Kauli ya Waziri Kivuli kuhusu uchaguzi wa marudio Zanzibar

KAULI YA WAZIRI KIVULI WA WIZARA YA MUUNGANO NA MAZINGIRA KUHUSU UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR


March 31, 2016

Wana Habari,

Tunaelewa sote kuwa Uchaguzi wa Marudio umefanyika Zanzibar na hivi sasa kuna harakati zinazoendelea kuunda Serikali kutokana na uchaguzi ambao umekosa uhalali wa kikatiba na kisheria.

Kambi Rasmi ya Upinzani inatamka wazi kuwa haitautambua uongozi huo wa Serikali ya Zanzibar na wala haitatoa ushirikiano wowote kwayo.

Uongozi mzima wa Serikali ya Zanzibar hauna uwezo wa kikatiba na kisheria kushiriki katika suala lolote la Muungano kwa sababu umekosa ridhaa ya Wazanzibar kutokana na kufutwa uchaguzi halali tarehe 28 Oktoba 28, 2015 na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya ZEC na pia hapakuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuwepo kwa Uchaguzi wa Marejeo wa Machi 20, 2015.

Ieleweke kuwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar una athari ya moja kwa moja kwa upande wa Jamhuri ya Muungano, na Kambi Rasmi ya Upinzani inapinga kwa vyovyote vile uchaguzi huo kuhusishwa na mambo ya Muungano na itapinga na kulaani kitendo chochote kitachoelekeza hivyo.

Mnasaba wa Uchaguzi huo na Muungano ni katika maeneo yafuatayo ambayo kwa hali ilivyo kwa sasa yameingia katika mashaka na mgogoro wa kikatiba:

Pamoja na mamlaka ya Zanzibar kutajwa katika Katiba yake ya 1984 lakini pia yanatajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Kifungu cha 4 (2) na hapana shaka Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatambua misingi ya demokrasia na kwa hivyo kwa utawala wa sasa kuingia madarakani kwa misingi isiyo halali na kufanya teuzi zinazohusu Baraza la Mawaziri, Mahakama na Baraza la Wawakilishi kunatia katika utata Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani hatutalikubali jambo hilo la kutiwa doa na kuipuuza Katiba ya Jamhuri ya Muungano na tutafanya kila njia kuonyesha kutoridhishwa kwetu kunajisiwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Uchaguzi Mkuu wa Marejeo na unyakuaji madaraka uliofanywa huko Zanzibar unakwenda kinyume kabisa na Malengo Muhimu na Msingi wa Mwelekeo wa Shughuli za Serikali kuhusu Serikali na Watu inasemwa katika Kifungu 8 (2):
Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vvyombo vyake na uendeshaji wa shughuli zake utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa
Uchaguzi wa kihuni uliofanywa Zanzibar huawezi kabisa kuwa unaakisi kifungu hiki cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano si kwa kuzingatia umoja wa kitaifa wala si kwa kudumisha heshima ya kitaifa.

Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani watalisimamia jambo hili kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa Marejeo hautasimama mbele ya macho ya sheria na katiba na tukijua kuwa kutakuwa na tishio la kutetereka umoja wa kitaifa..

Wala Wabunge wa Kambi ya Upinzani hawatakubali Tanzania ipate aibu mbeleya wananchi wake lakini pia mbele ya macho ya kimataifa ambapo jina la Tanzania limekuwa kubwa, la kuaminika na la kusifika lakini linaweza kabisa kuharibiwa na aibu hii.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano Kifungu 54 (1) Rais wa Zanzibar anakuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri wa Muungano, na kwa hivyo atatarajiwa kula kiapo kushika nafasi hiyo.

Kambi Rasmi ya Upinzani inasema Dk. Ali Muhammed Shein hakushinda katika taratibu zinazoendana na misingi ya demokrasia kwanza kwa kuhusika kwa kiasi kikubwa kwa nguvu za kijeshi kupitia vitisho vilivyokuwa vikionekana na kujiri hata majeshi yetu kuvaa soksi za usoni.

Dk. Shein amechaguliwa katika kipindi ambacho kamatakamata ilikuwa kubwa ambapo katika kipindi kabla ya Uchaguzi wa Oktoba zaidi ya watu 100 walikamatwa na katika kipindi cha baada ya Oktob hadi Machi 20 watu zaidi ya 150 wamekamatwa pamoja na kukamatwa na kuhojiwa viongozi wa Chama cha Wananchi CUF.

Kambi Rasmi ya Upinzani inasema kuwa Dk. Ali Muhammed Shein hana uhalali wa kushika nafasi hiyo kwa sababu matokeo ya Uchaguzi wa Marejeo yana kila dalili kuwa yalikuwa ni ya kupanga kitakwimu. Kwa mfano katika Jimbo la Malindi, Dk Shein alipata kura 2,334 katika Uchaguzi wa Oktoba, lakini katika Uchaguzi wa Machi 20 akapata kura 5,873 ikiwa ni ongezeko la kura 3,539. Na kwa Jimbo la Mwanakwerekwe, Dk. Shein alipata kura 4,003 Oktoba, lakini akaibuka na kura 9,5,97 hapo juzi ikiwa ni ongezeko la kura 5,594. Majimbo yote hayo Maalim Seif aliongoza kwa kura Oktoba.

Kwa mujibu wa majimbo ambayo Tume ilikuwa imeyatangaza mpaka Oktoba 28, 2015 ambayo yalikuwa ni 31, ZEC inaonekana imemuongezea Dk. Shein kura za chini kabisa kwa kiasi cha 61 na za juu kabisa ni 5,594 jambo ambalo halielekei, halina mantiki na haliwezekani. Maana hata majimbo yote ya Pemba, Dk. Shein amepata kura za ziada.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 66 (1) (c) Wajumbe 5 wa Baraza la Wawakilishi huingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na hushiriki katika shughuli zote za Bunge kama vile kutunga sheria na kushiriki katika Kamati mbali mbali za Bunge.

Pia kama itampendeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ana uwezo wa Kikatiba wa kumteua yoyote mmoja wao au wote kushika nafasi ya Uwaziri katika Jamhuri ya Muungano. Katika Uchaguzi huo wa Marejeo pia alipigiwa kura Mbunge pekee aliyekuwa amebakia Shamsi Vuai Nahodha wa Jimbo la Kijitoupele.

Ushiriki wa Wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi utalivunjia hadhi Bunge kwa kuwa watakuwa wanatokana na uchaguzi ambao haukukidhi vigezo vya kidemokrasia na inawezekana pia wakatoka katika majimbo ambayo hata Uchaguzi wa Oktoba majimbo wanayoyashika sasa yalikuwa yamekwenda kwa upinzania na kukabidhiwa vyeti vya ushindi na ZEC.

Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga ushiriki wa Wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi kwa sababu wameshiriki katika zoezi zima la kubaka demokrasia pia wanatokana na Baraza la Wawakilishi ambalo uhalali wake unakwenda kinyume na matakwa ya katiba na sheria kwa kupokea Wajumbe ambao hawakupitia mchakato unaokubalika wa kikatiba.

Kambi ya Upinzani inaonya kuwa kutakuwa na migongano kadhaa ya Kikatiba katika suala hili bila ya kuwepo na ulazima isipokuwa itatokea kwa sababu Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeamua kuitia kwenye mbeleko Serikali ya Drk Shein ili kuendeleza ubabe wa CCM kuitawala Zanzibar kwa nguvu na kudhihirisha nia ya Serikali ya Jamhuri kutokubali kuruhusu maamuzi ya kidemokrasia huko Zanzibar.

Kambi ya Upinzani inasema wazi kuwa kubebwa kwa utawala wa Dk. Shein kutozorotesha uimara wa Muungano na kuutia mtihani mkubwa hasa kwa vile matokeo ya Uchaguzi wa Marejeo yameshindwa kujenga mazingira ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ilileta utulivu na kuupa pumzi Muungano, lakini hali hii mpya inatoa fursa kwa upinzani kudai kwa nguvu zote kuwepo kwa Katiba Mpya ambayo tutaidai kwa nguvu zetu zote.

Ally Saleh (Mbunge)
Waziri Kivuli wa Muungano na Mazingira
Machi 31, 2016

0715 4300 22 / 0777 4300 22

Mvua na upepo waezua mapaa ya nyumba Nyabisindu, Ngara


Ofisi ya CCM Tawi la Nyabisindu iliyopo Kata ya Kabanga wilayani Ngara,mkoani Kagera.

Shule ya sekondari Nyabisindu iliyopo Kata ya Kabanga wilayani Ngara,mkoani Kagera.

Enjoy KLM on Messenger and win 2 tickets! Facebook can now be your boarding pass

KLM is offering a new way to receive your flight documentation: Facebook’s Messenger service. After booking your flight on klm.com you can choose the option to receive booking confirmation, check-in notification, boarding pass and flight status updates via Messenger.

 Any questions? No problem. Ask away and contact KLM directly through Messenger, 24/7.

Win a ticket!

Choose for KLM info on Messenger on the booking or check-in page on KLM.com. If you do so between 30 March and 27 April, you automatically have a chance at winning 2 KLM return tickets to a destination of your choice.

Source/More info: https://messenger.klm.com

You should not use Hydrogen Peroxide to clean wounds - Explained


Now you can 'unread'; 'quick reply' from notification on WhatsApp (Android)


In addition to the previous updates, here are some notable new ones in the recently released WhatsApp apk (version 2.16.4 available for download from APKMirror)
 • When attaching a PDF, you can now tap "Browse other docs..." to pick a PDF from another source, like Google Drive or Microsoft OneDrive (Android 4.4+).
 • View PDFs you've sent and received by tapping Media from contact info or group info
 • You can now view starred messages for a given chat from contact info or group info
 • When clearing a chat, you can choose to keep your starred messages
 • The ability to quickly reply to a message without opening up the app and the entire conversation. The expanded notification now show s a Reply button that opens up WhatsApp's own overlay. The window that pops up shows the message's sender, text, and includes a couple of options to answer. There's a text box, a vertically aligned emoji panel, a voice message option, and buttons to close it (which dismisses the notification without sending an answer) and view it (which opens the full conversation in WhatsApp) 
 • When you tap the profile or group image of any conversation (single contact or group), you get an overlay window with a faster way to perform the actions of the long-tap menu in the app's title bar. For a single contact, you get: Archive, Delete, Mute/Unmute, Add chat shortcut, View contact, and Mark as read/unread. For a single group, you get: Archive, Leave group, Mute/unmute, Add chat shortcut, Group info, and Mark as read/unread. You can multiple select chats, regardless of their muted, read, or contact/group state. 
 • The grey Default wallpaper icon is replaced wit a new circle icon with a color reminiscent of WhatsApp's own shade of teal green. A fifth option has also been added: solid color. This opens up a list of different solid colors that you can preview and apply for a bit of an added personal touch to your conversations.
Tips via Android Police

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 31, 2016How a 17-year-old started a poultry business in the slums of Dar es Salaam


Tackling hunger in Tanzania with low-cost chickens

At the age of 17, Sirjeff Dennis from Dar es Salaam in Tanzania had 50 dollars to his name. But he had a grand plan for his savings - to end malnutrition in his community. Five years later, Sirjeff runs a successful business supplying local people with low cost chickens and vegetables from his farms. He told Matthew Bannister it all started when he was growing up in a very poor area.More donors 'pull Tanzania aid', Why are Western donors withdrawing?

The embassies of Sweden and the Republic of Ireland in Tanzania have confirmed that they are no longer providing the Tanzanian government with budgetary support, the BBC's Sammy Awami reports from the commercial capital Dar es Salaam.

The Tanzanian finance ministry said on Wednesday that 10 Western donors were withdrawing the direct financial support they give the government (see earlier entry quoted below).
A group of 10 Western donors have announced they are withdrawing budgetary support to the Tanzanian government.
It follows a decision by a US government aid agency to pull $472m (£331m) of funding for development projects because of concerns over the electoral process in Zanzibar.
About a third of Tanzania's budget last year depended on donor support, so this latest move is a blow to the new government’s development plans. [end of earlier entry]
It leaves the European Union (EU), the World Bank, the African Development Bank (AfDB) and Denmark as the four remaining donors, according to the finance ministry, local media reports.

It represents another blow to the government of President John Magafuli after the US pulled $472m (£331m) of funding for development projects because of concerns over recent elections in Zanzibar.

The Swedish embassy said in a statement that their decision was not connected to Zanzibar, but rather due to "corruption surrounding the energy sector" and the scheduled expiration of the current agreement.

The Republic of Ireland embassy said it had "no further plans to release budget support" and that the last payment was made in June 2015.

One regional analyst has tweeted a cartoon that Tanzania's privately-owned Guardian newspaper, portraying the apparent dash for the exit by donors in recent days.

Kasheshe la mwekezaji wa NMC Arusha vs serikali


Serikali imeshindwa kuipokonya kampuni ya Monaban Trading & Farming uendeshaji wa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) tawi la Arusha na badala yake, katika mazingira tata, imeongezewa miaka 10 kuanzia 2014.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kuwa tangu mwaka 2008, wajanja wachache serikalini wamehusika katika njama za kuzuia shirika hilo kurejea mikononi mwa Serikali na baadaye kukabidhiwa kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPB).

Taarifa kutoka kwa viongozi kadhaa na nyaraka mbalimbali zinaonyesha kuwa katika kikao chake cha Novemba 7, 2008, Baraza la Mawaziri lilijadili na kushauri mali zote za NMC zilizoko chini ya mwekezaji huyo zichukuliwe na kukabidhiwa kwenye bodi hiyo baada ya kuona uwekezaji huo haukuwa na tija kwa Taifa.

Mali za NMC zilizotakiwa kukabidhiwa kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko tangu mwaka 2008 ni mashine za unga zenye uwezo wa kuzalisha tani 47,000 kwa mwaka, maghala yenye uwezo wa kihifadhi tani 38,000 pamoja na nyumba kadhaa. Mali zote za NMC zilizopo Arusha zinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola 100 milioni za Marekani, zikiwa katika eneo lenye ukubwa wa heka 4,489.

Mbali ya mashine na maghala, NMC inamiliki nyumba za wafanyakazi mjini Arusha ambazo mpaka sasa hazijulikani ziko chini ya nani.

NMC ni moja ya mashirika ya umma yaliyoshindwa kujiendesha ambayo yaliwekwa chini ya Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC). Baadaye PSRC ilivunjwa na likaundwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) na lilikabidhiwa mashirika machache ambayo hayakubinafsishwa, likiwamo tawi la NMC mkoani Arusha.

CHC ilifanikiwa kurejesha mali za NMC zilizokuwa katika mikoa ya Iringa Aprili 2011; Mwanza, Aprili 2012 huku mali za Dodoma zikirejeshwa Agosti 2013. Lakini mali za NMC Arusha hazikurejeshwa na badala yake zikaachwa kuendelea kuwa mikononi mwa mwekezaji ambaye Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Agosti 23, 2007 kampuni ya Monaban iliingia mkataba wa miaka mitano na NMC wa kukodisha mali zote za shirika hilo zilizopo eneo la Unga Limited, yakiwamo maghala na kinu cha kusaga unga.

Juni 23 mwaka 2014, mwekezaji huyo aliingia mkataba mwingine na CHC ambao unatarajiwa kuisha mwaka 2023.

Ingawa uamuzi ulifikiwa mwaka 2008 na ukasisitiziwa Februari 4, 2011 na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe alipokuwa akizindua COPB, hakuna kilichofanyika na badala yake ni mawaziri wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kushindana kuandika barua zinazopingana kuhusu uwekezaji NMC.

Juni 24, 2014 ilipewa mkataba mwingine wa miaka 10 ambao unatarajiwa kuisha mwaka 2023. Mkataba huo mpya uliongezwa huku Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ikiwa imeshamwandikia barua katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Novemba 20, 2013 kumueleza kuwa hawautambui mkataba wa NMC na Monaban kwa kuwa serikali iliuona kuwa hauna manufaa kwa Taifa.

Vilevile, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko katika barua hiyo kwa katibu mkuu ikimtahadharisha kuwa kukosekana kwa msimamizi wa mali za NMC zilizopo Arusha kutaikosesha serikali mapato, kwa kuwa Monaban hailipi tozo kutokana na shughuli inazoendesha.

Barua juu ya barua

Mwaka 2013, CHC ilimwandikia barua katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kumtaarifu kuhusu mali hizo na kwamba wanataka kutekeleza agizo la Baraza la Mawaziri la kukabidhi mali hizo kwa Bodi.

Katika barua hiyo Agosti 16,2013, ambayo nakala yake ilipelekwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchaganyiko walieleza kuwa kazi hiyo wataifanya Agosti 31, 2013.

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, kupitia barua ya Agosti 29, 2013 ilikubali kukabidhiwa mali hizo kama ilivyokubaliwa na Baraza la Mawaziri.

Mwkaa huo Agosti 30, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Elimpaa Kiranga alifika mjini Arusha akiwa ameambatana na Ofisa Ugavi wa Bodi, Alfan Semindu na Mwanasheria wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Ernesto Doriye kwa ajili ya makabidhiano.

Hata hivyo, makabidhiano hayo yalikwama kufanyika kutokana na maagizo kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha ambayo yalitaka kusitishwa kwa shughuli hiyo mpaka itakapojulikana hatima ya fedha zilizotumiwa na Monaban kuwekeza kwenye kiwanda hicho.

Baada ya makabidhiano kushindikana, Septemba 23, 2013, Bodi hiyo iliamua kulifikisha suala hilo kwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.

“Mheshimiwa waziri, kutokana na suala hili la makabidhiano ya mali katika kinu cha Arusha kutokamilika kwa agizo la uongozi wa Mkoa wa Arusha, napenda kuliwasilisha suala hili kwako kwa hatua zaidi ili liweze kutafutiwa ufumbuzi wa haraka, Bodi ikabidhiwe mali hizi kama ilivyoagizwa na Serikali,” inasema barua hiyo iliyotiwa saini na Kiranga.

Septemba 19, 2013 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sophia Kaduma alijibu barua ya Kiranga akielekeza mali za NMC Arusha zikabidhiwe kwa Bodi hiyo kama ilivyoagizwa na Serikali.

Katika barua hiyo, Wizara ilipendekeza baada ya Bodi kukabidhiwa inaweza kuipangisha Monaban kwa mkataba wa muda mrefu ili iweze kurejesha fedha ilizowekezwa katika kinu hicho.

Baada ya Stephen Wasirra kuteuliwa kuwa waziri, alikutana na viongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Februari 3, 2015, mjini Dodoma na aliiagiza taasisi hiyo ya serikali ikabidhiwe kinu cha Arusha kama ilivyoagizwa na waraka wa Baraza la Mawaziri namba 40/2008.

Juhudi za Bodi kukabidhiwa kinu hicho zilififia Novemba 27, 2013 baada ya ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Uwezeshaji na Uwekezaji, Mary Nagu kutoa maagizo tofauti kwa CHC kwamba kampuni ya Monaban ipatiwe maghala yote ya kuhifadhia nafaka na kwamba iwe mkodishaji pekee hadi uamuzi wa Serikali juu ya kinu hicho utakapotolewa.

Katika barua hiyo, ofisi ya Waziri Mkuu ilishauri kuwa mwekezaji huyo asibughudhiwe katika shughuli zake. Uamuzi huo ulikinzana moja kwa moja na ule wa Baraza la Mawaziri ambao ulitolewa miaka sita iliyopita kwamba mali za NMC zirejeshwe serikalini.

Mkanganyiko huo uliivutia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambayo ilianza kufuatia kujua kama kuna harufu ya rushwa. “Suala hilo lipo lakini linashughulikiwa na makao makuu, mimi siwezi kulizungumzia kwa kuwa nitaingilia uchunguzi,” alisema kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Juventus Baitu.

Mkurugenzi wa Monaban Trading and Farming Co Ltd, Philemon Mollel alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema ameshindwa kukabidhi kwa kuwa mpaka sasa ametumia fedha nyingi kuwekeza katika kinu hicho na hajui hatima yake.

Alisema alipoingia mkataba wa upangaji aliwekeza Sh6.2 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa kinu cha kusaga ngano na kwa utaratibu maalumu fedha hizo zingerejeshwa kupitia tozo iliyopaswa kulipwa.

Mollel alitaja uwekezaji alioufanya katika eneo hilo kuwa ni kujenga ukuta kuzunguka kiwanda, kuweka sakafu ya matofali madogo kwenye eneo lote, kutengeneza na kuweka mashine ya kusaga na kuweka mfumo wa majitaka, kukarabati na kuweka mashine yenye uwezo wa kusaga mahindi na mtama tani 120 tofauti na ile iliyokuwapo awali iliyokuwa na uwezo wa kusaga tani 60.

Uwekezaji mwingine ni mashine ya kukamua mafuta ya alizeti, kuweka jenereta lenye uwezo wa kuzalisha umeme wa KVA 300, kuchimba kisima cha maji na kuanzisha kiwanda cha kisasa cha mikate.

Alipoulizwa sababu za kutumia fedha nyingi kuwekeza katika kiwanda ambacho si mali yake, Mollel alisema alifanya hivyo akiamini kuwa yeye ni Mtanzania mzalendo atauziwa kama walivyouziwa watu wengine mali za NMC sehemu mbalimbali nchini.

Hata hivyo, alisema ana matumaini ya kupatikana ufumbuzi suala hilo baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage kutembelea kiwanda hicho hivi karibuni na kuahidi kuwa atalifanyia kazi.

Kiranga alipoulizwa alisema wana matumaini makubwa kuwa suala hilo litakwisha na kwamba sasa Serikali itaanza kunufaika na mali zake ambazo zilikuwa zinatumika kwa maslahi ya mtu mmoja.

Mhadhiri SUZA ashikiliwa na polisi akituhumiwa kuhusika kulipua nyumba ya Kamishna wa Polisi

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Saleh Mohammed Saleh, anashikiliwa na polisi mjini Zanzibar kwa madai ya kuhusika kulipua nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame.

Mhadhiri huyo ambaye ni Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF)Zoni ya Magharibi A Unguja na aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Welezo, alikamatwa na saa nane za usiku wa kumkia jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu,Habari na Uenezi, Pavu Juma Abdalla alisema polisi walivamia nyumbani kwa mhadhiri huyo na kuvunja mlango.

Alisema kiongozi mwingine aliyekamatwa ni Mwenyekiti wa chama hicho Zoni ya Mfenesini, Omar Hassan Issa.

Alisema kutokana na hali hiyo, jana kutwa nzima walizunguka vituo vingi ya polisi lakini hawakuwaona.

“Polisi walivamia nyumbani kwao saa nane usiku, wakavunja milango na kuwapiga na kuondoa nao.

“Tumewatafuta vituoni hatukuwaona,tumeambiwa ni miongoni mwa watu wanaoshutumiwa kwa kulipua nyumba ya Kamishna Hamdani,” alisema Pavu.

Alisema CUF wanaendelea na jitihada za kuwatafuta viongozi hao waweze kujua hatima yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alikiri kushikiliwa kwa viongozi hao.

Alisema hakuwa tayari kutaja majina ya watu wengine waliowakamatwa akisema wanaendelea na upelelezi.

“Bado tunaendelea na upelelezi, tukiwa tayari tutatoa kila kitu, kwa sasa hatuko tayari kuwataja majina yao,” alisema Kamanda Mkadam.

Alisema polisi wanaendelea na msako mkali dhidi ya watu wote wanaotuhumiwa kuhusika na ulipuaji wa nyumba hiyo.

“Kutokana na uchunguzi wetu tuliofanya, tunayo orodha ya washukiwa wote na tutaendelea kuwakamata na ikithibitika tutawachukulia hatua,” aliongeza.

Mahakamani kwa kutaka kukusanya kodi kwa kughushi barua ya Ikulu na jina la WM Majaliwa

WAKAZI wanne wa jijini Dar es Salaam wamefikishwa mahakamani kwa kutumia jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kutaka kukusanya kodi ya Sh milioni 175 kwa kutumia barua ya kughushi kutoka Ikulu.

Washtakiwa watatu kati ya hao walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba.

Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi aliwataja washtakiwa kuwa ni mwanafunzi Issa Mohammed (27) ambaye hakuwapo mahakamani kwa sababu amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na mwandishi wa habari, Hamisi Tembo (37).

Washtakiwa wengine, ni Wakati Mungi (51) na mtengeneza mihuri, Nicolaus Obado (32), walisomewa mashtaka 12 yanayowakabili.

Nchimbi alidai shtaka la kwanza, washtakiwa wote wanadaiwa Machi 16 na 17 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika Manispaa ya Ilala kwa pamoja, walikula njama na watu wengine ambao hawapo mahakamani kutenda kosa la kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Shtaka la pili, washtakiwa wanadaiwa kati ya Machi 10 na 17,mwaka huu katika maeneo yasiyofahamika jijini, walijitambulisha kwa nyakati tofauti kwamba ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati si kweli.

“Mheshimiwa hakimu, shtaka la tatu washtakiwa wote, kati ya Machi 10 na 17 mwaka huu, walighushi barua wakionyesha ni halali imetoka Ofisi ya Rais ikielekezwa kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Usangi Logistics Ltd kuweka Sh milioni 25 kwenye akaunti namba 1801833619 katika Benki ya ABC kwa jina la TRA.HR.Mwenge kwa ajili ya kodi.

“Washtakiwa katika shtaka la nne, wanadaiwa kughushi barua wakionyesha imetoka ofisi ya Rais ikielekeza Mkurugenzi wa Bakhresa kuweka benki ya ABC Sh milioni 25, ikiwa ni punguzo la kodi,”alidai Nchimbi.

Washtakiwa katika shtaka la tano, wanadaiwa kuipeleka barua hiyo inayodaiwa kutoka ofisi ya Rais kwa Mkurugenzi wa IPP Media, wakitaka aweke benki Sh milioni 25, ikiwa ni punguzo la kodi.

Katika shtaka la saba, nane, tisa na kumi, washtakiwa wanadaiwa kupeleka barua hiyo kwa Mkurugenzi wa OIL COM , GAPCO Ltd, Lake Oil Tanzania Ltd na Kampuni ya PUMA Ltd.

Washtakiwa wanadaiwa kupeleka barua kwa wakurugenzi wa kampuni hizo, wakionyesha imetoka ofisi ya Rais, ikielekeza kila kampuni iweke benki ya ABC Sh milioni 25 katika akaunti namba 1801833619 iliyopo kwa jina la TRA.HR.Mwenge, malipo hayo ni punguzo la kodi wakati si kweli.

Wakili wa Serikali alidai shtaka la 11 linamkabili mshtakiwa wa kwanza ambaye hakuwepo mahakamani, mashtaka atasomewa akiwa hospitali, katika hati ya mashtaka anadaiwa kuwasilisha nyaraka hizo za kughushi kwa Kampuni ya Usangu Logistics Limited.

Akisoma shtaka la mwisho, Nchimbi alidai linawakabili washtakiwa Issa na Hamisi, wanadaiwa Machi 10, mwaka huu katika ofisi za TSN walijipatia Dola 1000 za Marekani kutoka kwa Farough Ahmad maarufu Bagozah kwa kudanganya fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya gharama za ufadhili aliopata Issa nchini Marekani.

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo, upelelezi haujakamilika na upande wa Jamhuri ulipinga washtakiwa kudhaminiwa kwa sababu wanaweza kuvuruga upelelezi.

Hakimu alikubali na aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa wa kwanza atakwenda kusomewa mashtaka yanayomkabili Muhimbili Hospitali.

Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja Issa ni mwanafunzi wa shule gani wala Tembo ni mwandishi wa habari wa chombo gani.

Job Opportunities at SUA in 3 Projects

Applications are invited from suitably qualified Tanzanians to fill the following vacant positions.

It appears you don't have a PDF plugin for this browser. You can click here to download the PDF file.

Kauli ya TANESCO kuhusu habari ya mishahara iliyochapishwa MTANZANIASIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli, kusema kwamba Serikali inafanya marekebisho ya viwango vya mishahara kwa watendaji wa mashirika ya umma, hatimaye MTANZANIA imebaini viwango mbalimbali vya mishahara wanavyolipana vigogo katika mashirika hao.

Katika mashirika hayo, baadhi ya vigogo hulipana viwango vikubwa vya mshahara, ambapo kigogo mmoja hulipwa Sh Sh milioni 36 kwa mwezi na wengine hufikia kiwango cha Sh milioni 40 kama alivyoeleza Rais Magufuli juzi.

Akizungumza na wananchi wa Chato, Dk. Magufuli alisema watu hao wanaolipwa kiwango kikubwa cha mishahara wamekuwa wakiishi kama malaika na sasa ni lazima washushwe ili waishi kama shetani.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Serikali kiliambia MTANZANIA kuwa, ulipwaji wa viwango vikubwa kwa watendaji wa mashirika ya umma umetengeneza tabaka kubwa la wenyenacho na wasionacho.

Uamuzi huo wa Rais Magufuli, umetajwa kuwa huwenda ukaleta heshima na utu kwa Watanzania, kwani baadhi ya taasisi na mashirika ya umma watendaji wake wa ngazi za juu wameonekana kulipana mishahara ya kufuru.

“Kuna taasisi watendaji wa ngazi za juu wamekuwa wakilipwa mishahara minono zaidi ambapo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hulipana Shilingi milioni 24 kwa mwezi pamoja na marupurupu,” kilisema chanzo chetu.

Taasisi nyingine zinazolipwa kiwango kikubwa kwa watendaji wake ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sh milioni 36, Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Sh milioni 36.

Mashirika mengine ambayo yanaongoza kwa kulipana kiwango kikubwa ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Sh milioni 36 na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambapo watendaji wa juu hulipwa Sh milioni 36.

Mbali na taasisi hizo pia timu ya waatalamu ya Rais Magufuli inaangalia taasisi kama za Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), Ngorongoro, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Taasisi nyingine ni Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Bodi ya Bima ya Amana, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)

Hatua ya Rais Magufuli kupitisha panga na kuweka uwiyano wa mishahara kwa watendaji wa taasisi hizo unaelezwa kuwa utaisaidia uwajibikaji na usawa kwa watendaji.

“Kwa mfano kwa sasa zipo taasisi nyingine hupandishiana mishara kila wakati, unakuta mfagiaji analipwa hadi Shilingi milioni Moja, wakati katika sekta nyingine kama walimu wanaambulia Shilingi 400,000 kabla ya makato.

“Hatuwezi kujenga Taifa la wenye nacho na wasio nacho kwa mfumu huu na ikiwa Serikali italitekeleza hili kama Rais Magufuli alivyoamua ni wazi sasa tutapiga hatua mbele zaidi,” alisema mtoa habari huyo.

Azivaa bodi

Kiongozi huyo wa nchi, alishangazwa na baadhi ya bodi za wakurugenzi kushindwa kufanyakazi zao kwa mujibu wa sheria na badala yake wamekuwa na kazi ya kupandisha mishahara kwa viongozi.

Alisema kutokana na hali hiyo anashangazwa na bodi hizo kila kukicha zimekuwa zikifanya kazi ya kupandisha mishahara pamoja na kufanya vikao nje ya nchi.

Kutokana na hali hiyo, Rais Magufuli ameunda timu ya wataalamu ambayo imeanza kufanya kazi ya upunguzaji wa mishahara mikubwa kwa watendaji wakuu wa mashirika ya umma.

“Tena hawa wakurugenzi ndio wanaongoza kwa kulipwa fedha nyingi na hata kwenda kufanya vikao ulaya, ninasema hapa kwamba suala hili litaanza kushughulikiwa katika bajeti ya hivi karibuni,” alisema Rais Magufuli.

Juzi akiwa wilayani Chato, Rais Magufuli, alisema wapo watendaji wanalipwa Sh milioni 40 kwa mwezi na wengine wanalipwa Sh 300,000.

Alisema tayari ameunda timu ya wataalamu ambayo inafanya kazi ya kupunguza mishahara hiyo na kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi ili asipatikane Mtanzania anayelipwa zaidi ya kiwango hicho.

“Tunafanya hivi ili nyingine tuziteremshe kwa watu wa chini na yule atakayeng’ang’ania kwamba lazima alipwe Sh milioni 40 aache kazi tuweke mtu mwingine,” alisema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli, alishangazwa na watu namna wanavyolipana kile alichokiita mishahara ya ajabu kwa kushirikiana na bodi ambazo wakati mwingine huzihonga fedha ili zipandishe mishahara yao.

“Kuna watu wanaishi kuliko hata malaika lazima tuwashushe waishi kama shetani,” alisema Rais Magufuli.

Pamoja na hali hiyo kiongozi huyo wa nchi alianika madudu aliyoyakuta ndani ya Serikali ikiwemo mmoja wa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kulipwa mishahara ya watu 17 na kuagiza mfanyakazi huyo afikishwe mahakamani.

Pamoja na hali hiyo alisema wapo watumishi wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi Sh milioni 40 kwa mwezi, ambayo sasa itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi Sh milioni 15.

Dk. Magufuli alisema Serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 (single digit) kuanzia bajeti ijayo.

“Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800 na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia Serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za Watanzania.

Alisema anashangazwa na hatua ya baadhi ya watu kuishi kama malaika huku wengine wakiishi kama masheteni, jambo ambalo alisema halina nafasi katika Serikali yake.

“Nyiye mliokuwa mnaishi kama malaika, sasa zamu yenu kuishi kama mashetani,” alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.

Finance Minister: Tanzania "not surprised" by US aid cut


Finance Minister Philip Mpango says that the government had anticipated the move and was prepared with alternative funding.

The Tanzanian government has said the decision by American agency Millennium Challenge Corporation (MCC) to cancel $472 million (about Tsh1 trillion) in funding to the country did not come as a surprise.

Finance Minister Philip Mpango told The Citizen yesterday that the government had anticipated the move and was prepared with alternative funding.

The MCC funding was meant to implement various development projects in energy, road and water sectors.

The MCC board of directors which sat in Washington on Monday voted to suspend the agency’s partnership with the government of Tanzania over the Zanzibar election and application of the Cybercrimes Act run counter to this commitment.

Dr Mpango said the State is currently focussed on sourcing funding for its projects from domestic sources.

“We weren’t surprised at all because we were prepared for whatever the outcome. We will implement those project using local sources of fund and the support of from other development partners,” he said.

He added that since President John Magufuli took office, the government has put emphasis on revenue collection with the aim of cutting dependence on donor funds to implement of development projects.

However, the government said it is still waiting for official communication from MCC to determine the way forward.

“After receiving the official communication we will engage in discussion with MCC in order to know why the board has made that decision and what we (the government) should do in order to be reconsidered,” said Dr Mpango.

Meanwhile, Foreign Affairs and International Corporations minister Dr Augustine Mahiga said the government was disappointed by the MCC decision.

Dr Mahiga said “energy sector is very important for development of the community and now that MCC has suspended its funding wananchi most of projects to supply energy especially to rural areas will suffer.”

The Tanzania Electric Supplying Company Limited (TANESCO) -whose projects stand to suffer following the move - says the World Bank and African Development Bank (AfDB) have agreed to finance the projects that were to be implemented using the MCC fund.

Tanesco Managing Director Felischemi Mramba said the World Bank has agreed to fund a project to supply power in urban areas while AfDB has agreed to fund project to connect Tanzania and Zambia.

However, as the government is allaying fear on the impact of the MCC board decision, analysts fear that the move will have serious repercussions on the Tanzanian economy.

Professor Honest Ngowi, an economist from Mzumbe University, said since the money were intended to fund various development projects in key sectors - which would have speed up development in other sectors - the economy will suffer the most.

Prof Ngowi’s sentiments were echoed by Civic United Front (CUF) director of information and public communication Mr Ismail Jussa who accused the ruling party (CCM) of making decision (with regard to Zanzibar election) which will affect the lives of many Tanzanians especially those living in rural areas.

Mr Jussa added that even if Tanzania wants to become financially independent it shouldn’t deny other people’s rights or violate principles of democracy while doing so.

“I have heard some people who affiliated to the ruling party playing down the MCC board decision by claiming that Tanzania shouldn’t be interfered in its internal affairs; but they should remember that patriotism isn’t about denying other people’ rights,” said Mr Jussa, who was referring to the annulled Zanzibar election which CUF claimed it won.

Effort to have the ruling CCM comment on the development before going to press proved futile yesterday as its spokesperson Christopher Olesendeka’s phone went unanswered.

Wateja wataka meza na kiti alichokalia Rais Magufuli; Meneja aeleza ilivyokuwa


Mgahawa aliotumia Rais John Magufuli kupata mlo wa mchana na msafara wake juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza, umekuwa kivutio kwa wateja wengi wakinunua chakula na kutaka kukalia kiti na meza alivyotumia kiongozi huyo.

Meneja wa mghahawa huo wa Victoria, Elizabeth Maneno alisema jana kwamba hali hiyo ilijitokeza mara baada ya Rais kuondoka hapo.

“Hata leo tumepokea wateja wengi kulinganisha na siku nyingine, baadhi yao wanaagiza chakula kwa sharti la kutaka kukikalia kitu na meza aliyotumia Rais Magufuli,” alisema Elizabeth.

Akizungumzia hali ilivyokuwa juzi kabla na wakati wa ugeni huo meneja huyo alisema: “Ilikuwa ni hofu na woga uliochanganyika na furaha kumwona Rais akiingia kwenye mgahawa wetu wa chai ya rangi ya Sh200 na ya maziwa Sh300.

“Mshtuko wetu uligeuka furaha baada ya kubaini kuwa oda ya sahani 28 za kubeba (takeaway), tulizoagizwa mapema asubuhi bila kuelezwa zinakoenda zilikuwa za ujumbe wa Rais,” alisema na kuongeza: “Kabla Rais Magufuli hajaingia kwenye mgahawa wetu, alikuja mtu mmoja tusiyemfahamu na kuagiza sahani 28 za chakula kwa gharama ya Sh5,000 kila moja,”

Alisema baada ya kumtaarifu mteja wake kuwa chakula kiko tayari, alielekezwa kuandaa meza na viti kwa sababu wageni wake (wa mteja), sasa wameamua kula palepale mgahawani.

“Ghafla tulimwona Rais anaingia ndani ya mghahawa wetu; kwanza tulishikwa hofu, woga na kihoro tusijue tufanye nini hadi tulipogutushwa na aliyetoa oda kwa kutuagiza tugawe chakula alichoagiza,” alisema meneja huyo; “hapo ndipo tulipobaini kumbe chakula kile kilikuwa cha ugeni wa Rais.”

Aliyemhudumia Rais

“Ingawa nimewahi kumhudumia (Rais) akiwa mbunge na waziri, hii ilikuwa mara yangu ya kwanza na pengine inaweza kuwa ya mwisho ingawa siombei iwe hivyo kumhudumia akiwa Rais,” alisema Hamida Miraji aliyemhudumia Dk Magufuli na mkewe Mama Janeth.

Pamoja na chai ya rangi na ya maziwa, mghahawa huo pia unauza vyakula vya aina mbalimbali kwa bei kati ya Sh1,500 hadi Sh5,000 kwa vyakula vya kubeba, huku soda ikiuzwa kwa Sh500 kwa chupa.

Kubadili jina la mgahawa

“Bado hatujaamua, ingawa tangu juzi watu hawapaiti tena Victoria, bali mgahawa wa Magufuli; labda mkurugenzi anaweza kuamua hili,” alisema Elizabeth.
 • via MWANANCHI

Mkurugenzi wa halmashauri Itilima asimamishwa kazi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka 
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, John Aloyce amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kushindwa kuisimamia halmashuari hiyo na kusababisha kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kati ya madiwani na watendaji.

Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana mjini Langangabilili wilayani humo.

Mbali na uamuzi huo, amefuta posho zote kwa wakuu wa idara na vitengo katika halmashauri zote zilizoko mkoani hapa wanaoingia katika vikao vya madiwani.

Vikao hivyo ni pamoja na Baraza na kamati za halmashauri kwa madai kuwa hazina tija yoyote, na kuelekeza fedha hizo zilizotengwa zifanye kazi nyingine za maendeleo kama vile utengenezaji wa madawati.

Alisema alipata malalamiko dhidi ya Mkurugenzi huyo kupitia wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango wa halmashauri hiyo waliofika ofisini kwake, hivyo kuamua kuitisha kikao hicho cha dharura ili kuyasikiliza.


Katika kikao hicho madiwani hao walisema serikali ilitoa Sh milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika halmashauri hiyo lakini kazi hiyo haikufanyika, wanapohoji na kutoa uamuzi umekuwa haufanyi kazi.

“Wilaya yetu ni mpya na katika kuondoa tatizo la watumishi wa halmashauri hii kuishi mbali na makao makuu ya wilaya tuliamua kuanza ujenzi wa nyumba za watumishi na tukaletewa Sh milioni 450. Lakini kila tunapohoji matumizi ya fedha hizo hatupatiwi majibu na tunapomwagiza Mkurugenzi atuletee hakubaliani na maamuzi yetu,”alisema Kuzenza William (CCM), ambaye ni Diwani wa Kata ya Zagayu.

Walisema kuwa hata mapato ya ndani yanayopatikana hayafahamiki licha ya kuwepo kwa ushuru wa mazao mchanganyiko haulipwi na wafanyabiashara walio wengi, hivyo kusababisha shughuli nyingi za halmashauri kukwama na kuzua migogoro ya mara kati ya madiwani na ofisi ya Mkurugenzi.

“Mapato ya ndani hayafahamiki kabisa kuwa ni kiasi gani cha fedha kimepatikana, maana hatusomewi na inaonekana hata ushuru wa mazao mchanganyiko wafanyabiashara hawalipi hii timu ya mkurugenzi inayosimamia mapato sina imani nayo,” alisema Diwani Kata ya Lugulu, Robert Jongela.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Daud Nyalamu alisema madiwani wa halmashauri hiyo wanaonekana hawana uamuzi kwani waliagiza kuwa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 320 vilivyokopwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa maabara 35 za shule za sekondari vifanye kazi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika na vingi vimeharibika.

“Tulikopa benki Sh milioni 320 kwa ajili ya ujenzi wa maabara 35 zilizoko katika halmashauri yetu, vifaa vimenunuliwa lakini hadi sasa vimesambazwa maeneo mbalimbali havijafanyiwa kazi. Vimeharibika kwani saruji imeganda na mbao zimepinda na hazifai kwa ujenzi. Hii inatokana na uzembe wa Mkurugenzi wetu na kila kukicha halmashauri inadaiwa hadi madiwani hatulipwi stahili zetu,” alisema.

Akizungumzia tuhuma dhidi yake, Aloyce alisema tangu ateuliwe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo miezi sita iliyopita alikuta Sh milioni 126 zilizokuwa zimebaki katika ujenzi wa nyumba za watumishi.

“Mimi wakati nafika katika halmashauri hii nilikuta kati ya Sh milioni 450 za ujenzi wa nyumba za watumishi zilikuwa zimebaki Sh milioni 126, tulikaa na wakuu wa idara tukaamua tuzikope na kujenga ukumbi ukizingatia ya kuwa tulikuwa tunaelekea uchaguzi mkuu hivyo tungeshindwa mahali pa kukusanyia matokeo ya kura,” alisema.

Alisema licha ya tuhuma mbalimbali dhidi ya halmashauri hiyo, iliundwa tume kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuzichunguza lakini hadi sasa hawajawaletea majibu, hivyo kuomba iundwe tume huru kutoka nje ya mkoa ili kuweza kuzichunguza tuhuma zilizotajwa na madiwani dhidi yake na ikibainika yuko tayari kuachia ngazi.
 • via Malunde1 blog

Taarifa ya TAKUKURU na CCM kuhusu Wabunge 3 waliofikishwa mahakamani
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha Mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a). Wabunge hao ni Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero ; Mheshimiwa Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibala.

Wabunge hao wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mh.Thomas Simba. Akisoma mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiwa wote watatu waliomba rushwa ya shilingi Mil.30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo kwa lengo la kumsaidia ili Taarifa ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa kwa wakati huo ijadiliwe tahere 16/3/2016 ipitishwe bila marekebisho.

Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na washtakiwa wote watatu mahakama imewaachia kwa dhamana ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 5. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 14/4/ 2016 itakapotajwa tena.

TAKUKURU inawajulisha wananchi wote kwamba hakuna mtu ambaye yupo juu ya Sheria. Rushwa haivumiliki!

IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
31 MACHI, 2016

Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibara, Mhe. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero  Mhe.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa, Mhe.Victor MwambalaswaFor first time! The annual AfPIF 2016 will be held in Dar es Salaam, Tanzania


The Internet Society brings African Peering and Interconnection Forum to Tanzania for first time


The Internet Society will bring its annual Africa Peering and Interconnection Forum (AfPIF) to Tanzania for the first time. The organisation has partnered with the Tanzania Internet Service Providers Association (TISPA) to hold the seventh annual AfPIF in the country’s capital, Dar es Salaam, 30 August- 1 September, 2016. Serving as a platform to expand Internet infrastructure and services across Africa, the event will bring together key players to address the opportunities in interconnection, peering and traffic exchange on the continent.

The forum seeks to build cross-border interconnection opportunities and facilitate discussions on African Internet infrastructure challenges, including terrestrial capacity, development of national and regional Internet Exchange Points (IXP) and local content.

“Internet connectivity in Africa has increased over the last few years delivering access to close to a third of the population on the continent. Improving interconnection and traffic exchange has become even more important today as an increasing number of Africans rely on the Internet in their daily lives,” explained Dawit Bekele, Regional Director for Africa of the Internet Society.

“Since we first launched this event six years ago, we have seen a notable increase in investments and initiatives that have led to improvements in the extent and quality of national and regional interconnection. This has been possible thanks to the connections people make at AfPIF. The forum has in particular enabled Africans to collaborate and work together towards the development of the Internet infrastructure on the continent,” he added.

"TISPA remains committed to advancing and protecting the interests of its members while promoting the advancement of the Internet sector. We believe by working with AfPIF to host this auspicious event in August will be one leap forward for Tanzania in terms of network optimization" said Vinay Choudary, the chairman of TISPA.

AfPIF has previously been held in Kenya, Ghana, South Africa, Morocco, Senegal and Mozambique. Last year’s event featured 232 participants from 57 countries and an online participation of 978 people in 77 different countries.

The Internet Society aims to advance the African interconnection agenda at AfPIF-2016, in line with the vision to achieve 80% local and 20% international Internet traffic by the year 2020. The event welcomes sponsors as well as past attendees and new participants to join the leading peering and interconnection forum for Africa.

Promising more than just a forum – AfPIF connects Internet service, infrastructure, and content providers, with government regulators and policymakers to provide an opportunity to advance peering and interconnection arrangements and to make a positive contribution to Africa’s Internet resources.

Read last year’s event summary report: http://www.internetsociety.org/afpif-2015/meeting-summary

Visit AfPIF 2016 websites in English: http://www.internetsociety.org/afpif-2016/home

Visit AfPIF 2016 websites in French: https://www.internetsociety.org/afpif-2016-fr

Media Contact:

Internet Society
Betel Hailu
[email protected]

TISPA
Ismail Settenda
[email protected]

About the Internet Society 

The Internet Society (www.InternetSociety.org) is the trusted independent source for Internet information and thought leadership from around the world. It is also the organizational home for the Internet Engineering Task Force (IETF). With its principled vision and substantial technological foundation, the Internet Society promotes open dialogue on Internet policy, technology, and future development among users, companies, governments, and other organizations. Working with its members and Chapters around the world, the Internet Society enables the continued evolution and growth of the Internet for everyone.

About Tanzania Internet Service Providers Association (TISPA)

TISPA (http://TISPA.or.tz) is an association that is also non profit organization (NGO) whose members are the Internet Service Providers operating in Tanzania and aims to bring together the Internet community to collectively make the Internet accessible to as many people as possible by encouraging the proliferation of Internet services in the sector, and have their effects be as positive as possible to the users and the country in general.
For more information, visit http://TISPA.or.tz

Sehemu ya III: Wimbi la PhD za Heshima Tanzania – Utoposhwaji uliofumbiwa macho

Wimbi la PhD za Heshima Tanzania – Utoposhwaji uliofumbiwa macho
Sehemu ya Tatu
Nianze sehemu hii ya tatu ya makala hii kwa kuweka kumbukumbu sawa kwamba mimi sio mpinzani wa shahada za heshima. Nikiwa nimepata neema ya ufahamu kidogo kuhusu dhana ya taaluma na elimu kwa kiwango cha chuo kikuu, naelewa jinsi ambavyo heshima hii inaweza kutolewa kwa kuzingatia vigezo na kwa watu ambao wanastahili na ikawa na tija kwa anayeitoa na anayepewa. Shahada za heshima zinatambulika vema katika ulimwengu wa kisomi kote duniani kama namna ya kutambua mchango wa watu katika jamii kupia ubunifu, uongozi, utafiti, na mengine yenye kuleta mchango chanya katika kuboresha maisha ya mwanadamu, utamaduni wake, na mazingira yanayomzunguka. Kwa mfano: wakati natunukiwa shahada ya kwanza pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Mzee Mkapa alitunukiwa shahada ya PhD ya heshima (Honoris Causa) kwa mchango wake katika kukuza Kiswahili katika kipindi cha uongozi wake. Pamoja na kwamba sijabahatika kusoma andiko la kisomi la sababu za kutunukiwa kwake, lakini nadhani hakuna mtu ambaye anaweza kuhoji ni kwa jinsi gani Rasi Mkapa aliheshimu lugha ya Kiswahili katika urais wake.
http://news.mak.ac.ug/documents/award.JPG
Mzee Mkapa akitunukiwa PhD ya heshima ya sheria ya Chuo Kikuu cha Makerere mwaka 2009.


Katika hotuba zake hasa zile za kila mwisho wa mwezi kwa taifa zilitolewa kwa Kiswahili kilichonyooka na ziliepuka kabisa kuchanganya na lugha ya kigeni hata pale ambapo ufafanuzi kwa lugha hiyo ungeweza kuweka mkazo au uelewa zaidi. Katika kipindi chake maneno mengi ya Kiswahili ambayo yalikua mageni kwa watu wengi yalipata umaarufu kupitia hotuba zake kama vile mshikadau (likaja kuwa mdau), teknohama (likaja kuwa tehama), utandawazi, ukwasi, asasi, uwekezaji,nk. Mzee Mkapa alitumia Kiswahili kwa ufasaha huku akijulikana  wazi kwamba ni msomi mwenye uwezo mkubwa sana wa matumizi ya lugha ya kingereza. Sidhani kama kuna mtu kipindi kile angeweza kutilia shaka uamuzi wa baraza la chuo la UDSM kuheshimu mchango wake kwa ustawai wa lugha yetu maridhwa ya Kiswahili. Kuna watu wengi hapa Tanzania ambao wamepewa shahada mbalimbali za heshima na vyuo vya ndani na nje ya nchi lakini naomba nisiwataje maana sio msingi wa mada hii.
Umakini katika kutoa na kupokea Shahada za Heshima.
Utoaji na upokeaji wa shahada za heshima sio jambo jepesi na halitakiwi kuchukuliwa kimzahamzaha na chuo kinachotoa heshima hiyo au yule anayepokea. Wale wanaoshiriki katika michakato hii kwenye vyuo vikuu wanajua ni kwa kiasi gani mchakato huu “unapitishwa kwenye moto” ili kuhakikisha chuo hakifanyi hivyo kwa aibu na kumpa mtu asiyestahili. Jambo hili hufanyika kwa umakini na usiri mkubwa sana na jopo la wahadhiri waandamizi


 • Baadhi ya vyuo huko Magharibi, majina ya watu wanaotarajiwa kupewa shahada za heshima katika mahafali yanayofuata pamoja na sababu za kuwatunuku huwekwa hadharani mapema kama namna ya kuweka uwazi zaidi katika mchakato.
 • Pamoja na kwamba utoaji huu wa shahada za heshima ni sehemu ya tamaduni katika mahafali ya vyuo vikuu kila mwaka, wakati mwingine vyuo makini huamua kutokutoa heshima hizi kwa miaka kadhaa iwapo mchakato wao hutapata mtu ambaye anastahili na anabeba heshima ya chuo chao.  Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na kuwa na umri wa miaka 55 sasa tangu kuanzishwa kwake, kimeshatoa shahada za heshima kwa watu wasiozidi 30. Hii inamaanisha, kuna miaka zaidi ya 25 ambapo chuo hiki kikongwe nchini hakikuona mtu anayestahili heshima yao na hivyo kutolazimisha kuitoa. Wakati vyuo vingine huko Magharibi huwa vinatunuku hadi watu 10 PhD za heshima kwa mwaka mmoja, sina hakika kama UDSM imewahi kutoa kwa zaidi ya mtu mmoja kwa wakati/mwaka mmoja.
 • Vyuo vikuu makini huchukua taadhari kubwa katika utoaji wa shahada za heshima kwani vyakua kwamba mtu anayepokea heshima yao huendelea kufungamana na chuo hicho na anabeba taseira ya chuo husika maisha yake yote. Ni aibu kwa chuo kutoa shahada ya heshima kwa mtu ambaye yuko kwenye hatari ya kufanya jambo la aibu kwenye jamii na hivyo kuaibisha chuo kilichomtunuku heshima
 • Shahada ya heshima ni mali ya chuo kilichoitoa kwa kuwa anayepewa hajahusika kwa vyoyote vile katika kuitafuta na kuipata. Hivyo, chuo husika kina uwezo wa kumnyang’anya (revoking) mpokeaji shahada ya heshima waliyompa iwapo itathibitika kwamba mwenendo wake haustahili heshima waliyompa. Vyuo hulazimika kufanya hivyo kama namna ya kujitenga na mambo maovu yamuhusuyo mtu huyo na kuendelea kutunza heshima na taswira yao kwenye jamii
 • Kwa mfano, Mchekeshaji maarufu nchini Marekani aitwaye Bill Cosby ameshatunukiwa PhD za heshima na vyuo zaidi ya 60. Hata hivyo siku za karibuni Cosby ameshutumiwa kwa udhalilishaji na kubaka wanawake zaidi ya 60 nchini humo kitendo aanachoshutumiwa kukifanya kwa miaka mingi. Kesi inayomkabili Cosby imepelekea vyuo kadhaa kati ya vilivyomtunuku PhD za heshima kumwondolea heshima hiyo kwa kufuta PhD waliyompa.
 • Kama njia ya kutunza heshima zao, baadhi ya vyuo duniani vimejiwekea sera ya kutokutoa kabisa shahada za heshima. Mingoni mwa vyuo hivyo ni vyuo bora kabisa duniani kama vile Stanford University (USA), Cornell University (USA), Massachusetts Institute of Technology (USA) na Rice University (USA).


Kwa upande mwingine, kila anayepewa taarifa ya kuteuliwa kupewa shahada ya heshima na chuo kikuu chochote kile, ana mambo kadhaa ya kuzingatia kabla hajakubali heshima hiyo. Ni vema kujipa muda wa kufanya utafiti kidogo na kujiridhisha ustahili wako wa heshima usika kabla ya kuipokea.
 • Ajipime na kujitizama iwapo anastahili shahada ya heshima anayopewa. Je, sababu za heshima hiyo zilizoainishwa zinalingana na anavyojiona au alichofanya kwenye jamii? Ni ajabu sana iwapo utaitiwa tuzo ya kuwa baba aliyeonesha mfano wa malezi mazuri kwa watoto na ukaikubali wakati hujawahi kuoa, huna watoto wa kuwazaa, na hujawahi kulea watoto tegemezi.
 • Hao wanaotaka kukupa shahada hiyo ni kina nani? Wanatambulikaje na heshima yao ikoje mbele ya jamii? Itakua ajabu sana pale utakapoitiwa tuzo ya kuwa kiongozi bora na kundi la wauza unga, au wakwepa kodi, au majambazi na ukaenda kuipokea kwa sababu tu inaonesha umeheshimiwa.
 • Je kuna kitu kilichojificha nyuma ya heshima unayopewa? Wanaoataka kukupa wana jambo la siri lililojificha nyumba ya heshima yao? Tutamshangaa waziri wa elimu au mkuu wa nchi kuitiwa PhD ya heshima na chuo cha nje ambacho kiko kwenye mchakato wa kutafuta kibali cha uwekezaji nchini na akaenda kuipokea.
 • Heshima hiyo ina tija gani kwako na itakupa taswira gani kwenye jamii unayoitumikia? Unaweza kusimama mahali na kuitetea heshima hiyo kwa maneno na matendo yako?
 • Je kuna jambo la mbeleni linalokuhusu ambalo laweza kuwa chanzo cha wengine kukufungamanisha nao kaa PhD ya heshima ili waje kufaidika nawe hapo baadaye?
 • PhD unayopewa unaigharamia au yaendana na masharti yoyote? Unatakiwa kuingia gharama zozote kwa maana ya fedha au rasilimali kuigharamia heshima unayopewa? Itakua ajabu sana chuo kimuitie PhD ya heshima mtu mwenye staha na shahiki ya kuheshimika kwenye jamii, halafu kumuhitaji alipie ada na gharama zingine za mahafali ya kumtunuku.
 • Je, wajiona ukisumbuliwa na “mchecheto” wa kujitambulisha kwa degree ya heshima mara utakapopewa? Unajiona ukitaka kuitumia kujitafutia maslahi kwenye jamii au kwa nafasi uliyo nayo? Unajiona ukiitumia kulazimisha heshima kwako? Ukiyaona haya, jua kabisa hukustahili heshima uliyopewa. Nimetazama taarifa za Mzee Mkapa na kukuta hadi sasa ametunukiwa PhD za heshima tisa na zingine ni za vyuo vinavyoheshimika duniani. Hata hivyo sijawahi kumsikia akijitambulisha au kutambulishwa kama Dr. Benjamini Mkapa.
 • Je, unashangazwa au kushtuka unapopata habari za kupewa heshima na chuo kikuu? Je wajiona kama hustahili na umependelewa? Unapata kitu (substance) kwa maana ya mchango wako ukilinganisha na zilizotolewa na wanaotaka kukuheshimu? Kama wajiona hivyo baada ya kutaarifiwa, ni wazi hustahili heshima hii.


Maswali haya na mengine, yanaweza kumsaidia mtu anayependekezwa kutunukiwa PhD ya heshima kuwa kwenye nafasi nzuri ya kukubali heshima hiyo au vinginevyo. Hulazimiki au kushurutishwa na mtu yoyote kukubaliana na kila pendekezo la chuo chochote kinachotaka kukutunuku shahada ya heshima.  Mara nyingine utajikuta umeonesha kwamba unastahili heshima zaidi ya unayotaka kupewa iwapo utatazama vigezo na kusema, “Nashukuruni sana kwa kunifikiria lakini nasitikita kwamba siko tayari kupokea heshima munipayo”


Mara nyingi (kama sio zote) kwa vyuo makini duniani, wale wanaoalikwa kupewa shahada za heshima, hutakiwa kutoa hotuba ya kisomi katika sherehe za mahafali husika. Muhusika huandaa hotuba katika mada mahususi na mara nyingine wengi hutoa hotuba zao zikielekea kwenye mwelekeo wa heshima waliyopewa. Pamoja na kwamba huu ni utamaduni wa tukio hili, kwa upande mwingine husaidia kumwelewa yule anayetunukiwa na ni kwa jinsi gani anastahili kile alichotunukiwa.


Ni vema kukiri kwamba, utoaji wa shahada za heshima hata katika vyuo vyenye heshima, umeingiliwa sana na maslahi ya kisiasa. Ndio mana wingi wa shahada za PhD za heshima umekua ukielekezwa kwa marais au wakuu wa nchi hata pale ambapo uongozi wao ulikua na utata na kukosa kukidhi viwango vya utawala bora. Vyuo vingi hasa katika nchi maskini vimekua vikishindana kuwatunuka wakuu wa nchi zao PhD za heshima huku ikijulikana kwamba wakuu hao wana mamlaka na maamuzi makubwa juu ya uendeshaji wa vyuo hivyo na viongozi wake. Wako watu wengi kwenye jamii wanaostahili  kutambulika ikiwa ni pamoja na wanasiasa/viongozi kama vile mabunge na mawaziri lakini ni ngumu sana kuona wakitambulika na vyuo kwa kutunukiwa PhD za heshima. Badala yake heshima hizo zimekua zikielekezwa kwa wakuu wa nchi na kuonekana kama hazina mashiko na kuhoji iwapo viongozi wa vyuo vikuu hawafanyi hivyo kwa lengo la kujipendekeza kwa mkuu wa nchi.


Katika sehemu ya nne na ya mwisho ya makala nitaonesha kwa vielelezo maigizo ya utoaji shahada za heshima hapa Tanzania.


Imeandikwa na Mwalimu MM - Waweza mwandikia kupitia mmmwalimu(at)gmail.com

HESLB yaanza kutekeleza mikakati ya kukusanya malipo ya wadaiwa

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (katikati) wakati Kamati hiyo ilipotembelea ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jijini Dar es Salaam
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeanza kutekeleza mikakati mipya ya ukusanyaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wadaiwa ambayo itaongeza wastani wa ukusanyaji wa Tshs 2.6 bilioni za sasa hadi kufikia Tshs 8 bilioni ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi ameyasema hayo leo (Jumatano, Machi 30, 2016) jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyotembelea ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mwenge. 

“Hadi mwezi uliopita (Februari, 2016) tulikuwa tunakusanya wastani wa shilingi bilioni 2.6 kwa mwezi, lakini sasa tumeongeza kasi na mikakati mipya ambayo itawezesha kukusanya shilingi bilioni 6 mwezi Aprili na shilingi bilioni 8 ifikapo mwezi Juni mwaka huu,” amesema Bw. Sabi aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo na miezi miwili iliyopita. 

HESLB ilianzishwa ilianza kazi mwaka 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na pia kukusanya mikopo kwa wanufaika. 

Hadi sasa, zaidi ya shilingi 2.1 trilioni zimetolewa kwa wanufaika na kati ya fedha hizi, mikopo iliyoiva na inayopaswa kukusanywa ni shilingi 258 bilioni ambazo wanufaika wake wamemaliza au kusitisha masomo yao na vilevile kumaliza muda wa kujipanga kuanza kulipa (grace period). 

Kwa mujibu wa Bw. Sabi, hadi sasa, HESLB imekusanya shilingi 91 bilioni kati ya shilingi 258 bilioni zilizoiva na hivyo kupaswa kukusanya. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alikuwa akijibu hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati hiyo waliokutana na watendaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi na HESLB wakiongozwa na Waziri Prof. Joyce Ndalichako na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya. 

Bw. Sabi alitaja mikakati mipya iliyobuniwa na HESLB kuwa ni pamoja na kuimarisha mtandao baina ya Bodi na waajiri kutoka sekta binafsi na umma ambao unalenga kubaini na kukusanya kiasi cha shilingi 7.02 bilioni kwa mwaka kutoka kwa wanufaika 136,252. 

“Tunapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa taasisi za Serikali na sasa tumejipanga kupitia upya mitandao ya waajiri kwa kushirikiana na taasisi kama Chama cha Waajiri (ATE), Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF) na Shirikisho la Asasi zisizo za Kiserikali (TANGO) ili kuhuisha takwimu zetu kuhusu waajiri ili kukusanya taarifa za wadaiwa wapya kwa haraka,” alifafanua Bw. Sabi. 

Mikakati mingine ni kutoa elimu na kuimarisha ushirikiano na wadau mahsusi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii (SSRA), Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na vyama vya kitaaluma.
 
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Peter Serukamba ameitaka HESLB kuongeza kasi ya kudai mikopo iliyoiva na kuutaka uongozi wa HESLB kuandaa orodha ya wadaiwa wote na kuiwasilisha kwa kamati ili ifanyiwe kazi.
“Ni lazima kuwe na fedha ili kuwezesha kutoa mikopo kwa wahitaji wengine ...haiwezekani mtu anapata mkopo halafu halipi...andaeni orodha ya wote walionufaika na mikopo ambayo itaonyesha nani halipi, nani analipa na nani amemaliza na tutaamua tufanye nini,” alisema Sekukamba. 

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai mwaka 2005 kwa lengo la kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji waliopata nafasi za masomo katika vyuo vya elimu ya juu na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wadaiwa walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba (aliyesimama) akiongea na watendaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Machi 30, 2016). Kulia ni Waziri Prof. Joyce Ndalichako

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Dkt. Ely Macha (kulia) wakati Kamati hiyo ilipotembelea ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Machi 30, 2016). Katikati mwenye suti ya kijivu ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi. (Picha: HESLB)

Ufafanuzi wa SSRA kuhusu kima cha chini cha mafao ya wastaafu

UFAFANUZI KUHUSU KIMA CHA CHINI CHA MAFAO YA WASTAAFU (MINIMUM PENSION BENEFITS)


Hivi karibuni Mamlaka imekuwa ikipokea Malalamiko mengi kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kuhusu kuwepo kwa tofauti ya kima cha chini cha malipo ya mafao ya wastaafu. Malalamiko haya yanajitokeza kufuatia kutolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 285 la mwaka 2015 kuhusu kupandishwa kwa kima cha chini cha Mafao kwa baadhi ya wastaafu. Kufuatia malalamiko hayo, Mamlaka inatoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
 • Mnamo mwezi Julai mwaka 2015, Wizara ya Fedha kupitia Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 30/6/2015 (the Public Services Retirement Benefits (Minimum Pensions) Order, 2015 (Government Notice No GN N. 285 of 30/06/2015) baada ya kuridhiwa na Bunge, ilipandisha kima cha chini cha malipo ya mafao kwa wastaafu chini ya kifungu cha 30 cha Sheria ya PSPF. Kwa mujibu wa Tangazo hilo, kima cha chini kwa malipo ya pensheni ya kila mwezi kiliongezeka kwa kiasi cha shilingi 45,000/- pamoja na asilimia 10 ya mafao ya zamani na hivyo kufanya kima cha chini kupanda kufikia kiasi cha takribani Shilingi laki moja (100,000/=).
 • Mamlaka inapenda kufafanua kwamba, ongezeko hilo liliwalenga wastaafu waliokuwa kwenye mfumo wa pensheni wa zamani wa kutochangia (Non-Contributory) wanaolipwa mafao yao na Hazina kupitia Mfuko wa PSPF na HALIKUWAHUSU wastaafu waliopo katika Mifuko ya Msingi (Mandatory Schemes) yaani NSSF, PPF, LAPF, PSPF na GEPF.
 • Aidha, ni muhimu ikaeleweka kwamba, utaratibu wa kuweka kima cha chini cha mafao kwa wanachama wa Mifuko ya Msingi (Mandatory Schemes) yaani NSSF, PPF, LAPF, PSPF, GEPF, NHIF & WCF umeainishwa katika kifungu cha 25 cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135 kikisomwa pamoja
na kifungu cha 36 cha Sheria hiyo. Kwa mujibu wa vifungu hivyo, kima cha chini cha malipo ya mafao ya wastaafu hupangwa na Mamlaka baada ya kufanya tathimini (Actuarial Valuation) na kushirikisha wadau. Lengo la kufanya tathimini kabla ya kupandisha kima cha chini cha malipo ya mafao ni kujiridhisha juu ya uwezo wa Mfuko husika kubeba ongezeko linalopendekezwa. Kwa kupitia utaratibu huu, mwaka 2014 Mamlaka ilitengeneza na kutoa Kanuni za Uwianishaji wa Mafao (Pensheni Benefit Harmonisation Rules). Kanuni hizi pamoja na mambo mengine zinaainisha kima cha chini cha malipo ya mafao kwa wastaafu kuwa ni asilimia 40 ya kima cha chini cha mshahara wa Sekta husika. Kununi hizi zinatumika kwa Mifuko ya Msingi ambayo ni NSSF, PPF, LAPF, PSPF & GEPF.
 • Vile vile katika jitihada za kuendelea kuimarisha Sekta, Mamlaka imekamilisha zoezi la kufanya tathimini ya Mifuko na Taarifa ya Mtathmini hiyo ipo katika hatua ya majadiliano na wadau wakiwemo wawakilishi wa wanachama. Pamoja na mambo mengine, taarifa hiyo itakuja na mapendekezo mahsusi ya namna bora ya kuboresha mafao ya wanachama. Hivyo, Mamlaka inawasihi wanachama na wadau wengine wote wawe na subira wakati huu ambao taarifa ya Mtathimini inafanyiwa kazi.
Imetolewa na Kitengo Cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz

Dar Es Salaam