 • Kiswahili ndio lugha hii pekee yenye asili ya kiafrika inayotambulika kama lugha rasmi ya mawasiliano katika Umoja wa Nchi za Africa (African Union). Hii ina maana, kwa wale wanaoifahamu, wanaweza kuitumia katika shughuli za umoja huu. Miezi kama mitatu iliyopita, nilimsikiliza Rais Kikwete akiwa nchini Afrika Kusini akitoa hotuba yake ya mwisho kama mkuu wa nchi katika umoja huo kwa Kiswahili. Hii haikua mara ya kwanza, kwani alishawahi kutoa hotuba kwa Kiswahili pale Addis-Ababa makao makuu ya AU.
 • Kiswahili ni kati ya fahari na utambulisho wa Mtanzania. Wakati nchi nyingi za kiafrika zimegawanyika kwa misingi ya lugha za asilki huku zikitegemea lugha za wakoloni (kifaransa, kingereza, kiaarabu na kireno) kama njia kuu za mawasiliano rasmi; sisi ni nchi pekee Afrika ambayo unaweza kwenda mahali popote, ofisi yeyote, na kijiji chochote bila kua na hofu kubwa ya kushindwa kuwasiliana na unaowaendea. Unapokua nje ya Tanzania na unapomuona mtanzania mwenzako, cha kwanza kinachowafanya mujisikie ni wamoja ni uwezo wa kuongea Kiswahili.
 • Tanzania ina wasomi waliobobea katika lugha ya kiswahili na wamejaa kwenye ngazi zote za elimu. Taasisi ya Lugha ya Kiswahili pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni kati ya taasisi kubwa kabisa za chuo ikiwa imesheheni wabobezi wa kutosha hadi ngazi ya Uprofesa. Hivyo basi, hii sio tu ni lugha tunayomudu vizuri, bali, ni lugha tunayojifunza kisomi na kisayansi. Uwezo huu wa kitaaluma, ndio unaopelekea watu toka nchi zingine kuja kujifunza Kiswahili katika chuo chetu maana ndipo penye msingi.
 • Kiswahili kimetumika kuandika machapisho mengi ya kila aina na maduka mengi ya vitabu yamejaa wingi wa machapisho ya kiswahili. Pamoja na kwamba hatujafanya bidiii ya kutosha kuandika vitabu vya kiswahili, tulivyonavyo si haba sana kwa kudhihirisha ukuu wa lugha yetu.
Nisiendelee kutoa sababu nyingi ila itoshe kusema, lugha yetu adhimu ya Kiswahili ina umuhim mkubwa sana kwa mtanzania na nina ujasiri wa kusema ndio utambulisho mkubwa wa kwanza tunapokua nje ya mipaka ya nchi yetu. Pamoja na kwamba nchi zinazotuzunguka zinatumia Kiswahili kama moja ya lugha zao, ukweli unabaki kuwa, wanabahatisha tu, na wanajua kwamba mama wa kiswahili duniani ni Tanzania, na kama unataka kukisikia Kiswahili, lazima umtafute mtazania.Maswali la Kujiuliza

Pamoja na umuhimu huu wa Kiswahili kwa watanzania, yako maswali ya msingi ya kujiuliza:
 1. Tumekitumiaje Kiswahili zaidi ya kuwa lugha ya mawasiliano miongoni mwetu?
 2. Tumekitumiaje kama rasilimali ya kutuwezesha kiuchumi?
 3. Tumekitumiaje kutengeneza ajira za wananchi wetu wa makundi mbalimbali?
 4. Kiswahili kama lugha, kimeajiri watanzania wangapi na wa kada zipi na wanalipwaje?
 5. Tumekitumiaje kujijengea heshima kama taifa kubwa na lenye uwezo na utamaduni wenye nguvu barani Afrika?
 6. Tumekitumiaje kuwafanya wengine watuone hawana pa kukimbilia isipokua kwetu wanapohitaji suluhisho la lugha ya Kiuswahili?
 7. Tumekitumiaje kuwafanya watanzania wasiojione wanyonge na dhaifu kwa kuwa "watumwa wa Kiswahili" na badala yake wajione wenye fahari na wajanja kama ilivyo kwa lugha zingine?
 8. Je, yatosha kujivunia Kiswahili kama utambulisho wa Utanzania wetu?
Maswali ni mengi na huenda majibu yake sio magumu na hayahitaji nguvu kubwa kuyapata. Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, nikiwa nafuatilia kipindi cha maswali na majibu bungeni, Mh Mariam Nassoro Kisangi (mbunge wa Viti Maalum) aliuliza swali ambalo majibu yake yalinisumbua na kujikuta nina hasira na kulalamika. Mbunge huyu alirejea kauli ya Rais wa Gabon ambaye kwa "mahaba aliyoyajenga kwenye lugha hii adhimu", aliiomba serikali ya Tanzania impelekee mtaalamu wa kumfundisha Kiswahili kwa gharama zake. Mbunge huyu alitaka kujua swala hilo lilikua limefikia wapi na serikali iliitumiaje fursa hiyo kwa nchi yetu kujitangaza zaidi kwa lugha ya Kiswahili.

Nakumbuka aliyejibu swali hili alikua Naibu waziri wa Elimu (Mh Jenister Mhagama) ambaye siku hiyo ndio ilikua ya kwanza kwake bungeni kama naibu waziri baada ya kuapishwa siku iliyotangulia. Siku hiyo alikua na jukumu la kujibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa wizara ya Elimu. Katika majibu yake, alitoa mlolongo mrefu wa majibu. Kwa kifupi,mtu huyo alikua bado hajapelekwa na "kwamba eti" kulikua na "michakato/taratibu za kiserekali" za kufuata ili kumpata mtu sahihi baada ya aliyekua kateuliwa kupata matatizo. Hadi anajibu swali hili, ilikua imeshapita miezi 9 tangu ombi la rais huyo litolewe na kusema ukweli majibu haya yalinisonenosha sana kama yalivyomsonensha mbunge aliyeuliza swali. Hata alipoulizwa swali la nyongeza, alijibu kikawaida sana kama vile hayo ndio maisha ya "kiserikali" katika kufanya maamuzi. Ilikua shida kidogo kuingia akilini kwamba, kati ya maelfu ya waalimu wa kiswahili walioko kwenye mashule ya sekondari, vyuo vikuu, na wale waliojaa kwenye taasisi zingine; serikali yetu sikivu haikuweza kumpta MTU MMOJA kwa miezi tisa kupewa jukumu la kwenda KULA BATA na mshahara mnono kwenye jumba la rais kwa kufundisha kiswahili. Huu ni mujiza ambao huenda unapatikana Tanzania tu. Niliwaza kuwa iwapo nafasi hiyo ingepekekwa Kenya, mtu huyo angepatika siku hiyohiyo na angekua kafika Gabon kesho yake kabla ya jua kuzama (Rejea jibu la waziri hapa).Kwa nini nimekumbusha habari hii?

Nimetaka kukuonesha ni kwa jinsi gani serikali yetu na taasisi zake, haijawahi kukifikiria Kiswahili kama MGODI WA MADINI. Hakuna mkakati wa kitaifa (kama hupo sijawahi kuuona au haujatendewa kazi), wa kukibadili Kiswahili kutoka kuwa tu lugha ya kuwasiliana na bibi na kupata huduma za kijamii, na kukifanya kuwa UWEKEZAJI wenye tija za kitamaduni na kiuchumi kwa taifa. Kukitazama kama uwekezaji unaohitaji mtaji mdogo sana na wataalamu wa ndani bila msaada wa wafadhili na wataalamu wa nje. Sio lengo langu kuisema vibaya serikali au kuukosoa, lakini kama mdau wa maendeleo ya nchi yangu, nalazimika kusema ukweli kwamba hakuna fikra za uzalishaji mali (zilizo wazi) kwenye matumizi ya Kiswahili kama moja ya utajiri wa nchi yetu. Kwangu mimi, nakiopna KISWAHILI KAMA MADINI YENYE THAMANI KULIKO DHAHABU NA YAKO KWENYE KINA KIFUPI SANA CHINI YA ARDHI tunayoikanyaga kila kukicha. Mgoni huu ni wa uhakika kwani hautakwisha (depleted), hauna athari za kimazingira, na mapato yake hayataporwa na wawekezaji kwenda nje maana yatakua yetu kwa manufaa yetu. Tuna wataalamu na kila kifaa tunachohitaji kw auchimbaji huu na kinachotakiwa ni utayari tu.Sio serikali pekee haijakipa Kiswahili umuhim wake kama rasilimali, bali hata watanzania katika ujumla wetu, hatujakitazama kwa sura hiyo. Wafanyabiashara na wawekezaji kwenye taaluma na mafunzo mbalimbali, hawajaweza kukichukua Kiswahili kama rasilimali na malighafi inayohitaji kuchakatwa ili kuongezwa thamani na kuuzwa kwa bei nzuri ya soko kubwa linalotuzunguka duniani kote. Tembelea shule zote za lugha mijini, utakutana na kozi za kifaransa, kingereza, kiispania na hata kichina; lakini huwezi kukuta kozi za Kiswahili kwa maana ya mafunzo ya kuwasaidia wageni na wenyeji kukijua vizuri zaidi na kwa ufasaha. Tuna watanzania wengi (hata miongoni mwa wasomi), hawajui kiswahili fasaha na wakikiongea wanakichanganya sana. Wengi wetu tumeathirika na lugha zetu za asili (kikurya, kihaya, kipare, kinyakyusa, nk) na athari hiyo imeharibu ladha ya kiswahili. Lakini, nani kaona uhitaji wa kujifunza zaidi Kiswahili? Na hata akitaka atakwenda kujifunza wapi? Na ajifunze ili iwaje?

Serikali yetu sikivu, haijaweka masharti yoyote ya wageni yatakayowalazimisha kuona umuhim wa Kiswahili. Nchi nyingi duniani zinazoezi lugha zao, huweka masharti kwa wageni kuhusu lugha zao. Kwa mfano, wanafunzi wanaokwenda kusoma shahada za juu kwenye nchi kama Ujerumani, China, Japani na kwingineko, hulazimika kutumia miezi 6 hadi 12 kabla ya kuanza masomo rasmi kujifunza lugha za wenyeji pamoja na kwamba masomo yanatolewa kwa lugha ya Kingereza. Nchi kama Uingereza, hawakuruhusu kuingia kwenye nchi yao kama mwanafunzi au mfanyakazi bila kuonesha uwezo wa kutosha wa lugha ya kingereza na unapimwa kwa mtihani unaoulipia zaidi ya shilingi laki tatu. Masharti haya na mengine mengi, pamoja na kwamba humsaidia muhusika kuishi bila ugumu wa mawasiliano katika nchi husika, pia yanazisaidia nchi huzo kukuza lugha zao na kuzipa umuhim mbele ya walimwengu.

Nitaendelea katika Sehemu ya Tatu kuhusu Lugha ya Kiswahili, nikijikita katika kuonesha fursa na kutoa mapendekezo yangu ya nini cha kufanya kukirasimisha Kiswahili kama rasilimali na uwekezaji wenye tija.

---
Mwalimu MM ni mhadhiri katika kitengo cha Sayansi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mtafiti wa mifumo ya TEHAMA katika Huduma za afya (Health Informatics). Unaweza kuwasiliana naye kupitia [email protected].
Blog: www.mwalimumm.blogspot.com

Jaji Lubuva azungumzia: Mbadala wa waliofariki; Muda siku ya kupiga kura; Walemavu; Matusi


MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva ametoa ovyo kali na kuahidi kuwachukulia hatua za kisheria, wanasiasa na wagombea wanaofanya kampeni chafu kwa kutaja majina ya watu, pamoja na kuingilia kazi za NEC.

Anadai, amekuwa akishangwazwa sana na kitendo cha baadhi ya wagombea kupanda majukwaani kuwasema vibaya wagombea wenzao na kuwakashifu badala ya kutumia nafasi hiyo kwa kutangaza sera za chama na wagombea.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya New Afrika alipokutana na wawakilishi wa walemavu nchini ili kuzungumzia masuala mbalimbali ya uchaguzi likiwemo la kuwapo utaratibu wa kupiga kura.

Kabla ya utaratibu wa upigaji kura kwa walemavu kutolewa, Lubuva pia amevitaka vyama vya siasa kutokuwa na wasiwasi na NEC kama ilivyo kwa baadhi ya vyama ambavyo vinaonekana kutoiamini tume hiyo na kuwataka wanasiasa wanaona mwanya wa kuiba kura, wampe taarifa ili wazifanyie kazi.
“Kuna baadhi ya wanasiasa sitawataja lakini nawasikia wakiwasisitiza wanachama wao kutoondoka katika vituo vya kupigia kura siku hiyo kwa kigezo cha kulinda kura.
“Huo ni upotoshaji na ni kujisumbua, kwani hakuna kura itakayoibiwa kila mtu akimaliza arudi kwao na kusubiri matokeo” 
Neye Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Emmanuel Kawishe wakati akitoa maelekezo kwa walemavu hao amesema, siku hiyo ya uchaguzi, walemavu wote hawatakaa foleni bali watapita moja kwa moja sehemu ya kupigia kura. Kawishe amesema kundi hilo na makundi maalumu likiwemo la wazee, wajawazito hawatakaa foleni pia. Na kwa wale walemavu wa macho wataruhusiwa kwenda na wasaidizi wao ndani ya chumba cha kupigia kura.
“Lakini tunawakumbusha tu makundi hayo ya walemavu wachague wasaidizi wasiohusika na uongozi katika chama chochote na wala asiwe wakala wa chama au Tume ili kuepusha ulaghai na wizi wa kura” 
Pia amesema NEC inampango wa kuweka makaratasi maalumu ya kuandikia kwa wale wenye ulemavi wa macho pamoja kuandika maandishi makubwa ya wagombea ili kuwasaidia wenye matatizo ya kuona kama walemavu wa ngozi (albino).
“Nadhani tutakuwa tumezingatia maombi yenu kwenye mchakato wa upigaji kura, tumeweka vituo katika maeneo rafiki kwenu na tumefanya hivyo, vituo vyote 72,000 vilipo katika maeneo mazuri mtakayoweza kwenda”
Amesema vituo vyote vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufugwa saa 12:00 ambapo mawakala wote wanatakiwa kuwepo katika chumba cha kupigia kura.
“Lakini kwa wakala ambaye hatakuwepo zoezi litaendelea kama kawaida hatutasitisha zoezi ili kumsubiri” 
Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa ufafanuzi juu ya Majimbo na Kata zote ambazo vyama vya siasa vimepoteza wagombea wao, Oktoba 12 hadi Novemba 22 vyama vinatakiwa kumteua mgombea mwingine ili kuziba pengo.
 • via MwanaHALISI Online

Polisi Arusha yaua raia wa ndani na nje watuhumiwa wa ujambaziWatu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa na askari Polisi wakati wa mapambano ya majibizano ya risasi usiku wa tarehe 17.09.2015 saa 3:30 maeneo ya Chekereni mpakani mwa wilaya ya Arumeru na halmashauri ya Jiji la Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alielezea mazingira ya tukio hilo kuwa jeshi hilo lilipokea taarifa za Kiintelejensia juu ya kuwepo kwa kundi la majambazi lililotaka kufanya uvamizi na uporaji ndani ya jiji la Arusha.

“Tulipata taarifa tangu Agosti 19 mwaka huu kuwa kutakuwepo kundi la majambazi toka nchini Kenya ambalo wangeshirikiana na wengine wa hapa nchini kwa nia ya kufanya uhalifu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo taasisi za fedha”. Alisema Sabas.

Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hiyo waliendelea na ufuatiliaji na kufanikiwa kukamata kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Sixtus Alfredy Ngowi (51) Mtanzania, Mkazi wa Ngulelo katika jiji hilo juu ya kushirikiana na majambazi wenzake wanaodaiwa toka nchini Kenya ambao hufanya matukio mbalimbali ya kiuhalifu hapa nchini.

Baadhi ya matukio ambayo majambazi hayo yameyafanywa ni pamoja na tukio la uporaji wa fedha zaidi ya dola 2,000,000 lilitokea jijini Dar es salaam mwaka 2005 kwenye Kampuni ya Security Group 4.

Mbali na tukio hilo pia mwaka 2002 wanadaiwa kuhusika na tukio la uvamizi wa Benki ya NBC tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro huku Mwaka 2014 jambazi huyo amewahi pia kushtakiwa nchini Kenya kwa matukio ya uhalifu katika Mahakama ya Mlimani Law Court iliyopo jijini Nairobi lakini baadae aliachiwa huru.

Alizidi kukiri kuhusika katika matukio ya ujambazi huku akishirikiana na wenzake katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika jiji la Arusha ambalo lilikuwa linawalenga wafanyabiashara wakubwa wa Madini ya Tanzanite na Hoteli za Kitalii.

Miongoni mwa tukio walilolifanya ni kumjeruhi mfanyabiashara wa madini aitwaye Mathius Manga ambaye alipigwa kwa risasi kwenye ubavu wa kulia.

Kamanda Sabas alisema kwamba mara baada ya kuridhishwa na mahojiano baadae jambazi huyo alikubali kushirikiana na Polisi ili aweze kufanikisha juu ya upatikanaji wa wenzake ambao siku ya jana walipanga kuvamia katika duka la kubadilishia fedha liitwalo Sanya lililopo jijini Arusha.

Walipokuwa wanaelekea kwenye eneo la tukio akiwa anaongozana na askari Polisi kwa nia ya kufanikisha kuwapata majamabzi wengine, mara tu baada ya kufika kabla hawajawakamata majambazi hao ambao walikuwa kwenye gari aina ya Noah rangi ya silver yenye namba za usajili T. 981 AVK walishtuka na kuanza kulishambulia gari lililokuwa na askari Polisi na kumjeruhi mwenzao Sixtus Alfedy Ngowi ambaye alifariki muda mfupi wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali. Mara baada ya kuona hivyo, Polisi nao walijibu mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi watatu huku wengine wakifanikiwa kukimbia. Katika upekuzi kila mmoja alikutwa na bastola pamoja na risasi. Pia walikuta mabegi matatu meusi ambapo ndani yake kulikuwa na bunduki mbili aina ya AK 47 zenye namba 83 LG 3953 56-1 na nyingine yenye maandishi ya kirusi pamoja na SMG moja yenye namba 56-1 28038394.

Bastola ambazo zilikutwa toka kwa majambazi hao zilikuwa na namba CZ 75 Compact Luger-9mm namba A. 269206, CZ 85 B Luger 9mm namba 051967 na Chines Pistol namba 967741. Pia zilipatikana magazine nne tupu za SMG, risasi 85 za SMG/AK 47 na risasi 28 za bastola.
Mbali na silaha hizo pia walikutwa na Radio “Call” mbili aina ya Kenwood zilizokuwa hewani na wimbi la Polisi Arusha, bullet proof moja, vifaa vya kusafishia bunduki, mifuko mitatu ya kubebea pesa na vifaa vingine.

Majambazi hao ambao kwa sasa miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Mount Meru walikutwa pia na vitambulisho mbalimbali vya Jamhuri ya Kenya pamoja na simu tano aina ya Nokia, Tecno na Samsung. Kamanda Sabas alisema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine waliofanikiwa kukimbia na kubaini mtandao mzima wa kundi hilo.

Kamanda Sabas alimalizia kwa kuwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushirikiana na Jeshi hilo juu ya utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuonya yoyote ambaye atajiingiza katika matukio ya kufanya uhalifu Jeshi hilo litamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Pichani chini Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) akiwaonyesha waandishi wa habari silaha zilizokutwa toka kwa majambazi hao pamoja bullet proof huku picha ya mwisho waandishi wakishuhudia gari lililokuwa linatumiwa na majambazi hao. 
 • Picha na taarifa kutoa kwa Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha.

Afungiwa kucheza soka miaka 2 kwa kudhalilisha tena kiwanjani

Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.

Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tano katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.

Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.

Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.

Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.

Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.

Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=

Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)

Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).

Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.

Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. 

Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said

Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.

Taarifa ya Magereza kukanusha uvumi wa tangazo la ajira

Jeshi la Magereza nchini limetoa taarifa ifuatayo, kukanusha taarifa za tangazo la ajira katika Jeshi hilo ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na Uongozi wa Jeshi kwa ujumla.

Magereza Statement

Statement by TANAPA re: Deaths of wildebeest in Mara River 2015

Below is an update from TANAPA in regards to the news alert: Kwa nini nyumbu wote hawa wamekufa? Hundreds of wildebeest found dead in Tanzania

Below is an update from TANAPA in regards to the news alert: Hundreds of wildebeest found dead in Tanzania

Takwimu za uchawi Tanzania zilitolewa 2010, sasa ndiyo zinakuwa gumzo

Hizi takwimu zilizungumziwa mwaka 2012 (na CNN) lakini kabla, zilichapishwa mwaka 2010 (na BBC), kutokana na utafiti wa Pew na Gallup, leo ndiyo inakuwa gumzo, narudia kwa marejeo:

Here are 10 things that were learnt from the study, which surveyed 25,000 people in 19 countries.


1. 75% of South Africans think polygamy is "morally wrong" - bad news for their president, as Jacob Zuma took his third wife earlier this year and is engaged to a fourth. However, the survey also revealed some possible double-standards. While only 7% of Rwandans approved of polygamy (although this did include women), a rather higher number - 17% - of men said they had more than one wife.

2. An overwhelming majority of respondents disapproved of homosexual behaviour. In three countries - Zambia, Kenya and Cameroon - this was a massive 98%. Interestingly, one of the countries with the highest numbers of people - 11% - accepting homosexuals is Uganda, where an MP is trying to get legislation passed which would punish homosexual acts with life in prison and even death in some cases. The former Portuguese colonies of Guinea-Bissau and Mozambique were also relatively tolerant of homosexuality.

3. Africa is probably the world's most religious continent, with more than 80% saying they believed in God in most countries. At least half of the Christians questioned expect Jesus Christ to return to earth during their lifetimes. In Ethiopia, 74% of Christians say they have experienced or witnessed the devil or evil spirits being driven out of a person and in Ghana, 40% of Christians say they have had a direct revelation from God. About half of all Muslims expect to see the reunification of the Islamic world under a single ruler, or caliph, in their lifetimes.

4. Zimbabwe, where the Lemba people say they are the lost tribe of Israel, was not one of the countries surveyed. But 26% of Nigerian Christians said they traced their origins back to Israel or Palestine.5. Belief in witchcraft is also common - about 40%; a similar percentage also visit traditional healers to cure sickness. Belief in witchcraft is highest in Tanzania with 93% - this is the country where witchdoctors say that magic potions are more effective if they contain body parts of people with albinism. Ethiopia had the lowest levels of belief in witchcraft - at just 17%. Belief that juju or sacred objects can prevent bad things happening was generally lower - between 20 and 30%. In Senegal, however, 75% thought such things worked - far higher than in Tanzania (49%). It may come as a surprise to learn that South Africa had the highest number of people - 52% - saying they took part in ceremonies of traditional religions, or honoured or celebrated their ancestors.

6. Predictably, there was also a religious split concerning alcohol, banned by Islam. Surprisingly, however, more Muslims in Chad (23%) approved of booze, than Ethiopian Christians (5%).

7. Attitudes to divorce showed a strong divide along religious lines in Nigeria. A massive 79% of Christians thought it was "morally wrong", while among Muslims, a narrow majority (46-41%) accepted divorce.

8. In recent years, Islamist hardliners in Somalia and Nigeria have introduced strict punishment based on Sharia law, such as amputating the hands of thieves and even stoning to death for adultery. The majority of people disapproved of such Sharia punishments. In Nigeria, they were backed by about 40% of Muslims and less than 10% of Christians. However, a majority did approve of whippings and amputations in Senegal and Mali. In nearby Guinea-Bissau, even 50% of Christians backed them. This was double the rate among Muslims in Ethiopia (25%) - maybe it feels like a more realistic prospect to them, as they share a border with Somalia and most Muslim Ethiopians are ethnic Somalis.

9. The survey also asked about material well-being in the world's poorest continent. Not so long ago, Cameroon regularly topped surveys of champagne consumption per head. However, a shocking 71% of Cameroonians surveyed said there were times in the past year when they did not have enough money to buy food. In Ethiopia, which is commonly seen as a country struggling to feed itself, the rate was far lower - at 30% - the lowest of all countries surveyed.

10. Ethiopia did, however, have the lowest numbers of people - 7% - who said they regularly used the internet. Rwanda's President Paul Kagame is striving to turn his country into Africa's answer to Silicon Valley and is being helped by the arrival of several new fibre optic cables off the east coast of Africa. He will be encouraged by the finding that 30% of his countrymen - the highest number - regularly browsed the web. Mobile phones, were far more common - with 81% of respondents in Botswana owning one. Many countries reported more than 50% having phones but here, Rwanda lagged behind at just 35%.


[video] Siasa harusini...Wasimamizi, Waratibu Iringa na Mbeya watakiwa kujiepusha na upendeleo kwa wagombea

Baadhi ya wakurugenzi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.
Baadhi ya wakurugenzi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29, 2015.

Wito umetolewa kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa ya Iringa na Mbeya.

Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo.

Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.

Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.

Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura, kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.


Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Sanif Khalifan akitoa maelezo kwa washiriki wa semina ya mafunzo ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,Wasimamizi wa uchaguzi ,Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na Maafisa wa uchaguzi Halmashari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.
Daniel Kalinga, Afisa Uchaguzi akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku mbili ikihusisha waratibu wa uchaguzi,Maafisa Uchaguzi ,Maafisa wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi Halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa .


Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini - Tume, Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo.---
Kahema Emanuel,
Mbeya
JamiiMoja blog

Mazungumzo kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015 kwenye Jukwaa Langu Septemba 28

Kipindi hiki hukujia kila Jumatatu, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Uchaguzi Mku wa Tanzania 2015.

Hiki ni kipindi kilichosikika Septemba 28, 2015.

Kutoka Tanzania tuliungana na Liberatus Mwang'ombe. Mgombea ubunge jimbo la Mbarali kwa tiketi ya CHADEMA.

Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, na kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani.

Karibu


Taarifa nzima ya habari ChannelTEN Septemba 28, 2015
Yaliyojiri magazetini leo Septemba 29, 2015

Waliochaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya

MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VYA AFYA


1. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi mbalimbali za afya kwa ngazi ya Cheti (Astashahada) na Diploma (Stashahada) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi wa awali umefanyika na waombaji 9306 kati ya 21228 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji.

2. Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 16 Oktoba 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine. Kuweza kuthibitisha bonyeza hapa.

3. Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu nyingine siku ya Jumatatu 19 Oktoba 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo kwani hadi sasa nafasi zipatazo 11566 hazijajazwa.

Imetolewa na:

Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE)
27 Septemba 2015

Two of 100 don't understand you, so what? Be content!

When you find yourself overwriting, embracing redundancy and overwhelming people with fine print, you're probably protecting yourself against the 2%, at the expense of everyone else. (And yes, it might be 10% or even 90%.... that's okay).

When we hold back and dumb down, we are hurting the people who need to hear from us, often in a vain attempt to satisfy a few people who might never choose to actually listen.

It's quite okay to say, "it's not for you."
Seth Godin via blog

Mndeme: Tanzania tuna migodi ya thamani kuliko dhahabu na gesi

Unapoutazama ulimwengu kiuchumi, unagawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni nchi tajiri, nchi za kipato cha kati na nchi za kipato cha chini (high-income, middle-income and low-income countries). Ninapenda kutumia vigezo vya kipato kutofautisha makundi haya kuliko kile cha "nchi maskini na nchi tajiri" kwa kuwa sio kweli kwamba nchi zote zenye kipato cha chini ni maskini na zote zenye kipato cha juu ni tajiri. Utajiri na umaskini wa nchi ni zaidi ya kuzalisha mali zinazohesabika kama mapato. Huu ni msimamo wangu na sio lazima ukubaliane na kanuni na tafsi za wachumi wabobezi au wanasiasa. Nyingi ya nchi zinazoitwa tajiri, zimepata utajiri huo kwa kupora mali kutoka nchi zinazoitwa maskini kwa hila na ujanjaujanja wa aina nyingi wanaoulinda na mifumo na kisheria zinazoitwa za kimataifa. Mara nyingine, wanalazimisha nchi zenye rasilimali zijitungie na kujiwekea sheria mbovu zinazawapa wao uhalali wa kuja kupora huku mukiwatazama na kuwapigia makofi kwa jina la uwekezaji.Tofauti kubwa kati ya nchi za kipato cha juu na zile za kipato cha chini inaweza kutazamwa zaidi katika tofauti ta maendeleo ya kiviwanda na tafiti za sayansi na kiteknolojia (elimu). Nchi tajiri zimepiga hatua kubwa katika tafiti za kisayansi na hivyo kuwa na maendeleo makubwa ya kiteknologia na viwanda na kupelekea kuwa wazalishaji wa bidhaa nyingi, ambazo mwisho wa siku, soko lake kubwa ni nchi zisizo na uwezo huo (za pato dogo). Siyo hivyo tu, bali maendeleo haya ya kisayansi na teknolojia yamewafanya kupiga hatu kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kila aina yenye kuboresha hali za maisha ya watu wao, kujitafutia kipato, pamoja na uhakika na ubora wa huduma za kijamii (afya, elimu, maji, nishati, usafiri, nk).

Wataalam wa kiuchumi wanatushauri kwamba, ili nchi iweze kuendelea, pamoja na mambo mengine ni lazima iweze kuwa na viwanda angalau vidogo na vya kiwango cha kati ambavyo vitaweza kubadilisha malighafi zinazopatikana katika nchi husika kuwa bidhaa zinazotumika. Mfano mzuri ni viwanda vinavyoweza kusindika vyakula na vinywaji vya matunda; kutengeneza mavazi kutokana na pamba; kutengeneza viatu na bidhaa zitokanazo na ngozi, nk. Historia ya uchumi wa dunia hasa ndani ya miaka 30 iliyopita imjenga tofauti kubwa sana kati ya nchi za kipato cha juu na cha chini na kuzifanya nchi za kundi la pili kuwa na wakati mgumu sana wa kuendelea kiviwanda kama njia kuu ya kupiga hatua za maendeleo. Kuna maelezo mengi ya kwa nini hali hii imekuwepo lakini ushahidi ni mkubwa kwamba nchi zilizoendelea kiviwanda na teknologia zimekua sababu kubwa ya kuzifanya nchi maskini kushindwa kupiga hatua. Kuna mifumo mingi ya kifedha, kiuchumi, kibiashara, uwekezaji na kisiasa ambayo imezifanya nchi maskini zisisogee na hivyo kuendelea kuwa wanyonge mbele ya nchi tajiri. Naomba nisiingie ndani sana katika hili maana kuna maelezo mengi, magumu na sababu zingine zinaleta maumivu ya kihisia.Mifumo hii ya uchumi unaondeshwa na kuamuliwa na nchi tajiri ni mgumu sana kuuvunja au kuupindua kwani waliouweka wamejenda misingi mikubwa sana yenye nguvu katika kila nyanja ya maisha. Kwa mfano, nchi zenye nguvu ya kiuchumi, zimeingiza baadhi ya dhana na kuzifanya kuwa vigezo vya kimataifa (international standards) ambazo nchi maskini ikivikeuka zinajikuta katika hali ngumu. Mojawapo ya vigezo hivyo ni msisitizo wa misingi ya kiutawala wa kidemokrasia; zinazoitwa haki za binadamu; mahusiano ya kibiashara; na mengine. Kinachoumiza zaidi ni ukweli kwamba, vigezo hivi vyote vinaungwa na wenye uwezo kwa kuzingatia maslahi yao na kisha nchi maskini zinalazimishwa kuzikumbatia na kuzilinda kisheria bila kujali misingi na tamadunia zao ambazo zinatofautina na anaowaletea taratibu hizo. Mambo haya yameiweka nchi maskini katika wakati mgumu na kujikuta zimejiingiza kwenye mikataba mibaya na mahusiano mabovu ya kibiashara. Haya yamepelekea kuendelea kuua uwezo wao wa kujitegemea na wakati huohuo kushuhudia utajiri na rasimaliza za nchi zao kuchotwa na kuwaacha wakiwa hawana chochote cha kuwanufaisha kwa muda mrefu. Tanzania inahusika sana katika hili na mifano ni mingi ya jinsi tulivyoumizwa na tunavyoendelea kuumizwa na mifumo hii.

Tufanyaje?

Serikali yoyote makini inayoangalia hali ya kiuchumi ya wananchi wake na taifa kwa ujumla na kuwa wakweli bila uyeyushaji wa kisiasa, ni lazima ikubali ukweli kwamba hawawezi kufurukuta kirahisi katika mazingira haya na ni lazima wajiulize swali la pili: tunafanyaje? Je, tuna mbadala?

Ili kutoendelea kuwa wahanga wa mifumo kandamizi ya uchumi wa kidunia inayozinyima nchi maskini kuendelea, ni lazima zirudi kwenye msingi (drawing board) na kuangalia ubunifu mbadala wa kujikwamua kwenye umaskini. Hili ni lazima lifanyike kwa umakini mkubwa sana ili kuona ni maeneo gani kika mazingira yetu twaweza kuyatumia kujikwamua na kubadili hali

za maisha yetu bila kuhitaji msaada wa mtu au nchi nyingine. Sio hivyo tu, bali tuweze kufanya hivyo huku tukiwapa wanyonyaji nafasi ndogo sana ya kutuingilia na tutumie rasilimali zetu tulizonazo ikiwa ni pamoja na wataalamu wetu tuliowandaa sisi wenyewe. Tukiweza hilo, tutakua na uwezo hata wa kujenga mahusiano sahihi na nchi zingine yenye usawa katika aina ya ushirika tunaojenga kuliko huu wa sasa.

Nchi makini zilizopitia mazingira haya ya uonevu wa kiuchumi, zimetumia njia hizi na zinafanikiwa sana. Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na China, India, Korea ya Kusini na Brazili. Kwa mfano, kwa kutambua umuhimu wa ushindani wa kimataifa na kujiandaa vuma kupambana na washindani (maadui!!) wa kiuchumi, China inapeleka raia wake zaidi ya milioni ishirini (20,000,000) kila mwaka kusoma kingereza nje ya nchi yao. Sio hivyo tu, ukienda vyuo vikuu vya nchi za Ulaya zinzosifika kwa elimu bora, utashangaa na wingi wa wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu toka chini za Asia na hasa China. Nimeshuhudia baadhi ya programu za uzamivu (hasa biashara na uhandisi) kwenye baadhi ya vyuo, vikiwa havina hata mwanafunzi mmoja wa nchi husika na badala yake ina mamia ya wanafunzi toka China. Vijana hawa wanapomaliza, hawatafuti kuzamia kubaki ulaya, bali wanarudi kwenye nchi zao kupeleka ujuzi huu na kushindana kikamilifu.Nchi ya Korea Kusini ambao uchumi wao unatisha kwa kutegemea viwanda hasa eneo la vifaa vya kielkroniki, kila mwaka linapeleka mami ya vijana kufanya shahada za uzamivu (PhD) katika vyuo bora kabisa duniani Marekani na Ulaya. Vijana hawa wanasomeshwa kwenye vyuo hivi kwa gharama kubwa ya serikali zao kwa lengo la kupeleka ujuzi sahihi wa ushindani kujenga nchi yao.

Nchi ya India, pamoja na maeneo mengi ya uazalishaji yakiongozwa na kilimo cha kisasa, imewekeza katika biashara ya tiba (medical tourism) kwa kuhakikisha imesomesha wataalamu bora; kutengeneza madawa; kujenga hospitali za kisasa; na kutengeneza vifaa bora vya tiba. Ndio maana imekua kimbilio la tiba na inavuna mabilioni ya fedha toka karibu nchi zote za kiafrika kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaopelekwa kupata tiba kila mwaka. Huduma hii sio tu kwamba imeipa India umaarufu na kuongeza kipato cha moja kwa moja, bali imetengeza wingi wa ajira na mapato yatokanayo na huduma zingine zitakazohitajika na watu wanaofuata tiba. Nchi zingine zinazoona mbali kama vile Omani na Dubai, zimeanza kuwekeza kwenye eneo hili la tiba pamoja na kwamba wanafanya vizuri sana kwenye maeneo mengi ya uzalishaji. Wamegundua kwamba katika dunia ya kisasa, tiba sio huduma tu bali ni biashara na uwekezaji unaolipa kwa uhakika.Sina haja ya kueleza ni kwa jinsi gani Brazil wametumia mpira wa miguu (football) kama uwekezaji usiohitaji mtaalamu wala msaada toka nje na ni kwa jinsi gani umpira umeitambulisha nchi hii katika uso wa dunia na kuwa ajira ya muhim na njia ya mapato kwa wengi. Mifano ni mingi ya jinsi nchi zinazoibukia zinafanya hivyo kwa ubunifu unaokwepa utegemezi wa nchi tajiri na kutumia ubunifu wao. Hata hivyo ngoja nijirudi kwa ninachotaka kusema kuhusu nchi yangu pendwa ya Tanzania.

Tuanzie wapi?

Serikali yetu kwa muda mrefu sasa imekua na mipango na mikakati mingi ya kujikwamua kwenye umaskini na kuijengea nchi uwezo wa kujitegemea. Mipango na mikakati hii ni mizuri tu na inaonesha nia njema kabisa ndani ya mioyo na mawazo ya waliyoiandaa. Hata hivyo tukubali kwamba mingi ya mikakati hii haijaleta matokeo tarajiwa. Kuna ambayo imekufa kabla ya utekelezaji wake; kuna ambayo imekua ni mifuko iliyotoboka ya kupoteza mabilioni ya fedha; kuna ambayo inasonga kwa kujikangoja; na kuna michache inaleta mafanikio yanayotia moyo. Nisingependa kuwa msemaji wa serikali katika makala hii kuelezea ni miradi na mikakati ipi imefanikiwa au imesindwa kuleta mafaniko. Sina ujasiri wa kufanya hivyo kwa sasa hasa ukizingatia ni kipindi cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu.

Pamoja na mikakati iliyoko, ambayo mingi inaendeshwa na nchi tajiri kwa namna mbalimbali (inategemea ufadhili wao; tau tunaiga wanachofanya wao; au unategemea ushauri na utaalamu wao; au wanatulazimisha kuitekeleza kwa malengo yao); ninaamini kuna vitu hatujavitazama kama rasilimali na kama tumefanya hivyo hatujavuka toka kwenye mtazamo kwenda kwenye vitendo. Katika makala hii, nataka nizungumzie maeneo matatu au manne ambayo ninashawishika tuna uwezo mkubwa sana wa kuyafanyia kazi, kuyaendeleza na kuyatumia kuboresha hali ya maishayetu. Makuzi na uzoefu niliopitia umenifundisha kutodharau mambo madogo na kutotamani mambo makubwa wakati madogo yamenishinda au sijafanikiwa kuyatekeleza. Kwa minajili hiyo, naamini katika dhana ya kukua, kuendelea na kufanikiwa hatua kwa hatua ili kuwa na maendeleo endelevu kwa mtu binafsi, jumuiya ya watu, na taifa pia. Historia ya watu na nchi nyingi zilizofanikiwa zinaonesha na kulithibitisha hilo. Siamini sana katika mafanikio ya kushtukiza, kusaidiwa, kuoteshwa, au ya miujiza isiyo na maelezo maana yana madhara yake. Hivyo ninataka nizungumzie maeneo matatu ambayo kwa udogo wake yanaweza kubadili mwelekeo wa baadhi ya mambo na kuleta maendeleo ya kichumi ya mtu mmoja mmoja na taifa, na kulijengea taifa letu sifa za kipekee kama zile tunazozifuata kwenye nchi nyingine.

Maeneo hayo sio mageni na nitakua muongo nikisema naleta uvumbuzi au ugunduzi mpya. Ninachotaka kufanya ni kuyaelezea katika mtazamo unaweza kumfanya angalau mtu mmoja kuyatazama kiuchumi/uzalishaji-mali, badala ya kuyatazama tu kwa mazoea kama huduma za kijamii. Sababu ya kufanya hivyo unajengwa katika msingi wa kwamba nchi yetu iko katika mazingira yenye fursa za kipekee (strategic position and opportunities) ukilinganisha na nchi nyingi zinazotuzunguka. Hivyo, tunaweza kutumia fursa hizo kujijenga sisi wenyewe na kuwafanya wengine watuone kama kimbilio lao kwenye baadhi ya mambo hivyo kutuletea mapato kwa watachokifuata kwetu.

Endelea kunisoma kwenye makala itakayofuata.

---
Mwalimu MM ni mhadhiri katika kitengo cha Sayansi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mtafiti wa mifumo ya TEHAMA katika Huduma za afya (Health Informatics). Unaweza kuwasiliana naye kupitia [email protected]

Tanzania Oil and Gas Almanac launches today

(image via WhatsApp)
On Tuesday 29th September 2015 FES Tanzania will launch the Tanzania Oil and Gas Almanac and present other tools aimed at promoting transparency in Tanzania's oil and gas sector.

We therefore invite senior government officials, policy makers, members of parliament, representatives of civil society and international organisations as well as journalists to a guided tour around the Tools for Transparency and Information Platforms with presentations from FESTanzania, OpenOil and the Natural Resource Governance Institute.

Please email [email protected] if you are interested in attending this event.
News/Event cross-posted from: fes-tanzania.org

Kwa nini nyumbu wote hawa wamekufa? Hundreds of wildebeest found dead in Tanzania

Update: >>  Statement by Tanzania National Parks on the death of wildebeest

Cross-posting this tragic news from africageographic.com

Hundreds of lifeless wildebeest were spotted this morning in the Mara River in northern Serengeti, Tanzania. The sad sight was captured on phone cameras by safari guides.
The images below can only be described as tear-jerking. The pile of carcasses stretches into the distance and scavenger birds have already started circling the wildebeest.
According to our source on the ground, the authorities have been contacted and the exact cause of death has yet to be confirmed. If the past is anything to go by, the wildebeest chose a crossing point that was too deep.
As an African travel operator with a love for our continent and wildlife inhabitants, the incident saddens us deeply and is a reminder of what happened in 2007 when 10,000 wildebeest died in a mass drowning.

I couldn't resist posting this video: Life lessons from people of all ages


Manifesto ya CUF kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015


Jipakulie nakala (pdf) kwa kubofya hapa.


[video] Magufuli aona isiwe taabu, ashuka garini kupitia dirishani


Kiwewe cha watu! Lowassa ashindwa kuhutubia Tangamano, mjini Tanga


Mgombea wa nafasi ya urais kupitia CHADEMA anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda UKAWA, Edwrad Lowassa amelazimika kuahirisha mkutano katika kiwanja cha Tangamano, mjini Tanga baada ya watu wengi kujitokeza na kusababisha msongamano ambao ulihatarisha maisha yao.

Taarifa zinasema kuwa kwa mara ya kwanza shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5, 6, 7, 8 zililazimika kusimama kwa muda kutokana na hali hiyo.

Juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo hazikuzaa matunda.


Kauli ya Wizara kuhusu Mahujaji kutoka TanzaniaTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Ubalozi wake mjini Riyadh, Saudi Arabia imepokea taarifa kuwa hadi kufikia tarehe 27 Septemba, 2015 watu waliopoteza maisha kufuatia tukio la mkanyagano (stampede) wa Mahujaji waliokuwa wakielekea Jamarat kutupa vijiwe huko Mina nje kidogo ya mji wa Makkah, lililotokea siku ya Alhamisi tarehe 24 Septemba, 2015 wameongezeka na kufikia 769 na majeruhi 934.

Aidha, Wizara kupitia Ubalozi huo inaendelea kufuatilia hatma ya Mahujaji wa Tanzania waliopotea katika tukio hilo la ajali ambapo hadi sasa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana. Vikundi wanavyotoka Mahujaji hao na idadi yao ni kama ifuatavyo:-
 1. Ahlu Daawa-Mahujaji 30;
 2. Khidma Islamiya-Mahujaji 16; na
 3. TCDO-Mahujaji 4
Vile vile juhudi za Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na viongozi wa vikundi vilivyopoteza Mahujaji wao zimefanikiwa kuutambua mwili wa hujaji mmoja aliyefariki dunia anayejulikana kwa jina la Shafi Khamis Ali kutoka kikundi cha Ahlu Daawa. Kutambuliwa kwa mwili wa hujaji huyo kunafanya idadi ya Mahujaji wa Tanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo kufikia watano (5).

Pia, Wizara kupitia Ubalozi wake imepokea taarifa ya kupatikana kwa hujaji mwingine anayeitwa Nasra Abdullah akiwa hai naye kutoka kikundi hicho cha Ahlu Daawa.

Kuhusu majeruhi, taarifa kutoka Ubalozini zinaeleza kuwa, hujaji mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahjabin Taslim Khan alipata majeraha yaliyopelekea kukatwa mguu na kwa sasa anaendelea kupata matibabu huku hali yake ikiendelea vizuri.

Ubalozi unaendelea na juhudi za kuwatafuta Mahujaji wengine wa Tanzania ambao bado hawajaonekana kwa ajili ya kubaini wale waliofariki au majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu.

Mahujaji wengine wa Tanzania wapo salama ambapo tarehe 26 Septemba, 2015 walimaliza ibada ya hija na tarehe 28 Septemba, 2015 wameanza safari ya kurejea nyumbani.

Wizara inaendelea kuwaomba Wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

28 Septemba, 2015