Tofauti ya GPA na GPT; Hatua zinazotumika kupata GPA; Mapendekezo


TANGU serikali ya awamu ya tano iingie madarakani kuna maamuzi kadhaa yamefanywa na kuibua mijadala miongoni mwa jamii, mojawapo ni uamuzi uliofanywa na Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako.

Prof. Ndalichako alibatilisha matumizi ya mfumo wa kupanga madaraja ya ufaulu shuleni kwa kuzingatia wastani wa pointi za daraja ya ufaulu, ambayo kwa Kiingereza ni “Grade Point Average” (GPA).

Badala yake, Ndalichako aliielekeza Wizara kufufua mfumo uliokuwepo hapo awali ili uendelee kutumika shuleni. Mfumo wa awali ulikuwa unapanga madaraja ya ufaulu kwa kuzingatia jumla ya pointi za gredi ya ufaulu, ambayo kwa Kiingereza ni “Grade Point Total” (GPT).

Bila kujali kama umetumika mfumo wa GPT au GPA, bado madaraja ya ufaulu yatatengenezwa, lakini yakiwa na majina tofauti.

Kwa mfano, kwenye mfumo wa GPT wa Tanzania, tunasema Daraja la Kwanza (Division One), Daraja la Pili, Daraja la Tatu, Daraja la Nne, na Daraja Sufuri.

Kwenye mfumo wa GPA, tunasema Daraja la ‘Distinction’ (la tofauti), Daraja la ‘Merit’ (Sifa), Daraja la ‘Credit’ (Stahili), Daraja la ‘Pass’ (Faulu), na Daraja la ‘Fail’ (Kufeli).

Kwa hiyo, sio sahihi kwa mtu kusema, “Dk. Kawambwa alifuta divisheni na Prof. Ndalichako amezirudisha,” kama ambavyo vyombo vingi vya habari vimekuwa vikiripoti. Ukweli ni kwamba, divisheni ziko pale pale siku zote, ila kinachobadilika ni namna ya kuzikokotoa na kuzitamka.

Kuhusu namna ya kuzikokotoa, divisheni za GPT zinapatikana kwa kutafuta jumla ya alama alizopata mwanafunzi, wakati divisheni za GPA zinapatikana kwa kutafuta wastani wa alama alizopata mwanafunzi.

Makala haya ni kwa ajili kuweka bayana mchakato huu wa kutafuta madaraja ya ufaulu shuleni.

Hatua 12 katika mchakato wa kutafuta GPA


Kama walimu wote wanavyofahamu, mchakato wa kutathmini maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi (academic assessment process) unazo hatua kumi na mbili, kama zinavyojadiliwa katika aya zifuatazo.

Katika hatua ya kwanza, mwanafunzi hufundishwa, kwa kutumia mtaala rasmi. Pili, mwanafunzi hutungiwa mtihani kwa ajili ya kupima uelewa wake.

Tatu, mwanafunzi hujibu mtihani kwa kujibu maswali yaliyoandaliwa na mwalimu wake, na chini ya usimamizi wa mwalimu.

Nne, mwalimu husahihisha majibu ya mtihani kama yalivyoandikwa na mtahiniwa. Hatimaye mwanafunzi hutunukiwa alama za ufaulu kwa mujibu wa skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa asilimia. Katika skeli hii, mwanafunzi anaweza kupata alama kati ya sufuri na mia moja.

Katika hatua ya tano, idadi ya herufi za ufaulu zitakazotumika katika kurekodi ufaulu katika mtindo wa herufi huamuliwa. Herufi hizi kwa pamoja kutengeneza skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi.

Kuhusu idadi ya herufi zinazopaswa kuwemo katika skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi, tunaweza kuwa na skeli yenye herufi mbili [mfano P(Pass), F(Fail)]; skeli yenye herufi tano [mfano A, B, C, D, na F]; skeli yenye herufi sita [mfano A, B, C, D, E na F]; skeli yenye herufi saba [mfano A, B+, B, C, D, E, na F]; na kuendelea. Kwa hapa Tanzania, uamuzi kuhusu idadi ya herufi zinazopaswa kutumika, hufanywa, sio na mwalimu, bali na serikali.

Kwa sasa, idadi ya herufi zilizo katika skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi inayotumika katika vyuo vingi vya elimu ya juu ni saba [A, B+, B, C, D, E, na F].

Skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi inayotumika katika elimu ya sekondari, kati ya kidato cha tano mpaka kidato cha sita, inazo herufi sita [A, B, C, D, E, na F] na skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi inayotumika katika elimu ya sekondari, kati ya kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne, inazo herufi tano [A, B, C, D, na F].

Katika hatua ya sita, skeli ya ufauli ulio katika mtindo wa asilimia (percentage scale) huoanishwa na skeli ya ufaulu ulio katika mtindo wa herufi (letter scale).

Kwa mfano, mchakato wa kuoanisha skeli hizi mbili unaweza kuwa kama ifuatavyo:

Gredi A sawa na ufaulu wowote ulio kati ya 100% na 81%; gredi B sawa na ufaulu wowote ulio kati ya 80% na 61%; gredi C sawa na ufaulu wowote ulio kati ya 60% na 41%; gredi D sawa na ufaulu wowote ulio kati ya 40% na 21%, na gredi F sawa na ufaulu wowote ulio kati ya 20% na 0%.

Nchini Tanzania, uamuzi kuhusu mipaka ya madaraja ya ufaulu kwa kuzingatia herufi yaliyopo kati ya asilimia sufuri mpaka asilimia mia moja, hufanywa, sio na mwalimu, bali na NECTA.

Pia, mipaka ya madaraja ya ufaulu kwa kuzingatia herufi yaliyopo kati ya asilimia sufuri mpaka asilimia mia moja, inatofautiana katika ngazi tofauti za elimu hapa nchini. Kidato cha kwanza mpaka cha nne wanayo mipaka yao; kidato cha tano mpaka cha sita wanayo mipaka yao; na vyuo vya elimu ya juu vinayo mipaka yake kwa kila daraja la kiherufi.

Katika hatua ya saba, kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi hubadilishwa kutoka kwenye gredi ya ufaulu iliyo katika mtindo wa asilimia (percentage score) kwenda katika gredi ya ufaulu iliyo katika mtindo wa herufi (letter score). Kazi hii hufanyika kwa kuzingatia skeli ya ufaulu ulio katika mtindo wa herufi (letter scale) kama ilivyojadiliwa hapo juu.

Nane, uamuzi hufanyika kuhusu utaratibu wa kubadilisha gredi ya ufaulu iliyo katika mtindo wa herufi (letter score) kwenda kwenye gredi ya ufaulu iliyo katika mtindo wa pointi (point score).

Kwa ajili hii, hutengenezwa skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi. Zipo njia mbili za kutengeneza skeli hii. Ama kwa kuhakikisha kwamba skeli hii inaanza na namba kubwa na kuishia na namba ndogo, au kinyume chake.

Katika skeli ya pointi inayoanza na namba kubwa kwenda namba ndogo kazi ya kuoanisha herufi na pointi huweza kufanyika kama ifuatavyo: Gredi A sawa na pointi 4; gredi B sawa na pointi 3; gredi C sawa na pointi 2; gredi D sawa na pointi 1, na gredi F sawa na pointi 0.

Na katika skeli ya pointi inayoanza na namba ndogo kwenda namba kubwa kazi ya kuoanisha herufi na pointi huweza kufanyika kama ifuatavyo: Gredi A sawa na pointi 1; gredi B sawa na pointi 2; gredi C sawa na pointi 3; gredi D sawa na pointi 4, na gredi F sawa na pointi 5.

Hapa nchini, uamuzi kuhusu skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi inayopaswa kutumika, hufanywa, sio na mwalimu, bali na serikali.

Kwa sasa, skeli za kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi zinatofautiana kutoka ngazi moja ya elimu mpaka ngazi nyingine.

Kwa mfano, shule za sekondari zinatumia skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi inayoanzia pointi 1 mpaka pointi 4 wakati vyuo vya elimu ya juu vinatumia skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi inayoanzia pointi 4 mpaka pointi 1. Hivyo, skeli inayotumika katika ngazi za chini imepinduliwa kichwa chini miguu juu, katika ngazi za juu za elimu.

Tisa, gredi ya ufaulu iliyo katika mtindo wa herufi (letter score) hubadilishwa na kuwa gredi ya ufaulu iliyo katika mtindo wa pointi za ufaulu (point score).

Kumi, jumla ya pointi za ufaulu wa mwanafunzi hutafutwa kwa kujumlisha pointi alizopata mwanafunzi kwa kila somo alilofanyia mtihani. Idadi hii huitwa Jumla ya Pointi za Gredi, ambayo kwa Kiingereza inaitwa “Grade Point Total” (GPT).

Kumi na moja, wastani wa pointi za ufaulu wa mwanafunzi hutafutwa kwa kugawanya GPT dhidi ya idadi ya masomo yaliyofanyiwa mitihani na mtahiniwa. Wastani huu huitwa Wastani wa Pointi za Gredi, ambayo kwa Kiingereza inaitwa “Grade Point Average” (GPA).

Na kumi na mbili, divisheni ya ufaulu ya mwanafunzi hukokotolewa ama kwa kutumia mfumo wa GPT au mfumo wa GPA kulingana na miongozo iliyopo kwa mujibu wa sera za serikali au sera za taasisi nyingine husika.

Hitimisho na mapendekezo

Kutokana na yaliyojadiliwa hapo juu, mambo kadhaa yanafuata kimantiki. Kwanza, kuna skeli tatu tofauti zinazotumika katika kukokotoa kiwango cha ufaulu wa mtahiniwa. Yaani, skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa asilimia, skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi, na skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi.

Pili, taasisi za kielimu zinatofautiana kuhusu idadi ya herufi zilizo katika skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi. Kwa mfano, idadi ya herufi zilizo katika skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi inayotumika katika vyuo vingi vya elimu ya juu ni saba [A, B+, B, C, D, E, na F].

Skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi inayotumika katika elimu ya sekondari, kati ya kidato cha tano mpaka kidato cha sita, inazo herufi sita [A, B, C, D, E, na F].

Na skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa herufi inayotumika katika elimu ya sekondari, kati ya kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne, inazo herufi tano [A, B, C, D, na F]. Kunakosekana ulinganifu (uniformity) hapa.

Tatu, mipaka ya madaraja ya ufaulu kwa kuzingatia herufi yaliyopo kati ya asilimia sufuri mpaka asilimia mia moja, inatofautiana katika ngazi tofauti za elimu hapa nchini. Kidato cha kwanza mpaka cha nne wanayo mipaka yao; kidato cha tano mpaka cha sita wanayo mipaka yao; na vyuo vya elimu ya juu vinayo mipaka yake kwa kila daraja la kiherufi. Kunakosekana ulinganifu (uniformity) hapa pia.

Nne, skeli za kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi zinatofautiana kutoka ngazi moja ya elimu mpaka ngazi nyingine. Kwa mfano, shule za sekondari zinatumia skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi inayoanzia pointi 1 mpaka pointi 4 na vyuo vya elimu ya juu vinatumia skeli ya kutunuku ufaulu kwa mtindo wa pointi inayoanzia pointi 4 mpaka pointi 1.

Hivyo, skeli inayotumika katika ngazi za chini imepinduliwa kichwa chini miguu juu, katika ngazi za juu za elimu. Kunakosekana ulinganifu (uniformity) hapa pia.

Tano, kuna njia mbili za kukokotoa divisheni ya ufaulu ya mtahiniwa. Yaani, mfumo wa GPA na mfumo wa GPA. Lakini, mfumo wa GPT ukitumika mahali, basi mfumo wa GPA hautatumika, na kinyume chake ni kweli.

Sita, kuna utofauti, kati ya mifumo hii ya GPT na GPA. Kwa mfano, mfumo wa GPT unazo hatua chache zaidi kuliko mfumo wa GPA.

Saba, mfumo wa GPT ni sehemu ya mfumo wa GPA. Yaani, haiwezekani kukokotoa GPA kabla ya kukokotoa GPT. Kwa maneno mengine, mfumo wa GPT unazo hatua chache zaidi kuliko mfumo wa GPA.

Na nane, kwa kuwa akili ya mwanadamu inaelewa haraka namna ya kutafuta “jumla” kuliko namna ya kutafuta “wastani,” inafuata kimantiki kwamba, mfumo wa GPT ni rahisi kueleweka kwa wadau wa elimu kuliko mfumo wa GPA.

Kwahiyo, tatizo lililo mbele yetu sio ama GPT au GPA. Ni tatizo kubwa zaidi kama tukizingatia utata uliomo katika mchakato mzima wa kutathmini maendeleo ya mwanafunzi.

Kuna haja ya kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu sera yetu inayoongoza mambo haya, ambao utazalisha mwafaka wa kitaifa katika sekta ya elimu. Lakini pia, mjadala wa aina hiyo utazalisha maarifa sahihi ndani ya jamii kuhusu namna wanafunzi wetu wanavyopimwa kitaaluma.
 • Imeandikwa na Deusdedit Jovin

NW, Dk Kigwangalla aagiza kufungwa chumba cha upasuaji hospitali ya Sanitas


Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.

Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.

Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:

Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO), Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv)


Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati walipowasilia katika ziara hiyo.
Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.

Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral

Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.

Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..

Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya maabara ya hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi


Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. 
 • Imeandaliwa na Andrew Chale, MODewji blog/MO tv

Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 29, 2016
Halima Mdee akosa dhamana


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za shambulio, mbunge huyo alikosa dhamana na anashikiliwa na Jeshi la Polisi. (Picha na Francis Dande)

Halima Mdee (katikati) akiwa na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (wa pili kushoto) pamoja na wafuasi wa Chadema wakati akielekea mahabusu.


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akisindikizwa na Ofisa wa Polisi aliyeshika faili kuelekea mahabusu baada ya kukosa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo.

Mwanasheria wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Prof. Abdallah Safari akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya mbunge huyo kukosa dhamana.

Tangazo la kupotea Said Abdallah Ismail: Ombi la maalbino kwa Bunge na Serikali


Taarifa ya EWURA kwa umma kuhusu ombi la TANESCO kurekebisha bei


TAARIFA KWA UMMA: MAOMBI YA TANESCO YA KUREKEBISHA BEI ZA UMEME- WITO WA KUKUSANYA MAONI YA WADAU

FEBRUARY 26, 2016

Mnano tarehe 24 Februari 2016, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ilipokea ombi toka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kutaka mabadiliko ya bei ya umeme kwa miaka miwili kuanzia tarehe 1 Aprili 2016.

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19(2) (b) cha Sheria ya EWURA, Sura Na. 414, Mamlaka inaanzisha mchakato wa kupata maoni ya wadau ili kujua uhalali wa maombi ya nyongeza ya bei za huduma iliyoyapokea kutoka TANESCO.

Kwa taarifa zaidi, soma nyaraka zifuatazo;
Chanzo cha taarifa ni tovuti ya EWURA

Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam - Yaliyojiri katika "Mada Moto" ya ChannelTENLalamiko la Bi Tatu lasababisha WM Majaliwa aagize Daktari mtuhumiwa asimamishwe kazi

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.
 • Ni baada ya kudai rushwa ya sh. 100,000/- kumfanyia upasuaji mgonjwa
 • Mama alilazimika kuuza shamba ili apate fedha za kumtibia baba yake
 • Aagiza maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo yafungwe leo hii
 • Amwagiza RAS aitishe kikao cha watumishi wote leo saa 9 alasiri


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-.

Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo kuanzia leo na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Alfred Luanda asimamie zoezi hilo mara moja.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Februari 29, 2016) kwenye kikao cha watumishi wa hospitali hiyo alichokiitisha baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu wenye wagonjwa waliolazwa.

Mara baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa nini wana dirisha moja la kupokelea wagonjwa wote. "Dirisha la wazee lipo?" akajibiwa hakuna. "Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo" nalo pia akajibiwa halipo. "Je wazee wana daktari wao", hakupata jibu. 

"Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee na uhakikishe wana daktari wao. Siyo kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana," alisema wakati akimwagiza Mgaga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Shaibu Maarifa. 

Akiwa njiani kuelekea wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa waliokuwa wakiimba "tuna jambo, tuna jambo" wakiashiria kutaka kusikilizwa. Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuu alipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei za juu kwenye maduka ya dawa binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.

Lakini kero ya Bi. Tatu Abdallah aliyelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5 ili apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula ndiyo ilimgusa zaidi Waziri Mkuu.

"Februari Mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za sh. 85,000/- hapo nje (pharmacy haikumbuki jina) pia uzi wa kushonea kwa sh. 25,000/-. Lakini pia daktari akasema anataka sh. 100,000/- ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji."

"Tarehe 12 Februari baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000/- na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani".

"Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?" 

Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza. 

Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.

Akiwa njiani kuelekea theatre, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi umefanyika leo waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo. 

Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika.

"Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu Daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho," alisema. 

Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu amemwagiza RAS, RMO na Afisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi wote wa hospitali hiyo leo saa 9 alasiri na kisha wamletee taarifa.
Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuwa na huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu. 

Aliwataka waache tabia ya kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake wanaojifungua kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya Serikali.

Sakata la hospitali ya Ligula lilianza juzi (Jumamosi, Februari 27, 2016) wakati Waziri Mkuu akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa ambapo baadhi yao walikuwa wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya kutumbua. 

Waziri Mkuu aliwajibu kuwa amesikia ujumbe wao na ataenda huko lakini alishindwa kutokana na ratiba za siku hiyo kumalizika jioni sana. 
 
Waziri Mkuu amerejea Jijini Dar es Salaam mchana huu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMATATU, FEBRUARI 29, 2016.Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea Dar es slaam Februari 29, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam Februari 29, 2016.

NW aagiza Shine Care Pharmacy kufungwa

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akitoka katika duka hilo la dawa baada ya kuagiza kulifunga


NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.

Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.

Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n ahata kumsababishia matatizo.

Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.

Mmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo kinyume na sheria.
Baadhi ya maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Afya. Dk Kigwangalla wakimsikiliza kwa makini, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akiongea kwa njia ya simu na mmiliki wa duka hilo la Shine Pharmacy , Abraham Mathayo...ambaye alieleza kuwa yupo Mkuranga, hivyo waliamua kuongea naye kwa njia ya simu kwa nini anaendesha duka bila ya kutokuwa na vibali.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Henri Irunde, akitoa taarifa yake ya ukaguzi katika duka hilo kwa wanahabari na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo ya kufungwa kwa duka hilo.
 • Imeandaliwa na Andrew Chale.

Tangazo la msiba wa Dk Kisamo

Dk Kisamo
Mrs Elipina Kisamo Mlaki na Linda Kisamo wanasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Dr Michael Kisamo aliyefariki Jumapili 28/2/2016.

Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwake Kinondoni Mkwajuni/Sokoni Magengeni. na Mazishi yanataraji kufanyika Usangi Jumatano 2.03.2016.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe

Ahsante kwa Ushirikiano.

Taarifa ya Bodi ya Utalii: Olduvai Gorge iko Tanzania


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

OLDUVAI GORGE IKO TANZANIA SI KENYA


BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTube
https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.

Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.

Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana. Tunapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.

Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani ya nchi au ya Kimataifa. Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii peke yake.

Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.

Imetolewa na:

Ofisi ya Uhusiano

BODI YA UTALII TANZANIA

No. I refuse!


Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 28, 2016


Taarifa ya Mkuu wa Wilaya, Makonda ya kuanza kwa walimu kusafiri bure katika 'daladala'

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu mpango aliouanzisha wa walimu kutotoa nauli kwenye daladala wakati wa kwenda na kurudi nyumbani wanapotoka kazini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DACOBOA), Sabri Mabrouk.

Taarifa kwa Umma kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda


Moja ya jambo ambalo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa John Pombe Magufuri imelifanya kuwa kipaumbele kikubwa kwenye mipango yake ya kimaendeleo ni suala la uboreshaji wa sekta ya elimu nchini na ndio maana serikali imeanza utekelezaji wa mpango huu kwa kufuta ada zote mashuleni.

Kimsingi ni ndoto hii ya Mheshimiwa Raisi ambayo nina hakika kila mmoja wetu anaelewa ukubwa wa faida zake kwenye ujenzi wa Tanzania mpya na yenye wasomi na wataalamu wa kila namna tena wanaopatikana bila kuzingatia hali ya kipato cha familia anayotokea mwanafunzi, iliyonifanya mimi kama msaidizi wake katika nafasi ya ukuu wa wilaya nijiulize kila wakati juu ya ushiriki wangu wa kuhakikisha inatimia kikamilifu.

Maswali ambayo yamenifikisha kwenye wazo la kuboresha sekta hii kwa kuchagua kufanya jambo ambalo wakati serikali ikiendelea kupigania changamoto nyinginezo za kuboresha ajira za walimu ikiwemo upandishwaji wa madaraja na mishahara, basi na mimi katika nafasi yangu nishiriki kwenye mchakato huu mzima kwa kutoa motisha ya usafiri wa bure kwa walimu wote wanaofundisha kwenye shule za serikali zilizopo jijini Dar es Salaam.

Kwa ufupi ni kwamba, wazo hili limejengwa juu ya msingi wa sababu kubwa tatu.

Moja, kwa kuzingatia changamoto za nauli za mara kwa mara wanazolazimika kuzilipa walimu ili kuyafikia kwa wakati maeneo yao ya kufanyia kazi na pili, ni kuhakikisha mimi na serikali yangu ya wilaya ya Kinondoni tunakuwa sehemu ya juhudi za Mheshimiwa Raisi za kuboresha maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi ili matarajio ya ndoto yake anayoipigania usiku na mchana ya kutaka kuiona sekta ya elimu nchini ikikua kwa kasi yanatimia.

Na tatu, ni kuwafanya walimu wa wilaya ya Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kama watumishi wenzangu wa serikali nao wanafaidi sehemu ya matunda ya serikali yao ambayo kwa dhati imedhamiria kubadilisha maisha yao ili na wao waweze kubadilisha maisha ya vijana wetu kupitia taaluma.

Kwasababu hizo nilizozianisha hapo juu ninaomba kuwatangazia walimu wangu wa shule zote za serikali kuanzia za msingi mpaka sekondari ya kwamba, sasa watasafiri bure wanapokwenda kutufundishia wadogo zetu na watoto wao.

Hii ni baada ya kufanya vikao na mazungumzo ya kina na wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kupitia vyama vyao vya Darcoboa na Uwadar na hatimaye mazungumzo hayo kuitimishwa na mkutano wa vyama vyote hivyo viwili vya wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao kwa sauti moja wamekubali kuniunga mkono kwenye utekelezaji wa wazo langu hili.

Kipekee na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wamiliki hawa wa vyombo vya usafiri wa umma pamoja na viongozi wa vyama vya Darcoboa na Uwadar kwani walikuwa na kila sababu ya kukataa hasa ukizingatia kuwa wao ni wafanyabiashara na tena wanazo changamoto nyingi katika sekta yao ya usafirishaji, wengine wakiwa hata wamekopa kwenye mabenki ili wapate uwezo wa kufanya biashara, lakini kwenye jambo hili wote kwa umoja wao wameseme ndio na wako tayari kuanza haraka iwezekanavyo.

Utaratibu kwa walimu juu ya utumiaji wa fursa ambayo tumeipata utakuwa kama ifuatavyo:- Moja, nimemuelekeza ofisa elimu wa sekondari na shule za msingi, kutoa maelekezo kwa wakuu wa shule zote za serikali zilizopo wilayani kwangu na wilaya nyinginezo za jiji la Dar es Salaam, kutengeneza vitambulisho vya shule zao vitakavyokuwa na picha ya mwalimu, jina lake kamili, jina la shule anayofundisha, namba ya simu ya mkuu wa shule husika pamoja na saini yangu mimi mwenyewe Paul Makonda ili kuepuka udanganyifu.

Nimewataka zoezi hili walifanye na kulikamilisha ndani ya wiki moja ambapo baada tu ya kukamilika itakuwa ni furaha yangu kuwatangazia walimu wote wa shule za serikali jijini Dar es Salaam kuwa, watakuwa wakipanda daladala bure ila tu kwa siku za jumatatu mpaka Ijumaa na kwa muda wa saa kumi na moja asubuhi mpaka saa mbili asubuhi na kati ya saa tisa mpaka saa kumi na mbili jioni. Ingawa, kila mwalimu atalazimika kuonyesha kitambulisho chake alichotengenezewa kwenye shule yake pamoja na kile cha ajira ya serikali


Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DACOBOA), Sabri Mabrouke (kushoto), akizungumzia mpango huo ambao wameuunga mkono. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Shaban Mdemu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (DACOBOA), William Masanja.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (DACOBOA), William Masanja (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Shaban Mdemu (kulia), akizungumza katika mkutano huo.

Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.

Mwonekano wa meza kuu katika mkutano huo.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Huduma za Afya na Elimu Bure katika siku 100 za Rais Magufuli


PAMOJA na serikali ya awamu ya tano kutangaza sera ya elimu bure, Manispaa ya Kinondoni inakabiliwa na changamoto katika kutekeleza sera hiyo, MTANZANIA limebaini.

Uchunguzi uliofanywa kwa wiki kadhaa katika baadhi ya shule za msingi na sekondari kwa nyakati tofauti, umebaini changamoto mbalimbali ikiwamo wanafunzi kukaa chini, uhaba wa walimu wa sayansi, vitabu, vifaa, baadhi ya masomo kufutwa na kupunguza baadhi ya mitihani.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, baadhi ya walimu walisema mfumo huo umeongeza changamoto katika elimu kutokana na fedha hizo kutolewa kila mwezi lakini shule zinashindwa kuzipangia bajeti.

Mwalimu wa Idara ya Fedha wa Shule ya Sekondari Mama Salma Kikwete, Salumu Ummy alisema fedha za elimu bure awamu ya pili zilitolewa Februari 2 mwaka huu ambazo ni Sh 4,475,000 lakini mchanganuo wa fedha hizo bado haujatolewa.

“Kwa awamu zote mbili fedha zimetolewa kwa kiasi tofauti, Januari ilikuwa Sh 4,483,000 na Februari Sh. 4,475,000.

“Fedha zimetolewa kwa kiasi tofauti awamu ya kwanza tulipokea Sh 4,483,000 na mgawanyo wake ulikuwa Sh 2,294,000 fidia ya ada na Sh 2,189,000 ni kwa ajili ya ruzuku,”alisema Ummy.

Ummy alisema mchanganuo wa fedha zilizotolewa Januari ulikuwa asilimia 35 kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi , asilimia 30 taaluma , asilimia 10 dawa za binadamu, asilimia 10 matengenezo na asilimia 15 mitihani .

Hata hivyo, alisema mchanganuo huo kwa shule za sekondari bado haukidhi mahitaji kwa shule ambayo ina wanafunzi 1,265.

Ummy alisema fedha hizo hutolewa na mchanganuo ambao baadhi ya mahitaji huwa hayamo hivyo kushindwa kuyaingiza katika bajeti hiyo.

“Katika mchanganuo huo hakuna fedha za kulipia bili za umeme, maji na huduma ya mlinzi ambako awali wazazi walichangia huduma hizo,” alisema Ummy na kuongeza:

“Changamoto nyingine ni upungufu wa walimu wa sayansi, kwa mfano, kwa sasa tuna mwalimu mmoja wa somo la Hesabu, Kemia wawili, Fizikia mmoja na Baiolojia watatu kwa shule nzima, hivyo vipindi vingi vya masomo hayo havifundishwi”.

Ili kukabiliana na hali hiyo kabla ya kuanzishwa mpango wa elimu bure, alisema walitumia fedha za ada kukodi walimu wa masomo hayo ili kukidhi mahitaji hayo lakini kwa sasa katika mchanganuo wa fedha zinazopelekwa na serikali hakuna fedha zilizopangwa kwa ajili ya kutafuta walimu hao wa ziada.

Serikali pia iliahidi kununua vitabu vya kufundishia na kujifunzia lakini hadi sasa havijapelekwa shuleni hivyo kuzidisha ugumu katika ufundishaji, alisema.

“Kuna uhaba wa samani za shule yakiwamo madawati na kusababisha wanafunzi wengi wa kidato cha kwanza kukaa chini na kuwafanya washindwe kuandika na kujifunza vizuri,” alisema Ummy.

Naye Makamu Mkuu wa Shule wa shule hiyo, Lucy Burreta, alisema shule imeamua kufuta masomo ya mchepuo wa biashara kutokana na kukosa walimu wake.

Alisema katika mchanganuo unaotolewa, fedha kwa ajili ya taaluma ni ndogo na zikigawiwa kwa mwezi kuna baadhi ya vifaa kama chaki, wino, karatasi za mitihani hazifiki mwisho wa mwezi.

Wanafunzi ni wengi kiasi ambacho darasa moja linakuwa na zaidi ya 64 hivyo kumpa wakati mgumu mwalimu anayefundisha, alisema.

Lucy alisema nguvu nyingi za mfumo wa elimu bure zimepelekwa katika shule za msingi na kusahau za sekondari.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Manzese, Linus Mwakasege alisema serikali ilisimamisha shule kununua vitabu tangu mwaka juzi, lakini tangu kuanzishwa kwa utaratibu huo vitabu vimekwisha kutolewa mara moja tu.

“Kuna ongezeko kubwa la wanafunzi kwa kuwa wale walioshindwa kuripoti miaka iliyopita kwa sababu ya kukosa ada wanaomba kuendelea na masomo jambo ambalo linazidi kuongeza idadi,” alisema Mwakasege.

MTANZANIA ilimtafuta Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera kulizungumzia suala hilo.

Alikiri kuwapo kwa changamoto katika suala la elimu akisema zimetokana na sera hiyo kuanzishwa katikati ya mwaka wa fedha hivyo hakukuwa na fedha zilizokuwa zimetengwa katika bajeti.

“Si kwamba changamoto hizo zote zimeletwa na sera ya elimu bure, zilikuwapo tangu michango na ada kwa wanafunzi ilipokuwapo…bado hakukuwa na madarasa ya kutosha, madawati na vitabu,” alisema Mhowera.

Mhowera ambaye alizungumza kwa niaba ya olfisa elimu manispaa hiyo, alisema ili kupunguza adha hiyo, manispaa imepunguza baadhi ya matumizi katika bajeti yake ili kupata fedha kwa ajili ya kusaidia elimu.

“Kisheria mabadiliko ya bajeti yanatakiwa yaidhinishwe na Baraza la Madiwani wa Manispaa yetu. Tulichelewa kuanza kutokana na sababu za siasa hivyo kushindwa kuidhinisha fedha tulizopunguza katika bajeti ya Sh bilioni 1.5 zitakazosaidia kwa miezi minne katika shule,” alisema Mhowera.

Kuhusu upungufu wa walimu wa sayansi, ofisa huyo alisema liko mikononi mwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ambaye ameishauri manispaa kuomba kibali cha kuajiri walimu wa ziada wanaohitajika.

Kuhusu miundombinu ya shule, alisema manispaa ina upungufu wa vyumba vya madarasa 1601 kwa shule za msingi na 466 sekondari ambavyo vinahitajika kabla ya Julai.

“Tuna upungufu wa madawati 18,816, matundu ya vyoo 6,805 na maabara sita,” alisema Mhowera.

Dk Mukhisa Kituyi amtolea mfano Rais Magufuli


Tip: Before introducing someone to colleagues via email, have them write one to you first


If you are going to need to introduce one of your colleagues to another by email, have the person you’re introducing write their own introduction email and send to you first.

Roy Bahat, head of venture capital firm Bloomberg Beta, says that the goal of this email should be to explain why you want to be introduced, who you are, and begin a new conversation. 

Avoid sending an email to a new person that says “You can just dig through this old conversation I had with someone else.”

Why? He says, "...do the things you’re best at – describing who you are, what your organization does, why you want to talk to the receiver, speaking in your own voice, etc. And I do only the things I’m best at – knowing the receiver, and sharing my opinion of you. It also optimizes for me spending as little time as possible, so I can make your introduction as quickly as possible.

5 tips for a good forward intro email:
 1. Says why you want to be introduced
 2. Includes its own context
 3. Uses only as many words as you need – the receiver is going to glance at the email, and decide whether to talk to you. A recap of other things we talked about when we met distracts.
 4. Sounds like you
 5. Starts a fresh chain, with a fitting subject line, for each introduction – if you write a forward intro email as a reply to a long string between us (including, for example, us talking about whether it makes sense for you to speak to the receiver) that costs me time. I’m editing all that out, re-titling the email, etc. – delaying your intro. Subject lines like “Forward intro email for Karin” also cost me time to fix.
As the person doing the introducing you can edit the introduction before it’s sent, so you don’t risk sending your friend someone that’s only going to waste their time. The smoother the introduction goes at the start, the easier it will be to connect.

Ukaguzi waanza kubaini madudu katika kulipa mgambo mishahara, mabango

MANISPAA ya Ilala, Dar es Salaam imeanza ukaguzi wa ndani ili kubaini ufisadi katika mfumo wa ulipaji mishahara ya askari mgambo.

Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa baadhi ya mgambo hao walikuwa wakilipwa mshahara tofauti na uliokuwa unafahamika wa Sh 280,000 kwa mwezi.

Badala yake baadhi yao walikuwa wakilipwa kati ya Sh 50,000 na 80,000 kama posho badala ya Sh 280,000 zilizokuwa zimeidhinishwa na manispaa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kukabidhiwa Ilani ya Ukawa pamoja na mwongozo wa kazi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, alisema baadhi ya maofisa ambao si waaminifu walikuwa wakijichotea fedha kupitia mishahara ya mgambo kinyume cha sheria.

Alisema Manispaa ya Ilala ilikuwa na mgambo 150 ambao walikuwa wakiajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, lakini watendaji walikuwa wakitumia mbinu chafu kuwapunja mishahara yao.

“Katika uchunguzi wetu tumebaini mgambo hao baada ya kumaliza mkataba wa miezi mitatu walikuwa wakipunguzwa na kubaki 100, huku 50 wakiondolewa kwenye ajira, lakini vitabu vya mishahara vilionyesha ni 150.

“Walikuwa wakisimamishwa kazi huku wakiendelea kuwatumikisha kwa ujanja bila kuwapa malipo yao stahiki, wakati vitabu vya manispaa vilikuwa vikionyesha wanalipwa mshahara kamili.

“Cha ajabu baada ya ukaguzi wa awali tulibaini baadhi ya mgambo walikuwa wakisitishiwa mkataba na kutumiwa kwa ujanja kisha kulipwa Sh 50,000 hadi 80,000 wakati kwenye vitabu vya manispaa vilikuwa vinaonyesha wamelipwa Sh 280,000 ambazo walikubaliana awali,” alisema Kuyeko.

MABANGO YA BIASHARA

Kuyeko alisema Manispaa ya Ilala imeingia mkataba na kampuni ambayo imeanza kufuatilia mabango yote yaliyokuwa yanakwepa kulipiwa ushuru pamoja na kodi kwa ujumla.

Aidha Kuyeko alizungumzia hali mbaya iliyopo katika miundombinu ya elimu ambapo alisema shule nyingi za Serikali zipo hoi kiasi cha kukatisha tamaa.

Alizitaja shule za sekondari Azania, Pugu Bangulo, Pugu Stesheni na Bonyokwa kuwa miundombinu yao imechakaa kiasi cha kutisha na kuhatarisha maisha ya walimu na wanafunzi.

Akitolea mfano Shule ya Bangulo, alisema darasa la kwanza lina wanafunzi 305, huku kila moja likiwa na wanafunzi 100, hivyo walimu wanalazimika kufundisha chini ya miti kutokana na uhaba wa madarasa.

Alisema katika Sekondari ya Azania wameshuhudia vyoo vikiwa vimefurika maji taka na wanafunzi wanalala chini kutokana na msongamano kuwa mkubwa.

Ili kukabiliana na hali hiyo, Kuyeko alisema wameweka mkakati wa kujenga madarasa matano kila shule.

Mradi mpya kuvunja nyumba 388 kando ya mto Ng'ombe - Ubungo Msewe - Bonde la Mkwajuni hadi Selander

NYUMBA 388 katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, zinatarajiwa kuvunjwa kupisha mradi wa kuboresha kingo za Mto Ng’ombe utakaoanza kujengwa hivi karibuni.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera, alisema Sh bilioni 4.4 zinahitajika kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi wa maeneo hayo.

Alisema ujenzi wa mradi huo utaanzia Ubungo Msewe kupitia Bonde la Mkwajuni na kuishia Daraja la Selander.

“Tayari tumeanza kuzitambua na kuzitathmini nyumba zote zitakazovunjwa kwa kuziwekea alama ya X. Zinahitajika Sh bilioni 4.4 tuwalipe fidia wananchi ndipo wafadhili wetu watoe fedha za mradi,” alisema Mhowera.

Alisema kata nane za manispaa hiyo zitapitiwa na mradi huo ambazo ni Ubungo, Sinza, Tandale, Manzese, Kijitonyama, Hananasif, Magomeni na Mwananyamala.

Kwa mujibu wa Mhowera, mradi huo utagharimu Dola za Marekani milioni 300 ambazo ni sawa na Sh bilioni 660/= ambazo zitatumika katika uboreshaji huo.

Mhowera alisema mbali ya kuboresha mto huo, fedha hizo zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) kama msaada pia zitaboresha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam kama barabara, madaraja, mifereji ya maji taka na uzoaji taka.

Wakati huo huo manispaa hiyo imeendelea kuweka alama ya X katika nyumba zilizojengwa katika hifadhi za barabara, maeneo ya wazi na mengine yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii kulingana na mpango mkuu.

Lugha ya Kichina kufundishwa Tanzania kuanzia shule za sekondari

KATIBU Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Leonard Akwilapo, amezindua mpango maalumu wa kufundisha somo la Kichina katika shule za sekondari.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Akwilapo alisema mpango huo umeanzishwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China, ambapo taasisi ya Confucius Philosophy itatoa mafunzo hayo.

“Tayari tumeanza kutoa elimu hiyo kwa kidato cha kwanza na cha tano ambapo kwa hapa Dar es Salaam tumeanza na sekondari ya Zanaki na Benjamin Mkapa, Mkoa wa Morogoro ni Kilakala na Morogoro Sekondari na mkoani Dodoma ni Uwanja wa Ndege na Dodoma Sekondari,” alisema Akwilapo.

Kauli hiyo ya Katibu Mkuu imekuja wakati ambao mwanafunzi raia wa China aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Feza ya Jijini Dar es Salaam, Congcong Wang, akiwa ameacha gumzo kutokana na kushika nafasi ya kwanza kwa kupata alama B katika lugha ya Kiswahili.

Alisema ni fursa sasa kwa wanafunzi na Watanzania kujifunza lugha hii itakayowezesha kuwasiliana na kufanya biashara na Wachina.

Aliongeza kuwa tayari wamepokea walimu wa kujitolea 12 kutoka China ambao watagawanywa katika shule sita ambazo ni za majaribio.

“Tumeanza kufundisha walimu wazawa watakaokuwa wakifundisha lugha hiyo shuleni ambapo masomo hayo yameanza katika vyuo vikuu vya Dodoma, Dar es Salaam na chuo cha waislamu cha Morogoro,” alisema Akwilapo.

Akwilapo alisema kutokana na nchi hizo mbili kubadilishana wanafunzi, mpaka sasa kuna wanafunzi wengi wa hapa nchini wanaosoma China, lakini changamoto kubwa ilikuwa lugha.

Naye Mkurugenzi wa Ubalozi wa China nchini, Gao Wei, alisema kuna umuhimu wa Watanzania kujifunza lugha hiyo kutokana na ukaribu na ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Manzese kufumuliwa na Waitaliano na kujengwa majengo ya kisasa


ENEO la Manzese lililopo jijini Dar es Salaam linatarajiwa kufumuliwa na kujengwa majengo ya kisasa kutokana na ramani ya mipango miji inayofanywa na wataalamu.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipogawa ramani 104 kati ya 329 kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ya Dar es Salaam ili kumaliza migogoro ya ardhi.

Lukuvi alisema hadi kufikia Julai, mwaka huu, Dar es Salaam itakuwa na mipango miji yake ambayo kazi hiyo inafanywa na wataalamu kutoka nchini Italia.

“Dar imejaa lakini lazima tujenge, Manzese ihame lazima ije Manzese mpya, iende juu. Hatufukuzi watu pale lakini watatafutiwa namna,” alisema Lukuvi.

Alilitaja eneo jingine litakalojengwa nyumba za kisasa, hoteli pamoja na kumbi za mikutano ni kando ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

“Eneo hilo lazima liwe transformed (libadilike) ili kuendana na uwanja wa ndege wa kisasa ambao unajengwa. Hatuna haja ya watu wamekuja kwa ajili ya mikutano kuja hadi katikati ya mji,” alisema Lukuvi.

Alitaja miji mingine ambayo inatengenezewa mipango miji ni Arusha ambayo itakwenda hadi Meru na Mwanza ambako wataalamu wanaohusika kuutengeneza wanatoka nchini Singapore.

“Hao Singapore ni watu wenye uwezo mkubwa, master plan ya Mwanza na Arusha tumeshawalipa fedha nyingi za wizara hivyo itakuwa tayari. Awali ya Dar ilivyoletwa niliikataa kwa kuwa ilikuwa na upungufu na haikuwa na basement wala data za sasa,” alisema Lukuvi.

Alisema ramani hizo zitawasaidia wenyeviti hao wa vijiji kujua ni yapi maeneo ya wazi na wapi panapaswa kujengwa nini pindi watendaji wa miji wanapokwenda kwa lengo la kufanya kazi.

“Hii ya kuvunja vunja nyumba za masikini kama mwenyekiti wa mtaa hana ramani anashindwa kumtetea mnyonge anayebomolewa. Leo hii mama masikini akivamiwa ardhi yake mwenyekiti anaweza kuingilia, leo hii wenyeviti 104 tunawapa ramani,” alisema Lukuvi.

Alisema hilo litasaidia kuwaondoa wote waliojenga katika maeneo ya wazi pamoja na maeneo ya huduma za kijamii.

Lukuvi alisema kuna watu waliuziwa viwanja tofauti na matumizi yanayofanyika ambapo ni lazima virudishwe.

“Nitaanza na Mbezi eneo ninakoishi, eneo la Shule ya Msingi ya Kata watu wamevamia, jamani mkiona uvunjifu toeni taarifa wilayani kuweni wa kwanza kuwa askari.

“Mfano kati ya majengo 48 yaliyobomolewa Kinondoni, 12 yalimaliziwa na matapeli, kuna waliokuwa wameanza msingi matapeli wakaja kumalizia hao wameshindwa hata kutufikisha mahakamani, lengo letu ni kuzuia uendelezaji holela wa majengo,” alisema Lukuvi.

Alisema Dar es Salaam haina haja ya kuwa na mabwana shamba au nyuki badala yake waongezwe wataalamu wa mipango miji.

Katika hatua nyingine, alisema awamu ya pili itafanya urasimishaji na nyumba zitakazokutwa zimejengwa maeneo mazuri hazitabomolewa.

“Mtaa ulio tayari kurasimishwa watuambie. Kwa uzembe wetu Serikali au kuchelewa, wananchi walituwahi kujenga sasa kama wako pazuri wasibomolewe, nyumba za masikini zitakazorasimishwa zipewe namba na hati,” alisema Lukuvi.

Aliwataka viongozi wa ardhi kwenda maeneo ya matukio wakiwa tayari wametoa taarifa kwa wenyeviti wa mitaa.

Pia aliwataka watendaji waliohudhuria hapo kumfikishia salamu mtu aliyemtaja kwa jina la Mahinga kuwa ndiye kinara wa kutoa vibali vya ujenzi hadi barabarani katika eneo la Kibaha.

Alisema mipango miji itaondoa uvunjifu wa maadili kwa kuweka shughuli moja katika eneo husika.

“Watu wanapiga muziki hadi asubuhi huku grocery wanauza kitimoto hatua mbili ya msikiti, eneo jingine wanauza pombe hatua mbili kanisa. Zipo nyingi lakini zinapaswa kuendeshwa kwa maadili, lazima kurudisha nidhamu, mwenyekiti aanze kurudisha nidhamu,” alisema Lukuvi.

Alisema watu wanaokuja kuomba kujenga wasiangaliwe sura bali waambiwe utaratibu ulivyo na kama ni eneo la kujenga ghorofa moja lijengwe hivyo na si vinginevyo.

“Nyie msivunje lakini mtoe taarifa hata kama ni ujenzi wa choo ambao hauna kibali toeni taarifa lengo ni kuwapa silaha ili tuijenge Dar es Salaam ambayo ndio kioo cha nchi. Jiji limejaa lakini hadi Julai utaona mabadiliko hakutakuwa na uvamizi,” alisema Lukuvi.

Aliwataka wenyeviti hao ambao wana matatizo katika maeneo yao na walikwishatoa taarifa wilayani lakini hazifanyiwi kazi kwenda moja kwa moja ofisini kwake au kutuma ujumbe mfupi kupitia namba ya simu aliyowapatia.

Alisema ili kuboresha waliitoa Pwani katika Kanda ya Dar es Salaam ambako kwa sasa wana uwezo wa kumpatia mtu hati ya nyumba ndani ya mwezi mmoja.

Alisema hadi sasa kuna hati 3,000 za nyumba ambazo wananchi hawajakwenda kuzichukua huku wizara hiyo ikijitahidi kuboresha ili kuingia katika mfumo wa elektroniki ambako hati inaweza kupatikana kwa siku moja.

Awali, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Mikoa, Profesa John Lupala, alisema michoro ya mitaa 104 ilikamilika kati ya mitaa 329 huku iliyobaki ikisubiri urasimishaji.

Alisema katika michoro hiyo, Wilaya ya Kinondoni ilipata 33, Temeke 10 na Ilala 61.

Profesa Lupala alisema katika sensa iliyofanyika ilionyesha Kinondoni ina kata 35 na mitaa 113, Temeke kata 36 na mitaa 105 huku Ilala ikiwa na kata 35 na mitaa 111.

“Kwa maeneo ambayo hayana utata, Machi 30 itakuwa tayari lakini yenye urasimishwaji Juni yatakamilika,” alisema Profesa Lupala.

Tukaupande mlima Kilimanjaro na Rashid MatumlaHabari wapendwa!

Tunazindua Tamasha maalum la Pasaka la utalii wa ndani kwa kupanda mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Marangu kwa siku sita (6) Kuanzia tarehe 20/03/2016 na kumaliza tarehe 25/03/2016.

Huu ni mpango maalum chini ya bidhaa yetu mpya iitwayo “Tamasha la Pasaka la utalii wa ndani” Kama ilivyoandikwa katika magazeti ya Nipashe na Mwananchi juzi tar 10/02/2016.

Karibu ushiriki katika tukio hili muhimu sana na utengeneze kumbukumbu ya muhimu sana maishani mwako kwa kupanda Mlima Kilimanjaro na Kili Base Adventures Limited.

Wageni kutoka Dar es Salaam wataongozwa na bondia maarufu wa zamani wa ngumi za kulipwa Rashid Matumla.

Na Sehemu ya fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo zitakwenda kusaidia baadhi ya vituo vya kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magum katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Pia sehemu ya fedha hizo zitatumika katika kuchangia vita thidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, na zingine tutazielekeza katika kusaidia kupiga vita uwindaji haramu wa wanyama pori.

Gharama za kushiriki ni shilingi Milioni moja na laki mbili tu. (TZS 1,200,000)

Gharama zitajumuisha:
- Gharama za malazi hotelini kwa siku 2
- Vifaa vyote vya kupandia mlima
- Chakula mlimani –asubuhi –mchana – na jioni
- Usafiri kutoka Moshi kwenda getini na siku ya kurudi Moshi.
- Mishahara kwa; wabeba mizigo, wapishi, maguide wasaidizi na viongozi wa msafara (Guides)
- Gharama zote za ada ya kupanda mlima

Kwa maelezo zaidi na ushiriki piga simu; +255 (0) 756 522 865
Au barua pepe: [email protected]

Special Kilimanjaro Climb for East Africans: Let's go with Rashid MatumlaEast Africans - Come and Enjoy your Mountain!

Let’s Climb Kili Together!

We’re launching a special Kilimanjaro Climb for East African residents starting on 20th March and finishing on 25th March 2016 along the Marangu Route.

This is a special hike launched to celebrate the Easter Domestic Tourism Festival (EDTF)

Former World Boxing Union Champion (WBU) Rashid Matumla, who was also International Boxing Union (IBU) Champion will be accompanying the hikers.

This special Kilimanjaro Climb was recently featured in the Nipashe and Mwananchi news papers and entries are now open. Everyone is welcome to join this very special event hosted by Kili Base Adventures.

The tour cost per person is one million two hundred thousand Tanzania shillings. (1,200,000) Usd $550 - donations also welcome.

Part of the money raised on this tour will be used to support orphanages centers around Kilimanjaro region and Arusha as well as supporting programs against wild life poachers and against killing Albinos.

International residents wanting to take part in this event, are more than welcome. There are special rates for residents from outside East Africa as well.

Inclusive of:
- 2nights hotel accommodation in Moshi
- Mountain climbing equipments
- All meals while on mountain
- All transfers from Moshi to Marangu gate and back to Moshi
- Salaries for; porters, Chefs, Asst guides, and certified Kilimanjaro guides.
- All Kilimanjaro National Park fees.

For inquiries and bookings please contact Wallace +255 (0) 756 522 865

NW Mpina kipa siku 7 kiwanda cha A to Z kulipa faini ya sh mil 70/=Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Luhaga Mpina amekiamuru kulipa faini kiwanda cha A to Z cha mjini Arusha , chenye kufanya kazi ya kuzalisha nguo na bidhaa za plastiki kutokana na ukiukwaji wa utekelezaji wa sheria namba 20 ya mwaka 2004 ya utekelezaji na usimamizi wa mazingira.

Mhe. Mpina alitoa agizo hilo jijini Arusha siku ya Jumamosi katika ziara yake ya kukagua usafi wa mazingira, kupanda miti na kutembelea viwanda, ambapo alibaini kuwa mnamo Septemba mwaka 2015, kiwanda hicho kilipewa adhabu ya kulipa faini ya shilingi milionni 70 na kukaidi kufanya hivyo kwa kipindi cha miezi sita sasa.

Mhe. Mpina amekitaka kiwanda hicho kulipa faini hiyo kwa kipindi kisichopungua siku saba kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa.

Aidha Naibu Waziri Mpina alitembelea viwanda vya Sunflag na Lothia Steel vya jijini humo na kujionea namna ambavyo vinakabiliana na utunzaji wa mazingira katika uzalishaji wao na changamoto ya kuzimikazimika kwa umeme jijini Arusha.

Mhe. Mpina alikitaka kiwanda cha chuma cha Lothia Steel kupima moshi unaotoka katika kiwanda hicho ili kujua kama una athari kwa mazingira na viumbe vinavyozunguka maeneo ya kiwanda hicho.

Ziara na Mhe. Waziri katika jiji la Arusha ni matokeo ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais John Pombe Magufuli la usafi wa mazingira unaotakiwa kufanyika kitaifa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.


Kikao kikiendelea.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina, ziarani katika baadhi wa viwanda jijini Arusha. (Picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais)

WM Majaliwa akagua bandari ya Mtwara

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua bandari ya Mtwara na kunusa harufu ya ufisadi katika utoaji wa zabuni ya ujenzi wa gati mpya tatu. 

Waziri Mkuu ambaye alikagua eneo la ujenzi wa gati hizo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), alisema anazo taarifa juu ya utolewaji wa zabuni hiyo na mzabuni ameshashinda lakini kuna madai kwamba watu wa manunuzi kupitia PPRA ndiyo wanakwamisha zabuni hiyo.

Aliwaomba wabunge wa mkoa wa Mtwara washirikiane kusimamia suala hilo ili ujenzi wake uweze kuanza mara moja na kuleta ajira kwa wana Mtwara. "Ujenzi ukikamilika siyo tu ajira zitaongezeka bali hata meli nyingi zitaleta mizigo katika bandari hii na mapato ya mkoa yataongezeka", alisema.

"Natambua kwamba kuna mpango wa kujenga gati nne ambapo moja kati ya hizo itajengwa na TPA (Mamlaka ya Bandari) lakini hizi tatu zilitangazwa na kupata mzabuni ambaye ni kampuni ya Hyundai kutoka Japan. Lakini hii kampuni imekuwa ikizungushwa bila sababu. Tutafuatilia kubaini tatizo liko wapi," aliongeza. 

"Sasa hivi tuna uwezo wa kupaki meli moja tu, lakini gati zikikamilika tutaweza kuwa na meli tatu kwa mpigo, cha msingi tusimamie maamuzi yetu kwamba lazima wafanyabiashara wa korosho watumie bandari hii kusafirisha mizigo yao na si kuipeleka kwingine." "Kwenye Bodi ya Korosho nako kuna majipu yanahitaji kutumbuliwa. RCC ilishakaa na kupitisha uamuzi kuwa mizigo yote ipitie bandari ya Mtwara lakini kuna watu ndani ya Bosi hiyo wanatoa vibali vya kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Dar es Salaam."

Alimtaka mkuu wa bandari ya Mtwara (Port Master) Bw. Prosper Kimaro awe makini na watu wa kitengo cha manunuzi katika bandari hiyo kwani kimekuwa chanzo cha upotevu wa fedha za Serikali kutokana na ujanja wa watu wachache. 

"Hapa si kuna mtu alitaka kuiba sh. milioni 300 kwa kufoji saini za wakubwa wake? alihoji Waziri Mkuu swali ambalo lilijibiwa na Bw. Kimaro kwamba ni kweli lakini uongozi uliingilia kati kabla wizi huo haujakamilishwa.

Kuhusu fidia kwa wakazi wa vijiji vya Kisiwa na Mgao ambao wamekubali kuhama ili kupisha upanuzi wa bandari hiyo, Waziri Mkuu aliwahakikishia wabunge hao pamoja na uongozi wa bandari kwamba kiasi cha sh. bilioni 13.8/- kimekwishatengwa na Wizara na kitatolewa mapema mwezi ujao.

Alitumia fursa hiyo kusisitiza udhibiti wa bandari bubu ambazo zinatumiwa kuingiza sukari na mchele mchezo ambao unaikosesha Serikali mapato. "Mkuu wa Mkoa, nilikwishatoa agizo kama hilo wakati nimeenda kukagua bandari ya Tanga. Kaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa nanyi pia muweke mbinu za kudhibiti upenyo huu wa kuingiza bidhaa za magendo kwa sababu hawa ndiyo wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali," alisisitiza.

Mkuu wa bandari hiyo, Bw. Kimaro wakati akitoa taarifa ya utendaji wa bandari mbele ya Waziri Mkuu, alisema bandari hiyo ilianzishwa mwaka 1950 na imekuwa inakabiliwa na ufinyu wa gati ya kuegesha meli, vifaa vya kupakulia na kupakia mizigo na kwamba hivi sasa wamekwishapata winchi ya bandarini (harbour crane) yenye uwezo wa kubeba tani 100 na tayari wako kwenye mpango wa kujenga gati moja.

METOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 28, 2016.

Rais Magufuli awasili Arusha kuongoza Mkutano 17 wa Wakuu wa nchi za EAC

Rais Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi na wananchi waliojitokeza kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Arusha ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Jumatano tarehe 02 Machi, 2016 Mjini Arusha.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amelakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja na vikundi vya burudani za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.

Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.Kabla ya kuongoza kikao hicho Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tarehe 03 Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili - Taveta - Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.

Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam

28 Februari 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha Mhe. Lekule Laizer baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akiendelea kusalimia viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassary katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mhe CAtherine Magige baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa dini baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Afande Liberatus Sabas baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na viongozi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bw. Allan Kijazi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamanda wa JWTZ baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Bw. Elishilia Kaaya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akifurahia kikundi cha utamaduni cha Chuo Kikuu cha Tumaini cha Makumira mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akipiga ngoma baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akiangalia vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akifurahia burudani ya ngoma ya Mdumange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akifurahia ngoma ya kinamama baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda akipungia wanannchi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana kwa furaha na aliyekuwa Katibu Myeka wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Samweli Kasori mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

Picha zote na IKULU